text
stringlengths 10
3.8k
|
---|
<s>[INST] Mradi wa Kuzidisha Ubora wa Chakula cha Siku zijazo (AVCD) nchini Kenya- Kitengo cha Mifugo [/INST] Mwongozo wa Nyanjani wa magonjwa ya mifugo kwa kutegemea dalili zao katika maeneo ya Kaskazini mwa Kenya </s> |
<s>[INST] Dibaji [/INST] Magonjwa ya mifugo hupunguza kiwango cha ufugaji na biashara za mifugo, hasa katika maeneo ya ufugaji ambako huduma za tiba ya mifugo ni adimu. Mifumo mipana ya ufugaji inayotumiwa maeneo haya- kama vile ufugaji wa kuhamahama, uhamaji wa kila msimu na mifumo-mseto ya ufugaji na ukuzaji wa mazao kwa pamoja- inazua changamoto zaidi kutokana na ulishaji wa pamoja wa mifugo, uhamaji wa kila mara na mwingiliano kati ya mifugo na wanyamapori. Tafiti za hivi majuzi katika ukanda wa kaskazini mwa Kenya (miongoni mwa jamii za Waborana, Warendille, Waturkana, Wasomali na nyingine za wafugaji) zinaonyesha kuwa magonjwa ya kuambukiza kama vile Homa ya Mapafu inayosambaa haraka, ugonjwa wa mapafu ya mifugo, sotoka ya wanyama wa kucheua (PPR), kimeta, ugonjwa wa vinundu vya ngozi na ugonjwa wa miguu na midomo hutokea kila mara. Tafiti hizo, kadhalika, zinaonyesha kuwa jamii hutumia kiwango kikubwa cha dawa za tiba ya mifugo kudhibiti magonjwa haya lakini tiba nyingi hutumika bila ushauri wa kitaalamu. Kwa hivyo, kuna uwezekano kwamba nyingi ya tiba hizi hazifai. Muhimu zaidi ni kuwa, kipindi cha baada ya matumizi ya dawa hizo ni kifupi kuliko inavyotakiwa, hali inayozua hofu kuwa bidhaa za mifugo waliopewa dawa hizo zina kiwango kikubwa cha mabaki ya dawa, hivyo basi, upo uwezekano kuwa hali hii inachangia mifugo kuwa sugu kwa dawa. Idara ya Huduma ya Afya ya Mifugo, kwa ushirikiano na mashirika ya kimaendeleo ya humu nchini na kimataifa, imetekeleza mikakati mseto ya kufuatilia na kukabiliana na magonjwa katika eneo la kaskazini mwa Kenya. Hata hivyo, hatua hizi zinapaswa kutekelezwa na wadau wote katika sekta hiyo ili zifanikiwe. Wamiliki wa mifugo, kwa mfano, wanao mchango mkubwa katika uhamasishaji/ ufundishaji kuhusu magonjwa kwa kutoa ripoti zinazohusu mikurupuko ya magonjwa. Usahihi wa taarifa zinazotolewa unaweza kuimarishwa kupitia mafunzo kuhusu dalili za magonjwa ambayo wafugaji wanakumbana nayo mara kwa mara. Mwongozo huu utatumiwa kuwapa mafunzo wafugaji wa kieneo, watoaji wa taarifa za magonjwa katika kiwango cha kijamii, matabibu/wahudumu wa kibinafsi wa afya ya wanyama, wauzaji wa dawa, wafanyabiashara na wadau wengine husika kuhusu magonjwa na mbinu za kuyadhibiti magonjwa ya kieneo ili kuimarisha uwezo wao wa kusaidia kufaulisha harakati za utekelezaji wa mikakati ya ufuatiliaji na ukabilianaji na magonjwa hayo. Muundo wa Mwongozo huu umechochewa na Mwongozo wa Nyanjani wa Magonjwa ya Wanyama unaotegemea Dalili (yaani A Field Manual of Animal Diseases by Syndromes) - uliochapishwa mwaka wa 2013 na Mradi wa Viwango, Mbinu na Taratibu za Afya ya Wanyama (yaani Standards Methods and Procedures in Animal Health -SMP-AH) kama sehemu ya Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani, Ukanda wa Afrika Mashariki; Ofisi ya Umoja wa Afrika, Interafrican, kuhusu Rasilimali za Wanyama; Idara ya Marekani ya Kilimo - Kitengo cha Kilimo cha Kigeni; na Chuo Kikuu cha Georgia, Athens nchini Georgia. Hata hivyo, mwongozo huu ni sehemu ya jozi/awamu tatu za miongozo inayoangazia magonjwa ya kieneo ambayo huathiri hasa ng’ombe, kondoo, mbuzi na ngamia katika ukanda wa kaskazini mwa Kenya. Hii ni tofauti na mwongozo wa SMP-AH uliokarabatiwa mahsusi kwa ajili ya magonjwa yanayoathiri biashara za mifugo. </s> |
<s>[INST] Utaratibu wa mwongozo wa ngamia [/INST] Mwongozo huu wa ngamia umewasilishwa kama Awamu ya 3 inayoangazia magonjwa ya ngamia. Magonjwa hayo yameanishwa katika makundi tisa kulingana na dalili zayo kuu; kama vile, kuathiriwa kwa mfumo wa kupumua, maambukizi na uvamizi wa ngozi, madonda ya miguu na midomo, ukosefu wa utulivu, kuharibika kwa mimba/ujauzito, kuhara/mharo, magonjwa ya kutokwa na damu ghafla, mkojo mwekundu na magonjwa mengine ya kieneo yanayoambukiza ngamia. Mada zilizoangaziwa chini ya kila ugonjwa ni majina ya wenyeji, umri wa ngamia wanaoathiriwa, uambukizaji, idadi ya wanyama wanaoathiriwa katika kundi, idadi ya wanaokufa, msambao, hali hatari zinazochangia maambukizi, dalili za ugonjwa, wanyama waliokufa/mizoga, udhibiti na uzuiaji/kinga. Mwongozo huu ni nakala inayoweza kuimarishwa baada ya muda kutegemea michango ya wadau mbalimbali watakaohusishwa. </s> |
