content
stringlengths
1
17.8k
category
stringclasses
5 values
label
int64
0
4
WADAU wa bandari kutoka Afrika na baadhi ya nchi za Bara la Ulaya wamekutana jijini Dar es Salaam kujadiliana kuhusu masuala yanayohusu bandari zikiwemo fursa za kiuchumi za uendelezaji wa bandari hizo.Mkutano huo wa tatu ujulikanao kama ‘Utanuzi wa Bandari Afrika’ pamoja na kujadili masuala yanayohusu upanuzi wa bandari, pia unahusisha miradi mingine ya maendeleo ya ujenzi wa barabara kuu, madaraja inayoendelea kufanywa katika nchi za Afrika.Akizungumza baada ya ufunguzi wa mkutano huo, Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Fransisca Muindi alisema mkutano huo pamoja na mambo mengine, utatoa nafasi kwa wadau hao kutumia fursa za bandari ya Dar es Salaam na kuitumia.Muindi alisema mkutano huo pia utatumika kuitambulisha bandari hiyo hususani kuhusu upanuzi unaoendelea kufanywa na serikali ukihusisha mipango iliyopo ya kupunguza mizigo bandarini na kuipeleka katika bandari kavu zilizopo na zinazoendelea kujengwa, hatua aliyosema itasaidia kuongeza ufanisi wa bandari hiyo.“Kupitia mkutano huu tunaamini nchi yetu itazidi kujiweka katika nafasi nzuri ya kukua kiuchumi ikizingatiwa kuwa sekta ya bandari hapa nchini kwa sasa inazidi kupata msukumo wa kipekee unaoendana na mipango ya serikali kukuza uchumi wake,” alisema Muindi.Aidha, alisema Tanzania kwa sasa inazidi kupiga hatua kubwa katika sekta hiyo ya bandari ikijiandaa kuziunganisha nchi ya Rwanda kupitia ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ambao unaoendelea kwa awamu tofauti kuanzia Dar es Salaam kwenda Dodoma, baadaye Mwanza na Kigoma kisha kuifikia Rwanda kupitia Isaka.Katika hatua nyingine, mkurugenzi huyo alisema ipo mipango inayoendelea chini ya serikali kupitia TPA kuwezesha mizigo inayokwenda na kutoka Rwanda kutumia bandari ya Dar es Salaam kama zamani.
Biashara
1
KOCHA wa zamani wa timu ya Soka ya Taifa,Taifa Stars Dk. Mshindo Msolla amemshauri kocha wa timu hiyo Emmanuel Amunike kufanya kazi kwa uhuru hususani kwenye uteuzi wa kikosi kinachoenda kuiwakilisha nchi kwenye michuano mikubwa.Msolla ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache zimepita baada ya Amunike kuteua kikosi cha wachezaji 31 tayari kwa maandalizi ya michuano ya Afcon inayotarajiwa kufanyika Misri mwezi ujao. Akizungumza na gazeti hili jana, Dk. Msolla alisema kuifunga timu ya Uganda sio kwamba timu hiyo imekamilika kwani bado kikosi hicho kina mapungufu makubwa ya kiufundi yanayohitajika kuyafanyia kazi kabla ya kuingia kwenye michuano hiyo mikubwa.“Tukichukulia kwamba tumeifunga Uganda basi kila kitu tumemaliza tukienda Misri tutaendelea kulitia taifa aibu , nivema benchi la ufundi lifanye kazi ya kuijenga timu kwa kuaandaa mipango ya haraka kuisaidia,”alisema.Aidha Msolla alisema kwenye uteuzi wa wachezaji ni vema akawashirikisha na makocha wengine wamsaidie kwa kuwa nchi inamakocha wengi ambao wanaweza kumsaidia kuibua wachezaji wengine wenye vipaji walio maeneo mbalimbali na wanaweza kuisaidia timu kulikokuendelea kuchagua walewale kwakuwa lengo ni kujenga sio kubomoa “ Mimi ni mfano hai nilipokuwa kocha timu hiyo niliwashirikisha makocha mbalimbali akiwemo Charles Mkwasa kuifundisha timu, lakini hadi sasa siamini kama kweli kikosi kile anateua mwenyewe ninawasiswasi na watu wanaomzunguka wanafanya kazi hiyo jambo ambalo ni hatari,” alisema.
Kitaifa
0
HOSPITALI ya Rufaa ya taifa ya Mirembe haikujengwa mkoani Dodoma kutokana na mkoa huo kuwa na wagonjwa wengi wa akili (vichaa) bali kuwepo kwa gereza la Isanga ambalo wanafungwa wahalifu wakubwa na wauaji wanaotakiwa kupimwa akili zao.Naibu Waziri wa Afya, Maendelelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile alitoa kauli hiyo baada ya Spika Job Ndugai kutaka kujua kama hospitali hiyo ya kutibu wagonjwa wa akili ilijengwa hapo kufuatia Dodoma kuwa na wagonjwa wengi wa akili.Dk Ndugulile alisema hospitali hiyo ilijengwa hapo kutokana na Dodoma kuwa na gereza la Isanga lenye wafungwa wa mauaji na wahalifu wakubwa ambao hutakiwa kupimwa akili zao.Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM) aliyetaka kujua kwa nini dawa za kifafa na ugonjwa wa akili wilayani Ulanga mgao wake ni kidogo wakati wilaya hiyo inaongoza nchini kwa kuwa na wagonjwa wengi wa maradhi hayo. Dk Ndugulile alisema ni kweli Morogoro hasa wilaya ya Ulanga kuna wagonjwa wengi wa kifafa na akili, lakini atafuatilia kujua kwa nini dawa hizo hazifiki huko wakati zipo za kutosha.Akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Njombe Mjini, Edward Mwalongo (CCM) aliyetaka kujua serikali inajipangaje kuwatibu, kuwapa mavazi na makazi wagonjwa wa akili mitaani. Dk Ndugulile alisema wizara inaendelea kuimarisha huduma za afya nchini ikiwemo huduma ya afya ya akili. Uimarishaji huo wa huduma ya afya ya akili unakwenda hadi ngazi ya afya ya msingi ambako ndiko jamii ilipo.“Pamoja na kuongezeka kwa wagonjwa wa akili wanaorandaranda barabarani, sheria ya afya ya akili ya mwaka 2008 inawataka ndugu na jamii kuibua wagonjwa wa akili na kuwapeleka vituo vya kutolea huduma wapewe tiba,” alisema. Alisema wagonjwa wakipata nafuu, huruhiswa kukaa na familia zao na jamaa zao. Jukumu la kwanza la kulinda afya ya jamii huanzia ngazi ya familia, lakini jamii zinawanyanyapaa, kuwabagua, kuwatenga hivyo kuranda mitaani.
Kitaifa
0
KAMATI ya Kudumu ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, imeipongeza kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) kwa kuja na mbinu mpya za kujiendesha kibiashara.Kwa sasa kampuni hiyo inayozalisha magazeti ya HabariLEO, Daily News na SpotiLeo, imekuja na miradi mipya ikiwamo kuwa na shirika la habari (news agency) litakaloandaa habari na kuziuza kwa vyombo vingine vya habari ndani nan je ya nchi.Pamoja na hayo, kampuni hiyo ya TSN imekuja na mradi wa uchapishaji kidigitali, kuwa mshauri wa masuala ya habari, kupiga picha kibiashara na kutengeneza dokumentari.Akizungumza wakati wa ziara ya kamati hiyo kwa kampuni ya TSN jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Musa Foum Musa, alisema ubunifu huo wa TSN utaiwezesha kampuni hiyo kujiongezea mapato, lakini pia kufikia lengo la kuwahabarisha Watanzania habari kutoka maeneo mbalimbali ikiwamo vijijini.“Tunaomba tu hii miradi mingine mnayofikiria kuianzisha muanze kuitekeleza haraka ili kama kuna watu wanaotaka hata kuwaiga ikiwamo sisi Zanzibar tuwaige. Maana hata wahenga walisema chema chajiuza,” alisema.Kaimu Meneja wa kiwanda cha uchapishaji cha TSN, Boniface Mwajombe, akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mhariri Mtendaji wa kampuni hiyo, Tuma Abdallah, alisema mipango na mikakati hiyo ina lenga kukuza kipato cha kampuni hiyo, lakini pia kuwa chombo bora na cha kuaminika cha habari nchini.“Vision (dira) ya kampuni yetu ni kuwa chombo kinachokubalika na kuaminika nchini. Tunataka TSN iwe mouth piece (mdomo) wa serikali, kuelezea sera za serikali, kuwawezesha wananchi kupata habari kuhusu nini serikali yao inafanya na kuchukua mawazo ya wananchi na kuyachapisha kwenye vyombo vyetu vya habari,” alisema.Mwajombe alisema TSN ina amini katika kasi na teknolojia kutokana na mabadiliko ya duniani, ubunifu wa miradi mipya na kutumia njia rahisi kufanya biashara na kufikia masoko na umma ili wateja na wadau wapate bidhaa zenye ubora na kwa muda muafaka.Ametoa mfano namna TSN ilivyomuinua mwanafunzi wa Simiyu, aliyefanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha nne licha ya kusoma katika mazingira duni, hali iliyosababisha sasa kijana huyo kupata misaada mbalimbali ikiwamo kuendelezwa kielimu na wazazi wake kujengewa nyumba na wadau mbalimbali.“Katika eneo la ubunifu, TSN inataka kuwa shirika la habari, mradi wa uchapishaji ikiwamo uchapishaji wa kidijitali, huduma ya ushauri, kupigapicha kibiashara na kuziuza kwa wateja na kutengeneza dokomentari.”“Katika eneo hili la dokomentari tunawakaribisha wabunge na wawakilishi kupitia mradi wetu wa jimbo kwa jimbo hasa kipindi hiki cha uchaguzi. Hii ni fursa ya kuitumia ili watu wajue kiongozi wao amefanya nini kipindi chote cha uongozi wake,” alisema.Mwanjombe alieleza namna kampuni hiyo ya magazeti ya serikali inavyoshirikiana na Wakala wa Uchapaji ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Shirika la Magazeti ya Serikali (SMS).Alisema ushirikiano huo ulianza zamani kwani wamekuwa wakishirikiana kitaaluma, ambapo wamekuwa wakibadilishana ujuzi, lakini pia kwa TSN imekuwa ikichapisha gazeti la Zanzibar Leo.“Mara ya mwisho kuchapisha Zanzibar Leo ilikuwa mwaka 2016 lakini kwa bahati mbaya tulikuwa tunadai zaidi ya Sh milioni 300, lakini walipunguza hadi kufikia Sh milioni 289, tunaomba wapunguze angalau Sh milioni 10 au 20 kila mwezi,” alisema.Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Saleh Mneno, alikiri kufahamu deni hilo na kuahidi kukutanisha pande zote mbili TSN na SMS ili kuangalia namna ya kulilipa.
Biashara
1
WASOMI wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) wakishirikiana na Umoja wa maveterani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamemuomba Rais John Magufuli kuruhusu lugha ya Kiswahili kutumika kufundishia elimu ya sekondari nchini.Wasomi hao wakiongozwa na Profesa Aldin Mutembei walikutana jana Dar es Salaam na uongozi wa umoja huo uliongozwa na Mwenyekiti wake, Kapteni Mohamed Ligola. Akizungumzia jinsi walivyojipanga kufanikisha malengo hayo ya kutumia Kiswahili kufundishia nchini, Mutembei alibainisha kuwa wameanza kwa kutunga vitabu vya kufundishia kidato cha kwanza.Alivitaja vitabu hivyo kuwa ni vya siasa, fizikia, kemia, hisabati, kilimo na vingine huku akibainisha vikiruhusiwa kufundishia kidato hicho cha kwanza wawekezaji wengi watajitokeza na kuwawezesha kutunga vitabu vya kidato cha pili na kuendelea hadi vya vyuo vikuu.Alisema, tangu mwaka 2015 walishatunga vitabu hivyo na wanachosubiria kwa sasa ni ruhusa ya kuanza kutumika kwake ili ichangie kuinua kiwango cha elimu nchini. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Walimu wa Hesabati nchini na Mhadhiri wa Hisabati UDSM, Saidi Sima aliyetunga kitabu cha hisabati kidato cha kwanza kwa Kiswahili, alisema matumizi ya lugha hiyo kufundishia itaongeza kiwango cha ufaulu nchini.Alisema, nchi itaendelea zaidi na kubainisha kuwa mwaka 1973 vitabu vya masomo mbalimbali vilivyokuwa kwa lugha ya kiingereza vilitafsiriwa kwa kiswahili na kuongeza kuwa ni muda mwafaka wa kurejesha lugha hiyo shuleni na vyuoni.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Veterani hao wa CCM, Ligola alibainisha, mchakato wa kuwasilisha mapendekezo hayo kwa Rais Magufuli ulishaanza na kuwa wana imani atafanyia kazi hoja hiyo. Alisema, Rais Magufuli amekuwa mstari wa mbele kuendeleza lugha ya Kiswahili na hasa kutokana na tabia yake ya kukipigania kwa kukizungumza kila mahala anapokuwapo.
Kitaifa
0
MITI 4,170,076 sawa na asilimia 73.4 kati ya mti 5,356,887 iliyopandwa kati ya mwaka 2017 na 2018 mkoani Lindi imepona na kuendelea kukua.Taarifa hiyo imetolewa na Ofi sa Maliasili na Mazingira wa Mkoa wa Lindi, Zawadi Jilala wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji miti kimkoa iliyofanyika wilayani Kilwa. Jilala alisema katika taarifa yake hiyo kwamba lengo la kupanda miti kwa miaka hiyo lilikuwa 7,500,000 hivyo miti iliyopandwa 5,356,887 ni na asilimia 71.3 ya lengo.Katika hafla hiyo iliyofanyika shule ya sekondari ya kutwa ya Kilwa ambapo miti 600 ilipandwa katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi aliwataka watendaji wakuu wote wa halmashauri sita za mkoa huo kuhakikisha kwamba shughuli ya upandaji miti ni endelevu na wala si la matukio.Alisema Mkoa wa Lindi wenye jumla ya kilometa 67,855.32 sawa na hekta 6,785,532 ambazo kati ya hizo hekta 5,238,431 sawa na asilimia 77.2 ya eneo la mkoa zimefunikwa na uoto wa asili ambao ni misitu na mapori, ni lazima kukazana kupanda miti ili kuendelea kuwa na hali njema.Zambi alisema mapinduzi ya viwanda yanawezekana kwa kuhifadhi mazingira na kuhakikisha uvunaji wake unakwenda kwa mujibu wa taratibu. “Ingawa mkoa una misitu isiyoingiliwa sana na kuharibiwa sana ukilinganisha na mikoa mingine, ipo haja ya kuhakikisha rasilimali hizi haziharibiwi,” alisema mkuu wa mkoa katika hotuba iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai.Mkoa wa Lindi una msitu ya hifadhi isiyopungua hekta 829,510.5 ambayo imehifadhiwa kisheria. Miongoni ma misitu hiyo kuna msitu ya hifadhi ya taifa hekta 370,504, misitu ya hifadhi ya vijiji hekta 453,283.5;misitu ya mikoko hekta 44,038 na misitu ya kupandwa hekta 3,000. Misitu ya hifadhi ya vijiji mingi ipo katika Mradi wa usimamizi shirikishi wa misitu (PFM) ambao umewezeshwa na Shirika la kuendeleza na kuhifadhi Mpingo (MCDI) chini ya ufadhili wa WWF.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Abuu Mjaka alisisitiza haja ya upandaji wa miti kuwa endelevu kwa kuwa kila kitu anachohitaji binadamu msingi wake mkubwa ni miti na misitu. Mtendaji wa zamani wa misitu na Mwenyekiti wa bodi ya MCDI, Dk Felician Kilahama aliwataka wanamuziki kuhamasisha upandaji wa miti kupitia muziki ambao upo katika kila basi la abiria. Aidha Kaimu katibu tawala mkoa wa Lindi Dk Bora Haule alitaka kuwepo na kanzidata ya miti iliyopandwa na kupona.
Kitaifa
0
Mgomo huo ulileta tafrani kati ya uongozi wa TRA jijini Mwanza na Meya wa Manispaa ya Ilemela, Henry Matata na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao kwa pamoja waliwaunga mkono wafanyabiashara kugomea mashine hizo.Wafanyabiashara hao waliamua kutofungua maduka yao, wakipinga kulazimishwa kununua mashine wanazodai zinauzwa kwa bei kubwa kati ya Sh 600,000 na Sh 800,000.Mbali na kufunga maduka yao, wafanyabiashara hao walikuwa wamepanga kuandamana kwenda katika ofisi za Mamlaka ya Mapato majira ya saa mbili asubuhi, lakini maandamano yao yalizuiwa na Polisi .Ulinzi uliimarishwa jijini kuhakikisha hakuna mikusanyiko yoyote ya makundi ya watu.Akizungumza ofisini kwake, Meneja TRA Mkoa wa Mwanza, Jeremiah Lusana alisema mashine hizo lazima zitumiwe na wafanyabiashara ili kuepuka taifa kupoteza muda na mapato.
Biashara
1
MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba jana walilipa kisasi baada ya kuifunga Mashujaa ya Kigoma kwa bao 1-0 katika mchezo wa kirafi ki uliofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.Ushindi huo wa Simba ni sawa na kulipa kisasi baada ya vigogo hao wa soka nchini kufungwa 3-2 na kutolewa katika michuano ya Kombe la Shirikisho na timu hiyo ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam msimu uliopita.Katika mchezo huo ulioshuhudiwa na watazamaji wengi kwenye uwanja huo, bao hilo pekee la Simba lilifungwa katika dakika ya 56 na mchezaji wa kimataifa wa Sudan, Sharaf Shaiboub aliyeunganisha mpira wa pasi ndefu ulipigwa na kiungo wa kati Said Ndemla.Aidha, huo ni ushindi wa pili mfululizo kwa Simba baada ya juzi kuibuka na ushindi kama huo kwenye mechi nyingine ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Bandari FC ya Kenya kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Katika mchezo mwingine wa kirafiki jana, Azam FC ilifunga African Lyon kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi, huku mabao yake yakifungwa na Iddi Kipagwile na Joseph Mahundi.Yanga nayo iliifunga Friends Rangers kwa mbaoa 4-3 katika mchezo wa mazoezi kwenye Uwanja wa Polisi Kurasini wakijiandaa kwa mechi ya mtoano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids ya Misri Oktoba 27 CCM Kirumba Mwanza.
michezo
2
WIZARA ya Fedha na Mipango imetoa orodha ya kwanza ya wadaiwa sugu wafanyabiashara 15 walionufaika na Mpango wa Kusaidia Uingizwaji wa Bidhaa nchini (CIS) na FACF, wafanyabiashara Mohamed Dewji na Yusuf Manji ni kati ya wadaiwa hao.Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na wizara hiyo, imewataka wadaiwa hao kulipa madeni yao haraka iwezekanavyo kabla hatua za kisheria kuchukuliwa. Watu wengine mashuhuri waliopo kwenye orodha hiyo ni pamoja na mwanasiasa aliyekuwa Waziri kwenye utawala uliopita, Stephen Wassira kupitia kampuni yake ya Siza Cold Storage Co. Ltd pia mwanasiasa Hashim Rungwe kupitia kampuni yake ya Bahari Motor Co. Ltd.Ikizungumzia madeni hayo, taarifa hiyo ilifafanua kuwa yanatokana na mkopo wa masharti nafuu kwa Taasisi, Kampuni, Viwanda na Wafanyabiashara ambapo wakopaji walitakiwa kulipa deni husika bila ya kutozwa riba katika kipindi cha miezi 18 tangu muda waliopewa mikopo hiyo.Ilinukuu kifungu cha sheria cha CIS ya mwaka 2008 (1)(b), inayosema kuwa mkopaji akichelewa kulipa katika kipindi cha miezi 18 tangu kupatiwa mkopo, atapaswa kulipa riba ya asilimia sawa na kiwango kinachotozwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inapoikopesha serikali katika kipindi husika. Ilielezea kuwa zaidi ya kampuni 980 zimekopeshwa chini ya utaratibu huo ambapo tangazo hilo lililotolewa jana lilikuwa ni la mara ya mwisho kwa kuwa imeshatangaza mara kwa mara na wadaiwa wameshindwa kuitikia mwito.Ilisema matangazo yalitolewa mnamo Desemba 30 mwaka 2015 na Aprili 4 mwaka jana, lakini hakuna jitihada za ulipaji wa madeni hayo zilizofanyika. Ilielezea kuwa wadaiwa ambao majina yao yametajwa jana kwa hiyo mara ya mwisho wakishindwa kujitokeza na kulipa hatua za kisheria zitachukuliwa. Kwa upande wa mfanyabiashara Mohamed Dewji anadaiwa kupitia kampuni zake za 21st Century Textiles na Afritex Ltd huku Manji akidaiwa kupitia kampuni zake za Farm Equipment Tanzania Ltd, Quality Group Ltd, Dunhill Motors Ltd, Quality Seed Ltd, Quality Garage Ltd.
Kitaifa
0
RAIS John Magufuli leo anatarajiwa kupokea Mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano (TTMS) katika Viwanja vya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) jijini Dar es Salaam.Mfumo huo uliofungwa na Kampuni ya Société Générale De Surveillance and Global Voice Group (SGC/GVB) ya Uswizi, ulizinduliwa Februari 2014 na unatakiwa kuhamishiwa TCRA kwa udhibiti kamili baada ya miaka mitano.Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba alivieleza vyombo vya habari Dar es Salaam jana lengo la mfumo huo ni kufuatilia ubora wa huduma za makampuni ya simu za mkononi nchini na kudhibiti mapato ya kodi.Kilaba alisema mfumo huo, umekuwa ukifanya kazi tangu Oktoba 2013 na umeonesha matokeo mazuri, kuiwezesha TCRA kupata takwimu sahihi za mawasiliano ya ndani na ya kimataifa.“Kupitia mfumo huu, tumegundua udanganyifu, takwimu za miamala ya fedha ya simu za mkononi na ubora wa huduma zinazotolewa na kampuni ya simu za mkononi,”alieleza Kilaba.
Kitaifa
0
UBALOZI wa Tanzania nchini Ujerumani umesikitishwa na kitendo cha Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kutoa tuhuma nzito dhidi ya Rais John Magufuli na serikali kuhusu ufi nyu wa demokrasia nchini.Kwa mujibu wa ubalozi huo, kitendo anachoendelea kukifanya mbunge huyo cha ziara za vyombo vya habari katika nchi mbalimbali duniani, kinaonesha ameshapona na anahitaji kurejea nchini Tanzania, kuendelea na majukumu yake kama mbunge.Katika taarifa yake aliyotoa kwa vyombo vya habari, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dk Abdallah Posi , amesema ubalozi huo umesikitishwa na tuhuma alizotoa mbunge huyo dhidi ya serikali ya Tanzania katika mahojiano yake na Kituo cha Televisheni cha DW.Amesema tuhuma nyingi anazotoa Lissu ikiwemo kushambuliwa kwake na ukosefu wa demokrasia hazina ukweli, zaidi ya kumchafua Rais Dk Magufuli na serikali ya Tanzania.“Inasikitisha Mbunge huyu ambaye bado anaendelea na matibabu anaanzisha ziara katika nchi mbalimbalina kutunga tuhuma nzito dhidi ya nchi yetu,” alisema Dk Posi.Amesema watanzania pamoja na wapiga kura wa jimbo lake, walitarajia mbunge huyo kama ameshapona na ana uwezo wa kusafiri sehemu mbalimbali duniani, kama anavyofanya sasa, angerejea nyumbani Singida na kuendelea na majukumu yake ya kuwatumikia wananchi wake.Balozi huyo alieleza kuwa inaeleweka kuwa shambulio la risasi dhidi ya Mbunge huyo lililotokea Dodoma Septemba 17, mwaka juzi, lilikuwa la kutisha, kwa kuwa ni moja ya matukio machache kutokea nchini, ingawa yanaweza kutokea pia katika nchi nyingine.“Ilikuwa ni siku moja pia ambayo jijini Dar es Salaam alishambuliwa ofisa wa juu wa jeshi aliyestaafu na watu wasiojulikana na kumjeruhi vibaya na risasi. Rais alitoa taarifa ya kukemea matukio yote mawili na kuagiza uchunguzi wa kina ufanyike,” amesema.Amesema Dk Magufuli alimuagiza Makamu wa Rais na viongozi wengine waandamizi wa serikali, kumjulia hali Lissu alipokuwa hospitali Dodoma, Nairobi nchini Kenya na Brussels, Ubelgiji akipatiwa matibabu.“Inasikitisha kuona mbunge huyu anageuza hatua hizi zenye nia njema za Rais na kumtuhumu mambo mazito yasiyo na ukweli. Kwa sasa nchini Tanzania anasubiriwa mbunge huyu na dereva wake watoe maelezo ili uchunguzi uendelee,” amesema.Hata hivyo, alieleza kuwa baada ya tukio tu, uchunguzi ulianza, lakini ni lazima mbunge huyo atoe maelezo yake, kwa kuwa ni muhimu katika kesi hiyo.“Mpaka sasa vyombo vya dola havijaupata upande wa mbunge huyo kuhusu kile kilichotokea,” amesema.Akielezea madai ya ukosefu wa demokrasia nchini, hasa baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe kuwekwa mahabusu, alisema suala hilo liko kisheria.Posi alisema kiongozi huyo alipatiwa dhamana, lakini alirejeshwa mahabusu baada ya kuvunja masharti ya dhamana, baada ya kutotokea mahakamani bila sababu za msingi.
Kitaifa
0
SERIKALI imesema itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuhakikisha kuwa inaongeza uwiano wa jinsia baina ya wanaume na wanawake katika vyombo vya uamuzi ili kufi kia 50 kwa 50.Ili kufikia hilo, imetaja mikakati iliyoanza kuchukuliwa ili kuzijengea uwezo jinsia zote, ikiwemo ya kufuta kodi za pedi za kike ili kuwezesha watoto wa kike kupata elimu bila kuathiriwa na siku za hedhi.Mikakati mingine ni kujenga zahanati ili kupunguza vifo vya wanawake na watoto wakati wa kujifungua, kuimarisha elimu ya sekondari ili kupanua wigo wa elimu, na kuanzishwa kwa kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani ili kumpa muda zaidi wa kushiriki katika shughuli za maendeleo.Mikakati hiyo iliainishwa jana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizindua Mkakati na Mpango Kazi wa Kujumuisha Masuala ya Jinsia Ndani ya Bunge, wenye lengo la kuhimiza uwiano wa jinsia wakati wa uendeshaji wa shughuli za mhimili huo.Mbali ya kusifu Bunge kwa hatua mbalimbali za utekelezaji wa uwiano wa kijinsia, alisema serikali pia imekuwa inachukua hatua mbalimbali kufikia azma hiyo kupitia Sera ya Jinsia ya mwaka 2000 na itifaki mbalimbali za kimataifa.“Bado haitoshi, ni lazima jitihada zaidi zifanywe ili uwiano huu wa kijinsia uweze kufikia 50 kwa 50,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa. Alisema miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na serikali ni kuondoa kodi kwenye taulo za kike, yanayoagizwa kutoka nje ili kushusha bei ya taulo hizo na kuwafanya watoto wengi wa kike kuyanunua na kuyatumia wakiwa shuleni wakati wa hedhi bila kuhofia kudhalilika.Alisema baada ya hatua hiyo ya serikali, imebainika kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto wa kike wanaohudhuria masomo wakati wote kutokana na kumudu gharama za kununua taulo hizo na kuzitumia wakati wa hedhi wakiwa masomoni.Hata hivyo, alionya kuwepo kwa wafanyabiashara ambao bado wanauza taulo hizo kwa bei ya juu licha ya serikali kufuta kodi. Alisema hatua kali zitachukuliwa dhidi yao, ikiwa ni pamoja na kuwafutia leseni za biashara.Alisema pia serikali imeendelea kuimarisha utoaji wa elimu ya sekondari ili kuwafanya watoto wengi, kunufaika na elimu hiyo huku ikiongeza madarasa na kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia.Alisema hadi sasa takwimu zinaonesha kuwa katika elimu ya juu uwiano wa kijinsia ni kati ya asilimia 30 kwa wasichana na asilimia 70 kwa wavulana, kwenye ajira ni asilimia 37 kwa wanawake na asilimia 63 kwa wanaume na kwenye uongozi ni asilimia 15 ya wanawake na asilimia 85 kwa wanaume.“Nichukue nafasi hii kulipongeza Bunge kwa kufikia asilimia 40 kwa wanawake na asilimia 60 kwa wanaume, lakini ni matakwa yangu kuona uwiano unaongezeka na kufikia asilimia 50 kwa 50,” alisema.Awali, Naibu Spika wa Bunge, ambaye ni pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Mpango huo, Dk Tulia Ackson alisema mpango huo utaongeza ushiriki sawa wa wanawake na wanaume ndani ya Bunge na katika utekelezaji wa kazi zake zote.Kwa upande wake, Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Godfrey Mulisa alisema Tanzania ni moja ya nchi, ambazo zimepiga hatua kubwa katika kuhamasisha uwiano wa kijinsi katika uendeshaji wa vyombo mbalimbali vya uamuzi.
michezo
2
SERIKALI imeeleza mpango wake wa kusukuma mbele viwanda na kufanya biashara nchini kwa kuhakikisha inatekeleza mfumo rafi ki wa uwekezaji na ufanyaji biashara nchini. Imesema katika kuendeleza ujenzi wa uchumi wa viwanda serikali itaendelea kuweka vivutio na kufanya maboresho katika maeneo kadha yanayoleta vikwazo ili sekta binafsi ishiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi. “Pamoja na kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji katika viwanda na biashara, utekelezaji wa Blue Print utakuwa tiba ya changamoto zinazotatiza sekta binafsi,” alisema Waziri wa Viwanda na Biashara Joseph Kakunda wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake Bungeni jana. Alisema sekta binafsi ni injini ya kujenga uchumi wa viwanda hivyo serikali itafanya kila linalowezekana kuhakikisha sekta hiyo inashiriki kikamilifu ujenzi wa uchumi.Alisema lengo ni kushawishi ujenzi wa viwanda vitakavyo ongeza thamani ya mazao yanayozalishwa nchini ili kuondokana na uuzaji wa malighafi nje ya nchi. Aidha, kwa msukumo wa sasa wa serikali, inatarajiwa kwamba sekta binafsi itajenga viwanda vinavyotoa ajira kwa wananchi kwa wingi na vile vinavyozalisha bidhaa zinazotumiwa na Watanzania walio wengi. Pia, serikali imesema itaimarisha taasisi zake za viwango na mfumo wa stakabadhi ghalani katika manununuzi, vituo maalumu vya mauzo ili kuwa chachu ya ulinzi wa viwanda na mlaji. Imesema itaboresha mifumo ya usajili wa biashara na leseni kutoka Brela na pia halmashauri kwa kuhakikisha inatoa mafunzo ya Tehama ili kumudu mfumo wa Dirisha la Taifa la Biashara (NBP) ambao ndio unaotoa leseni za biashara. Kakunda alisema kwa mwaka 2019/2020 serikali itaendelea na miradi ya kimkakati, urasimishaji wa viwanda na biashara ndogo na za kati, uongezaji thamani ya mazao ya kilimo na malighafi na kuunganisha masoko. Alisema ni lengo la serikali kufanya tathmini ya hali halisi ya uzalishaji na mahitaji ya bidhaa viwandani katika viwanda vya sukari, korosho, mafuta ya kula chuma, ngozi nguo na dawa za binadamu.
Kitaifa
0
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeanza kuhakiki malipo kwa ajiri ya wanachama wake, waliokuwa wakifanya kazi zisizo za weledi kwenye sekta mbalimbali kabla ya kuachishwa kazi.Hatua hiyo imekuja baada ya agizo la Rais John Magufuli alilolitoa, alipokutana na viongozi wa vyama vya wafanyakazi Desemba 28 mwaka jana Ikulu, Dar es Salaam, la kutaka wafanyakazi wa aina hiyo kupewa fao lao la kuachishwa kazi.Akizungumza na waandishi wa habari jana, Meneja Kiongozi wa Matekelezo wa NSSF, Cosmas Sasi alibainisha kuwa malipo yatalipwa mara tu baada ya mfanyakazi husika kuhakikiwa.Sasi alisema uhakiki huo utachukua siku 30, tangu mfanyakazi kuwasilisha ombi lake na kuwa kwa maombi yatakayotiliwa shaka, yatafanyiwa uchunguzi kwa muda wa mwezi mmoja.Alisema NSSF imejipanga vyema kutekeleza uhakiki huo kwa wakati na muda mwafaka ili kila mwenye haki apewe haki yake kwa wakati, huku akiwataka wenye kustahili kulipwa fao hilo kutosita kuwasilisha maombi kwenye ofisi za NSSF zilizopo kila mkoa.“Tumejipanga kuwalipa kwa wakati hawa wafanyakazi wote waliokuwa kwenye ajira ya muda na ambao labla ajira imesitishwa au mradi kuisha, hawa watapewa mafao yao yote,” alisema. Alifafanua kuwa kila mhusika akishapewa fedha zake zote, alizokuwa amechangia NSSF, ataongewezewa na asilimia nyingine ya fedha kama nyongeza, ambazo hakuwa tayari kuziweka wazi kuwa ni ngapi.Alisema kwa wafanyakazi wanaofanya kazi za kitaaluma na walikuwa wakichangia zaidi ya miezi 18, wakisitishiwa ajira zao, watalipwa asilimia 33.3 ya mshahara waliokuwa wakilipwa kwa miezi sita kabla ya kupata ajira nyingine.Alibainisha kuwa kwa wale waliokuwa wakichangia chini ya miezi 18, watalipwa asilimia asilimia 50. Kwa upande wake, Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Lulu Mengele akizungumzia kuhusu malipo ya pensheni kwa wastaafu wanaonufaika na mfuko huo, alibainisha kuwa wastaafu ambapo hawatakuwa wamehakikiwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu, malipo yao yatasitishwa.“Wastaafu ambao hadi sasa hawajahakikiwa wanaombwa kuwasilisha nakala stahiki kwenye ofisi za NSSF kwenye mikoa wanayotokea ili uhakiki ufanyike wakati,” alisema Mengele. “Kwa kuwa tunazo ofisi 65 Tanzania Bara ni dhahiri kuwa hakuna sababu za wastaafu hao kushindwa kwenda kuhakikiwa wajitokeze kwa wingi wakahakikiwe ili waje kunufaika na mapato na pia hata wale waliokuwa wakifanya kazi za muda mfupi na wamesitishiwa au kufukuzwa kazi au mradi kuisha, nao walete vielelezo wahakikiwe tayari kwa malipo stahiki,” aliongeza.Katika kikao cha Rais Magufuli na viongozi wa vyama vya wafanyakazi, aliagiza wastaafu kulipwa mafao yao kwa kufuata vikokotoo vya awali kwa muda wa miaka mitano ya mpito kuanzia sasa, tofauti na mapendekezo yaliyokuwa yametolewa chini ya Kanuni za Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).SSRA ilipendekeza kikokotoo cha asilimia 25 kwa wastaafu kwa mkupuo, kisha kuendelea kulipwa asilimia 75 kila mwezi hadi kufa kwao. Rais Magufuli alipinga hatua hiyo na kuagiza kuwa kuanzia sasa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na wa sekta binafsi NSSF, iliyoanza kufanya kazi mwaka jana, ianze kulipa wastaafu kwa kutumia kikokotoo cha zamani kwa mujibu wa mifuko waliyokuwemo kabla haijaunganishwa.
