content
stringlengths 1
17.8k
| category
stringclasses 5
values | label
int64 0
4
|
---|---|---|
Mkopo huo unalenga kuwezesha waendesha bodaboda wa Dar es Salaam kukua, kuinuka kimtaji na kumiliki bodaboda zao kwa kuwa wengi si za kwao bali wameajiriwa.Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’i Issa alisema hayo baada ya kutiliana saini ya makubaliano ya kudhamini NSSF kutoa mikopo kwa Dabosa itoe mikopo kwa wanachama wake.“Fedha hizo za kudhamini mikopo hii zitawekwa kwenye akaunti ya mfuko huo,” alisema na kuongeza kuwa watatoa mkopo kwa riba ya asilimia 9.32 na Dabosa itatoza kwa wanachama wake kwa asilimia 12.3.Alifafanua zaidi, Issa alisema mpango huo ni wa kitaifa wenye lengo la kuwezesha wananchi kiuchumi, hivyo watashirikiana na mfuko huo kuwapatia mafunzo ya utawala bora, kuweka akiba na ujasiriamali. “Mafunzo yameshaanza kutolewa Dar es Salaam na yataendelea kufanyika pia katika mikoa mingine nchini,” alisisitiza.Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhani Dau alisema mikopo hiyo ni njia ya kuwezesha vijana kuondokana na tatizo la ajira linalowakabili.“Mfuko umejiweka tayari kutoa mikopo hii, lakini jambo la msingi ni kwa vijana waweze kufanya kazi kwa bidii na kuwa waaminifu katika biashara zao ili waweze kurejesha mikopo,” alisema Dk Dau.Mkurugenzi huyo mkuu aliwaelezea waendesha bodaboda kuwa mfuko unatoa huduma za jamii zikiwemo za mafao ya ajali na mafao ya afya, hivyo wanaweza kujiunga na kunufaika nayo wakati wanaendelea na shughuli zao.Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji, Omari Issa ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais Utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), alisema programu ya kuwezesha bodaboda ni moja ya mambo yaliyomo katika BRN.“Baraza limeondokana na mfumo wa zamani wa kutoa mikopo kwa wananchi moja kwa moja na sasa inadhamini taasisi za kifedha kutoa mikopo kwa wananchi,” alisema.Alisema wanafanya hivyo na Benki ya Posta, TIB, NSSF na watashirikiana na taasisi nyingine ili kuendelea kuwafikia wananchi wengi zaidi. Mwenyekiti wa Dabosa, Said Kagomba alisema chama chao ni cha vijana wa jiji la Dar es Salaam kina wanachama 439. Kinondoni wako wanachama 135, Ilala ni 163 na Temeke ni 141.“Lengo ni kuinua, kustawisha na kuboresha hali ya maisha yetu” na mpaka sasa wamekusanya kiasi cha Sh milioni 24.7,”alisema Kagomba. | Biashara | 1 |
['Manchester United inaweza kushawishika kujaribu kumrejesha tena mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic katika Old Trafford.', ' Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 38- -mchezaji wa kimataifa wa Sweden atakuwa huru kutokana na kwamba mkataba wake na klabu ya ligi ya MLS - LA Galaxy unakaribia kumalizika. ', '(TuttoMercatoWeb, via Mail)', 'Uongozi wa Arsenal uko nyuma kwa "100%" ya meneja Unai Emery na mpango wa kusubiri hadi ufike msimu mwingine kabla ya kufanya maamuzi kuhusu hali ya baadae ya Muhispani huyo. (Athletic - subscription required) ', 'Meneja wa zamani wa Spain Luis Enrique, ambaye amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwa meneja mbadala atakayechukua nafasi ya Emery katika klabu ya Arsenal, hatafikiria kurejea kwenye utawala kwa sasa . (ESPN)', 'Tottenham watamuhamisha winga wa Ajax na Morocco, Hakim Ziyech, mwenye umri wa miaka 26, wakati ambao Mchezaji wa kimataifa wa Denmark Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 27, ataondoka katika klabu hiyo. (90min)', 'Baba yake mchezaji wa kimataifa wa Brazil Neymar anasema kuwa hatafanya mazungumzo na Barcelona juu ya kurejea kwa mwanae katika klabu ya Nou Camp na kwamba mchezaji huyo wa safu ya mashambulizi mwenye umri wa miaka 27 atabaki katika klabu ya Ufaransa ya Paris St-Germain. (ESPN Brazil, via Mail)', "Kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N'Golo Kante, mwenye umri wa miaka 28, amekana taarifa zinanazomuhusisha na kuhamia katika klabu ya Real Madrid na anasema kuwa anaweza kumalizia taaluma yake ya soka katika Stamford Bridge. (Sun)", 'Burnley wamekamilisha mipango ya kumaliza mkopo wa kiungo wa kati wa Chelsea mwenye umri wa miaka 29 Dann Danny Drinkwater katika klabu hiyo ifikapo mwezi Januari. (Sun)', 'Inter Milan wana nia ya kumchukua kiungo wa mashambulizi wa Ubelgiji Dries Mertens, mwenye umri wa miaka 32, ambaye mkataba wake na Napoli unafikia ukingoni msimu ujao. ', 'Klabu San Siro pia iko makini na mchezaji wa Paris St-Germain mwenye umri 28- -Thomas Meunier wa Ubelgiji na mchezaji mwenzake katika safu ya ulinzi Layvin Kurzawa, mwenye umri wa miaka 27, wa Ufaransa. (Calciomercato)', 'Mshambuliaji wa Wolves (Mbwa mwitu) Adama Traore ni mchezaji anayepiganiwa baada ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 kuitwa kuchezea timu zote Spain pamoja na Mali. Traore alizawa Spain na wazazi wenye uraia wa Mali. (Sun) ', 'Meneja wa Leicester City Brendan Rodgers amehoji ikiwa aliungwa mkono ipasavyo na wamiliki wa klabu ya Liverpool alipokuwa akishikilia wadhifa huuo katika Anfield. (Liverpool Echo)', 'Meneja wa Middlesbrough Jonathan Woodgate amesema kuwa ukosoaji unaomlenga kwenye mitandao ya kijamii unaweza kuwa unatoka kwa mashabiki wa Newcastle United na Sunderland. (Evening Gazette)', 'Kiungo wa kati wa Leeds United Muingereza Kalvin Phillips, mwenye umri wa miaka 23, na mshirika wa Ben White, na mchezaji wa safu ya ulinzi ya Elland Road mwenye umri wa miaka 22 kutoka Brighton ambaye anacheza kwa mkopo wanafuatiliwa kwa karibu na Manchester United. (Football Insider) ', ' Klabu ya Arsenal imefanya mazungumzo na meneja wa zamani wa Uhispania na Barcelona, Luis Enrique kuhusu mpango kuchukua nafasi ya Unai Emery. (El Confidencial, kupitia Metro)', 'Klabu ya Tottenham wapo tayari kutoa ofa ya pauni 50m kwa Memphis Depay mshambuliaji wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 25, ambaye alihamia Klabu ya Ufaransa Lyon kutoka Manchester United mnamo Januari 2017.(Sunday Mirror)', "Paris St-Germain kwa mara ya kwanza wamefanya majadilano ya kuongeza mkataba na mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20 Kylian Mbappé lakini hakuna ofa yoyote iliyotolewa. (L'Equipe, via Marca)", 'Meneja wa Liverpool Jürgen Klopp hayupo tayari kumuachia Dejan Lovren, mwenye umri wa miaka 30, aondoke klabuni hapo kwenye dirisha dogo la uhamisho Januari.(Football Insider)'] | michezo | 2 |
Mwili wa Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe utazikwa kwenye eneo la makaburi ya viongozi wa taifa hilo, jijini Harare, siku ya Jumapili Septemba 15, 2019. Hii ni baada ya familia ya kiongozi huyo kufikia muafaka na serikali ya nchi hiyo kuhusiana na wapi azikwe Mugabe. Akizungumza baada ya muafaka huo, msemaji wa familia Leo Mugabe akizungumza na kituo cha televisheni cha Zimpapers asubuhi ya leo, Ijumaa, amesema familia na wazee wa kimila wamekubali ombi la serikali kushughulikia mazishi.“Nachukua nafasi hii kukanusha uvumi kuwa wazee wa mila wamelipwa ili kufanya maamuzi hayo, hakuna aliyelipwa kufanya maamuzi haya,” ameeleza. | Kimataifa | 3 |
MFANYABIASHARA raia wa Uganda, Zari Hassan ameibuka upya na kudai kuwa hakumpenda msanii Diamond Platnumz kwa sababu ya pesa, kwa kuwa amewahi kuwa na wanaume wenye pesa kuliko msanii huyo.Wawili hao walikuwa kwenye mahusiano kwa miaka minne na walifanikiwa kupata watoto wawili, lakini mahusiano yao yaliingia shubiri mapema mwaka jana baada ya Diamond kuchepuka na Hamisa na kuzaa naye mtoto.Zari amesema hayo jana wakati akijibu moja ya maoni ya mdau wake katika mtandao wa Instagram, ambapo alihoji kuwa kama Diamond asingekuwa tajiri na maarufu basi Zari asingeweza kuwa naye kwenye mahusiano na Zari alijibu Diamond hana pesa.“Siongei haya ili kuonekana na roho mbaya lakini nimeshawahi kuwa na wanaume wenye pesa nyingi na yeye hayupo kwenye hao watu hivyo sikuwa naye kwaajili ya pesa na umaarufu. | michezo | 2 |
Kamishna Mkuu wa TRA nchini, Charles Kichere amesema katika taarifa yake kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara atakayebainika kusafirisha bidhaa kwa magendo na kukwepa kodi nchini.Amewataka wafanyabiashara hao kuacha mara moja vitendo hivyo vinginevyo mali zao zote zitakazokamatwa na chombo kilichotumika kusafirisha au nyumba iliyohifadhi bidhaa hizo zitataifishwa na serikali kufidia ukwepaji kodi.Kichere alisema kukwepa kodi ni kosa la jinai kwa mujibu wa Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mwaka 2005 na Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya Mwaka 2015.Alisema ukwepaji kodi husababisha mambo mengi ikiwemo kuikosesha serikali mapato.Kichere alisema ukwepaji kodi huhatarisha maisha ya walaji kwa kuingiza bidhaa ambazo hazijathibitishwa viwango vya ubora na usalama wake kupitia mamlaka husika kama Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), lakini pia huhatarisha uchumi na usalama wa nchi kwa sababu ya kuweza kuingiza vitu vya hatari kama silaha.TRA imewataka wananchi kutoa taarifa ya mfanyabiashara au kampuni inayojihusisha na magendo na kukwepa kodi kwa kupiga simu namba +255 22 2137638 au +255 784 210209.Hivi karibuni TRA ilitaifisha tani moja ya sukari na chumvi, majani ya chai mifuko 18, mirungi kilogramu 16, vifaranga vya kuku 5,000 na mayai kasha 416 mpaka wa Namanga, Arusha zikitokea Kenya kwa njia zisizo rasmi. | Biashara | 1 |
MASHINDANO ya Vyama vya Michezo kwa Shule za Msingi na sekondari kwa nchi za Afrika Mashariki (Feasssa) yanaanza leo jijini hapa huku wenyeji Tanzania wakiahidi makubwa.Timu za Tanzania kutoka maeneo mbalimbali tayari zimewasili jijini hapa na kuweka kambi katika shule ya Trust St. Patrick kwa ajili ya kushiriki michezo hiyo.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Katibu Tawala Mkoa wa Arusha ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo Mkoa, Richard Kwitega amesema timu hizo zinatoka katika maeneo mbalimbali ndani ya nchi na kusema zitashiriki zipo katika michezo tofauti.“Ushiriki wetu kama nchi ni kushinda michuano hiyo na tunaamini ni fahari kubwa kupata matokeo mazuri, kwani timu zilizopatikana ni kutoka katika mashindano ya Umitashumta na Umisseta na mwisho tutatoka na vikombe na medali za kutosha kulingana na maandalizi yaliyofanyika,” alisema Kwitega.Alisema hawategemei kuwa wasindikizaji kwani timu zipo imara kabisa na zimejiandaa vilivyo.“Mashindano ya Feasssa tunatarajia kupokea wanamichezo kati ya 3,500 ambao wataambatana na viongozi mbalimbali, wakiwemo walimu, wazazi na waamuzi ambao wanakadiriwa kufika 1,500 kutoka nchi wanachama ambazo ni Kenya, Rwanda, Burundi, Uganda na Zanzibar pamoja na Malawi ambao watashiriki kama waalikwa,” alisema.Alisema wageni wote hadi kufikia leo watakuwa tayari wameshawasili kutoka nchi hizo, ambazo zilithibitisha kushiriki michezo hiyo, ambayo hufanyika kila mwaka na mwaka itafanyikia kwenye viwanja vya Magereza, Sheikh Amri Abeid, ISM, St. Constantine, TGT na ukumbi wa michezo wa Paloti.“Michezo itakayoshindaniwa ni mpira wa miguu, netiboli, magongo, mpira wa mikono, vinyoya, raga, mpira wa meza na mpira wa kengele ambao utawahusu wanamichezo wenye uoni hafifu au wasioona kabisa,” alisema Kwitega.Alitoa mwito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kutembelea viwanja hivyo na kutoa hamasa kwa wanamichezo pia watumie michuano hiyo kuona fursa katika maeneo mbalimbali na alisema yatazinduliwa rasmi Agosti 16 na kiongozi mkubwa wa taifa, ambaye hakumtaja.Wakati huohuo, Chama cha Wamiliki wa Shule zisizo za Serikali Mkoa wa Arusha (TAMONGSCO) kimetoa msaada wa maji katoni 1,785 yatakayotumika katika michezo ya Feasssa inayoanza leo hapa. | michezo | 2 |
MKUU wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo ameitaka ofisi ya takwimu kukokotoa vizuri pato la mkoa kupitia viwanda ili mchango wake uonekane na kuutoa mkoa huo kwenye nafasi tatu za mwisho kitaifa.Aliyasema hayo mjini Kibaha wakati wa kikao cha ushauri cha mkoa RCC na kusema kuwa ofisi hiyo inapaswa kufanya tathmini kwani kuna baadhi ya mambo hayakuwekwa sawa.Ndikilo alisema kuwa wakati takwimu za pato zinafanyika viwanda vya mkoa huo havikujumuishwa na kuufanya mkoa kuendelea kuwa kwenye kiwango cha chini.“Mkoa wa Pwani ni moja ya mikoa inayoongoza kwa kuwa na viwanda vingi nchini ambapo viwanda hivyo vinazalisha bidhaa mbalimbali,” alisema Ndikilo na kuongeza kuwa kuna viwanda vikiwemo vya nondo, marumaru, sabuni na vingine vingi huku wawekezaji wakiendelea kujenga kwa kasi hivyo hivyo kupitia sekta hiyo lazima mkoa uwe kwenye nafasi nzuri ya kuchangia pato la wananchi na taifa kupitia viwanda.“Watu wa takwimu kwa kushirikiana na wenzenu wa kanda na benki kuu hakikisheni mnaweka takwimu kwa kuzingatia vigezo kwani kwa sasa tumepiga hatua hatuwezi kuwa palepale,” alisema Ndikilo.Meneja NBS mkoa wa Pwani, Kalisto Lugome alisema kuwa baadhi ya viwanda vimekuwa havitoi ushirikiano wanapokwenda kuchukua taarifa mbalimbali na kuwa hiyo ni moja ya changamoto wanayoipata katika kufuatilia namna wanavyozalisha ili taarifa hizo ziweze kuingizwa kwenye mchango wa pato la taifa.Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama amesema, baadhi ya viwanda vimekuwa vikifanya shughuli nyakati za usiku na kuongeza kuwa viwanda hivyo vimekuwa vikikwepa baadhi ya taasisi zinazofuatilia uendeshaji pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). | Biashara | 1 |
NAIBU Waziri wa Madini, Doto Biteko amewataka wachimbaji wadogo wa madini kuwa wazalendo na waaminifu kwa nchi kwa kulipa kodi stahiki zinazotokana na biashara ya madini wanayoifanya.Biteko alisema hayo juzi mjini hapa wakati akifungua mafunzo kwa wachimbaji wadogo katika eneo la Katente. Alisema anashangazwa kuona mchango wa wachimbaji wadogo katika pato la taifa ni mdogo ili hali asilimia 96 ya shughuli za uchimbaji zinafanywa na wachimbaji wadogo na asilimia nne tu zimeshikwa na wachimbaji wakubwa na ndio wanachangia Zaidi katika ukuaji wa pato la taifa. Biteko alibainisha kuwa hayo ni matokeo ya ukwepaji wa baadhi ya wachimbaji wadogo katika kulipa kodi stahiki zitokanazo na uchimbaji wa madini.Akifungua mafunzo hayo, Biteko alisema 2016 serikali ilitenga zaidi ya dola za Marekani milioni 3.7 kwa ajili ya utafiti wa kina wa jiosayansi chini ya mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP). Mradi huo umelenga kuboresha maisha ya wachimbaji wadogo na kutatua changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na uzalishaji mdogo na uchimbaji usiozingatia usalama na afya kwa mchimbaji.Biteko alibainisha kuwa kazi ya utafiti katika mji wa Katente umekamilika kama inavyoshuhudiwa kupitia mafunzo yanayotolewa kwa wachimbaji wadogo wa eneo hilo yatakayosaidia kupunguza upotevu wa muda, uharibifu wa mazingira, upotevu wa mitaji pamoja na upotevu wa madini ya dhahabu yanayotokana na uelewa wa namna ya kufanya kazi hiyo.Alisema baada ya matokeo ya utafiti huo uliofanywa kwa ushirika baina ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Shirika la Madini la Taifa (Stamico)walibaini changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo katika kukua kiuchumi. Kutokana na changamoto zilizobainishwa na utafiti huo, Serikali kupitia Wizara ya Madini imeanza kujenga madarasa na kufunga mitambo kwa ajili ya mafunzo zaidi na kubainisha kuwa eneo la Katente ni moja kati ya maeneo ambayo mafunzo hayo yatatolewa. | Kitaifa | 0 |
Ngoma aliwaweka roho juu, mashabiki na wanachama wa Yanga kufuatia habari kuwa, angesaini juzi kuichezea Simba kiasi cha Yanga kudaiwa ‘kumteka’ uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) aliporejea kutoka kwao.Habari zilizopatikana jana kutoka kwa Kaimu Msemaji wa Yanga, Anderson Chicharito zilisema Ngoma amesaini mkataba wa kuichezea Yanga wa miaka miwili lakini hakutaja dau lake.Hata hivyo, Ngoma ambaye ni raia wa Zimbabwe amesaini Yanga huku vyombo vya habari nchini Afrika Kusini vikiwa pia vimeripoti amefaulu majaribio na vipimo vya afya kuichezea Polkwane City inayoshiriki Ligi Kuu ya soka ya nchi hiyo.Chicharito jana alisambaza picha ya Ngoma akionekana na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga, Hussein Nyika akisaini. Katika picha hiyo, Kiongozi Baraka Desdedit anashuhudia.Ngoma aliwaweka Yanga roho juu baada ya mchezaji mwingine wa Yanga, kiungo mshambuliaji Haruna Niyonzima wa Rwanda kudaiwa kusajiliwa Simba kwa dola 60,000 ingawa kakanusha.Wakati Yanga ikimnasa Ngoma, timu ya soka ya Majimaji FC imepanga kusajili wachezaji 11 wapya kuimarisha kikosi chake. Msemaji wa timu hiyo, Zakaria Mtigandi alisema tayari uongozi wao umeanza kufanya mazungumzo na wachezaji wanaotaka kuwasajili na mazungumzo yanaenda vizuri mpaka sasa.Alisema msimu huu wanahitaji wachezaji 25 badala ya 30 wa msimu uliopita watakaoweza kupambana kuipa timu mafanikio. Alisema wameacha wachezaji 16 na kubakiwa na 14 hivyo hao 11 watafanya kuwa na idadi ya wachezaji 25 wanaohitajika.Mtigandi aliongeza timu yao haina mpango wa kwenda nje kusaka wachezaji kwani wanaamini wanaweza kupata wachezaji ndani ya nchi na kuifanya timu kuwa ya ushindani. Alisema ili kunyakua wachezaji hao, wameunda kamati ya usajili inayofanya kazi usiku na mchana kupata wachezaji walio bora.Alisema kamati hiyo inaongozwa na Mwenyekiti Hersi Said akisaidiwa na Katibu Steven Ngonyani, na Kocha Kally Ongala. Imeandikwa na Mohammed Akida na Mohammed Mdose | michezo | 2 |
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalumu ya SMZ, Haji Omar Kheir alisema hayo wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi kwa tiketi ya CUF, Saleh Nassor Juma aliyetaka kujua lini Serikali itajenga soko la kisasa ili kuepuka wafanyabiashara wa mnada wa samaki kufanya shughuli zao katika maeneo ambayo sio rasmi.Alikiri na kusema wapo wafanyabiashara wengi wa samaki wanafanya biashara katika maeneo ya nje, ikiwemo barabarani na sio maeneo rasmi yaliyowekwa.Alisema zipo sababu nyingi zinazosababisha wafanyabiashara wa samaki kufanya kazi zao katika maeneo ambayo sio rasmi, ikiwemo ufinyu wa sehemu zilizotengwa kwa kazi hiyo.“Wafanyabiashara wetu wa samaki wanafanya kazi zao katika maeneo ambayo sio rasmi, ikiwemo barabarani na kusababisha usumbufu mkubwa na kuweka mazingira ya uchafu,” alisema.Aidha alisema baadhi ya wafanyabiashara wanakwepa kufanya kazi zao za kuuza samaki katika maeneo yaliyotengwa kwa kukwepa kutoa kodi iliyowekwa na Manispaa.Alisema kujengwa kwa soko kubwa la kisasa katika eneo la Malindi kwa kiasi kikubwa kutasaidia na kuwafanya wafayabiashara hao kutambuliwa na kulipa kodi sahihi.Kheir alisema kilichojitokeza kwa sasa ni kwamba wafanyabiashara wa samaki hulazimika kupambana na askari wa Manispaa kwa sababu ya kufanya kazi zao kinyume na sheria.Alisema ujenzi wa soko la kisasa la samaki katika eneo la Malindi unatazamiwa kugharimu jumla ya Sh bilioni 14 ambazo zitatolewa na Serikali ya Japan. | Biashara | 1 |
MFUMUKO wa bei nchini umeongezeka kwa pointi moja kutoka 3.0 Februari hadi 3.1 Machi, mwaka huu.Akizungumza na vyombo vya habari, jijini hapa, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraimu Kwesigabo alisema mfumko wa bei umeongezeka kidogo.Amesema kuongezeka kwa mfumuko wa bei nchini kwa mwaka unaoishia mwezi Machi mwaka huu, kumechangiwa hasa na kuongezeka kwa bei za baadhi za bidhaa zisizo za vyakula.“Baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumko wa bei wa mwezi Machi mwaka huu ni pamoja na mavazi na viatu kwa asilimia 3.4,” alisema.Pia zimechangiwa na kodi ya pango kwa asilimia 4.7, mafuta ya taa kwa asilimia 8.0, mkaa kwa asilimia 13.1, kuni kwa asilimia 27.2, huduma za afya kwa asilimia 1.8, dizeli kwa asilimia 8.3, chakula na vinywaji kwenye migahawa kwa asilimia 4.6 na malazi kwenye mahoteli kwa asilimia 5.7.Gwesigabo alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Machi, mwaka huu umepungua hadi asilimia 0.1 kutoka asilimia 0.5 kwa mwaka unaoishia Februari mwaka huu.Alisema mfumuko wa bei wa taifa unapima kiwango cha kasi ha mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.Alisema mfumuko wa bei nchini Kenya umeongezeka kutoka asilimia 4.14 Februari hadi 4.35 Machi mwaka huu.Huku mfumuko wa bei nchini Uganda haujaongezeka umebaki ule ule wa asilimia 3.0 katika mwaka unaoishia Machi kama ilivyokuwa kwa mwaka unaohishia Februari, mwaka huu.“Kiujumla mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki ni wa mwaka unaoishia mwezi Machi, mwaka huu, umepanda kwa Tanzania na Kenya lakini kwa Uganda umebaki ule ule kwa mwaka unaoishia Februari mwaka huu.Akizungumza mfanyabiashara wa mchele katika Soko la Majengo jijini Dodoma, Juma Khalfan alisema biashara ya bidha nyingi za chakula hazikubadilika kushuka katika kipindi cha Januari, Februari hadi Machi zimebaki kuwa za kawaida ambapo unauzwa kati ya Sh 1,500 hadi 2,000. | Biashara | 1 |
['Bruno Fernandes, 25, ameambia Sporting Lisbon anataka kujiunga na Man United na mazungumzo zaidi yamepangwa wiki hii baada ya kugonga mwamba kuhusu thamani ya mchezaji huyo wa Portugal. (Sky Sports)', 'Beki wa Paris St-Germain na Ufaransa Layvin Kurzawa, 27, atajiunga na Arsenal kwa uhamisho wa bila malipo wakati kandarasi yake itakapokamilika mwezi Juni na amekubali mkataba wa miaka mitano na The Gunners.. (France Football - in French)', 'Arsenal itajaribu kumsaini beki wa Bayern Munich na Ujerumani Jerome Boateng, 31, kwa mkopo mwezi Januari kabla ya kuwasilisha ombi la £50m ili kumnunua beki wa kati wa Ufaransa na klabu ya RB Leipzig Dayot Upamecano, 21, mwisho wa msimu. (Star)', 'Inter Milan inataka kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27, kwa wakati mzuri ili aweze kushiriki katika mechi ya ligi ya Serie A dhidi ya klabu ya Cagliari mnamo tarehe 26 mwezi Januari. (Mail)', 'Afisa mkuu wa klabu ya Inter Beppe Marotta anasema kwamba klabu hiyo ina hamu ya kumsaini winga wa Chelsea Victor Moses, 29, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Fenerbahce, pamoja na mshambuliaji wa klabu hiyo Olivier Giroud, 33, mbali na Eriksen. (Sky Sports)', 'Antonio Conte amemshutumu Jose Mourinho kwa kubadilisha maneno yake baada ya mkufunzi huyo wa Spurs kumkosoa mwenzake wa Inter kwa kuzungumzia kuhusu mchezaji wake Eriksen. (Mirror)', 'Inter Milan pia ina hamu ya kumsaini kiungo wa kati wa Croatia Luca Modric , 34, kutoka Real Madrid(Sport - in Spanish)', "Atletico Madrid imeipatia Paris St-Germain Yuro milioni 10 (£8.5m) ili kumnunua mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 32. (L'Equipe - in French)", 'Tottenham huenda ikamnunua mshambuliaji wa Leicester na Algeria Islam Slimani, 31, ambaye kwa sasa anacheza Monaco kwa mkopo. (Telegraph)', 'Leicester na Aston Villa zinamlenga mshambuliaji wa Ufaransa Serhou Guirassy, 23, kutoka klabu ya Ligue 1 Amiens mwezi Januari. (Mail)', 'Maombi ya Manchester City na Barcelona ya kutaka kumsajili beki wa kati wa Inter Milan Alessandro Bastoni, 20, yamekataliwa. (La Gazetta dello Sport - in Italian)', 'Liverpool inafikiria kumsajili kinda wa Portugal na klabu ya Nice mwenye umri wa miaka 17 Pedro Brazao. (RMC Sport, via Mail)', "Klabu ya Lyon ina hamu ya kumsajili beki wa Athletico Bruno Guimaraes, 22, ambaye pia ameripotiwa kunyatiwa na Arsenal. (L'Equipe - in French)", "Real Madrid itatangaza usajili wa dau la 30m euro (£25.6m) la mchezaji wa Flamengo's Reinier Jesus siku ya Jumatatu wakati ambapo kiungo huyo wa kati wa Brazil amefikisha miaka 18. (AS)"] | michezo | 2 |