<s>[INST] Shukrani [/INST] Watu wengi walichangia katika utayarishaji wa mwongozo huu. Wanajumuisha maafisa wa afya ya wanyama kutoka kaunti za Turkana, Marsabit, Isiolo, Garissa na Wajir walioshiriki katika warsha za mafunzo; Michael Baariu, Dabasso Barako, Changayo Orkhobeshe, Ehele Haile, Stephen Mutahi, Boku Bodha, Adano Umuro, Dennis Mwongela, Joseph Muriira, John Koskei, Siyat Onle Takal, Abubakar Siraj, Job Ronoh, Jane Akale, Daud Abukar na Anthony Ngugi. Joseph Mathooko kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo pia alishiriki. </s> |
<s>[INST] Marejeleo yaliyopendekezwa [/INST] Bett, B., Kihu, S., Wamwere-Njoroge, G. and Kiara, H. 2019. Field manual for livestock diseases in pastoral areas in northern Kenya based on syndromes. Camel diseases (Volume 3). Accelerated Value Chain Development (AVCD) Program - Livestock Component. Nairobi, Kenya: ILRI. Bett, B., Kihu, S., Wamwere-Njoroge, G. na Kiara, H. 2019. Field manual for livestock diseases in pastoral areas in northern Kenya based on syndromes. Camel diseases (Volume 3). Mpango wa Accelerated Value Chain Development (AVCD) - Livestock Component. Nairobi, Kenya: ILRI. </s> |
<s>[INST] Magonjwa ya maambukizi na uvamizi wa ngozi kwa jumla [/INST] Sehemu hii inahusu magonjwa ambayo dalili zake hujidhihirisha kupitia maambukizi ya ngozi. Yanajumuisha upele unaowasha (ambao huathiri aina zote za mifugo), majipu, mapunye na tetekuwanga (Camel pox) ya ngamia. </s> |
<s>[INST] Mifugo wote [/INST] Picha 1.1.1 Ngamia aliyeathirika na upele unaowasha hupoteza manyoya na ngozi kujikunjakunja(wrinkles). </s> |
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Mnyama aliye mzima kiafya hupata ugonjwa huu kwa kugusana na mwenzake aliyeambukizwa au kwa kujisugulia mahali ambapo wanyama wagonjwa walijisugulia. Upele wa Kuwasha husababishwa na wadudu wanaopenyeza na kukaa kwenye ngozi. Wadudu hao huweza kuishi katika mazingira hayo kwa hadi muda wa wiki mbili. </s> |
<s>[INST] Idadi inayoambukizwa katika kundi la wanyama [/INST] Hadi asilimia 20 ya wanyama katika kundi moja huambukizwa ila hii hutegemea ubora wa mbinu zinazotumika kuudhibiti ugonjwa huu. </s> |
<s>[INST] Kutoka manyoya katika sehemu za ngozi zilizoathirika [/INST] Huanzia sehemu yoyote iliyogusana na mnyama mgonjwa/ mnyama aliyeathirika na kuenea katika sehemu nyingine za mwili </s> |
<s>[INST] Epuka kuchanganya makundi ya wanyama [/INST] Tenganisha wanyama wageni, uwatibu kwa kufuata ushauri wa afisa wa tiba ya mifugo ndipo uwachanganye na wengine </s> |
<s>[INST] [Ni mifugo wepi wengine wanaothirika] [/INST] Picha 1.2.1 Majipu pembeni mwa jicho Picha 1.2.2 Jipu hatari kwenye kiwiko cha kushoto </s> |
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Majipu yanaweza kutokana na maambukizi kwenye sehemu zilizokwaruzwa au majeraha, kiwewe (trauma), au kutumia sindano chafu kumdungia mnyama mwingine. </s> |
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Ugonjwa huu hausababishi vifo isipokuwa iwapo viini vimeingia ndani ya damu na kusababisha maambukizi. </s> |
<s>[INST] Majipu haya yanaweza kupasuka na kutoa usaha wenye rangi ya manjano isiyokolea [/INST] Hutokea mahali popote mwilini lakini mara nyingi huwa kwenye tezi, kichwa, shingo, kifua, mgongo na miguuni. </s> |
<s>[INST] Wanyama wote huambukizwa [/INST] Picha 1.3.1 Sehemu ya madonda ya mviringo iliyoathiriwa na mashilingi (mapunye) kwenye shavu la mguu wa ngamia </s> |
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Mgusano wa moja kwa moja baina ya Wanyama wagonjwa na wazima kiafya. Wanyama hao pia wanaweza kushikwa na mapunye kwa kujisugulia mahali ambapo mnyama aliyeambukizwa alijisugulia. </s> |
<s>[INST] Idadi ya Wanyama wanaoambukizwa katika kundi [/INST] Wanyama wachanga kiumri ndio hasa huambukizwa, na wengi wa wanyama (hasa wanaofugwa pamoja) huambukizwa. </s> |
<s>[INST] Hakuna [/INST] Picha 1.4.1 Vipele vya tetekuwanga (Camel pox) sehemu ya mdomo Picha 1.4.2 Vipele sehemu ya chini ya mkia </s> |
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Ni ugonjwa wa kuambukizana sana wa ngozi unaosababisha vipele, na unaosambazwa kupitia migusano baina ya wanyama wagonjwa na wasio wagonjwa. </s> |