Kitaifa
0
Katika mkutano wake wa kwanza na vyombo vya habari baada ya kurudi Everton, Rooney amesema kuwa anafarijika kurejea Everton baada ya kuondoka miaka 13 kuichezea United na kunukuliwa na BBCSport akisema kuwa “sijarudi nyumbani kustaafu.Ninataka kucheza na kuwa na mafanikio katika klabu hii.” "Nilikuwa na wakati mzuri nikiwa Manchester United lakini soka husonga mbele na wachezaji husonga mbele,” amenukuliwa nahodha huyo wa zamani wa United ambaye leo ameanza mazoezi na Everton leo. Rooney anachukuwa namba ya jezi iliyokuwa ikivaliwa na straika Romelu Lukaku anayetimkia Old Traford.
michezo
2
MBUNGE wa Chemba, Juma Nkamia (CCM) amesema ni aibu Tanzania kuchukua makocha kutoka nje huku kukiwa na wazawa wenye uwezo mkubwa.Akichangia taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa mwaka 2018-2019, Nkamia alisema ni aibu kwa kocha wa mpira wa miguu kutoka Burundi. “Ni aibu kocha wa mpira wa miguu kutoka Burundi huku wazawa wakiwa hawapewi nafasi,” alisema.Nkamia aliyewahi kuwa kiongozi kwenye klabu ya Simba miaka ya nyuma alisema pia kwa sasa Ligi ya Soka ya Wanawake na Ligi Kuu imekuwa mahututi kutokana na timu kulia njaa. “Hata Ligi ya Wanawake hali sio nzuri, mfano timu inatoka nyumbani na ugenini timu inatoka Njombe haina hata sehemu ya kulala kwa sababu ya ukata, hatuwezi kuendesha mpira hivyo.”Kutokana na kauli hiyo, Spika Job Ndugai alisema: “Mheshimiwa Nkamia, sio timu za kina dada tu hata timu fulani zinatembeza bakuli mheshimiwa Nkamia.” Katika hatua nyingine, Mbunge wa Konde Khatibu Said Haji (CUF) amehoji ni kiasi gani cha fedha ambacho kimekuwa kinatolewa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) kwa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA).Akiuliza swali jana bungeni, Haji alihoji: “FIFA inatoa misaada ya fedha kwa kupitia TFF. Je, ni kiasi gani cha fedha TFF imekuwa ikiipatia Zanzibar kupitia ZFA?” Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza alisema ni kweli FIFA inatoa msaada wa fedha kwa mashirikisho ya mpira wa miguu ikiwemo TFF kwa ajili ya miradi na programu mbalimbali.Alisema fedha hizo huwa ni maelekezo maalum kwa lengo la kusaidia na kuendeleza maeneo ya Ligi ya Wanawake, Vijana pamoja na masuala ya kiutawala. “Kuanzia mwaka huu FIFA itakuwa inatoa jumla ya dola za Marekani milioni 1.25 kila mwaka kwa wanachama wake ikiwemo ZFA ambayo ni sehemu ya TFF,”alisema. Akifafanua mchanganuo wa fedha hizo, Shonza alisema fedha za miradi kiasi cha dola za Marekani 750,000, fedha kwa ajili ya kuendesha ofisi dola za Marekani 500,000.“Hata hivyo kwa muda wa miaka mitatu kutokana na kutokuwepo kwa uwazi katika matumizi ya fedha na kukidhi vigezo vya utawala bora, TFF wamekuwa hawapati hizo fedha,” alisema Shonza. Shonza alisema kazi kubwa imefanyika kurekebisha dosari zilizokuwepo za kiuhasibu na utawala bora hivyo uwezekano ni mkubwa TFF na ZFA kuanza kupokea msaada huo wa fedha mapema mwaka huu.
michezo
2
Hatua hiyo inatoa fursa kwa huduma hii mpya ya malipo ya kabla ya kutumia kadi ya kielektroniki la daraja la juu inayotumia mfumo wa kibenki, kufanyika katika wigo mpana ndani na nje ya Tanzania.Makubaliano hayo sasa, yatamwezesha mtumiaji wa huduma za B-PESA kuweza kufanya mwamala nje ya Tanzania katika mashine za kutolea fedha milioni 1.6 na kwa mawakala zaidi ya milioni 12 katika nchi 142.Mbali na UnionPay, taasisi nyingi za kibenki hapa nchini zimeonesha nia ya kushirikiana na Kampuni ya Smart Banking Solution (SBS) kuanza kutoa kadi za B-PESA kwa wateja wake, huku wakurugenzi wakuu wa taasisi hizo, wakiahidi kutoa kadi hizo kwa wateja wake mapema ili kunufaika na fursa hii.Haya yanatokea siku chache tu baada ya huduma ya malipo ya awali ya B-PESA kuzinduliwa nchini Tanzania, ikiwa na lengo la kutengeza mfumo madhubuti wa malipo kwa taasisi za kibenki na wateja walioko Tanzania na Afrika kwa ujumla.Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini makubaliano hayo jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mwakilishi Mkuu wa UnionPay International Kanda ya Afrika Mashariki na Kati, Li Zhixian alisema kampuni yake ina furaha kubwa kushirikiana na B-PESA, sababu huduma zote mbili zinalenga kuleta mapinduzi katika mfumo wa malipo wa kielektroniki.“Baada ya kuangalia kwa undani sifa za B-PESA, naamini huduma hii itaweza kuubadilisha muundo wa malipo nchini Tanzania na hususani zaidi kuweza kuiboresha miundombinu ya malipo katika nchi hii. “Ukiwa kama mfumo wa malipo wa kimataifa unaochipukia, Union- Pay imekuwa ikijizatiti zaidi kurahisisha huduma ya malipo katika kila nchi. Wazo hili linaendana na la B-PESA. UnionPay na B-PESA tumesaini makubaliano haya leo kuangalia ni jinsi gani tunaweza kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja ili kuiongezea nguvu B-PESA kuweza kufikia masoko ya kimataifa,” alisema Li.Aliongeza “tungependa kuzikaribisha taasisi zenu za kibenki kujiunga na mpango huu ili kutoa kadi za UnionPay - B-PESA nchini. Wateja wenu watapata fursa ya kufurahia matumizi ya kadi za B-PESA nchini, na kwa kupitia UnionPay huduma yenu itatolewa kwenye nchi zaidi ya 140 duniani.”Alisema kuwa wazo la kushirikiana na B-PESA liliendana na lengo la kutumia mifumo hiyo miwili ya malipo ili kuipa msukumo zaidi sekta ya biashara baina ya China na Afrika.Kwa mujibu wa rekodi za kibiashara, China ni mbia mkubwa zaidi wa kibiashara nchini Tanzania na chanzo cha pili kwa ukubwa katika uwekezaji.Biashara baina ya nchi hizi mbili mwaka 2012 zilikuwa ni zaidi ya dola za Marekani bilioni 2.47, ambayo ni ongezeko la asilimia 15.2. China ni chaguo la kwanza kwa wafanyabiashara wa Tanzania katika masuala ya ugavi.Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SBS, Gustav Vermaas alisema ushirikiano huo unaziongezea ubora kadi hizo na upekee zaidi, kwa maana wateja wa B-PESA watakuwa katika mstari wa mbele wa kuibadilisha Tanzania na Afrika kwa ujumla kuwa jamii isiyotegemea fedha taslim.
Biashara
1
WATAZAMAJI wanatakiwa kutoa kiasi cha Sh 5,000 ili kuiona Simba ikicheza dhidi ya Mbabane Swallows ya eSwatini katika mchezo wa awali wa kuwania kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa wa Afrika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.Mchezo huo wa kwanza wa raundi ya awali, umepangwa kuanza majira ya saa 10:00. Ofisa Habari wa mabingwa hao wa Tanzania Bara, Haji Manara alisema kuwa kiingilio cha chini katika mchezo huo kitakuwa Sh 5,000 kwa majukwaa ya mzunguko.Viingilio vingine ani pamoja na Sh 7,000 kwa eneo la VIP C, 10,000/- eneo la VIP B na 20,000/- kwa watakaokaa VIP A. Manara alisema kwamba maandalizi ya mchezo huo yamekalika na tayari kikosi cha Simba kinasubiri kushuka dimbani kwa ajili ya mchezo huo. “Tunakwenda kuwakabili Mbabane Jumatano (leo) tukijua ni timu nzuri na mabingwa wenzetu, lakini tunajua matarajio ya Watanzania na wana Simba kwetu.Kwa kweli hatutawaangusha na tunaahidi furaha kwenu,” alisema Manara. Simba imepania kufika mbali msimu huu katika michuano ya Afrika baada ya msimu uliopita kutolewa katika Raundi ya Kwanza tu na Al Masry ya Misri kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.Na ikiwa chini ya kocha mpya, Mbelgiji Patrick Aussems – Simba imepania kutimiza hazma yake, baada ya kusajili kikosi kiapana chenye kusoka la kuvutia. Kikosi cha Simba ni kipana na kinataka kudhihirisha kuwa kiko vizuri katika mashindano ya kimataifa, hivyo leo kinaweza kutoa kichapo kwa wageni wake hao, ambao nao wako vizuri katika mashindano ya Afrika.
Kitaifa
0
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imekuwa inatumia wastani wa Sh bilioni tatu kila mwaka kusafi risha wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya kupata huduma za matibabu, tayari imeanza kuchukua hatua za kukabili changamoto hiyo.Hatua iliyochukuliwa ni ile ya kuingiwa kwa makubaliano baina ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Hospitali Kuu ya Rufaa ya Mnazimmoja mjini Unguja, ili wagonjwa wa Zanzibar waweze kutibiwa Muhimbili.Mkurugenzi wa Hospitali ya Mnazimmoja, Jamala Taib alisema jana kuwa makubaliano hayo ya miaka mitatu lengo lake ni kuboresha huduma za afya kwa kushirikiana kwa pamoja.Alisema wapo zaidi ya wagonjwa 110 wanaosubiri huduma za matibabu ya nje ya nchi, idadi ambayo ni kubwa inayohitaji fedha nyingi. ‘’Makubaliano yetu ya miaka mitatu lengo lake kubwa ni kuwapatia huduma za matibabu wagonjwa wetu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo ina uwezo mkubwa wa kutoa matibabu ya aina mbalimbali,” alisema.Jamala alisema Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imepiga hatua kubwa katika kufanya upasuaji wa aina mbalimbali kwa kutumia teknolojia ya kisasa ambayo hufanyika katika baadhi ya nchi za Ulaya.Alisema makubaliano hayo yataokoa fedha nyingi za kigeni ambazo zilikuwa zitumike kusafirisha wagonjwa kwenda katika nchi mbalimbali za Ulaya na Asia. Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Shufaa Nassor Ali alisema hayo ni makubaliano muhimu ambayo yamelenga katika kuimarisha huduma za afya za wananchi wa Zanzibar kuwa bora.Alisema Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeridhishwa na aina ya huduma ambazo zitapatikana katika Hospitali ya Muhimbili kwa wananchi wanaohitaji matibabu nje ya nchi. Wizara ya Afya ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar husafirisha wagonjwa wengi kwenda nje ya nchi ikiwemo India na Israel, wakiwemo watoto wanaokabiliwa na maradhi ya moyo.
Kitaifa
0
Katika mchezo huo, Simba walilazimika kufanya kazi ya ziada kusawazisha bao hilo kupitia kwa Mrundi Laudit Mavugo aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Juuko Murshid.Akizungumza na gazeti hili, Lechantre alisema wachezaji wake walishindwa kujituma na kutoa nafasi kwa Lipuli kufanya wanavyotaka jambo ambalo liliwaweka kwenye wakati mgumu kusaka bao la kusawazisha.“Mbinu walizoingia nazo Lipuli ndiyo ziliwachanganya wachezaji wangu wakashindwa kufuata maelekezo tuliyowapa na kucheza ovyo jambo lililowapa Lipuli kutawala mchezo na kupata bao lao kipindi cha kwanza; kipindi cha pili walitulia baada ya kuzungumza nao wakati wa mapumziko,” amesema Lechantre.Baada ya mechi na Lipuli, Simba waliopo mbele kwa mechi tatu dhidi ya Yanga hawatakuwa na mchezo wowote mpaka Aprili 29 watakapokutana na wapinzani wao wakubwa Yanga mchezo utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
michezo
2
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Gor Mahia, Meddie Kagere ameibuka na kusema kuwa nusura atue kwa wapinzani wa timu hiyo ya Kenya, AFC Leopards kabla ya kusajili Gor.Akizungumza katika mahojiano na Sunday Nation, Kagere mwenye umri wa miaka 32 aliendelea kuichezea K’Ogalo kwa sababu tu viongozi hawakutokea kuzungumza naye kuhusu maslahi binafsi, ili ajiunge na Leopards.Kagere, ambaye kwa sasa ni mchezaji wa Simba ya Tanzania aliongeza kusema kuwa pia alifikiria kujiunga na Tusker, lakini aliwamwaga baada ya uongozi wa timu hiyo kumtumia tiketi ya basi ya safari ya kama kilometa 1200, badala ya kumpatia tiketi ya ndege, usafiri ambao angetumia saa moja tu.“Gor walikuja lakini nilikuwa nataka kujiunga na AFC Leopards. Ukweli, makubaliano yalikuwa katika hatua ya juu kabisa.Tatizo kubwa la Tusker wenyewe walitaka niende Nairobi kwa basi kutoka Kigali.“Walitakiwa kunitumia mimi tiketi ya ndege na badala yake Gor Mahia walifanya hivyo na nikawakwepa Tusker na kutua Gor," alisema Kagere.“Wakati huo, Gor walikuwa hawajanifikia mimi bado. Kupitia Musa (Mohammed), walipata mawasiliano yangu na kunipatia tiketi ya ndege, wakisisitiza nisijiunge na wapinzani wao (AFC Leopards).”“Baada ya msimu wangu wa kwanza pale Gor Mahia, Zamalek ya Misri walinifuata lakini matatizo ya viza yaliua mpango huo.Wakati fulani mambo hayakuendei vizuri sio kwa sababu hauna bahati ila Mungu anakuwa hajapanga ufanikiwe kwa hilo.Hivyo tangu dirisha lifungwe ilinibidi kukaa miezi sita bila ya klabu," alisema Kagere.Kagere, ambaye aliwahi kuichezea timu ya Tunisia na Ulaya, sasa ameitosa Gor Mahia na kutua Simba na yuko timu hiyo katika kambi ya mazoezi Uturuki wakijiandaa kwa msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa.
michezo
2
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekanusha taarifa zisizo rasmi kuhusu kuwepo kwa viwango vipya vya michango ya uanachama katika kupatiwa huduma za afya.Hata hivyo ilibainishwa jana kuwa upo mchakato wa kuunda vifurushi tofauti vya uchangiaji kwa makundi tofauti ya uanachama ili kuwezesha watu kujiunga kulingana na uhitaji wao. Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya uhusiano, taarifa zinazosambaa sio rasmi kwa hiyo zipuuzwe. Ilieleza kuwa mfuko umeanzisha vifurushi vya makundi mbalimbali ya wanufaika kama waajiriwa, watoto, wakulima na hata wajasiriamali. Kuhusu taarifa rasmi ikoje katika eneo hilo la kuongeza viwango vipya vya uchangiaji, Ofisa Mahusiano na Elimu kwa Umma, wa NHIF, Grace Kisinga alisema taarifa ya mfuko kuhusu suala hilo ndivyo ilivyo na kwamba wanachama wanachangia kwa taratibu zilizopo.Kuhusu kuongeza wigo wa wanufaika, alisema ili kuongeza wanufaika, mfuko pia ulishaanza mchakato wa kuunda vifurushi tofauti vya uchangiaji kwa makundi tofauti ya uanachama ili kuwezesha watu kujiunga kulingana na uhitaji wao. Alisema mchakato huo upo katika hatua za kukamilika katika ngazi mbalimbali za uongozi na utakapokamilika taarifa rasmi zitatolewa na mfuko wa umma. Iliongeza kuwa kwa sasa Mfuko unaendelea kusajili wanachama kupitia taratibu zilizopo za uchangiaji..Hata hivyo, NHIF, iliomba radhi kwa usumbufu wowote uliosababishwa na taarifa hizo zisizo rasmi na kuendelea kuwahimiza wananchi kufuatilia taarifa za NHFI kupitia tovuti yake. Wakati huo huo, kupitia tovuti ya mfuko huo, umeanza utaratibu wa uhakiki wa wanachama waliosajiliwakwa kwa wastaafu ili kuhuisha taarifa na kuweka kumbukumbu sahihi tangu Januari Mosi ukitarajiwa kukamilika Machi 30, mwaka huu.Ilielezwa kuwa kazi ya uhakiki unawahusu wanachama wastaafu walioandikishwa katika mfuko huo kuanzia Julai 2009 hadi Septemba 2018. Ilieleza kuwa uhakiki huo unafanywa kwa ofisi zote NHIF zilizopo Tanzania bara na Ofisi za Zanzibar. Mwanachama mstaafu atahitajika kufika katika ofisi yoyote ya NHIF akiambatana na mwenza wake (endapo yupo) na iwapo mwanachama mstaafu amefariki, mwenza aliyebaki atatakiwa kufika katika ofisi za mfuko huo kwa ajili ya uhakiki.Aidha mstaafu huyo atatakiwa kufika katika uhakiki huo akiwa na vitambulisho vya NHIF, cheti cha ndoa (mstaafu mwenye mwenza), na kitambulisho cha uraia, mpiga kura, leseni ya gari au hati ya kusafiria. Iliongeza kuwa wanachama wastaafu wanahimizwa kufuatilia taarifa hiyo na muda uliowekwa ili kuepuka usumbufu wakati wa kupatiwa huduma za afya.
Kitaifa
0
KOCHA wa Tanzania Prisons, Mohammed ‘Adolf’ Rishard, amesema hawatakubali rekodi yao ya kutokufungwa kwenye Ligi Kuu ivunjwe na Yanga kwenye mchezo utakaochezwa kesho katika Uwanja wa Sokoine, mkoani Mbeya.Tanzania Prisons ambayo imecheza michezo 13 na kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 23 na ikiwa imeshinda mechi tano, sare michezo nane, inakutana na Yanga inayoshika nafasi ya tisa ikiwa na pointi 18.Adolf Richard ametoa tahadhari hiyo kwa Yanga ikiwa ni siku moja baada ya kupunguzwa kasi kwa kugawana pointi na Mbeya City kwenye mchezo wa ligi hiyo uliochezwa kwenye Uwanja Sokoine ambao ndio utakaotumika kwa mchezo wa kesho. “Tumejijengea falsafa moja ya kuwaheshimu wapinzani na tutaindeleza kwa Yanga ila wasije wakatarajia watakuja kupata matokeo kirahisi.Baada ya kutoka sare mechi iliyopita hatuwezi kukubali rekodi ya kutokufungwa ivunjwe na Yanga tena katika uwanja wetu wa nyumbani,” alisema. Alisema wanaiheshimu Yanga ni timu kubwa na ina wachezaji wazoefu na wenye uwezo wa kubadilisha matokeo wakati wowote, lakini kupitia mechi iliyopita wameona udhaifu wao mwingi, hivyo wamejipanga kuhakikisha dakika 90 zitaamua mshindi kuwa wao.“Wachezaji wote wako fiti kwa mchezo, kikubwa tubaomba mashabiki wa Mbeya na sehemu za jirani kujitokeza kwa wingi kutushangilia kwani ushindi wetu ni sifa ya mkoa wa Mbeya na Nyanda za Juu Kusini,” alisema Adolf Richard.Gazeti hili lilipomtafuta kocha wa Yanga, Charles Mkwasa, kuzungumzia maandalizi ya mchezo dhidi yaTanzania Prisons, aligoma kuzungumza kwa madai yupo kwenye mapumziko ya sikukuu ya Krismasi“Kama unataka taarifa kuhusu maandalizi ya timu kujipanga na mchezo ujao mtafute Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, atakuambia lakini kwa sasa nimechoka na sitaki kuongelea maana nipo mapumziko nasheherekea sikukuu ya Krismasi hapa Mbeya,” alisema Mkwasa.
michezo
2
UONGOZI wa JKT Oljoro ya jijini Arusha ambao ndio wamiliki halali wa timu ya Arusha United wameiuza timu hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti. Hatua hiyo imekuja wiki chache baada ya Mkuu wa Mkoa Arusha, Mrisho Gambo kudaiwa kushindwa kuiendesha timu hiyo ikiwa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza.Meneja wa timu hiyo, Jumanne Ahmed alisema ni kweli timu imenunuliwa na Alexander Mnyeti, ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara ambaye sasa ndiye mkuru- genzi wa timu hiyo. Meneja huyo alisema timu hiyo inaitwa Gwambina FC na itaendeshwa kwa mfumo wa kisasa wa kampuni.“Timu itakuwa na mas- kani yake Misungwi mkoani Mwanza, ambako pia tunajenga uwanja mkubwa utakaojulikana kama Gwambina Complex na timu pamoja na uwanja vitazinduliwa Juni 21 mwaka huu, itaendeshwa kisasa kwa mfumo wa Kampuni,” alisema Ahmed.Akithibitisha hilo Meja Iddy Musila ambaye ni kaimu wa kikosi 833 Oljoro JKT alisema ni kweli wameamua kuiuza timu kumpa mdau mwingine wa soka ili aiendeleze mwenyewe, kwani awali waliitoa timu hiyo bure kwa mkuu wa mkoa Arusha kwa sababu alionesha nia ya kuiendeleza na kukuza michezo.Alisema wakati timu iko katika Ligi Daraja la Kwanza haikufikia hatua ya kumaliza ligi hiyo, mkuu wa mkoa aliamua kujitoa kuisimamia kutokana na kutofautiana na waendeshaji wa Bodi ya Ligi kwa madai kuwa hawakuwatendea haki hivyo timu ikabaki haina mwenyewe.“Tulihakikisha inamaliza ligi hiyo na baada ya hapo akatokea mdau ambaye alikuwa anatafuta timu na hatukuwa na sababu ya kuendelea nayo kwani uwezo hatukuwa nao katika suala zima la kiuchumi,” alisema Musila.Alisema suala la uchumi limepelekea timu waiuze kwani kuendesha timu ni gharama na ikizingatiwa kipindi kile mkuu wa mkoa ameiacha walitumia gharama sana kumalizia zile mechi tano zilizokuwa zimebaki, hivyo wakaona kabla ya kuanza kwa msimu waitoe kwa mdau.“Hivi sasa hatuna mpango wowote wa kuanzisha timu, kwani tayari JKT ina timu hivyo hatuna sababu ya kuwa na timu ila tutakuwa na timu za huku kikosini ambazo vijana watacheza mechi za ujirani mwema, lakini kwa upande wa timu katika ligi hatuna mpango huo tena,” alisema Musila.
Kitaifa
0
UPELELEZI katika kesi ya kuchapisha video ya ngono kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram inayomkabili, Msanii wa Filamu nchini, Wema Sepetu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, bado haujakamilika.Wakili wa Serikali, Jenipher Masue alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Maira Kasonde kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi bado unaendelea.Hakimu Kasonde aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 12, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na kwamba dhamana ya mshitakiwa bado inaendelea. Akisoma mashitaka hayo katika kesi namba 322, Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono alidai kuwa Oktoba 15, mwaka huu katika sehemu tofauti za Mkoa wa Dar es Salaam, Wema alichapisha video za ngono kupitia ukurasa wake wa Instagram jambo ambalo ni kinyume na sheria.Hii ni mara ya pili kwa mlimbwende huyo ambaye alishinda taji la Miss Tanzania mwaka 2006, kufikishwa mahakamani hapo kwa mashitaka tofauti ambapo awali alikuwa akikabiliwa na mashitaka ya kukutwa na kutumia bangi. Wakili wa utetezi, Reuben Simwanza aliomba mahakama hiyo impatie dhamana yenye masharti nafuu mteja wake kwa kuwa ni haki yake.Hata hivyo, Wakili Kombakono aliomba mahakama hiyo kumpatia mshitakiwa masharti magumu ya dhamana ili iwe fundisho kwake na kwa wengine kwa sababu ni msanii mwenye wafuasi wengi wanaomuangalia hususan watoto. Hakimu Kasonde alimtaka mshitakiwa Wema kuwa na mdhamini mmoja watakaosaini kulipa bondi ya Sh milioni 10 pia alimpiga marufuku Wema kuchapisha au kuweka picha na maneno yoyote ya kingono katika ukurasa wake huo wa mtandao wa Instagram.Oktoba 25, mwaka huu Wema katika mkutano wake na waandishi wa habari aliomba radhi watanzania kwa video za ngono zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii hususani Instagram.Katika maelezo yake, Wema aliomba radhi kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bodi ya filamu, familia yake, ndugu, jamaa na marafiki ambao wanamuangalia kama kioo cha jamii pamoja na kumuomba radhi mama yake mzazi.Pia alikiri kuwa aliwadharirisha na kuwafedhehesha watu wengi pamoja na kuwaathiri na kwamba lengo la kuomba radhi si kwa kuomba huruma ya mtu yoyote bali kwa kugundua kosa lake. Hata hivyo, baada ya kuomba radhi Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) lilimfungia muigizaji huyo kutojihusisha na kazi zozote za sanaa kwa muda usiojulikana.
Kitaifa
0
MAREKEBISHO ya Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Sura ya 230 yanayojumuisha mapendekezo ya kuzirasimisha kumbi au vibanda vinavyotumika kuoneshea video na hivyo kuratibiwa na sheria hiyo ya filamu, yamepitishwa rasmi na Bunge.Aidha, marekebisho hayo yameweka masharti kwa mtu au kampuni ya kigeni inayotaka kutumia eneo lolote Tanzania kutengeneza filamu, ikiwemo kuwasilisha nakala ya awali iliyotumika kutengeneza filamu husika.Marekebisho hayo yamepitishwa kupitia Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali 8, namba 3 wa mwaka 2019, unaojumuisha marekebisho ya sheria hiyo ya filamu uliowasilishwa bungeni Dodoma jana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi.Akiwasilisha marekebisho hayo alibainisha kuwa muswada huo unapendekeza marekebisho yaliyolenga kuboresha usimamizi na kuweka ubora wa kumbi za sinema na vibanda vinavyoonesha video. Pia alisema yamelenga kuongeza mapato kupitia maboresho ya usambazaji wa filamu kwa watendaji wa filamu pamoja na kuongeza mapato ya serikali.Profesa Kilangi alieleza kuwa lengo la marekebisho hayo ni kuhakikisha kumbi na vibanda vinavyotumika kuoneshea video vinapaswa kurasimishwa chini ya kifungu cha 10 cha Sheria hiyo.“Sehemu hiyo pia inapendekeza kuongezwa kwa kifungu kipya cha 6A, ambacho kimeweka masharti mapya kuhusu utengenezaji wa filamu nchini, yanayomtaka mtu au kampuni ya kigeni kuwasilisha nakala ya awali iliyotumika kutengeneza filamu husika ili kupata kibali cha kutumia eneo la Tanzania katika kutengenezea filamu hiyo,” alisema Profesa Kilangi.
michezo
2
Akizungumza jana Dar es Salaam wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa, Uchuuzaji na Mikakati wa Benki hiyo, Musa Kitoi alisema mashine hizo za kisasa za i-ATMs zimetengenezwa kwa teknolojia ya juu na zina sifa ya kipekee.Alisema huduma mbalimbali kama kuweka na kutoa fedha taslimu na hundi sasa zinaweza kufanyika kupitia mashine hizo mpya na kurahisisha huduma za kibenki kwawateja wao.Aliongeza kwamba benki hiyo itaendelea kutoa huduma mbalimbali kwa wateja wake kwa ufanisi wa hali ya juu ikizingatia uhakiki wa huduma bora kwa wateja wake na kurahisisha maisha yao kwa ujumla.“Barclays tunawajali wateja wetu na siku zote tunanuia kuwapa huduma za hali ya juu kufuatana na matakwa yao, pia bidhaa na huduma zetu hupangwa kufuatana na mahitaji ya wateja wetu.“Tunapenda kuwathibitishia kwamba tuko katika kiwango cha juu sana kiteknolojia. Katika soko na baadhi ya huduma zetu za kiteknolojia ya juu kama mfumo wa kutoa na kuchukua fedha bila kujaza fomu, utumaji wa fedha kwenye mashine, benki kwa njia ya simu na mwaka jana tumezindua service guarantee ikimaanisha uhakiki wahuduma na kutimiza ahadi na kuwapa wateja huduma bora na za uhakika,” alisema.Meneja Miradi na Mikakati wa Benki hiyo, Jane Mbwilo alisema huduma hiyo ni saa 24 na mteja anaweza kuweka kiasi chochote kwenye mashine hizo za ATM hapa nchini.Alifafanua kwa sasa mashine zipo 24, lakini wapo katika mkakati wa mwisho kuongeza mashine hadi kufika 30 katika maeneo kadhaa ya jijini la Dar es Salaam.
Biashara
1
TIMU ya Yanga jana ilipindua meza kibabe baada ya kuwa nyuma kwa mabao 3-1 na kulazimisha sare ya 3-3 na kunusurika na kichapo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.Huu ni mchezo wa pili kwa Yanga kushuka dimbani baada ya kucheza mchezo wa kwanza, ambao walipoteza dhidi ya Ruvu Shooting kwa mabao 2-0 katika mchezo wa mwanzo.Yanga ilikuwa na jukumu la kuliwakilisha taifa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika, na ndio maana haikucheza mechi zake za awali. Sasa timu hiyo inasubiri ratiba ya mechi za mtoano kwa ajili ya kucheza hatua ya makundi ta Kombe la Shirikisho Afrika. Katika mchezo huo wa jana, Yanga ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mchezaji wake mkongwe, Mrisho Ngassa.Hata hivyo, Polisi Tanzania walisawazisha katika dakika ya 32 kupitia kwa Ditram Nchimbi, huku timu hiyo nusura ifunge tena katika dakika ya 39 baada ya Marcel Kaheza kushinda kutumia vizuri nafasi ya kufunga baada ya kupaisha juu mpira. Dakika ya 55 Polisi Tanzania waliandika bao la pili kupitia kwa Ditram kabla ya dakika mbili baadaye mchezaji huyo kufunga la tatu na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza msimu huu kufunga hat-trick na kuondoka na mpira.Yanga walifunga bao pili katika dakika ya 65 likiwekwa wavuni na Dsvis Moliga baada ya kupata pasi kutoka kwa Makame kabla ya kufunga la tatu katika dakika ya 68 kwa mpira wa adhabu, uliokwenda moja kwa moja wavuni. Katika dakika ya 90, Polisi walipata pigo baada ya mchezaji wake, Yassin Mustapha kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuupiga mpira nje wakati tayari mwamuzi alipuliza filimbi.Yanga katika mchezo huo walionekana kucheza bila kujituma zaidi na wengi walitarajia timu hiyo ingefungwa na Polisi Tanzania iliyocheza vizuri. Vikosi, Yanga: Meacha Mnata, Juma Abdul, Ali Mtoni, Kelvin Yondani, Lamine Moro, Abdulaziz Makame, Mrisho Ngasa, Feisal Salum, David Molinga, Juma Balinya/Balama Mapinduzi na Sadney Urikhob/Desu Kaseke.Polisi Tanzania: Kulwa Said, William Lucian, Yassin Mustapha, Pato Ngonyani, Idd Mobby, Baraka Majogoo, Andrew Chamungu, Hassan Maulid, Ditram Kapama na Sixtus Sabilo/Mohamed Mkopo.
michezo
2
SERIKALI ilitenga Sh bilioni 54.5 kugharamia mafunzo ya ndani na nje kwa watumishi wa umma nchini katika mwaka 2017/18 pia imetenga Sh bilioni 39.8 katika kipindi cha mwaka 2018/19.Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Dk Mery Mwanjelwa ametoa takwimu hizo wakati kijibu swali la Mbunge wa Kuteuliwa, Janeth Masaburi.Masaburi alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kutenga fedha kwa ajili ya mafunzo ndani na nje ya nchi kwa watumishi wa umma ili kuwajengea uwezo na kuleta tija kwa Taifa.Dk Mwanjelwa alisema serikali ilitenga fedha hizo katika mwaka wa fedha 2017/18 kutokana na kutambua umuhimu wa kuwapatia mafunzo watumishi wa umma ili kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi.Alisema kwa kutambua hilo, ofisi ya rais, menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora huandaa sera, kanuni na miongozo inayohusiana na mafunzo katika utumishi wa umma na kufuatilia utekelezaji wake.Dk Mwanjelwa alisema, sera ya menejimenti na ajira ya mwaka 1999 na marekebisho yake ya mwaka 2008 kifungu namba 4.8, sera ya mafunzo katika utumishi wa umma ya mwaka 2013 kifungu 4.2 na kanuni za kudumu za utumishi wa umma za mwaka 2009 kifungu G 1 zinasisitiza kuhusu umuhimu wa kila mwajiri katika utumishi wa umma kuandaa na kutekeleza Mpango wa Mafunzo kwa mujibu wa tathmini ya mahitaji ya mafunzo.Alisema serikali imeimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali wa maendeleo hususani Australia, India, Japan, China, Indonesia, Jamhuri ya Korea ambapo katikamwaka 2016/17 kupitia wadau hao jumla ya watumishi wa umma 654 walipatiwa mafunzo ya muda mfupi na mrefu katika nchi hizo.Aidha, katika mwaka 2017/18 fursa za mafunzo zilitolewa na washirika hao ziliongezeka hadi kufikia 827.Fursa hizo zimewezesha watumishi wa umma kupata uelewa, ujuzi na maarifa mapya ya kumudu majukumu yao katika kutekeleza majengo la taifa.Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) aliyeonesha wasiwasi kwamba baadhi ya ajira serikali zinatolewa kikanda au kimikoa.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika alisema serikali ya CCM inatoa ajira kwa kuzingatia sifa haifuati mikoa, dini wala ukabila.Alisema serikali inatoa uamuzi wake kwa wakati, mfano katika Mkoa wa Kilimanjaro katika Wilaya ya Rombo waliopigana mmoja amesimamishwa kazi na mwingine yupo katika uchungzi. Pia serikali inafanya uchunguzi kutokana na uwezo na nafasi walizopo watendaji, japokuwa hao ni binadamu lakini wanazingatia msingi ya kazi.