KIUNGO wa Manchester United, Paul Pogba ana ushawishi unaowaweka watu pamoja klabuni hapo, kwa mujibu wa mchezaji mwenzake Juan Mata.Kumekuwa na tetesi kuhusu Pogba kutaka kuondoka Old Trafford baada ya kusema anatafuta fursa mpya Juni, huku wakala wake akisema mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa anataka kuondoka.Mapema Julai, kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer pia alisema Pogba hana matatizo na kusema hakuna cha kujadili kuhusu mchezaji huyo. Mata anataka hatima ya Pogba, 26 iwe kuisaidia klabu kuanza kubeba mataji makubwa chini ya Solskjaer, baada ya misimu miwili bila kushinda chochote.“Hakuna shaka kama mchezaji mwenzake na rafiki yangu ningependa abaki na we na furaha kwa sababu ni mchezaji mzuri kwetu,” alisema mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 31 ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili Juni. “Tunajua tunahitaji kufanya vizuri zaidi ya msimu uliopita, klabu hii imeshinda mataji mengi kuliko yeyote England.”United haijashinda taji la Ligi Kuu tangu mwaka 2013, mwaka aliostaafu Sir Alex Ferguson na taji lao kubwa la mwisho lilikuwa la ligi ya Europa Mei 2017 chini ya Jose Mourinho, miezi mitatu baada ya kushinda kombe la Carabao. Solskjaer ni kocha wa tano wa Mata Old Trafford mpango wake umeifanya klabu kujipambanua kama ilivyokuwa kwa Ferguson aliyeiongoza klabu hiyo kwa miaka 26 na nusu. David Moyes alikuwa kocha wakati kiungo huyo alipojiunga United kutoka Chelsea kwa ada ya rekodi ya pauni milioni 37.1 Januari 2014 na tangu wakati huo amefanya kazi chini ya Ryan Giggs, Louis van Gaal, Mourinho na Solskjaer. | michezo | 2 |
Alisema hayo juzi Dar es Salaam wakati wa semina ya ubunifu katika sayansi na Teknolojia, iliyohusisha wafanyabiashara kutoka taasisi za umma na binafsi.Alisema kwa njia hiyo bidhaa, huduma, ubunifu, biashara pamoja na ufumbuzi wa mambo mbalimbali utaweza kukidhi mahitaji ya soko la ndani na kuchangia katika maendeleo ya nchi."Nina furaha kuona Finland tunajihusisha kwa kiasi kikubwa katika kuunga mkono maendeleo ya mfumo wa ubunifu Tanzania kupitia ushirikiano wa kimaendeleo uliopo baina yetu," alisema.Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Patrick Makungu alisema lengo la semina hiyo ni kuangalia mchango unaoweza kupatikana katika uhusiano wa kimataifa . | Biashara | 1 |
['Kundi la vijana wa Mexico linafufua mchezo wa jadi wa mpira uliowahi kuchezwa na jamii za Aztecs, Maya and Incas.', "Mchezo wa 'Ulama' ulichezwa huko Mesoamerica zaidi ya karne tano zilizopita kabla ya watawala wa Uhispani kuwasili katika eneo hilo mnamo 1519.", 'Wachezaji wanaovaa mikanda maalum na vitambara vy kujifinika sehemu zao za siri wanasukuma mpira kwa viuno vyao. Mpira wenyewe unaweza kuwa na uzito wa hadi 4kg. ', 'Wakati inaaminika kuwa kuna aina tofauti za mchezo huo, mara nyingi ilidhaniwa ulihusisha timu hasimu zilizokabiliana ana kwa ana, kila upande ukiwa unasalia katika sehemu nusu ya upande wake na kupasisha mpira kutoka timu moja hadi nyingine pasi kuuangusha mpira.', ' Katikaaina nyingine za mchezo huo, ulichezwa katika eneo lililozungukwa kwa kuta za mawe lenye mduara uliomfano wa vikapu kama katika mpira wa vikapu.', 'Wakati mchezo wa Ulama unafufuliwa katika baadhi ya maeneo ya kale Mexico, mji mkuu hauku na sehemu ya kuchezea mchezo huo hadi hivi karibuni wakati kumejengwa eneo la kitamaduni katika sehemu ya kutupa taka katika mtaa wa Azcapotzalco.', 'Emmanuel Kakalotl ni mkufunzi katika uwanja huo mpya. "Mchezo huu ulikuwa umesahaulika," ameliambia shirika la habari la AFP.', '"Ulipinduliwa miaka 500 iliyopita, lakini sasa tunaufufua upya," anafafanua.', ' Wanawakepia wanaingia katika utamaduni huu wa jadi. ', 'Beatriz Campos mwenye umri wa miaka 25 ni mmojawapo. "Sisi ni mashujaa wanawake moyoni, kwasababu sio rahisi. sio kila mu anaweza kucheza mchezo huu. Inataka mazoezi mengi, na mwili huchoka," anasema. ', 'Kabla ya mchezo kuanza hufanya tambiko kwa kuchoma na kufukiza matawi ya mti maalum.', 'Mchezo wa Ulama unaaminika kuwa tambiko za kitamaduni na kidini na wachezaji hii leo mjini Mexico huvaa mavazi maalum kufanya tambiko kabla ya kuingia uwanjani.', 'Huwakilisha mambo toafuati tukufu kama Mictlantecuhtli, Mungu wa wafu. ', 'Mchezo huo umekubalika na wengi mjini Mexico baadhi ambao wanasema badala ya kuuokoa mchezo wa Ulama, mchezo huo umewaokoa wao kwa kufanikiwa kuwapa malengo mapya.', 'Picha zote zina hatimiliki'] | michezo | 2 |
VINARA wa Ligi Kuu Bara, Yanga jana waliingia kwa shangwe mjini hapa baada ya kupata mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki na wanachama wake.Mashabiki hao waliipokea timu hiyo mpakani mwa Kilimanjaro na Arusha kwa maandamano ya magari na waenda kwa miguu ambapo walizunguka karibu jiji zima la Arusha na viunga vyake.Yanga inayoongoza Ligi Kuu ikiwa na pointi 44 katika michezo 16 ipo mjini hapa kwa ajili ya mchezo wa ligi hiyo dhidi ya African Lyon iliyohama Dar es Salaam na sasa itautumia uwanja wa Sheikh Amri Abeid kama uwanja wake wa nyumbani. Makamu Mwenyekiti wa tawi la Yanga Kaloleni Arusha,,Adamu Masota alisema kila mwanayanga wa Arusha na maeneo jirani anatamani kuiona timu yao na kwamba kwa sasa wao ni wamoja.Alisema wao mashabiki na wanachama wa timu hiyo watafanya wanaloweza kuhakikisha timu yao inapata ushindi katika mechi hiyo muhimu inayotarajiwa kuchezwa kesho. Naye Katibu wa Chama cha Soka mkoani Arusha (ARFA), Zakharia Mjema alisema kuwa maandalizi kwa ajili ya mchezo huo yamekamilika na kinachosubiriwa ni mpambano huo kuanza na aliyejiandaa ndiye atakayeibuka na ushindi.“Sisi kama ARFA kila kitu tumemaliza, ikiwa ni pamoja na maandalizi ya tiketi na uwanja kilichobaki ni kwa timu kutimiza wajibu wao uwanjani,’’alisema Mjema. Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’azi alisema kuwa jeshi hilo litatimiza wajibu wake kama kawaida hivyo aliwataka wapenzi wanaotaka kuangalia mpira huo kukata tiketi mapema ili kuingia uwanjani kwa uhuru bila vurugu. | michezo | 2 |
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeeleza kuongezeka kwa joto juu ya wastani kufi kia nyuzi joto 34 na litadumu mpaka Januari mwakani kutokana na kuwapo kwa jua la utosi na mvua hafi fu za vuli.Imeeleza kuwa wastani wa joto Novemba na Desemba ni nyuzi joto 31.5 kwa mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba. Meneja wa kituo kikuu cha utabiri, Samweli Mbuya alisema jana kuwa sababu ya kuongezeka kwa joto ni mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa kusini mwa mstari wa Ikweta na kusababisha jua la utosi katika miezi hiyo hivyo kuwapo ongezeko la joto.Sababu nyingine ni mtawanyiko wa mvua za vuli hafifu, hivyo kusababisha jua la utosi ambalo ni kawaida kwa nyakati hizi kukosa mvua za vuli za kupooza. Alisema katika kipindi hiki, kunakuwapo mvua za vuli na za msimu lakini kumekuwa na ongezeko la joto katika maeneo mbalimbali hususani kanda ya pwani ambapo joto limekuwa juu ya wastani.Novemba na Desemba ni nyuzi joto 33, lakini kwa sasa mpaka Desemba juu ya wastani mpaka nyuzi joto 35 Pwani na 34 Dar es Salaam. “Katika baadhi ya maeneo hapa nchini ikiwemo mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Morogoro, Dar es Salaam, Pwani pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, msimu wa mvua za vuli unaendelea kukumbwa na mtawanyiko hafifu wa mvua,” alisema.Alisema zipo sehemu mvua zimenyesha kwa wastani lakini sehemu nyingine chini ya wastani. Alisema kwa muda uliosalia hakutarajiwi mvua nyingi bali wastani na chini ya wastani.“Tunatarajia hali hii itaendelea mpaka katikati ya Desemba, tukitarajia mvua kidogo na kupooza lakini …hali hii itaendelea mpaka Januari na baadaye kurejea tena mwezi Februari,”alisema. Mbuya alisema kwa kawaida Oktoba hadi Machi kila mwaka, jua la utosi huwa katika maeneo ya kizio cha kusini mwa dunia. Aliwataka wananchi kufuatilia taarifa za mwenendo wa joto zinazoendelea kutolewa katika utabiri wa kila siku na TMA na kuchukua hatua stahiki kila inapobidi. | Kitaifa | 0 |
WINGA nyota wa timu ya Bandari na timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, Abdallah Hassan amethibitisha kufuatwa na vigogo vya soka vya Tanzania, Simba na Yanga vikitaka kumsajili.Hata hivyo, Hassan hajasema kama yuko tayari kwenda kucheza soka katika timu ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Alisema ni jambo la kawaida kwa klabu kujaribu kumchukua mchezaji katika kila mwisho wa msimu.“Ni kweli Simba wameonesha nia ya kutaka huduma zangu, lakini katika kipindi hiki sipendi kuzungumza chochote kuhusu uamuzi wangu kuhusu suala hilo,” alisema Hassan, ambaye alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka wa klabu wa Januari. Alisema kuwa ana furaha kwa wote waliomuunga mkono hadi kuwa mchezaji bora, na hasa kupata nafasi ya kuichezea timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars.“Napenda kushukuru wachezaji wenzangu kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiutoa kwangu, benchi la ufundi kwa mazoezi mazuri na siwezi kuwasahau viongozi wa klabu kwa kile walichofanya kututia moyo ili tuweze kucheza soka vizuribila matatizo yoyote,” alisema.Mashabiki wa Pwani wa klabu hiyo wamewataka viongozi wa Bandari kuhakikisha wachezaji wote wanabaki kwa ajili ya msimu wa mwaka 2019-2020. Hassan pia alikanusha taarifa kuwa amekuwa akitakiwa na mabingwa wa Kenya Gor Mahia. “Sina hizo taarifa kwa sababu sijawahi kuzungumza na kiongozi yeyote wa Gor na wengine, siwezi kusema kama kuna ukweli wowote katia taarifa hizo, “alisema. | michezo | 2 |
ALIYEKUWA Meneja wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) tawi la Mkwepu, Dar es Salaam Priscus Shirima (37), amefi kishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka ya matatu, ikiwemo utakatishaji fedha Sh milioni 120.Shirima alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mfawidhi, Kelvin Mhina na kusomewa mashitaka ya uhujumu uchumi. Wakili wa Serikali, Wankyo Simon, alidai Juni 20, 2016, katika Benki ya TWB tawi la Mkwepu, wilaya ya Ilala, akiwa kama Meneja wa tawi hilo, aliyeajiriwa na benki hiyo, akiwa na nia ya uovu, alifanya muamala wa uongo kwa kuhamisha Sh milioni 120 kutoka akaunti namba 0310137001 ambayo ni ya Florah Lyatuu kwenda akaunti namba 0380073121, ambayo ni ya kwake.Katika mashitaka ya pili, siku na eneo hilo hilo, mshitakiwa akiwa kama meneja wa tawi hilo, aliyeajiriwa na benki hiyo, aliiba Sh milioni 120. Wankyo alidai katika mashitaka ya tatu ambayo ni utakatishaji fedha, mshitakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo, kati ya Juni 2016, katika benki hiyo.Ilidaiwa kuwa mtuhumiwa alijihusisha na muamala wa Sh milioni 120 kwa kuruhusu na kufanya malipo kutoka akaunti namba 0380073121 inayomilikiwa na taasisi hiyo, akilipa Kampuni ya Sekorizi Ltd kupitia hundi tatu zenye namba 000127, 648806 na 1648791, huku akifahamu kuwa fedha hizo ni zao la uhalifu.Mshitakiwa hakutakiwa kusema chochote kwa sababu mahakama haina mamlaka wa kusikiliza kesi hiyo. Hakimu Mhina aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 27, mwaka huu itakapotajwa na mshitakiwa amerudishwa rumande kutokana mashitaka ya utakatishaji fedha kutokuwa na dhamana | Kitaifa | 0 |
Kocha wa timu hiyo Jurgen Klopp amesema kuwa amefurahishwa sana na matokeo hayo, kwani yanazidi kuiweka Liverpool katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi hiyo.Washambuliaji wao, Mohamed Salah, Roberto Firmino na Sadio Mane wote walizifumania nyavu katika kipindi cha pili katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Anfield. Klopp aliiambia BBC Sport:"Unatarajia mchezo kama huu, na unataka kuuona, lakini ni mara chache sana unaweza kufanya hivyo. "Leo tumepata na huwezi kuamini ni muhimu kwetu kwa sababu ya hali yenyewe kwa sababu hali ya msimamo na kipindi cha msimu wenyewe.”Emre Can aliipatia Liverpoo bao la kuongoza akifungwa kwa mpira wa kona baada ya lile la Salah ya kushindwa kuingia wavuni baada ya kugonga mwamba.Salah aliifanya Liverpool kuwa mbele kwa mabao 2-0 baada ya kupiga shuti hafifu baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Alex Oxlade-Chamberlain, kabla Firmino hajaongeza baada ya kosa la kipa Adrian.Mchezaji aliyeingia akitokea benchi Michail Antonio, aliifungia West Ham na kuirejeshea matumaini, lakini Mane, aliyegonga mwamba muda mfupi kabla, alikamilisha ushindi kwa Liverpool."Kiwango cha wachezaji wa Liverpool walichonacho ndicho kimesababisha matatizo makubwa kwetu," alisema kocha wa Hammers, David Moyes. | michezo | 2 |
UONGOZI wa Azam umemtuma daktari wake Mwanandi Mwankemwa kumfuata mchezaji wake Aggrey Morris mjini hapa.Morris yupo na timu ya taifa, Taifa Stars inayoshiriki michuano ya Afcon lakini ameshindwa kucheza baada ya kuumia goti siku chache kabla ya kuanza kwa michuano hiyo Juni 21.Nafasi yake imechukuliwa na mchezaji mwingine wa Azam, David Mwantika. Hata hivyo, pamoja na kuumia, Morris aliendelea kubaki kambini na wenzie kufuatilia matibabu yake.Akizungumza mjini Cairo, Dk Mwankemwa amesema amekuja kufuatilia matibabu ya mchezaji huyo.“Uongozi umenituma nije kufuatilia matibabu ya Morris, tumeambiwa kuna daktari wazuri hapa (Misri) kwa hiyo tutawasiliana na madaktari wetu kuona kama anaweza kuanza matibabu,” amesema.Meneja wa Stars, Daniel Msangi alisema taarifa ya daktari wa timu ya Taifa inasema Morris anahitaji kufanyiwa upasuaji. | michezo | 2 |
TANZANIA imeendelea kuwa juu katika sekta ya utalii Afrika Mashariki (EAC) kwa kuingiza kipato kikubwa, baada ya kuingiza dola za Marekani bilioni 2.4 mwaka jana.Mapato hayo ya Tanzania ni mbele ya Kenya, iliyoingiza dola za Marekani bilioni 1.55, sawa na takribani shilingi za Kenya bilioni 157.Aidha, watalii walioingia nchini wameongezeka kutoka 1,327,143 mwaka 2017 hadi watalii 1,505,702 mwaka jana. Hali hiyo imetokana na jitihada za serikali kutangaza vitutio vya utalii kupitia vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi.Nchini Kenya mwaka jana sekta hiyo ilikua kwa kuingiza watalii milioni mbili kwa mara ya kwanza na ikaingiza shilingi za Kenya bilioni 157.Waziri wa Utalii wa Kenya, Najib Balala alisema kiasi hicho ni ongezeko la asilimia 31.2 kutoka shilingi za Kenya bilioni 119 mwaka 2017.Takwimu za nchi hiyo zinaonesha kuwa watalii 2,025,206 walitembelea nchi hiyo ukilinganisha na waliotembelea mwaka 2017 ambao ni 1,474,671.Watalii kutoka Marekani wanaendelea kuongoza kwa wingi na walikuwa 225,157 ikiwa ni asilimia 11, wakati watalii kutoka Uingereza ni asilimia tisa, India asilimia sita, Ujerumani na China asilimia nne kila nchi.Kwa upande wake, Uganda ilitembelewa na watalii milioni 1.8 mwaka jana, hilo likiwa ni ongezeko kutoka watalii milioni 1.4 wa mwaka 2017.Sekta hiyo iliingizia Uganda dola bilioni 1.4 na kuchangia asilimia 10 katika Pato la Taifa. Waziri wa Utalii Uganda, Godfrey Kiwanda, alisema wanatarajia kuongeza idadi ya watalii nchini humo kwa kulenga mataifa ya Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Qatar, Oman, Japan na China.Pia alisema wamekuwa na programu za ndani za ‘Twende Uganda’ iliyolenga wananchi wa Afrika Mashariki, ‘Destination Uganda’ kwa wasiozungumza Kiswahili na kampeni ya ‘The Pearl of Africa’ iliyowalenga watalii wa kimataifa. Kiwanda alisema mwaka jana waliwatumia Zarinah Hassan, maarufu kama Zari Hassan na Kanye West kuwa balozi wa utalii.Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangwalla akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2019/2010, alisema Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeanzisha chaneli maalumu kutangaza vivutio vya utalii, ambayo itasaidia kuwavutia wageni wengi kutembelea nchini na kwamba wizara ya maliasili na utalii imeendelea kuchangia katika kugharamia uanzishaji na uendeshaji wa chaneli hiyo.Alisema katika kuendeleza utalii, wizara imeendelea kufanya jitihada za kupanua wigo wa mazao ya utalii, ikiwa ni pamoja na utalii wa fukwe, utalii wa mikutano, utalii wa meli, utalii wa majini, utalii wa michezo, utalii wa utamaduni na kuanzisha shughukli mpya ya utalii katika maeneo ya hifadhi.Waziri Kigwangalla alisema katika kipindi cha Januari hadi Machi 2019, Wakala wa Biashara za Utalii 1,330 walisajiliwa na kupatiwa leseni za kufanya biashara ya utalii kwa kutumia mfumo funganishi wa kielektroniki.Katika hatua nyingine, wizara imefanya uhakiki wa huduma ya malazi 428 katika mkoa wa Dodoma na kati ya huduma za malazi zilizohakikiwa 45 zimekidhi vigezo vya daraja la ubora.Pia, alisema wizara hiyo imekamilisha maandalizi kwa ajili ya kuhakiki na kupanga huduma za malazi katika viwango vya ubora wa nyota moja hadi tano katika mikoa ya Mwanza, Kilimanjaro na Tanga. | Biashara | 1 |
KESHO Jumamosi wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika, Simba itakuwa uwanjani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR C) kuvaana na wenyeji wao AS Vita Club.Mchezo huo wa Kundi D ni wapili kwa kila timu baada ya michezo ya awali, ambapo Simba walipata ushindi wa mabao 3-0 mbele ya JS Saoura na Vita Club kufungwa na Al Ahly 2-0.Kuelekea mchezo huo kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera ambaye ni raia wa DR Congo ameitabiria Simba kutoondoka mikono mitupu katika mchezo huo. Simba ndio wanaongoza Kundi D wakiwa na pointi tatu sawa na Al Ahly, lakini wanaidadi kubwa ya mabao.Zahera alisema kuwa Simba ina wachezaji wazuri wenye uzoefu wa kutosha, hivyo wataweza kuhimili vishindi vya wapinzani wao hao. “Simba bado ina wachezaji wazuri na wenye uwezo mkubwa ambao wanaweza kupambana na wapinzani wao, hivyo mchezo utakuwa hamsini kwa hamsini,” alisema Zahera.Katika mchezo huo Simba inahitaji angalau ipate sare ugenini ili kuweza kujikusanyia pointi zitakazowaweka kwenye nafasi nzuri katika kundi lao.Hatua hii ya makundi inajumuisha jumla ya timu 16 zilizogawanywa kwenye makundi manne, ambapo mbili za juu katika kila kundi zitapata nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali.Mara ya mwisho Simba kufika hatua hii ya makundi ilikuwa mwaka 2003 lakini haikufanikiwa kuvuka hatua inayofuata hivyo mwaka huu imejiandaa kufika mbali zaidi. | Kitaifa | 0 |
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa mwito kwa Watanzania kumuenzi Askofu mstaafu, Gabriel Mmole (80) wa Jimbo Katoliki Mtwara kwa wema, upole na utumishi mwema wakati wote wa maisha yake.Alitoa mwito huo jana wakati wa maziko ya Askofu huyo yaliyofanyika ndani ya Kanisa la Watakatifu Wote la mjini Mtwara na kuhudhuriwa na viongozi, waumini wa Kanisa Katoliki pamoja na wakazi wa mkoa wa Mtwara Katika Ibada ya maziko iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea, Mhashamu Askofu Damian Dallu, Waziri Mkuu alitumia muda huo kuwaasa Watanzania kuishi katika maadili mema na kuheshimiana.Waziri Mkuu amesema enzi za uhai wake Askofu Mmole alitoa kipaumbele katika masuala muhimu ya maendeleo ya jamii ikiwemo elimu ambapo alisaidia sana watawa waliomaliza darasa la saba na kuwasaidia wajiunge na shule za sekondari. “Hata uanzishwaji wa Chuo Kikuu cha STEMMUCO ambacho ni tawi la SAUT hapa Mtwara ni moja ya jitihada zake alizozifanya katika kuhakikisha anawapa elimu bora vijana na jamii.Askofu Mmole alizaliwa Januari Mosi, 1939 katika Parokia ya Nangoo, ambapo alibatizwa na kupata kipaimara Oktoba 5, 1952. Mwaka 1971 alipata daraja ya upadre na kuwa Askofu kuanzia mwaka 1988, alifariki Mei 15, 2019 mkoani Mtwara baada ya kuugua kwa muda mrefu.Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa aliwashukuru viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini mkoani Mtwara kutokana kwa ushirikiano mzuri anaopata unaomwezesha kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Maziko hayo yamehudhuriwa na maelfu ya wananchi, maaskofu wa majimbo mbalimbali nchini, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na mkewe, Mama Anna, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika. | Kitaifa | 0 |
TAASISI ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), inawashikilia watu watatu akiwamo Diwani wa Kata ya Ukonga wilayani Ilala Mkoa wa Dar es Salaam, Jumaa Mwipopo na Ofi sa Mtendaji wa kata hiyo, Rozalia Silumbe kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Sh 400,000 kwa mwananchi aliyetuhumiwa kufanya uharibifu wa mazingira.Aidha, inamshikilia mtu aliyejifanya mtumishi wa taasisi hiyo ambaye aliwahi kufungwa jela miaka sita kwa kuomba rushwa ya Sh milioni 70 na tangu atoke jela ana wiki mbili.Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ilala, Christopher Myava alisema Silumbe na Mwipopo ambaye ni diwani kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), walikamatwa Mei 22, mwaka huu, saa 9 alasiri katika ofisi za Kata ya Ukonga. Myava alisema watuhumiwa hao walishawishi na kuomba rushwa ya Sh 400,000 na kupokea Sh 300,000 kutoka kwa mwananchi huyo.“Watuhumiwa watafikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu tuhuma chini ya kifungu cha 15 (1) (a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007,” alisema Mkuu wa Takukuru Ilala. Myava alisema katika tukio lingine, Takukuru inamshikilia Deogratias Mgasa (43), mkazi wa Temeke kwa tuhuma za kujifanya Ofisa wa Takukuru.Alisema Takukuru ilibaini Mgasa anatumia kitambulisho bandia kinachoonesha yeye ni Ofisa Takukuru mwenye cheo cha Mchunguzi Daraja la Kwanza ambacho alikuwa akikitumia katika kufanya utapeli. Alisema mtuhumiwa huyo alikutwa na kitambulisho hicho chenye jina la Patrick Ushilobo kilichotolewa Januari 2, 2014 na taasisi hiyo kilionesha kama ni Ofisa wao.Myava alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Mei 23, mwaka huu, saa 10 jioni, Kituo cha Mafuta cha Big Born, ambako aliomba rushwa ya Sh milioni 50. Alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa pia na bangi misokoto saba, na uchunguzi unaendelea na atafikishwa mahakamani. Aliongeza kuwa mtuhumiwa huyo alishawahi kufungwa jela miaka sita, baada ya kuomba rushwa pia ya Sh milioni 70 na tangu atoke jela ana wiki mbili. Takukuru imewatahadhalisha wananchi kuacha kurubuniwa na matapeli na badala yake watoe taarifa mapema. | Kitaifa | 0 |