<s>[INST] Idadi ya wanaoathirika kwenye kundi [/INST] Huathiri zaidi wanyama wachanga, hasa wenye umri usiozidi miaka mitatu (wanyama waliozaliwa baada ya mkurupuko wa mwisho wa upele huo). Ikiwa wakomavu wataathirika, fahamu kuwa ugonjwa huo ni hatari zaidi. </s> |
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Ugonjwa huu hausababishi vifo lakini panapotokea mkurupuko hatari, kati ya ngamia 10 wachanga walioathirika 3 wanaweza kufa; wale wa kike huavya mimba, na kiwango cha maziwa kuvurugwa. </s> |
<s>[INST] Vipele na vidonda kutokea kwenye pua, mdomo, macho na chini ya mkia [/INST] Picha 1.4.3 Vidonda vingi vigumu kwenye mdomo Picha 1.4.4 Vidonda vigumu katika sehemu kadhaa za mwili wa ngamia </s> |
<s>[INST] Magonjwa yenye dalili za kukosa utulivu/kiwewe [/INST] Sehemu hii inaangazia magonjwa yenye dalili za kukosa utulivu kama vile kuzungukazunguka kila mara, kufinyilia kichwa kwenye kitu miongoni mwa nyingine. Magonjwa yaliyoangaziwa katika sehemu hii yanajumuisha kichaa cha mbwa na maji kujaa kwenye moyo. </s> |
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Maambukizi hutokea baada ya mnyama aliyeambukizwa kumuuma mwingine, hasa mbwa na wanyamapori wa jamii ya mbwa. </s> |
<s>[INST] Ndogo zaidi--- mara nyingi huwa ni mnyama mmoja tu katika kundi [/INST] Idadi ya vifo </s> |
<s>[INST] Dalili kuu za ugonjwa huu [/INST] Mnyama anaweza kuwashambulia wanyama wengine, watu na vitu vilivyo katika mwendo lakini mashambulio hayo huwa hayajakusudiwa. </s> |
<s>[INST] Mbwa kuchanjwa [/INST] Mfungie mnyama aliyeathiriwa mahali na upige ripoti iwapo kisa chochote cha kichaa cha mbwa kimetokea. </s> |
<s>[INST] Maji kujaa kwenye moyo [/INST] Hakuna jina la wenyeji kwa ugonjwa huu wa ngamia. Ugonjwa huu uligunduliwa na kuripotiwa kwa mara ya kwanza miongoni mwa ngamia mnamo mwaka 2016. </s> |
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Viini vinavyosababisha ugonjwa huu hupitishwa na kupe, hasa wenye rangi nyingi. Kupe huyo huchukua viini hivyo wakati akimfyonza damu mnyama aliyeambukizwa. Viini hivi hukua ndani ya kupe huyo na baadaye kupitishwa hadi kwa mnyama mwingine anayefyonzwa damu na kupe huyo huyo. </s> |
<s>[INST] Idadi ya mifugo wanaoathiriwa [/INST] Idadi ya wanyama wanaoathirika hutofautiana kutegemea eneo husika kulingana na idadi ya kupe, wanyama kuwahi kuambukizwa hapo awali, na mbinu zinazotumika kuudhibiti ugonjwa huu. Mkurupuko wa mwisho wa ugonjwa huu miongoni mwa ngamia nchini Kenya, uliripotiwa kuchangia vifo vya ghafla vya ngamia vilivyozidi kwa mbali vifo vyote vilivyowahi kushuhudiwa na wafugaji hapo awali. </s> |
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Idadi ya wanyama wanaokufa baada ya kuambukizwa ni ya juu katika maeneo yanayoshuhudia ugonjwa huo kwa mara ya kwanza. </s> |
<s>[INST] Usambaaji [/INST] Ingawa ugonjwa huu unapatikana katika kaunti zote, kaunti ya Marsabit ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuripoti kisa cha kwanza cha ugonjwa huu wa maji kwenye moyo. </s> |
<s>[INST] Kifo cha ghafla [/INST] Dalili za kukosa utulivu na uthabiti kama vile kushindwa kutembea vizuri, kuchomoza ulimi nje, kuinua miguu juu zaidi wakati wa kutembea, kujizungusha na mwili kutetemeka. </s> |
<s>[INST] Wanyama waliokufa/Mizoga [/INST] Maji mengi yenye rangi kwenye moyo, sehemu inayohifadhi moyo na kwenye chemba ya tumbo (abdominal cavity) </s> |
<s>[INST] Magonjwa yanayosababisha mimba kuharibika [/INST] Magonjwa yanayohusiana na kuharibika kwa mimba kama vile Homa ya Rift Valley (RVF) na Ugonjwa wa Mimba Kutoka (Ugonjwa wa Maziwa na Nyama kwa binadamu) yameangaziwa katika sehemu hii. </s> |
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Mbu hupata virusi kutoka kwa mnyama mgonjwa anapomfyonza damu. Kisha husambaza virusi hivyo kwa mnyama asiye mgonjwa baadaye anapomfyonza damu mnyama mwingine. Watu huambukizwa ugonjwa huu kwa kugusa damu, majimaji ya mwili na sehemu nyingine za mwili wa mnyama aliyeambukizwa. </s> |
<s>[INST] Idadi ya wanyama wanaoambukizwa katika kundi [/INST] Homa ya Rift Valley huathiri wanyama wengi hasa baada ya msimu wa mvua nyingi na ya kipindi kirefu, ambapo mbu wengi huwa wanazaana na kukua. </s> |
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Ugonjwa huu unaweza kuua karibu asilimia 10 hadi 50 ya wanyama wenye umri mdogo. Wanyama waliokomaa wanaweza kuambukizwa lakini ni wachache (asilimia 10) ambao hufa. </s> |