Kitaifa
0
RAIS John Magufuli amewaweka kikaangoni wakuu wa mikoa ambayo haijaanzisha masoko ya madini na kuwapa siku saba wawe wametimiza agizo hilo, huku akiwaonya pia viongozi wote wasiotekeleza maagizo yake.Kauli hiyo aliitoa jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wilayani Chunya baada ya kuzindua barabara ya Mbeya-Chuya kilometa 72 na kuweka jiwe la msingi la kipande cha kilometa 39 Chunya-Makongorosi.Rais Magufuli alisema wananchi wanasafirisha madini kwa sababu viongozi wameshindwa kuwajengea soko la kuuza madini na kwamba wenye makosa sio wananchi bali ni viongozi hao wasioweza kutekeleza wajibu wao katika mikoa yao.Aidha, Rais Magufuli pia amekemea vitendo vya imani potofu vya ubakaji kwa watoto na mauaji ya watu kwenye ulemavu wa ngozi ambapo amewataka viongozi kutofumbia macho sheria ichukue mkondo wake.Kuhusu soko la madini, Rais Magufuli ametoa siku saba kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila kujenga soko la madini wilayani Chunya na kuwataka wakuu wengine wote wa mikoa kufanya hivyo.“Agizo hili sio kwa wachunya tu, wa Katavi ajiandae, wa Rukwa, Arusha... siwezi kuwa na wakuu wa mikoa ambao natoa maagizo hawatekelezi kwangu ni kufanyia kazi na kazi yenyewe ni kuwatumikia wanyonge walinichagua Magufuli kafunge makufuli hayo” amesema Rais Magufuli.Rais Magufuli alisema katika sekta ya madini serikali imejitahidi kuondoa kodi nyingine ili kuhakikisha wananchi wanaondokana na kero.Aidha, alisema Waziri ya Madini ameeleza kwamba Chunya ni ya pili kwa kuzalisha dhahabu na kwamba aliagiza soko la madini kujenga kila Mkoa lakini cha ajabu ni kwamba hajaona soko hilo Chunya na kwingineko.“Lakini Mkuu wa Mkoa yupo, Mkurugenzi yupo, wachimbaji wapo lakini soko hamjaanzisha maana yake nini? Sasa ninataka katika mwendo huohuo ndani ya siku saba liwe limefunguliwa,”amehoji Rais Magufuli.“Nimeshatoa maelekezo nimemaliza, jana Mkuu wa Mkoa nimekusifia lakini kwa hili hapana, kuna wakuu wa mikoa mingine wananisikia hawataki kufanyia kazi, sheria imeshapitishwa na Bunge, kama Mkuu wa Mkoa wa Geita ameweza nyie mnashindwa nini? chukua hata gari ya mkuu wa mkoa uzeni humo madini” amesema.“Barabara ya lami ipo, umeme na ninyi mpo, na mishahara mnalipwa tarehe 18, magari mnayo, kamati ya ulinzi na usalama mpaka na mabomu,” amesema Rais Magufuli na kuongeza kuwa anaamini mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya anafanya kazi nzuri lakini kwa hilo la madini hajafurahishwa nalo.Kuhusu barabara aliyoizindua,alisema barabara hizo isiwe chanzo cha ajali na kwamba itasaidia kuimarisha huduma za usafiri ambapo awali usafiri katika njia hiyo gharama ilikua kubwa na pia kulikua na ajali nyingi hasa kwenye milima.“Ilikua inachukua hata siku nzima kufika Mbeya, gharama ilikua kubwa, kwenye milima wapo watu walipoteza maisha, vijana wanaweza wasikumbuke, serikali na nyie wana Chunya sasa mmepata barabara mzuri, kikubwa mkatumie barabara katika kujenga uchumi,” alisema.Alisema wananchi wa wilaya hiyo walimchagua lakini sasa ana deni la kuwafanyia kazi watanzania pamoja na wana Chunya.Aliwapongeza wananchi wa wilaya hiyo kwa maendeleo makubwa yaliyopo sasa tofauti na hali aliyoikuta alipoenda wakati wa kampeni Tatizo la maji Rais Magufuli alisema pia kuwa wilaya hiyo anafahamu kuna tatizo la maji tatizo ambalo lipo toka Tanzania ipate Uhuru, na kwamba ameambiwa kuna mradi ambao umekamilika juzi.Rais alisema baadhi ya watendaji Wizara ya Maji sio wazuri, baadhi ya miradi ni hewa, zaidi ya Shilingi bilioni 100 amebaini ni miradi hewa hivyo inawezekana na mradi huo ukawa hewa.“Hata kama umemalizika jana, wiki iliyopita, wananchi wa Chunya wanataka kuona maji yakidondoka, Waziri wa Maji umenisikia, umeeleza kuna mradi umetokana na mkopo wa India wakati tukisubiri hayo mngetengeneza maji yafike... Hakikisha maji yashuke hapa,” alitoa maelekezo kwa Waziri wa Maji.Aliwataka kutenga fedha za dhalura kukarabati miundombinu ili maji ya kutosha yawafikie wananchi hao kwani katika ilani aliahidi katika miji maji kuwafikia wananchi kwa asilimia 85 na miji mikuu asilimia 95.Alisema haiwezekani mradi huo wa maji ukamilike lakini watu hawajayaona maji huku alisema atachunguza mradi huo kwanini ukamilike juzi, gharama yake na kwanini haujafika kwa wananchi.Ujenzi wa hospitali Katika afya, Rais Magufuli alisema idadi ya watu Chunya inaongezeka ambapo ameahidi kuongeza Sh milioni 200 katika ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo na ujenzi wa kituo cha afya cha Makongorosi Sh milioni 200. Alisisitiza hopitali ya wilaya kupanuliwa na kuwa na hadhi ya wilaya.Alisema katika afya, serikali ilitenga Sh bilioni 17 kukarabati vituo vya afya na pia kujenga hospitali za wilaya. Serikali pia imejenga na kukarabati shule mbalimbali. Aliwapongeza wananchi wa wilaya hiyo kwa jitihada zao katika kilimo. Rais Magufuli alitoa mwito kwa mara nyingine kwa viongozi kusimamia wananchi wanaosafirisha mazao yao chini ya tani moja bila kutozwa tozo zozote.“Msiwatoze tozo watu wanaosafirisha mazao yao chini ya tani moja, na niwaombe madiwani hizo ushuru zimeshapitishwa na Bunge ambalo ndio sheria mama, na tulifanya hivyo makusudi,” alisema. Aliagiza pia kwa wafanyabiashara wadogo, waliopewa vitambulisho wasisumbuliwe.“Na nyie ndugu zangu wakurugenzi muwaelimishe hawa wamama na wababa, wakati mwingine wameshapata vitambulisho bado mnawadai, akikudai wapeleke mahakamani,” alisema.Aliwaomba watanzania kuendelea kutunza amani na muungano ambao uliasisiwa na waasisi.Aidha, alisema Tanzania ni tajiri, watu wakishikamana na kutengeneza Tanzania ya kesho tutakuwa mbali.Rais aliwataka viongozi kunapotokea tatizo waangalie pia na ubinadamu na kutekeleza sheria kwa uangakifu na uaminifu huku akiwataka wananchi kuzingalia sheria.Mawaziri Awali Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa alisema mbali na serikali kutenga fedha zake kwa ajili ya kusambaza maji, lakini pia serikali imepata Sh Trilioni 1.2 kutoka serikali ya India fedha ambazo bilioni 12 zimeletwa katika wilaya hiyo.Aidha alisema maji yanazalishwa kwa wingi lakini miundimbinu ni chakavu, kazi iliyopo ni kutanua ili kuwafikia wengi pamoja na kukarabati miundombinu kuzuia upotevu wa maji.Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Profesa Paramagamba Kabudi alisema kufanikisha mambo ya ndani kuna umuhimu wa kuimarisha uhusiano na nchi za nje ambapo alisema kuna umuhimu mkubwa pia kukuza sekta ya utalii.“Pia tunatakiwa kutumia ndege kupeleka mazao ya Mbeya nje ya nchi na pia mkifungua soko la madini kutafuta wanunuzi kuja kununua na rais sasa ameanza kufanya safari za kimkakati nje ya nchi na si kusafiri tu,” alisema Profesa Kabudi.Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe alisema wananchi wa Chunya wanapata vizuri chaneli ya TBC vizuri ingawa matangazo ya radio hayafiki baadhi ya maeneo ndio maana waliomba fedha wafungue vituo vya FM radio.Waziri wa Madini, Dotto Biteko alisema sekta ya madini baada ya marekebisho ya sheria ya mwaka 2017 madini yote hapa nchini yalitamkwa kuwa ni mali ya watanzania chini ya Rais, kwa mkoa wa Mbeya, Chunya ni eneo la pili kwa dhahabu.Wachimbaji wadogo 1,167 na wakati 27, mitambo uchenjuaji 148 na mitambo 38 ya kuchoma dhahabu.Eneo lililokua lilokuwa likiongoza kwa kwa utoroshaji madini ni Chunya kwa mwaka mzima walitorosha kilo 30 za dhahabu ambapo ilichukuliwa hatua ya kufunga mitambo na sasa mambo yanakwenda vizuri.Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alisema Chunya inalima vizuri zao la Tumbaku ambapo tani 9598 kwa mwaka lakini tatizo ni masoko.Aidha alisema wilaya hiyo sasa imeanza kilimo cha korosho na kwamba katika miaka mitatu ijayo itakua kati ya watu wanaozalisha korosho kwa wingi na kwamba serikali inajipanga kwa kuwapatia mbolea wanayoihitaji.Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Miundombinu ya Bunge, Suleiman Kakoso alisema kamati hiyo haipati mashaka na serikali katika ujenzi wa miundombinu kwa sasa. Imeandikwa na Regina Mpogolo, Dar na Joachim Nyambo, Mbeya
Kitaifa
0
WAWAKILISHI pekee nchini kwenye michuano ya kimataifa, Yanga, wanatarajiwa kutoana jasho dhidi ya Pyramids ya Misri katika mchezo wa ply-off kusaka nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Kombe la Shirikisho Afrika katika mchezo utakaopigwa Jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.Yanga awali ilishiriki katika michuano ya Kombe la Ligi ya Mabingwa wa Afrika, lakini baada ya kutolewa na Zesco ya Zambia, ikaangukia katika Kombe la Shirikisho na inacheza mchezo huo wa mchujo ili kusaka kucheza hatua ya makundi.Timu itakayopata ushindi wa jumla katika mechi mbili za nyumbani na ugeni, basi itakuwa imekata tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa mgumu kwa kila upande kwa kuwa kila timu inahitaji matokeo chanya hususani kwa Yanga wanahitaji zaidi ushindi wa mabao mengi kumaliza mapema mechi kabla ya kujipanga kwa mchezo wa marudiano unaotarajiwa kupigwa Novemba 2 nchini Misri ili kutinga hatua ya makundi.Ushindi kwa Yanga ni muhimu sana hasa ukizingatia kuwa Tanzania licha ya kuingiza timu nne katika mashindano mawili ya Afrika (Ligi ya Mabingwa na yale ya Kombe la Shirikisho), lakini imebaki peke yake baada ya Simba, Azam na KMC kutolewa.ZAWADI NONOPamoja na Yanga kuangukia katika mashindano hayo ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambayo ni ya pili ukilinganisha na yale ya Ligi ya Mabingwa, bado zawadi zake ni nono endapo watafanya vizuri. Shirikisho la Soka Afrika (Caf) lilisema kuwa limetenga kiasi cha dola za Marekani milioni 14.2 (sawa na zaidi ya Sh bilioni 32), ambazo zitagawanywa kwa timu nane bora ambazo zitafanikiwa kutinga hatua ya makundi.Caf inaendelea kueleza kuwa endapo timu itafanikiwa kutinga hatua ya mtoano kutoka katika robo fainali, ambayo ni hatua ya makundi, nchi hiyo itaondoka na kitita cha dola za Marekani 800,000 (sawa na Sh bilioni 1.8).USHINDI MUHIMUAidha, wanahitaji kupata matokeo chanya ili kujihakikishia kutinga hatua ya makundi na kunyakua kitita hicho cha fedha, lakini hilo halitawezekana kama hawatapambana kufa au kupona. Yanga sio tu inahitaji ushindi, bali inatakiwa kupata ushindi mnono ili kujiweka vizuri kupata ushindi wa jumla watakaporudiana ugenini Misri.MAANDALIZI YANGAKila timu inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na morali ya ushindi baada ya kutoka kushinda kwenye michezo yao ya ligi za nyumbani wakati wenyeji Yanga wenyewe walipata ushindi kiduchu wa bao 1-0 dhidi ya Mbao ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Ligi ya ndani wenyeji Yanga walitoka kuvuna ushindi mbele ya Mbao kwa bao 1-0 mchezo wa muendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye uwanja huohuo wanaotarajiwa kuutumia kesho.Matokeo yanayowafanya kushika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi hiyo baada ya kucheza mechi nne, huku wakiwa na balaa la kuanza ligi hiyo kwa kusuasua. Aidha, wapinzani wao Pyramids nao walitoka kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya El Entag El Harby kwenye mchezo wa Ligi Kuu Misri uliopigwa Uwanja wa Al Salaam. Matokeo ambayo yanawaweka kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakiwa na hazina ya pointi 11. Kwa ujumla michezo hiyo ilikuwa ni maandalizi ya mwisho kwa timu zote kabla ya kukutana katika mpambano wa kesho wa mchujo ili kutinga hatua ya makundi.UGUMU WA MCHEZOMchezo huo utakuwa mgumu lakini Yanga kama watajipanga vizuri wanaweza kushinda, lazima wapambane na wachezaji wake wajitume mwanzo mwisho. Pyramids sio timu maarufu sana Misri, lakini ile tu kumaliza katika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu ya nchi hiyo msimu uliopita, kunatosha kabisa kuichukulia timu kwa umakini mkubwa, kwani sio timu ya kuibeza. Klabu za Misri kwa miaka mingi zimekuwa zikiisumbua Yanga bila kujali ukubwa au ukongwe wao, hivyo Yanga wanahitaji kuwa makini sana kesho wanapokutana na timu hiyo pamoja na kucheza kwenye uwanja wao wa nyumbani.Yanga wana uwezo mkubwa wa kupata ushindi kama benchi la ufundi litakuwa limefanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye michezo iliyopita ya kimataifa na ile ya Ligi Kuu Tanzania Bara, kitu ambacho kinaweza kuwapatia mabao mengi katika mchezo huo.REKODI ZA KIMATAIFAYanga pamoja na mechi za ligi kuanza kwa kusuasua, lakini kwenye mechi za kimataifa walikuwa wanaonesha uhai kwa kutoa ushindani mkubwa ingawa hawakupata matokeo ambayo walikuwa wanategemea kuyapata. Tatizo hilo linachangiwa zaidi kwa asilimia kubwa kikosi hicho kimetawaliwa na wachezaji wageni ambao wanahitaji muda wa kuzoeana na kupata muunganiko mzuri.Rekodi zinaonesha Yanga wameshinda mchezo mmoja wa mkondo wa pili dhidi ya Township Rollers kwa bao 1-0 ugenini, huku wakipoteza mechi moja mbele ya Zesco kwa mabao 2-1 ugenini Zambia na kupata sare mechi mbili dhidi ya Rollers na United yote ya mkondo wa kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa. Wakati wapinzani wao Pyramids walishinda michezo yote miwili dhidi ya Etoile du Congo kwa jumla ya mabao 5-2 na kupata ushindi wa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya CR Belouzizdadi ya Algeria na kufanikiwa kukutana na Yanga.Idadi hiyo ya mabao waliyokwishafunga inaifanya Pyramids kuwa ni miongoni mwa timu yenye safu bora ya ushambuliaji inayowafanya kuwa na wastani mzuri wa kufunga mabao matatu kwenye kila mchezo waliocheza. Rekodi ambazo zinatakiwa kuchungwa zaidi na wachezaji wa Yanga ambao safu yao ya ulinzi hadi sasa imeruhusu mabao manne ikiwa sambamba na kufunga idadi ya mabao matatu.MKALI WA PYRAMIDSPyramids wanajivunia mshambuliaji wao matata, Abdalla Said analiyeibeba timu hiyo kwa kuifungia mabao sita kwenye ligi yao ya ndani akiwa na wastani wa kufunga angalau bao moja kila mchezo. Kikosi hicho kinachonolewa na aliyewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Uganda, Sébastien Desabre kina thamani kubwa ya kifedha Sh bilioni 52.7 huku wachezaji wake 12 ni miongoni mwa nyota wanaunda kikosi cha timu ya taifa ya Misri.WANACHOTAKIWA KUFANYAKuhakikisha wanatumia vema faida ya uwanja wa nyumbani na uwingi wa mashabiki, Yanga wanatakiwa kupambana kufa au kupona ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi mnono, kwani Wamisri wanajulikana wanacheza kwao, hivyo ni muhimu Yanga wakashinda kesho. Yanga wanatakiwa kuingia uwanjani huku wakijiamini na kuondoa kabisa dhana kuwa timu za Misri hazifungiki, kwani hilo litawezekana tu kama wachezaji wake watapambana vizuri tena bila kuchoka.
michezo
2
CHUO Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani (UDSM) kinatumia maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF) kueleza namna ya kutumia majani ya miwa katika kutengeneza karatasi.Mtafiti kutoka UDSM, Said Issa alisema hayo Dar es Salaamjana katika banda la UDSM lililoko katika maonesho hayo maarufu kama sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa. Alisema wazo la kufanya utafiti huo lilitokana na kuangalia kipindi cha mavuno ya miwa katika mashamba yanayozalisha bidhaa hiyo ambapo wahusika huyachoma kwa kiwango kikubwa. Issa alisema lengo la kuchoma nyasi hizo katika mashamba hayo hutokana na kuwalinda wafugaji na wanyama hatarishi kama nyoka na kusahau kuwa hatua hiyo inasababisha athari za uchafuzi wa mazingira. Alisema athari hizo pia zinawakumba wakazi wanaozunguka shamba husika kwani kipindi cha kuchoma nyasi zilikuwa zikisababisha moshi kuzagaa hovyo na wakati mwingine moshi huo huambatana na vimelea vya nyasi na kusababisha athari za kiafya kwa jamii.Said alisema kutokana na hali hiyo, chuo hicho kikaibuka na wazo la kufanya utafiti wa kutengeneza karatasi kwa kutumia majani ya miwa, lengo likiwa ni kupunguza wigo wa kuyachoma na kusababisha athari mbalimbali.“Katika kufikia hatua ya kupata karatasi, tunachukua majani hayo makavu au mabichi na kuyakausha na kutoa nyuzinyuzi zilizopo, kisha hupikwa na kuwezesha kufikia hatua ya kupata bidhaa hiyo ya karatasi,” alisema Said ambaye ndiye mwanzilishi wa wazo la utafiti huo. Kuhusu ulinganisho wa utengenezaji wa karatasi kwa kutumia miti na majani hayo alisema kwa kutumia miti ni gharama kubwa kwa kuwa kuna vimelea ambavyo huhitajika kuondolewa tofauti na ilivyokuwa kwa kutumia majani ya miwa. Saidi alisema lengo la utafiti huo ni baadaye kuupeleka kwa jamii na kuiweza kusaidia jamii kwa kuwa karatasi hizo zinaweza kutumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kutengenezea bahasha. Aidha alisema changamoto kubwa katika kufanikisha hilo ni pamoja na kukosa fedha za kuwezesha kununua mashine ya kutengenezea karatasi hizo na hata mashine za kupikia malighafi za kutengeneza karatasi hizo.
Kitaifa
0
Mzee alisema hayo wakati alipozindua huduma za simu za mkononi za kusafirisha fedha kwa ushirikiano na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ)pamoja na kampuni ya simu za mkononi ya Zantel.Alisema alipokuwa Naibu Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2007, wabunge walikuwa wakimuuliza mara kwa mara katika kipindi cha maswali na majibu lini Serikali itazifikisha huduma za benki hadi vijijini.Aidha alisema akiwa Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walikuwa wakimuuliza mara kwa mara lini huduma za fedha za kibenki zitafika vijijini na kumpunguzia gharama za usafiri mkulima kwenda mjini.Mzee alisema jibu lake sasa limepatikana ambapo kwa sasa wateja wa Ezypesa wenye akaunti ya Benki ya watu wa Zanzibar kufanya miamala kupitia simu ya mkononi ikiwemo kujua salio katika akaunti yake pamoja na kupata taarifa fupi za akaunti zao.
Biashara
1
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustin Mahiga amekitaka Chuo cha Diplomasia nchini kutoa mafunzo mtambuka ili kukiwezesha chuo hicho kuzalisha wahitimu wanaoendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano.Mahiga aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati wa mahafali ya 28 ya chuo hicho na kuongeza kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa kuwa pia itasaidia utekelezaji wa mipango mbalimbali ya serikali iliyopo katika utekelezaji wa mpango wa uchumi wa kati kupitia viwanda ifikapo Mwaka 2025.Alisema ili kufikia malengo hayo, chuo hicho kinapaswa kufundisha diplomasi ya uchumi sambamba na uchumi wa viwanda ili kuzalisha wahitimu watakaoisaidia serikali kufikia malengo yake kwa kuwa chuo hicho kipo katika nafasi nzuri zaidi ya kufanya hivyo ikilinganishwa na vyuo vingine nchini.Balozi Mahiga alisema chuo hicho pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kina mchango mkubwa katika kukuza masuala ya kidiplomasia, kwa sasa kinapaswa kuwa mstari wa mbele kuisaidia Serikali kwa kufundisha masomo yatakayoendana na mabadiliko hayo ya kiuchumi.“Naombeni maprofesa, walimu na wakufunzi watafsiri hilo na kuja na mipango itakayosaidia kuzalisha wahitimu watakaokuwa na uwezo wa kupata mitaji lakini wawezekezaji watakaokuja nchini kuwekeza katika maeneo mbalimbali kwa kuwa mambo haya yote yanahitaji diplomasia,” alisema Balozi Mahiga.Aliwataka wahitimu pia kutumia elimu waliyoipata kuwatafuta na kuwashawishi wawekezaji wa mataifa mengine, lakini pia kutambua heshima iliyonayo Taifa katika utatuzi wa migogoro mbalimbali na kuitumia nafasi hiyo kuilinda na kuiendeleza.Kwa upande wake, Mkuu Chuo cha Diplomasia, Dk Bernard Achiula alisema katika kuhakikisha chuo hicho kinaenda sanjari na mipango ya serikali kinatarajia, katika mwaka ujao wa masomo kitaongeza udahili wa wanafunzi hatua ambayo pamoja na mambo mengine kitasaidia kuzalisha wahitimu wa kutosha katika soko.Alisema hatua hiyo inatokana na mipango ya serikali ya kukiboresha chuo hicho baada ya kukipatia fedha za ujenzi wa majengo mbalimbali kiasi cha Sh bilioni mbili, jambo litakalosaidia kuongeza nafasi ya udahili kwa wanafunzi chuoni hapo.Aidha alisema katika kutimiza majukumu yake ya utoaji elimu, chuo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo mbalimbali yakiwemo ya ushauri wa kitaalam, pamoja na elimu ya mahusiano, hatua iliyokifanya kizidi kujizolea sifa mbalimbali ndani na nje ya taifa.Naye Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Balozi Ombeni Sefue, pamoja na kuipongeza serikali kwa juhudi mbalimbali inazozifanya kukiboresha chuo hicho, alisema matarajio ya mbeleni kwa chuo hicho ni kuzalisha wahitimu watakaoleta tija kwa taifa.Alisema katika kufikia malengo ya serikali ya kuzalisha wataalam hao, chuo hicho kimeendelea kujikita katika mipango mikakati mbalimbali yenye lengo la kuendana na kasi ya mabadiliko ya serikali ya awamu ya tano ili kuliletea maendeleo taifa.
Kitaifa
0
['Tottenham wanasuka mipango ya kumrejesha mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 30, kabla ya dirisha la usajili kufungwa mwishoni mwa mwezi. (Express)', 'Manchester United wanaweza kumtimua kocha Ole Gunnar Solskjaer iwapo matokeo yao hayataboreka msimu huu, huku kocha timu ya taifa ya England Gareth Southgate akipigiwa upatu kumrithi Solskjaer. (Mail)', 'Barcelona hawatarajiwi kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, na badala yake wanaelekeza nguvu zao kwa mshambuliaji wa Valencia Rodrigo Moreno, 28. (Sport)', 'Aubameyang hata hivyo anaweza kusajiliwa na Paris St-Germain kama mbadala wa mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 32. (Foot Mercato - in French)', 'Cavani, anahusishwa na uhamisho kuelekea klabu kadhaa zikiwemo Chelsea na Manchester United. Mchezaji huyo amekubali, japo kwa mdomo tu, kuhamia klabu ya Atletico Madrid kabla ya dirisha la usajili kufungwa mwishoni mwa mwezi. (Goal.com)', 'Cavani amekataa mapendekezo ya mkataba wa mshahara wa Pauni milioni 10 kwa mwaka na marupurupu tele uliowasilishwa na Manchester United. (Mirror)', 'Tottenham na Aston Villa wamegonga mwamba kumsajili mshambuliaji wa Serbia Aleksandar Mitrovic baada ya timu hizo kushindwa kutoa dau la Pauni milioni 40 kwa klabu ya Fulham.', 'Arsenal wanakaribia kumsajili beki wa Flamengo ya Brazil Pablo Mari, 26. (Mail)', 'Mitrovic, 25, anaweza kuchagua kuikacha Fulham mwishoni kwa msimu endapo klabu hiyo itashindwa kupanda daraja na kurudi katika Ligi ya Primia. (Star)', 'Manchester United bado wanavutiwa na kiungo wa Sporting Lisbon Mreno Bruno Fernandes, 25, lakini klabu hizo mbili bado hazijaafikiana juu ya bei ya usajili wa kiungo huyo. (A Bola - in Portuguese)', 'Marcos Rojo, 29, anarejea kwa mkopo katika klabu Estudiantes - baada ya Manchester United kushindwa kupata klabu inayotaka kumnunua beki huyo wa Argentina. (Mirror)', 'Southampton wamefanya mazungumzo zaidi na Tottenham juu ya usajili wa beki wa pembeni Kyle Walker-Peters, 22. (Mail)', 'Birmingham City wanatarajiwa kukataa ofa za usajili wa mchezaji wao kinda Jude Bellingham, 16, wakiamini kuwa wanaweza kuendelea kubaki naye licha ya kunyemelewa na vigogo Manchester United na Liverpool. (90 Min)', 'Unaweza Kusoma:']
michezo
2
MAENEO takribani 9 katika hotuba ya Msemaji Mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jana, yalikataliwa kusomwa na Kiti cha Spika kutokana na kukiuka taratibu za Bunge.Kabla hajaanza kusoma hotuba yake, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu alimtaarifu Msemaji wa kambi hiyo, Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe (Chadema), kuondoa maeneo hayo. Pamoja na kuambiwa kuondoa maneno hayo, Mwambe alipoanza kuhutubia, alikatizwa na Mwenyekiti kwa kukiuka amri, lakini akajirekebisha na kuendelea kusoma.Maeneo yaliyoondolewa ni kifungu cha 3,4,5,6, 81,82,83,84, na 85. Pamoja na kuondolewa kwa vipengele hivyo, kambi rasmi katika hotuba yake ilipongeza Jeshi la Ulinzi na Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa utumishi wao uliotukuka katika kuilinda Tanzania.Aidha kambi hiyo imelitaka jeshi kujikita zaidi katika sayansi na teknolojia jeshini ili liwe kitovu cha fikra na ugunduzi, hivyo kuwezesha fursa mbalimbali za kiuchumi kwa wananchi.Akizungumzia mafunzo ya JKT, Mwambe alisema kwamba ipo haja ya mafunzo hayo ya kijeshi kuchanganywa na programu za ufundi za Veta ili wahitimu waweze kujitegemea katika ajira halali pindi wanapomaliza mafunzo yao. Aidha, msemaji huyo alisema kwamba kambi rasmi ya upinzani bungeni inaitaka serikali kuiongezea bajeti Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Kitaifa
0
KAMATI ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashehe imesema itamkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kamishna wa Polisi, Diwani Athumani orodha ya majina ya vigogo wanaoendekeza tabia za kula rushwa kutoka katika taasisi zote za serikali ikiwamo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu inayoshirikisha maaskofu na mashehe, William Mwamalanga alisema jana kuwa wapo wanasiasa, wajumbe wa bodi mbalimbali pamoja na wafanyabiashara waliopo kwenye mtandao wa rushwa pamoja na kukwepa kodi uliotengenezwa mahususi kuinyima serikali mapato stahiki.Aliutaja mtandao huo kuwa upo kwenye mikoa ya Kagera, Arusha, Mbeya, Unguja na Morogoro, na ile ya kikodi ya Kinondoni na Ilala, ambao alipendekeza watendaji walioikumbatia rushwa kwenye taasisi za umma wafilisiwe mali zao zilizopatikana kwa njia ya rushwa kwa kuwa kuwasimamisha kazi peke yake sio njia mbadala.“Tunampongeza Rais kwa hatua aliyoichukua hapo jana (juzi) ya kufanya mabadiliko kwenye utendaji kwa kuwa yanalenga kuleta mabadiliko stahiki ya kiutendaji, tunampongeza kwa kumtumbua kigogo wa TRA, Charles Kichere,” alisema askofu huyo.Alipendekeza kuwa mamlaka za kiutendaji kuwaajiri watendaji wake kwa mkataba wa miaka miwili miwili ikiwa kama njia mojawapo ya kupima utendaji kazi wao. Pia aliwataka wanasiasa wa chama tawala, CCM kuacha malumbano na vikao vya kusaka urais, badala yake washirikiane na Rais John Magufuli kutatua kero katika jamii.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na ilisisitiza kuwa kumekuwa na hali ya taharuki kwa baadhi ya wanachama kuanza kupanga mipango ya kutaka urais ilhali muda bado na kwa sasa wanapaswa kumsaidia Rais Magufuli kuleta maendeleo.Mwamalanga alisema Rais Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kupigania maendeleo ya nchi na hasa katika kukusanya kodi na kukabiliana na rushwa, na kuwa kamati hiyo ipo tayari kufanya naye kazi bega kwa bega kuwafichua wala rushwa na wakwepa kodi nchini.Kwa upande wake, Shehe Maulidi Mahmoud na mwenzake, Profesa Athumani Mali, walibainisha kuwapo kwa njia mbovu za ukwepaji wa kodi, ambazo wafanyabiashara wanaficha makontena ya bidhaa zao kisiwani Zanzibar na kisha huziingiza Dar es Salaam kwa njia za panya hasa kupitia bandari bubu za Msasani, Kigamboni na Bagamoyo.Waliitaka serikali kuweka ulinzi makini kwenye fukwe hizo ikiwa ni pamoja na kufumua misitu ya wakwepa kodi Zanzibar ambako ni hatari kwa ukwepaji wa kodi. Kamati hiyo pia imemtakia heri na baraka Rais John Magufuli ikiwa ni baada ya kuridhishwa na utendaji kazi
Kitaifa
0
MKUTANO wa Rais John Magufuli na wafanyabiashara umeibua mambo mazito ikiwamo udanganyifu na ukwepaji kodi unaofanywa na wafanyabiashara huku baadhi ya taasisi na watendaji serikalini wakinyooshewa vidole kuchangia hali hiyo.Kwenye mkutano huo uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana ambao Rais Magufuli alisema anataka akitoka madarakani aache mabilionea Watanzania zaidi ya 100, alifichua wafanyabiashara wenye vitabu vya fedha zaidi ya kimoja kwa lengo la kukwepa kuwasilisha serikalini kodi stahiki.Kwa upande wao, wafanyabiashara walizilipua baadhi ya taasisi na mamlaka za serikali ikiwamo Mamlaka ya Mapato (TRA) na bandari wakisema baadhi ya watumishi wanachangia ukwepaji kodi kutokana na kuwawekea mazingira magumu yanayoshawishi watoe rushwa.Wanavyokwepa kodi Akimulika mambo yanayokwamisha biashara nchini, Rais Magufuli alisema changamoto zipo kwa wafanyabiashara wenyewe na pia kwa serikali. Upande wa wafanyabiashara alisema baadhi wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali kukwepa kodi ikiwamo kuwa na vitabu vya mapato zaidi ya kimoja.Alitaja baadhi ya kampuni zinazodaiwa kufanya ‘mchezo huo’ mchafu, kwamba zimekuwa na kitabu cha benki; kingine chenye hesabu za kweli ambacho ndicho chenye faida na cha TRA. Vile vile imebainika kuwapo kampuni 17,447 zinatuhumiwa kufanya biashara hewa ambazo ameagiza kama zilikwepa kitu chochote, zijipange kulipa ndani ya siku 30.“Baadhi yenu siyo waaminifu mnakwepa kodi; wengine mnafanya udalali na kufanya vitendo vya ushirika wa uhalifu,” alisema. Alisema wapo wafanyabiashara waliobinafsishwa viwanda na kupewa kuendeleza ardhi lakini hawajafanya hivyo badala yake wameuza mitambo na kutumia maeneo waliyopewa kukopa benki kuendeleza shughuli tofauti.Magufuli alisema anazo taarifa za baadhi ya wafanyabiashara waliojenga viwanda kama geresha na kuvitumia kupokelea bidhaa kutoka nje bila kulipa kodi kana kwamba bidhaa hizo zimetengenezwa nchini. Alisema upo ununuzi hewa hasa kwenye madini na viwanda ambako baadhi wanaanzisha viwanda na kudanganya gharama ya vifaa ili wakidai VAT wapate kiwango cha juu zaidi.Wafanyabiashara wengine wanadaiwa kufanya mauzo ya bidhaa na kukusanya VAT lakini hubaki na fedha bila kuziwasilisha serikalini. Vikwazo serikalini Akizungumzia upande wa serikali, Rais Magufuli alitaja utitiri wa taasisi za udhibiti akisema zimekuwa nyingi na wakati mwingine zinaingiliana. Alitoa mfano wa taasisi hizo ni pamoja na TBS, TFDA, OSHA, ofisi ya Mkemia Mkuu, NEMC, Wakala wa Vipimo, Tume ya Ushindani, Ewura na Sumatra.“Taasisi hizi wakati mwingine zimekuwa kikwazo cha kuanzisha na kuendesha shughuli za biashara nchini kwa kuwa zinahusika kutoza tozo na ada mbalimbali,” alisema. Alisema tatizo halipo kwenye udhibiti pekee bali pia kwenye taasisi za ukuzaji na urasimishaji ambako alitoa mfano wa Tirdo, Temdo, CAMATEC na kusema kutokana na utitiri z hazihudumiwi na hivyo kushindwa kutimiza majukumu yake.Changamoto nyingine inayoathiri biashara ni utitiri wa kodi, tozo, ushuru na ada ambao unachangiwa pia na utitiri wa taasisi ikiwamo mamlaka za serikali za mitaa ambazo zimekuwa zikiamrisha ushuru na tozo nyingi wakati mwingine bila kuwasiliana na serikali kuu hivyo kubebesha wafanyabiashara mzigo mkubwa. Rushwa kwa baadhi ya watumishi ni changamoto nyingine aliyoitaja Rais Magufuli ambako alitoa mfano wa rushwa bandarini, TRA, kwenye vizuizi vya barabarani na mipakani.Alisema licha ya jitihada zinazofanywa na serikali kukabili vitendo hivyo, wapo watu hususani watumishi wachache wanaoendeleza rushwa. “Ndiyo maana Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru yupo hapa ikiwezekana wala rushwa muwataje akashughulike nao. Nina imani wafanyabiashara hamtakuwa wanafiki mtasema ukweli mzizi wa fitna tuumalize leo,” alisema Magufuli.Rais Magufuli alitaja pia kutokuwapo mikakati madhubiti kuendeleza wafanyabiashara wadogo na wa kati ikiwa ni pamoja na kushindwa kuwajengea maeneo ya biashara. “Tunawaacha wahangaike katika maeneo yasiyo rasmi. Hata TRA imeshindwa kuwatambua. Ndiyo maana wigo wa walipa kodi ni mdogo,” alisema na kutaja pia ukosefu wa mitaji kuwa kikwazo kingine.Alisema taasisi za kifedha zimekuwa na mitaji midogo na wakati huo huo zikitoza riba kubwa huku nyingi zikiendesha shughuli zake zaidi mjini na kushindwa kujitangaza kwa walengwa. Vikwazo vingine vya biashara kwa upande wa serikali ni uwapo wa mifuko zaidi ya 17 ambayo alisema hana uhakika kama walengwa wanaifahamu.Mifuko hiyo ni pamoja na mfuko wa kutoa mikopo kwa wajasiriamali; Kilimo Kwanza; Mzunguko katika mikoa; Maendeleo ya vijana; Maendeleo ya wanawake; Mfuko wa taifa wa kuendeleza wajasiriamali wananchi; Mfuko wa pembejeo wa taifa na Mfuko wa kusaidia kilimo cha mboga na maua. “Sina uhakika kama walengwa wanafahamu mifuko hii. Lakini ipo na inawekewa fedha sina hakika hata wanaofaidi mifuko hii kama ni walengwa wenyewe.Hata mawaziri na makatibu wakuu hawawezi wakakupa majibu ni wangapi wamenufaika,” alisema na kusisitiza kuwa upo umuhimu wa kuunganisha mifuko hiyo. Magufuli alisema pia serikali kupitia Benki Kuu (BoT) imekuwa ikikopa fedha nyingi kwa ajili ya kukopa kuwapatia wajasiriamali lakini hakuna hakika kama fedha hizo zinawafikia. Changamoto nyingine aliyotaja ni mawakala wa Shirika la Viwango (TBS) nje ya nchi kutokuwa waaminifu kutokana na kuidhinisha bidhaa lakini zikifika nchini zinaonekana hazina viwango.TRA, bandari walipuliwa Wakichangia, baadhi ya wafanyabiashara walikiri kuwapo ukwepaji kodi huku wakilipua taasisi na mamlaka kadhaa ikiwamo TRA ambazo baadhi ya watumishi wanatengeneza mazingira magumu ili wawape rushwa. “TRA (Mamlaka ya Mapato) ina usiri mkubwa …Naamini asilimia 99 ya wafanyabiashara wana madhambi ya ukwepaji wa kodi na sababu kubwa ni usiri wa TRA… Kuna baadhi ya wafanyakazi wasio waaminifu,” alisema mfanyabiashara Hussein Nassoro. Nassoro ambaye ni Mbunge wa Bukombe, alitoa mfano, wakati mwingine wafanyabiashara hujikuta wanaingiza nchini kontena zenye mali zinazofanana lakini hulipa gharama zisizofanana. “Naamini usiri ukiondoka, tutakusanya kodi nyingi.Kwa nini kusiwe na mfumo ulio wazi wa kueleza kuwa kontena fulani la bidhaa fulani ushuru wake ni kiasi fulani?,” alihoji na kusisitiza kuwa fedha nyingi za serikali zinapotea. MfanyabiasharaJoseph Musukuma alinyooshea kidole kitengo cha ukadiriaji na hesabu cha TRA na kumuomba Rais Magufuli ikiwezekana kivunjwe.“Hawa watu wa kati, ukiondoa ngazi ya makamishna, ni tatizo,” alisema.Alitoa mfano wa kiwanda katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam kilichofungiwa shughuli zake baada ya watumishi kukikadiria kiwango kikubwa cha kodi. Rais Magufuli alimtaka Kamishna wa TRA kueleza ni namna gani suala hilo lilitatuliwa. Kamishna alikiri suala hilo kufika kwake na kwamba lilitatuliwa na kamishna wa kodi za ndani. Kamishna wa kodi ambaye alikuwapo kwenye mkutano huo, alikiri kujadiliana na kumwamuru meneja wa kodi Kariakoo kurekebisha kodi hiyo. Rais alihoji sababu ya Meneja wa Mkoa wa kikodi Ilala kutoa makadirio yasiyoakisi uhalisia. “Kwa nini atoe assessment anayojua kwa dhamira yake haipo? Huyo meneja mshushe cheo akawe chini na muhamishe hapo,” Rais aliamuru.Magufuli ambaye alitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza waliotoa makadirio hayo, alisema “Kuna mameneja wa TRA wanatoa assessment ya juu kumkatisha tamaa mfanyabiashara na kwa ajili ya kutaka rushwa.” Alisisitiza kuwa serikali inahitaji wafanyabiashara kwa sababu inakusanya mapato Sh trilioni moja na inataka yafikie Sh trilioni tatu lakini yapatikane kwa haki.“Watu wa TRA wanazungumza kwa gharama ya juu ili wahongwe na wakifika wanasemna ‘Hapa Kazi Tu…’ Lazima niwaeleze ukweli msipowashughulikia ninyi nitawashughlikia ninyi,” aliwaambia watendaji wakuu wa mamlaka. Kwa upande wa bandari, Musukuma alihoji sababu ya kontena kuelekezwa kwenda bandari za nchi kavu licha ya eneo la bandari kutojaa.“Ukiritimba uliopo unalipa dola 40 kwa siku saba na baada ya hapo unaanza kulipa dola 80,” alisema Musukuma. Vile vile alimuomba rais kutuma kikosi kidogo cha jeshi kwenda kusimamia ununuzi wa dhahabu kwa kile alichosema taarifa za mauzo zinazotolewa haziakisi uhalisia. Mzindakaya alipua Miongoni mwa wafanyabiashara waliochangia ni pamoja na Dk Chrisant Mzindakaya kutoka Rukwa aliyesema wizara inayoangusha nchi tangu nchi ipate uhuru, ni ya kilimo. Mzindaya ambaye amewahi kuwa mbunge anayejishughulisha na kilimo na kuendesha kiwanda cha nyama, alisema: “Waziri mpya aamke. Nimeshamwambia niko tayari kumshauri. Mimi sijazeeka naweza kukushauri na siombi kazi, nashauri tu.Maana napenda unavyoendesha nchi.” Mbunge huyo wa zamani alihoji pia sababu za kutumia fedha za kigeni kuagiza vyungu vya maua kutoka nje na maua bandia wakati bidhaa hizo zinapatikana nchini. “Juhudi za nchi za kujenga miundombinu faida yake itaonekana kesho si leo. Tunaomba fedha za kigeni zitumike vizuri. Kwa nini tuagize vyungu vya maua kutoka nje? “Vijana wanatengeneza vyungu kila barabara.Mimi ni shahidi, natumia maua ya Mungu situmii ya bandia. Tuache kutumia fedha zetu vibaya. Kwa nini tuagize ya bandia kutoka nje wakati yamejaaa ndani?” Wilbard Mdee kutoka Kilimanjaro alimuomba Rais wafanyabiashara wadogo wapewe miezi sita tangu wanapoanza biashara kabla ya kuanza kutozwa kodi. Aliomba VAT ipunguzwe hadi asilimia 16. “Asilimia 18 ni kubwa ndiyo maana watu wanatengeneza vitabu vingi,” alisema.Kwa upande wake, Saul Amon kutoka Mbeya alikiri kuwa utiriri wa taasisi zinazosimamia biashara unachangia nchi kukosa mapato kutokana na wafanyabiashara wengi kutopenda kusumbuliwa. Aliomba TBS kufanya kazi kama ilivyo TFDA kwa maana ya kufanya ukaguzi wao nchini kuliko kukaguliwa nje ya nchi. “Mfano mimi nachukua mzigo SADC ambako hakuna kodi.Lakini ukifika hapa nchini unakuja kulipa faini ya TBS…lakini wasioweza lazima wapite njia za vichochoro,” alisema. Amon alisema ukaguzi nje ya nchi ni kazi kubwa kiasi kwamba mtu hawezi kusubiri takribani miezi minane ndip mizigo yake ikaguliwe. Awali, akifungua mkutano huo, Rais Magufuli alishukuru mwitio wa wafanyabiashara hao kushiriki licha ya mwaliko kuwa wa muda mfupi.Alisema kikao hicho ni mwendelezo wa vikao ambavyo amekuwa akifanya na makundi mbalimbali. Alisema tangu aingie madarakani amekuwa akikutana na makundi mbalimbali wakiwamo wazee, watendaji wa idara, wafanyakazi, viongozi wa dini, wakulima wanamichezo kubadilisha mawazo juu ya namna ya kuiletea nchi maendeleo. “Leo nimeamua kukutana na wafanyabiashara kujua changamoto zenu; nisikilize kutoka kwenu mawazo yenu na ushauri wenu ili tufike mahali upande wa serikali na wafanyabiashara tuelewane vizuri,” alisema.Rais Magufuli alisema anafahamu sekta binafsi inachangia kitu kikubwa katika uchumi wa nchi. Alisema ili shughuli za biashara zistawi zinahitaji amani na usalama ndiyo maana serikali imekuwa ikilinda na kushughulikia usalama wa nchi. Alisema serikali itaendelea kufanya marekebisho katika viwango vya kodi na tutaendelea kufanya marekebisho. Idadi na viwango vya kodi ni kichocheo cha kukuza au kudumaza biashara. Kodi zikiwa chache na viwango kuwa vikubwa vinadumaza biashara.