MAOFISA wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wamefanikiwa kumkamata muagizaji wa jumla wa nguo za ndani za mitumba zilizopigwa marufuku kutumika nchini kwa mujibu wa Sheria ya Viwango namba 2 ya mwaka 2009. Kukamatwa kwake ni mafanikio makubwa kwa maofisa wa TBS kwani kupitia msako huo, wengi waliokamatwa ni wachuuzi wadogo kutoka kwenyemaeneo mbalimbali nchini.Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ghala la mfanyabiashara huyo Kiwalani, Ilala, jijini Dar es Salaam, Mkaguzi wa TBS, Juma Nandule, alisema kukamatwa kwake kulitokana na taarifa kutoka wasamaria wema.Alisema Watanzania wengi wameshajua nguo hizo hazitakiwi kwenye soko letu, ndiyo maana baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa nguo hizo za ndani za mitumba walitoa taarifa TBS.Alisema, kwenye ukaguzi wa awali ulioanza Jumanne wiki iliyopita walifanikiwa kukamata mabelo matano kila moja likiwa na uzito wa kilo 100 na bado ukaguzi ulikuwa unaendelea. Alisema ukaguzi wa ghala la mfanyabiashara huyu bado unaendelea ili kuhakikisha nguo ambao hazitakiwi zinazuiwa na kuharibiwa. Alisema nguo hizo zinaondolewa kwenye soko kutokana na mamlaka ya shirika hilo chini ya sheria ya viwango namba 2 ya mwaka 2009.Alifafanua kuwa waagizaji wote wa mitumba walishaambiwa nguo za ndani za mitumba haziruhusiwi kwenye soko la Tanzania sasa. “Lakini bado wafanyabiashara wanakaidi na kuziingiza nchini kupitia njia za panya,” alisema na kusisitiza operesheni ya kuondoa nguo hizo za mitumba kwenye soko ni endelevu na awali walianza na wachuuzi wadogo kupitia misako inayoendelea kwa kushtukiza kwenye masoko.Alisema nguo hizo zina madhara kwa watumiaji hivyo alitoa mwito kwa Watanzania kuzikataa. Alisema nguo hizo zinachangia Watanzania kuendelea kuzitumia kutokana na bei kuwa ya chini.Akieleza sababu za kupigwa marufuku kwa nguo hizo za ndani za mitumba, Nandule alisema zimekuwa zikichangia magonjwa. Alipoulizwa hasara za waigizaji wa nguo za ndani za mitumba zilizopigwa marufuku, alisema ni kutozwa faini, kulipa gharama za ukaguzi wa mizigo, kulipa gharama za kuharibu shehena au kurudisha walikozitoa kwa gharama zao. | Kitaifa | 0 |
WAFANYAKAZI wa serikali watalazimika kuwa na subira mpaka kufi kia ndoto ya misha- hara yao kupanda. Hiyo ni kutokana na serikali kushindwa kuweka katika bajeti yake fedha mahususi kwa ajili ya ongezeko la mishahara.Wabunge walio katika Kamati ya Bajeti waliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita kutokana na kushindwa kwa serikali kutenga fedha kwa ajili ya mapendekezo ya kupandisha mishahara ya watumishi wa serikali.Kamati hiyo ya Bajeti iliyokuwa chini ya Uenyekiti wa Mbunge wa Ntenjeru Kaskazini, Amos Lugoloobi kupitia chama tawala cha NRM, ilikutana katika kikao cha pamoja na kamati nyingine ya Serikali za Mitaa.Mwenyekiti wa Kamati ya Serikali za Mitaa, Godfrey Onzima ambaye pia ni Mbunge wa Aringa Kaskazini alikiambia kikao hicho cha Kamati ya Bajeti kuwa nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa serikali inahitaji Sh bilioni 279 za Uganda ambazo hazionekani katika bajeti ya taifa. “Tunathibitisha kuwa serikali inatilia maanani asilimia 30 ya nyongeza hiyo katika mapendekezo ya miaka mitano ijayo ambayo yanahitaji shilingi bilioni 279 za Uganda kuongezwa katika bajeti ya kawaida,” alisema Onzima.Onzima alisema serikali lazima ijitolee kuhakikisha kuwa inatekeleza malengo yake ya mwanzo ya nyongeza ya mishahara yaliyokubaliwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Mwaka jana serikali ilir- idhia kuwaongeza mishahara watumishi wake katika kada za taaluma, watumishi wa umma wa utamaduni, watumishi wa mahakama, watumishi katika sekta ya afya, wanasayansi na viongozi wa serikali za mitaa. | Kitaifa | 0 |
WATANZANIA wanaotumia dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi (ARVs) wametakiwa kuendelea kutumia pasipo kuacha ili waweze kuishi maisha yenye afya iliyoimarika.Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Anthony Mavunde ameyasema hayo wakati anafungua kongamano la kitaifa la Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani mwaka 2018.Amesema kati ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi(VVU) wenye umri wa miaka 15 hadi 64 ambao walitoa taarifa kuwa wanatumia dawa za kufubaza virusi, asilimia 87.7 ndio wamefubaza virusi ambapo wanawake ni asilimia 89.2 na wanaume ni asilimia 84."Napenda kuhamasisha Watanzania wote wanaotumia dawa za kufubaza VVU waendelee kuzitumia pasipo kuchoka na kwa kufanya hivyo wataweza kuishi maisha yenye afya iliyoimarika na furaha na hivyo kuendelea kulitumia taifa vyema," alisema.Amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni Pima VVU, Jitambue Ishi anbayo inaonesha ushahuidi kutokana na matokeo ya utafiti wa viashiria vya Ukimwi wa mwaka 2016/2017 hapa nchini. Mavunde amesema matokeo yameonesha ni asilimia 52 tu ya wanaoishi na virusi vya ukimwi (WAVIU) nchini wanajua hali zao."Hii ina maana kwenye eneo la kupima kuna vikwazo vingi vinavyowafanya watu hasa wanaume kutojua afya zao, pengine nchi bado hatujapata ufumbuzi bado kwani kutokana na matokeo ya utafiti huo ni asilimia 45 tu ya WAVIU wanaume wanajua hali zao," amesema.Amesema utafiti wa mwaka 2016/2017 umeonesha kati ya watu wanaoishi na VVU wenye umri katri ya miaka 15 hadi 64 ambao wanajua hali zao za maambukizi asilimia 90.9 walianzishiwa dawa za kufubaza VVU, wanawake wakiwa asilimia 92.9 na wanaume ni asilimia 86.1.Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa UNAIDS, Dk Leo Zekeng amesema Tanzania imepiga hatua kubwa kupambana na Ukimwi tangu miaka ya 1980 na kwa upatikanaji wa tiba tangu mwaka 2010 na misaada ya pamoja kutoka serikalini, mashirika ya kiraia yanayowakilisha watu wanaoishi na VVU pamojka na mashirika ya kimataifa ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa.Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk Leonard Maboko alisema kongamano hilo pia litaazimia mikakati mahususi itakayotoa matokeo zaidi katika kufanikisha dira ya kuwa na Tanzania isiyokuwa na Ukimwi kufikia mwaka 2030. | Kitaifa | 0 |
Mwenyekiti wa wa Taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi amezindua Maktaba ya Shule ya Msingi Tandale Magharibi, Dar es Salaam na kutoa wito kwa wanafunzi kuitumia vyema maktaba hiyo kujenga maarifa.Aidha amewataka wanafunzi kuilinda maktaba hiyo kama chanzo cha maarifa na weledi. Maktaba hiyo imewezeshwa na taasisi hiyo kufuatia shindano la Andika Challenge kwa shule za za serikali nchini.Aliwataka pia wazazi kushawishi watoto kusoma vitabu na kutumia maktaba na kujisomea wawe weledi.Akizindua maktaba waliyoikarabati, kuweka mashubaka na vitabu vya aina mbalimbali, Jacquiline alisema amejisikia furaha kutimiza ahadi ya kukabidhi maktaba kwa shule hiyo iliyotoa mshindi.Shindano hilo linafanyika mikoa yote Tanzania na kushirikisha wanafunzi wote wa shule za msingi za Serikali kuanzia darasa la nne hadi la saba ambapo wanafunzi huandika hadithi na kutuma kwa sanduku la Posta 163 Dar es salaam na washindi huzawadiwa tuzo na shule aliyotoka husaidiwa kuwa na maktaba.Shule ya Msingi Tandale Magharibi imepata maktaba hiyo baada ya mwanafunzi wake, Nuurat Venance kushinda shindano la kutunga hadithi la wanafunzi wa shule za msingi za manispaa za Kinondoni na Ubungo, i Dar es salaam.Hivi sasa shindano hilo linashindanisha wanafunzi shule za msingi hapa nchini.Alisema baada ya mshindi kupatikana mwaka jana wa shule hiyo, taasisi ilibaki na changamoto ya kuwezesha kupatikana maktaba. Alisema anafurahishwa taasisi imetekeleza ahadi kwa mshindi huyo.Jacqueline alisema nia kubwa ya shindano hilo ni kusaidia watoto kujua kusoma na kuandika na kuwa wabunifu na kutumia ubunifu wao kusonga mbele.Alisema taasisi ya Dk Ntuyabaliwe ilianzishwa kwa ajili ya kumuenzi baba yake aliyekuwa anapenda kujisomea vitabu na kuwahimiza watoto wake kusoma.Anasema msimu huu mashindano hayo yanaendelea na vigezo vinavyostahili kufanywa na wanafunzi kuanzia darasa la nne hadi la saba ni kusoma na kuandika kwani ndio njia pekee ya kukabiliana na wanafunzi wanaomaliza shule bila kujua kuandika.Alisema kwa sasa wamewezesha shule nne kuwa na maktaba, wanafunzi 4,406 kusaidia mambo mbalimbali na vitabu takribani 20,827 | Kitaifa | 0 |
WAISLAMU nchini wametakiwa kudumisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwao na Watanzania wote ili kulifi kisha taifa kwenye maendeleo ya kweli. Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Rais John Magufuli kwenye maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata).Rais Magufuli ambaye alikuwa mgeni rasmi, aliwahimiza Waislamu na Watanzania wote nchini, kuudumisha umoja, amani katika kulijenga taifa. Alisema kwa kuzingatia umoja na uzalendo na kwa kuitanguliza mbele Tanzania, taifa litafanikiwa kwa kiasi kikubwa katika mambo mengi.Alisema katika nchi nyingi ambako watu wanauana wakiwemo watoto, wanafanya hivyo kwa sababu walishindwa kuvumiliana, kusameheana na kuitunza amani yao. Alisema katika hali kama hiyo ya migogoro au mauaji, taifa linahitaji kufanya toba kwa ajili ya kuchoma dhambi ili watu na taifa liwe safi.“Miaka 50 ina changamoto, nawapongeza kwa kuadhimisha miaka 50 ya Bakwata ambayo ilianzishwa tarehe 17/12/1968. Mimi kama Kiongozi wenu ndani ya Serikali, natambua mambo mengi yaliyofanywa na Bakwata, hata huu umoja miongoni mwa Waislamu ni kitu kikubwa sana, lakini mmetoa mchango mkubwa katika huduma za jamii kama vile elimu, afya na maji,” alieleza Rais Magufuli.Akizungumza awali, Kaimu Katibu Mkuu wa Bakwata, Ustaadhi Nuhu Jabir Mruma, alisema katika kipindi cha miaka 50, Bakwata limefanikiwa kuanzisha shule na vyuo vinavyotoa elimu katika ngazi mbalimbali zaidi ya 34 pamoja na vituo vinavyotoa huduma za afya zaidi ya 24. Pia, Bakwata ina mpango wa kujenga chuo kikuu kikubwa wilayani Korogwe mkoani Tanga.Mali za Waislamu Kuhusu mali za Waislamu, Rais Magufuli aliwataka Waislamu chini ya uongozi wa Mufti Abubakar Zubeir, kuhakikisha mali zilizoanza kurejeshwa, hazitolewi tena kwa watu wasiohusika, bali zitumike kwa manufaa ya Waislamu. Kwa mujibu wa Rais Magufuli, chanzo kikubwa cha mali hizo kutoka mikononi mwa Waislamu ni Waislamu wenyewe.Alisema alianza kushughulikia suala la kuzirejesha mali za Waislamu tangu alipokuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi. Alisema alipokutana na Mufti wa wakati huo, kujadili kuhusu suala la mali hizo, na baada ya kupitia nyaraka mbalimbali, aligundua kuwa waliohusika kuzigawa mali hizo ni Waislamu wenyewe.“Nimeanza kushughulikia migogoro ya mali za Waislamu tangu nikiwa Waziri wa Ardhi, nilichokigundua waliohusika ni Waislamu wenyewe kwa kuingia mikataba ambayo mingine ilikuwa ni migumu kuirudisha na watu wakachukua mali hizo,” alisema Rais Magufuli. Alisema baada ya kuchaguliwa kuwa Rais, Mufti Zubeir alimfuata na kumweleza kuwa wakati ule alishindwa kwa kuwa alikuwa Waziri, lakini leo yeye ndiye Rais, hivyo awasaidie kuzirudisha mali za Waislamu.Kutokana na umuhimu wa jambo hilo, Rais Magufuli aliamua kuita Waziri wa Ardhi, wakuu wa mikoa na viongozi wengine, kuanza kushughulikia kurudishwa kwa mali hizo, kama alivyofanya hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Hai kwa kurudisha shamba la Waislamu. Alisema mali ambazo ilikuwa ni vigumu kuzirudisha, aliamua kuzifuta na kwa kuwa walionyang’anywa mali hizo hawakufurahi, akawaomba wamuombee.Rais Magufuli alisema kuongoza, siyo jambo rahisi na ndiyo maana hata miradi mikubwa ya maendeleo, ambayo serikali yake inaitekeleza, ikiwemo ununuzi wa ndege mpya, ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa Mto Rufiji, imewezekana baada ya kuwabana mafisadi ,ambao walikuwa wakinufaika na rasilimali za nchi hii.Amsifu Mufti Katika kuonesha namna Mufti Zubeir ni kiongozi anayejali watu wake, Rais Magufuli alisema kuwa alishangaa kumuona akichimba kaburi wakati alipokwenda kushiriki mazishi wa mmoja ya ndugu za Rais mstaafu Jakaya Kikwete huko Msoga, Chalinze mkoani Pwani. Rais Magufuli alisema siyo kitu cha kawaida kumuona kiongozi wa dini, mwenye wadhifa wa juu kama Mufti, kushiriki kuchimba kaburi. Ujenzi wa Msikiti Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Mufti Zubeir alimshukuru Rais Magufuli kwa kumuomba Mfalme Mohamed VI wa Morocco kuwajengea Msikiti Mkubwa kwenye Makao Makuu ya Bakwata yaliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.“Nilimuomba Mfalme wa Morocco kujenga msikiti kwa sababu naamini sote tunatakiwa kufanya mambo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na hata jana (juzi) niliongea naye amefurahi sana nilipomuomba ajenge msikiti,” alieleza Rais Magufuli. Mufti Zubeir alisema ujenzi wa msikiti huo wenye uwezo wa kuchukua watu 9,000 kwa wakati mmoja ni juhudi za Rais Magufuli.Awali, Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, pia alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kuwajengea Bakwata jengo la ofisi la ghorofa tatu. Rais atoa fedha Pia katika tukio hilo, Rais Magufuli alitoa Sh milioni 30 kwa Bakwata na kumkabidhi Mufti ili wazitumie kadri watakavyoona inafaa. Kauli ya Waziri Mkuu Kwa upande wake, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alimpongeza Mufti Zubeir kwa kukomesha migogoro ya kugombea uongozi ndani ya misikiti.Alisema hiyo ni hatua kubwa kwa kuwa dini ni taasisi muhimu katika kuwajenga wanadamu kimaadili, umoja na mshikamano. Waziri Mkuu pia aliipongeza Bakwata kwa maadhimisho hayo, kwa kuwa ni jambo jipya, ambalo halijawahi kufanyika tangu Bakwata ianzishwe. Hata hivyo, alitoa wito kwa Bakwata kufanya maadhimisho hayo kila mara, ikiwezekana kila mwaka ili kujitathmini kuhusu mafanikio na changamoto.Viongozi mbalimbali walihudhuria maadhimisho hayo, wakiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Philip Mangula, Katibu wa CCM, Dk Bashiru Ally, Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma, mabalozi wa mbalimbali, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, masheikh wote wa mikoa na viongozi wa taasisi mbalimbali za Kiislamu nchini. | Kitaifa | 0 |
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Stella Ikupa amesema alichokipenda katika matembezi yake kwenye maonesho ya Utamaduni ya Jamafest ni kuona namna wasanii wenye ulemavu wakionesha ubunifu wao wa kutumia vifuu vya nazi kutengeneza pochi.Ikupa alitembelea maonesho hayo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana na kuwaunga mkono baadhi akisema amevutiwa na vitu vingi wanavyotengeneza akitolea mfano wa pochi hiyo sambamba na viti vilivyotengenezwa kwa kutumia vifuniko vya maji.“Nimefurahi kupata fursa ya kuja kwenye maonesho, nimeona wasanii wenye ulemavu wamefanya kazi nzuri zenye ubora natoa mwito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono kwa kuthamini vya kwetu, “alisema. Mmoja wa walemavu wa ngozi, Hadija alisema, “pamoja na ulemavu tulionao, tumekuwa tukifanya shughuli za mikono ili kujikwamua kiuchumi”. Alisema yeye licha ya kwamba ni mwanafunzi wa shahada ya pili kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii, ame- kuwa akitengeneza mapambo mbalimbali kama hereni, cheni, bangili na vitu vingine vya sanaa za mikono.Naye Boniface Kiyenze ambaye ni mlemavu wa macho alisema amekuwa akitengeneza fenicha kwa ubunifu wa kutumia vifuniko vya maji na watu wamekuwa wakivinunua na kuvifurahia.Katika hatua nyingine, Waziri huyo ameomba wadau mbalimbali kuzisaidia timu za michezo za wenye ulemavu ili ziweze kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa. Hivi karibuni Rais John Magufuli aliisaidia timu ya taifa ya soka ya watu wenye ulemavu ‘Tembo Warriors’ kiasi cha Sh milioni 10 kwa ajili ya kwenda Angola kushiriki Mashindano ya Afrika. | michezo | 2 |
WATENDAJI wazembe na watoro wa kuhudhuria vikao vya kisheria, ambavyo vipo kwenye ratiba ya mwaka mzima katika ngazi ya mkoa na wilaya, wameonywa kuacha tabia hiyo.Onyo hilo limetolewa jana jijini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) na kusisitiza kuwa vikao vya kikanuni na kisheria, hivyo vinapaswa kuheshimiwa na kuhudhuriwa na wajumbe wote wanaohusika na vikao hivyo.“Si jambo jema na na haipendezi kwa mkuu wa wilaya au wa mkoa ambaye ndio mwenyekiti wa kikao anandaa kikao halafu wajumbe wanakipuuzia, tabia hii ni kukwamisha shughuli za maendeleo, nawaonywa wote wenye tabia hiyo muache mara moja,” alisema Dk Mahenge.Akizungumzia mvua zilizoanza kunyesha, aliwahimiza viongozi wa ngazi zote mkoani humo kusimamia na kujipanga vizuri kuzitumia mvua hizo kwa wakati kwa kuwaelekeza wananchi kupanda mazao ya kimkakati, kama ilivyo sera ya mkoa.Aidha, Dk Mahenge aliwakumbusha kuendelea kutekeleza agizo la Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, la kuifanya Dodoma kuwa ya kijani kwa kutumia mvua hizo kupanda miti ya kutosha katika maeneo yote ya Jiji na Halmashauri zake. “Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) tayari imeshaandaa miti ya kutosha hivyo tuitumie vyema, kupitia mvua hizi,” alisisitiza. Pia aligusia migogoro na malumbano yanayokuwepo katika halmashauri kuhusu eneo halisi la kuweka jengo fulani liwe la zahanati ama soko, akitaka kuachwa kwa tabia hiyo. | Kitaifa | 0 |
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema kuwepo kwa mabaraza ya biashara lengo lake kubwa ni kukuza uchumi na kuibua changamoto zinazokwamisha maendeleo ya sekta hiyo.Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Hassan Khamis Hafidh wakati akizindua Baraza la Biashara la Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.Amesema serikali imejipanga na mpango wake wa kuipeleka nchi katika sekta ya viwanda ili kukuza uchumi na kuongeza ajira.“Mikakati yetu ni kuelekea katika nchi ya viwanda na ndiyo maana tumeunda chombo cha kufuatilia muelekeo huo Snida ambacho kitafuatilia na kuibuwa changamoto zinazojitokeza,” alisema.Amewakumbusha viongozi wa mikoa ikiwemo serikali za halmashauri kuhakikisha kwamba wanatenga maeneo ambayo watayatumia kwa ajili ya kukuza biashara.Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Ayoub Mohamed Mahmoud alisema Serikali ya Mkoa wa Mjini imejipanga kuhakikisha huduma za kijamii ikiwemo ujenzi wa viwanda unaimarishwa.Amesema kuwepo kwa viwanda vingi vya aina mbalimbali kwa kiasi kikubwa kutasaidia kukuza uchumi na kuongeza ajira kwa vijana.Alifahamisha utafiti zaidi unaendelea kufanywa pamoja na kutenga maeneo ambayo yatatumiwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vya aina mbalimbali katika mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.“Tumejipanga kuona Baraza la Biashara linakuja na fursa mbalimbali kwa wananchi wetu zitakazowasaidia kupiga hatua kubwa ya maendeleo,”amesema.Aidha amesema baraza limelenga zaidi kuona fursa za kiuchumi kwa kundi la vijana zinaimarishwa pamoja na ajira.Mohamed ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Biashara mkoa wa mjini magharibi, aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kazi kubwa ya kukuza uchumi na biashara ambayo ndiyo itakayoleta mabadiliko katika maendeleo. | Biashara | 1 |
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Karatu, Arusha Mkurugenzi wa mbio hizo, Meta Petro alisema jana kuwa mamlaka hiyo imekubali kudhamini mbio hizo zitakazofanyika Aprili 21 mwaka huu.Petro alisema kuwa NCAA ndio mdhamini mkuu wa mbio hizo, ambazo mwaka huu ni za 11 kufanyika tangu zilipoanzishwa na zimekuwa zikikua mwaka hadi mwaka.Alisema kuwa anatarajia mbio za mwaka huu kushirikisha wanariadha wengi kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo wakimbiaji mbalimbali nyota.Mbali na NCAA, wadhamini wengine ni Kampuni ya Vinywaji ya Bonite, ambao wamekubali kuendelea kudhamini mbio hizo kwa kutoa bidhaa mbalimbali zenye thamani ya Sh milioni 15.Petro alisema kuwa anawashukuru wadhamini hao na bado milango iko wazi kwa wengine kujitokeza kusaidia kudhamini ili kuzidi kufanikisha mbio hizo, ambazo zitaanzia katika lango kuu la kuingilia na kutokea katika Hifadhi ya Ngorongoro na kumalizika katika viwanja vya Mazingira Bora mjini Karatu. | michezo | 2 |
TIMU ya Taifa ya soka ya wanawake chini ya umri wa miaka 20, ‘Tanzanite’ leo inashuka kwenye Uwanja wa Taifa kusaka ushindi katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Uganda.Mchezo huo wa kwanza Tanzanite inahitaji matokeo mazuri kuhakikisha inajiweka pazuri kabla ya kwenda kurudiana nao ugenini baadae nchini Uganda.Kocha wa Tanzanite, Bakari Shime amewatoa hofu Watanzania kwa kujinadi kuwa ana hazina kubwa ya wachezaji wenye uzoefu hivyo ana imani watafanya vizuri.“Maandalizi yetu ni ya muda mrefu, tuna wachezaji wengi na tulikuwa kambini pamoja na wachezaji wa timu ya umri wa miaka 17 na tunaruhusiwa kuwatumia hivyo tunategemea mambo yatakuwa mazuri,” alisema Shime.Shime alisema amewaandaa wachezaji kufanya vizuri sio tu katika uwanja huo wa nyumbani bali hata watakapokwenda ugenini.Alisema anaijua Uganda ni moja ya timu nzuri ukanda huu wa Afrika Mashariki hivyo, amejipanga kimbinu dhidi yao ili kupata matokeo mazuri.Kocha huyo alisema mapungufu aliyaona katika mchezo wa timu ya wasichana chini ya umri wa miaka 17 aliyafanyia kazi kwa vile baadhi ya wachezaji wapo katika kikosi hicho cha Tanzanite.Viingilio vya mchezo huo utakaochezwa saa 10:00 jioni ni Sh 5,000 kwa VIP A na Sh 1,000 kwa VIP B huku mzunguko ikiwa bure. | michezo | 2 |