<s>[INST] Hutokea hasa baada ya kunyesha kwa mvua kubwa na ya kipindi kirefu inayosababisha mafuriko [/INST] Visa vichache pia vinaweza kutokea nyakati za mvua ya kiwango cha kawaida, lakini visa hivi ni vigumu kutambuliwa. </s> |
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Njia kuu ya uambukizaji wa ugonjwa huu ni ulaji wa lishe au unywaji wa maji yaliyochafuliwa na vijusi/vitoto na uchafu mwingine kutoka kwa ng’ombe au ngamia walioambukizwa. Njia nyingine zinazoweza kuchangia hili ni kama vile dume aliyeambukizwa anapomtungisha mimba ngamia jike. Watu wanaweza kupata ugonjwa huo kutoka kwa wanyama walioambukizwa kupitia unywaji wa maziwa yasiyochemshwa, ulaji wa chakula kisichopikwa vizuri na kushika sehemu za mwili wa mnyama aliyeambukizwa. </s> |
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Idadi ndogo ya wanyama hufa kwa kuathiriwa na minyoo, ingawa ndama wanaoathiriwa na minyoo wanaweza kufa kuliko wanyama waliokomaa. </s> |
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Ulaji wa chakula kilichoambukizwa na viini vinavyosababisha tatizo hili kama vile rotavirus na bakteria wengine wanaosababisha mharo huo. Unywaji wa maziwa kupindukia pia husababisha kuhara. </s> |
<s>[INST] Idadi ya Vifo [/INST] Idadi ya vifo hutofautiana, na athari ya matibabu huwa hafifu. Kiwango cha vifo cha karibu asilimia 25 kimewahi kuripotiwa. </s> |
<s>[INST] Ndama kunyonya maziwa mengi kupindukia [/INST] Ndama wanaozaliwa na majike wachanga wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa huu kuliko wanaozaliwa na majike waliokomaa kiumri </s> |
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Bakteria wanaosababisha ugonjwa huu hubebwa kwenye pumzi ya wanyama walioambukizwa (kwa njia ya matone). Pia hubebwa kwenye mate, uchafu unaotoka mdomoni na puani, na kwenye kinyesi. </s> |
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Asilimia kubwa (hadi 80%) ya wanyama walioambukizwa hufa. Kifo kinaweza kutokea ghafla lakini wakati mwingine huwa kati ya siku 2 — 8 baada ya dalili za kwanza kuonekana. </s> |
<s>[INST] Usambaaji [/INST] Ugonjwa huu hutokea hasa katika msimu wa mvua, na wakati mwingine unahusishwa na unywaji wa maji ya mafuriko. Mara nyingi hutokea ghafla na kuua wanyama haraka. Unaathiri wanyama wanaoonekana kuwa na hali nzuri kiafya hasa walioanza kukomaa na ndama wanaoanza kula nyasi. </s> |
<s>[INST] Shingo iliyofura [/INST] Tezi (limfu) iliyofura na yenye uchungu hasa pembeni ndani ya mashavu na chini ya shingo (tezi au limfu ni kiungo kinachobeba majimaji yenye kinga ya mwili) </s> |
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Kimeta husababishwa na bakteria wanaoweza kuishi kwenye udongo kama viini kwa muda wa hadi miaka 60 na ni sugu au hustahimili joto jingi na ukame. Ugonjwa huu unaweza kuzuka katika maeneo ambayo wanyama hukusanyika, kwa mfano, mahali pa kunywa maji na pa kuramba udongo wa magadi. Mnyama huingiza bakteria hawa mwilini anapokula nyasi zilizo katika udongo wenye maambukizi. Watu wanaweza kupata kimeta kwa kugusana na mnyama au uchafu wake ulio na maambukizi moja kwa moja au vinginevyo. </s> |
<s>[INST] Wanyama waliokufa/mizoga [/INST] Usiwahi kumchinja mnyama aliyekufa kutokana na kimeta. Mzoga wake haujikazi (kushikamana au kukakamaa) kama inavyotarajiwa kwa mnyama mfu. </s> |
<s>[INST] Weka katika karantini/watenganishe wanyama wanaougua na wasiougua [/INST] Hakikisha mzoga wenye kimeta na vifaa vilivyoambukizwa vimezikwa vizuri kwenye shimo refu (futi sita) WEKA BANGO LENYE MAANDISHI ‘USIENDELEE KUNA HATARI’: USIPASUE MZOGA WA MNYAMA ALIYEKUFA KUTOKANA NA KIMETA. </s> |
<s>[INST] Idadi inayoathirika kwenye kundi [/INST] Kifo cha ghafla cha ngamia hutokea kwa wingi wakati wa mikurupuko ya maradhi ambayo huambukiza wanyama wengi kwa wakati mmoja </s> |
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Wanyama wachache kwenye kundi hufa, lakini huwa na athari kubwa ya kiuchumi kwa sababu vifo huwaathiri wanyama wenye thamani kubwa. </s> |
<s>[INST] Dalili kuu za ugonjwa huu [/INST] Kifo cha ghafla cha ngamia hutokea kwa kiwango kikubwa hasa miongoni mwa ngamia waliokomaa, wa kike wajawazito na wanaonyonyesha, madume ya kuzalisha na kubeba mizigo, wenye uzani mwingi na/au walio na afya nzuri. </s> |
<s>[INST] Kifo katika muda usiozidi saa moja baada ya kuanguka. [/INST] Hakuna dalili zinazoweza kutoa tahadhari kabla ya mnyama mgonjwa kuanguka. Wanyama kwenye kundi moja hufa mmoja mmoja kwa muda fulani kisha wanaacha. </s> |