Kitaifa
0
TIMU ya Taifa ya soka ya wanawake chini ya umri wa miaka 17, leo inatarajia kushuka kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kucheza na timu ya Burundi katika mashindano ya kufuzu Kombe la Dunia 2020 nchini India.Mchezo huo ambao ni wa hatua ya awali unatarajiwa kuwa na ushindani kwa sababu timu hizi zinafahamiana na mara ya mwisho kukutana ni mwezi uliopita katika mashindano ya Cecafa yaliyofanyika nchini Uganda na kumalizika kwa sare ya mabao 3-3. Baada ya mchezo wa leo timu hizi zitarudiana kati ya Januari 24, 25, na 26 Bujumbura, Burundi na mshindi atakutana na mshindi kati ya Uganda dhidi ya Ethiopia.Akizungumza jana kocha wa timu hiyo Bakari Shime alisema wanatarajia kushinda mchezo kwani wanawafahamu vema washindani wao na hivi karibuni walikutana nao pia makosa yaliyowafanya kutoka sare wameyafanyia kazi.“Burundi tunaifahamu vizuri kwani tulikuwa nayo katika mashindano ya Cecafa U17 yaliyofanyika mwezi uliopita nchini Uganda, na tulitoka sare ya kufungana mabao 3-3, makosa yaliyojitokeza hadi wakasawazisha niliyaona na niliyafanyia kazi hivyo mchezo ujao tutafanya vizuri,” alisema Shime.Pia Shime alisema wachezaji wote wako vizuri na wana ‘mechi fitinesi’ na hakuna majeruhi hivyo anaomba sapoti ya mashabiki ukizingatia hakuna kiingilio. Naye nahodha wa timu hiyo Irene Kisisa alisema wamejiandaa vya kutosha hivyo kesho (leo) wana kila sababu ya kushinda mchezo huo.“Tumepata maandalizi mazuri na tumekaa kambini kwa muda mrefu hivyo tunaamini tutapata ushindi katika mchezo wetu ili tusonge mbele,” alisema Irene.Pia aliwaomba Watanzania wajitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo na kuwapa nguvu w kwa kuwashangilia kwani hakuna kiingilio isipokuwa VIP B Sh 2000 na VIP A Sh 5000.
michezo
2
Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa kongamano la pili la biashara kati ya Tanzania na China juzi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye alisema taasisi hiyo inakaribisha wawekezaji kutoka nchi hiyo katika juhudi za kufikia maendeleo endelevu hapa nchini.Kongamano hilo lilishirikisha kampuni zaidi ya 100 kutoka China na kampuni zaidi ya 120 za kitanzania.Hadi sasa China imesajili miradi 522 kwenye Kituo cha Uwekezaji(TIC) yenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 2.4 ambayo inatarajiwa kuzalisha ajira 77,335.“Tunahitaji uwekezaji wao ufikie dola za kimarekani bilioni tano katika kipindi cha miaka mitatu ijayo,” alisema.Alisema sekta binafsi inapenda waje kuwekeza zaidi katika sekta ya viwanda na siyo kutumia fursa waliyopewa na watanzania kuja kuuza bidhaa zao.Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Raymond Mbilinyi alisema Tanzania imejitahidi kwa kiasi kikubwa kuboresha mazingira ya biashara ambayo yanavutia wawekezaji kutoka nchi mbalimbali kuja kuwekeza kwa faifa ya nchi na wawekezaji.
Biashara
1
Katika hafla hiyo ya chakula cha usiku iliyofanyika hoteli ya Serena, wafanyabiashara hao wa makampuni makubwa hamsini ya Ufaransa wakiongozwa Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak walikula huku wakitumbuizwa na mwanamuziki gwiji nchini Zahiri Ally Zoro.Akizungumza kabla ya kukaribisha wageni wake katika chakula hicho, Mengi amesema kiotendo alichokifanya ni njia mojawapo ya kuonesha shukurani kwa wafanyabiashara hao kwa kuamua kuja nchini kuwekeza.Alisema: "Jioni hii ya leo sina maneno mengi ya kuzungumza zaidi ya kuwakarimu wageni hawa ambao ni muhimu sana kwa Watanzania, sekta ya uchumi na taifa kwa ujumla."“Ujio wenu nchini ni wa kufurahisha sana, utatunufaisha taifa na nyie pia; hii ndiyo tunayoita win win situation,” amesema Mengi na kuongeza kuwa ujio wao utasaidia kujenga uwezo wa teknolojia wa taifa hili wakati taifa linaelekea katika uchumi wa viwanda.Aidha amesema kwa kuwa Ufaransa ni miongoni mwa mataifa yenye msuli wa kiuchumi na kwamba kwa kuwa rafiki wa Tanzania kutasaidia Watanzania kuwa na rafiki mwenye uwezo wa kuwasaidia kuwa na uwezo pia.Amesema uhusiano wa Tanzania na Ufaransa una historia yake na kwamba kwa sasa utaendelezwa zaidi. Naye Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak alisema kwamba amefurahishwa sana na ukarimu wa Dk Mengi na kusema kwamba yeye anaamini biashara na urafiki ni kitu muhimu katika kuimarisha mahusiano.“ …Business and friendship goes together.(biashara na urafiki vinakwenda pamoja).” amesema balozi huyo na kuongeza kwamba kutokana na chakula hicho anaamini kwamba urafiki wa watu wa Ufaransa na Tanzania si wa kubahatisha unakua.
Biashara
1
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa mfumo huo unaotarajiwa kuanza mwaka huu utasaidia wakulima kuwa na soko la uhakika, bei nzuri na inayostahili. Alisema hayo baada ya kufungua warsha iliyolenga kuzungumzia mfumo wa soko la bidhaa, faida na changamoto zake.“Ni kwa kufanya hivi ndipo wakulima wataanza kuona kilimo kama biashara nyingine na kufanya maamuzi sahihi ya kuwekeza na hivyo kuimarisha sekta hiyo na kupambana na umasikini,” alisema Sefue.Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Kiongozi, tayari serikali imeshawekeza fedha nyingi kuhakikisha mfumo huo unaanza nchini ambapo tayari kampuni inayoitwa Tanzania Mercantile Exchange Public Limited Company imeshasajiliwa ili kusimamia mfumo huo.Katika kampuni hiyo, serikali ina asilimia 49 wakati wadau toka sekta binafsi nchini kama ushirika na vyama vya wakulima wana asilimia 51 ya hisa. “Serikali inafanya juhudi kubwa kuhakikisha mfumo huu muhimu unaanza haraka,” alisema.Mfumo huu unawezesha wauzaji na wanunuaji kukutana na kufanya biashara kwa uwazi na kwa kufuata taratibu maalumu zilizowekwa. Nchi kama Ethiopia zimefanikiwa sana katika kuendeleza sekta yake ya kilimo na kufaidisha wakulima wake.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Soko la Mitaji (CMSA), Nasama Massinda alisema mfumo wa soko la mitaji ni muhimu katika kufanikisha sera ya taifa ya Kilimo Kwanza. Alisema kampuni hiyo itaanza na bidhaa zilizo chini ya mfumo wa stakabaadhi ghalani kama korosho, alizeti na mpunga.“Bidhaa nyingine zitaongezeka kadiri mfumo huu utakavyokuwa unakomaa,” alisema. Alisema mfumo huu utasaidia kuleta uwazi, bei nzuri, kupunguza mianya ya rushwa na kuongeza kuaminiana miongoni mwa wadau kwa ujumla.Mshiriki mmojawapo wa warsha hiyo, James Shimbe alisema mfumo huo utasaidia kuimarisha vipato vya wakulima. “Hii ni hatua nzuri…tunaiunga mkono,” alisema Shimbe ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma na Usimamizi, Bodi ya Pamba Tanzania.Washiriki wa warsha hiyo walikuwa ni pamoja na maofisa waandamizi wa serikali, sekta binafsi, muungano wa vyama vya Ushirika, chama cha wafanyabiashara, viwanda na kilimo (TCCIA) miongoni mwa wengine.
Biashara
1
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, Dk. John Pima amesema eneo hilo ni la kimkakati kibiashara na kiuchumi.Amesema, Kaliua ni 18.8% ya eneo la mkoa wa Tabora, linafaa kwa uwekezaji kwenye sekta mbalimbali, kuna malighafi za kutosha na miundombinu rafiki.“Tunazo fursa nyingi kwa Kaliua , nyingi sana, nyingi sana, nyingi sana, Kaliua kama tulivyosema jiografia yake inaipendelea sana Kaliua kwa maana kwamba, kwanza Kaliua inafikika kirahisi, inafikika kirahisi kwa sasa kwa maana kwamba kuna barabara kuu inayotoka Tabora kufika hapa Kaliua, nyingine inamaliziwa upande wa matengenezo kutoka Urambo kuja Kaliua kilomita 30 ndiyo zipo na mkandarasi atazimalizia wakati wowote” amesema Dk. Pima.Ameyasema hayo wakati akizungumza na timu ya kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN) iliyopo Tabora kuzitangaza fursa za biashara na uwekezaji zilizopo mkoani humo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Jukwaa la Fursa za Biashara za Uwekezaji litakalofanyika kuanzia Novemba 21 hadi 23.“Lakini tunafikika pia kwa njia ya reli, reli inatoka Dar es Salaam mpaka hapa, utoke Mwanza pia unafika moja kwa moja mpaka hapa. Lakini jambo lingine linaloifanya Kaliua iwe ni strategic point (eneo la kimkakati) ni standard gauge, ile standard gauge ambayo inajengwa itakuwa na hub kaliua, kwa hiyo standard gauge ikifika Kaliua inagawanyika inaelekea Mpanda na inaelekea pia upande wa Kigoma. Kwa hiyo chochote kitakachofanyika Kaliua kitafika popote Tanzania na nje ya nchi kwa uharaka zaidi kuliko maeneo mengine ambayo yapo katika kanda yetu hya magharibi” amesema.Amesema Kaliua pia ina misitu ya miombo iliyopo katika sehemu ya asilimia 89 ya eneo la Mkoa wa Tabora linalotumika kwa hifadhi na kwamba, eneo hilo lina mvua nyingi na za uhakika kuliko sehemu yoyote ya Tabora hivyo ni eneo la uhakika kuwekeza katika kilimo.“Kilimo tunafanya vizuri sana ndiyo maana umeona Kaliua imekuwa ya nne kimapato kitaifa kwa maana kwamba performance yetu inategemea kilimo na shughuli na products (bidhaa) zinazotokana na kilimo na hivyo sasa yeyote ana-invest (anayewekeza) hapa hawezi aka-regret (akajuta), hawezi akajuta” amesema Dk. Pima.Amesema, Kaliua pia eneo bora la kuwekeza kwenye sekta ya nyama na ranchi kwa kuwa kuna ng’ombe zaidi ya 500,000 wanaolishwa vizuri kwa kuwa kuna majani mengi kutokana na wingi wa mvua.“Kwenye mazao ya ng’ombe kuna ngozi, lakini sehemu ambayo tunahitaji sisi pia tumefanya maandalizi makubwa ni investment (uwekezaji), ni uwekezaki katka sekta ya kilimo”amesema.
Biashara
1
KIFO cha bilionea maarufu nchini Tanzania na Afrika Mashariki na mmiliki wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi, kimewashtua wengi, huku akiwa ameacha pengo kubwa katika maeneo ya biashara na vyombo vya habari.Dk Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni hayo ya IPP, alifariki dunia usiku wa kuamkia jana Dubai katika Falme za Kiarabu baada ya kuugua muda mfupi. Mfanyabiashara huyo anayemiliki vyombo mbalimbali vya habari amefariki, ikiwa ni takribani miezi sita tangu kifo cha aliyekuwa mtalaka wake, Mercy Mengi aliyekutwa na umauti akiwa Afrika Kusini.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na familia yake, Dk Mengi aliyezaliwa mwaka 1942 mkoani Kilimanjaro, alikutwa na umauti wakati akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mfupi.Dk Mengi, mwandishi wa kitabu cha I Must, I Can, I Will kinachoelezea safari ya maisha ya dhiki akiwa mtoto hadi kuwa msomi mkubwa wa fani ya uhasibu na kisha tajiri, maisha yake yatakumbukwa na mambo mbalimbali, yaliyosaidia kukuza uchumi wa Taifa sambamba na misaada ya kijamii kwa watu wasio na uwezo.Rais Magufuli amlilia Rais John Magufuli ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya Dk Mengi na Watanzania wote kutokana na kifo hicho, huku akielezea mambo mengi yaliyofanywa na Mengi wakati wa uhai wake. Kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Rais Magufuli alisema ataendelea kumkumbuka Mengi kwa mchango wake katika maendeleo ya taifa lake.Kupitia ukurasa huo, Rais Magufuli ameandika “Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Mzee na Rafiki yangu Dk Reginald Mengi. Nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Taifa letu na maono yake yaliyopo katika kitabu chake cha I Can, I Will, I Must. Poleni wanafamilia, wafanyakazi wa IPP na Jumuiya ya Wafanyabiashara”.Viongozi wazungumza Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbas pia ameandika kupitia ukurasa wake wa Twitter akitoa salamu hizo za rambirambi, akinukuu kauli yake aliyowahi kuitoa wakati wa uhai wake. “Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mwenyekiti wa IPP, Mzee Reginald Mengi. Kama alivyopata kusema yeye mwenyewe siku za uhai wake kuwa watu wanaoacha alama hawafi, basi mawazo, falsafa, ubunifu na kujitoa kwake vitaendelea kuishi nasi,” alisema Dk Abbas kupitia ukurasa wake huo wa mtandao wa kijamii.Mbali na hao, kifo cha Mzee Mengi kimewagusa watu mbalimbali akiwemo bilionea na mfanyabiashara mwenzake, Mohammed Dewji maarufu Mo na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ambaye aliandika kupitia ukurasa wake kuwa amejifunza mengi kupitia kwa mfanyabiashara huyo, ambaye kwake alikuwa rafiki, kiongozi na mzazi akimfundisha suala zima la kuwa kukata tamaa ni dhambi.Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alitoa pole kwa familia na wafanyakazi wote wa IPP kutokana na msiba huo. “Ni wazi tumepata pigo kubwa ila Mwenyezi Mungu awasimamie na kuwapa nguvu katika kipindi hiki kigumu. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Amen,” alisema. Nao wabunge wameeleza kwa nyakati tofauti, hisia zao kuhusu msiba huo, huku wengi wao wakielezea ushiriki wa Mengi wakati wa uhai wake katika kuendeleza vyombo vya habari na biashara nchini na ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki.Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya (Chadema) alisema jumuiya ya wafanyabiashara, imempoteza mtu muhimu na alikuwa nguzo ya taifa. “Nimepokea kwa masikitiko sana kifo cha Dk Reginald Mengi, mimi namuita kaka yangu, kwanza kwenye jumuiya ya wafanyabiashara tumempoteza mtu muhimu sana aliyekuwa anapigania mambo ya kibiashara, sio hilo tu alikuwa mtu wa watu, kama taifa tumepoteza nguzo muhimu sana,” alisema.Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ (Chadema), alisema: “ nimeshituka sana na taarifa za msiba kwa sababu siku si nyingi nilikutana naye. “Dk Mengi ni mtu pekee aliyewavutia vijana wakati wa uhai wake akiwasihi kupambana na kuwataka wasikate tamaa katika ungozi na utafutaji. Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM) alisema Mengi ni alama ya matajiri wachache wenye unyenyekevu na hofu ya Mungu. “Ni matajiri wachache wenye utu, ameacha alama kubwa ya kusaidia watu masikini, watu wenye ulemavu na watu wenye mahitaji mbalimbali,” alisema.Alisema katika maisha yake, amekuwa kioo na mfano mkubwa sana wa kujinyenyekeza mbele za wenzake. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Muungano na Mazingira) ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, January Makamba (CCM), alisema: “ Nimepokea taarifa hiyo kwa masikitiko na mshtuko mkubwa na kwamba mzee Mengi ukizungumza historia ya biashara, vyombo vya habari hapa nchini jina lake lazima liwepo na amekuwa mwanzilishi au mtengeneza njia kwenye tasnia ya habari nchini.“Amegusa maisha ya watu wengi sana na kwa kweli tutamkosa kama taifa kwa sababu ametoa mchango mkubwa sana karibu katika kila eneo la uhai wa nchi yetu, kwenye uchumi kwenye biashara. Ni pigo kubwa kwa nchi”. Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) alisema: “Niombe watanzania tuwe na utulivu wa ndani hasa wanatasnia ya habari nchini, sekta binafsi nchini na familia yake. “Nilibahatika kuwa na Mengi karibu sana na nilikutana naye Machi 17 mwaka huu alipoandaa chakula kwa ajili ya watu wenye ulemavu.Alinishirikisha mambo yake, inanibidi nitafakari zaidi. Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde (CCM) ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, alisema Mengi ameacha alama kubwa katika taifa la Tanzania. “Amekuwa ni mtu mwenye msaada kwa watu wengi wenye uhitaji na hasa watu wenye ulemavu watamkumbuka sana kwa mchango wake mkubwa wa kubadilisha fikra, mitizamo lakini pia kuwawezesha kiuchumi kufikia ndoto zao kwamba na wenyewe wanaweza wakasimama na kujitegemea,” alisema.Mbunge wa Bukene, Seleman Zedi (CCM) alisema Mengi alikuwa ni mtu aliyejali makundi kwenye jamii ambayo hayapewi nafasi, kama vile watu wenye walemavu, watu wanaoishi kwa mazingira magumu, albino na watu wa kawaida Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo Peneza (Chadema) alisema kuwa Mengi amekuwa nguzo katika mafanikio yake kisiasa.“ Mimi nimemfahamu Mzee Mengi miaka mitano iliyopita wakati nagombea nafasi ya mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Taifa (Chadema) na aliniona nikihojiwa kwenye luninga na akaandika kwenye twitter kwamba ‘Ninamuangalia binti Upendo Peneza ni binti ambaye ana uwezo na uelewa mpana na kwangu mimi Upendo ni shujaa’.” “Baada ya ku-twitt alitafuta namba yangu mwenyewe akanipigia simu tukaongea, akanitia moyo na akaniambia niendelee na jitihada hizo za kutafuta nafasi katika uongozi mpaka hatimaye nikawa Mbunge,” alisema.Alisema twitter ya Mengi kwa kiasi fulani, ilimsaidia wakati wa kampeni kwa sababu nilikuwa naitumia wakati wa kuomba kura. Umoja wa Mataifa (UN) Kupitia ukurasa wa Twitter wa UN Tanzania, Umoja wa Mataifa (UN) umeandika, “Tumesikitishwa na taarifa za msiba wa Reginald Mengi. Tunaungana na Watanzania wote kuiombea familia ya marehemu katika kipindi hiki.Ubalozi wa Marekani Ubalozi wa Marekani pia kupitia taarifa yake, umeeleza kusikitishwa na kifo cha Dk Mengi, ukisema kuwa kwa siku za nyuma uliwahi kufanya kazi na marehemu na kushirikiana katika mambo mbalimbali. Taarifa iliyotolewa na ubalozi huo, ilisema kuwa utamkumbuka Dk Mengi kutokana na mchango wake katika ukuaji wa muda mrefu wa uchumi na maendeleo ya Tanzania.Ubalozi huo ulitoa pole kwa familia na kuungana na watanzania wote katika kuombeleza msiba huo mkubwa. Mpaka anaaga dunia, Mengi anatajwa kuwa mmoja wa matajiri wakubwa nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki, akiwa na himaya ya biashara ya vyombo vya habari, kiwanda cha vinywaji baridi, kampuni za madini na kampuni zingine mbalimbali.Mwaka 2014 Jarida maarufu duniani la Fobes, lilimuorodhesha Mengi akiwa nafasi ya 45 kati ya matajiri 50 zaidi barani Afrika akiwa na utajiri wa Dola za Marekani 560 milioni sawa na zaidi ya Sh 1.2 trilioni za Tanzania. Wanahabari Waandishi wa habari wakiongozwa na Katibu wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Nevil Meena wamesema msiba wa Mengi ni pigo katika tasnia ya habari, kwani hakuna mwanahabari asiyetambua mchango alioutoa katika tasnia hiyo.Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uhuru Media, Ernest Sungura alisema kamati ya maandalizi, itatoa taarifa ya pamoja ya wanahabari kuhusu msiba huo. Alisema taarifa hiyo inayoandaliwa na nguli wa habari nchini, Theophil Makunga itaeleza kinaga ubaga mchango wa Dk Mengi katika kuikuza tasnia hiyo, ambaye kwa nafasi mbalimbali alizokuwa nazo, mbali ya umiliki wa vyombo kadhaa vya habari, kwa kiasi kikubwa alisimamia maendeleo ya tasnia hiyo.Uongozi wa makampuni ya IPP yanayomilikiwa na Dk Mengi, umetoa wasifu na historia ya Mengi. Hata hivyo, uongozi huo haujaeleza ni lini mwili wake utaletwa nchini na taratibu nyingine za mazishi. Baraza la EABC Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Baraza la Biashara Afrika Mashariki (EABC), imetoa pole kwa familia, marafiki na kampuni nzima ya IPP kwa msiba huo wa Dk Mengi.“Maneno hayawezi kuelezea pengo hili aliloliacha Dk Mengi ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa bodi ya EABC katika kipindi cha mwaka 2008/9. Alikuwa mchapakazi, mwenye upendo, kiongozi na kiongozi wa biashara,” ilisema taarifa iliyotolewa na bodi hiyo. Ilisema Dk Mengi alipokuwa mwenyekiti wa baraza hilo, alisisitiza juu ya ushirikiano wa kikanda kwa kuongoza mtazamo wa sekta binafsi ili kuingizwa katika Itifaki ya Soko la Pamoja la EAC.Historia yake fupi Dk Mengi alizaliwa Mei 29, mwaka 1942 katika familia duni mkoani Kilimajaro. Baadae alianzisha makampuni ya IPP ambayo yamekuwa yakihudumu nchini Tanzania na baadhi ya maeneo ya Afrika Mashariki. Kwa mujibu wa jarida la Forbes hadi kifo chake alikuwa anamiliki magazeti 11, vituo kadhaa vya redio na vituo kadhaa vya televisheni.Pia, ana kampuni zinazotengeneza sabuni, kampuni kubwa zaidi ya maji ya kunywa nchini. Pia, alikuwa akijihusisha na biashara ya uchimbaji madini kama ya urani, shaba na makaa. Mwaka 2014 aliwekwa nafasi ya 50 miongoni mwa watu matajiri barani Afrika, akikadaliwa kumiliki utajiri wa dola milioni 560. Kabla ya kuingia katika shughuli za kibiashara, Mengi alifanya kazi kwenye kampuni maarufu ya ukaguzi wa mahesabu ya Cooper Brothers. Mengi alisomea taaluma ya uhasibu nchini Uingereza. Mengi ameacha watoto kadhaa.
Kitaifa
0
TANGU Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani ikiongozwa na Rais John Magufuli, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeonesha ari na kasi kubwa zaidi katika kurasimisha makazi mijini.Hali hiyo imeiwezesha serikali kuongeza mapato yake kupitia ukusanyaji wa pango la ardhi, ada na tozo mbalimbali zitokanazo na shughuli za sekta ya ardhi. Katika mazungumzo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, anasema mwanzoni mwa mwaka huu kuwa, kutokana na juhudi hizo, mapato ya serikali yameongezeka kutoka Sh bilioni 54.55 Mwaka 2014/15 hadi kufikia takriban Sh bilioni 100 katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18.Mara nyingi katika ziara zake mbalimbali nchini, Waziri Lukuvi amekuwa akisisitiza programu ya kupanga, kupima na kumilikisha kila kipande cha ardhi. Imefahamika kuwa, ili kufanikisha hilo, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inahakikisha ardhi inapangwa, inapimwa na kumilikishwa hivyo, inakamilisha programu ya kupanga, kupima na kumilikisha kila kipande cha ardhi nchini.Kimsingi hili ni jambo jema linalofanywa na wizara kwa sababu, upimaji, upangaji na umilikishaji ardhi una faida nyingi zikiwamo za kiuchumi kwa wananchi wanaomiliki ardhi au majengo, na hata kwa taifa.Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita) ulio chini ya Ofisi ya Rais, Ikulu, Seraphia Mgembe anazitaja faida za urasimishaji ardhi na makazi mijini kuwa ni pamoja na mmiliki kuwa na nguvu za kisheria za umiliki, kuongeza fursa za kukuza mitaji kupitia urahisi wa kupata mikopo toka taasisi za fedha na hata uwezekano wa kupata wabia katika uwekezaji.Kupitia mazungumzo na wadau mbalimbali wa uchumi na mandeleo, imebainika pia kuwa urasimishaji wa makazi huongeza thamani ya makazi ya mtu na hata kuondoa migogoro katika jamii. Kimsingi, zipo faida nyingi za kijamii na kiuchumi zitokanazo na upangaji, upimaji na urasimishaji ardhi katikia maeneo mbalimbali nchini.Hivi karibuni wakati akimwakilisha Rais John Magufuli katika Mkesha wa Kitaifa Kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2019 na kuuaga mwaka 2018 uliofanyika katika Uwanja wa Karume Dar es Salaam, Lukuvi alisema Serikali imetoa miezi mitatu kwa halmashauri zote nchini kuanza kutoa leseni za makazi mijini kama mchakato wa kurasimisha makazi hayo ili kuwafikia watu wote wanaomiliki vipande vya ardhi mijini na kuwafanya watambulike.Kutambulika kwa watu hao kuhusu umiliki wao, kunawapa uhakika wa usalama wa miliki zao na pia, kunawapa fursa za kiuchumi kukuza mitaji na hata kuongeza pato la taifa kupitia kodi ya pango la ardhi na tozo nyingine muhimu kwa maendeleo ya jamii na nchi kwa jumla.Waziri Lukuvi anasema, utoaji wa leseni hizo ambazo ni nyaraka halali na inayotambulika kisheria inayomwezesha mmiliki hata kuchukua mkopo wa fedha benki, ni hatua ya awali ya kutambua makazi na baadaye lifuate zoezi la kupima, kupanga na kurasimisha makazi hayo kwani wamiliki watapewa hati ya umiliki wa ardhi ya miaka 99.Kwa mujibu wa Lukuvi, asilimia 70 ya miji yote nchini watu wake wanaishi katika maeneo yasiyopangwa na yasiyopimwa. Anasema kwa kuwa leseni hizo za makazi zitadumu kwa muda wa miaka mitano tangu zianze kutolewa, halmashauri zote na watu wote watakaopata leseni hizo, waanze mchakato wa kurasimisha makazi yao ili wapate hati.Mpaka sasa zaidi ya makazi 100,000 yamesharasimishwa nchini, na zoezi hili la utoaji wa leseni za makazi haliwahusu watu ambao tayari wana hati au wale ambao wameshaanza mchakato wa kupata hati, bali linawahusu wanaomiliki vipande vya ardhi na hawajaanza mchakato wa kupata hati.Kimsingi, hii ndiyo maana Programu hii watu wengi wanaisubiri kwa matumaini wakiamini kwa dhati kuwa ikitekelezwa, ardhi nchini itatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii na huo ndio hasa msisitizo wa Waziri Lukuvi katika hili.Anasema: “Katika program hii ya kupanga, kupima na kumilikisha kila kipande cha ardhi nchini, Serikali itasajili kila kipande cha ardhi, kuimarisha utunzaji wa kumbukumbu za ardhi kwa njia ya kielektroniki kwa kujenga hatua kwa hatua Mfumo Unganishi wa Kuhifadhi Kumbukmbu za ardhi (Integrated land management Information System- ILMIS) katika awamu ya pili katika halmashauri zote nchini.”Kwa mujibu wa jarida la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Mandelezo ya Makazi liitwalo; URASIMISHAJI MAKAZI NCHINI: TOLEO MAALUMU, makazi holela nchini ni hali inayoendelea kila siku kutokana na wakazi wengi kujenga bila kufuata taratibu maalumu zilizowekwa kisheria.Kwamba, makazi holela ni ujenzi wa makazi pamoja na maendeleo unafanyika katika makazi bila kufuata utaratibu wa mipango miji unaoongozwa na Sheria ya Mipango Miji Namba 8 ya Mwaka 2007.Jarida linasema: “Lengo la urasimishaji ni kuwafanya watu waliokuwa wanaishi katika makazi holela wawe na nyaraka rasmi za kuweza kukopesheka.” Wakati akitoa taarifa ya urasimishaji wa makazi holelea mijini wakati wa mawasilisho ya Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ya Mwaka 2017/18, Waziri Lukuvi alisema wizara kwa kushirikiana na mamlaka za upangaji, Mkurabita (Mpango wa Kurasimisha rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania) na sekta binafsi, imeendelea kurasimisha makazi katika halmashauri 27 mchini.Kwamba hadi mwezi Mei mwaka jana, viwanja 142,992 vilikuwa vimepimwa katika halmashauri mbalimbali nchini. Hata hivyo, ni jambo la ajabu kuona kuwa wakati serikali inahangaika kuhudumia watu wake, baadhi ya watumishi wasio waadilifu, wanajaribu kurudisha nyuma juhudi hizo kwa kufanya ubadhirifu na matumizi mabaya ya nafasi zao, jambo ambalo kimsingi, hakuna Mtanzania halisi anayelikubali.Ndiyo maana Wizara hii imeanzisha operesheni maalum kubaini wamiliki hewa wa viwanja zaidi ya 9,000 vilivyoandikishwa na kumilikiwa na watumishi wa wizara hiyo kwa njia haramu.Taarifa ya Waziri Lukuvi kwa vyombo vya habari hivi karibuni inabainisha kuwepo kwa idadi kubwa ya viwanja vinavyomilikiwa na wafanyakazi hao kwa majina bandia au anuani za uwongo.Anasema watumishi hao wamejimilikisha isivyo halali ili baadaye waviuze kwa udanganyifu na kwa bei ya juu. Anaongeza kuwa, idadi kubwa ya viwanja hivyo havijalipiwa kodi na pia havijaendelezwa kwa kuwa vimeachwa kwa muda mrefu bila ya shughuli za kibinadamu kufanyika hali inayowaathiri wakazi wengine wa maeneo hayo.Kimsingi hapana shaka kuwa, hao ndio wengi waliosababisha mlundikano wa hati na nyaraka katika Wizara hizo ambazo hivi karibuni, wizara imetoa mwito wakazichukue, lakini wanaogopa kwenda kwa kuwa ‘uhuni wao’ uitabainika.Eee! Ndivyo Watanzania wamekuwa “wakinyonywa” na baadhi ya watumishi kwa miaka mingi iliyopita. Katika taarifa hiyo Waziri Lukuvi anasema: “Wizara imejipanga kunasa viwanja vyote ambavyo umiliki wake una mashaka na vitachukuliwa na kurejeshwa serikalini hivyo…”Anasema kutoendelezwa kwa viwanja hivyo ni sawa na kuwadhulumu wananchi wengine haki ya kumiliki ardhi na kuitumia kujiongezea pato na pia, kulikosesha taifa mapato yake.Ndiyo maana Waziri Lukuvi anawataka wenye taarifa mintarafu wanaomiliki viwanja visivyoendelezwa kwa muda mrefu, kumpigia simu namba 0755333334 huku akiwahakikishia usalama wao kuwa hawatojulikana kuwa ndio waliotoa taarifa hizo. Ndiyo maana urasimishaji wa makazi hauna budi kulindwa na kuendelezwa ili kukuza uchumi nchini.
Kitaifa
0
KUNA uwezekano mkubwa kwamba miongoni mwa watu wazima wanaopata maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya homa ya ini B, hupona kutokana na afya ya miili yao, Imeelezwa. Aidha, imeelezwa pia kuwa watu hao baada ya kupona kupitia kinga yao ya asili kupambana na kuviua virusi hivyo, hatimaye miili yao hujitengenezea kinga ya kudumu, hivyo hawapati tena virusi hivyo. Akizungumza na HabariLeo kwenye mahojiani maalum jijini Dar es Salaam, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini, John Rwegasha alisema homa hiyo ni tishio na kuwataka wananchi kuzingatia ulaji wa mlo kamili wenye virutubisho vyote. Alisema ulaji wa mlo kamili wenye virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini hujenga kinga ya mwili ambayo huufanya mwili kupambana na maradhi mbalimbali pamoja na homa ya ini B. Dk Rwegasha ambaye anasimamia mradi wa uchunguzi na tiba ya Homa ya Ini katika hospitali hiyo, alisema mwili wenye afya bora una uwezo wa kupambana na kuviondoa virusi hivi mwilini. “Asilimia 95 ya watu wazima wanaopata maambukizo ya awali wana uwezo wa kupambana na virusi hawa na kuviondoa mwilini kwa kutengeneza kinga zao za mwili dhidi ya ugonjwa huu, Ipo idadi ya watu wazima ambao wameshawahi kupata tatizo hili na mwili ukapambana wakapona bila ya wao kujua,” alisema.Hata hivyo alisema kuwa kwa watoto ni kinyume chake, zaidi ya asilimia 90 ya waliopata maambukizi hayo huendelea kuishi navyo mwilini kwa sababu watoto wanapopata maambukizi haya miili yao haina kinga ya kutosha kupambana na magonjwa, hivyo virusi hao wakiingia mwilini hugeuka na kuwa sugu.Dk Rwegasha alisema uchunguzi umeonesha kuwa idadi ndogo ya asilimia tano ya watu wazima walioshindwa kupona katika kipindi cha awali na huendelea kuwa na ugonjwa huo sugu.Aidha, alisema kati ya hawa zaidi ya asilimia 80 ya watu ambao wamepima na kukutwa na maambukizo sugu katika mradi huu unaoendelea katika hospitali ya Muhimbili, tayari wamethibitisha kuwa na kinga ya awali mwilini ambayo inaendelea kupambana na virusi hawa ili kuwadhibiti na hatimaye kuwaondoa kabisa. “Katika hatua zote za ugonjwa huu za awali na usugu kinga ya mwili ikifanikiwa kuwaondoa virusi hawa, mwili hujitengenezea kinga ya kudumu na anakuwa sawa na ambaye amechanjwa chanjoya ugonjwa huu,” alisema. Aidha alisema lishe ni jambo muhimu na la msingi watu kula mlo kamili wenye virutubisho sahihi ili kujijengea kinga kwani kila kundi la chakula lina kazi yake mwilini. “Tunapokula chakula kila kitu kinaenda kufanya kazi kulingana na mahitaji ya mwili, maendeleo ya mfumo wa kinga thabiti za mwili pia hutegemea na virutubisho vipatikanavyo katika chakula,” alisema. Alisema kuna mambo mengine yanayoweza kuathiri mfumo wa kinga, hivyo muathirika kuendelea na ugonjwa sugu unaombatana na magonjwa nyemelezi ya ini kama kusinyaa kwa ini na kansa ya ini. Pia kupata maambukizo ya Ukimwi, matumizi ya pombe na dawa za kienyeji zisizokuwa na uthibitisho wa kitaalamu.