Imeelezwa kuwa madini hayo hupitia Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), hivyo hukaguliwa na kusimamiwa ipasavyo.Hayo yalibainishwa mjini hapa juzi na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliakim Maswi alipotembelea na kukagua maendeleo ya mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka unaoendeshwa kwa ubia kati ya Kampuni ya Australia ya Tancoal na Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC).Alisema TMAA wapo katika kila mgodi nchini kwa ajili ya kusimamia na kukagua kiasi cha madini kinachochimbwa na kuuzwa ikiwa ni pamoja na kuhakiki vyeti vya mauzo ya madini hayo kwa kuhakikisha kuwa vinakwenda sambamba na kiasi cha mrabaha kinachotolewa na wawekezaji.“Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa sekta hii ya madini inawanufaisha Watanzania na si kuishia mikononi mwa wachache, ndio maana kuna TMAA ambao kazi yao ni kusimamia na kukagua kila kitu kinachoendelea katika migodi yetu yote hapa nchini,” alisema Maswi.Kamishna wa Madini nchini, Paul Masanja alisema Serikali kupitia maofisa hao wa TMAA wamekuwa wakifanya ukaguzi kuhakikisha kwamba Serikali inapata mrabaha stahili kupitia madini yanayouzwa ambapo alibainisha kuwa katika madini ya makaa ya mawe ya Ngaka Serikali inapata asilimia 100 ya mrabaha.Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tancoal, Tan Brereton alisema mgodi huo ni mradi mkubwa kwa Tanzania, kutokana na ukweli kuwa makaa yanayozalishwa hapo ni ya kiwango cha hali ya juu tofauti na migodi mingine kutoka nchi za jirani ikiwemo Afrika Kusini.Aidha alisema kutokana na uwepo wa kiasi kikubwa cha makaa hayo ya mawe katika mgodi huo unaokadiriwa kuwa na akiba ya tani milioni 450 itakayodumu na kutumiwa kwa takribani miaka 200, itawezesha kuuzwa kwa makaa hayo ndani na nje ya nchi, lakini pia kutumika katika kuzalisha umeme.“Makaa haya ya Ngaka yana ubora wa hali ya juu sana tofauti na makaa yanayochimbwa Afrika Kusini kwa kuwa madini haya hayahitaji kusafishwa baada ya kuchimbwa kabla ya matumizi tofauti na mengine ambayo husafishwa kabla ya kutumiwa, alisema Brereton. | Biashara | 1 |
NAIBU Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa ameliambia Bunge kuwa ndani ya miezi sita ijayo Wizara ya Kilimo itakamilisha utaratibu wa usajili wa wakulima wa mazao mbalimbali nchini.Pia amekiri kuwa viungo vya chakula (spices) ni muhimu katika afya hususani kwa wanaume na kusisitiza kuwa watatumia faida hizo kuimarisha soko la ndani.Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Najma Giga (CCM), Bashungwa amesema ni kweli viungo vimekuwa na umuhimu katika afya hususani kwa wanaume na kutumia faida hizo kuimarisha soko la ndani.Katika swali la nyongeza, Giga alitaka kujua mikakati ya serikali kutoa elimu kwa jamii kuhusu faida ya viungo kwenye afya ili kuimarisha soko la ndani. Aidha, katika swali la msingi, Mbunge wa Ziwani, Nassoro Suleiman Omari (CUF), alisema:“Kilimo cha mazao ya viungo vya chakula ni biashara yenye tija kubwa duniania kwa sasa. Je, serikali ina mpango gani wa kuhamasisha kilimo hicho hapa nchini.Akijibu swali hilo, Bashungwa alisema serikali inatambua umuhimu wa mazao hayo ya viungo kutokana na mchango wake katika kipato cha mkulima mmoja mmoja na pia katika kuliingizia Taifa fedha za kigeni.“Kutokana na umuhimu huo, serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi imeandaa Mkakati wa Kuendeleza Mazao ya Viungo (2014) ambao umelenga kuongeza uzalishaji wa tija,” amesema.Alisema maeneo mahususi katika mkakati huo ni utoaji mafunzo ya kuongeza ujuzi katika uzalishaji kwa wataalamu na wakulima, uzalishaji wa vituo vya kukusanyia mazao na kupanga madaraja na kuunda masoko ya pamoja ya wakulima.“Maeneo mengine mahususi yanayofanyiwa kazi ni kuhamasisha na kusimamia uanzishaji wa vitalu vya kuzalisha miche na mashamba na miti mama kwa ajili ya kuzalisha michezo bora ya aina za mazao hayo,” alisema.Alisema mkakati huo unatekelezwa kwa pamoja na wadau mbalimbali ikiwemo taasisi zisizo za kiserikali na vyama vya wakulima na ambazo ni pamoja na Sustainable Agriculture Tanzania –SAT, Chama cha Wakulima wa Viungo Amani (CHAWAVIA) na Jumuiya ya Wakulima wa viungo Wilaya ya Muheza.Bashungwa amesema Serikali pia imeandaa mwongozo wa uzalishaji wa mazao ambao umeainisha maeneo yanayofaa kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali yakiwemo mazao ya viungo.“Mwongozo huu umelenga kuonesha fursa za uzalishaji wa mazao mbalimbali yakiwemo mazao ya viungo.“Aidha, ndani ya miezi sita, Wizara itakamilisha zoezi la usajili wa wakulima wa mazao mbalimbali nchini ikiwamo mazao ya viungo kwa kubaini idadi yao, ukubwa wa mashamba na mahali yalipo ilikuwahudumia kwa ufanisi zaidi na kuongeza tija,” alisema Bashungwa. | Kitaifa | 0 |
IKOSI cha Simba kimeingia kambini jana tayari kujifua na mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya UD Songo inayotarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam Jumapili ya wiki hii.Katika mechi hiyo ya raundi ya awali, Simba inahitaji ushindi kusonga mbele baada ya kutoka suluhu ugenini Beira, Msumbiji wiki mbili zilizopita.Akizungumza na waandishi wa habari jana, Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara alisema maandalizi ya mchezo huo yanaenda sawa na kikosi cha timu hiyo kimeshaingia kambini.“Maandalizi yanaendelea vizuri kuhakikisha tunapata ushindi kwenye mechi yetu ya kimataifa,dhidi ya Songo, kikosi kimeshaingia kambini,tunawaomba mashabiki wajitokeze uwanjani kuwaunga mkono wachezaji kuhakikisha tunapata ushindi,” alisema Manara.“Sisi kwetu shabiki sio mchezaji wa 12 tu uwanjani, bali ni mchezaji muhimu kwenye kila idara, tunawaomba mashabiki wetu na wanachama twendeni Taifa Jumapili tukaujaze uwanja.”Aidha, Manara amewaomba mashabiki wa timu hiyo kuziunga mkono na timu nyingine zinazoiwakilisha nchi kwenye michuano hiyo ya kimataifa kwa kujitokeza kwa wingi kuwashangilia.Timu nyingine zinazoshiriki michuano ya kimataifa mwishoni mwa wiki hii mbali na Simba ni Yanga, itakayokuwa ugenini kucheza na Township Rollers kwneye mechi ya Ligi ya Mabingwa, na Azam na KMC zinazocheza kombe la Shirikisho zitamenyana na Fasili Ketema ya Ethiopia na AS Kigali ya Rwanda. | michezo | 2 |
Dk Kigoda aliyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa maonesho ya bidhaa za China yanayofanyika jijini hapa.“Unaweza ukanunua kahawa kwa mkulima ambayo haijatengenezwa kwa Sh 1,000 lakini ikipelekwa nje ikatengenezwa ikirudishwa inauzwa Sh 10,000 hivyo mapato yetu tunayapeleka nje,” alisema Kigoda.Aliwataka kuzingatia ubora wa bidhaa wanazozalisha kwani zikienda sokoni zitakuta ushindani.Alisema kupitia maonesho hayo ni vyema wafanyabiashara wakatumia fursa hiyo kujifunza kupitia China.Dk Kigoda alitaka urafiki wa Tanzania na China usaidie katika uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. | Biashara | 1 |
WABUNGE wamesisitiza haja ya serikali kuboresha huduma za matibabu katika hospitali, vituo vya afya na zahanati ili kulinda maisha ya Watanzania hususani wa vijijini na wasio na uwezo.Kwa nyakati tofauti, wakichangia bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na kupongeza juhudi za serikali katika kujenga miundombinu ya sekta ya afya ameonesha kuwa mazo zaidi utolewe kwenye kuboresha matibabu katika sehemu za kutolea huduma za afya. Baadaye jana wabunge walipitisha bajeti hiyo ya Wizara ya Afya.Akichangia hotuba hiyo, Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka (CCM) amesema katika kuhakikisha huduma za afya zinatolewa ipasavyo kwa wananchi ni vyema serikali kuimarisha ushirikiano wa sekta binafsi katika utoaji wa huduma za afya.“Utaratibu kushirikisha serikali na watu binafsi utaratibu muhimu ambao unapaswa kuendelea kwa mapana yake. Pia tunapoboresha hospitali za serikali tusisahau umuhimu wa kuhakikisha kwamba zile ambazo tulikuwa nazo tunalinda uwezo wake kwa sababu tusije ikawa kama ule msemo wa ‘tusiwibie Paulo kumlipa Petro.’“Sina budi kusema kwamba hospitali siyo majengo ila ni huduma na katika hili, waziri pia aangalie hali halisi ya hospitali za Referal (rufaa), napongeza juhudi za serikali ya awamu ya nne iliyokamilisha Hospitali ya Mloganzila lakini hospitali hiyo ni hospitali majengo kwani hakuna hospital town pale kwa ajili ya madaktari kukaa karibu na hospitali,” aliongeza Profesa Tibaijuka.Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (Chadema) aliwapongeza wauguzi na madaktari kwa kazi nzuri wanazofanya nchi nzima na kuomba wizara kusaidiana na Tamisemi kuwezesha hospitali ya wilaya ili kupunguza mzigo wa wagonjwa. | Kitaifa | 0 |
Hatua hiyo imeelezwa ni moja ya sababu ya kushindwa kufikia malengo ya kujikwamua na lindi la umasikini.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema aliyewakilishwa na Ofisa Elimu Sekondari, Benjamini Sipetro aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mnara wa mawasiliano ya simu wa Kampuni ya Airtel katika kijiji cha Nyakasungwa wilayani Sengerema mkoani Mwanza utakaohudumia zaidi ya vijiji saba.“Naamini mawasiliano ya uhakika yatamfanya mkulima kutumia teknolojia inayomzunguka kufanya biashara na kupata masoko ya mazao yao na malipo kupitia huduma mbalimbali za Airtel ikiwemo huduma ya Airtel Money,” alisema.Kwa upande wake Meneja Masoko wa kampuni ya Airtel Kanda ya Ziwa, Emmanuel Raphael alisema” Tunajisikia furaha kusogeza huduma za mawasiliano ya simu ya uhakika kwa wakazi wa Sengerema na Geita, na maeneo ya pembezoni ya nchi.”Wakati huo Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Mangochie amekabidhi vitabu vya masomo ya Sayansi kwa shule ya sekondari ya Nyakusungwa vilivyotolewa na Airtel kuwawezesha wanafunzi wa maeneo hayo kupata nyenzo muhimu katika kuboresha elimu. | Biashara | 1 |
Kutokana na hatua hiyo, Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), limeelezea kuridhishwa hatua hiyo, huku Mwenyekiti wake, Michael Mwanda akisema sasa ataanza kupata usingizi.Kuthibitika kuanza kwa majaribio hayo mwezi ujao kumeelezwa na Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni tanzu ya TPDC, Kampuni ya Gesi ya Taifa (GASCO), Kapuulya Musomba wakati wa ziara ya wajumbe wa Bodi ya TPDC waliokagua maendeleo ya ujenzi huo mwishoni mwa wiki katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara.Walikagua vya kupokelea gesi Kinyerezi na Tegeta, Dar es Salaam, vituo vya udhibiti wa usalama wa miundombinu ya bomba vilivyojengwa kuanzia Mtwara hadi Dar es Salaam kwa umbali wa kilometa 30, kituo cha kupokea gesi cha Somanga Fungu wilayani Kilwa, MnaziBay mkoani Mtwara inakopatikana gesi na pia kijiji cha Madimba, Mtwara unakojengwa mtambo wa kuchakata gesi.Akizungumzia maendeleo ya mradi huko, Musomba alisema unakwenda vizuri na kwamba kwa hatua iliyofikiwa, sasa majaribio yanaweza kuanza mwezi ujao.“Pamoja na changamoto kadhaa, naweza kusema tumefika pazuri na wakati wowote mwezi ujao majaribio ya kusafirisha gesi yanaweza kuanza…nia yetu ni kuhakikisha kama ilivyokuwa imepangwa, Juni mwaka huu tuwe tumekabidhi mradi kwa serikali,” alisema Musomba.Kutokana na kauli hiyo ya msimamizi mkuu wa mradi, Mwanda alisema kutokana na kazi hiyo mradi huo utakamilika kama ulivyopangwa Juni, mwaka huu. Maelezo hayo yalimkuna Mwanda na kusema: “Tujaribu kuwaeleza wananchi juu ya maendeleo ya mradi, kwamba unakwenda vizuri." | Biashara | 1 |
WAKATI Klabu ya Simba wakidhamiria kumpeleka mwanachama wa timu hiyo Hamisi Kilomoni kwenye Kamati ya Midhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, achukuliwe hatua kwa kosa la kutumia kivuli cha udhamini kudhoofisha brand ya timu hiyo, suala hilo limemuibua mwenyekiti wa zamani wa timu hiyo, Ismail Rage.Rage amezishauri pande zote mbili kukutana na kumaliza tofauti zao na sio kuendelea kubishana kwenye vyombo vya habari, jambo ambalo si muharobaini wa kumaliza sintofahamu hiyo inayoendelea kila siku.Ni muda mrefu sasa Simba imekuwa ikitunishiana misuli na Kilomoni jambo lilofanya uongozi wa wekundu hao kutoka hadharani na barua kutoka serikalini iliyoweka bayana kwamba Kilomoni sio mdhamini.Akizungumza jana Rage alisema viongozi wa Simba wanapaswa kufahamu Kilomoni ameitumikia timu hiyo toka inaitwa Sunderland si mtu mdogo wanapaswa kumuita kuongea naye.“Sidhani kama kuendelea kubishana kila siku kwenye vyombo vya habari kunaweza kuleta suluhisho ni vyema uongozi wa Simba ukubali kukutana kuyajenga masuala haya kwa busara, “ amesema Rage.Amesema Kilomoni hapaswi kujibiwa na Magori, kwa kuwa Magori ni mwajiriwa analipwa mshahara kama wafanyakazi wengine kinachotakiwa viongozi wa bodi wafanye mchakato wa kukutana kuweza kumaliza jambo hili.“Unajua Kilomoni anachokidai ni cha msingi kabisa kutaka mwekezaji aweke kiasi cha bilioni 20 kwenye akaunti ndipo wapatiwe hati sasa tatizo liko wapi anachokidai ni sahihi wanatakiwa kufanya hivyo asikilizwe wayamalize,“ amesema Rage. | michezo | 2 |
MFUKO wa Mawasiliano kwa Wote nchini (UCSAF) inatarajia kutumia takribani Sh bilioni 26.5 kwa ajili ya kufi kisha huduma za mawasiliano katika kata 214 zenye vijiji 521.Aidha, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajia kuzindua maadhimisho ya miaka 10 ya mfuko huo yanayofanyika jijini hapa kwenye viwanja vya Nyerere. Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Mtendaji Mkuu wa mfuko huo, Peter Ulanga na kuongeza kuwa ifikapo Mei mwaka huu watatangaza zabuni ya kufikisha huduma za mawasiliano katika kata na vijiji hivyo ambapo utekelezaji utaanza mara moja baada ya tathmini kukamilika mwishoni mwa Juni.“Bado kuna maeneo ambayo hayana huduma za mawasiliano ambapo mfuko huo umejikita kuhakikisha yanapata huduma muhimu na Mei mwaka huu mfuko utatangaza zabuni ya kufikisha huduma za mawasiliano katika kata 214, zenye vijiji 521,”alisema. Alisema serikali itatenga fedha kwa ajili ya maandalizi ya zabuni nyingine yenye vijiji zaidi ya 500 itakayotangazwa katika mwaka wa fedha 2019/20 kwa gharama ya Sh bilioni 26.Akizungumzia mafanikio ya ndani ya kipindi cha miaka 10 ya mfuko, Ulanga alisema Sh bilioni 118 zimetumika kufikisha mawasiliano tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009. Alisema serikali kupitia mfuko huo imeshafikisha huduma za mawasiliano katika kata 703, zenye vijiji 2,501 na wakazi zaidi ya milioni tano kote nchini.Ulanga alisema mchango huo wa serikali ni wastani wa asilimia 26 ya gharama za ujenzi na uendeshaji wakati watoa huduma wamechangia asilimia 74 kufanikisha uwekezaji huo. Alisema tangu kuanzishwa kwa mfuko huo, umejikita kutambua mahitaji ya mawasiliano nchi nzima, kushirikiana na wadau mbalimbali wa mawasiliano nchini, kushirikisha wananchi katika kutambua na kutatua kero za mawasiliano.“Wakati mfuko huu unaanza takribani asilimia 45 tu ya watanzania walikuwa wanaishi katika maeneo yaliyofikiwa na mawasiliano ya simu, mpaka tunavyoongea takribani asilimia 94 ya watanzania wanaishi kwenye maeneo yanayofikiwa na mawasiliano ya simu, ambapo zaidi ya asilimia 70 ni watumiaji wa huduma hizo huku asilimia 10 imechangiwa na mfuko,”alisema.Aidha, Ulanga alisema hadi sasa mfuko umepeleka vifaa vya Tehama katika shule zaidi ya 500 ambapo kila shule ilipata kompyuta tano na printa moja kwa wastani. Akizungumzia maadhimisho hayo yatakayofikia kilele chake Aprili 30 mwaka huu yakiwa na kauli mbiu ya ‘Mawasiliano kwa Wote ni Kichocheo cha Kuufikia Uchumi wa Kati’, Ulanga alisema yatakwenda sambamba na uzinduzi wa Klabu za Tehama katika Shule za Sekondari za Dodoma na Msalato. “Mfuko pia utagawa kompyuta kwa Wilaya ya Gairo pamoja na kuzindua mnara wa mawasiliano uliopo wilaya ya Bahi ikiwa ni kielelezo cha miradi ambayo inatekelezwa maeneo mengi nchini Tanzania Bara na Visiwani,”alisema. | Kitaifa | 0 |
KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) limemfungia maisha Michael Wambura kujihusisha na shughuli yoyote ya soka duniani kote.Kifungo hicho kinamfanya Wambura kutojihusisha na soka maisha katika maisha yake yote. Hukumu hiyo ya Kamati ya Maadili ya Fifa inaelezwa kukazia ile hukumu ya Kamati ya Rufaa ya TFF, ambayo Wambura licha ya kuwa Makamu Mwenyekiti wa TFF, hakutakiwa kujihusisha na soka.Katika uamuzi wake uliotumwa kwa TFF Januari 22, Kamati ya Nidhamu ya Fifa chini ya mwenyekiti wake Anin Yeboah wa Ghana, imekazia hukumu ya Kamati ya Rufaa na Maadili ya TFF, iliyotolewa Aprili 24, 2018, hivyo Wambura hatakiwi kujihusisha na shughuli yoyote ya soka duniani kote. Tayari TFF imemkabidhi Wambura barua hiyo ya Fifa na imewataka wadau wote wa soka kuzingatia maadili na nidhamu kwa kufuata taratibu zake kwa mujibu wa Katiba za TFF, Caf na Fifa. | michezo | 2 |
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndungulile amesema wana mpango wa kuhamishia kambi ya upimaji virusi vya ukimwi kwenye viwanja vya michezo ili kuhamasisha wanaume kujitokeza kupima. Akizungumza na waandishi wa habari juzi baada ya kutembelea maonesho ya Utamaduni ya Jamafest, Dk Ndungulile alisema sababu kubwa ya kutaka kuhamishia kambi viwanjani ni baada ya kugundua wanaume wengi wanakwepa kupima, huku baadhi yao wakionekana kufa zaidi kwa kutozingatia maelekezo.“Wanawake wengi wamekuwa wakijitokeza kuliko wanaume, tumeona twende kwenye makambi kuwafuata na mojawapo ni viwanja vya michezo ili kutoa elimu ya upimaji kwao,”alisema. Alisema hata kwa baadhi wanaokutwa na maambukizi huchelewa kuanza dawa za kuua makali jambo ambalo limechangia baadhi kufa mapema huku akiwahimiza kuuona ugonjwa huo wa kawaida kama yalivyo mengine.Katika hatua nyingine, Naibu Waziri huyo alisema ujio wake katika tamasha hilo una mahusiano makubwa na Utamaduni kwasababu wamekuwa wakifanya kazi n’a wasanii mbalimbali kufikisha jumbe za afya. “Michezo, sanaa na Utamaduni yana mahusiano tumekuwa tukifanya nao kazi, lakini pia ningependa kuona wasanii wanaibua mada mbalimbali za afya kwa mfano masuala ya lishe na mambo mengine tuweze kuyafanyia kazi,”alisema. Alizungumzia Jamafest alisema ameona kazi nyingine nzuri na kuona kuna bidhaa nyingi ambazo zinauzwa kuuzwa nje na kuwapongeza wizara ya Habari na Maliasili na utalii kwa maandalizi mazuri. Alisema tamasha lijalo wawashirikishe wawe pamoja kwani kuna mambo mengi yanahitaji kuzungumziwa kwa ushirikiano na wasanii. | michezo | 2 |
SIKU moja baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kutangaza kuwavua nyadhifa zao makamanda wa polisi wa mikoa mitatu kwa sababu tofauti, zikiwemo kukaidi agizo la kutokomeza rushwa na kulinda wauzaji wa dawa za kulevya na biashara ya magendo, imebainika baadhi yao bado wanaendelea na majukumu yao kama kawaida.Juzi Waziri Lugola aliwataja makamanda waliopoteza nyadhifa ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Salum Hamdun, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Emmanuel Lakula na Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Ramadhan Nganzi.Pamoja na uamuzi huo, Waziri Lugola alimtaka Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (Trafiki) nchini, Fortunatus Muslim, kujitafakari na kujipima kama anatosha katika nafasi yake. Hata hivyo, jana baadhi ya makamanda hao walipoulizwa walisema wanaendelea na kazi.Muslim na ‘Operesheni Nyakua’ Kamanda Muslim alisema hana taarifa kuwa ameambiwa na Waziri Lugola, ajitathmini na kujipima kama anatosha katika nafasi yake hiyo. Alipoulizwa saa sita mchana jana kuhusu agizo hilo, Kamanda Muslim alisema hajui lolote kuhusu agizo la Waziri na kuanza kumuuliza mwandishi wa habari hii lini agizo limetolewa.“Alisema kuna nini? Hebu niambie maana mimi nipo huku mikoani kwenye operesheni, sina taarifa kama nimetakiwa kujitathimini wala kujipima … hebu niambie nini kimetokea?” Alisema anaendelea na operesheni, kuhamasisha vita dhidi ya wavunjifu wa usalama barabarani, huku akielezea kuwapo kwa maendeleo mazuri ya Operesheni hiyo maarufu kama “Nyakua”.“Yani hadi sasa sina hizo taarifa, ila labda pengine kwa baadaye, ila sasa sijui lolote kuhusiana na hilo ndugu mwandishi,” alisema. Hamduni aendelea kuchapa kazi Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Hamduni ambaye naye alitajwa na Waziri Lugola kuvuliwa wadhifa wake, jana alibainika kuendelea na majukumu yake kama kawaida.Wakati gazeti hili lilipokuwa linafuatilia tukio la kuzuka kwa moto katika majengo ya Seminari ya Segerea wilayani Ilala, liliwasiliana na Kamanda huyo na akapokea simu, akieleza kutokea kwa tukio hilo na alipohojiwa wadhifa wake, alijitaja kuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo wa Kipolisi wa Ilala.Maoni ya wadau Baadhi ya wadau waliozungumza na gazeti hili, walieleza kuwepo kwa ukakasi wa kisheria kutokana na Waziri Lugola kuwavua nyadhifa zao makamanda hao, badala ya kuacha suala hilo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP),Simon Sirro.Akitoa ufafanuzi wa kisheria kuhusu suala hilo, Wakili Jebra Kambole alisema Sheria ya Jeshi la Polisi Sura Namba 322 iliyorejewa Mwaka 2002, ndiyo inatoa Mamlaka ya Waziri na IGP ambapo Kifungu cha 7(1) cha sheria hiyo kinampa Waziri uwezo wa kumpa IGP, maelekezo na miongozo mbalimbali kisera.Alisema Kifungu cha 7(2) cha sheria hiyo, kinampa mamlaka IGP uwezo wa kupanga maofisa na kuwapandisha na kuwashusha vyeo. “Japo sheria pia inampa uwezo waziri kutoa maelekezo kwa IGP juu ya utendaji kazi huo, kifungu hicho cha sheria kimetumia neno “May” ambalo kwa mujibu wa Sheria ya Tafsiri Tanzania Kifungu cha 53 Sura Namba 1 ya Sheria za Tanzania Kama ilivyorejewa 2002, ‘May’ lina maana hiari, sio sharti la lazima.“Hivyo Waziri hana mamlaka ya kuwaondoa kwenye nafasi zao, bali kumpa maelekezo mwenye mamlaka afanye hivyo, ambaye ni IGP ambaye naye si lazima atende alivyoambiwa, bali anatumia akili yake na mamlaka yake kuamua…hafanyi kama kasuku.Kwa maoni yangu haikuwa sahihi Waziri kuwatimua wakuu hao kwa mujibu wa sheria,” alisema Kambole. | Kitaifa | 0 |
Wafanyabiashara hao, walifanya ziara kwenda kujionea fursa mbalimbali za kibiashara katika eneo hilo ambalo linatarajiwa kuwa wa viwanda na biashara.“Serikali imetenga eneo la hekari 22,000 sawa na hekta 9,000 katika eneo hili maalumu la uwekezaji hapa Bagamoyo, na tunahamasisha wawekezaji wakiwemo wa mji wa Vallejo kuja kuwekeza hapa,” alielezea ujumbe huo ambao umeongozwa na Meya wa Vallejo, Osby Davis.Zawadia alisema kwa sasa Serikali inayo mipango ya kujenga miundombinu mbalimbali kwa kushirikiana na sekta binafsi, hivyo wafanyabiashara hawanabudi kuchangamkia fursa hiyo kwa kuanzisha viwanda na biashara na huduma mbalimbali.“ Mji wa Bagamoyo kutokana na kuwa eneo maalumu la uwekezaji, kutajengwa Bandari kubwa ya kisasa kupita zote nchini ili kuunganisha na maeneo mengine ya nchi na nje ya nchi,” alisema Mkurugenzi huyo na kuongeza kuwa Bagamoyo itakuwa kiungo kikubwa kwa biashara nchini.Mbali na bandari, Zawadia alisema kuna mradi mwingine wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa kisasa na reli itakayounganishwa na Reli ya Kati na Tazara na miundombinu yote hiyo, inalenga kuweka mazingira bora ya kibiashara na uwekezaji.Ugeni huo wa wafanyabiashara hao kutoka mji wa Vallejo, walitembelea maeneo hayo ya uwekezaji, likiwemo eneo la hekta 300 la Kamal Industrial Estate, linalomilikiwa na mtu binafsi.“ Ujumbe wa wafanyabiashara hawa wengi wao wamefurahishwa na Serikali ya Tanzania kutenga maeneo hayo kwa ajili ya viwanda na biashara,” aliongeza mkurugenzi huyo na kuongeza kuwa wako tayari kuja nchini kuitumia fursa waliyoiona Bagamoyo kwa ajili ya maendeleo ya nchi hizi mbili.Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Weusi wa Mji wa Vallejo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho, Carl Davis Jr alisema wao wanahitaji kufanya biashara katika mji wa Bagamoyo kwa faida ya miji hiyo miwili. | Biashara | 1 |