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Maambukizi ya ugonjwa huu yanatokana na kugusana kwa wanyama walioathirika na wazima kiafya. Wanyama hawa wazima kiafya huwa kwenye hatari ya kuambukizwa ugonjwa huu wanapogusa vidonda vya wanyama walioambukizwa. Maambukizi haya mara nyingi hufanyika kupitia kwa majeraha yaliyo kwenye ngozi ya mnyama yaliyosababishwa na kuchubuka/kudungwa wakati akila nyasi ngumu au mimea yenye ncha kali. Virusi vya ugonjwa huu vinaweza kudumu kwenye vidonda hivyo kwa muda mrefu hasa katika misimu ya kiangazi. </s> |
<s>[INST] Idadi ya mifugo wanaoathiriwa kwenye kundi [/INST] Wengi wa wanyama hao hasa wachanga huathirika. Maambukizi mapya baada ya kupona ni ya kawaida kwa sababu ugonjwa huu haujengi kinga thabiti mwilini. </s> |
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Ugonjwa huu kwa kawaida hauui bali majeraha yanayotokea kwenye midomo yanaweza kuwazuia kula hasa wanyama wachanga. Vidonda hivi pia vinaweza kupata viini na kuzua maambukizi hatari zaidi yanayoweza kusababisha kifo. </s> |
<s>[INST] Vidonda hivyo hutokea kwenye mdomo na wakati mwingine kwenye pua. [/INST] Vidonda hivyo hugeuka kuwa upele mbaya kwenye mdomo na wakati mwingine husambaa hadi ndani ya mdomo, sehemu ya chini ya miguu, na hata kwenye matiti ya mnyama anayenyonyesha. </s> |
<s>[INST] Dalili nyingine [/INST] Ugonjwa huu mara nyingi hudumu kwa wiki nne hadi sita kisha baadaye mnyama huyo huanza kupona polepole. </s> |
<s>[INST] Safisha maboma ya wanyama kwa dawa za kuua viini [/INST] Osha mikono kwa sabuni baada ya kushika vidonda vya ugonjwa huu kwa sababu virusi hivyo vinaweza kumshika binadamu. </s> |
<s>[INST] Mifugo wengine wanaoathiriwa [/INST] Ng'ombe, kondoo, na mbuzi ingawa panaweza kuwapo tofauti za aina ya vimelea vinavyoambukiza kila jamii ya mnyama. </s> |
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Ngamia wanaweza kuambukizwa ugonjwa huu kupitia kwa mbung'o au nzi wanaouma yaani pange/kipanga walio na viini (pange au kipanga wanajulikana kisayansi kama Tabanids au Stomoxys) </s> |
<s>[INST] Idadi ya wanyama wanaoathirika kwenye kundi [/INST] Hadi thuluthi moja (yaani mmoja kati ya watatu) ya ngamia wanaweza kuambukizwa ugonjwa huu kwenye kundi lakini idadi hii hutofautiana zaidi kutegemea idadi ya mbung'o na nzi wa kuuma walio katika eneo hilo. </s> |
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Karibu ngamia wote walio na ugonjwa huu hufa ikiwa hawatatibiwa. Huwa wanaugua kwa muda mrefu. Kwa kawaida, karibu asilimia 3 hivi ya ngamia hufa kutokana na ugonjwa huu. </s> |
<s>[INST] Usambaaji [/INST] Ugonjwa huu unapatikana katika maeneo yote ambayo yana mbung'o. Nzi wanaouma huongeza hatari katika eneo hilo, hasa ikiwa kuna mnyama aliye na ugonjwa huo mwilini. </s> |
<s>[INST] Wanyama waliokufa/mizoga [/INST] Wanyama waliokufa huwa wamedhoofika sana. Ugonjwa huu hausababishi vidonda kwenye viungo vya ndani ya mwili. </s> |
<s>[INST] Kinga [/INST] Angamiza mbung'o na nzi wanaouma kwa kutumia dawa za kuua wadudu, kama ulivyoagizwa na afisa wa tiba ya mifugo. </s> |
<s>[INST] Mbuzi na twiga. [/INST] Picha 7.2.1 Hatua ya awali ya ugonjwa wa kupinda shingo isiyokuwa hatari Picha 7.2.2 Hatua hatari ya ugonjwa wa kupinda shingo kwa ngamia </s> |
<s>[INST] Mradi wa Kuzidisha Ubora wa Chakula cha Siku zijazo (AVCD) nchini Kenya-Kitengo cha Mifugo [/INST] Mwongozo wa Nyanjani wa magonjwa ya mifugo kwa kutegemea dalili zao katika maeneo ya Kaskazini mwa Kenya </s> |
<s>[INST] Dibaji [/INST] Ufugaji ni mbinu kuu ya kujipa riziki miongoni mwa jamii za wafugaji katika ukanda wote wa Kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika. Jamii hizi nchini Kenya huishi katika kanda za malisho ya mifugo ambazo hupata huduma duni sana za tiba ya mifugo na miundomsingi hafifu inayohitajika kwa ufugaji bora wa mifugo na biashara yao. Kadhalika, mitindo ya maisha inayofuatwa eneo hili kama vile ufugaji wa kuhamahama, uhamaji wa kila msimu na mifumo mseto ya kilimo, yaani, ufugaji na ukuzaji wa mazao, kwa pamoja, huimarisha mwingiliano baina ya wenyeji, mifugo yao na wanyama-pori. Uhusiano huu, mbali na kuchangia katika kuzuka kwa migogoro baina ya binadamu au mifugo na wanyama-pori, pia huchangia katika uambukizanaji wa viini vya magonjwa ya aina nyingi miongoni mwao. Tafiti za hivi majuzi zaidi katika ukanda wa kaskazini mwa Kenya zilidhihirisha uwepo mkubwa wa