Kitaifa
0
NAIBU Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (pichani) amesema ifi kapo Julai mwaka huu, jiwe la msingi litawekwa kuashiria kuanza kwa utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa ufuaji umeme wa Mto Rufi ji maarufu kama ‘Stiegler’s Gorge’.Hayo aliyabainisha bungeni jana wakati akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na wabunge kwenye bajeti ya wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2019/20 ikiwemo mradi Stiegler’s Gorge.Mgalu aliwaeleza wabunge na watanzania kuwa mradi umeanza na inatarajiwa mwezi Julai kuwekwa jiwe la msingi na kazi mbalimbali za mazingira wezeshi zimekamilika “Itakuwa ni kupoteza muda kujadili kwa misingi ya kwamba turudi nyuma, haturudi nyuma nataka niliseme wazi kabisa kwamba,”alibainisha Mgalu na kulitaarifu bunge kuwa mradi huo ulifanyika kwa mujibu wa tafiti mbalimbali na kwamba kimsingi tafiti hizo hakuna ambayo iliainisha kwamba mradi huo hauna faida yoyote “Kwa sasa tunapotekeleza mradi huu imeshafanyika tathimini hivyo sisi tumeangalia faida na hasara zake hususani kumpunguzia mtanzania gharama za kubwa ya matumizi ya umeme... tumetathimini vyanzo mbalimbali na kwa kuwa tunatekeleza mpango kabambe wa umeme ambao umeanisha kila chanzo kinatakiwa kizalishe megawati ngapi ili kufanya upatikanaji wa umeme uwe kwa urahisi,”alisema.Alilitaarifu bunge kuwa chanzo hicho cha maji kinagharimu Sh 36, umeme unaozalishwa na gesi unagharimu Sh 147, unaozalishwa na mafuta Sh 526 na kuongeza kuwa ukiangalia gharama za uwekezaji unapowekeza kwa kutumia mahitaji ya joto ardhi unatumia Sh 10,000 tofauti na unapowekeza kwa kutumia maji unatumia 6,000 kwa megawati moja hivyo inaonesha hata gharama za uwekezaji zina nafuu kwenye miradi ya maji.Alisema chanzo cha joto ardhi, serikali imewekeza ambapo wizara ya fedha imetoa sh bilioni 32 kwa ajili ya mambo ya uchorongaji wa visima vya majaribio hivyo mradi huo wa Stiegler’s Gorge ndio mkombozi kwenye uchumi wa viwanda. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Fedha, Dk Ashatu Kijaji alisema kuwa hawajawahi kupata taarifa rasmi kutoka kwa serikali nyingine kuhusu utekelezaji wa mradi mbadala ya uzalishaji umeme wa mto Rufiji.Alisema kulingana na sheria ya misaada, mikopo na dhamana ni wizara ya fedha pekee inayoshughulika na masuala hayo kutoka sehemu yoyote nchini na kwamba anaposimama Mbunge kusema serikali ilipata ofa na ikakataa anapaswa kujitathimini. Dk Kijaju alisema wanapopata taarifa ya aina hiyo wao kama wizara huwa wanapeleka kwenye kamati ya taifa ya madeni kufanyia tathimini kuwa uitwe msaada au upewe ofa na kuwa wakishamaliza kwenye kamati hiyo huwa wanamshauri waziri wa fedha na inapofika kwenye majumuisho.“Sasa unaposimama kwenye bunge tukufu na kudanganya watanzania dhamira yako ni ipi hilo lazima tulielewe, sisi kama wizara yenye mamlaka ya kushughulika na masuala ya dhamana na mikopo hatujawahi kupata barua rasmi kutoka sehemu yoyote kutoka dunia hii kwa ajili ya utekelezaji wa mradi mbadala,” alisema na kuwataka watanzania kuendelea kumpuuza Mbunge Catherine ambaye awali alisisimama kuchangia na kudai hayo. Alisema dhamira ya Rais John Magufuli ni njema nchi inaelekea kwenye uchumi wa viwanda hivyo ni utekelezaji wa mpango wa pili wa maendeleo na dira ya 2025 ya kujenga uchumi utakaoleta matokeo chanya kwa wananchi na umeme wa bei nafuu.“Tupo tayari na tumeanza kutenda na mbunge huyu amesema kwamba serikali haina uwezo naomba nimwambie kwamba tumejipanga... tumejiandaa na tuko tayari kutekeleza mradi huu na utakamilika kwa wakati na watanzania watafaidi matunda ya serikali yao,”alisema. Aliwataka watanzania wasikubali kutumika na kwamba serikali imesimama na mradi huo, na kuhakikisha utatekelezwa kwani tayari Sh milioni 688.6 zimepelekwa kama fedha ya kuanza utekelezaji. “Fedha zake zipo wala hatuhitaji kwenda kukopa au kuomba ipo kwa ajili ya mradi wa umeme mto Rufiji,”aliongeza.Awali mbunge wa viti maalum Catherine Ruge(CHADEMA) alisema kuwa wao kama kambi rasmi ya upinzani bungeni watazungumza mradi wa Stiegler’s Gorge kama kitabu cha ushairi cha Song of Lawino and Okol ili watanzania wote wenye masikio wasikie kwamba mradi huo una madhara na hautawafaidisha.Awali wakati Ruge akiendelea kuchangia Naibu Waziri wa nishati Subira Mgalu aliomba kutoa taarifa kwa mujibu wa kanuni ya 64 inayoeleza kuwa mbunge hatatoa bungeni taarifa yoyote ya uongo na kuongeza kuwa mbunge huyo alitoa taarifa ya uongo wakati akichangia kuhusu mradi huo wa umeme rufiji ambapo alimjulisha kuwa mradi huo ulifanyiwa tathimini na tenda ilitangazwa na wakandarasi waliomba kufanya mradi huo.“Na ndio maana tumeingia mkataba nao kwa kiasi cha trilioni sita ambazo wakandarasi na timu ya wataalamu ya serikali iliyoundwa kwa pamoja na kwa majadiliano wamekubaliana... sasa Ruge anaposema kwamba mradi utagharimu trilioni 21 na kwamba serikali imeingia mkataba na mabenki kugharamia mradi huo.Napenda niwaambie Serikali kwa vyanzo vyake vya ndani imeshatoa asilimia 15 kiasi cha Sh bilioni 685 sasa Naibu spika, anaposema serikali imetumia mabenki ambayo hayapo asilipotoshe bunge,”alisema.Baada ya Mgalu kutoa taarifa hiyo, Naibu Spika Tulia Ackson alisimama na kueleza kuwa wakati Ruge akichangia alitoa taarifa za uongo kwa mujibu wa kanuni hiyo hivyo kumtaka kuthibitisha kama ni za kweli na ana ushahidi au afute maneno hayo. Alisema kwa mujibu wa kanuni ya 63 na 64 ya mbunge kutosema uongo bungeni alimtaka Ruge kutoa maelezo kwa kumpelekea uthibitisho kama upo Ruge aliporuhusiwa alisimama na kusema kuwa hayo ni maneno yake na kwamba ni ripoti ya utafiti imeonesha hivyo kama hana atapelekewa.Naibu Spika alisema kwa kuwa Ruge amesema ana ushahidi anamruhusu aendelee kuchangia na apeleke ushahidi wake ambao kama taratibu zilivyo ili kumbukumbu ziwekwe sawasawa na kumtaka apeleke ushahidi wake kwenye kamati ambayo itasaidia kuangalia uhalisia wa hiyo taarifa na alimpa muda hadi wiki ijayo Jumatano awe amewasilisha ushahidi kwa kamati.Juzi pia wakati kambi ya rasmi ya upinzani bungeni katika maoni yake kuhusu utekelezaji wa bajeti ya wizara ya maliasili na utalii kwa mwaka 2018/2019 na mpango wa mapato na matumizi ya wizara ya maliasili na utalii kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020 ilisema ikolojia ya Bonde la Kilombero na Mto Rufiji ni muhimu kwa sasa na kwamba utekelezwaji wa mradi wa ufuaji umeme utaleta hasara kwa mazingira kwa kusababisha uharibifu mkubwa wa misitu na kuondoa mazalia ya wanyama na ndege wengi ambao walikuwa wanaleta utofauti mkubwa na wa kipekee wa mbuga ya Selous.Ilidai kuwa ni fedheha kwa serikali kuwa mstari wa mbele kwa kuyafuta mazuri hayo yaliyoridhiwa na taifa ili kulinda mazingira ya sasa na vizazi vijavyo baada ya serikali mapema mwaka jana kufanya upembuzi ili kuanzisha mradi mkubwa wa kuzalisha nishati ya umeme yaani Stiegler’s Gorge katika pori la akiba la Selous kwa bei nafuu.Kwa mujibu wa kambi hiyo ya upinzani, pamoja na serikali kusema imefanya upembuzi yakinifu, ni vyema ikaamua kufanya mkakati wa tathmini ya mazingira kwa miaka ijayo, kwa kile walichoeleza kuwa endapo chanzo hicho cha maji kitaharibiwa basi hata umeme unaotaka kuzalishwa hautakuwa endelevu kwa miaka mingi ijayo.Ilisema inatambua umuhimu mkubwa wa upatikanaji wa nishati ya umeme nchini lakini serikali itambue umuhimu wa kuhifadhi vyanzo vya maji hususan chanzo hicho muhimiu kwani bila maji hakuna uhai, bila maji hakuna umeme, bila maji hakuna chakula na kuitaka serikali kuangalia upya mikakati ya kimazingira ya muda mrefu kabla ya kuanza kwa mradi huo.
Kitaifa
0
MABINGWA wa soka Bara, Simba wanatarajiwa kuweka kambi Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.Simba inayotarajiwa kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, juzi ilitangaza orodha ya wachezaji 27 iliyowasajili kwa ajili ya michuano mbalimbali. Kwa mujibu wa ofisa habari wa Simba, Haji Manara, kikosi chao kinatarajiwa kwenda Afrika Kusini keshokutwa. “Wachezaji wote tuliowasajili watakuwa wameshafika kabla ya siku ya safari… na timu ikiwa kule itacheza mechi kadhaa za kirafiki,” alisema Manara.Kwa misimu ya karibuni imekuwa utaratibu kwa baadhi ya timu kufanya kambi ya maandalizi ya msimu nje ya mji ama nchi. Msimu uliopita Simba iliweka kambi Uturuki. Mbali na Simba, wengine wenye utaratibu huo ni Yanga ambao walishawahi kuweka kambi yao Uturuki na Afrika Kusini pia, msimu huu kama ilivyokuwa msimu uliopita, wamepiga kambi yao Morogoro.Wachezaji waliosajiliwa na Simba na ambao wanatarajiwa kwenda kambini Afrika Kusini ni Aidhi Manula, Beno Kakolanya, Ally Salim, Paschal Wawa na Erasto Nyoni. Gerson Viera, Tairone Da Silva, Wilker Da Silver, Francis Kahata, Deogratius Kanda, Hassan Dilunga, Mzamiru Yassin, Said Ndemla, Meddie Kagere na Clatous Chama.Wengine ni John Bocco, Mohamed Hussein,Yusuph Mlipili, Paul Bukaba, Kenedy Juma, Ibrahim Ajibu, Gadiel Michael, Jonas Mkude, Rashid Juma, Miraji Athumani, Shomari Kapombe na Shiboub Sharaf.
michezo
2
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amesema hatowavumilia watumishi wa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo watakaokwamisha wafanyabiashara na wawekezaji wenye viwanda na kuwahimiza watumishi hao kuwa wawezeshaji.Aidha, amesisitiza haja ya kuja na sera maalumu itakayounganisha sekta za kilimo, biashara na viwanda.Bashungwa aliyasema hayo wakati wa kufungua siku ya pili ya kikao kazi kilichowakutanisha viongozi kutoka taasisi zote zilizo chini ya wizara hiyo.“Lazima tubadili mtazamo katika kutoa huduma. Tunatakiwa kuwa wawezeshaji na sio wakwamishaji. Nikisikia mtumishi anashindwa kuwasaidia wafanyabiashara na wenye viwanda, hatutaelewana, tunataka tuwe mfano kwa wizara nyingine,”alisema.Bashungwa aliongeza: “kama taasisi yako ni ya udhibiti tekeleza wajibu wako kulingana na taratibu na sheria, lakini udhibiti huo usiwe ule wa kuvuka mipaka wenye lengo la kukwamisha.”Alisema wizara hiyo ni muhimu katika kufanikisha taifa kufikia uchumi wa viwanda, hivyo taasisi za usimamizi na udhibiti zilizopo nchini ya Wizara ya Viwanda na Biashara, zinapaswa kutimiza majukumu yake kwa lengo la kumsaidia mwekezaji au mfanyabiashara.“Azma si kudhibiti kwa kupitiliza, tunataka tumsadie mfanyabishara au mwenye kiwanda hatua zipi anapaswa kuzifuata. Tunapaswa kusimamia na kuratibu maendeleo ya viwanda na biashara,” alibainisha.Bashungwa alisema moja ya changamoto aliyoibaini kwamba taasisi zote zilizopo kwenye wizara hiyo kukosa muunganiko na kusababisha kila taasisi kutekeleza majukumu kivyake.Kadhalika, alisema tozo 54 zilizopendekezwa kuondolewa kupitia bajeti kuu ya serikali iliyowasilishwa Alhamisi bungeni, Dodoma ni sehemu ya utekelezaji wa mpango kazi wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.“Ni mshukuru Mheshimiwa Rais John Magufuli, kwani mkutano wake na wafanyabiashara wakubwa umenipa mwanga kufahamu maeneo mengi ninayopaswa kuanza nayo,” alisema.Aliongeza: “ Mkutano wa Rais John Magufuli na wafanyabiashara umetupa mwanga. Hivyo hatupaswi kuwa na mipango ya kushtukiza. Tumeanza na mkakati kwa wizara kushirikiana na Wizara ya Kilimo, kupitia bodi ya mazao mchanganyiko, kutafuta masoko hususani kwenye mazao ya kimkakati ya pamba, kahawa na korosho.Alisema hatua nyingine ni kuangalia fursa ya masoko zilizopo kwenye jumuiya mbalimbali za kikanda ambazo Tanzania ni mwnachama wa Afrika Mashariki (EAC) pamoja na kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara kimataifa.Akizungumzia siku ya kwanza kwa kikao kazi hicho, Bashungwa alisema wameona haja ya kuja na sera ambayo itasaidia kufunganisha sekta ya kilimo na sekta ya biashara na viwanda ikiwa ni njia ya kuwapeleka watanzania katika uchumi wa kati kupitia viwanda.“Tumeoana sera, sheria na kanuni zetu haziendani na ari ya sasa, hivyo tumeona kuna haja ya kufanya mabadiliko ya haraka ya sera itakayofungamanisha sekta ya kilimo na biashara na viwanda,” alisema.Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara Tanzania (BRELA), Emannuel Kakwezi, alisema wakala huo unaendelea kutimiza majukumu yake katika kusajili na kurasimisha na kusaidia uanzishwaji wa biashara mpya nchini.“Kuhusu wafanyabiasha wanaotaka kusajili kampuni kuwa na kitambulisho cha taifa ambapo alisisitiza lengo ni kutaka wamiliki wake au wanahisa watambulike.Kakwezi alisema BRELA imeanzisha dirisha maalum kuwasaidia wanaotaka kusajili kampuni ambao hawana vitambulisho vya taifa katika mikoa na wilaya “Wafanyabiasha hao watapatiwa namba ya kitambulisho ambayo itawawezesha kupitia mfumo wetu, kusajili kampuni bila ya kuwa na kitambulisho kamili,” alisema.Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Ushindani, Profesa Humphrey Moshi, alisema wamejipanga kufanya ukaguzi wa saa 24 kwa mizigo yote inayoingia nchini ili kuongeza kasi ya utoaji huduma na kurahisisha mazingira ya ufanyaji biashara.“Tume itatimiza majukumu yake ya kulinda afya za watumiaji bidhaa pamoja na kuweka mazingira sahihi ya ufanyaji biashara nchini.”
Kitaifa
0
SERIKALI ya China kupitia Jeshi la Ukombozi la China, kikosi cha Anga limetoa msaada wa ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Taifa kilichopo Kunduchi, Dar es Salaam unaogharimu Shilingi Bilioni 56.Ujenzi huo wa awamu ya pili ya chuo hicho utakifanya kuwa cha kisasa na miundombinu rafiki na kukiwezsha chuo hicho kudahili zaidi ya wanafunzi 100 kwa wakati mmoja baada ya ule wa awamu ya kwanza uliofanyika 2013 na kumalizika 2015. Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi, aliishukuru Serikali ya China kupitia jeshi la ukombozi la watu wa China kwa msaada huo kwani utasaidia kuongeza kozi na idadi kubwa ya wanafunzi.“Tunashukuru serikali ya China kwa msaada huu wa ujenzi wa awamu ya pili ya majengo ya chuo chetu. Msaada huu utakifanya chuo kuweza kuchukua wanafunzi wengi kwa wakati mmoja pia kuboresha sehemu ya kuishi vifaa vya mafunzo,” alisema Dk Mwinyi Alisema mafunzo yanatolewa katika chuo hicho yanalenga ulinzi wa taifa na kimataifa kwa sasa na baadaye kiuchumi, kisiasa, kijeshi na kisayansi katika mikakati ya maendeleo ya taifa.Dk Mwinyi pia alisema mbali na ujenzi wa chuo hicho pia wamejenga kituo maalumu kwa mafunzo maalum ambacho kipo Mapinga Bagamoyo, Pwani na hivi karibuni wataanza ujenzi wa makao makuu ya jeshi mkoani Dodoma eneo la Kikombo. Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke, alisema urafiki wa Tanzania ulianza wakati wa uongozi wa awamu ya kwanza wa Rais wa Tanzania, Julius Nyerere na Mao Tse Tung na sasa umerejea kwa kasi na kuahidi serikali yao itaendelea kuisaidia Tanzania kulingana na uwezo wao.“Ninafurahi kualikwa katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi wa jengo hili ambalo linajengwa na Serikali ya watu wa China kupitia Jeshi la Anga. Urafiki wa Tanzania na China ni wa kihistoria hivyo nikianza kueleza mambo ambayo serikali hizi mbili zimefanya nitachukua muda mrefu. “Tunaahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika miradi mbalimbali na hata mafunzo ya ndani kwa jeshi la maji, jeshi la anga na jeshi la nchi kavu ili kufanya jeshi liwe la kisasa na kukidhi malengo ya taifa,” alisema Wang Ke.Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Yakubu Mohamed, Ofisa Mwandamizi, Mwelekezi Mambo ya Nje katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Balozi Peter Kallaghe na maofisa mbalimbali wa JWTZ na jeshi la Anga la China ambao ndio wanajenga na kusimamia ujenzi huo.
Kitaifa
0
Utekelezaji wa mfumo huu unafanyika kutokana na kubainika kuwa na mafanikio makubwa baada ya majaribio yake kufanyika tangu Julai mwaka jana.Unalenga kupunguza gharama na kuweka mazingira rafiki ya kufanya biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki, hali ambayo itavutia uwekezaji katika nyanja mbalimbali za uchumi.Inakadiriwa kuwa mfumo huo utakapotekelezwa kwa asilimia 100 , zaidi ya asilimia 70 ya gharama za kufanya biashara zitakuwa zimeondolewa.Naibu Kamishna Mkuu wa Forodha (Uwezeshaji Biashara), Patrick Mugoya alisema hayo jana wakati wa mahojiano maalumu juu ya utekelezaji wa mfumo wa himaya moja ya forodha.Alisema katika kipindi hiki cha majaribio, pamejitokeza changamoto kadhaa katika utekelezaji wa mfumo huu lakini hatua zimechukuliwa kutafuta suluhisho la matatizo haya kabla ya mwezi wa nne mwaka huu kwa ajili ya kutumika rasmi kwa mfumo huu mwaka wa fedha ujao.“Tumefikia hatua nzuri katika kutatua changamoto hizi ili kufanya utekelezaji wa mfumo huu uwe na manufaa tarajiwa na kuwezesha biashara ifanyike katika mazingira stahiki na ya gharama nafuu,” alisema.Baadhi ya changamoto ambazo zinafanyiwa kazi na wataalamu wa forodha kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki ni pamoja na kutokuwa na mwingiliano wa mifumo ya forodha katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na hofu kwa maofisa wa forodha kupoteza kazi kutokana na mfumo mpya.Nyingine ni pamoja na taasisi za udhibiti katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambazo ni wadau wa karibu katika kufanikisha shughuli za forodha kutoupokea haraka mfumo huu wa himaya moja.Alisema katika utekelezaji wa mfumo huu, mchakato wa kuandaa nyaraka za kutoa mizigo bandarini hufanyika katika nchi ambayo mzigo huo hupelekwa na hasa baada ya kupokea kibali maalumu kutoka kwenye bandari ambapo mzigo umefikia.
Biashara
1
Huduma zinazotolewa na duka hilo ni pamoja na kukusanya ankara, kurudisha namba zilizopotea, mauzo ya simu, kutuma fedha, kusajili namba na huduma za kimitandao. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jana, Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma kwa wateja wa Airtel, Adriana Lyamba alisema ”uzinduzi wa duka hili ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kutoa huduma bora na kuwapatia wateja wetu uzoefu tofauti katika huduma zetu.Leo tunawawezesha wateja wetu na wakazi wa mkoa wa Tanga kupata hudumu muhimu kama vile za kifedha za Airtel Money kwa usalama zaidi pamoja na kuwaunganisha na simu za kisasa za smartphone na huduma zetu za intaneti”.“Sambamba na hilo, duka letu pia litatoa ofa kabambe za simu na vifaa vya aina tofauti na kuwawezesha wateja wetu kunganishwa na tecknolojia ya simu za mkononi ya kisasa. Tunaamini vifaa vya kisasa ni sehemu muhimu ya mahitaji ya wateja wetu kwa sasa, hivyo kupitia watoa huduma wetu waliobobea kwenye masuala ya teknolojia tunawawezesha wateja wetu kuchagua vifaa na simu bora na kuwaunganisha na huduma za intaneti.“Ni matumanini yangu kuwa wateja wetu sasa watapata suluhisho la mahitaji yao ya huduma za simu kwa urahisi kupitia duka hili,” aliongeza Lyamba. Akizindua duka hilo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga , Magalula Said Magalula alisema ” Mawasiliano yanachangia kwa kiasi kikubwa katika kuwaunganisha watu na biashara na kukuza uchumi wa nchi.Nawapongeza Airtel kwa kuongeza wigo kupitia huduma kwa wateja na kuleta mabadiliko ya kibunifu. Tunaamini ubunifu huu utawawezesha wakazi waTanga kupata huduma bora wakati wote, na kwa hilo tunawashukuru sana Airtel.“Natoa wito kwa wakazi wa Tanga na wateja wa Airtel kutembelea duka hili na kufurahia huduma na bidhaa za kisasa, ikiwemo huduma ya Airtel Money inayotoa suluhisho kwa mahitaji yao ya huduma za kifedha, kufanya malipo na kutuma pesa kirahisi zaidi.” Mkuu wa Mkoa aliziasa kampuni nyingi zaidi, kuiga mfano wa Airtel katika kutoa huduma bora.
Biashara
1
WALIONYANG’ANYWA taa za sola na jenereta wakati wa oporesheni ya kutokomeza uvuvi haramu nchini watarudishiwa zana zao bila masharti yoyote.Kauli hiyo aliitoa bungeni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina wakati akitoa maelezo ya nyongeza kwenye jibu la Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Abdallah Ulega aliyekuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nyamagana, Stanislaus Mabula (CCM). Mabula alitaka kufahamu kauli ya serikali kuhusu katazo la kutumia taa za sola na jenereta katika uvuvi katika maeneo mbalimbali ya uvuvi yakiwemo maziwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa.Waziri Mpina alisema malalamiko mbalimbali kuhusu matumizi ya jenereta na taa za sola yaliyotolewa wakati wa oporesheni yanatakiwa kuachwa na wananchi waruhusiwe kutumia vifaa hivyo hadi hapo Julai Mosi mwaka huu. Alisema Julai Mosi, mwaka huu atatoa kauli lakini si ya kukataza matumizi ya taa za sola, bali atatoa maelekezo ya taa gani na zenye wati ngapi zinatakiwa kutumika katika uvuvi katika maeneo mbalimbali nchini. inawaelekeza wawekezaji wa uvuvi katika ziwa Tanganyika kuhamisha uwekezaji wao na kuupeleka mahali pengine nchini.Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACTWazalendo) aliyetaka kujua kwa nini serikali inaonekana ina mkakati wa kukwamaisha maendeleo ya Mkoa wa Kigoma katika uvuvi wa samaki wa ziwa Tanganyika. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Ulega alisema si kweli kwamba serikali ina mkakati wa kukwamisha maendeleo ya mkoa huo na watu wake, isipokuwa kwa sasa haina uhakika na wingi wa samaki waliopo katika ziwa Tanganyika.Alisema mara ya mwisho kufanyika utafiti wa tathamini kujua uwingi wa samaki katika ziwa hilo ulifanyika mwaka 1998. Ulega alisema iwapo utaachwa uvuvi kuendelea katika ziwa hilo, bila kufanya tathmini ya wingi wa samaki wavuvi wadogo, wazawa wa Kigoma na mazingira yanaweza kuathirika.
Kitaifa
0
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora ipo kwenye mchakato wa kujenga kiwanda cha asali na inakaribisha wawekezaji wa viwanda vya bidhaa zinazotokana na zao hilo la nyuki.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Martha Luleka amesema, kiwanda hicho kitaongeza thamani na matumizi ya asali inayozalishwa kwa wingi wilayani humo.Amesema ofisini kwake mjini Sikonge kuwa, kuna warina asali zaidi ya 6500 wilayani Sikonge wanaozalisha tani 2,000 na kama watawezeshwa na mnyororo wa ongezeko la thamani wataweza kuzalisha tani 6,000 hadi 7,000.“Kwa hiyo mwekezaji asiwe na wasiwasi kwamba pengine malighafi itashuka hapana, sana sana itaongezeka kwa sasa wanafanya tu kwa mazoea yao ya kupata mapato kama ilivyokuwa awali lakini ikija kiwanda kikakaa sawa tutakuwa na warina asali wakubwa” amesema.Luleka ameyasema hayo wakati anazungumza na timu kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) iliyokwenda Sikonge kuzifahamu fursa zilizopo na kuufahamisha umma ili wenye mitaji wakawekeze.“Na asali inatangazika kweli ya miombo forest (misitu ya miombo), lakini kiwanda chetu kwa sababu tayari kimo mbioni kuanza tuna hakika ya kwamba tutapata. Lakini nikuambie kitu kimoja kwamba, matumizi ya duniani kwa takwimu za mwaka 2015 zinatakiwa metriki tani milioni 1.9 na kwa dunia nzima hii unaweza ukaona kuwa hii ni ajira kubwa sana” amesema.Kwa mujibu wa Luleka nchini zilizowekeza kwenye utengenezaji asali zinatengeneza fursa nyingi za ajira na kwamba, kiwango cha asali inayopatikana kote duniani ni kidogo kuliko mahitaji.“Hivi tu tunavyosema asali ya Tanzania itumike kuuzwa tu hapa nchini bado na haitoshi. Watumiaji ni wengi kwa sababu hata dawa asilia sasa hivi zinaitumia hiyo. Na sisi tunasema hivi huu mnyororo wa thamani utakapoenda kuboreshwa utaona mahitaji ya watumiaji wa asali yataongezeka”amesema.Luleka amesema, Halmashauri itatengeneza maarifa ili wananchi wapende kuitumia asali kama ilivyo kwa watu wanaotembea na chupa za maji ya kunywa.“Yaani kabla hujalala unaambiwa kwamba kunywa maji ya mbadalasini tumbo lako mafuta, kolestro na vitu kama hivyo. Yaani nakwambia ile dawa watu mtakunywa tu.Ukiwa na hangover, kining’inio kile kunywa maji ya asali ya asubuhi ya motomoto kimeondoka, watu hawatakunywa? Watalamba na wataitumia asali kwa wingi. Nataka niwaambie kwamba, asali ndio zao litakalopiku maji kwa siku za usoni” amesema Luleka.
Biashara
1
TANZANIA imepaa kwa nafasi mbili kwenye ubora wa viwango vya Fifa vilivyotolewa jana na sasa inashika nafasi ya 135. Kwa mujibu wa viwango hivyo, Ubelgiji bado inashika namba moja ikifuatiwa na mabingwa wa dunia Ufaransa, Brazil ikishika nafasi ya tatu, England ya nne na Ureno ni nia tano. Kupanda kwa nafasi mbili za Stars kunatokana na kufanya vizuri katika michuano ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia Qatar 2022 ambapo imefuzu hatua ya makundi. Uganda bado inaongoza kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ikishika nafasi ya 80, ikifuatiwa na Kenya kwenye namba 107 na Sudan inayotarajiwa kucheza na Taifa Stars kesho kutwa iko nafasi ya 128. Rwanda ni ya 130, Burundi 144, Ethiopia ya 151, Sudan Kusini ya 173,Djibouti ya 186, Somalia 199 na Eritrea ya 207. Senegal ndio kinara wa Afrika ikishika nafasi ya 20 ikifuatiwa na Nigeria nafasi ya 34 huku Mabingwa wa Afrika Algeria ni wa 38, Morocco 39 na Misri ni wa 49. Kwenye 10 bora zimeendelea kuwa nchi zilezile zikibadilishana tu namba, ambapo Uruguay ni ya sita, Hispania inashika nafasi ya saba, Croatia ni ya nane, Colombia ya tisa na Argentina inashika nafasi ya 10.
michezo
2
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Simba leo wanashuka dimbani kuwakabili Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa ligi hiyo utakaochezwa kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.Mchezo huo ni muhimu kwa Simba kama itashinda itafikisha pointi 81 katika michezo 31 na kuishusha Yanga iliyokaa kwa muda mrefu kileleni mwa msimamo ikiwa na pointi 80 katika michezo 34 iliyocheza. Wekundu hao wanapewa nafasi kubwa ya kushinda mechi hiyo kwasababu hawajapoteza mchezo wowote kwenye uwanja wa nyumbani tangu kuanza kwa msimu huu.Timu hizo zilikutana katika mchezo wa raundi ya kwanza kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga, na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1. Mwenendo wao kwenye ligi hivi sasa ni kama hawakamatiki kutokana na ubora wa kikosi chao kuanzia safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Meddie Kagere anayeongoza kwa mabao 17, John Bocco 14 na Emmanuel Okwi 11.Mpaka sasa unaweza kusema Simba ni bora zaidi kwenye ushambuliaji ikiongoza kwa kufunga mabao 61 ikifuatiwa na Yanga yenye mabao 54. Lakini pia, safu ya ulinzi iko vizuri kwani imefungwa mabao 12 kwenye nyavu zake ikiwa ndio timu pekee yenye mabao machache. Coastal Union inayoshika nafasi ya 10 kwenye msimamo, imeshacheza michezo 33 na ina pointi 41.Timu hiyo licha ya kuonyesha ushindani katika baadhi ya mechi zao zilizopita inaonekana kuwa na mapungufu kwenye safu ya ulinzi ikifungwa mabao mengi 33 kuliko mabao iliyofunga wao 29. Ni timu inayoonekana kucheza kwa kulinda na kushambulia kiasi kwani sare walizopata ni 14.
michezo
2
VINARA wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara Yanga wamesema mchezo wa leo dhidi ya Alliance hawana budi kuja na mbinu tofauti na ile waliyotumia katika mchezo uliopita wa Kombe la FA dhidi ya Namungo kutokana na aina ya timu wanayocheza nayo.Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 10.00 jioni kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza. Akizungumzia mchezo huo Kocha Mkuu Mwinyi Zahera alisema wapinzani wake wengi ni vijana wadogo na wana nguvu hivyo, anauona mchezo huo utakuwa wenye nguvu.“Tuko na morali na tuna mipango mizuri, kama wachezaji wataitumia katika mchezo huo tutaibuka na ushindi,”alisema. Alisema, kikosi chake kiko vizuri kutokana na kucheza michezo mingi ya ugenini.Vinara hao wanahitaji ushindi kuendelea kujiweka pazuri katika mbio za ubingwa. Iwapo watafungwa au kupata sare watakuwa kwenye uwezekano wa kushuka baadaye ikiwa tu mpinzani wake Simba atashinda michezo sita ya viporo vilivyobaki.Tofauti na Alliance haina cha kupoteza, ikishinda itazidi kujiimarisha na pengine kuendelea kujiweka katika nafasi za juu ila ikipoteza inaweza kushuka pia, nafasi moja au nne kutegemea na wengine walioko chini yake watakavyoshinda.Yanga inaongoza ligi kwa pointi 61 katika michezo 25 waliyocheza huku Alliance ikionekana kuwa na mwenendo mzuri hasa mzunguko huu wa pili baada ya kutoka kwenye mstari wa hatari hadi nafasi ya saba ikiwa na pointi 36 katika michezo 28.Mara ya mwisho kukutana na Yanga, Alliance ilifungwa mabao 3-0 kwenye uwanja wa taifa. Bila shaka timu hiyo itataka kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani kulipiza kisasi kwa Yanga kwa kuhakikisha inapata matokeo mazuri. Kikosi hicho kinachofundishwa na Kocha Malale Hamsini kimekuwa na mwenendo mzuri tangu kuchukua mikoba ya Mbwana Makata.Lakini kitakuwa na kazi kubwa ya kumdhibiti mshambuliaji bora wa Yanga Heritier Makambo aliyeifungia timu yake mabao 12. Bila shaka hawamtasahau katika mechi ya raundi ya kwanza alikuwa ni miongoni mwa waliowafunga katika ushindi wa 3-0.Wengine waliofunga ni Mrisho Ngassa na Ibrahim Ajibu. Yanga pia, haipaswi kuwabeza wapinzani wake kwasababu watataka kuweka rekodi bora ya kumfunga kigogo. Mwenendo wa timu zote katika mechi tano zilizopita inaonyesha kuwa wote hawakufanya vizuri sana kwa hivyo, kila mmoja anahitaji matokeo. Katika idadi hiyo, Yanga imeshinda miwili, sare mbili na kupoteza mmoja matokeo sawa na aliyopata Alliance. Yeyote anaweza kuibuka na ushindi kutegemea na maandalizi yao.
michezo
2
Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu wa Asasi hiyo David Msuya alisema, wajasiriamali hao ambao ni watumishi wenye ajira wameweza kupata mikopo hiyo kwa awamu mbalimbali.Alisema, wajasiriamali walionufaika na mkopo huo ni kutoka Mpwapwa mkoani Dodoma, Mbezi na Manzese jijini Dar es Salaam, Pwani, Kilombero na Mbuyuni mkoani Morogoro.Aidha aliwataka wajasiriamali kuhakikisha wanatambua sheria za mikopo na kuzitimiza ili waweze kupata mkopo na kuacha tabia ya kulalamika na kudai kuwa asasi mbalimbali zinatoa mikopo kwa njia ya rushwa au kwa kujuana jambo ambalo si la kweli.Hata hivyo Msuya alisema kuwa wamekuwa wakitoa mkopo kwa wajasiriamali mbalimbali nchini kupitia mradi wa boresha makazi ya mtumishi unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Ujerumani (Global It) ili kuwawezesha kuboresha biashara zao na hatimaye kuboresha makazi yao.
Biashara
1
WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani amewasha umeme kwa ‘Babu wa Kikombe’ Mzee Ambilikile Mwasapila eneo la Samunge wilayani Ngorongoro Mkoa wa Arusha.Dk Kalemani amewasha umeme huo jana nyumbani kwa Mzee Ambilikile katika Kata ya Samunge, na kueleza kuwa serikali imetoa Sh bilioni 28 kwa Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kuhakikisha umeme wa kawaida na ule wa vijijini (REA) unasambazwa katika wilaya mbali mbali.“Nashukuru leo hii kuja hapa kuzindua umeme wewe Mzee Ambilikile na naomba wakandarasi wa Kampuni ya Nipo Group kuendelea kusambaza umeme wilayani hapa kwa kasi kubwa na msiache nyumba hata moja,” alisema Dk Kalemani. Naye Mzee Ambilikile ameshukuru serikali kwa kumwashia umeme yeye na wananchi wa kata hiyo ya Samunge kwani ni ishara kubwa ya maendeleo.“Kuwashwa kwa umeme huu kunatimiza maono ya ndoto yangu niliyooneshwa na Mungu mara kadhaa kuwa Tanzania ni kioo cha Afrika na hii leo imejidhihirisha,” alisema. Naye Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William ole Nasha alishukuru serikali kwa kuleta umeme katika wilaya hiyo na kusisitiza kuwa maendeleo ya jimbo hilo yanaimarika siku hadi siku.