Makamu Mwenyekiti wa klabu ya soka ya Yanga Clement Sanga ajiuzulu.Ametangaza uamuzi huo leo wakati anazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam."Na ninajiuzulu kwa masikitiko kwa sababu pia naamini bado na kipindi kingine cha kuitumikia Yanga mpaka 2020 aah kwa mujibu wa Katiba yetu lakini kilichonipelekea kufanya hivyo ni namna ambavyo sehemu ya utamaduni mpya ambao unaanza kujitokeza" amesema.Kwa mujibu wa Sanga, ameamua kujiuzulu kwa kuwa yeye na familia yake wametishiwa usalama."Siku ya Ijumaa iliyopita nimeona clip mbalimbali zinatembea kwenye mtandao lakini clip hizi, zipo nyingi za kubeza za kufanya nini hizo sio shida sana kwa sababu ndiyo dhamana ambayo tumepewa na unaongoza watu wenye tabia tofauti lakini shutuma zimekuja, zimefikia kwenye clip inayotembea inaelezea kwa uwazi kabisa kwamba, inahamasisha watu mbalimbali kuja nyumbani kwangu na mapanga, na majembe, na shoka, aah sasa mimi nikafikiria huku mimi nina shamba ninapoishi kiasi kwamba wanataka kuja kulima au kuna nini" amesema Sanga."Hizi ndio tuhuma pekee nzito katika maisha yangu kuzisikia zinaelekezwa kwa kiongozi wa mpira wa miguu kwamba watu kuhamasishana kuna na mapanga kwenye nyumba ya mtu anapoishi, unatafuta sababu huwezi kuielewa"amesema.Sanga ameiongoza Yanga tangu Yusuph Manji alipojiuzulu uenyekiti. | michezo | 2 |
BARAZA la Chuo Kikuu Mzumbe limeiomba Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kushughulikia tatizo la ukosefu wa takwimu sahihi za wanafunzi wanaohitimu elimu ya juu zinazoonesha mwenendo wa ajira, kuajiriwa katika sekta ya umma na binafsi ili kubaini ukubwa wa changamoto ya ajira na kusaidia kuwa na mipango maalumu.Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Profesa Mathew Luhanga (pichani) alisema hayo hivi karibuni kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji Mkuu mstaafu Barnabas Samatta kuwatunuku wahitimu Shahada ya Uzamivu, Shahada ya Umahiri, Shahada ya Kwanza, Stashahada na Astashahada kwenye Mahafali ya 17 mjini hapa.Profesa Luhanga alisema changamoto kubwa ya Chuo Kikuu Mzumbe ni uhaba wa ajira kwa wahitimu ambayo ni pamoja na kwa vyuo vikuu vingine nchini, licha ya baadhi ya wahitimu kujiajiri wenyewe.Pia alisema changamoto hizo hazijapewa kipaumbele kutokana na kutokuwa na tawimu sahihi ya idadi wanaohitimu vyuo vikuu na hawafahamiki ni asilimia ngapi ya wahitimu wa vyuo vikuu wanaajiriwa kuwa kazini, kazi zipi pamoja na takwimu za walio katika ajira za sekta binafsi.Alitumia fursa hiyo kuiomba TCU yenye jukumu la kufanya tathimini na kutangaza takwimu sahihi za ukusanyaji wa ajira wa wahitimu wa elimu ya juu kuja na majawabu hayo kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ili hatimaye changamoto zitakazojitokeza zifanyiwe kazi na mamlaka zinazohusika.Makamu wa Mkuu wa chuo hicho, Profesa Lughano Kusiluka aliishukuru serikali kwa kukiwezesha kupatiwa fedha kiasi cha Sh bilioni 6.5 kwa ajili ya kujenga hosteli za kisasa kulaza wanafunzi.Katika mahafali hayo, wanachuo 2,233 kati yao watatu wa Shahada ya Uzamivu (PhD) kutoka Kampasi Kuu Mzumbe walitunukiwa shahada zao, ambapo wahitimu wa mwaka huu kwa kampasi zote tatu za Chuo Kikuu hicho ni 3,724, wanawake wakiwa ni asilimia 49.5 na wanaume ni asilimia 50.5. | Kitaifa | 0 |
Hii ni mra ya kwanza kwa Wakenya kutamba katika mbio hizi, ambazo mwaka huu zilianzishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangala, ambapo mwaka jana nafasi tatu za mwanzo zilishikwa na Watanzania.Mshindi wa kwanza kwa wanaume katika mbio hizo za mwaka huu alikuwa Mkenya, Joseph Mbata kwa kutumia saa 1:04.54.12 akifuatiwa na Mkenya mwenzake, Benard Mussa aliyetumia muda wa saa 1:05:09.59 Wakati Mtanzania wa kwanza ni Pascal Mombo aliyeshika nafasi ya tatu kwa saa 1:06:05.71.Kwa upande wa wanawake, Wakenya waliendelea kutamba baada ya mwanariadha wake, Monica Cheruto kumaliza wa kwanza kwa kutumia saa 1:15:07 huku Mtanzania Failuna Abdul alimaliza wa pili kwa saa 1:15:20. Failuna alikuwa miongoni mwa wanariadha wa Tanzania walioshiriki Michezo ya Jumuiya ya Madola iliyofanyika Gold Coast, Australia iliyomalizika Aprili 15.Hakufanya vizuri katika mbio za meta 5,000 na 10,000.Kwa upande wa kilometa tano, mkimbiaji wa siku nyingi wa Tanzania, Mary Naali (Arusha) alimaliza wa kwanza kwa upande wa wanawake alipotumia dakika 17:40.65 wakati mshindi wa pili ni Rozalia Fabiani alitumia dakika 17:55.56 (JKT) wakati wa tatu ni Anastazia Mkama wa Mara alitumia dakika 18:01.40 .Katika mbio za kilometa tano kwa wanaume mshindi wa kwanza ni Elibariki Buko wa JKT alitumia dakika 14:14.81 huku mshindi wa pili ni Marco Sylvester wa JKT alitumia dakika 14:14,86.Kwa mwaka jana katika mbio za kilometa 21 kwa wanaume na wanawake washindi wa kwanza wa mbio hizo zinazodhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro alikuwa Faraja Lazaro wa JKT na Failuna Abdi wa Talent Club ya Arusha, ambao walishinda mbio hizo kwa kutumia saa 1:03.42 na 1:03.52.Mshindi wa kwanza wa mbio hizo kwa upande wanaume na wanawake, kila mmoja mwaka huu ameondoka na Sh milioni 1 wakati mshindi wa pili amebeba Sh 500,00 huku wa tatu Sh 250,000, mshindi wa nne Sh 100,000 na watano Sh 80,000.Mbio hizo zilishirikisha zaidi ya wakimbiaji 700 kutoka ndani na nje ya Tanzania. Mbali na mbio za kilometa 21 na tano, pia kulikuwa na mbio za watoto ambao walikimbia umbali wa kilometa 2.5. | michezo | 2 |
WAFUGAJI samaki katika maji baridi mkoani Morogoro wameshauriwa kuchukua tahadhari wakati wa kuandaa mabwawa ya samaki ili kuzuia magonjwa ya aina mbalimbali ukiwemo wa kupasuka na kukatika kwa vichwa vya kambale.Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Ugani wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Dk Claudius Luziga alisema hayo hivi karibuni wakati alipotoa maelezo juu ya ufugaji bora wa samaki, magonjwa ya samaki, kinga na tiba wakati wa maonesho.Dk Luziga alisema samaki huugua magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na minyoo, fangasi na pia hupatwa na chawa, na wanaweza kubeba vimelea vya magonjwa kama taifodi na kipundupindu.Hata hivyo, alisema kituo kimeendelea kufanya utafiti wa kupata tiba ya kukabiliana na magonjwa ya samaki na hasa ugonjwa unaowashambulia samaki ujulikanao kama kuvu au ukungu ama fangasi, unaojulikana kitaalamu kama Saproleniass.Dk Luziga alisema ugonjwa wa kupasuka na kukatika vichwa kwa kiwango kikubwa unawaathiri zaidi samaki aina ya kambale, wanaofugwa katika mabwawa yaliyojengwa kwa saruji, yenye kina kifupi yasiyo na matope na kupitisha mwanga wa jua.Alisema, ugonjwa huo husababishwa pia na lishe duni na hasa ukosefu wa upungufu wa Vitamin C na tatizo hilo huwapata kambale wa rika zote ingawaje tatizo hilo ni kubwa zaidi kwa samaki wa miezi minne na kuendelea.Alitaja dalili zake ni samaki kuvimba tumbo, macho kuwa makubwa na kutoka nje ikiwa na kujitokeza mstari mwekundu kati ya kichwa na kiwiliwili, samaki kuwa na kidonda kikubwa kati ya kichwa na kiwiliwili, kichwa kukatika au kupasuka na mwishowe samaki kufa.“Tunashauri kinga ni bora kuliko tiba,” alisema Mwenyekiti wa Kamati ya huduma za ugani wa SUA, Dk Luziga. Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, ufugaji wa samaki ni miongoni mwa shughuli zinazokua kwa kasi nchini katika miaka ya hivi karibuni.Dk Luziga aliyataja baadhi ya maeneo ambayo samaki hufugwa kwa wingi katika maji baridi (maji yasiyo chumvi) ni pamoja na Dar es Salaam, Pwani, Mwanza, Arusha, Mbeya na Morogoro.Baadhi ya wafugaji wa samaki kutoka Manispaa ya Morogoro waliopata fursa ya kupatiwa elimu hiyo kwa nyakati tofauti walisema kuwa, elimu waliyopata itawasaidia vyema katika kuboresha ujenzi wa mabwawa ya samaki ili kuzuia magonjwa. | Kitaifa | 0 |
SERIKALI imetoa onyo la mwisho kuhusu matumizi mabaya ya simu za mkononi yanayofanywa na baadhi ya watu wanaopiga picha miili ya watu wanaokufa kwenye ajali na kuzirusha mitandaoni.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ametoa onyo hilo jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga miili ya wafanyakazi watano wa Azam Media Limited waliokufa juzi mkoani Singida kwenye ajali ya barabarani.“Acheni kurusha picha za vifo vya ajali mitandaoni, utakuta mtu anarusha picha bila kujali kuwa waliokufa ni binadamu na wana ndugu zao, unadhani ndugu zao wanapoziona picha hizo wanajisikiaje, onyo hili ni la mwisho, hatutasema tena, Sheria ya Makosa ya Mtandao itaanza kufanya kazi yake,”alisisitiza Waziri Mwakyembe.Wafanyakazi hao waliokufa kwenye ajali hiyo na kuagwa jana Makao Makuu ya Kampuni hiyo ni Salim Mhando, Silvanus Kassongo, Charles Wandwi, Florence Ndibalema na Said Haji.Marehemu Salim Mhando alizikwa jana kwenye makaburi ya Manzese- Sweetcorner jijini Dar es Salaam, Charles Wandwi atazikwa leo kwenye makaburi ya Sinza, wakati mwili wa Said Haji ulisafirishwa jana kwenda Hale-Tanga, Kassongo alisafirishwa kwenda Iringa na mwili wa Florence Ndibalema utasafirishwa leo kwenda Bukoba kwa maziko.Katika salamu zake za rambirambi, Dk Mwakyembe alisema kuanzia sasa serikali haitaongea tena kuhusu tabia ya watu kurusha matukio ya vifo vya ajali mitandaoni badala yake Sheria ya Makosa ya Mtandao itaanza kuwashughulikia wenye tabia hiyo.Pamoja na onyo hilo, Dk Mwakyembe pia aliipongeza Azam Media Limited kwa mchango mkubwa wanaoutoa katika tasnia ya habari na taifa kwa ujumla.Naibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, alisema kuwa uchunguzi wa ajali hiyo umeshaanza na dereva wa lori lililogongana uso kwa uso na basi aina ya Coaster lililowabeba wafanyakazi hao wa Azam ameshakamatwa.Alisema Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani linaendelea kukusanya ushahidi kutoka kwa mashuhuda wa ajali hiyo ili taratibu nyingine za kisheria zifuate.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando, alisema wafanyakazi hao waliokufa waliondoka Jumapili jioni kwenda Chato mkoani Geita kwa ajili ya kurusha moja kwa moja uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato uliofanywa na Rais John Magufuli jana.Alisema wafanyakazi hao walilala Singida na saa moja asubuhi waliendelea na safari yao, lakini baada ya muda wa saa moja na nusu baadaye wakapata ajali na kupoteza maisha.Kutokana na msiba huo Tido aliishukuru serikali na Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA) kwa ushirikiano mkubwa waliowapatia, lakini pia akatoa wito kwa familia zilizowapoteza wapendwa wao hao kuwasiliana na menejimenti ya Azam Media Limited wakati wowote kama wanahitaji ushauri au msaada wa jambo lolote.Aidha taasisi na watu mbalimbali walituma salamu za rambirambi kwa msiba huo.Miongoni mwa taasisi hizo ni Chama Cha Mapinduzi.“Wafanyakazi hawa wa Azam Media Limited wamekufa kishujaa kwa sababu wamekufa wakiwa kazini, Chama Cha Mapinduzi (CCM) tumefanya nao kazi kwa karibu sana,” alieleza Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole wakati akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya chama hicho.Wengine waliotoa salamu za rambirambi ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Mbunge wa Ilala (CCM), Musa Azan Zungu, Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF), Wilfred Kidao.Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dk Ayoub Rioba, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk James Kilaba, Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One, Joyce Mhavile, Deodatus Balile aliyetoa salamu kwa niaba ya Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania na Hamisi Mzee alitoa salamu kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT). | Kitaifa | 0 |
Hata hivyo, mamlaka hiyo imeonya kuwa bei hiyo ya mafuta nchini haitaweza kupungua kwa kiasi kikubwa, kutokana na kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya dola ya Marekani pamoja na kutokubadilika kwa ushuru mbalimbali wa ndani wa mafuta.Pamoja na hayo, Kampuni ya Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PICL) imeiomba Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini kuingilia kati na kuihamasisha Serikali iongeze ulinzi katika mabomba na matangi ya mafuta Kurasini, ambayo kwa sasa hayako salama na ni hatari kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.Akiwasilisha taarifa ya ukokotoaji wa mafuta kwa kamati hiyo Dar es Salaam jana, Mtaalamu kutoka EWURA, Lorivii Long’idu, alikiri kuwa ni kweli kwa sasa bei ya mafuta katika soko la dunia imekuwa ikishuka kwa kasi ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.“Bei hizi zimeshuka kutoka dola 100 hadi kufikia dola 60 kwa pipa ambayo ni sawa na asilimia 40 kutokana na kudorora kwa uchumi wa bara la Ulaya katika kipindi hiki na kuwepo kwa tofauti za mitazamo ya kisiasa hasa katika nchi za Marekani na Urusi,” alisema Long’idu.Hata hivyo, alisema pamoja na bei hizo kushuka tangu Julai hadi Desemba mwaka jana, kwa kawaida kwa Tanzania huchukua takribani miezi miwili bei hiyo kuweza kufikia soko la ndani.Alisema bei zote za mafuta katika soko la ndani, zimekuwa zikishuka kuanzia robo ya mwisho wa mwaka jana sambamba na kushuka katika soko la dunia na kwamba bei hizo hukokotolewa na Ewura kwa kutumia kanuni maalum, inayotumia gharama halisi za uagizaji mafuta nchini, zinazotokana na meli za mafuta yaliyopokelewa mwezi husika yaliyonunuliwa mwezi wa nyuma yake.Alisema uhusiano wa bei za soko la dunia na soko la ndani, unapishana kwa miezi miwili na kwamba mafuta yanayotumika mwezi huu, Ewura ilikokotoa bei zake tangu Novemba kulingana na bei ya mafuta yaliyonunuliwa katika soko la dunia mwezi huo.Long’idu alisema kwa hali ilivyo sasa bei za mafuta ghafi katika soko la dunia, zitaendelea kushuka kama hakutakuwa na tukio lisilo la kawaida duniani, hali itakayochangia kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo katika soko la ndani japo si kwa kiwango sawia.Alisema pamoja na bei kushuka katika soko la dunia kwa kiwango chochote kile, bei ya ndani itashuka kulingana na thamani ya Shilingi dhidi ya dola ya Marekani lakini pia ushuru uliopo ambao katika petroli unatozwa Sh 878, dizeli Sh 754 na mafuta ya taa Sh 701 kwa lita ambao wenyewe haubadiliki.Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Nishati na Madini, Jerome Bwanausi, aliagiza Ewura na PICL wanapokokotoa bei za mafuta kuhakikisha wanatoa ufafanuzi wa hali halisi ya bei za soko la dunia na utaratibu mzima wa uingizaji wa mafuta nchini ili kuondoa habari potofu zinazosambazwa juu ya bei hizo za mafuta.Aidha, aliagiza Wizara ya Nishati na Madini kuchukua hatua za haraka na kushughulikia suala la ulinzi katika mabomba na matangi ya mafuta ili kudhibiti hali ya hatari ya kulipuliwa kwa matangi hayo na kuhatarisha usalama wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.“Hii ni hatari sana kwa namna yale mabomba yalivyo hayana ulinzi, watu wanatoboa mabomba na kuiba mafuta na kuweka maboya, endapo mtu yeyote akitupa moto pale Dar es Salaam nzima itakuwa haipo, hatua za haraka zichukuliwe, na kamati ipatiwe taarifa za ulinzi wa sasa katika eneo hilo,” alisisitiza.Aidha, alisema kutokana na hali ya hatari ya usafirishaji wa mafuta iliyopo sasa kupitia malori hasa katika vijiji malori hayo yanakopita na kulala, ni vyema Serikali ikaanza mchakato wa kuchimba mabomba ya kusafirishia mafuta na kufufua reli ili kudhibiti usalama wa wananchi. | Biashara | 1 |
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja wa Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Emmanuel Mongella, alisema matawi hayo mapya yatahudumia wateja wa rejareja na wa biashara.Naye Meneja Usambazaji na Matawi wa benki hiyo, Masala Karosso, alisema benki hiyo imechagua kuwekeza katika maeneo hayo ya Sinza na Mbagala, kutokana na ukuaji kasi wa Jiji la Dar es Salaam na hasa biashara ndogo katika maeneo hayo.Alisema ufunguzi wa matawi hayo utaongeza huduma za benki hiyo jijini humo ambayo kwa sasa ina matawi katika maeneo ya Kariakoo, Posta, Viwandani, Oysterbay na Msasani.FNB ilianza kusambaza huduma zake katika maeneo ya kusini mwa Jangwa la Sahara, tangu 1874. Benki hiyo pia iko katika nchi za Afrika Kusini, Namibia, Botswana, Zambia, Msumbiji, Lesotho na Swaziland. | Biashara | 1 |
BINGWA mtetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara na wawakilishi wa kimataifa Simba leo wana kazi nzito ya kusaka ushindi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali dhidi ya TP Mazembe ya Congo.Kitendo cha kutinga hatua hiyo ni historia nyingine mpya baada ya mara ya mwisho kufanya hivyo mwaka 2003. Kipindi hicho kutinga hatua ya makundi ilikuwa ndio robo fainali tofauti na sasa mambo mengi yamebadilika kwenye michuano hiyo. Sasa wawakilishi hao wanatamani mafanikio zaidi na nia yao ni kucheza fainali za michuano hiyo. Wekundu hao wa Msimbazi waliwahi kufika hatua hiyo miaka 26 iliyopita mwaka 1993 na tangu hapo uwakilishi wao kwenye michuano ya kimataifa haukuwa wa kuridhisha.Bila shaka kutokana na ubora walionao sasa chini ya mwekezaji wao Mohamed Dewji anayependa mafanikio, kila kitu kinawezekana lakini mtihani walionao ni kuwatoa TP Mazembe. Simba ilibezwa kufika mbali ikadhihirisha mbele ya mashabiki wake na watanzania kwa ujumla kuwa inaweza. Ikahakikisha maadui zake wote hawatambi nyumbani kwake. Ili kuwadhibiti kwa kutumia uwanja wa nyumbani Al Ahly ya Misri anayeogopwa Afrika kwa ubora lakini kwenye uwanja wa Taifa alifungwa bao 1-0, ikampiga AS Vita ya Congo aliyefanya vizuri Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita kwa kufika fainali, mabao 2-1, JS Saoura ya Algeria.Hiyo ilikuwa ni harakati za makundi lakini leo wapo katika hatua ya robo fainali hatua ngumu kwa vile ni mtoano. Simba inatakiwa kuendeleza ule moyo wa kushinda nyumbani ila ni muhimu kwao kubadilika kwa kushinda mabao mengi zaidi na kutowapa nafasi wapinzani wao kupata bao la ugenini. Kuna makosa yalifanyika kwa wekundu hao katika mechi tofauti kuanzia hatua ya awali walizocheza nyumbani kwa kuruhusu wapinzani kupata mabao ya ugenini. Dhidi ya Mbabane walishinda 4-1, dhidi ya Nkana 3-1 na dhidi ya Vita 2-1 jambo ambalo ni hatari kwao hasa katika hatua hii waliyofikia sasa ambapo umakini unahitajika.Kingine wamekuwa wakiwadharau Mazembe na kusema msimu huu eti sio bora kama miaka mingine. Kama wangekuwa sio bora wasingefika hatua hii muhimu hivyo, wakiwadharau wanaweza kuwaadhibu kwasababu ni timu yenye uzoefu mkubwa na ina wachezaji wengi wazuri. Mazembe sio mara ya kwanza kuja kucheza katika ardhi ya Tanzania, wanaujua vizuri uwanja wa taifa, Dar es Salaam. Waliwahi kucheza nao mwaka 2011 katika mchezo wa pili hatua ya makundi kwenye uwanja huo Mazembe ikashinda 3-2 na ule wa kwanza uliochezwa kwao ikashinda 3-1.Kwa maana nyingine, mechi hii ni wakati sahihi kwa Simba kulipa kisasi kwa Mazembe. Timu hiyo ya Lubumbashi, Congo tayari itakuwa imeshawasoma wapinzani wake kwa kujua kuwa kumbe inakuwa wakali hasa kwenye uwanja wa nyumbani, wanaweza kuja na mbinu zao nyingine kuwadhibiti wekundu hao. Udhaifu uliopo kwa Simba ni kushindwa kumudu michezo ya ugenini.Takwimu za hatua ya makundi katika michezo iliyopita inaonyesha hawakupata bao hata moja katika michezo mitatu tena wakiruhusu kufungwa mabao mengi. Ukitizama kule Misri ilifungwa 5-0 dhidi ya Al Ahly, kule Congo ikafungwa 5-0 dhidi ya Vita na kule Algeria ilifungwa 3-0 dhidi ya JS Saoura. Kutokana na udhaifu huo, hawana budi kubadilika kama wanataka kusonga mbele kwa sababu huenda Mazembe wakaja kutafuta sare kisha wakaona wanaweza kumaliza mchezo wakiwa kwao. Ni ukweli usiopingika kuwa Simba kwa upande wa Tanzania ndio timu tishio kwa sasa kwa sababu kati ya timu 20, ndio pekee imepoteza mchezo mmoja tu katika michezo 22, ikishinda 18 na kupata sare tatu, ikishika nafasi ya tatu kwa pointi 57.Wanapewa uwezekano wa kuwaengua vinara Azam inayoshika nafasi ya pili kwa pointi 62 katika michezo 29 na Yanga inayoongoza katika michezo 29. Sababu wekundu hao wako nyuma michezo saba, ikiwa watashinda watachukua uongozi huo kiulaini. Ukiachana na ubora wao katika ligi, wana kikosi kizuri chenye washambuliaji hatari na tegemeo kama Mnyarwanda Meddie Kagere, Mganda Emmanuel Okwi na Mtanzania John Bocco. Kagere ameifungia timu yake mabao 15 kwenye ligi na michuano hiyo ya kimataifa mabao sita hivyo sio wa kubezwa.Bocco ana mabao 11 na Okwi ana saba kwenye ligi. Simba ikiwa nyumbani bado inajivunia safu bora ya ulinzi baada ya kuruhusu nyavu zake kuguswa mara saba pekee ikiwa ndio timu iliyofungwa mabao machache ingawa kimataifa bado hawako vizuri. Kwa upande wa TP Mazembe sio timu ya kudharauliwa kwani katika ligi ya kwao bado wapo kwenye ubora, wanashika nafasi ya pili kwa pointi 58 nyuma ya AS Vita inayoongoza kwa pointi 65. Timu hiyo ina wachezaji wengi hatari na wenye uzoefu mkubwa kama Tresor Mputu, Kelvin Zatu, Meshaki Elia na Jackson Muleka.Katika michezo yao iliyopita ya hatua ya makundi timu hiyo inaonekana kutokuwa na rekodi nzuri ugenini. Michezo mitatu waliocheza, miwili walipata suluhu dhidi ya Africain, sare ya bao 1-1 dhidi ya Ismaily na kufungwa 3-0 dhidi ya Constatine. Kwa kutizama na takwimu hizo inaonesha kuwa wanaweza kuja na lengo la kutafuta sare wakiamini nyumbani kwao ndio sehemu wanakoweza kupindua matokeo.Mechi zao za marudiano dhidi ya timu hizo walizocheza kwao zinaonesha namna gani matokeo ya nyumbani yaliwabeba. Ilishinda mabao 8-0 dhidi ya Africain, 2-0 dhidi ya Constatine na 2-0 dhidi ya Ismaily. Mchezo wa leo utakuwa mgumu kwa kila mmoja, hasa wekundu hao wanahitaji matokeo mazuri kwenye uwanja wa nyumbani kisha kujipanga na mechi ya marudiano ya ugenini itakayochezwa April 13, mwaka huu. Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems anasema anawaheshimu Mazembe hivyi ataingia kwa tahadhari. “Mazembe nimeifuatilia, ni timu bora na inafanya vizuri kwenye mechi zake, nimewaandaa wachezaji wangu, tutaingia kwa tahadhari kubwa,” anasema. | michezo | 2 |