viini vya kila mara vya magonjwa ya kieneo pamoja na kuibua ushahidi wa kina wa uzukaji na uibukaji mpya wa viini vya maradhi yanayoathiri mfumo wa kupumua ya Mashariki ya Kati, virusi vya Korona, virusi vya Homa ya Rift Valley (RVF), homa ya Q n.k. Kwa hivyo, matumizi ya dawa za tiba ya mifugo katika maeneo hayo yameongezeka kila kukicha katika juhudi za wafugaji hao kukabiliana na matatizo ya kiafya ya wanyama wao. Kutokana na changamoto hizi za kipekee katika maeneo kame nchini Kenya, jitihada nyingi zimetekelezwa ili kuzidisha ufuatiliaji na ukabilianaji na magonjwa haya. Jitihada hizo hufanikishwa kupitia kwa harakati za uhamasishaji wa jamii na ukumbatiaji wa mifumo bora ya kuripoti matukio, inayochangia mafanikio ya viwango mbalimbali. Takwimu kuhusu utokeaji wa magonjwa haya mashinani hufuatiliwa na kurekodiwa na maafisa wa nyanjani wa afya ya mifugo wanaoshirikiana na watoaji taarifa za magonjwa katika kiwango cha kijamii. Mfumo huu huwa unafaulu zaidi unapotekelezwa kama mradi wa kukabiliana na magonjwa makuu ya mkurupuko yanayoweza kubainishwa ambayo hutokea katika eneo kubwa, lakini ufanisi wake hauwi mkubwa iwapo unahusu aina nyingi za magonjwa ya kieneo ambayo hasa husababisha hasara kubwa ya uzalishaji katika eneo lililoathiriwa. Mwongozo huu unakusudiwa kuzidisha maarifa kuhusu magonjwa na mbinu za kuyadhibiti miongoni mwa wafugaji wa kieneo, watoaji wa taarifa za magonjwa katika jamii, matabibu/wahudumu wa kibinafsi wa afya ya mifugo, wauzaji wa dawa, wafanyabiashara na wadau wengine husika. Lengo hapa ni kuimarisha ufanisi wa juhudi za kukabiliana na kufuatilia magonjwa, zinazobuniwa na Idara ya Huduma za Afya ya Mifugo. Muundo wa Mwongozo huu unafanana na wa Mwongozo wa Nyanjani wa Magonjwa ya Wanyama unaotegemea Dalili (yaani A Field Manual of Animal Diseases by Syndromes) uliochapishwa mwaka wa 2013 na Mradi wa Viwango, Mbinu na Taratibu za Afya ya Wanyama (Standards Methods and Procedures in Animal Health -SMP-AH) kama mkakati wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani katika Ukanda wa Afrika Mashariki, Ofisi ya Umoja wa Afrika, Interafrican, kuhusu Rasilimali za Wanyama, Idara ya Marekani ya Kitengo cha Kigeni cha Kilimo, kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Georgia, Athens nchini Georgia. Maboresho muhimu kutokana na toleo la SMP-AH yalijumuisha (i) kuangazia ng'ombe, kondoo, mbuzi na ngamia wanaofugwa katika eneo lengwa, (ii) magonjwa mbalimbali pamoja na magonjwa yanayovuka mipaka ya kimaeneo ambayo mwongozo wa awali uliangazia, (iii) mbinu zinazoweza kutumika kudhibiti kila aina ya ugonjwa, na (iv) kutafsiriwa katika lugha za wenyeji ili kuwawezesha wengi kuusoma katika ngazi ya kieneo. Dalili kuu za ugonjwa na viungo vya wanyama vilivyobainika kuathiriwa, pia vimechapishwa kwenye picha/michoro. Mwongozo huu ni nakala inayoweza kuboreshwa hatua kwa hatua kulingana na michango ya wahusika mbalimbali watakaohusishwa. </s> |
<s>[INST] Utaratibu [/INST] Mwongozo huu unaangazia magonjwa ya ng'ombe. Magonjwa haya yameainishwa katika makundi tisa kulingana na dalili kuu ambazo magonjwa hayo yanaonyesha, kwa mfano: kupumua, maambukizi ya ngozi/uvamizi wa viini, vidonda vya miguu na midomo, ukosefu wa utulivu, mimba kutoka, mharo/kuendesha, ugonjwa wa kuvuja damu ghafla, mkojo mwekundu na magonjwa mengine ya kieneo. Mada zinazozungumziwa chini ya kila magonjwa hayo zinajumuisha, majina ya wenyeji, mifugo iliyoathirika, uambukizaji, idadi ya wanyama walioathirika kwenye kundi, idadi ya vifo, msambao, dalili za ugonjwa, dalili za magonjwa katika wanyama wafu (uchunguzi wa mizoga) na kinga. </s> |
<s>[INST] Shukrani [/INST] Watu wengi walichangia katika utayarishaji wa mwongozo huu; wanajumuisha maafisa wa afya ya mifugo na maafisa wengineo katika Kaunti za Turkana, Marsabit, Isiolo, Garissa na Wajir; walioshiriki katika vikao vya mafunzo: Michael Baariu, Dabasso Barako, Changayo Orkhobeshe, Ehele Haile, Stephen Mutahi, Boku. Bodha, Adano Umuro, Dennis Mwongela, Joseph Muriira, John Koskei, Siyat Onle Takal, Abubakar Siraj, Job Ronoh, Jane Akale, Daud Abukar na Anthony Ngugi. Dk Joseph Mathooko wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Kilimo na Chakula pia alishiriki. Waandishi hawa mahiri pia wanatambua mchango wa Maafisa Waratibu wa Nyanjani wa AVCD LVC (Haret A. Hambe (Garissa), Adan A. Kutu (Isiolo), Abdisemed Osman (Wajir), Simon Chuchu (Marsabit) na Viola Chemis (Turkana)) katika kaunti zinazolengwa, ambao waliboresha mwongozo huu, kwa kujumuisha maoni yaliyotolewa na maafisa wa kwanza wa nyanjani katika kaunti, watoaji wa ripoti za magonjwa katika ngazi ya kijamii na wafugaji katika ngazi ya kijiji. </s> |