Kitaifa
0
TIMU ya taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano ya 17 ya dunia inatarajia kuagwa jijini Arusha Septemba 23, imeelezwa. Tanzania katika mashindano hayo ya Dunia yatakayofanyika Qatar mwaka huu kuanzia Septemba 27 hadi Oktoba 6, itapeleka wanariadha wanne tu, watatu wakiume na mmoja wakike, wote wakishiriki mbio za marathoni.Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Wilhelm Gidabuday alisema jana kuwa, timu hiyo ambayo itakuwa na wanariadha wanne na viongozi watatu wa RT, itaagwa jijini Arusha tayari kwa safari siku inayofuata. Wanariadha hao na muda wao bora katika mabano ni Augustino Sulle (2:07:44), Alphonce Simbu (2:08:27) na Stephano Huche (2:12:24) wakati mwanamke pekee katika msafara huo ni Failuna Abdi (2:27:36).Gidabuday alisema mwanariadha mwingine aliyefuzu kushiriki mashindano hayo ya dunia ni Ezekiel Ngimba 2:13:34, lakini kutokana na kanuni za Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Riadha (IAAF) kuruhusu nchi kuwa na wachezaji watatu katika mchezo mmoja, Ngimba ameenguliwa sababu ya muda wake kutokuwa mzuri. Gidabuday alisema kuwa hivi karibuni watamtangaza mgeni rasmi atakayekabidhi bendera timu hiyo, ambayo watu wengine wanaotarajia kuwemo ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa RT, William Kallaghe, ambaye anamuwakilisha Rais wa shirikisho hilo, Antony Mtaka. Wengine wanaotarajia kuwemo katika msafara huo ni Gidabuday mwenyewe na makamu wa pili wa RT, Dk Hamad Ndee. Timu hiyo kwa mujibu wa Gidabuday, itaondoka mafungu mawili, ambapo kundi la kwanza, ambalo litakuwa na Kallaghe na Failuna wataondoka mara baada ya kuagwa wakati fungu jingine litaondoka Oktoba 2. Alisema Failuna anawahi kwa kuwa mbio yake itachezwa siku ya ufunguzi wa mashindano hayo Septemba 27 wakati Kallaghe anawahi sababu ya Mkutano Mkuu wa IAAF, ambao utakuwa pia na Uchaguzi Mkuu.Mkutano Mkuu wa 52 wa uchaguzi utafanyika Septemba 25 na 26 na utawachagua Rais wa IAAF, makamu wanne wa rais na wajumbe 13 wa Kamati ya Utendaji.
michezo
2
Aidha, mkutano huo ambao kwa mara ya kwanza utafanyika jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine utapambwa na maonesho mbalimbali ya bidhaa zitokanazo na zao hilo.Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo, Dk Herman Moshi, alisema tafiti zinaonesha kaya nyingi za Watanzania zinapenda kufuga kuku ikilinganishwa na mifugo mingine, lakini ufugaji huo umekuwa chini ya kiwango kutokana na kukosa mbinu bora na za kisasa.“Jumuiya zote za wafugaji wa kuku ndani ya SADC zinakutana Dar es Salaam kuanzia Desemba 3 mwaka huu, hivyo nawaomba Watanzania mjitokeze kujifunza mbinu bora za ufugaji wa kuku na mazao yake kutoka kwa wenzetu wa mataifa mbalimbali,” alisema Dk Moshi.Alifafanua kuwa kuku wakifugwa ipasavyo kwa muda mfupi wanaweza kutoa mayai mengi, uzito mkubwa, hivyo kukuza uchumi wa kaya na taifa kwa kasi kubwa.Alisisitiza kuwa mkutano huo, ambao utakaribisha watu wote, utatoa taswira chanya ya namna bora na ya kisasa ya ufugaji wa kuku wenye tija utakaokuwa na malengo ya kukuza uchumi wa mtu na taifa kwa ujumla.“Wadau wa zao hili na wafugaji watapata fursa ya kuwasilisha aina ya kuku wanaowafuga na wataruhusiwa kuwauza lengo likiwa ni kukuza zao hili."Kwa upande wake, Mratibu wa Mkutano huo kutoka Baraza la US GRAINS, Tawi la Tanzania, Mary Ngalaba, alisema mbali ya maandalizi ya mkutano huo, pia kwa sasa wako kwenye mchakato wa kumalizia kazi ya uundaji wa Chama Kikuu cha Kitaifa cha Ufugaji Kuku ambacho hakipo nchini ikilinganishwa na mataifa mengine.Alisema uundaji wa chama hicho kwa kushirikisha jumuiya za ufugaji nchini unatarajia kumalizika Septemba mwaka huu.
Biashara
1
Wamesema hatua hiyo itaongeza mitaji, pia kutoa hamasa kwa wanachama kupata mikopo mingi zaidi itakayowasaidia katika shughuli za kiuchumi.Meneja wa Saccos hiyo, Abbas Rajab akisoma taarifa ya Saccos kwa Rais Jakaya Kikwete, jana kabla ya kuizindua, alisema Saccos hiyo yenye wanachama 1,779 kati ya hao wanawake wakiwa ni 500 imefanikiwa kuwa na mtaji wa Sh bilioni 4.3 na mikopo iliyokopeshwa na kurejeshwa ni Sh bilioni 3.3 , wakati mikopo ya kiasi cha Sh bilioni 1.04 haijarejeshwa na wanachama.Kwa mujibu wa meneja huyo chama kinajiendesha chenyewe bila kutegemea mikopo kutoka nje na kwamba hadi sasa kina mtaji wa Sh bilioni 1.4 zikiwa ni akiba, amana na limbikizo la ziada.Hata hivyo, alisema kutokana na hayo, Saccos hiyo imepata mafanikio kupunguza kero mbalimbali za kiuchumi na kijamii na kutengeneza ajira kutokana na wanachama wake kununua magari 100, pikipiki 150 na kufungua maduka.Kwa mujibu wa meneja huyo kuna changamoto kubwa kwa baadhi ya wanachama kutorejesha mikopo kwa wakati na tozo la kodi kubwa ya TRA ya asilimia 30 na kumwomba Rais kuwapatia majawabu ombi hilo.Kwa upande wake, Rais Kikwete, kabla ya kujibu hoja hizo, aliwapongeza wananchi hao kwa kuanzisha Saccos ambayo inajitegemea kimtaji na kukopesha wanachama wake fedha nyingi.Rais alisema utaratibu wa kuanzisha Saccos lilikuwa ni jambo zuri kwa kuwa ni chombo kinachoweza kumkomboa mwananchi wa kawaida kwani mabenki si rafiki wa watu masikini.“Vyama hivi vimeanzishwa ili kumkomboa mtu wa chini kwani mabeki si rafiki yao na Saccos zina faida ya kuwawezesha wanachama kujikopesha kwa ajili ya maendeleo yao ya kukuza uchumi wa mtu moja mmoja na taifa,” alisema Rais.Katika hotuba hiyo alikubali ombi lao kwa kuwapatia kompyuta hizo tatu na kuwasihi wanachama kujenga tabia ya kurejesha mikopo kwa wakati ili wanufaishe na wenzao.
Biashara
1
UJENZI wa gati namba moja katika Bandari ya Dar es Salaam uliokuwa ukamilike Desemba mwaka huu, umekamilika mwezi mmoja kabla hivyo kufungua milango kuanza kuhudumia meli kubwa nyingi zaidi.Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana ilisema gati hiyo imejengwa kisasa zaidi na kuvutwa ndani ya maji kwa ukubwa wa mita 200, huku kina cha maji kikiwa mita 15 na kuifanya yenye kina kirefu zaidi.Akizungumza jana jijini Dar es Salaam mara baada ya kukagua mradi huo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, alisema amefurahi kukuta mradi huo ambao utakabidhiwa Novemba 28, mwaka huu ukiwa umekamilika mapema zaidi ya ilivyotarajiwa awali na wajenzi wa mradi huo.“Mwanzo tulikuwa tunatumia gati namba saba pekee kuhudumia meli kubwa zilizoingia bandarini, lakini sasa wigo umekuwa mpana zaidi kwani zitakuwa zikihudumiwa hapa,” alisema Waziri Kamwelwe.Alisema gati namba saba inayotumika kuhudumia meli kubwa kwa sasa ina urefu wa kina cha maji cha mita 10, hivyo kukamilika kwa gati mpya yenye urefu wa kina cha maji cha mita 15 ni ukombozi zaidi.Alisema kukamilika kwa gati hiyo, kutapunguza foleni ya meli zinazokaa nje ya eneo la bandari na kadri gati nyingine zinavyokamilika, itafikia wakati hakutakuwa na meli inayosubiri nje ya eneo la bandari.“Ikifikia wakati meli zinaingia na kutoka kwa haraka, ndio bandari yetu itakavyovutia wafanyabiashara wengi zaidi na hivyo kuifanya iwe shindani na kuongeza pato la taifa,” alisema Waziri Kamwelwe.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko alisema waziri amefanya vyema kutembelea na kujionea maendeleo ya mradi wa “Dar es Salaam Maritime Gateway Project”.Alisema maboresho hayo yamefanyika ndani ya kipindi kifupi kwani hadi sasa, hata nusu ya muda wa mradi uliopangwa haujafika, wakandarasi wameomba gati nyingine mbili na wamewapa wajenge.“Tayari tumeshawakabidhi gati namba mbili na tatu ili waendelee na ujenzi na matumaini yetu ni kwamba, mradi huu utakamilika kwa muda uliopangwa,” alisema Kakoko na kuongeza kuwa gati maalumu ya kushushia magari (RoRo), nayo inatarajiwa kukamilika mwezi wa sita mwakani.“Hii maana yake ni kwamba mwezi wa sita mwakani tutakuwa tumekamilisha ujenzi wa gati hii ya magari na gati nyingine mbili (namba mbili na tatu) na meli kubwa zitahudumiwa bila shida,” alisema.Kakoko alisema ujenzi wa gati hizo utakapokamilika, hakutakuwa na meli inayosubiri nje ya eneo la bandari tena kwa sababu watakuwa na uwezo wa kuhudumia meli nyingi kubwa kwa wakati mmoja.Mkataba wa kuboresha gati namba moja hadi saba na ujenzi wa gati jipya la kuhudumia meli za magari (RoRo Berth) Gerezani Creek kati ya TPA na Mkandarasi M/s China Habour Engineering company limited CHEC, ulisainiwa Juni 10, 2017, kwa jumla ya Sh 336,410,302,688.90 ikiwa ni pamoja na VAT.Mkataba huo ni wa miaka mitatu na mkandarasi alikabidhiwa eneo la mradi Juni 29, 2017 na kuanza maandalizi ya ujenzi. Ulizinduliwa na kuwekwa jiwe la msingi na Rais John Magufuli Julai 2, 2017.Hata hivyo, mradi wa upanuzi wa bandari, ujenzi wa magati na kuongeza kina cha kupakia na kupakua mizigo, utaiwezesha bandari kuhudumia meli kubwa zaidi ambapo hivi sasa hamna kina cha mita 12 ambapo inazifanya meli nyingi kuwa kwenye foleni na kulazimika kusogeza meli moja moja. Kukamilika kwa mradi huu pia kutaiwezesha TPA kuwa na uwezo wa kushusha mizigo ya kutoka kwenye meli kubwa saba kwa wakati mmojab.
Kitaifa
0
Ikiwa umepita mwaka mmoja tangu wanajeshi 15 wa Tanzania ambao walikuwa ni walinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa kuuawa huko Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, Mkuu wa Shughuli za Ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa, Jean Pierre Lacroix ametembeleza familia za wanajeshi hao.Lacroix ametembelea familia hizo za marehemu visiwani Zanzibar kama sehemu ya ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania, ambayo imemalizika jana.Akizungumza na familia hizo, Lacroix aliwaambia kuwa Umoja wa Mataifa unaomboleza vifo vya mashujaa hao kwani ni idadi kubwa ya walinda amani kuwahi kupoteza maisha kwa wakati mmoja wakiwa kwenye majukumu yao.Mashambulizi yaliyofanyika Semuliki yalikuwa mashambulizi hatari kuliko yote yaliyowahi kutokea miaka ya nyuma, ndugu zenu hawa waliotangulia ni mashujaa wa Tanzania” alisema Bwana Lacroix.Walinda amani hao waliopoteza maisha katika eneo la Semuliki, Kivu Kaskazini wakifanya shughuli za kulinda amani.
Kitaifa
0
MFANYABIASHARA Rostam Aziz, Kampuni ya GSM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete wameichangia Yanga zaidi ya Sh milioni 500 katika hafl a iliyofanyika Dar es Salaam jana.Katika hafla hiyo iliyofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam na Waziri Mkuu Majaliwa akiwa mgeni rasmi, GSM iliahidi kuchangia Yanga Sh milioni 300 huku Rostam akichanga Sh milioni 200, Majaliwa akichangia Sh milioni 10 na Kikwete milioni tano.Harambee hiyo iliendelea hata baada ya kuondoka kwa Waziri Mkuu na baadae Kikwete, ambapo wanachama waliendelea kutoa fedha na ahadi ili kuisaidia Yanga kufanya usajili wa nguvu pamoja na uendeshaji wa klabu hiyo.Akizungumza kabla ya kuchangia, mgeni rasmi huyo aliwapongeza Yanga kwa kuwa watulivu kipindi ambacho walikuwa wakikabiliwa na changamoto ya kifedha, lakini timu yao ilifanya vizuri kwa kumaliza ligi katika nafasi ya pili na kupata ushiriki ujao kimataifa.“Timu ya mpira ili iweze kufanya vizuri ni lazima iwe na fedha kwa ajili ya uendeshaji kuwalipa makocha na wachezaji, bila Yanga imara hatuwezi kuwa na Simba imara, kila mmoja achangie kuiwezesha timu kuwa na uchumi mzuri,” alisema.Aliupongeza uongozi mpya akisema umeanza kuonesha mwanga wa mafanikio mbele akiwahimiza watengeneze mfumo utakaosaidia kuongeza mapato ya ndani. Pia, akimpongeza Kocha Mwinyi Zahera kwa kufanya vizuri msimu uliopita.Kwa upande wake mgeni maalumu wa tukio hilo , Kikwete alisema kuna haja kwa klabu za Tanzania ku- fanya uwekezaji kwa vijana ili kupata wachezaji bora watakaosaidia timu ya taifa baadaye. Kikwete alisema klabu zinatumia pesa nyingi kuleta makocha kwa ajili ya kufundisha wachezaji wa nje huku watu wakibaki kuwasifia lakini kwenye timu ya taifa hawamo na kusisitiza kuwa wasipoweka juhudi kwenye timu za watoto watabakï kuwa mafahali wa wengine.Aliwataka Yanga kuten- geneza mfumo mzuri wa uendeshaji, kuwa wa kisasa na kuwekeza kwenye timu za watoto. Pia, alihimiza viongozi wapya wa Yanga kurudisha hamasa kwa mashabiki kama iliyokuwa zamani. “Mnabaki kuwasifia akina Kagere (Meddie) waki- ondoka hatuwaoni kwenye timu za taifa. Ifike mahali muone fahari kwa wachezaji wa ndani na kuwaendeleza wale wenye vipaji, “alisema.Aliwahimiza Yanga kutengeneza mfumo endelevu utakaosaidia kuongeza mapato ya ndani badala ya kuwategemea wafadhili na mwisho wa siku wakipata matatizo na klabu inateter- eka. Pamoja na hayo, alimpongeza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kushiriki tukio hilo bila kujali ushabiki wake akisema huo ndio uongozi bora na kuongeza kuwa kama mtu akiwa kiongozi haipendezi kutumia ushiriki wake wa kimpira kukandamiza klabu nyingine.Mbali na michango hiyo pia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliwapatia Yanga eneo Kigamboni kwa ajili ya kujenga uwanja wa soka. Katika hatua nyingine, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakale- bela aliwatambulisha wachezaji wapya wawili, Abdulaziz Makame na mfungaji bora wa Uganda Juma Balinya aliyejiunga nao kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Polisi FC ya Uganda.
michezo
2
VANILA ni zao linalojulikana zaidi mkoani Kagera kama ‘dhahabu ya kijani’ kutokana na kuwa mkombozi wa wakulima wengi. Hii ni kwa kuwa, ukiwa na miche japo mitano, ni kama vile tayari una dhahabu shambani kwako.Tangu mwaka 2015 dhahabu ya kijani (vanilla) imekuwa mkombozi hali iliyochochea kasi ya kilimo cha zao hili kiasi kwamba, kijana wa miaka 20 au mzee wa miaka 70 kumiliki Sh milioni 20 hadi 30 ni jambo la kawaida hasa katika msimu wa mavuno. Kimsingi, vanila ni zao linaloweza kufanya mabadiliko makubwa na kuinua uchumi katika familia, jamii na taifa kwa jumla.Kadri muda unavyopita ndivyo idadi ya wakulima inavyoongezeka kwani mpaka mwaka 2013 Mkoa wa Kagera ulikadiriwa kuwa na wakulima 600 wa vanilla 600, lakini idadi hiyo imeongezeka na sasa wakulima wa zao hilo ni zaidi ya 6,000. Zao hili linalimwa katika sehemu yenye kivuli hasa kwenye migomba au kwenye miti na linahitaji kiasi cha mwanga kuwa sawa na kiasi cha kivuli; yaani kwa asilimia 50 kwa 50.Vanila inapopandwa, huwekewa mti aina ya jatrofa ili kukua kwa kupanda mti huo na mazao yake ni kama maharage. Hadi sasa bei ya vanila kwa walanguzi wa vanila changa ni kati ya Sh 20,000 hadi 30,000 kwa kilo moja. Mwaka 2017/18 bei ya vanilla mkoani Kagera ilifikia kati ya Shi 100,000 hadi 150,000. Katika siku za nyuma, vanilla iliwahi kuzalishwa mkoani Kagera hadi kufikia tani 103.Katika kipindi hicho, bei ya vanila ilikuwa chini hadi kufikia Sh 4,500 kwa kilo moja. Kwa sasa zinazalishwa tani 10 hadi 12 za zao hili. KILIMO CHA VANILA KAGERA Kilimo cha vanila mkoani Kagera huwafanya wakulima wengi kulala katika mashamba yao au kuajiri vibarua kwa muda na kungoja mazao hayo yakomae shambani ili kulinda shamba usiku na mchana.Katika miaka ya nyuma, wakazi wa Kata ya Kanyigo iliyopo wilayani Missenyi hawakuona umuhimu wa kulima vanila na badala yake, wakajikita katika mazao mengine kama kahawa na ndizi, lakini sasa kuna wakulima 1,500 wa vanilla wanaolenga kujiinua kiuchumi na kuongeza pato la taifa. Mpaka sasa kata hii kupitia Shirika la Maendeo Kanyigo (Kadea), imeunda umoja wa wakulima unaolima mazao matatu ili kujikwamua kiuchumi ambayo ni kakao, chai na vanila.Shirika hili linahimiza walau kila mwananchi kuwa na zao mojawapo kati ya hayo na kuachana kabisa na kasumba ya kulalamikia uchumi huku wengine wakikalia kusema hakuna fedha wakati hawana cha kuuza.Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima wa Kata ya Kanyigo, Yese Mshobozi, anasema mwitikio ni mkubwa japo changamoto ni baadhi ya watu wasiopenda kufanya kazi ambao wengine, hushiriki vitendo vya wizi vinavyowatesa wakulima na kurudisha nyuma kasi ya maendeleo ya wakulima hao. Anasema uwepo wa wizi katika mashamba ya vanilla umesababisha kuitishwa kikao cha dharura chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Marco Gaguti na Mkuu wa Wilaya ya Missenyi, Denice Mwila ili kuweka mikakati itakayoimarisha ulinzi wa zao hilo na kuongeza uzalishaji wake.Kikao hicho kiliwashirikisha wakulima takriban 2,000 kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Missenyi waliokutana na Mkuu wa Mkoa katika Kata ya Kanyigo. Miongoni mwa mambo makubwa yaliyodaiwa katika kikao hicho, ni pamoja na mikakati imara ya kuwanufaisha wakulima na kuinua uchumi wa mkoa, badala ya wananchi kutegemea mazao kama ndizi na kahawa pekee. Hii ni kwa kuwa mazao hayo yamekuwa yakilimwa kwa mazoea, hivyo kutomnufaisha mkulima kutokana na uwezekezaji mdogo na teknolojia duni katika mnyororo wa thamani hadi sokoni.Mkuu wa mkoa alipofika Kanyigo, pia alitembelea na kukagua shamba la vanila la Mwalimu Jovin Mbanga na baada ya hapo, alikutana na wakulima na kusikiliza kilio chao hususan kuhusu kero ya wizi wa vanila changa na marando katika mashamba. Ilidaiwa kuwa, vanilla inapoibwa shambani, huuzwa nchi jirani ya Uganda.Wakulima hao walimweleza Mkuu wa Mkoa (Gaguti) kuwa, changamoto kubwa inayowakabili ni wizi wa vanila, hali inayowalazimisha kulala katika mashamba usiku mzima ili kulinda mazao yao yasiibwe. Ilielezwa kuwa, wizi huo hufanywa na baadhi ya Watanzania wasiokuwa wazalendo wanaoshirikiana na wafanyabiashara kutoka nje nchi kwa kupewa mitaji ya kununulia vanila za wizi, hali inayowafanya kuwahujumu Watanzania wenzao.Changamoto nyingine walizomwambia Mkuu wa Mkoa, wakulima walisema ni kutokuwa na masoko rasmi ya kuuza vanila inapokomaa na kuvunwa sambamba na wanunuzi wa vanilla kutosajiliwa na kutambulika kiserikali ili mwananchi mwenye vanila, auwauzie kupitia soko maalumu yaani, kwa mnunuzi maalumu. Baada ya kusikiliza kero hizo za wakulima, mkuu wa mkoa huyo aliagiza kila mmoja kuhakikisha vanila inakuwa na muda maalumu wa kuvunwa katika mashamba na kwamba, kutakuwa na vituo maalumu kama masoko ya kununulia vanila.Alisema ni marufuku na kosa kubwa kwa mfanyabaishara yeyote kwenda kwa wakulima moja kwa moja kununua zao hilo. “Sisi kama serikali hatujafikia uamuzi wa kumfunga kamba kila mwananchi kulima, isipokuwa kwa kuwa kuna soko la kutosha, kila mwananchi aone umuhimu na atumie fursa zilizopo kulima na kujiinua hivyo maamuzi ninayoyatoa kuanzi sasa ni kwamba, mwananchi yeyote atakayekamatwa na vanilla kabla ya tarehe ya kuvunwa kutangazwa atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi,” anasema Gaguti.Anasema bila wakulima wa vanila kujiunga kwa njia ya ushirika na kutambuliwa, hata kubaini wezi itakuwa vigumu hivyo ni vyema wakulima wa vanilla wajiunge katika ushirika wa vyama vya msingi hali itakayowasaidia katika mambo mengi likiwamo hili la kubaini wezi wa mazao yao shambani. Aidha, Gaguti alisema hali hiyo itawapa soko la uhakika la kuuza mazao (vanila) ambayo tayari imeongezwa thamani na hivyo, kupata bei nzuri zaidi. Alisema hali hiyo pia itaweka urahisi zaidi kwa Serikali kuwasimamia kama ushirika kuliko mwananchi mmoja mmoja.Mkuu wa mkoa anawataka wafanyabiashara wote zikiwamo kampuni zinazojihusisha na ununuaji wa vanila kujisajili na kupewa leseni ya kununua zao hilo kuliko ilivyo sasa. Akazitaka pia kampuni zinazotoa ruzuku kwa wakulima, kununua vanila kwa wakulima kwa kadiri ya bei ya soko, badala ya kuwapunja na kuwanyonya wakulima.Akawataka watendaji wa vijiji na kata kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kikamilifu kama wanataka kuendelea kubaki kazini hasa jukumu la ulinzi na usalama kwa mfumo wa Nyumba Kumi Bora za Usalama ambapo wezi wa vanila watabainika kirahisi kila eneo. Wakulima Erick Godison na Deogratias Tibakilana wanasema mbele ya mkuu wa mkoa kuwa, wezi wa vanila wanajulikana kwani vijiji vilishafanya upigaji kura na kuwabaini wezi ambao majina yao yalipelekwa kwa mkuu wa wilaya ya Missenyi.Walishauri watu waliotajwa katika kura hizo kuhusika na wizi wa vanila wahojiwe ili wabainishe hizo vanilla wanazitoa na kuziuza wapi wakati hawalimi. Mkuu wa Mkoa anamwagiza Mkuu wa Wilaya ya Missenyi, kuwachukulia hatua wote waliotajwa wakituhumiwa kuhusika na wizi wa vanila. Katika mkutano huo, Mwila (Mkuu wa Wilaya) anawataka wananchi wilayani kwake wakiwamo wakulima wa vanila katika Kata ya Kanyigo, kubadilika kwa kuwa wizi mwingine wa vanila hutokea ndani ya familia.Mwila anatoa mfano kuwa, unakuta shamba ni la baba na akitoka kwenda pengine Bukoba Mjini kufanya shughuli zake mama au mtoto anavuna vanilla haraka haraka na kuziuza na baba akirudi, anaambiwa vanila zimeibwa.
Kitaifa
0
OFISA Maendeleo ya Jamii katika Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Sophia Swai amesema wamebaini mbinu mpya ya wazazi kuwakatisha watoto wao wa kike masomo. Watoto hao wanakatishwa masomo ili wakafanye kazi za ndani kwa kuwazuia wasiende shule kwa makusudi kwa siku 90 ili waandikwe mtoro wa kudumu na afutwe.Hayo yalibainika juzi wakati wa mkutano wa watendaji wa kata na vijiji ulioandaliwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali la Woman Wake Up (WOWAP) ambalo linatekeleza mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia,mimba na ndoa za utotoni.Alisema wamegundua mbinu hiyo mpya wanayotumia wazazi ili baada ya miezi mitatu mtoto huyo aonekane kuwa mtoro wa kudumu na afutwe shule. “Kwenye kijiji cha Manchali, wazazi walifanya makusudi ili mtoto asifike shuleni kwa siku 90, mtoto akafutwa shule kisha wakampeleka Dar es Salaam kufanya kazi za ndani” alisema.Alisema sasa wataanza kuwafuatilia watoto watoro ili kuona kama wazazi wanahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria. Swai alisema kumekuwa na changamoto kubwa ndani ya wilaya hiyo kwa wazazi kutaka watoto wao hasa wa kike waandike madudu kwenye mitihani ili wasifaulu na wabaki nyumbani kwa lengo la kuwaoza au kuwapeleka mijini kwenda kufanya kazi za ndani.Alisema tatizo hilo lilikuwa kubwa sana katika shule ya msingi ya Mapinduzi lakini baada ya wanafunzi kuelimishwa matokeo yameanza kuwa mazuri kwa shule hiyo. Alisema mwaka 2015 walifaulu wasichana watatu, mwaka 2016 hakuna mwanafunzi wa kike aliyefaulu, 2017 mwanafunzi mmoja na mwaka 2018 wanafunzi 17 wa kike walifaulu kati ya wanafunzi 23.“Tunajivunia ufaulu huo na tutatoa hamasa kwenye shule za msingi ili watoto wa kike wafanye vizuri darasani ili hatimaye wafikie ndoto zao” alisema.Alisema sasa watakwenda kuongea na wazazi wa watoto 17 waliofaulu ili kuhakikisha wote wanaripoti na kuanza kidato cha kwanza.“Tunaenda kuongea na wazazi wa watoto hao 17, tutaawaambia ukweli ole wao mtoto aache shule, tunajua tusipokuwa makini wataripoti tu wawili kuanza kidato cha kwanza” alisema Kwa upande wake, Mtendaji wa kata ya Mpwayungu, Peter Chugu alisema wazazi bado wanaendelea kuoza watoto wa kike wakiwa katika umri mdogo.Alisema katika tukio la hivi karibuni wanafunzi wawili wa kidato cha tatu na nne wamepata ujauzito lakini walikataa kuwataja wahusika. Alisema hali kama hiyo imekuwa ikisababisha wahusika kutojulikana na kuendelea kuharibu maisha ya watoto wa kike.Pia katika kijiji cha Nagulo, mwanafunzi wa shule ya msingi Nagulo aligundulika kuwa na ujauzito na uongozi wa shule ukaripoti tukio hilo polisi ambao wanasema upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea. Mtendaji wa kata ya Mlowa barabarani George Mzuri alisema Oktoba 6, mwaka huu, mkazi wa kata hiyo Bahati Ndahani alikutwa na mwanafunzi kwenye nyumba ya kulala wageni.Alisema baada ya kupimwa mwanafunzi huyo aligundulika kuwa mjamzito na hatimaye kesi hiyo kufunguliwa polisi na kwenda mahakamani. Alisema vitendo vya ukatili katika jamii vipo na vimekuwa vikiibuliwa na wananchi wamekuwa wakitoa taarifa pindi wanapobaini kuna njama za kufungwa kwa ndoa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 18.Mratibu wa WOWAP, Nasra Suleiman alisema wataendelea kushirikiana na watendaji hao ili kubaini vitendo vyote vya ukatili vinavyoendelea katika jamii sambamba na kuibua matukio ya mimba na ndoa za utotoni.
Kitaifa
0
Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi alipokuwa anazungumzia ripoti ya utafiti wa watalii walioingia nchini mwaka 2014.Alisema utafiti huo ulifanywa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Uhamiaji na Kamisheni ya Utalii Zanzibar (ZCT).Alisema Zanzibar ilipata Dola za Marekani milioni 269.3 mwaka 2014 ikilinganishwa na Dola za Marekani milioni 210.5 mwaka 2013.Dola moja ni sawa na Sh 2,100 kwa sasa.Aidha, alisema wastani wa matumizi yote kwa mtalii kwa siku ilikuwa Dola za Marekani 221 chini kidogo ya Dola za Marekani 284 zilizoripotiwa mwaka 2013.Pia alisema masoko makuu 15 ya utalii yanachangia asilimia 82 ya watalii wote wa kimataifa Zimbabwe, Uholanzi na China ni masoko mapya katika masoko makuu 15 kwa mwaka 2014 ambayo yamechukua nafasi ya Sweden, Uswisi na India katika masoko makuu 15 yaliyopatikana mwaka 2013.Aidha, alisema utalii wa wanyamapori Tanzania Bara ulichangia asilimia 43.5 na wageni wengi waliokuja kwa ajili ya wanyampori walitokea Uingereza, Ufaransa na Italia.Pia alisema ripoti hiyo inaonesha watalii wengi walionekana kutofurahishwa na kutokuwa na huduma ya malipo ya fedha kwa kutumia kadi katika maeneo yanayotoa huduma za kitalii na asilimia 87 ya watalii walilipia huduma mbalimbali za kitalii kwa kutumia fedha taslimu.
Biashara
1
Tayari wapinzani wao, Simba wako kambini nchini Afrika Kusini kujiandaa na ligi hiyo inayotarajiwa kuanza Agosti 26, 2017. Meneja wa Yanga, Hafidh Salehe (pichani) alisema wamechagua Morogoro kwani kuna mazingira tulivu yatakayowasaidia.Alisema wachezaji wote waliosajiliwa wataenda ili kutoa nafasi kwa Kocha kutengeneza kikosi bora cha msimu ujao. Yanga imesajili wachezaji kadhaa na kuwaongezea mkataba waliomaliza.Imewasajili Ibrahim Ajibu, Youthe Rostand, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ Baruan Yahya, Pius Buswita na imewaongezea mkataba Donald Ngoma, Amis Tambwe na Thaban Kamusoko. Yanga itacheza mechi ya kwanza ya ligi dhidi ya Lipuli FC ya Iringa Agosti 27, uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam
michezo
2
MKUU wa wilaya ya Arusha, Fabian Daqaro (pichani) amewakaribisha wawekezaji katika sekta ya burudani ili kuvutia watalii na kusaidia viwanda vya ndani vinavyozalisha vinywaji vikali na vilaini kuimarisha masoko yao ya ndani.Rai hiyo ameitoa jijini Arusha wakati alipozindua Klabu Mpya yenye hadhi ya kimataifa ya Cocoriko Anex iliyopo katika ukumbi wa Papa King zamani ikijulikana kwa jina la Tripple A na kueleza kuwa ukumbi huo uwe kichocheo cha utalii katika Jiji la Arusha.Alisema kuwa Jiji la Arusha linahitaji kumbi za starehe za kisasa ili kukidhi matakwa ya wa- geni mbalimbali wanaoingia mkoani hapa kwa ajili ya utalii hivyo aliwaalika wawekezaji kuja kuwekeza katika sekta hiyo ili kusaidia viwanda vya ndani vinavyozalisha vinywaji vikali na vilaini kupata masoko ya uhakika. “Kufunguliwa kwa Klabu hii ya Cocoriko kuwe kichocheo cha viwanda vyetu vinavyozalisha vinywaji vikali na vilaini kuimarisha masoko ya ndani na hivyo kuendana na sera ya Rais John Magufuli ya ujenzi wa viwanda,” alisema Daqaro.Awali mwekezaji wa Klabu hiyo, John Mdenye, ambaye pia ni mmiliki wa Klabu ya Cocoriko iliyopo Kijenge na Mjengoni Classic. Alisema kuwa uwekezaji wa klabu hizo umemfanya kutoa ajira kwa watu 200. “Tumetengeneza klabu yenye hadhi ya kima- taifa na itakayosaidia kuongeza idadi za kumbi za starehe katika jiji la Arusha na hivyo kuwa kichocheo kipya cha burudani kwa wageni mbalimbali watakaofika katika Jiji la Arusha,” alisema Mdenye.
michezo
2
KINARA wa mabao Ligi Kuu Bara, Salim Aiyee wa Mwadui hajajumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars chini ya kocha Emmanuel Amunike, suala ambalo amekiri limezidi kumuongezea hasira na changamoto ya kufanya vizuri zaidi ili wakati mwingine ajumuishwe katika kikosi hicho.Aiyee, ambaye ana mabao 15 dhidi ya wapinzani wake wa karibu; Meddie Kagere wa Simba na Heritier Makambo wa Yanga, ambao kila mmoja amefunga mara 12, tofauti ilivyotarajiwa na wengi mshambuliaji huyo hajajumuishwa katika kikosi hicho kinachojiandaa kucheza dhidi ya Uganda kuwania kushiriki michuano ya Afcon.“Hapo awali sikuwahi kuitwa Stars kwa hiyo kwangu si kitu cha kushangaa sana ingawa kwa kasi na juhudi nilizonazo msimu huu wengi walitarajia itakuwa hivyo, pamoja na hayo naona bado nina nafasi ya kuitwa katika siku za usoni.Stars ipo Kundi L katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 5 sawa na Lesotho iliyo nafasi ya tatu.Kinara ni Uganda yenye pointi 13 wakati Cape Verde ikiwa ya mwisho na pointi zake nne. Stars itahitaji ushindi katika mchezo huo huku ikiombea Lesotho ifungwe na Cape Verde.
michezo
2
BEKI ya Taifa Stars, Erasto Nyoni amesema kwa sasa anaendelea vizuri, hivyo kama kocha Emmanuel Amunike atampanga mechi dhidi ya Kenya, Alhamisi, atacheza bila shida yoyote.Nyoni yupo mjini hapa na Taifa Stars inayoshiriki michuano ya Afcon na juzi alishindwa kucheza mechi ya kwanza dhidi ya Senegal kutokana na kusumbuliwa nyama.“Nina shida kidogo ya mguu, nyama zinanisumbua lakini nilishaanza mazoezi mepesi mechi ijayo naweza kucheza kocha akinipa nafasi,” alisema.Kukosekana na Nyoni kuliipa Stars pengo kubwa katika nafasi ya ulinzi, jambo lililofanya Senegal kuipenya ngome ya Stars kirahisi na kuwa mzigo mkubwa kwa kipa Aishi Manula aliyelazimika kuokoa hatari kibao langoni mwake mara kwa mara.Katika mechi hiyo, Stars ilifungwa mabao 2-0 na kujiweka kwenye mazingira magumu, kwani sasa italazimika kushinda mechi ijayo dhidi ya Kenya kama inataka kuweka hai matumaini ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.Stars inatarajia kucheza na Kenya Alhamisi kwenye Uwanja wa June 30, jijini hapa.
michezo
2
Maalim alisema hayo katika kikao cha pamoja kilichowakutanisha watendaji wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko pamoja na ZSTC Ikulu mjini hapa.Alisema wakulima kwa sasa hawana sababu ya kuuza karafuu zao kupitia njia ya magendo ambayo ni ya kubahatisha zaidi kama mtu atakamatwa na karafuu hizo.“Nawapongeza sana wakulima wa karafuu kwa kujitokeza na kuitikia wito wa Serikali kuuza karafuu zao kupitia ZSTC...Serikali inawahakikishia wakulima hao kuwa hawatokopwa karafuu yao,” alisema.Naibu Mkurugenzi wa shirika hilo, Suleiman Jongo alisema kazi za kununua karafuu kutoka kwa wakulima zaidi katika kisiwa cha Pemba kinachozalisha zaidi ya asilimia 90 zinaendelea vizuri.Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Taifa la Biashara, tayari limenunua jumla ya tani za karafuu 1,250 ambapo lengo kununua jumla ya tani 4,500 za karafuu katika msimu huu.Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo katika hatua za mwisho za kuifanya karafuu ya Zanzibar kutambuliwa kimataifa kwa kuwa na nembo ya utambulisho wake katika soko la dunia kupitia Shirika la Kimataifa la Ubunifu (WIPO).Hatua hiyo itawafanya wakulima wa karafuu kupiga hatua kubwa ya maendeleo pamoja na mikakati ya kuundwa kwa mfuko wa karafuu wenye lengo la kutoa mikopo kwa jamii ya wakulima wa zao hilo.