Fainali hizo zimepangwa kufanyika Juni 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.Dilunga ambaye amekuwa kwenye kiwango cha juu tangu kuanza kwa msimu huu ameeleza kuwa wengi wamekuwa wakiitazama Singida kama timu iliyowatoa Yanga kwenye robo fainali na inapewa nafasi kubwa kutokana na hilo kitu ambacho si sahihi.Aliongeza kuwa, ingawa Singida ni timu iliyopanda Ligi Kuu msimu huu na kuonesha ushindani wa kutosha lakini siyo kigezo cha kuonekana wanaweza kuibuka mabingwa mbele yao.“Unajua Singida siyo timu ngeni kwetu, watu waelewe kwamba tulishakutana nayo mara mbili msimu huu kwa hiyo tunawafahamu na isitumike kigezo cha kuwatoa Yanga ikaonekana kama inaweza kupata ubingwa mbele yetu.“Ila niseme tu, wao wamepambana kufika hapo ina maana wapo vizuri kwa hiyo na sisi tunajipanga zaidi na zaidi ili kuhakikisha tunafanya vizuri katika mchezo huo wa fainali,” alisema Dilunga aliyefunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 2-0 kwenye nusu fainali dhidi ya Stand United.Kabla ya kukutana kwenye fainali hiyo tayari timu hizo zilishakutana mara mbili kwenye Ligi Kuu ambapo katika mechi ya kwanza iliyopigwa Manungu, Morogoro zilitoka suluhu na ile ya marudiano kwenye uwanja wa Namfua, Mtibwa ilishinda kwa mabao 3-0. | michezo | 2 |
WABUNGE wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (AEAC) kutoka Tanzania, wameeleza njia muafaka ya kuondoa vikwazo visivyo vya ushuru katika jumuiya hiyo ni uanzishwaji wa kamati ya kusimamia biashara.Aidha, wabunge wamepongeza jitihada za serikali katika kuharakisha kupitisha makubaliano, yanayofanywa kwenye jumuiya hiyo, huku ikiwa makini katika kulinda maslahi ya nchi. Pia, wabunge hao wametaka Watanzania kujivunia nchi yao, kwa kuwa na amani, huku Rais John Magufuli akisifika kwa kuhakikisha rushwa inaondoka nchini. Wabunge hao wameitaka Tanzania kuenzi Kiswahili katika EAC na kuhakikisha wimbo wa jumuiya hiyo, unaimbwa katika shule za msingi.Walisema hayo walipozungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kabla ya kuanza ziara ya siku tano nchini Tanzania. Katika ziara hiyo, watakutana na wadau mbalimbali nchini ili kujua vikwazo, mafanikio na nini cha kufanya kwa watanzania katika kukamata fursa za kibiashara zilizopo katika mtangamano wa jumuiya hiyo.Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano wa waandishi wa habari, kabla ya kuanza ziara hiyo, walieleza bayana kuwa bado kuna changamoto kwa Watanzania kutambua na kukamata fursa zilizopo katika jumuiya hiyo. Mwenyekiti wa wabunge hao, Dk Abdullah Makame (pichani) alisema moja ya changamoto kubwa kwa watanzania na wananchi wengine ndani ya jumuiya hiyo ni kushindwa kuundwa kwa kamati ya kusimamia biashara EAC, ambayo ni utekelezaji wa Ibara ya 24 katika makubaliano ya Umoja wa Forodha na Soko la Pamoja.“Kuundwa kwa kamati hii kutakuwa mwarobaini wa matatizo, kwani kutapunguza vikwazo visivyo vya kibiashara, kwani itifaki inazungumzia kuwa kila nchi inatakiwa kuwa na wajumbe watatu wenye utaalamu wa sheria na forodha, kwani kazi ya kamati hii kwa sasa inafanywa na mawaziri,“alisema. Alipongeza kazi za kukabili vikwazo zinavyofanywa na mawaziri, lakini kwamba ni vema kuwa na wataalamu.Alisema vikwazo hivyo siyo suala la kuvusha bidhaa pekee, bali pia binadamu kwenda katika nchi nyingine kupata ajira na kupata fursa mbalimbali. Makame alisema katika ziara yao iliyoanza jana, watakutana na wataalamu katika sekta binafsi na ile ya umma, kuona jinsi Tanzania inavyotekeleza makubaliano ya Umoja wa Forodha na Soko la Pamoja pamoja na changamoto zake.Pia, watakutana na wanafunzi wa vyuo vikuu katika ukumbi wa Nkrumah katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Aidha, watapata nafasi ya kukutana na asasi za kiraia, wananchi na wafanyabiashara katika Kituo Kikuu cha Mabasi ya kwenda mikoani na nchi jirani cha Ubungo, Dar es Salaam, ambapo watapata nafasi ya kutoa elimu kwa watanzania kuhusu mtangamano wa EAC.Wakizungumzia tuhuma zinazotolewa mara kwa mara na baadhi ya vyombo vya habari ndani ya EAC, kuwa Tanzania inakwamisha utekelezaji wa makubaliano kadhaa, Mbunge wa jumuiya hiyo, Adam Kimbisa alibainisha kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza, kwa kupitisha na kutekeleza mikataba mingi ya jumuiya hiyo. “Ni vema kueleza kuwa Tanzania ndiyo nchi kubwa katika EAC huku ikiwa ni mmoja wa waanzilishi, kuna baadhi ya maamuzi ni lazima kufanywa kwa umakini sana,” alibainisha Kimbisa.Mbunge mwingine wa jumuiya hiyo, Fancy Nkuhi alisema kuna baadhi ya masuala ya utekelezaji wa makubaliano, yanakuwa shida kutekelezwa kutokana na sheria kuwa tatizo, hivyo ni vema kufanyia kazi ili kurahisisha utekelezaji wake, kwani watendaji wanabanwa na sheria. Alitaka vijana kujitokeza katika mkutano, watakaofanya Jumatano jioni UDSM ili kufahamu namna ya kujiandaa kiutendaji na kutumia fursa zilizopo katika jumuiya.Mbunge Habib Mnyaa alisema Tanzania imejiweka mbali katika kuhakikisha umoja wa EAC unaimarika, kwa wimbo wake kuimbwa kwa ufasaha na watu wake, hivyo kutaka kuanza utaratibu wa kutumika katika shule za msingi. Alisema kwa sasa wimbo huo unaotumia lugha ya Kiswahili, hutumika katika nchi za Rwanda, Burundi na nyingine. Alisema pia bendera ya EAC ni vema ianze kupeperushwa katika wizara zote ili kujifahamisha na siyo kuwapa nguvu wengine.Alisema Tanzania ni mmoja wa waanzilishi wa EAC lakini nadra kuona bendera hiyo. Mbunge Ngwaru Maghembe alitaka watanzania kujivunia kuwa na amani katika ukanda huo. Alisema hivi karibuni walifanya ziara katika kambi za wakimbizi kwenye Jumuiya hiyo na ni Tanzania pekee ambayo haina wakimbizi kwenye makambi.Pia alieleza kuwa Tanzania inajivunia Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli ambaye anasifika katika ukanda huu katika kupambana na rushwa na amedhamiria kuiondoa nchini. Mbunge Pamela Maasay alitaka watendaji kuhakikisha kunakuwa na viwango sawa vya bidhaa katika EAC, ili kuwezesha wananchi kutoka pande zote kuvifuata na kunufaika. Kuhusu uanzishwaji wa Baraza la Vijana EAC, alisema muswada umepitishwa tayari na lengo ni kuwezesha vijana kukamata fursa mbalimbali. | Kitaifa | 0 |
KIUNGO wa zamani wa Yanga Athumani China amewatipia lawama mabeki na kipa wa timu yake hiyo zamani kwa kuruhusu bao kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Stand United.Yanga ilipoteza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara kwa kufungwa bao 1-0 na Stand United na kuhitimisha safari ndefu ya timu hiyo kutokupoteza mechi kwenye ligi hiyo.China aliyewahi pia kutamba na Simba kwenye miaka ya 1990 alitazama goli hilo kupitia video na kuwatupia lawama mabeki Kelvin Yondani, Andrew Vicent’Dante’ na kipa Claus Kindoki.“Wote wanastahili lawama, huyu beki wa pembeni(Yondani) kwa kuruhusu krosi kwani alikuwa na muda mwingi wa kumsogolea yule wingi kisha akazuia krosi. Lakini kipa nae(Kindoki) na mabeki wa kati(Dante na Gadiel) walitakiwa kujiandaa na tukio lolote ikiwa krosi imepigwa na hawakufanya hivyo.“Ndio mpira wa kitanzania mapungufu yapo lakini hatujifunzi kile tunachotazama kwenye televisheni. Kitu cha kwanza kwa mchezaji yoyote aliyepo nafasi ya pembeni ni lazima afanye kila afanyalo kutoruhusu krosi kuingia golini kwenu kwani unakuwa haujui wenzako wamejipangaje, kwani krosi ni nusu goli,”alisema.China baada ya kuangalia kipande hicho cha video. Hata hivyo nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania alisema kuwa bado timu yake hiyo ya zamani ina nafasi ya kushinda taji la Ligi Kuu msimu huu kama hawataruhusu makosa kama hayo yajirudie. | michezo | 2 |
POLISI mkoani Mwanza inamshikilia mwanafunzi wa kidato cha pili anayesoma Shule ya Sekondari St Apostos, Yela Sylvester maarufu Cosmas (17), kwa kosa la kudanganya wazazi wake kuwa ametekwa ili ajipatie fedha.Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Jumanne Muliro amewaeleza waandishi wa habari kuwa tukio hilo ni la Aprili 27, mwaka huu saa nne usiku katika Mtaa wa Mahaha wilayani Magu.Amesema hiyo ni baada ya kijana huyo kusindikizwa kwenda shule na mzazi hadi kwenye Kituo cha Mabasi cha Buzuruga jijini Mwanza na kupakizwa kwenye basi la Sheratoni, linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Geita.Lakini, hakwenda shule na badala yake aliitumia simu namba 0689447247 na kutuma ujumbe mfupi kwa baba yake, huku akiificha laini yake ya zamani ya simu, kwa madai kuwa alikuwa ametekwa kwa lengo la kujipatia fedha.“Kwenye ujumbe aliomtumia baba yake, alidai kuwa endapo wasipomtumia fedha hizo atapelekwa na watekaji nchini Zambia kufanya kazi, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria,” amesema Kamanda Muliro.Amesema polisi walifanya ufuatiliaji wa taarifa hizo za kutekwa kwa mwanafunzi huyo na kumtia nguvuni kijana huyo akiwa salama Lamadi wilayani Magu, akiwa na laini ya simu aliyoitumia kumdanganya baba yake kuwa alikuwa ametekwa.“Tunaendelea kumhoji na uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yake,” alisema Kamanda Muliro.Katika tukio jingine, Polisi imewakamata watu watatu kwa kosa la kupatikana na kilogramu 15 za bangi na watuhumiwa wengine wawili kwa kosa la kupatikana na pombe ya moshi lita 33.Kamanda Muliro alisema tukio hilo ni la kati ya Machi na Aprili katika operesheni kabambe inayoendelea.Aliwataja watu waliokamatwa na bangi kuwa ni John Marwa (26), Bhoke John (30) na Maria Stephano (25) wote wakiwa ni wakazi wa Kishiri Wilaya ya Nyamagana.Aliwataja watuhumiwa waliokamatwa na lita 33 za pombe ya moshi kuwa ni Mkemwa Matono (45), mkazi wa Fumagila na Vedastina Tibikunda (30) ambaye ni mkazi wa Bugarika jijini Mwanza.“Tunaendelea kuwahoji watuhumiwa, na siku hizi mtaona waliokamatwa ni wanawake, siku hizi unakuta mwanamke anasafirisha bangi kama furushi,” alifafanua. Aliongeza kuwa polisi inaendelea na mahojiano na watuhumiwa watafikishwa mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika. | Kitaifa | 0 |
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Wateja Binafsi wa NBC, Mussa Jallow, alisema ujumbe wa simu utawawezesha wateja kwa haraka kufuatilia miamala inayofanyika katika akaunti zao.“Kwa kuleta, huduma hii itawawezesha wateja wetu kutambua muamala uliofanyika isivyo halali hivyo kuweza kuchukua hatua ya haraka,” alisema Jallow. Kwa mujibu wa Jallow, taarifa za ujumbe zitatumwa kutoka katika miamala itakayokuwa ikifanyika katika mashine za ATM au vituo vya mauzo vitavyokuwa vimetoa huduma kwa kutumia kadi zao za benki.Huduma hiyo inatolewa bure, hivyo wateja wa NBC hawatalipia chochote watakapokuwa wakipokea ujumbe katika simu zao. Wateja wa NBC hawatahitajika kujisajili kwa huduma hiyo, kwani ujumbe utatumwa kupitia namba zao za simu zilizohifadhiwa katika kumbukumbu za NBC.Ofisa huyo wa benki alisema, wateja wote wenye namba za simu zilizo hewani watapokea ujumbe mara watakapofanya muamala kwenye ATM au katika vituo vya mauzo wakitumia kadi za manunuzi.“Mteja yeyote asipopokea ujumbe, basi inawezekana hatuna namba yake ya simu iliyosajiliwa na benki katika kumbukumbu zetu ama namba iliyosajiliwa siyo sahihi,” alisema. Aliendelea kusema, “Ikitokea hivyo tunashauri wateja kuchukua hatua ya haraka kwenda katika tawi la NBC lililo karibu ili kuhakiki taarifa zao, ili waanze kufurahia huduma hii.” | Biashara | 1 |
MENEJA wa timu ya Mbao FC Almas Moshi amesema timu yao ipo tayari kuhakikisha inapambana kwa hali na mali ili iweze kuibuka na ushindi katika mchezo wao wa leo dhidi ya Simba SC kwenye Kombe la Sportpesa jijini Dar es Salaam.Timu hizo zitacheza leo kuanzia saa nane mchana kuwania nafasi ya tatu ya michuano hiyo, huku mechi nyingine ya fainali itazikutanisha timu za Kenya, ambazo ni Kariobangi Sharks dhidi ya Bandari FC.Moshi amesema kuelekea mchezo huo wachezaji wake wote wapo kamili kuweza kuikabili Simba SC,ambayo msimu uliopita ilimaliza nafasi ya pili katika mashindano hayo.Alisema mpaka sasa anafarijika sana na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake katika mashindano hayo.Katika michezo miwili, timu hiyo iliyocheza, Mbao FC imeshinda mechi moja dhidi ya bingwa mtetezi wa mashindano hayo, Gor Mahia kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya sare ya bao 1-1, huku ilifungwa mechi moja dhidi ya Kariobangi Sharks kwa penalti 6-5 baada ya sare ya bila kufungana.Moshi alisema anawaomba wadau na wapenzi wa soka wa klabu yao wajitokeze kwa wingi kuhakikisha wanaishangilia timu yao katika mchezo wao wa leo pamoja michezo mingine ya Ligi Kuu iliyobakia.Kwa upande wake, nahodha wa timu hiyo David Mwasa alisema watapambana ili waweze kutimiza lengo lao la kushika nafasi ya tatu ya michuano hiyo, baada ya kuikosa ya kwanza. | michezo | 2 |
SERIKALI imewashauri wanaume nchini kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume ambazo zimethibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) pindi watakapokuwa na uhitaji huo. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi ametoa ushauri huo Bungeni Dodoma, leo Jumatatu, wakati akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii baada ya Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga kutaka kujua sababu za kuongezeka kwa matumizi ya dawa hizo na ikiwa serikali imezichunguza na kujua zinafaa. Hata hivyo, Dk Mwinyi ameeleza kuwa zipo dawa ambazo hazina kemikali na zimethibitishwa na TFDA kutokuwa na madhara, hivyo wanaohitaji watumie hizo, na sio dawa zisizothibitishwa. Aliongeza kuwa hakuna dawa za kuongeza maumbile ya kiume ambazo zimefanyiwa utafiti na kubainika kuwa salama kutumia, hivyo wananchi wasirubunike kununua dawa hizo. “Wananchi acheni kutumia dawa hizi kwani mtapata madhara, taarifa niliyo nayo ni kwamba hakuna dawa ambazo zimethibitishwa kitaalamu na kupewa kibali kwa ajili ya kuongeza maumbile,” alifafanua. | Kitaifa | 0 |
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema hakuna nchi au ukanda, unaoweza kuwa na uchumi endelevu pasipokuwa na maendeleo ya kidijiti, hususani katika sekta ya afya.Amebainisha hayo Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa saba wa Afya na Sayansi wa Afrika Mashariki. Mkutano huo hufanyika kila baada ya miaka miwili.Samia alisema juhudi zinazofanywa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika kuleta mabadiliko ya haraka ya teknolojia na kidijiti katika kusaidia utekelezaji wa mipango ya sekta ya afya, ni hatua sahihi katika kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) Namba 3 na mpango wa afya kwa wote.Aliwaeleza washiriki wa mkutano huo kuwa kuwekeza katika sekta ya afya na teknolojia sahihi za kidijiti ni muhimu kwa maendeleo ya jumuiya nzima, lakini pia utekelezaji wa Mkataba wa EAC hususani Kifungu cha 118 kinachotaka kuwepo kwa ushirikiano katika sekta ya afya, na vipengele vingine ninavyohusu soko la pamoja.“Nimefurahi kuona kwamba mkutano huu, siyo tu kwamba unahudhuriwa na wanasayansi kutoka Afrika Mashariki pekee, lakini pia umewaleta pamoja washiriki na wajumbe kutoka Afrika nzima na nje ya Afrika. Naamini mkutano huu utawapatia fursa ya kubadilishana taarifa kuhusu maendeleo ya sasa na kuja na mbinu za kukuza teknolojia za ubunifu ambazo zitaharakisha kufikia mpango wa maendeleo endelevu,” alisema Samia.Kwa kuwa sayansi na teknolojia ni nyenzo muhimu katika kushughulikia changamoto zinazoikabili sekta ya afya, Samia aliwapongeza waandaaji wa mkutano huo kwa kuchagua kaulimbiu inayoendana na wakati, inayosema “Teknolojia kwa ajili ya mageuzi ya mifumo ya afya na kufikia Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa.”Kwa mujibu wa Makamu wa Rais, kaulimbiu hiyo imekuja wakati mwafaka ambao dunia iko katika mageuzi ya nne ya viwanda, ambapo matumizi ya sayansi na teknolojia yanaongoza katika nyanja zote.Alisema suala la kuwa na maendeleo endelevu halitawezekana, kama uwekezaji katika teknolojia za kisasa hautafanyika ili kuzisaidia nchi hizo kuwa na majibu na ufumbuzi kwa matatizo na changamoto nyingi za kiafya kwa umma.Samia alisema Tanzania tayari imeshaanza kujenga mfumo wa kidijiti wa huduma za afya kupitia Wizara ya Afya na taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo, ikiwemo Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).Alisema matumizi ya kidijiti yameiwezesha serikali kufuatilia usafirishaji wa dawa tangu zinaponunuliwa na hadi zinapopokelewa katika eneo husika.Lakini, pia kupitia NHIF, imesaidia katika usimamizi wa uanachama wa mteja, madai na mchango na kupitia TFDA, imesaidia kupata taarifa za uagizaji bidhaa na uuzaji nje bidhaa pamoja na kupata taarifa kimtandao kuhusu madhara yanayotokana na matumizi ya dawa na vipodozi.“Kuhusu kile kinachofanyika katika taasisi zetu, tumeweka mfumo wa usimamizi wa hospitali katika hospitali zote za serikali. Mfumo huu hutoa taarifa za wakati na unaweza kufuatilia hali ya mgonjwa na akiba ya dawa, hivyo tumekuwa na matokeo mazuri tangu tuanze matumizi ya mfumo wa kidijiti ikiwemo kuboresha huduma za afya, kuongeza ufanisi na kuokoa muda na kuimarisha usalama wa taarifa,” alieleza Makamu wa Rais.Samia aliwaeleza washiriki hao kuwa ufanisi katika kutekeleza mpango huo wa kikanda, unategemea siyo tu ufanisi wa uratibu kutoka kwa Tume ya Utafiti wa Afya ya Afrika Mashariki, bali pia kutoka kwa nchi washirika wa EAC, washirika wa maendeleo na kila mdau wa sekta ya afya katika nchi washirika. | Biashara | 1 |
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewataka wazazi na walezi wilayani Karatu kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule hata kama hawana sare za shule.Aidha ameagiza uongozi wa serikali ya kijiji cha Lositete kuchukuliwa maelezo na polisi kuhusu sababu za kutochangia maendeleo ya elimu, badala yake wanaingiza siasa na kusababisha saruji kuganda.Gambo ametoa agizo hilo leo katika kijiji cha Lositete, kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu alipokwenda kukagua hali halisi ya madarasa pamoja na idadi ya wanafunzi walioanza masomo ya kidato cha kwanza.Ameagiza hivyo kutokana na taarifa ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Upper Kitete, Josephat Mau iliyodai kuwa wanafunzi tisa kati ya 171 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza shuleni hapo wameripoti shule.Mwalimu Mau amesema wanafunzi hao 162 hawajaripoti shuleni hapo kutokana na kukosekana na sare za shule huku walioripoti wakiwa ni tisa kwa sababu ya wazazi au walezi wao kutouza maharage kwani hakuna soko.Baada ya mwalimu huyo kutoa taarifa hiyo, Gambo aliagiza wazazi na walezi kuhakikisha watoto wote waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza kuripoti shuleni na nguo za nyumbani hata kama hawana sare ili waendelee na masomo wakati wazazi wao wakisubiri kuwanunnulia mahitaji ya shule."Rais ameagiza elimu bure hivyo wazazi au walezi watoeni watoto wenu majumbani ili waende shule bila ya kuwa na sare za shule huku mkiendelea kutafuta sare lakini pia nasisitiza nyie wananchi acheni kuingiza siasa kwenye masuala ya maendeleo, "amesema.Akizungumza na wananchi wa vijiji vya Lositete na Upper Kitete, Gambo aliagiza mwenyekiti wa kijiji cha Upper Kitete, William Safari pamoja kuhakikisha wanasoma mapato na matumizi ya kijiji ambayo wananchi wanadai hawajasomewa tangu mwaka 2017 hadi mwaka jana.Awali, baadhi ya wananchi walidai kuwa wameshindwa kujenga madarasa pamoja na maabara kwa sababu walichanga fedha ambazo inadaiwa zililiwa na aliyekuwa mkuu wa shule hiyo, Andrew Sulle.Anadaiwa kuchukua Sh milioni nane.Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Theresia Mahongo amesema wananchi zaidi wa vijiji vya Lositete na Upper Kitete wanapenda kuingiza masuala ya siasa katika maendeleo.Amesema amejitahidi kutatua changamoto zao ikiwamo kuhakikisha mwalimu huyo anachukuliwa hatua za kinidhamu na ameshahukumiwa kifungo.Amesema wanafunzi 5,313 walifanya mtihani wa darasa la saba mwaka jana huku wanafunzi 4,000 sawa na asilimia 75.3 walifaulu.Wanafunzi 3,446 wamepangwa kwenye shule za kata zilizokuwa na madarasa 83 na wanafunzi 539 walikosa nafasi.Alisisitiza kuwa wanafunzi hao 539 waliokosa nafasi hivi sasa wameshaanza masomo katika shule mbalimbali za wilaya hiyo kutokana na kubainika kuwapo shule ambazo wanafunzi hawakupangwa.Alisema wanaandika barua kwa wadau na kuhamasisha wanananchi kujenga madarasa pamoja na kukarabati viti na meza ili wanafunzi waweze kusoma. | Kitaifa | 0 |
ZIKIWA zimebakia siku chache, tamasha la Sauti za Busara 2020 kuanza, waandaaji wake wamesema mwaka huu wanataka kutumia katika kukemea unyanyasaji wa kijinsia suala ambalo linaendelea kutesa tasnia ya muziki na jamii. Tamasha hilo linatarajiwa kuanza Februari 13 hadi 16 katika eneo la kihistoria la Ngome Kongwe Zanzibar ambapo watazamaji wataweza kupata burudani ya muziki mubashara kutoka kwenye majukwaa matatu tofauti. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam, Mkurugenzi wa tamasha hilo, Yusuf Mahmud alisema tamasha la mwaka huu linaunga mkono juhudi za kukuza muziki unaopigwa mubashara wakati huo huo, kukemea unyanyasaji wa kijinsia. “Suala hili la unyanyasaji wa kijinsia litashughulikiwa chini ya kauli mbiu isemayo ‘Paza sauti yako, sema hapana kwa unyanyasaji wa kijinsia’ ikikusudia kubadilisha mitizamo, kuhamasisha mazungumzo na kuhimiza heshima kwa wanawake kwa kukuza uelewa juu ya udhalilishaji wa kijinsia,”alisema. “Hivi sasa nchini Tanzania, tunaona ni wanawake wachache tu wanaofanya muziki wa asili na wenye kuvutia. Hii ndiyo sababu kwa tamasha la Sauti za Busara la 2020 tulichagua wasanii kama Siti & the Band (Zanzibar), Thaïs Diarra na Mamy Kanouté (kutoka Afrika Magharibi), Pigment (Reunion), Evon na Apio Moro (Uganda) na wengine kutoka mkoa wa Afrika Mashariki,”aliongeza. Alisema hao ni wanawake wenye hisia kali ambao hutumia muziki kufikisha ujumbe na kujielezea. Wakati huo huo, bado wote ni waburudishaji wazuri kwa kupiga mubashara. | michezo | 2 |