<s>[INST] Marejeleo [/INST] Bett, B., Kihu, S., Kiara, H. and Wamwere-Njoroge, G. 2018. Field manual for livestock diseases based on syndromes in pastoral areas in northern Kenya: Cattle diseases. Accelerated Value Chain Program (AVCD) program-Livestock Value Chain Component, Nairobi, Kenya: ILRI. </s> |
<s>[INST] Magonjwa yanayobainika kwa namna ya kupumua [/INST] Magonjwa yaliyoangaziwa katika sehemu hii ni yale ambayo dalili zake kuu hugunduliwa kwa kuangalia jinsi mnyama anavyopumua. Maradhi hayo yanajumuisha Homa ya Mapafu na Ndigana Kali almaarufu East Coast Fever (ECF). </s> |
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Ng'ombe walio katika hatari ya kupata ugonjwa huu, huambukizwa kwa kuvuta ndani ya mwili pumzi kutoka kwa mnyama aliyeathirika. Pia ugonjwa huu unaweza kuambukiza kupitia matone ya mkojo kutoka kwa mnyama anayeugua. Maambukizi hayo yanaweza kutokea hata ikiwa ng’ombe asiye mgonjwa yuko mita 20 hadi 200 kutoka kwa yule aliyeathirika. Mchoro 1: Kielelezo cha jinsi homa ya CBPP inavyosambazwa — mnyama aliyeathirika na ugonjwa wa CBPP husambaza kiini cha ugonjwa huo kupitia kwa matone ya pumzi yanayomtoka anapokohoa (mchoro wa kushoto). Mnyama mzima kiafya au dhaifu anapovuta ndani matone hayo, huambukizwa na kuendeleza ugonjwa huo (mchoro wa kulia). </s> |
<s>[INST] Idadi inayoathirika kwenye kundi [/INST] Katika maeneo ambayo hayajawahi kushuhudia ugonjwa huu, hadi asilimia (%) 100 ya wanyama huathirika. Katika maeneo ambayo hushuhudia ugonjwa huu mara kwa mara, kati ya 10%—%60 huathirika. </s> |
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Katika maeneo ambayo hayajawahi kushuhudia maambukizi haya, ugonjwa huu huua zaidi ya 50% ya wanyama. Katika maeneo ambayo maambukizi hutokea mara kwa mara, chini ya 10% ya wanyama hao ndio hufa kutokana na ugonjwa huu. </s> |
<s>[INST] Dalili kuu za ugonjwa huu [/INST] Mwili kujivuta nyuma kisha mbele anapopumua, pamoja na sauti ya kunguruma kutokana na maumivu —upumuaji wa juujuu na wa haraka </s> |
<s>[INST] Kikohozi kikavu anaporukaruka [/INST] Ng’ombe kupinda mgongo kwa juu akiwa amesimama, visugudi au viwiko vikiwa nje huku kichwa na shingo vimerefushwa </s> |
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Ugonjwa huu huambukizwa kupitia kwa kupe wa kahawia wa masikioni. Kupe hawa hubeba viini vya ugonjwa huu kutoka kwa mnyama aliyeambukizwa wanapomfyonza damu yake. Halafu kupe hao huambukiza mnyama anayefuatia wanapomnyonya/kufyonza damu.. Kupe hawa wanaweza kuishi na viini hivyo kwenye malisho kwa miaka miwili. Idadi kubwa ya mifugo inaweza kuathirika kulingana na wingi wa kupe hao walioambukizwa. Mchoro 1.5: Kielelezo cha jinsi ugonjwa wa ECF unavyoambukizwa—kupe wa kahawia wa masikioni hubeba viini vinavyosababisha ECF. Kupe hao hupata viini hivyo kutoka kwa wanyama aliyeambukizwa na kuvisambaza kwa wanyama wazima kiafya wanaponyonya damu yao. </s> |
<s>[INST] Idadi inayoathiriwa kwenye kundi [/INST] Inategemea idadi ya kupe walioambukizwa katika eneo hilo pamoja na afya ya mnyama. Miongoni mwa ng'ombe wa kiasili (Zebu, Borana), maambukizi yanaweza kufika 100%, lakini kwa kawaida vifo huwa vichache. Lakini kwa ng'ombe wa kigeni, vifo vinaweza kufika 100% ikiwa ugonjwa huo hautakabiliwa mapema. </s> |
<s>[INST] Magonjwa ya maambukizi na mavamizi ya ngozi kwa jumla [/INST] Sehemu hii inashughulikia magonjwa ambayo maambukizi au uvamizi wa ngozi ndio dalili kuu. Haya yanajumuisha Vinundu vya Ngozi na Upele Unaowasha/Ukurutu ambao huathiri kila aina ya mifugo. </s> |
<s>[INST] Ugonjwa huu husambazwa kupitia kwa angalau njia tatu kuu: [/INST] Wanyama wasio wagonjwa wanapogusana na walioathirika, wanapata viini vya ugonjwa huu hasa kupitia kwa mate. Nzi wa kuuma (pange/vipanga) na mbu wanaweza kupata viini kutoka kwa mnyama anayeugua wanapomfyonza damu na kuvihamisha hadi kwa wanyama wazima kiafya. Wanyama wazima wanaweza kupata ugonjwa huu kwa kunywa maji yaliyochanganyika na mate ya mnyama aliyeathirika. </s> |
<s>[INST] Idadi ya wanyama wanaoathiriwa [/INST] Hii hutofautiana sana, na hutegemea iwapo mnyama huyo aliwahi kuugua ugonjwa huo hapo awali au la. Kati ya asilimia 3-80 ya mifugo wanaweza kuambukizwa. </s> |