Biashara
1
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Gaston Kikuwi alisema jana kuwa viwango vilivyowekwa na Serikali kwa sasa, siyo rafiki kwa wafanya biashara wadogo, kwani ni vikubwa mno.Alisema wafanyabiashara wameonesha katika utafiti waliofanya, kumudu viwango visivyozidi Sh 20,000 kwa mijini na Sh 10,000 vijijini.Alitaka viwango hivyo vilipwe mara moja tu; na siyo kila mwaka, ili kuwavuta wananchi wengi kuingia katika biashara iliyo rasmi.“Baada ya Serikali kurudisha ada za leseni za biashara, tumefanya utafiti na kugundua kuwa viwango hivyo vya Sh 50,000 kwa miji na halmashauri, Sh 30,000 wilayani na Sh 10,000 kwa wafanyabiashara wa vijijini, bila kujali kiasi cha mtaji alichonacho mtu, vitawaondoa wengi na kuwafanya washindwe kujikimu kimaisha,” alisema Kikuwi.Alifafanua kuwa mwaka 2003, Serikali iliondoa ada za leseni baada ya kuonekana kuwa zilikuwa ni kero kubwa, ambayo ilizuia malengo ya Serikali ya kukuza biashara na hasa biashara ndongo ili kuinua kipato cha mwananchi wa kawaida na kupunguza umasikini.Lakini mwaka 2011, Serikali ilianza tena mchakato wa kurudishwa ada hizo kupitia Sheria ya Fedha Namba 5 ya mwaka 2011.Mwaka huo serikali ilitunga sheria ya usajili wa biashara, iliyoruhusu mabadiliko ya ada hizo na biashara tofauti, kuwekewa ada tofauti, mijini, wilayani na vijijini.Kikuwi alisema cha kushangaza zaidi ni kwamba viwango hivyo, vilikuwa vikubwa zaidi ya vile vilivyokuwa vimerudishwa kupitia Sheria hiyo ya Fedha Namba 5 ya mwaka 2011.Alisema lengo la Vibindo, kufanya utafiti wa athari za ada hizo, lilikuwa kujua viwango ambavyo wafanyabiashara ndogo wangependa vitumike.Aliongeza kuwa utafiti huo ulifanyika katika miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Morogoro, Songea na Masasi na ulihusisha wafanyabiashara ndogo na wakati wapatao 616.“Asilimia 98 ya wafanyabiashara ndogo na wa kati waliohojiwa, walieleza kutofurahishwa na kurudishwa kwa ada hizi na vile vile kupanda kwake, wakitoa sababu kuwa biashara zao nyingi zina mitaji isiyozidi Sh 200,000,“ alisema Kikuwi.Alisema ada hizo za leseni ni sehemu tu ya mlolongo wa ushuru, ambao wafanyabiashara wadogo na wakati, hulazimika kulipa ili kuweza kufanya biashara.Ushuru mwingine ni wa soko, malipo ya kukodi duka/sehemu ya kufanyia biashara, ushuru wa usafi, malipo kwa ajili ya ulinzi, kodi ya mamlaka ya mapato, kodi ya huduma na malipo ya ukusanyaji taka.Kikuwi alisema duniani kote Ripoti ya Maendeleo Duniani ya mwaka 2005, zimeonesha kwamba kuweka mazingira mazuri ya kukuza ajira za uhakika na kuruhusu ukuaji wa biashara ndogo na za kati ni vitu muhimu, iwapo Serikali itadhamiria kuondoa umaskini katika jamii.“Pamoja na kwamba takwimu za mwaka 2012 za Wizara ya Viwanda na Biashara zinaonesha kuwa Tanzania ilikuwa na biashara ndogo na za kati zinazofikia 3,100,000, utafiti wetu umebainisha kuwa endapo Serikali haitafikiria kuondoa au kupunguza viwango hivi vipya vya ada za leseni, biashara ndogo na za kati 300,000 zipo hatarini kufungwa,” alisema.Kufungwa kwa biashara hizi, ambazo ni asilimia 10.3 ya wafanyabiashara waliohojiwa, kutaathiri maisha yao na ya familia na kuongeza kwa kiasi kikubwa tatizo la ukosefu wa ajira nchini.
Biashara
1
Washindi hao, walikabidhiwa pikipiki zao jana katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya ofisi za Vodacom zilizoko Mlimani City, Dar es Salaam.Nyangige aliyekuwa kivutio katika makabidhiano ya zawadi hizo, akizungumza jana alisema; “Mimi ni dada wa kazi za ndani sasa nitaendelea kufanya kazi zangu na kumtafuta kijana ambaye ataiendesha bodaboda hii na kuniletea fedha ili niweze kujiendeleza zaidi na ninaamini baada ya siku sitaweza tena kuendelea kuwa dada wa kazi na nitakuwa mjasiriamali.”Mshindi mwingine, Steven Masawe ambaye ni Mwalimu wa Chuo cha VETA Dar es Salaam, akiwa mwenye furaha baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya pikipiki, alisema; “Nimeshiriki promosheni hii kwa ari sana nikijua ipo siku nitashinda.“Imekuwa kweli pikipiki hii nitaipeleka kijijini kwetu migombani, Kibosho- Moshi, ikawasaidie katika usafiri kwani kutoka kijijini kwetu hadi kufika mjini ni takribani kilomita 45 na usafiri ni wa taabu sana sasa kutokana na kuwa mteja wa Vodacom nimewatatulia tatizo la usafiri.”
Biashara
1
WAZIRI wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amesema kukamilika kwa Mradi wa Ukarabati Mnara wa Kuongozea Ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Pemba, kutaongeza ufanisi wa utoaji wa huduma za kuongozea ndege na usalama wa sekta.Mradi huo umegharimu Sh.milioni 3.1 zilizotolewa na serikali kupitia Mamlaka ya Usalama wa Anga Tanzania (TCAA), ambayo ina jukumu la kisheria la kusimamia sekta ya usafiri wa anga, ikiwa miongoni mwa taasisi zinazotekeleza majukumu ya Muungano. Mbarawa alisema hayo juzi wakati wa hafla ya kukabidhi mradi huo, ikiwa ni maandalizi ya Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar.Profesa Mbarawa alisema hatua hiyo, itasaidia kuongeza imani ya watumiaji wa uwanja huo na anga ya Tanzanaia, hivyo kuvutia wawekezaji wengi. “Wito wangu ni kwa wadau wote wa sekta ya usafiri wa anga kufanya kazi kwa bidii na kwa weledi ili kuhakikisha tunafikia malengo ya serikali ya kuifanya Tanzania nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo 2025, hili linawezekana endapo kila mmoja wetu atafanya wajibu wake,” alisema.Alisisitiza kuwa shughuli hiyo ya kukabidhi mradi huo wa ufungaji vioo mnara wa kuongozea ndege, inachangia ustawi wa sekta ya usafiri wa anga na uchumi wa nchi hasa sekta ya usafirishaji na utalii. Alisema kupitia mradi huo, zimefanyika kazi kubwa ikiwemo kubadilisha vioo vyote vinavyozunguka mnara wa kuongozea ndege pamoja na kurekebisha paa na kuzuia kuvuja. Pia kumewekwa vizuizi vya usalama, mfumo mpya wa viyoyozi, mfumo wa umeme, mfumo wa simu na data, ceiling upya na kupaka rangi.“Hafla hii inafanyika ikiwa ni miezi minne tu tangu kuzinduliwa kwa mradi wa Mfumo wa Kuongoza Ndege Kutua Salama yaani Instrumental Landing System- ILS kwa ajili ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA). Naambiwa mandalizi ya utekelezaji wa mradi huu wenye thamani ya shilingi bilioni 4.6 yanaendelea vizuri na ujenzi utaanza muda wowote kutoka sasa. “TCAA inaendelea na utekelezaji wa mradi mkubwa wa ufungaji mfumo wa rada nne za kuongozea ndege ambao unatekelezwa kwa thamani ya shilingi bilioni 67.3.Tayari rada ya kwanza kati ya nne zinazotarajiwa kufungwa, imefungwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA),tayari rada itakayofungwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza, imewasili nchini na imeshasafirishwa kwenda Mwanza. Rada nyingine zinatarajiwa kufungwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na Songwe,” alisema.Alisema mbali na uimarishaji wa miundombinu ya kutoa huduma za uongozaji ndege unaotekelezwa na TCAA, serikali pia imeendelea kuimarisha Kampuni ya Ndege (ATCL) na wiki chache zilizopita ilipokea ndege mpya kabisa aina ya Airbus A220-300, ambayo inaifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuwa na ndege ya aina hiyo.Awali, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari alisema kwa mara ya kwanza mnara huo umefanyiwa ukarabati mkubwa tangu ulipojengwa mwaka 1974. Alisema kufanyika ukarabati huo mkubwa, kumeboresha mazingira ya kazi, ufanisi wa utendaji na usalama wa sekta ya usafiri wa anga. Aliongeza kuwa ukarabati huo wa mnara, umefanywa na kampuni ya ujenzi ya Future Century. Mkataba wa ukarabati ulitiwa saini na mkandarasi na Mamlaka ya Usafiri wa Anga mwezi Oktoba 2017 kwa gharama ya Sh.milioni 300.Aliongeza kuwa idadi ya ndege zinazohudumiwa na uwanja huo wa Pemba, imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka, hivyo kuhitaji uboreshwaji wa mazingira ya kufanyia kazi na vitendea kazi. “Kwa sasa kiwanja hiki kinarekodi miruko ya ndege 114, 660 kwa mwaka ikiwa ni wastani wa safari 9,555 kwa mwezi,” alisema. Johari alisema inakadiriwa abiria 8,844 hutumia uwanja huo kwa mwaka, ikiwa ni wastani wa abiria 737 kwa mwezi. Uzinduzi huo wa mnara wa kuongozea ndege ni mwendelezo wa utekelezaji wa miradi kadhaa inayotekelezwa na TCAA, kwa lengo la kuboresha miundombinu ya usafiri wa anga hapa nchini.Alisema TCAA imedhamiria kutekeleza azma ya serikali ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati na viwanda, kwa kuboresha miundombinu ya kuongozea ndege, kuweka mazingira yenye ushindani wenye tija kwenye sekta pamoja na kuimarisha wataalam wake wanaosimamia udhibiti wa sekta ya usafiri wa anga, hivyo imeendelea kuimarisha Chuo chake cha Usafiri wa Anga (CATC), kwa kununua mtambo wa kisasa wa kufundishia waongoza ndege.
Kitaifa
0
SERIKALI hupoteza Sh bilioni 31.8 kila mwaka kutokana na uvuvi haramu katika bwawa la Nyumba ya Mungu, linalozungukwa na Halmashauri za Simanjiro mkoa wa Manyara, Moshi na Mwanga mkoani Kilimanjaro.Bwawa hilo lenye ukubwa wa kilometa za mraba 140 lina uwezo wa kuzalisha tani 5,173 za samaki kwa mwaka zenye thamani ya Sh bilioni 36 ikiwa uvuvi endelevu utazingatiwa.Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira alisema jana uzalishaji sasa ni tani za samaki zisizozidi 600 kwa mwaka sawa na asilimia 11 ya uwezo wa bwawa kuzalisha kitoweo hicho.‘’Uzalishaji huu wa tani 600 sawa na asilimia 11, una thamani ya Sh bilioni 4.2, mtaona kiwango hiki ni kidogo na kinatokana na madhara ya uvuvi haramu.... mikoa hii miwili imeendeleza kampeni za kudhibiti uvuvi huo,’’ alisema. Alisema mikoa hiyo imefanya vikao vya ujirani mwema baina ya wilaya zinazozunguka bwawa. Waliazimia kufungwa kwa bwawa kwa miezi sita, azimio ambalo tayari limeshatekelezwa.‘’Kipindi bwawa limefungwa tumefanya doria 85 zilizohusisha maeneo ya majini na nchi kavu kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ambapo kiasi cha Sh milioni 35.5 zimekusanywa kutokana na zoezi la kudhibiti uvuvi huo haramu, ‘’ alisema. Wachuuzi wa samaki katika soko maarufu la Manyema manispaa ya Moshi, Jabir Abubakar na Musa Swalehe waliomba serikali kudhibiti uvuvi huo badala ya kuwapora samaki sokoni.
Kitaifa
0
MAWAZIRI sita wametoa maazimio tisa, yanayolenga kuuokoa Mkoa wa Kigoma dhidi ya uharibifu wa mazingira, ambao tayari athari zake zimeanza kuonekana na kusababisha madhara.Wamesema operesheni hiyo itachukua miezi sita kuanzia sasa, ambayo wanaofanya shughuli za kibinadamu kwenye hifadhi, wanapaswa kuondoka kwa hiari kabla ya kutolewa kwa nguvu na serikali. Maazimio hayo yamefikiwa jana kwenye kikao cha pamoja cha mawaziri hao ambao ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Maliasili na Utalii, Kilimo, Mifugo na Uvuvi pamoja na Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.Mawaziri hao ni Selemani Jafo (Ofisi ya Rais, Tamisemi) aliyekuwa Mwenyekiti wa mawaziri hao waliotembelea Kigoma. Wajumbe ni Dk Hamis Kingwangalla (Maliasili na Utalii), Luhaga Mpina (Mifugo na Uvuvi), Mussa Sima (Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira), Dk Angeline Mwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Maliasili na Utalii, ilibainisha kwamba mapendekezo ya mawaziri hao yametokana na tathmini ya mazingira ya Kigoma iliyobaini kuwapo kwa athari mbalimbali za kimazingira.Ilisema athari hizo ni abula (Naibu Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), na Katibu Mkuu Kilimo, Mathew Mtigumwe aliyemwakilisha Waziri wake, Japhet Hasunga. Kzimesababisha kuvamiwa kwa hifadhi za misitu na mapori ya akiba kwa shughuli za kilimo, ufugaji, ukataji miti kwa ajili ya nishati na ujenzi na makazi, huku baadhi ya vijiji vikisajiliwa ndani ya maeneo hayo.Taarifa hiyo ilibainisha kuwa utekelezaji wa maazimio hayo utachukua miezi sita kuanzia sasa, ambao utahusisha operesheni ya kuondoa uvamizi wa wakulima, wafugaji na wanaofanya shughuli zisizo halali kwenye misitu na mapori yaliyohifadhiwa kisheria zikiwemo hifadhi za misitu ya Serikali Kuu, hifadhi za misitu za halmashauri za wilaya na vijiji.Azimio jingine ni kuwaondoa kwa watu wanaoishi au kuendesha shughuli zozote kwenye mapori na misitu hiyo ikiwa pamoja na kuimarisha utekelezaji wa sheria, zinazohusu wakimbizi ili kuhakikisha hawachangii uharibifu wa mazingira, maliasili na usalama. Pia wahamiaji haramu kutoka nje ya nchi, wanachangia katika uharibifu wa misitu na mapori wataondolewa nchini mara moja.Azimio jingine ni wananchi wote waliovamia eneo lililoko kwenye mpango wa uanzishwaji wa vitalu vya ufugaji na mashamba ya kilimo katika Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza (Mwanduhubanhu), watapangwa na mamlaka husika kwa ufugaji na kilimo chenye tija, baada ya tathimini iliyoelekezwa na Waziri wa Mifugo kukamilika.Aidha, ilisema mawaziri wamedhamiria kuwa serikali itasaidia vijiji katika maeneo yao kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi na katika mipango hiyo watenge maeneo kwa ufugaji na kilimo kulingana na mahitaji yao. Pia wamedhaminia kuhakikisha mamlaka za serikali za mitaa zenye mashamba, ambayo hayajaendelezwa zihakikishe taratibu za ubatilisho wa miliki hizo umefanyika ili ardhi itakayopatikana ipangwe kwa matumizi ya kilimo na ufugaji wenye tija. Uongozi wa Mkoa na Wilaya umetakiwa kuhakikisha kuwa usafirishaji wa mifugo unazingatia Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa Mifugo Namba 12 ya mwaka 2010.Awali, kabla ya kufikia uamuzi huo ilifanyika tathmini ya mazingira na kubaini kuwa baadhi ya athari ilizozibaini ni pamoja na sehemu kubwa ya hifadhi za misitu na mapori ya wanyamapori kupoteza uoto wake wa asili, kuharibika kwa vyanzo vingi vya maji ikiwemo mito mikubwa (mfano Mto Malagarasi) na kupungua kwa bioanuai.Nyingine ni kuongezeka kwa matumizi ya dawa za mifugo katika hifadhi ambazo husababisha kuchafuka kwa vyanzo vya maji na kuua viumbe hai, ongezeko la mmomonyoko wa ardhí na kusababisha mito na mabwawa kujaa udongo.Taarifa hiyo ilisema imeibainika kuwapo kwa tishio la kuzuka kwa magonjwa hatari kutokana na mwingiliano wa mifugo na wanyamapori katika maeneo yaliyohifadhiwa ikiwemo kimeta, midomo na miguu, kichaa cha mbwa, malale na nagana.
Kitaifa
0
“Tap Tap” itawawezesha wateja wa Airtel Money kufanya miamala kwa haraka na urahisi kwa kugusisha kadi zao ambazo zimeunganishwa na akaunti ya Airtel money wakati wowote wanapotaka kulipia huduma mbalimbali.Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Ofisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde alisema:” Leo (jana) kwa mara nyingine tena Airtel tunachua hatua thabiti katika kuboresha maisha ya mamilioni ya wateja wetu kupitia uzinduzi wa huduma hii ya Tap Tap. “Aidha aliongeza kuwa kadi hiyo ni rahisi kutumika kwani ili kufanya malipo mteja atagusisha kadi yake kwenye kifaa cha muuzaji na moja kwa moja kufanya malipo kwa kuweka namba yake ya siri.Aliongeza kwa kusema , huduma ya “Tap Tap” inadhihirisha dhamira yetu ya kuboresha matumizi ya huduma za kifedha kupitia simu za mkononi na kutengeneza njia mpya ya kufanya malipo katika teknolojia ya simu za mkononi na kuwaondolea wateja wetu athari zitakazowapata kwa kutembea na pesa nyingi mfukoni.
Biashara
1
['Inter Milan imefungua mazungumzo na Manchester United kuhusu kiungo wa Chile Alexis Sanchez, mwenye umri wa miaka 30, na wanataka kukamilisha mkataba wa mkopo katika siku tatu zijazo. (Mirror)', 'Barcelona imewasilisha ombi jipya kwa mshambuliaji wa kiungo cha mbele wa Paris St-Germain na wa timu ya taifa ya Brazil Neymar, mwenye umri wa miaka 27, linalojumuisha "fedha zaidi na wachezaji zaidi". (Telefoot )', 'Tottenham inahofia itampoteza mchezaji wa kiungo cha kati wa Denmark Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 27, fkwa kitita kidogo cha £30m kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho Ulaya. (Star)', 'Mchezaji wa kiungo cha kati wa Spurs na timu ya taifa ya Kenya Victor Wanyama amepewa mkataba wa miaka mitano kwa malipo ya £65,000- kwa wiki na Club Bruges wakati anapokaribia kukamilisha uhamisho. (Scottish Sun)', 'Kalbu ya Fiorentina katika ligi ya Serie A inajitayarisha kuwasilisha ombi kwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester United na timu ya taifa ya Brazil Fred, mwenye umri wa miaka 26. (Calciomercato)', 'Norwich itamfukuzia kipa wa Stoke na timu ya taifa ya England Jack Butland, mwenye umri wa miaka 26, ifikapo Januari na iwapo thamani yake itashuka. (Sun)', 'Bordeaux inataka kumchukua mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal na Misri Mohamed Elneny, mwenye umri wa miaka 27, kwenda Ligue 1 kwa mkopo. (Foot Mercato)', 'Leeds inatarajiwa kuanza mara moja mazungumzo na mchezaji wa kiungo cha kati Kalvin Phillips kuhusu mkataba mpya. Mchezaji huyo wa miaka 23 anataka kulipwa £40,000 kwa wiki ili kuendelea kusalia Elland Road. (Football Insider)', 'Aliyekuwa beki kamili wa Chelsea Filipe Luis, mwenye umri wa miaka 34, amekataa ombi la Manchester City, Lyon na Borussia Dortmund msimu huu wa joto kabla ya kujiunga na Flamengo kutoka nchini anakotoka Brazil. (Globo Esporte)', 'Aliyekuwa beki wa kulia wa Leicester Danny Simpson, mwenye umri wa miaka 32, anafanya mazungumzo na klabu ya Ligue 1 - Amiens kuhusu uhamisho. (Sun)', 'Meneja wa Chelsea Frank Lampard amemkaribisha mchezaji wa kiungo cha kati wa Exeter Ben Chrisene kufanya mazoezi na klabu hiyo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 15 kutoka timu ya vijana wa timu ya taifa England alifanikiwa kucheza katika kikosi cha kwanza mwezi huu. (Sun)', 'Watford inafikiria hatma ya mkufunzi wake Javi Gracia baada ya kuanza kampeni yao ya Premia baada ya kupoteza mara tatu na hivyobasi kushindwa mara saba mfululizo kutoka msimu uliopita.. (Mail on Sunday)', 'Real Madrid itawasilisha ombi la kumsaini kipa wa Everton mwenye umri wa miaka 36 Maarten Stekelenburg iwapo mlinda lango wao raia wa Chile Keylor Navas, 32, atahamia PSG. (Football Insider)', 'United itafikiria kumsaini kipa wa Croatia Dominik Livakovic, 24, kwa dau la £20m kutoka Dinamo Zagreb iwapo raia wa Uhispania David de Gea, 28, hatotia saini ya mkataba mpya katika uwanja wa Old Trafford. (Sun on Sunday)', 'Real Sociedad imekubali kumsaini beki wa Arsenal na Uhispania Nacho Monreal, 33. (Marca - in Spanish)', 'Tottenham wana matumaini kwamba beki wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 30 Toby Alderweireld atatia kandarasi mpya . (Sun on Sunday)', 'Fiorentina imejiunga katika harakati za kumsaini mshambuliaji wa Liverpool na Enlgand Bobby Duncan kwa mkataba wa msimu huu . (Mail on Sunday)', 'Paris St-Germain inajaribu kutatua haki za mauzo za Paulo Dybala huku wakitaka kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 raia wa Argentina kutoka Juventus.(Calciomercato)', 'Southampton inamchunguza mshambuliaji wa QPR mwenye umri wa miaka 21 Eberechi Eze kabla ya uhamisho wa mwezi Januari . (Sun on Sunday)', 'Sampdoria ina hamu ya kumsaini kipa wa Aston Villa na Croatia Lovre Kalinic, 29. (Il Secolo XIX - in Italian)', 'Fifa inachunguza iwapo Roboti zinaweza kuchukua mahala pao marefa wa usaidizi ili kutoa maamuzi ya mipira ya kuotea kwa kuwa tayari wanasaidia katika VAR. (Sunday Mirror)']
michezo
2
TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imefanikisha kutopeleka mgonjwa wa moyo kwenda nje ya nchi kwa matibabu kwa mwaka huu.Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya Moyo wa taasisi hiyo, Dk Peter Kisenge alisema hayo ni mafanikio makubwa kwa taasisi hiyo kwani imesaidia kuokoa fedha nyingi za serikali ambazo hutumika kugharamia matibabu kwa wagonjwa ambao hupelekwa nje ya nchi.Alisema mafanikio hayo yametokana na taasisi kuwa na vifaa vya kutosha vinavyohitajika kwa matibabu ya moyo na pia kuwa na wataalamu. Wagonjwa waliokuwa wakipelekwa nje ya nchi kwa matibabu kwa gharama za serikali imekuwa ikipungua mwaka hadi mwaka tangu kuanzishwa kwa JKCI. Kwa mwaka wa fedha 2016/17, wagonjwa wa moyo waliopelekwa nje ya nchi walikuwa ni 17. Mgonjwa mmoja kwenda nje ya nchi kwa matibabu gharama zake ni zaidi ya Sh milioni 30.Dk Kisenge alisema taasisi hiyo kwa sasa imekuwa na jina kubwa kutokana na matibabu ya kibingwa ambayo yanatolewa na pia wamekuwa wakitibu wagonjwa wa ndani ya nchi na pia Afrika Mashariki na Kati. Alisema kutibu wagonjwa kutoka nje ya nchi ina maana wana imani na huduma ambazo zinatolewa na taasisi hiyo. Alisema kwa sasa taasisi inapokea wagonjwa wa nje 300 kwa siku, wagonjwa 10 hadi 15 ni wa rufaa na wagonjwa wawili ni kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati.Aidha, alisema JKCI pia inatoa mafunzo kwa madaktari mbalimbali ambao kwa mwaka madaktari hadi 20 wanapata mafunzo katika taasisi hiyo. Alisema hali hiyo ni tofauti na miaka ya nyuma ambayo madaktari walikuwa wakitumika kutibu wagonjwa mengi kutokana na kuwa na idadi ndogo ya madaktari, lakini kwa sasa hali ni tofauti. Dk Kisenge alisema taasisi hiyo hakuna mgonjwa ambaye anaweza kufika na asipatiwe huduma, wagonjwa wote wanatibiwa bila kujali hali zao kifedha.
Kitaifa
0
Rais John Magufuli ameingilia kati suala la rangi ya njano kwenye bendera na matumizi ya wimbo wa Taifa, mambo ambayo yamekuwa gumzo mitandaoni kwa siku za hivi karibuni.Taarifa rasmi kutoka Ikulu leo mchana, Rais Magufuli ameeleza kuwa amefuta mara moja maelekezo ya barua iliyotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iliyoeleza kuwa rangi ya njano kwenye bendera ilitakiwa kuwa ya dhahabu, kuwakilisha madini ya dhahabu yanayopatikana nchini.“Hata mimi mwenyewe tangu nasoma shule hadi leo nafahamu kuwa Bendera ya Taifa ina rangi ya njano na sio rangi ya dhahabu, na rangi hiyo ya njano inawakilisha madini yote sio dhahabu peke yake,” imeeleza taarifa hiyo. Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa “kwa hiyo nimeamua kuifuta barua hiyo na kama kuna mabadiliko basi ni lazima yafanyike kwa kuzingatia taratibu zote kwa kuwa jambo hili ni la kitaifa, sio la mtu mmoja.”Rais Magufuli ameongeza kuwa Bendera, nembo na wimbo wa Taifa viendelee kutumika kama ilivyokuwa awali na kutoa wito kwa Watanzania kuendelea kuwa wazalendo, kuipenda na kuitangaza nchi huku wakizingatia sheria na maslahi ya taifa.
Kitaifa
0
["Chelsea itazishinda Manchester United na Liverpool katika kinyang'anyiro cha usajili wa winga wa England Jadon Sancho, 19, kwa sababu wako tayari kufikia dau la £120m iliyotolewa na Borussia Dortmund. (Sun on Sunday)", 'Mikel Arteta amekubali kuwa kocha mkuu wa Arsenal baada ya kukosa kupata hakikisho kutoka kwa Manchester City kwamba atakuwa mrithi wa Pep Guardiola katika uwanja wa Etihad. (Sunday Mirror)', 'Tottenham Hotspur wamefanya mazungumzoya kumsaini kiungo wa kati wa Flamengo Gerson na ina mpango wa kumsajili mchezaji huyo wa Brazili wa miaka 22 kabla ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili wa wachezaji mwezi Januari. (90min)', 'Spurs pia wanataka kumleta beki wa Ufaransa Issa Diop, 22, ambaye thamani yake inakadiriwa na West Ham United kuwa £50m .(Sky Sports)', 'Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anasema kuwa klabu hiyo iko tayari kufanya kazi na Mino Raiola kumnasa mshambuliaji wa miaka 19-kutoka Norway Erling Haaland kutoka Red Bull Salzburg.(Sunday Mirror)', 'Raiola pia anamwakilisha kiungo wa kati wa United Paul Pogba, 26, na ameambiwa na Real Madrid kuwa hawataweka dau la kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwezi Januari. (Marca) ', 'Kiungo wa kati wa Tottenham wa miaka 27-raia wa Denmark, Christian Eriksen yuko tayari kukataa uhamisho wa kwenda Manchester United mwezi Januari, licha ya kutokuwa na mkataba wowote msimu ujao. (Daily Star Sunday)', 'Chelsea imefikia makubaliano ya kumsajili imekubali mshambuliaji wa Norway wa chini ya miaka -17 Bryan Fiabema kutoka Tromso. Kiungo huyo wa miaka 16- sasa atajiunga na chuo cha mafunzo ya soka ,Stamford Bridge. (Metro)', 'Arsenal, Borussia Dortmund na Bayern Munich zinapania kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji wa miaka 32-Dries Mertens kutoka Napoli kwa kima cha £8.5m. (Calciomercato)', 'AC Milan na Atletico Madrid zinataka kumsaini kiungo wa kati wa Manchester United na Serbia, Nemanja Matic, 31. (La Gazzetta dello Sport, via Football Italia)', 'Manchester United, Everton na Southampton ni miongoi mwa vilabu vinavyotaka kumsajili beki wa Barcelona wa miaka 19 Mfaransa Jean-Clair Todibo kwa £17m. (Sport)', 'Mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, anataka kuihama Arsenal kwa udi na uvumba. (Mirror)', 'Manchester City na Manchester United wanakumbana na ushindani kutoka Liverpool, Real Madrid na Barcelona kumsajili kiungo Mjerumani Kai Havertz, 20 kutoka Bayern Munich. (Sun)', 'Manchester City walishtushwa na tangazo rasmi la Arsenal kumteua Mikel Arteta kuwa kocha wao mpya kupitia runinga na mitandao ya kijamii. (Mail)', 'Mustakabali wa Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City utategemea vile kikosi chake kitakavyoandikisha matokeo kwenye Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. (The Athletic, via Mirror)', 'Bordeaux wanataka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud mwezi Januari, lakini mshambuliaji huyo wa Ufaransa anatumai kujiunga na Inter Milan. (Goal)', 'Msambuliaji wa zamani wa Manchester United na Sweden Zlatan Ibrahimovic, 38, yupo radhi kuhamia Everton pale Carlo Ancelotti atakapokabidhiwa rasmi klabu hiyo. (Talksport)']
michezo
2
WATOTO mapacha wa Elmenesia na Anisia Benatus, wanaendelea vema na tayari wametengenezewa miguu ya bandia. Pacha hao wapo kwenye matibabu nchini Israel, baada ya kutenganishwa, na kila mmoja amebaki na mguu mmoja.Hatua hiyo imewafanya madaktari wa Hospitali ya Riyadhi (pichani) ambao waliwatenganisha, kuwatengenezea miguu ya bandia. Kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la nchini Saudi Arabia, saudigazette. com, pacha hao wanaendelea vizuri na wapo chini ya uangalizi maalum hadi hapo hali zao zitakapotengemaa sawa sawa. Pacha hao walitenganishwa na jopo la wadaktari 32 kwa muda wa saa 13 Desemba 23 mwaka jana.Upasuaji huo uliofanyika katika Hospitali ya Mfalme Abdullah (King Abdullah Children’s Specialist Hospital), iliyopo mji wa Riyadh (King Abdulaziz Medical City), uliongozwa na Dk Abdullah Al-Rabeeah.Watoto hao, Almenesia na Anesia walizaliwa Januari 29, wilayani Misenyi mkoani Kagera katika Kituo cha Masista cha St Theresa Omukajunguti Kata ya Kyaka na kufikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam mwezi Februari mwaka jana. Watoto hao walikuwa wameungana eneo kubwa la kifuani na tumbo, lakini kila mmoja ana mfumo wake wa hewa.
Kitaifa
0
Mgahawa huo ulizinduliwa juzi na Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dora Msechu.Balozi Msechu alimpongeza Issa Kapande na Nimco Kapande kwa kufanikisha kuwapo kwa mgahawa huo ambao umeweka rekodi kuwa mgahawa mkubwa kuliko yote ya Kiafrika katika nchi za Ulaya.Aidha, alimshukuru Torvald Brahm mwenyeji wa mji huo kwa kumuunga mkono Issa hadi kufanikisha ndoto yake ya kuwa na mgahawa wa kitanzania utakatoa huduma ya chakula cha kitanzania.Katika uzinduzi huo ambapo wenyeji wa manispaa hiyo akiwemo Meya na Mwenyekiti wa Trollhattan, Paul Akerlund na msaidizi wake Peter Eriksson walikuwepo, balozi ambaye ndio kwanza ameanza kazi nchini humo alielezea kufurahishwa na juhudi za Kapande.Alisema Issa ameonesha njia kwamba inawezekana kwa watu waliopo ughaibuni sio tu kuajiriwa, bali kujiajiri katika nyanja mbalimbali.Alisema hilo linawezekana kutokana na kufuatilia kwa karibu taratibu za wenyeji na kisha kutumia mafunzo yaliyopo kukamilisha ndoto.“Ni dhahiri kuwa, Chef Issa kwa kupitia taaluma yake ya upishi amewezeshwa kumiliki mgahawa huu hapa Trollhattan,Sweden. kwa hilo, napenda tuishangilie na kuipigia makofi Sweden na Trollhattan.”Alisema akimpongeza kijana huyo ambaye pia amewekeza mkoani Mtwara anakomiliki hoteli ya Victoria.Katika mahojiano, Mpishi Mkuu Issa Kapande alisema mafanikio yake yanatokana na juhudi kubwa na nia aliyoiweka katika kujifunza na kufundisha wengine katika mitandao ya wapishi wakuu.Kapande ambaye mwaka jana alitwaa tuzo ya dhahabu katika upishi akiwa na timu ya Waswidi alisema kuna umuhimu mkubwa kwa wapishi wa nyumbani kukubali kubadilika na kufanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kujifunza na kufunza ili kuwa na aina nyingine ya mapishi katika kuendeleza sekta.Alisema akiwa amefanyakazi katika nchi 17 na tayari akiwa na vitega uchumi nchini alianzia nia ya kuwekeza Sweden mwaka 2009 wakati alipohamia nchini humo akitokea Uswisi. Alisema alianza kwa kuomba vibali, lakini mchakato kamili ulianza mwaka 2013.“Tulilazimika kufanya utafiti kidogo” alisema na kuongeza kuwa katika utafiti huo walihoji watu 300 na kujua mwelekeo hasa wa shughuli yao unastahili kuwaje.Kapande ambaye ni mhitimu wa chuo kikuu cha Manchester Metropolitan na Chuo kikuu cha kimataifa cha menejimenti ya hoteli cha Uswis amesema amepambana vikali na mkewe hadi kufikia hatua ya kuanzisha mgahawa huo ambao upo katika eneo la ukubwa wa mita za mraba 810.
Biashara
1
BARAZA la Uuguzi na Ukunga Tanzania limemsimamisha Martin Chama kutoa huduma za uuguzi na ukunga kwa muda wa mwaka mmoja kwa tuhuma za kufi ka kazini akiwa amelewa na kutaka kuhatarisha usalama wa wagonjwa na ndugu zao kwa kushindwa kutoa huduma kwa umakini na weledi.Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga, Agnes Mtawa alisema hayo katika taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari jana Dar es Salaam.Mtawa amesema kikao cha baraza hilo cha 196 kilimsimamisha kazi muuguzi huyo Chama kuanzia Februari 7, mwaka huu kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa makosa mawili kati ya manne yaliyowasilishwa katika baraza hilo Septemba, mwaka jana.Amesema awali Ofisi ya Msajili wa Baraza hilo lilipokea tuhuma kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mount Meru Arusha kupitia kwa Muuguzi Mkuu wa Mkoa ambaye pia ni Msimamizi wa Maadili wa Mkoa wa Arusha kwa mujibu wa Sheria N0 1 ya Mwaka 2010.“Kwa mujibu wa taarifa hiyo muuguzi huyo alifika kazini Septemba 26, mwaka jana zamu ya usiku majira ya saa tatu usiku akiwa amelewa na alianza kuwasumbua ndugu waliokuwa wakiwaangalia wagonjwa wao kutaka kuendelea kutoa huduma kwa wagonjwa ili hali akiwa amelewa sana hali ambayo ingehatarisha maisha ya wagonjwa kwa kuwa hakuwa na umakini.“Tuhuma hizi ziliwasilishwa na walalamikaji wawili waliokuwa wakiuguza wagonjwa wao,” amesema.Alisema baada ya hapo Ofisi ya Msajili ilituma ofisa kutoka Baraza la Uuguzi na Ukunga ambaye aliungana na timu ya mkoani Arusha ikiongozwa na Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, timu ambayo ilifanya uchunguzi wa awali na kubaini upungufu uliofanywa na muuguzi huyo kinyume na Maadili ya Uuguzi na Ukunga.“Taarifa hiyo ilipelekwa katika kikao cha dharura cha Bodi cha 195 ambacho pamoja na mambo mengine kilijadili taarifa hii na kuamua shauri hili lisikilizwe katika kikao cha Bodi cha 196 ambayo itahusisha mtuhumiwa na mashahidi ambao ni walalamikaji na watumishi waliokuwepo siku ya tukio,” amesema.Aliongeza kuwa shauri hilo lilisikilizwa Februari 7, mwaka huu ambapo ushahidi uliotolewa umemtia hatiani mlalamikiwa kwa kulewa na kushindwa kutoa huduma kwa wagonjwa kwa weledi na kutaka kuhatarisha maisha ya wagonjwa na ndugu zao.Baraza la Uuguzi na Ukunga ni Mamlaka iliyoanzishwa kisheria na kufanya kazi chini ya Sheria inayoitwa The Nursing and Midwifery Act, of 2010.Baraza lilianzishwa kwa ajili ya kulinda umma kutokana na huduma zinazotolewa na wauguzi na wakunga nchini na linafanya kazi kwa kusimamia ubora katika mafunzo na kuhakikisha huduma zinazotolewa zinazingatia viwango vilivyowekwa.