['Red Bull Salzburg imeweka bei ya pauni milioni 86 kama dau la usajili kwa mshambuliaji Erling Braut Haaland, 16. (Tuttosport - in Italian)', 'Arsenal inaweza kumuuza kiungo wake Granit Xhaka ,27, mwezi Januari baada ya kuvuliwa unahodha. (Mirror)', 'Manchester United wanafuatilia maendeleo ya winga wa Burnley na timu ya umri wa miaka 21 ya England Dwight McNeil, 19 (Sun)', 'Aston Villa itakataa ofa yoyote ya Manchester United kwa kiungo wa uskochi John McGinn,25.(Birmingham Mail)', 'Kocha wa zamani wa Juventus Massimiliano Allegri atafaa sana kwa Manchester United, anasema kocha wa zamani wa timu ya taifa Italia Marcello Lippi. (Mail)', 'Allegri atakua chaguo zuri kwa Bayern Munich, anasema mshambuiaji wa zamani Luca Toni.(Sport1, via Goal)', 'Kocha wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger amesema angependa kushika nafasi iliyoachwa wazi kwenye klabu ya Bayern Munich. (Bein Sports)', 'Kiungo wa pembeni wa Chelsea na timu ya taifa ya England Mason Mount, 20, amekana kauli ya mchezaji mwezake wa zamani Mitchel van Bergen kuwa huenda akajiunga na Madrid au Barcelona. (Express)', 'Makamu mwenyekiti wa Manchester United Ed Woodward alitaka kumsajili kiungo wa Paris St-Germain Marco Verratti,27 na mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa klabu ya Real Madrid Raphael Varane,26,(Manchester Evening News)', 'Real Madrid wamefanya mazungumzo na kiungo wa Napoli Fabian Ruiz,23, kuhusu uhamisho muhimu kuelekea Bernabeu msimu ujao. (ESPN)', 'Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino amesema ana furahia namna anavyojitoa Christian Eriksen, 27 ingawa mchezaji huyo amekuwa akihusishwa na taarifa za kuachana na klabu hiyo.(Football London)', "Arsenal inapaswa ''kutumia pesa nyingi'' kumpata Kocha wa Leicester City Brendan Rodgers kwenye klabu hiyo, anasema mchazaji wa zamani Paul Mason. (Sky Sports)", "Mshambuliaji wa timu ya taifa Argentina Mauro Icardi, 26, anafanya ''kila kitu'' kufanikisha uhamisho wake kwa mkopo kutoka Inter Milan kwenda Paris St-Germain kuwa wa kudumu (RMC - in French)", 'Barcelona itamtazama kwa karibu kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na timu ya taifa ya Ujerumani, Kai Havertz,20, juma hili katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Atletico Madrid.(ESPN)', 'Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 05.11.2019', 'Unalitamkaje jina la nyota huyu wa Liverpool?', "Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema anafahamu mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe,20 ''ana ndoto'' ya kukichezea kikosi cha mabingwa wa La Liga. (Goal)", 'Rangers striker Alfredo Morelos, reportedly a target for Aston Villa, says he has had no contact with any club but the Colombian, 23, added: "Many teams that would be offering a good amount of money for me." (Antena 2, via Birmingham Mail)', "Mshambuliaji wa Rangers Alfredo Morelos, anayeripotiwa kuwa na nia ya kujiunga na Aston Villa, amesema hana mawasiliano na klabu yoyote lakini mchezaji huyo 23, amesema ''labda itokee timu itakayotangaza ofa nzuri kwake.''(Antena 2, via Birmingham Mail)"] | michezo | 2 |
UGANDA imetimiza ndoto zake za kutengeneza magari ambapo inakuwa nchi ya nne kati ya sita za Afrika Mashariki.Nchi hiyo iko mbioni kutengeneza mabasi ya kisasa ya abiria kwa ajili ya biashara ndani na nje ya Afrika Mashariki wakati wa Krismasi kwa gharama ya Sh milioni 95 za nchi hiyo, huku kukiwa na fursa ya kulipa kwa awamu.Magari hayo yatatengenezwa na kampuni ya Kiira Motors Corporation (KMC) inayomilikiwa na Serikali kwa asilimia mia moja.Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa KMC, Paul Musasizi, wanajiandaa kutengeneza mabasi ya kisasa kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu.“Bado tupo katika maandalizi na tunaongezea ujuzi na Wizara ya Sayansi. Tumeshatengeneza magari ya mfano na kufanyia majaribio katika maeneo ya Kisoro na Karamoja, hatukuona shida yoyote, hivyo tupo tayari kuanza kutengeneza magari kwa ajili ya biashara,” alisema.Musasizi aliyasema hayo wakati wa hafla ya kuihamishia KMC kutoka Wizara ya Viwanda kwenda Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri Mkuu, Dk Ruhakana Rugunda.Alisema mabasi ya Kiira yatakayotumia nishati ya umemejua, yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria 90 kwa wakati mmoja.“Tutaajiri watu wetu na mabasi yatauzwa kwa gharama inayokadiriwa kuwa Sh milioni 95 za Uganda,” alisema na kuongeza kuwa, mbali ya mabasi, watatengeneza pia magari madogo, malori, magari madogo ya kubeba mizigo na mengine kwa ajili ya matumizi mbalimbali.Ajira 14,000 zikiemo 2,000 za moja kwa moja zinatarajiwa kuzalishwa na TMC kwa ajili ya mafundi mbalimbali, wakiwemo wa spea za magari.Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Elioda Tumwesigye alisema wanakamilikisha makubaliano na China juu ya kusaidia masuala ya ufundi na kwamba tayari wataalamu wa Uganda wapo nchini China kwa mafunzo zaidi ya teknolojia ya utengenezaji magari.Waziri Mkuu alisema mabadiliko ya kuihamisha taasisi hiyo ya Serikali ni ya kawaida, yenye lengo la kuhakikisha mradi unapata maendeleo zaidi.Alikipongeza pia Chuo Kikuu cha Makerere kupitia Kitivo chake cha Uhandisi, kwa kutoa fursa kwa vijana kuonesha ubunifu wao.Wazo la ujenzi wa kiwanda cha uzalishaji wa magari, lilianza mwaka 2011 baada ya juhudi na maarifa ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Makerere kutengeneza gari linalotumia umeme la Kiira EV na linalotumia nishati ya jua la Kayoola EV mwaka 2016.Kutokana na mafanikio hayo ya wanafunzi wa chuo kikubwa barani Afrika, mwaka 2014 serikali ilitenga kipande cha ardhi mashariki mwa Jinja kwa ajili ya kiwanda cha magari ya KMC, huku Rais Yoweri Museveni akiwa mstari wa mbele kuhakikisha dhamira ya Uganda kutengeneza magari yake inafikiwa.Uganda inayoagiza wastani wa magari 50,000 kwa mwaka, itakuwa na soko la uhakika na magari ndani na nje ya nchi, hasa Ukanda wa Afrika Mashariki ambayo kwa asilimia kubwa huagiza magari kwa gharama kubwa kutoka Ulaya, Marekani na barani Asia katika nchi za Japan, Korea, India na China.Inakadiriwa kuwa, nchi za Afrika Mashariki huagiza wastani wa magari 250,000 kwa mwaka na mahitaji yanatarajiwa kupanda hadi kufikia magari 500,000 kufikia mwaka 2030.Juhudi Afrika Mashariki Tayari nchi nyingine za Afrika Mashariki zikiwamo Tanzania, Rwanda na Kenya zinaongeza kasi ya uzalishaji wa magari kwa ajili ya soko la nchi hizo na nyingine jirani.Mathalani, Kampuni ya Hanspaul Automechs Limited (HAL) iliyopo eneo la viwanda Njiro jijini Arusha, Tanzania inatengeneza magari makubwa ya kubeba watalii maarufu kwa jina la ‘War Bus’.Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Satbir Hanspaul, yanauzwa Kenya, Afrika Kusini na nchi za Ulaya.Kampuni hiyo imebuni na kutengeneza pia magari maalumu ya kubeba taka, yanayofaa kwa mazingira ya Tanzania, ikiwemo hali ya hewa, aina ya barabara na mfumo wa maisha wa wananchi wake.“Watu wengi hawataamini kwamba, nchi zenye viwanda vya kutengeneza magari kama Afrika Kusini na zile za Ulaya sasa zinanunua magari kutoka Tanzania, lakini ukweli ndio huo, wananunua pia magari kutoka Afrika, hususan Tanzania.Magari hayo yenye nembo za Toyota, Nissan na Land Rover, yanatengenezwa Tanzania kwa kutumia mashine za kisasa zikiwemo roboti kama ilivyo kwenye viwanda vya magari katika nchi zilizoendelea.HAL ilianzishwa mwaka 2007 na imelenga kuteka asilimia 25 ya soko la magari na spea zake katika nchi za EAC.“Tuna kila kitu kinachohitajika, mitaji kutoka kwenye taasisi za benki, intaneti yenye kasi, mawasiliano ya simu, nguvukazi ya kutosha na ardhi ya kutosha, tunachohitaji sasa ni watu kubadili mitazamo yao,” alisema Hanspaul.Volvo yaingia Kenya Moja ya kampuni kubwa katika utengenezaji wa magari ya aina mbalimbali, Volvo imeingia nchini Kenya na kuwekeza Sh bilioni 2.5 za nchi hiyo ili kufanikisha ujenzi wa kiwanda kinachotarajiwa kuanza na uzalishaji wa magari 500 kwa mwaka na baadaye kufikia magari 2,000 kwa mwaka.Kiwanda hicho kilichoingia ubia na kampuni ya NECST Motors ya Kenya, kinatarajiwa kuzalisha ajira 300 za moja kwa moja kiwandani hapo, lengo likiwa kushika asilimia 20 ya soko la Afrika Mashariki.Ni kiwanda cha tatu barani Afrika, vingine vikiwa Morocco ambako imeshika asilimia 20 ya soko na Afrika Kusini inakoshika asilimia 18 ya soko la magari. Kwa Kenya, kitakuwa kiwanda cha nne cha magari.Volkswagen kimeanza tena kazi baada ya kusitisha uzalishaji miaka 40 iliyopita. Kampuni za Peugeot, Toyota zimeanza pia uzalishaji, huku Iveco, Ashok Leyland pia wakitangaza nia ya kuanza uzalishaji wake nchini Kenya.Rwanda nako safi Nchini Rwanda, Volkswagen ya Ujerumani walizindua kiwanda cha uzalishaji wa magari mwaka jana, wakianza na gari madogo ya kampuni hiyo aina ya Volkswagen Passat, Volkswagen Polo na Volkswagen Teramont.Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa VW nchini Afrika Kusini inayosimamia pia kiwanda cha Rwanda, Thomas Schafer, Wanatarajia kuzalisha magari 5,000 kwa mwaka, ajira zinazotarajiwa kuzalishwa ni kati ya 500 na 1,000 yakiwa ni matunda ya uwekezaji unaokadiria kufikia Dola za Marekani milioni 20.Rwanda pia kupitia Kampuni ya Pikipiki Rwanda (RMC) inatengeneza aina mbalimbali za pikipiki na tayari soko lake limeanza kukua katika nchi jirani, zikiwemo Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).RMC inatengeneza aina saba za pikipiki zikiwemo Ingenzi, Indakangwa, Indahigwa, Imparage, Infarasi na Inzovu. | Biashara | 1 |
Tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililokuwa lifanyike leo Jumamosi katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam halitafanyika tena.Taarifa hii imetolewa asubuhi ya leo na kamati ya tamasha hilo lililoandaliwa na uongozi Clouds Media Group (CMG) huku wakisema uamuzi huo umefanyika kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao.“Tunaomba radhi kwa madhara yoyote yatakayosababishwa na hili,” imeeleza taarifa hiyo. Taarifa hiyo imeongeza kwamba itarudisha fedha zote za tiketi kwa waliokwishazinunua kwa njia simu, na kwenye vituo vyote vilivyokuwa vikiuza tiketi hizo.Hata hivyo kumekuwa na barua inayosambaa mtandaoni kutoka kwa Afisa Utamaduni, Manispaa ya Kinondoni ambayo haina muhuri, yenye kichwa cha habari ‘Kusitisha kibali cha kufanya Fiesta Leaders Club Dar es salaam.’Barua hiyo imeeleza imefuta kibali hicho baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi waliolazwa hospitalini wakidai kuwa sauti kubwa ya muziki kutoka kwenye viwanja hivyo huwaathiri, hasa wagonjwa wa moyo. | Kitaifa | 0 |
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla anatarajiwa kuongoza maelfu ya washiriki wa Rock City Marathon zinazoratarajiwa kufanyika Octoba 20, kwenye viunga vya Jengo la Biashara la Rock City Mall, jijini Mwanza. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo, Clement Mshana, ushiriki wa Waziri Kigwangalla unaenda sambamba na ushiriki wa viongozi wengine waandamizi wa serikali kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella ambaye tayari amethibitisha kushiriki. “Uwepo wa Waziri mwenye dhamana na masuala ya utalii kwenye mbio hizi unatokana na yeye kuunga mkono agenda iliyobebwa na mbio hizi ambayo mbali na kukuza vipaji vya mchezo huo ni kutangaza utalii hususani katika ukanda wa Ziwa kupitia mchezo wa riadha,’’alisema. Mbio hizo zilizo anzishwa miaka 10 iliyopita zinatarajiwa kupambwa na burudani mbalimbali zikiwemo ngoma za asili na maonesho ya waadau mbalimbali wa utalii. Aidha, zikiwa zimesalia siku chache tu kabla ya kufanyika kwa mbio hizo, tayari wadau mbalimbali wanaotarajia kushiriki wameonesha kufurahishwa na zawadi zitakazotolewa kwa washindi na washiriki zikiwemo medali na fedha taslimu zaidi ya sh milioni 30. “Pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, sh mil 2 kwa washindi wa pili na sh. Milioni 1 kwa washindi wa tatu, huku washindi wanne hadi 15 watapata medali na fedha taslimu. “Kwa upande wa mbio za kilomita 21, pamoja na medali washindi wa kwanza kwa wanaume na wanawake watajinyakulia Sh milioni 2 kila mmoja, Sh milioni 1 kwa washindi wa pili na Sh laki 7 kwa washindi wa tatu huku pia washindi wanne hadi wa kumi na tano wakiibuka na zawadi za pesa taslimu na medali kila mmoja,’’ aselima. Kuhusu mbio za kilomita tano ambazo zitahusisha washiriki kutoka mashirika na taasisi mbalimbali (corporates), Mshana alisema inatarajiwa kuwa zitaongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dk Philis Nyimbi sambamba na washiriki wenye ualbino, ambapo zawadi za fedha taslimu zitatolewa kwa washindi watatu wenye ualbino pekee. | michezo | 2 |
NI mechi ya kufa ama kupona kwa Simba inayotarajiwa kucheza na AS Vita ya Congo DR mechi ya mwisho ya kundi D kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Mshindi wa mechi hiyo atafuzu robo fainali za michuano hiyo hivyo ushindi kwa yeyote ni jambo muhimu zaidi leo. Simba inatarajiwa kutengeneza historia nyingine mpya iwapo itatumia vyema uwanja huo wa nyumbani kupata matokeo baada ya kufanya vizuri katika mechi zote za nyumbani tangu kuanza kwa michuano hiyo msimu huu hatua za awali hadi makundi.Jambo la kufanya vizuri katika kila mechi ya nyumbani, ni moja ya sababu zinazoipa kiburi Simba leo ikijua kuwa inao uwezo wa kushinda mechi hiyo, hata hivyo haipaswi kujiaminisha sana kwani wapinzani wao si wa mchezo mchezo. Kwenye michuano hiyo, kundi D linaonekana kuwa gumu zaidi kwani mpaka leo timu yeyote inayo uwezo wa kusonga mvele ikishinda mechi yake.Zinahitajika timu mbili za kwenda robo fainali. Simba inashika mkia ikiwa na pointi sita, ikishinda inafikisha pointi 9 hivyo itakuwa rahisi kwake kufuzu. Katika mechi nyingine, Al Ahly ya Misri inacheza na JS Saoura ya Algeria, mechi hii nayo inatakiwa ushindi, sare yoyote itaivusha Saoura Timu zote mbili zinakutana zikiwa na rekodi mbaya ya kufanya vibaya mechi za ugenini.Je, Vita itaendeleza rekodi hiyo au itavunja uteja? Kama ni ubora timu zote mbili zinafanya vizuri kwenye ligi zao, Vita inaongoza kwao ikiwa na pointi 62 baada ya kucheza michezo 23, ikishinda 20, sare mbili na kupoteza mmoja. Simba imecheza michezo 20, imeshinda 16, sare tatu na kupoteza mmoja ikiwa nyuma michezo saba ili kulingana na wengine.Utofauti wa timu hizo mbili unakuja kwenye vikosi, ambapo Simba ina wachezaji wengi wa kulipwa kutoka nje karibu 10 tofauti na Vita yenye wachezaji wanne wa kulipwa na wengine wanatoka kwao. Furaha ya wekundu hao ni kurejea kwa beki wake aliyekuwa majeruhi Erasto Nyoni. Pia, Emmanuel Okwi na Paschal Wawa waliokuwa majeruhi huku ikitarajiwa kumkosa kiungo Jonas Mkude anayetumikia adhabu ya kadi mbili za njano. Washambuliaji hatari wa kuchungwa pande zote mbili ni Jean Makusu wa Vita na Meddie Kagere wa Simba ambao wamekuwa waking’ara katika michezo tofauti iliyopita. | michezo | 2 |
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi ameahidi serikali itakiboresha Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (CSC) kilichopo Duluti mkoani Arusha kwa lengo la kuwa na jeshi la kisasa na kuvutia zaidi maofisa waandamizi kutoka nje ya nchi.Akizungumza baada ya kuwatunuku maofisa 60 wa ngazi za juu wa majeshi kutoka Tanzania, Kenya, Burundi, Rwanda, Uganda, Zambia na Zimbabwe vyeti kwenye mahafali ya 33 chuoni hapo jana, Dk Mwinyi alisema sera ya Tanzania sasa ni kuwa na jeshi dogo lakini lenye kutumia teknolojia ya kisasa.Alisema amefurahishwa hadi sasa jinsi chuo kilivyoboreshwa, kikitoa mafunzo yanayokidhi vigezo kwa maofisa wa ngazi za juu kuanzia cheo cha meja hadi luteni jenerali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na nchi nyingine rafiki.Aliongeza wataendelea kuboresha miundombinu ya chuo hicho chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 65 kwa mpigo, akisema ana uhakika ndani ya muda mfupi ujao maboresho makubwa yatakuwa yamefanyika chuoni hapo. | Kitaifa | 0 |
Mwanaume katika kijiji cha Obama, jimbo la Migori nchini Kenya amejiua baada ya kuhisi mwanamke aliyemuoa ana uhusiano wa kimapenzi na mtu mwingine.Inadaiwa kuwa, mwanamke huyo alirithiwa na kuwa mke wa mwanaume huyo miezi saba iliyopita baada ya mumewe kufariki dunia.Mwili wa mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Milton ulikutwa nje ya nyumba yao baada ya ugomvi na mkewe. mwanamke huyo ajulikanaye kwa jina la Anyango amewaeleza waandishi wa habari kuwa, waligombana sana siku ya Jumamosi, lakini Jumapili baada ya mumewe kurudi aliamua kuondoka na kwenda kulala nyumba nyingine ili kuepuka ugomvi."Ni mwanamume mwenye hasira sana, hivyo alivyokuja mimi nikaondoka ili kuepusha ugomvi, jambo ambalo likamfanya ahisi kuwa nimekwenda kwa mwanaume mwingine," amesema Anyango.Kwa mujibu wa mwanamke huyo, mara kwa mara mumewe alikuwa akitishia kumuua. | Kitaifa | 0 |
Ombi hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fabian Massawe kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba aliyetembelea Uwanja wa Ndege wa Bukoba kukagua maendeleo ya mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja huo.Massawe alisema kutokuwepo na ushindani kunachangia wakazi wa mkoa huo kutozwa nauli kubwa.Alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa uwanja wa Bukoba kutafanya idadi ya abiria kuongezeka kwa hiyo pindi ikianzishwa safari nyingine kutoka ATCL jambo ambalo pia litapandisha pato la Mkoa wa Kagera na Taifa kwa ujumla .Massawe pia alisema changamoto nyingine kuwa ni suala la fidia kwa wananchi ambao walifanyiwa tathmini ili kupisha ujenzi wa uwanja huo ambapo zililipwa bilioni 1 kwa watu 18 kati ya 41 ambapo wamebaki watu 23 ambao wanadai Sh milioni 900, hivyo wamekuwa wakiibua manung’uniko ya mara kwa mara.Kwa upande wa Naibu Waziri wa Uchukuzi Dk Charles Tizeba akitoa ufafanuzi juu ya hayo alisema tatizo la ukiritimba wa shirika moja la ndege na kupandisha nauli ovyo kutokana na kukosekana ushindani litaisha kwa kuwa ATCL wako mbioni kuagiza ndege nyingine ya CRJ ambayo itakuwa ikifanya kazi za masafa ya mbali kwa hiyo ndege iliyokuwa ikitumika katika ruti hizo itafanya safari za hapa nchini. | Biashara | 1 |
Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Gift Msuya amesema kuna fursa ya kuwekeza kwenye ufugaji wa nyuki na uchakataji wa asali na mazao yake.Amesema ofisini kwake kuwa, wanahitaji viwanda vidogo kwa ajili ya kuongeza thamani ya zao la asali linalozalishwa kwa wingi kwenye wilaya hiyo.“Lakini pia kuibrand asali yetu katika ubora na kuiwezesha kufika katika masoko ya kitaifa na kimataifa. Branding ni pamoja na kuispecify (kuitambulisha) kwamba hii ni asali halisi ya Uyui, lakini branding katika packanging material ya packaging, mashine za kuichuja na kuiweka katika viwango ambavyo vinakubalika kitaifa na kimataifa.”amesemaAmesema kuna jumla ya ekari 38,078 za misitu inayofaa kwa uwekezaji kwenye ufugaji nyuki ikiwemo ya kwenye kata za Kizengi, Tura, Goweko, Loya, Igalula, Kigwa, Shitage, Ndono, Uvuruma, na Sikizya.Msuya pia amesema, wanahitaji wawekezaji kwenye maeneo ya utoaji huduma vikiwemo vituo vya mafuta, benki, hoteli, masoko, vituo vya mabasi, sehemu za watu kupumzika.“Tunahamasisha watu wetu waje kuwekeza kwenye maeneo hayo kwa sababu huduma nyingi za msingi tunazipata Tabora manispaa kwa sasa” ameyasema hayo wakati anazungumza na timu kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) iliyopo mkoani Tabora kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zilizopo mkoani humo.Amesema, baadhi ya kata zimeshatenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji zikiwemo za Goweko, Sikizya, Ilolangulu, Kigwa, Miyenze, Loya na Bukumbi.“Mpaka sasa Halmashauri yetu haina hata kituo kimoja cha mafuta, haina maduka, haina hoteli kwa hiyo ni hitaji kubwa ambalo tunafikiri ni muhimu sana kwa ajli ya huduma kwa wananchi wetu” amesema Msuya.Amesema, wilaya hiyo pia ina maeneo kwa ajili ya uwekezaji wa ranchi za mifugo.“Wilaya mpaka sasa ina ng’ombe wapatao 441,090 lakini hakuna maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kuanzisha ranchi. Maeneo makubwa yametengwa kama hifadhi kwa hiyo tunafikiria tukiazisha ranchi inaweza kuwa ni msaada kwa wakulima kwa ajili ya kuongeza lakini pia kwa Halmashauri kama chanzo kimojwapi cha mapato ya Halmashauri” amesema.Amesema, Wilaya hiyo inahitaji uwekezaji kwenye machinjio ya kisasa.“Lakini pia tunahitaji uwekezaji kwenye kiwanda cha kusindika ngozi, tuna wafugaji wengi na ngozi nyingi huwa wafugaji wakishapeleka pale ng’ombe zikichinjwa na kuuzwa ngozi huwa zitupwa au zinazikwa kwa sababu hatuna utaalamu wa kuzichakata na kuzitengeneza ili ziweze kutengeneza bidhaa nyingine. Kwa hiyo tunahitaji kiwanda cha kuiongezea thamani ngozi na bidhaa za ngozi” amesema.Amesema, kuna maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya viwanda vidogo, vya kati na vikubwa, na kwamba, hamashauri ya Wilaya ya Tabora (Uyui) ipo kwenye mchakati wa kuyapima na kuyapatia hati. | Biashara | 1 |
Alisema mradi huo wa nyumba unajengwa katika eneo la Iyumbu, karibu na Chuo Kikuu cha Dodoma. Alisema hatua hiyo itapunguza uhaba wa nyumba za makazi na biashara katika manispaa ya Dodoma, kwa kuwa miradi mingine ya nyumba za biashara itajengwa katika eneo Meledeli.Akifafanua, Gambalagi alisema NHC itatekeleza miradi miwili ya nyumba za gharama nafuu katika Halmashauri za Chamwino na Bahi ambapo zaidi ya nyumba 50 za kuuza zitajengwa katika mwaka huu wa fedha.Alisema katika kutekeleza miradi hiyo NHC itajenga nyumba za kuuza kwa zile halmashauri zitakazoonesha zina mahitaji na utayari wa kulipia au kuwepo kwa soko la nyumba zitakazojengwa.Gambalagi alisema kwa nyumba za kupangisha, shirika linaendelea kuzifanyia matengenezo makubwa nyumba zake inazomiliki katika Manispaa ya Dodoma. Alisema hivi karibuni, shirika lilibadilisha madirisha ya kizamani na kuweka madirisha ya kisasa kwenye nyumba zake zilizopo eneo Mpwapwa ya zamani na zile zilizoko barabara ya Iringa.Alisema shirika pia limesaidia vijana kwa kila halmashauri ya wilaya, mkoani hapa mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana ili kuwapa ajira na kuwaondolea umasikini. | Biashara | 1 |
Rais John Magufuli amewakaribisha wananchi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) waje kununua bidhaa zinazozalishwa nchini ikiwemo saruji, sukari, mafuta, bidhaa za chuma, na vyakula yakiwemo mahindi.Rais Magufuli pia amewakaribisha wananchi wa DRC waje kuwekeza kwenye sekta ya viwanda, kilimo, uvuvi, utalii, madini nk.Amewakaribisha wananchi wa DRC kuja kuuza madini kwenye masoko ya madini nchini.'Kwa hiyo kila kitu, tunakaribishana na sisi wote ni ndugu, na kwamba, watu wa DRC waione Tanzania kama nchi yao, na Watanzania waione DRC kama nchi yao" amesema Rais Magufuli Ikulu, Dar es Salaam.Amesema Tanzania na DRC zimekubaliana kuondoa vikwazo vya biashara na uwekezaji ili wananchi katika nchi hizo watumie fursa zilizopo."Na katika kufanikisha hilo tumekubaliana kuzihimiza taasisi zetu za kifedha hususani benki kufungua matawi kwenye nchi zetu mbili ili kuwarahishia wananchi kupata huduma za kibiashara..."Hii ni opportunity (fursa) nyingine kwa wakuu wa mabenki mbalimbali. Nakumbuka CRDB wamefungua matawi mpaka Burundi, sasa ni wakati wa kufungua matawi mpaka DRC ili kusudi kufacilitate (kuwezesha) biashara itakayokuwa inafanyika kati ya wananchi wa nchi hizi mbili"amesema Rais Magufuli.Amesema, Tanzania imeamua kuongeza muda wa kutunza mizigo ya DRC katika bandari ya Dar es Salaam kutoka siku 24 hadi 30, imeondoa katazo la ufunguaji makontena na imefuta tozo ya kusindikiza mizigo inayokwenda nchini humo.Amesema, Tanzania na DRC zimekubaliana kubadilishana uzoefu wa kutumia rasilimali ili ziwanufaishe wananchi katika nchi hizo.Rais Magufuli pia amesema, Rais wa DRC, Felix Tshisekedi amekubali Tanzania ipeleke walimu wa Kiswahili nchini humo wakafundishe kwenye vyuo vikuu. | Biashara | 1 |