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Wanyama wachache hufa, mara nyingi chini ya 5% ya wale walioathirika. Ni nadra sana idadi ya vifo vya wanyama wanaoathirika kufika 20%. </s> |
<s>[INST] Zuia migusano kati ya mifugo wa makundi tofauti (k.m. katika maeneo ya kunywa maji, malishoni) [/INST] Epuka kutumia wanyama (ndume), vifaa, magari, na wafanyakazi kutoka mashamba mengine katika kipindi cha ugonjwa huu. </s> |
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Mnyama mzima hupata ugonjwa huu kwa kugusana na aliyeathirika, au iwapo ataegemea sehemu zilizotumiwa na wanyama wagonjwa kujisugua, na/au kulala katika maeneo yaliyotumiwa na mnyama anayeugua ugonjwa huu. Unasababishwa na vimelea ambacho hujipenyeza hadi ndani ya ngozi. Kiroboto hicho kinaweza kuishi kwa hadi wiki mbili ardhini. Mchoro 2.2: Jinsi Upele Unaowasha unavyotoka kwa wanyama walioathirika hadi kwa wazima kiafya. Kielelezo hiki kinaonyesha wanyama walioathiriwa wajisugua kwenye miti kisha kuacha chembe za ngozi zenye viini vya upele huo, vinavyoweza kuganda kwa wanyama wasiokuwa wagonjwa wanapoegemea miti hiyo. </s> |
<s>[INST] Idadi inayoathirika katika kundi [/INST] Kwa kutegemea unavyowalisha, kuwatunza na ubora wa mbinu za kuyadhibiti maradhi haya, ni hadi 20% ya wanyama katika kundi moja wanaoathiriwa. </s> |
<s>[INST] Epuka kuchanganya mifugo katika eneo la kuwanywesha maji na malishoni [/INST] Watenge/kuwaweka katika karantini na kuwakagua kwa umakinifu wanyama wapya — tafuta usaidizi wa afisa wa tiba ya mifugo </s> |
<s>[INST] Magonjwa ya vidonda vya miguu na midomo [/INST] Sehemu hii inafafanua magonjwa yanayosababisha vidonda kwenye midomo na miguuni: ugonjwa huu huathiri wanyama wote wenye kwato zenye mwanya katikati, na mwozo wa miguu hasakwato. </s> |
<s>[INST] Wanyama wengine wanaoathiriwa [/INST] Wanyama wote wenye kwato zenye mwanya huathiriwa na FMD. Mara nyingi ng’ombe huathirika zaidi kuliko kondoo na mbuzi. Nguruwe hunya virusi zaidi kuliko ng'ombe, kondoo au mbuzi lakini makali ya ugonjwa huo hutegemea aina ya virusi na uthabiti wa afya ya nguruwe hao. </s> |
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Wanyama wazima kiafya hupata ugonjwa huu wanapogusana na uchafu unaotoka mwilini, k.m. mate, mkojo, maziwa, kinyesi au mbegu za kiume/manii kutoka kwa wanyama walioathirika. Ugonjwa huu husambaa kwa kugusana na wanyama walioathirika, vitu vilivyoambukizwa (vifaa vilivyoambukizwa) au magari. Ugonjwa huu pia unaweza kuenezwa kupitia kwa hewa pale mnyama mzima anapovuta pumzi iliyotolewa na mnyama aliyeambukizwa. </s> |
<s>[INST] Idadi ya mifugo wanaoathirika katika kundi [/INST] Husambaa kwa kasi miongoni mwa wanyama walio katika hatari ya kupata ugonjwa/wadhaifu kiafya. Pia kuna uwezekano wa wanyama wote kwenye kundi kuathirika. </s> |
<s>[INST] Idadi ya vifo [/INST] Ugonjwa huu hauui sana wanyama waliokomaa kwa sababu wengi huwa na uwezo wa kupona. Wanyama wachache wachanga hufa kutokana na matatizo ya moyo. Ndama wenye umri wa chini ya miezi 3 wanaweza kufa zaidi. </s> |
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Kukaa kwenye unyevu kwa muda mrefu au kuumia mguuni huwezesha viini vinavyoishi hasa katika ngozi kuingia miguuni/kwatoni, hivyo basi kusababisha ugonjwa huu. </s> |
<s>[INST] Dalili za ugonjwa huu kwa wanyama waliokufa/mizoga [/INST] Uchelewaji wa matibabu unaweza kuzidisha maambukizi hadi kwenye mifupa ya ndani, tando laini za viungo, na kupunguza uwezekano wa kupona. </s> |
<s>[INST] Magonjwa yenye dalili za Kuhangaika [/INST] Sehemu hii inashughulikia magonjwa yenye dalili za kukosa utulivu kama vile kuzungukazunguka, kufinyilia kichwa mahali na kadhalika. Magonjwa makuu yanayoangaziwa hapa ni Maji kujaa kwenye Moyo na Kichaa cha Mbwa (T9), ambayo huathiri aina nyingi za mifugo. </s> |
<s>[INST] Uambukizaji [/INST] Viini vinavyosababisha ugonjwa huu husambazwa na kupe, hasa kupe wa Kusini mwa Afrika (bont-. Kupe hubeba bakteria wa ugonjwa huu wanapowafyonza/kunyonya damu wanyama walioambukizwa. Bakteria hawa hukua zaidi kwenye kupe hao na kuambukiza mnyama asiyeugua wakati kupe huyo anapomnyonya damu. </s> |
End of preview. Expand
in Dataset Viewer.
README.md exists but content is empty.
Use the Edit dataset card button to edit it.
- Downloads last month
- 39