Kitaifa
0
TAASISI ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imesema lengo la kuanzishwa kwake mwaka 1981 limefanikiwa kwa kiasi kikubwa.Mtendaji Mkuu wa Tasuba, Dk Herbert Makoye amesema jana Jijini Dar es Salaam kuwa TaSUBa tangu ianzishwe imepata mafanikio mengi ikiwemo kutoa wataalamu mbalimbali.Alisema hayo katika mahojiano na kipindi cha 360 kinachorushwa Kituo cha Luninga Clouds. Alisema Tasuba imetoa maofisa utamaduni na sanaa wanaofanya kazi halmashauri za wilaya, manispaa, majiji na sekretarieti za mikoa.Aidha alisema Tasuba imetoa watendaji wakuu wa taasisi za serikali kama Bodi ya Filamu na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na maprofesa wanaofundisha vyuo vikuu ndani na nje na wasanii wa muziki na fani nyingine za sanaa.“Nasema hayo kufafanua ‘clip’ inayozunguka ambayo hata mimi nimeiona inayotokana na shughuli iliyofanyika Tandale ikidai TaSUBa wanalipwa mshahara wa bure,” alisema.“Jambo hilo ni la hatari ndio maana nimechelea kukutajia majina. Hiki chuo kilianzishwa mwaka 1981 kikiwa na malengo yake na sidhani kama kuna chuo kinaanzishwa kwa lengo la kutengeneza celebrities (wasanii nyota).Kwa kufanya hivyo basi tungekuwa tunachukua wanafunzi wawili tu. TaSUBa inatoa nafasi kwa vijana wote kujifunza sanaa na wanapofika kila mtu anachagua anachokitaka wengine kuwa waandishi wa filamu au waimbaji, ’’alisema.Akielezea historia ya chuo, Dk Makoye alisema ilianza mwaka 1962 baada ya uhuru ambapo Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere alianzisha Wizara ya Utamaduni lengo likiwa ni kulinda utamaduni wa Mtanzania ambao ulikuwa umeharibiwa kipindi cha ukoloni.
michezo
2
TANZANIA inahitaji taasisi za moyo kama ya Jakaya Kikwete (JKCI) 10 hivi, ili kukabiliana na tatizo la moyo nchini. Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa JKCI, Naiz Majani alisema hayo jana alipokua akitambulisha mashindano ya marathoni yatakayofanyika kesho katika fukwe za Coco jijini Dar es Salaam.“Tanzania tunahitaji taasisi kama hizi 10 ili kukabiliana na tatizo la moyo kwani kila taasisi moja inatakiwa kutibu watu milioni tano, sisi tuko milioni 50 tunaamini serikali inaendelea kufanya kazi na tunaamini mbele itawezekana,” alisema. Alisema tatizo la moyo kwa watoto hapa nchini bado ni kubwa ambapo kuna watoto zaidi ya 500 wanasubiri kufanyiwa upasuaji wa matatizo mbalimbali ya moyo walioko katika taasisi hiyo ndio maana mashindano hayo yameandaliwa ili kupata fedha za watoto 100 kufanyiwa upasuaji, yatafanyika Aprili 28 mwaka huu.“Kaulimbiu yetu mwaka huu ni kimbia kwa kila pigo la moyo, orodha ya watoto wanaohitaji upasuaji wa moyo inaongezeka kila mara kwa sababu kila watoto 100 hadi 120 wanaozaliwa, mtoto mmoja anazaliwa na tatizo la moyo, tunaendelea kupunguza tatizo kwa kufanya upasuaji,” alisema Dk Naiz.Akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Process Mohammed Janabi alisema lengo la marathoni hiyo ni kukusanya fedha zitakazowawezesha kusaidia watoto 100 kufanyiwa upasuaji ambapo upasuaji kwa mtoto mmoja gharama yake ni Sh milioni mbili. “Na hili tunalofanya ni kwaajili ya kuwasaidia watoto ambao wazazi wao hawana uwezo, upasuaji una gharama kubwa, lakini pia tumepata watu na taasisi ambazo zimejitokeza kusaidia watoto kadhaa, kwa watoto hawa 100 zinahitajika Sh milioni 200” alisema Profesa Janabi.Alisema marathoni hiyo ipo ya mita 700 kwaajili ya watoto, kilometa tano, kumi na pia nusu Marathoni yaani kilometa 21 na washiriki wote watapata fulana na medali kwa gharama ya Sh 30,000 ya kujiandikishia. Aidha, alisema pia kutakuwa na zawadi kwa mshindi wa kwanza ambapo atapata zawadi ya Sh milioni mbili, mshindi wa pili Sh milioni 1.5 na wa tatu Sh milioni moja.“Lakini nitoe tu wito kwa washindi wetu nawashauri fedha zao hizo za ushindi kuwachangia watoto hao katika matibabu yao, tunatarajia kuwa na watu elfu tatu na mpaka sasa watu zaidi ya elfu mbili wameshajisajili,” alisema. Mkurugenzi wa Idara ya Ukusanyaji Damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Judith Goshaji aliwaasa pia watu kujitokeza kuchangia damu kwaajili ya watoto hao ambao watafanyiwa upasuaji, uchangiaji wa damu utafanyika katika viwanja hivyo vya Coco siku hiyo.
Kitaifa
0
Salum aliyasema hayo jana jijini hapa wakati akizungumza kwenye mkutano Taasisi ya Kodi Barani Afrika (ATI) ulioshirikisha wadau wa kodi kutoka nchi 19 barani Afrika pamoja na wawekezaji kutoka nchi za nje wanaokutana kwa siku tatu kwa ajili ya kujadili masuala ya ukusanyaji wa kodi na kuongeza mapato.Alisema Tanzania ni kati ya nchi inayojitahidi kukusanya mapato yake ya ndani, lakini licha ya kukusanya mapato ya ndani bado ukusanyaji wa mapato katika sekta ya madini na gesi yanahitaji uzoefu zaidi kwa nchi mbalimbali utakaosaidia TRA kukusanya mapato kwenye sekta hizo.Alitoa rai kuwa wanasiasa nao wana mchango mkubwa katika sekta mbalimbali hivyo ni vyema nao pia wakashirikishwa kwenye majadiliano ili tija iongezeke kwenye ukusanyaji wa kodi za ndani.Naye Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade alisema lengo la mkutano huo ni kupata uzoefu wa kukusanya mapato katika sekta ya madini na gesi ndio maana wamealika wadau kutoka nchi 19 za Bara la Afrika pamoja na wawekezaji kwa ajili ya kubadilishana uzoefu juu ya kukusanya kodi zaidi na kuongeza mapato ya ndani.
Biashara
1
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kwa kushirikiana na serikali inaendelea kujadiliana na wawekezaji wa bandari mpya ya Mbegani- Bagamoyo ili kuangalia namna bora zaidi ya kuinufaisha serikali kimapato.Ujenzi wa bandari hiyo utakapokamilika itaongeza uwezo wa kuhudumia shehena ziingiazo nchini na ziendazo nchi jirani za Burundi, Kongo, Malawi, Rwanda, Uganda na Zambia.Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Deusdedit Kakoko amesema mradi huo utatekelezwa kwa awamu, ya awamu ya kwanza itatekelezwa ndani ya eneo lenye ukubwa wa hekta 100 na matarajio ni kuendelea kuitumia hadi mwaka 2030.“Mwaka 2009 TPA ilimwajiri Mtaalam Mwelekezi (M/s Hamburg Port Consulting GmbH) ambaye alifanya Upembuzi yakinifu ambao pamoja na mambo mengine alionyesha kwamba mradi wa ujenzi wa bandari mpya ya Mbegani-Bagamoyo ni wenye manufaa kiufundi, kifedha, kiuchumi na kijamii,” amesema Kakoko.Amesema jumla ya gharama za ujenzi wa bandari inakadiriwa kufikia dola za Marekani bilioni 1.2 ambapo kutokana na ukubwa wa gharama za mradi, serikali imeamua kuutekeleza kwa kushirikisha sekta binafsi.“Serikali ya China imeonesha nia ya kushiriki katika kuendeleza mradi huu na kuiteua kampuni ya China Merchants Holdings International Limited (CMHI) kushiriki katika majadiliano husika,” alisema.“Wakati majadiliano yanaendelea CMHI alipendekeza kumjumuisha Serikali ya Oman kupitia Tasisi yake ya State General Reserve Fund (SGRF) kuingia katika ubia huu. Vipengele vya mikataba ya mradi baina ya serikali na wawekezaji vilishasainiwa Oktoba, 2015 na majidiliano yanaendelea.”amesema.Aidha, amesema utekelezaji wa awamu nyingine zitaanza mwaka 2031 na kuendelea na kwamba bandari hiyo itakuwa na gati tatu za kuhudumia shehena ya makasha wastani wa TEUs 1,000,000, shehena mchanganyiko tani 600,000 na magari 150,000."Ili kuweza kuhudumia meli kubwa na za kisasa, bandari itakuwa na lango la kuingiza meli lenye urefu wa mita 4,000, upana mita 230 na kina cha mita 15.5,” alisema.Aidha, alisema eneo lililotengwa kwa ajili ya shughuli za kibandari lenye ukubwa hekta 887 lilifanyiwa uthamini na fidia ya Sh bilioni 57.067 ambapo ulipaji wa fidia kwa vijiji husika ulianza Agosti 31, 2015.“Hadi Machi 21, 2016 jumla ya wananchi 2,185 sawa na asilimia 98.82 ya wadai wote walikuwa wamelipwa jumla Sh bilioni 45.27 sawa na asilimia 79.32 ya malipo yote. Walipwaji 26 bado hawajalipwa na zoezi la kurekebisha kasoro zilizojitokeza linaendelea chini ya usimamizi wa mamlaka za serikali,” amesema.
Biashara
1
.Huu ndio ulikua muonekano wa Mwanamuziki Faustina Charles Mfinanga aka Nandy aka The African Princess, katika harusi ya dada yake Celine Mfinanga iliyofanyia mwishoni mwa Juma lililopita, huku Mshereheshaji akiwa MC Pilipili, na Billnass naye akihudhuria.
Burudani
4
RAIS John Magufuli amewataka Watanzania kuufanya Mwaka Mpya wa 2019 kuwa mwaka wa kazi kwa kujishughulisha na shughuli mbalimbali kama vile kilimo, biashara, uvuvi na nyinginezo ili kujiletea maendeleo.Alitoa mwito huo kwenye mkesha wa Kitaifa wa kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2019 uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam. Rais Magufuli ambaye aliwakilishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alisema Tanzania imebarikiwa kuwa nchi yenye amani, upendo na utulivu katika awamu zote, hivyo wananchi hawana budi kuitumia fursa hiyo kwa kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo.Alisema kutokana na kuimarika kwa hali ya amani, utulivu na upendo nchini, serikali yake imeamua kupambana na kuondoa kero mbali mbali kama vile rushwa, dawa za kulevya na nyinginezo ili kuinua hali za maisha ya wananchi wanyonge. Alisema mkesha huo wa kitaifa ni fursa muhimu kwa Watanzania kujitathimini kila mwaka kuona malengo waliyojiwekea kama taifa au mtu mmoja mmoja yamefanikiwa na kwa kiwango gani.Aidha, alisema katika miaka mitatu ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano kumekuwa na mkakati wa kujenga na kuimarisha uchumi wa Tanzania kwa kujenga miundombinu mbalimbali ya kiuchumi. Aliitaja baadhi ya miundombinu hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, ujenzi wa bwawa kubwa la kuzalisha umeme wa Mto wa Rufiji utakaozalisha zaidi ya megawati 2,000 pamoja na ujenzi wa barabara maeneo mbali mbali nchini. Kwa mujibu wake, ujenzi wa miundombinu hiyo inatokana na dhamira ya serikali kutimiza ndoto ya kuwa na Tanzania ya viwanda pamoja na kufikia uchumi wa kati na kuwapunguzia gharama za maisha wananchi.“Hivi sasa huduma za jamii kama vile afya na elimu zinazidi kuimarishwa; serikali inajenga hospitali za wilaya kwenye wilaya zote ambazo hazikuwa na hospitali hizo, inaimarisha upatikanaji wa dawa hospitalini, kutoa elimu bure pamoja na kuimarisha huduma mbalimbali za jamii,” alieleza. Mbali na ujumbe huo wa Rais wa Mwaka Mpya, baadhi ya viongozi wa dini pia walisisitiza umuhimu wa Watanzania kuendelea kutunza amani na utulivu uliopo nchini. Msaidizi wa Askofu wa Kanisa Kuu la KKKT-DMP Azania Front jijini Dar es Salaam, Chediel Lwiza alisema Taifa halina budi kumshukuru Mungu kwa kuendelea kuwapatia Watanzania tunu ya amani, lakini pia kuwaweka pamoja kwa utulivu kama taifa, familia, vikundi na mtu mmoja mmoja.“Tuendelee kuiombea nchi katika Mwaka Mpya wa 2019 ili iendelee kuwa na amani, utulivu na mshikamano; tuwajibike katika jamii, serikalini, nyumba za ibada pasipo kushurutishwa katika kutimiza kazi tunazopaswa kuzifanya,” alieleza Lwiza. Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum alisema katika mwaka mpya wa 2019, Watanzania hawana budi kujipanga kwa kufanya kazi kwa bidii, weledi na nidhamu kwa ajili ya kuliletea taifa maendeleo pamoja na kuendelea kutunza umoja wa kitaifa.Alisema Watanzania wanapaswa kubadilisha mtizamo wa kutoka kuwa miongoni mwa mataifa ombaomba na badala yake waifanye Tanzania kuwa taifa linaloweza kujiletea maendeleo ili kutunza heshima na hadhi yake. Kuhusu amani na utulivu, aliyataka madhehebu ya dini na wanasiasa kuendelea kudumisha amani na utulivu pamoja na kuvumiliana katika shughuli zao za kila siku ili taifa liendelee kuwa na utulivu.Kwa upande wake, Padri Msaidizi wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano jijini Dar es Salaam, Meshack Malilo, alisema kila Mtanzania ana wajibu wa kutunza amani na hilo siyo jukumu la viongozi peke yao. Alisema wajibu wa serikali ni kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani, lakini jukumu la kuitunza amani hiyo ni la wananchi wote. Katika mkesha huo, Lukuvi na viongozi wa dini waliongoza wananchi kumuombea mama mzazi wa Rais Magufuli, Suzana Magufuli ambaye anapatiwa matibabu kwa miezi mitatu sasa kutokana na maradhi ya kiharusi.
Kitaifa
0
VIONGOZI wa kitaifa wametakiwa kufanya kazi kwa pamoja na kuvumiliana kwani huo ndio msingi wa kufikia maendeleo ya kweli. Wito huo ulitolewa jana na Askofu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Central Tanganyika (Dodoma), Dk Dickson Chilongani, katika mahubiri ya Krismasi yaliyofanyika kanisa kuu la Roho Mtakatifu.Askofu Dk Chilongani alisema kuvumiliana kwa wanasiasa na kupendana kutaepusha mambo mengi, lakini kutalisaidia taifa kusonga mbele na watu wake lakini kinyume chake itakuwa ni bure. Alisema upendo ndiyo nguzo kuu na msingi wa maendeleo, lakini kuvumiliana kwa viongozi wa serikali na vyama vya siasa kutafanya wananchi wao kuwa na furaha na amani kama ilivyo kwa Wakristo walio na amani kuhusu kuzaliwa kwa mkombozi wao Yesu Kristo.“Lazima kuwepo na upendo na furaha kwa viongozi wa vyama vya siasa, waache misuguano, wavumiliane na hata wabunge wetu lazima wapendane siyo kukwaruzana pasipokuwa na msingi, lakini viongozi wafanye kazi pamoja huku wakisahau tofauti zao katika suala la maendeleo ya nchi.” “Kwa sasa taifa tuna furaha kupata ndege, kujenga miundombinu mizuri, kujenga standard gauge na kuhamia Dodoma, lakini sisi wapenzi wa Simba furaha imepitiliza kwa kuifunga Nkana na kuingia katika makundi huku tukisubiri Sh bilioni 1.3, naomba viongozi wetu wawe na furaha kama hiyo na wapendane na kuheshimiana,” alisema.Askofu wa Dayosisi ya Dodoma, Amon Kinyunyu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) amewataka watanzania kutoichezea amani iliyopo ndani ya nchi badala yake wailinde. Alisema kuwa bila amani wananchi hawawezi kupata huduma mbalimbali za kijamii na kiroho, hivyo ni lazima wailinde amani kwa kila njia. Kinyunyu alitoa wito huo alipokuwa akihubiri kwenye ibada ya sikukuu ya Krismasi ikiwa ni kuadhimisha kuzaliwa kwa Bwana Yesu Kristo iliyofanyika KKKT Usharika wa Dodoma Mjini. “ Ni wajibu wetu sote kushirikiana katika kuilinda amani ili isitoweke, ambayo kwa baadhi ya nchi wanaitafuta kwani wanaendelea kumwaga damu na kuwapoteza watu ambao hawana makosa,”alisema.Pia amewataka Watanzania kudumisha amani na upendo na kuwaheshimu viongozi walioko madarakani kwa kuwa mamlaka zote zinatoka kwa Mungu. Askofu Kinyunyu alisema kumsikiliza kiongozi mkuu ni sawa na kumsikiliza Mungu kwa kuwa maandiko yanasema hakuna mamlaka iliyopo ambayo haikutoka kwa Mungu. “Ni lazima kuwatii wenye mamlaka, tumtii Rais, Makamu, Waziri Mkuu na viongozi wengine kwani hakuna aliyejiweka pale kama siyo kusudi la Mungu, tukifanya hivyo itakuwa ni chanzo cha amani.”
Kitaifa
0
KOCHA wa Singida United, Ramadhan Swanzurimo amesema wamejipanga kimbinu kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya bingwa mtetezi Simba unaotarajiwa kuchezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.Singida wametangaza kutumia uwanja huo kwa michezo miwili ya ligi hiyo dhidi ya Simba na JKT Tanzania kupisha matengenezo kwenye uwanja wao wa Namfua, Singida. Swanzurimo aliyekinoa kikosi cha Mbeya City msimu uliopita alisema wanajua mchezo huo utakuwa mgumu kwao kwakuwa Simba ni timu iliyojipanga naimefanya uwekezaji mkubwa kuliko timu yeyote kwenye ligi hiyo na hawajapoteza mechi yoyote kwenye ligi na kwamba hicho sio kigezo cha kushindwa kuonesha ushindani kwao na kupata matokeo.Alisema kwa upande wake bado anajivunia kikosi chake kilichosheheni vijana wenye kasi hivyo atatumia uzoefu wa taaluma hiyo kuwapa mbinu mpya itakayowafanya wachezaji wake kubadilisha matokeo muda wowote kwenye mchezo huo. Alisema uwezo wa kupata matokeo wanao kwakuwa kwenye mchezo uliopita wa ugenini dhidi ya Coastal Union uliopigwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga walipata pointi moja na kwamba hiyo kwao ni zawadi na morali tosha kujipanga kwa kuwakabili Simba.“Tumejipanga kwa mbinu kupata matokeo chanya kwenye mchezo ujao dhidi ya bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Simba ingawa bado tunawaheshimu ni miongoni mwa timu zilizofanya uwekezaji mkubwa kwenye ligi na wanaongoza msimamo lakini hicho sio kigezo cha kusema hatuwezi kuleta ushindani nakupata matokeo kwao,” alisema Swanzurimo raia wa Burundi.Wakati huo huo kocha wa Simba Patrick Aussems amesema baada ya kupata ushindi wa pointi tatu dhidi ya Azam FC kwenye mchezo uliopita na kuendelea kuongoza msimamo wa ligi hali hiyo inazidi kuwapa wachezaji wake nguvu ya kuendelea kupambana kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Singida.Alisema bado anaamini timu yeyote inayoshiriki Ligi Kuu ni timu bora hivyo mchezo huo dhidi ya Singida utakuwa mgumu kwao licha ya wapinzani wao hao kushika mkia kwenye msimamo wa ligi hiyo.Alisema kikosi chake bado kipo fiti baada ya mchezo uliopita na leo wanatarajia kuingia kambini kujiwinda na michezo miwili dhidi ya Singida na Mwadui FC kabla ya kusafiri keshokutwa kwenda Arusha kisha Shinyanga . “Pamoja na kupata ushindi wa pointi tatu kwenye mchezo uliopita bado tunakibarua kigumu mbele ya Singida kwa kuwa ni timu bora pamoja na kuburuza mkia kwenye Ligi Kuu,tunajipanga kupata ushindi,” alisema Aussems.
michezo
2
JAMII imetahadharishwa dhidi ya watu wanaotumia eneo la imani, kwa ajili ya kujinufaisha. Pia, wale wanaojitoa kiimani, wametakiwa kutambua hawafanyi hivyo kwa manufaa binafsi.Hayo yamesemwa na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera, Dk Benson Bagonza. Alisema hayo jana katika mahubiri yake kwenye ibada ya Ijumaa Kuu, iliyofanyika kitaifa katika Kanisa Kuu la Lukajanga lililopo Karagwe. Alisema kanisa linatakiwa kuwa na watu wa kujitoa ili kupunguza mateso ya wengine, ikiwemo vilio vya rushwa, ufisadi magonjwa na hata kukomesha dhambi zingine, ambazo zimekuwa zikiitesa jamii.“Wanaojitoa watambue kuwa hawajinufaishi, hata katika eneo la imani ama ikawa ni mtaji wa kisiasa au kiuchumi,” alisema na kukiri kuwa katika eneo la imani pamevamiwa. Aliwataka waumini kuwa makini.Aidha, alitoa angalizo kwa jamii kutambua kuwa maradhi ya waumini, umaskini wao na matatizo wanayokumbana nayo, sio taji wa wasaka tonge, kwa kuwa hata Bwana Yesu Kristo hakunufaika na chochote alipojitoa na kusulubiwa. Askofu Bagonza alisema wanadamu hawapendi mateso, bali kuwatesa wengine na aliye tayari kuyaendea mateso huonekana mjinga, ilhali mateso ni lazima ili ukombozi kuweza kupatikana.Aliwahimiza waumini kukubali kuteseka, ingawaje watapewa ama kuitwa majina mabaya, kuzushiwa ama kuandikwa katika magazeti, lakini waamini kuwa Mungu hawezi kuwaacha kamwe. Alisema waumini waepuke kutesa wengine kwa kuwa utesaji ni sawa na mvuta bangi, kwani asipofanya hivyo huwashwawashwa ili kutekeleza. Kuhusu maadhimisho ya Ijumaa Kuu, alisema ni eneo ambalo bado limekuwa linaendelea kusumbua mioyo ya watu.Kwamba siku hiyo inasimama katika misingi miwili ya upendo na upatanisho na kuwasihi wakristo kutafakari tendo hilo, ambalo ni msingi wa Imani ya Kikristo. Kuhusu upendo, alisema Mungu aliupenda ulimwengu na kumtoa mwanae wa pekee afe na kuwa sadaka kwa ajili ya wanadamu, kwa maana kuwa Yesu alisimama kwa niaba ya ukombozi wa wanadamu.“Mungu alikuwa na upendo wa ajabu, wengi wetu tumezoea kupokea na sio kutoa lakini tofauti Mungu alitoa ikiwa ni fundisho kwa kila mmoja kwani upendo huo ndio uliomuweka Yesu Msalabani,” alisema Askofu Bagonza. Kuhusu upatanisho, alisema ndani ya yesu Kristo alikuwepo Mungu kwa ajili ya upatanisho, akishuka kutoka mbinguni na kuacha enzi na mamlaka, akawa kama mhalifu na kuteswa kwa ajili ya wanadamu.“Upendo wa nguvu, ukitaka kitu utafanya chochote, tunajifunza nini katika upatanisho huu kwamba ni kupendana kwa kuwa tuu watumwa tuliokombole nakuishi kwa shukrani kwa aliyetukomboa,” alisema. Alisisitiza kuwa ipo haja ya kujitoa kwa ajili ya wengine kwa mali, wakati na nafsi, kwani kutumika kwa uzalendo vinaongeza thamani kwa mwanadamu huku ikionesha utofauti ya watumwa waliokombolewa na walio bado utumwani.Askofu Bagonza alisema katika kizazi cha sasa, waliokombolewa hawafurahi kuona wengine bado wamefungwa. Kwamba ukombozi unatokana na Yesu, ukiwataka waumini wenyewe kupendana kwa dhati ili kuondoka utumwani na kumtii aliyewakomboa na kuweka huru.
Kitaifa
0
KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amefunguka kuwa tayari amepata dawa ya kumaliza tatizo la safu ya ulinzi kuruhusu kufungwa mabao kabla ya mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo keshokutwa.Katika mchezo uliopita wa Ngao ya Jamii uliozikutanisha Simba na Azam FC ambao ulimalizika kwa wekundu hao wa Msimbazi kushinda 4-2, safu yake ya ulinzi ilionekana kufanya makosa ya wazi hali iliyotia hofu kwa baadhi ya mashabiki juu ya mchezo wao dhidi ya UD Songo.Katika mchezo wa kwanza Simba na UD Songo zilimaliza dakika 90 bila kufungana hivyo ili Simba isonge mbele inahitaji kupata ushindi wa aina yoyote.Akizungumzia hali ya maendeleo ya timu yake kocha huyo raia wa Ubelgiji alisema kuwa, baada ya mchezo wa Azam alianza kulifanyia kazi tatizo hilo na tayari ameshalimaliza, Alisema kulikuwa na makosa kadhaa yaliyokuwa yakifanyika sio tu kwa mabeki bali timu nzima hivyo yote ameshayarekebisha.Aliongeza kuwa mchezo huo ni muhimu kwa timu yake hivyo amejaribu kuiandaa timu kuepuka kufanya makosa yatakayoigharimu timu.“Tunajaribu kadiri tuwezavyo kurekebisha makosa yetu tuliyoyabaini katika mechi zilizopita, wengi wanaona tatizo kubwa ni safu yetu ya ulinzi lakini nilichokifanya ni kuiboresha timu yote. “Kwenye mpira timu inapofungwa makosa huwa yanaanzia mbali, ushambuliaji kiungo na kumalizikia kwa mabeki,” alisema Aussems.
michezo
2
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara, Simba leo wanatarajiwa kuwakaribisha Stand United katika mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa taifa, Dar es Salaam.Wachezaji wa Simba wanatarajiwa kuonyesha morali ya hali ya juu kutokana na kupatikana kwa mwekezaji wake Mohamed Dewji ‘Mo’ baada ya kutekwa kwa wiki moja.Mo aliyetekwa na watu wasiojulikana wiki iliyopita, alipatikana jana maeneo ya Ghmkhana akiwa mzima wa afya.Wekundu hao wa Msimbazi hawajapoteza mchezo wowote miaka ya karibuni dhidi ya timu hiyo ya Shinyanga.Mara ya mwisho kukutana Machi 2, mwaka huu katika msimu uliopita wa ligi ambapo walitoka sare ya mabao 3-3.Simba licha ya kuwa na kikosi bora msimu huu, imekuwa ikipata upinzani mkali kwa timu inazokutana nazo.Mpaka sasa katika michezo saba, imeshinda minne, sare mbili na kupoteza mmoja ikiwa na pointi 14.Ina washambuliaji wenye uchu wa kutaka kufunga wakati wote ingawa wamekuwa wakishindwa kutumia vyema nafasi wanazopata kitendo ambacho Kocha Mkuu Patrick Aussems alisema hutokana na kukosa ufanisi.Aussems alisema amefanyia kazi mapungufu hayo hivyo, sasa anaamini kuanzia mchezo wa leo washambuliaji wake hawatakuwa tena butu. Washambuliaji hatari wa kikosi hicho ni Meddie Kagere, John Bocco na Emanuel Okwi.Mchezo wa mwisho kabla ya kusimama kwa ligi, Simba ilishinda mabao 2-1 dhidi ya African Lyon kwenye uwanja huo.Kwa upande wa Stand United imekuwa miongoni mwa timu zenye upinzani msimu huu, ikiwa imesheheni wachezaji wengi wa Kirundi.Timu hiyo imecheza michezo tisa, imeshinda mitatu, imepata sare mbili na kupoteza minne ikiwa na pointi 11.Imekuwa timu inayoruhusu kufungwa mabao mengi baada ya kufungwa 12 lakini pia hujitahidi kufunga ikiwa imetupia 10. Mchezo mwingine ni Mbao dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa kwenye uwanja wa CCM, Kirumba Mwanza.Bila shaka Mtibwa haitasahau kipigo cha msimu wa 2016/2017 Mbao ilipoitandika mabao 5-0 kwenye uwanja huo. Mara ya mwisho kukutana msimu uliopita Februari walitoka suluhu. Timu zote mbili zinaonekana ziko vizuri na kila moja ina nafasi ya kushinda.Mtibwa imecheza michezo tisa imeshinda mitano, sare mbili na kupoteza miwili ikiwa na pointi 17. Na Mbao imecheza michezo tisa, imeshinda minne, sare mbili na kupotea mitatu ikiwa na pointi 14.Mchezo mwingine ni Lipuli dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja wa Samora Iringa.Wenyeji msimu huu hawajaanza vizuri kwani mpaka sasa katika michezo minane, wameshinda mmoja, wamepata sare sita na kupoteza mmoja ikiwa na pointi tisa.Mchezo huenda ukawa mgumu kutokana na kwamba Kagera haijapoteza mchezo wowote katika michezo minane, ikishinda miwili na kupata sare sita ikiwa na pointi 12.
michezo
2
NEEMA sasa imeifikia Halmashauri ya Wilaya ya Ileje mkoani Songwe baada ya mgodi wa makaa ya mawe wa Kabulo uliopo wilayani hapa kuanza kufanya kazi.Kampuni ya CMG Limited ndiyo iliyoingia mkataba wa miezi sita wa kuchimba makaa ya mawe kwenye mgodi huo wa wazi ulio chini ya Shirika la Taifa la Madini (Stamico).Waziri wa Madini, Angella Kairuki alitembelea mgodi huo na kushuhudia shughuli za uondoaji wa tabaka la juu zikifanywa na Kampuni ya CMG ikiwa ni kazi iliyofanyika wiki moja tangu kampuni ianze kazi.Kairuki alisema mgodi huo unakadiriwa kuwa na mashapo zaidi ya tani milioni 300 alizosema si kidogo na kwa mkataba iliosaini, kampuni hiyo inatakiwa kuzalisha tani 12,800 za makaa ya mawe kwa mwezi.Alisema kutokana na wingi wa mashapo yaliyopo, serikali inaendelea na jitihada za kutafuta wakandarasi wengine zaidi ili waweze kuisaidia Stamico katika masuala ya kimtaji na pia weledi katika uchimbaji.“Ni kweli mgodi huu ulisimama kwa muda mrefu na ilikuwa kilio cha Watanzania wengi. Mpaka hivi sasa alichofanya mkandarasi kwa wiki moja ni kuondoa huu udongo wa juu. Katika kutoa udongo huo wamepata tani 600 za makaa ya mawe yanayofaa kwa matumizi ya viwandani na kwingine,” alisema.Alisema kuna makaa ya mawe kama tofali au jiwe na pia ya chengachenga na serikali kwa kushirikiana na Stamico imelenga kwenda mbali zaidi kwamba badala ya kuishia kuzalisha makaa ya mawe na kusambaza katika viwanda vya simenti na vinginevyo, watengeneze makaa yatakayotumika majumbani.Waziri Kairuki alisema kila mmoja atakayenunua makaa atasaidia serikali kupata gawio na kwamba kupitia mapato hayo, halmashauri itapata ushuru wa huduma na pia Mamlaka ya Mapato nchini(TRA).Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico, Kanali Sylvester Ghuliku alisema uzalishaji unaofanyika katika mgodi wa Kabulo una manufaa makubwa kwa wananchi wa jirani pamoja na halmashauri hiyo.Alisema wananchi wanaozunguka eneo hilo watanufaika na ajira ndogondogo na kufanya kazi za huduma za vyakula na ujenzi na pia ajira za kudumu ambapo wakazi watafundishwa kuachana na uharibifu wa mazingira na kuanza kuzalisha matofali ya makaa ya mawe ili kupata nishati ya kutumia majumbani.Ghuliku alisema uzalishaji utaongezeka kutoka tani 700 za sasa hadi tani 1,400 za makaa ya mawe kwa siku baada ya kuongeza wakandarasi kwa kuwa eneo lililopo ni kubwa na uzalishaji wake ni mkubwa.Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Ubatizo Songa alimpongeza Rais John Magufuli kwa kufufua mgodi huo na Kiwira.Alisema kwa tani 700 zitakazozalishwa kwa siku, ushuru wa halmashauri kwa tani moja ni Sh 1,000 hivyo 700 kwa siku watapata Sh 700,000 sawa na kodi ya Sh milioni 18 kwa mwezi.
Biashara
1
['Mshambuliaji wa Manchester City na England Raheem Sterling, 24, hatotia saini kandarasi ya £450,000 kwa wiki hadi pale atakapothibitisha kuwa mkufunzi Pep Guardiola atasalia katika klabu hiyo kwa kipindi cha muda mrefu. (Sun on Sunday)', 'Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anaamini hatowasajili wachezaji anaowalenga katika dierisha la uhamisho la mwezi Januari na sasa atalazimika kutafuta uhamisho wa mkopo badala yake. (Sunday Telegraph)', 'Man United na Paris St-Germain wako tayari kulipa Pauni 60m (£52m) ili kumnunua kiungo wa kati wa Itali Nicolo Zaniolo, 20. (Il Messaggero - in Italian)', 'Mkufunzi wa Ugelgiji na meneja wa zamani wa Everton Roberto Martinez alitaka kuwa mkufunzi wa Tottenham baada ya Mauricio Pochettino kufutwa kazi. (Star on Sunday)', 'Borussia Dortmund inataka kumsaini mshambuliaji wa Tottenham na Jamhuri ya Ireland kaskazini mwenye umri wa miaka 17 Troy Parrott, huku pia klabu ya Ujerumani ya Bayern Munich ikiwa na hamu ya kutaka kumsajili. (Sunday Express)', 'Crystal Palace inakaribia kukamilisha ununuzi wa klabu hiyo wa dau la £215m . (Sun on Sunday)', 'Palace imewasiliana na Liverpool kuhusu makubaliano ya kumnunua mshambuliaji wa England Rhian Brewster mwenye umri wa miaka 19. (Football Insider)', 'Lakini Aston Villa pia wana hamu ya kumsajili Brewster na wanaongoza katika kutafuta saini yake. (Sunday Mirror)', 'AC Milan inataka kumleta Zlatan Ibrahimovic, 38, katika klabu ya San Siro. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Sweden, ambaye kwa sasa hana klabu baada ya kuondoka katika klabu ya LA Galaxy, alishinda taji la Serie la mwaka 2010-11 Serie akiwa na klabu hiyo. (Calciomercato - in Italian)', 'Mkufunzi wa Bournemouth Eddie Howe anasema kwamba anataka winga Ryan Fraser kusalia lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anahusishwa na uhamisho wa kuelekea Arsenal na Liverpool ameweka chaguo lake wazi. Kandarasi yake Fraser na timu yake inakamilika msimu ujao. (Sunday Mirror)', 'Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez, 32, anasema kuwa uhamisho wake katika klabu ya MLS ni uwezekano mzuri huku raia huyo wa Uruguay akihusishwa na klabu ya David Beckam Inter Miami.. (ESPN)', 'Mshambuliaji wa Inter Milan na Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, amesema kwamba alijua kwamba wakati wake katika klabu ya Man United umekamilika wakati mkufunzi Solskjaer alipoanza kumtumia katika wingi . (Football Italia)', 'Manchester United itapokea £850,000 kutoka kwa Juventus msimu ujao kama mojawapo ya makubaliano ambayo yalimfanya mshambuliaji wa zamani wa United Cristiano Ronaldo, 34, kujiunga na klabu hiyo ya Italia kutoka Real Madrid 2018. (Sun on Sunday)', 'Arsenal wanakabiliana na Inter Milan katika kumsaini kinda mshambuliaji wa Flamengo na Brazil mwenye umri wa miaka 17 Reinier Jesus, 17. (Sun on Sunday)', 'Mario Balotelli analengwa na klabu ya Galatasaray. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na klabu yake ya nyumbani ya Brescia msimu uliopita. (Calciomercato - in Italian)', 'Newcastle United itamuuza kiungo wa kati wa South Korea Ki Sung-yueng, 30, in January. (Football Insider)']
michezo
2
JENGO la tatu la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) limekabidhiwa rasmi kwa serikali tayari kwa matumizi baada ya ujenzi wake kukamilika.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Julius Ndyamukama amesema jana mkandarasi alikabidhi kwa Wakala wa Barabara (Tanroads) na kisha kwa TAA.“Leo (jana) mkandarasi anatakiwa amalize akabidhi kwa Tanroads ambaye ndiye mwajiri wake. Tanroads watatukabidhi leo saa 8,” alisema Ndyamukama na kuongeza kuwa hatua hiyo imekamilika siku mbili kabla ya tarehe ya mwisho iliyopangwa ambayo ni Mei 31.Kampuni ya Kimataifa ya BAM kutoka Uholanzi, ndiyo iliyojenga jengo hilo, ambalo limekamilika ndani ya wakati na kukidhi matakwa ya mkataba. Msimamizi wa ujenzi huo ulioanza mwaka 2013, ilikuwa Kampuni ya Arab Consulting Engineers ya Misri. Mkandarasi (BAM) alitakiwa kukabidhi jengo kwa serikali Mei 31.Alipotembelea kiwanja hicho hivi karibuni, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema jengo hilo ambalo litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni sita kwa mwaka, litakabidhiwa Mei 29; hatua ambayo imetekelezwa.Katika ziara hiyo, waziri alisema baada ya Mei 29 (leo), TAA wataanza kufanya majaribio ya matumizi mbalimbali katika jengo hilo.Aidha, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembelea uwanja huo Machi mwaka huu, alitaka TAA kukamilisha taratibu za kuanza kutumika kwa jengo hilo akisisitiza kwamba mkandarasi akishakabidhi kwa serikali, lianze kutumika mara moja.Jengo la tatu la abiria na eneo jipya la kutua, kushushia abiria na kuegesha ndege la JNIA, limewekewa huduma na mifumo ya kisasa, ikiwamo ya kiusalama na kufanya kiwanja kuwa cha aina yake katika Afrika Mashariki.Kitahudumia abiria milioni sita kwa mwaka huku yakiwapo maegesho ya magari 2,075 kwa wakati mmoja. Miongoni mwa huduma zilizowekwa ni mifumo ya mawasiliano ya kisasa huku kukiwa na mifumo ya ukaguzi inayowezesha kuhudumia abiria 2,800 kwa saa.Zipo mashine zinazowezesha wenye pasipoti za kielektroniki kujihudumia haraka bila kusubiri kukaguliwa na watumishi wa uhamiaji.Aidha eneo la uchukuaji mizigo lina mikanda minne yenye urefu wa meta 80 inayowezesha watu wengi kuchukua mizigo kwa wakati mmoja.
Biashara
1