SERIKALI imepiga marufuku uchomaji matofali kwa njia ya tanuri kwa kutumia nishati ya kuni hasa katika maeneo ya mijini na badala yake imewataka wachomaji hao watumie pumba kama nishati mbadala.Onyo hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu wakati alipozungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Geita ikiwa ni ziara yake kwanza ya kikazi kwa mikoa ya kaskazini magharibi tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo. Kanyasu alisema uchomaji matofali kwa kutumia nishati ya kuni umekuwa ukichangia upotevu mkubwa wa misitu hali inayotishia sehemu kubwa ya nchi kuwa jangwa.Alifafanua kuwa matofali yachomwe kwa kutumia pumba za mazao badala ya kuni hali itakayosababisha kunusuru nchi kuwa jangwa huku akiagiza kamati hiyo ya mkoa huo kuanza kulisimamia agizo hilo mara moja.Alisema sehemu kubwa ya nchi kwa sasa uharibifu wa mazingira umeongezeka kutokana na ukataji miti ovyo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwemo uchomaji wa matofali kwa kutumia kuni.“Mimi sipo tayari kuona nchi inageuka kuwa jangwa, ni lazima nisimamie kwa kuanza katika maeneo ya mjini ikiwemo Geita ambapo unakutana na tanuri za kuchoma matofali kwa kutumia kuni, hili sikubaliani nalo,” alisisitiza.Alisema kwa mujibu wa takwimu, Tanzania imekuwa ikipoteza zaidi ya hekta 372,000 za misitu kila mwaka. Katika hatua nyingine, Kanyasu ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ihakikishe inasimamia ipasavyo mipaka mipya ya baadhi ya misitu ya hifadhi mkoani Geita ambayo imehaulishwa kwa kuhakikisha imetangazwa kwenye Gazeti la Serikali.Aidha, ameutaka uongozi wa mkoa huo kutii agizo lilitolewa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alilolitoa mwaka jana la kuhakikisha kila halmashauri inapanda miti milioni 1.5 kila mwaka, kwa kulitekeleza ipasavyo. | Kitaifa | 0 |
.Benki ya Afrika (BOA) Tawi la Tanzania, imeongezewa mtaji wa Shilingi Bilioni 22.9 na Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo, ili kuwawezesha Wateja wake kuendelea kupata huduma bora.Uamuzi wa bodi hiyo umefanyika katika kikao chake kilichofanyika mjini Madrid nchini Hispania, na kwamba pesa hizo zitaongeza nguvu katika mkakati wa benki hiyo wa kuwafikia Wajasiriamali wengi zaidi hapa nchini.Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo ya Afrika Tawi la Tanzania,- Joseph Iha amewaambia Waandishi wa habari jijini Dar es salaama kuwa, fedha hizo zinawaongezea uwezo wa kuwahudumia Wajasiriamali wengi zaidi ambapo mpaka sasa wameishawafikia Wajasiriamali Elfu Tisa ambao wamepewa mtaji wa zaidi ya Shilingi Bilioni 27.Ameongeza kuwa fedha zilizotolewa na Bodi pamoja na Wanahisa wa benki hiyo ya Afrika, zitasaidia kuboresha huduma za benki hiyo na kuwafikia Wajasiriamali wengi katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. | Biashara | 1 |
NAHODHA wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars na Klabu ya Aston Villa ya England, Mbwana Samatta amewaomba mashabiki Watanzania kuacha kutoa maneno ya kashfa au yenye malengo mabaya yanayoweza kusababisha mahusiano mabovu uwanjani na wachezaji wenzake.Samatta ametoa wito huo jana kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kufuatia mashabiki wengi Watanzania kuendelea kutoa maneno hayo kwa kuandika kwenye mitandao ya kijamii ya Villa kwa kuwatolea maneno makali baadhi ya wachezaji wakidai hawakumpa ushirikiano Samatta katika mechi alizocheza.Samatta alisema hafurahishwi na hali hiyo ingawa anafahamu mashabiki wanapenda afanye vizuri kwenye timu hiyo lakini anawaomba waache na kama wataendelea wanaweza kumtengenezea mazingira magumu na wachezaji wenzake.“Mashabiki wa soka Tanzania nafahamu kuwa mnanipenda kijana wenu na mnapenda nifanye vizuri katika timu yangu mpya, lakini nawaomba muache kutoa maneno ya kashfa au yenye malengo mabaya na timu na wachezaji, binafsi sifurahishwi nayo,” aliandika Samatta kwenye kurasa zake.Katika mtandao huo wa Villa mashabiki wengi Watanzania wanamlalamikia mchezaji, Jack Grealish ambaye ni kiungo mchezeshaji kwenye kikosi hicho baada ya kushindwa kuonesha ushirikiano kwa kumpasia pasi za mwisho kwenye mchezo uliopita dhidi ya Bournemouth FC ambao hata hivyo Villa walipoteza kwa mabao 2-1 huku Samatta akipachika bao la kufutia machozi.Samatta awali kabla ya mchezo huo, alishatoa kauli kwa Watanzania akiwataka kuwa na uvumilivu kwenye kipindi hiki kwani amejiunga na timu mpya amekutana na wachezaji wapya hivyo anahitaji muda wakutengeneza muunganiko na maelewano mapya na wenzake.Grealish ndiye mchezaji tegemeo kwa sasa ndani ya kikosi hicho amefunga mabao saba akiwazidi wengine na kutoa pasi tano zalizozaa mabao. | michezo | 2 |
Ahadi hiyo imetolewa na Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni hiyo, Peter Ngota. Alisema hayo alipokuwa akikabidhi zawadi za Mwaka mpya kwa vituo vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu jana jijini Dar es Salaam.TTCL ilitoa zawadi ya vyakula kwa vituo vya Kiwohede, Salvation Army na Msongola vyote vikiwa vya jijini Dar es Salaam.“Watanzania waendelee kutumia na kujiunga na huduma zetu kwa mwaka 2014,” alisema, na kuongeza kuwa wataimarisha na kuingia zaidi katika teknolojia mpya ili kukidhi mahitaji ya wateja.Alisema kampuni hiyo itaendelea kupanua huduma zake za simu za mkononi mijini na vijijini kama njia ya kutekeleza sera ya Serikali kufikisha huduma za mawasiliano kwa wananchi wote kwa maendeleo.Alisema mbali na teknolojia mpya, kampuni hiyo itaendelea kuunganisha wateja zaidi ndani na nje ya nchi katika Mkongo wa Taifa na ili kuyafanya mawasiliano kuwa ya haraka na uhakika zaidi.Kaimu Ofisa Mkuu Idara ya Fedha katika kampuni hiyo, Alinanuswe Mwakitalima mbali na kuwatakia mwaka mpya mwema watoto hao aliwataka kusoma kwa bidii ili waje kufanikiwa katika maisha yao ya baadaye Stella Mwambenja, ambaye ni ofisa kutoka kituo cha Kiwohede, ambacho ni miongoni mwa vituo vilivyopata zawadi, aliishukuru TTCL akisema kuwa zitawasaidia katika kuwatunza watoto katika kituo chao.Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Silvia Mulokozi, kutoka kituo cha Salvation Army alishukuru huku akiwataka watu na taasisi nyingine kuiga mfano wa kampuni hiyo ya mawasiliano.“Hatuna maneno ya kuonyesha furaha yetu…asanteni sana,” alisema. | Biashara | 1 |
Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Ocean Business Partners, Abdulsamad Abdulrahim wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu safari hiyo inayotarajiwa kufanyika Juni 8 mwaka huu.Alisema safari hiyo ambayo itakuwa ya siku tatu nchini humo, imeratibiwa kwa pamoja baina ya kampuni ya Ocean Business, Gallery Tours, chemba ya biashara ya Comoro na kampuni ya ndege ya ATCL ambayo imetoa punguzo kubwa la tiketi za kwenda na kurudi kwa ujumbe wa Tanzania.Alisema watakwenda kuwapa taarifa sahihi wafanyabiashara wa Comoro kuhusu fursa za kibiashara, zinazopatikana nchini ili wachukue uamuzi sahihi wa kuja kuwekeza nchini na kwamba wafanyabiashara wa Tanzania nao watapata fursa ya kupata taarifa sahihi kuhusu fursa za uwekezaji nchini Comoro.Alisema ujumbe huo wa watu 21, utajumuisha wafanyabiashara wakiwemo wanawake kutoka sekta mbalimbali kama mafuta, gesi, mawasiliano, uzalishaji, chakula, uchapishaji, wataalamu wa baharini, ulinzi, utalii na usafirishaji, waagizaji wa bidhaa teknlojia, hoteli, afya na sekta nyingenezo.Alitaja malengo mengine kuwa ni kuelezea maendeleo yaliyopo katika sekta mbalimbali kama njia ya kwenda kuwekeza kwa kutoa elimu ya kutosha kwa sekta ya umma na ya binafsi kuhusu uagizaji bidhaa toka nje, uuzaji bidhaa nje ya nchi zao na fursa nyinginezo za kibiashara.Alisema lengo la mpango huo ni kuwahamasisha watanzania wengi kwenda kufanya biashara nchini Comoro na wale wa nchini humo kuja kuwekeza Tanzania, kwa kuwapa wawekezaji watarajiwa taarifa sahihi kuhusu fursa za uwekezaji zilizoko hapa nchini na mazingira ya uwekezaji kwa ujumla.Alisema Tanzania ina uhusiano mzuri na visiwa vya Comoro na nchi hizi zimekuwa zikishirikiana katika nyanja mbalimbali za kibiashara, uchumi na kijamii. Nchi hizi zina fursa mbalimbali ambazo zinaweza kukuza na kuendeleza ushirikiano uliopo. | Biashara | 1 |
Akitoa mada kwenye mkutano unaohusu matumizi ya sayansi na teknolojia katika kukuza uchumi wa nchi jana jijini Dar es Salaam, Mhadhari wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Juma Kitima alisema vivutio hivyo vinaweza kuwa hasi au chanya.Alisema maji yanayotumika viwandani yakichujwa yanaweza kuhifadhiwa na yakatumiwa tena kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, uzalishaji wa umeme na matumizi mengine ya manufaa kwa maisha ya binadamu.Alisema miongoni mwa vivutio hivyo ni kuwasamehe ushuru wenye viwanda mara wanapoagiza mitambo hiyo ambayo alikiri kuwa gharama za ujenzi wa mitambo hiyo ni mkubwa.Alitoa mfano kuwa walifanya utafiti na wakashirikiana na kiwanda cha pombe kali cha Banana kilichoko mjini Arusha kujenga mtambo huo ambao uligharimu Sh milioni 800.Hata hivyo alisema mtambo huo ni bora zaidi na una faida kubwa kwa mwenye kiwanda na jamii inayokizunguka kiwanda hicho.Lakini pia alisema Serikali inaweza kutunga sheria kali zitakazowabana wenye viwanda na akasema kwa sasa wenye viwanda wanaendelea kuharibu mazingira kwa vile hakuna sheria inayowabana na hata kama ipo haiheshimiwi.Naye Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Dk Hassan Mshinda alisema mkutano huo ulikuwa unajadili mambo kadhaa kuhusu mradi ulionzishwa kati ya tume hiyo na Shirika la Maendeleo la Sweden kuona namna ambavyo sayansi inaweza kusaidia kukuza uchumi na utunzaji wa mazingira.Alisema mkutano huo pia ulikuwa na lengo la kuona namna ambavyo Serikali inaweza kushirikiana na sekta binafsi katika kufadhili tafiti mbalimbali kwa manufaa ya jamii na akatoa mfano kuwa utafiti wa Profesa Kitima kwenye kiwanda cha Banana ni mfano wa mashirikiano hayo.Naye Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha Banana Investiment cha mjini Arusha Adolf Olomi, alisema kabla ya kujenga mtambo huo, kulikuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuwa kiwanda hicho kilikuwa kinachafua mazingira, lakini kwa sasa mambo ni shwari.Alisema maji yanayotoka kiwandani yanachujwa tena na mtambo huo na wanayatumia kwa ajili ya umwagiliaji na wanaangalia namna ambavyo wanaweza kutumia maji hayo kuzalisha umeme utakaotumiwa na kiwanda hicho. | Biashara | 1 |
Alitoa mwito huo jana wakati akifungua semina ya siku tano juu ya mafunzo ya kuingia makubaliano na mikataba kwenye sekta ya madini kwa wanasheria wa sekta ya umma kutoka nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.Katika mkutano huo ulioanza jana jijini Dar es Salaam, Pinda alisema wanasheria wanapaswa kujali wananchi walio masikini kwa sababu wao hawana fursa ya kuingia kwenye vikao kama vyao na kutoa sauti juu ya kile wanachokitaka.“Licha ya umasi kini wao, wanaishi juu ya ardhi ambayo chini yake kuna utajiri tele wa madini na rasilimali nyingine. Ninawasihi sana muwafikirie watu hawa kabla ya kufanya uamuzi wowote,” alisisitiza.Alisema ili jambo hilo liweze kufanikiwa ni lazima, wanasheria kama wadau wa mwanzo kabisa, wakubali kukataa kupokea fedha chafu na vishawishi kutoka kwa wawekezaji na siku zote waweke uzalendo mbele kwa maslahi ya nchi zao.Alisema rasilimali za a Afrika hazijaleta maendeleo kwa wakazi wake kwa sababu wanaofaidika ni kampuni kubwa kutoka nje na watu wachache wenye nafasi huku walio wengi wakiambulia patupu.Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, ni theluthi moja ya mikataba ya uchimbaji madini inayofaidisha bara zima la Afrika ikilinganishwa na faida ambayo bara la Amerika Kusini inanufaika nalo.Ili kuepukana na hali hiyo, Waziri Mkuu alisema umefika wakati wa kukataa kutoa misamaha ya kodi kwa kampuni za kimataifa na kuhakikisha zinalipa kodi katika kila nchi husika ya Afrika Mashariki.Alisema umefika wakati wa kuhakikisha Serikali za nchi husika zinaweka sera madhubuti na miongozo ya kisheria itakayohakikisha mikataba inayoandaliwa kwa ajili ya utafutaji na uendelezaji wa madini na rasilimali zake inazinufaisha nchi kwanza.Akimkaribisha Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema sekta ya madini ni mojawapo ya sekta zinazokua kwa haraka nchini lakini inachangia chini ya asilimia moja ya ajira zote nchini. Washiriki wa mkutano huo ni kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Tanzania. | Biashara | 1 |
SERIKALI imenunua korosho ghafi za tani 214,269.684 zenye thamani ya Sh bilioni 717.1 sawa na asilimia 89.3 ya lengo la uzalishaji wa zao hilo.Takwimu hizo zilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba wakati akijibu swali la Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema). Mdee alitaka kujua hadi sasa ni kiasi gani kimetumika kununua korosho na fedha hizo zimetoka katika chanzo kipi na tani ngapi zimenunuliwa.Mgumba alisema kiasi hicho kimenunuliwa ni kwa makadirio ya uzalishaji ya korosho msimu wa mwaka 2018/19 ambacho ni zaidi ya tani 240,000 za korosho ghafi. Alisema ununuzi wa zao hilo unafanywa na taasisi ya serikali ambayo ni Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ambayo malipo yanaingizwa kwenye akaunti ya wakulima. Hadi Januari 30, mwaka huu, Sh bilioni 424.8 zimewekwa kutokana na mauzo ya korosho tani 134,535.4. Aidha, alisema Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ni taasisi ya kibiashara yenye lengo la kupata faida na mtaji wake unaotokana na ruzuku kutoka serikalini na mikopo kutoka taasisi za fedha kama Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), NMB na CRDB.Alisema jumla ya wakulima 390 wameshalipwa hadi kufikia Januari 30 mwaka huu. Aidha, vyama vya msingi 603 vimelipwa kati ya vyama vya msingi 605 vilivyohakikiwa. Alisema Operesheni Korosho inatarajia kukamilika Februari 15, mwaka huu. Akiuliza swali la nyongeza, Mbunge wa Ndanda, Cecily Mwambe (Chadema) alihoji kwa nini serikali iliahidi kununua korosho kwa Sh 3,300 lakini inalipa kwa Sh 2,600. Mgumba alisema ni kweli Rais John Magufuli aliutangazia umma kwamba korosho itanunuliwa kwa bei hiyo na kinachofanyika ni kwamba wakulima wanalipwa bei hiyo, isipokuwa kwa korosho daraja la kwanza. “Korosho daraja la pili wanalipwa asilimia 80 ya bei hiyo, ambayo ni sawa na Sh 2,640 na korosho za daraja la chini wanarudishiwa wakulima, kwani serikali haiwezi kulipa vigae na mawe badala ya korosho,” alisema. | Kitaifa | 0 |
WAKATA miwa wa Morogoro Mtibwa Sugar wameahidi ushindi leo dhidi ya KCCA ya Uganda katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi.Mchezo huo huenda ukawa mgumu hasa kwa Mtibwa ambao walipoteza mchezo wa kwanza ugenini kwa kufungwa mabao 3-0. Ili kusonga mbele katika hatua inayofuata Mtibwa inahitaji ushindi kuanzia mabao 4-0. Iwapo itapata sare au kufungwa basi itakuwa imejitoa moja kwa moja kwenye michuano hiyo. Kocha wa Mtibwa Sugar Zuberi Katwila alisema wana kazi kubwa ya kupambana kuhakikisha wanapata ushindi. “Tunajua kazi iliyopo mbele yetu sio rahisi, tumejipanga vizuri kusawazisha makosa yetu kwa kuhakikisha tunapambana kugeuza matokeo,”alisema.Alisema wachezaji wake wanapaswa kujitambua kwa kufanya kazi wanayoelekezwa. Mtibwa inawategemea nyota wake muhimu kama Jaffary Kibaya, Haruna Chanongo waliofunga mabao manne, katika mchezo wa hatua ya awali dhidi ya Northen Dyanamo ya Shelisheli. Lakini wakata miwa hao wanahitaji kuingia kwa tahadhari kubwa dhidi ya wapinzani wao, kwani wana uzoefu wa kutosha na michuano ya kimataifa. KCCA ni miongoni mwa timu zinazofanya vizuri Afrika na msimu uliopita walicheza hatua ya makundi. Yeyote atakuwa na nafasi kubwa ya kupata matokeo kulingana na maandalizi ya kila mmoja. | michezo | 2 |
ALIYEKUWA mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti katika uchaguzi wa Yanga, Yono Kevela na washirika wake wametoa Sh milioni 20 kwa uongozi wa klabu hiyo kwa ajili ya maandalizi ya mechi zilizosalia za Ligi Kuu.Yanga imekuwa kwenye wakati mgumu tangu kuondoka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wake, Yusuf Manji zaidi ya miaka miwili iliyopita, hali inayofanya ijiendeshe kwa michango.Kevela alikabidhi fedha hizo kwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Wilfred Mwakalebela Dar es Salaam jana. Akikabidhi fedha hizo Kevela alisema amevunja makundi yote na kuamua kusaidia timu yake, hivyo ametoa fedha hizo zisaidie katika mechi zilizosalia za Ligi Kuu.“Natoa mwito pia kwa wenzangu wengine waliokuwa wanagombea nafasi mbalimbali, tuvunje makundi tuwe kitu kimoja tuisaidie timu yetu,” alisema. Akipokea fedha hizo, Makamu Mwenyekiti Mwakalebela alimshukuru Kevela na wahisani wake na kusema kuwa fedha hizo zitatumika ilivyokusudiwa. | michezo | 2 |
SHULE ya Tusiime ya Tabata jijini Dar es Salam imeongoza kwa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kutoa wanafunzi wengi katika 10 bora kwa wasichana na wavulana na kupeleka wanafunzi wengi shule za vipaji maalumu.Hayo yalibainika jana wakati wa mchakato wa kuwapangia shule wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba ambao matokeo yake yalitangazwa Novemba mwaka huu na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA). Kwenye matokeo hayo, shule hiyo imetoa wanafunzi saba kwenye 10 bora kwa upande wa wasichana Mkoa wa Dar es Salaam na wanafunzi watano katika 10 bora kwa upande wa wavulana.“Mkoa wa Dar es Salaam umekuwa wa kwanza kitaifa na Tusiime kwenye wanafunzi 20 bora kwa upande wa wasichana na wavulana jumla ya inawanafunzi 12 hivyo ni dhahiri kwamba imesaidia sana kufanikisha ushindi huo wa Mkoa wa Dar es Salaam kitaifa na Wilaya ya Ilala,” alisema Mwalimu wa Taaluma, Makson Binomtonzi. Alisema shule ya Tusiime ilikuwa na watahiniwa 240 ambayo ni idadi kubwa kuliko shule zote na wote walipata alama A kwenye matokeo yaliyotangazwa hivi karibuni na Necta.“Vile vile shule hii imeongoza Mkoa wa Dar kwa kutoa wanafunzi wengi waliochaguliwa kujiunga na shule za vipaji maalumu nchini si jambo la bahati hili limewezekana kutokana na maandalizi ambayo huwa tunawapa wanafunzi wetu kwa kuwapa programu maalum ya masomo ya ziada,” alisema Binomtonzi. Alisema katika nafasi 28 zilizotengwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam kwa wanafunzi na kwenda kwenye shule za vipaji maalumu, Tusiime imepeleka wanafunzi 16 kwenye shule hizo za vipaji maalumu na kati ya hao, watano ni wasichana na 11 ni wavulana. | Kitaifa | 0 |
Kamati hiyo ilibainisha kuwa moja ya mapungufu ya mkataba huo ni pamoja na msamaha wa kodi usioeleweka, uliotolewa kwa kampuni inayotengeneza leseni hizo ya M/s Tracking Inovations LTD.Akiwasilisha taarifa ya mwaka ya kamati hiyo bungeni Dodoma juzi, Mwenyekiti wa PAC, Kabwe Zitto, alisema pia kamati hiyo imebaini kuwa mfumo mzima wa kusimamia na kufuatilia matumizi sahihi ya leseni, hautumiki kikamilifu hasa katika uwekaji wa kumbukumbu za makosa ya barabarani.“Mheshimiwa Spika askari wa barabarani huweka kumbukumbu za makosa ya barabarani kwa kutumia makaratasi badala ya kuweka kumbukumbu hizo kielektroniki,” alisema Zitto.Alisema katika eneo la msamaha wa kodi uliotolewa kwa kampuni hiyo ya M/s, haueleweki, kwa sababu kipengele cha 14 cha mkataba huo kinamruhusu kufidia kodi anayotakiwa kulipa, wakati huo huo kwenye kipengele kinachoelezea wigo wa kazi kinabainisha kuwa bidhaa zote zitakazoingizwa na kampuni hiyo nchini kwa kwa jili ya mradi wa leseni zitakuwa na msamaha wa kodi.“Vipengele vinavyokinzana kama hivi katika mkataba vinaweza kurahisisha ukwepaji wa kulipa kodi na kuikosesha Serikali mapato, ambao pia huweza kutumiwa kwa ajili ya kuongeza muda wa mkataba,” alisisitiza.Alisema Kamati yake inaitaka TRA ihakikishe inapitia upya mkataba huo na vipengele vyenye mapungufu ili virekebishwe.Aidha, aliitaka TRA na Jeshi la Polisi nchini kuhakikisha mfumo wa leseni za udereva unatumika kwa asilimia 100 ili kukuza mapato ya Serikali.“Kwa lengo la kuangalia tija iliyopatikana kutokana na utekelezaji wa mkataba huo, Kamati imemuomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya ukaguzi maalum na kuwasilisha taarifa yake kwenye Kamati,” alisema.Aidha, alisema kamati hiyo ya PAC inapendekeza kuwa mikataba itakayohusisha utoaji wa misamaha ya kodi iwe inapitiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kabla ya kusainiwa. | Biashara | 1 |
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alibainisha hayo jana baada ya kikao chake na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria ,Youcef Yousfi na wataalamu wa wizara hizo mbili.Alisema hatua hizo ni kati ya miradi mingi ya ushirikiano katika sekta hizo, ambapo ujenzi wao ukikamilika utapunguza gharama kwa asilimia 45 au nusu ya gharama ya sasa.Profesa Muhongo alisema Algeria ina uzoefu katika kusindika gesi asilia ambapo kwa mwaka jana pekee ilisambaza gesi hiyo tani milioni 115 mijini na vijijini nchini humo.Alisema wamekubaliana na wataalamu kuwa ifikapo Juni 30 kwenye mkutano wa kuandaa miradi hiyo utakaofanyika Algeria, wataalamu wapeleke namna ya utekelezaji wa miradi hiyo.“Wataalamu watueleze eneo wanalopendekeza kujenga kiwanda, gharama za ujenzi, masoko ya gesi pamoja na teknolojia itakayotumika ili kufahamu gharama za uwekezaji huo,” alisema Muhongo.Alisema kutokana na kiwanda hicho, Watanzania wataachana na matumizi ya mkaa na kuni, jambo litakalosaidia uhifadhi wa mazingira.Alisema kampuni za nchi hizo zinazohusika na masuala ya gesi zitahusika katika kujengwa kwa mitambo hiyo na uendeshaji wao.Akizungumzia usambazaji umeme alisema kampuni hizo mbili zitashirikiana kusambaza umeme mijini na vijijini na kisha kushirikiana katika ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha umeme masafa marefu.Profesa Muhongo alisema pia Algeria ina utaalamu na uzoefu mkubwa katika madini, na hivyo itaanzisha migodi ya Fosiforasi kutengeneza mbolea na kuuzwa ndani na nje ya nchi.Alisema nchini kuna aina nyingi ya madini hayo, lakini hakuna utaalamu wa kuyatumia ambapo kwa sasa inatengenezwa mbolea ya aina moja ya Minjingu. Alisema pia nchi hizo mbili zimekubaliana kushirikiana katika utunzaji wa takwimu na taarifa.Waziri Muhongo alisema ili kusaidia Watanzania kuwa na wataalamu wake, Algeria inatoa ufadhili wa mafuta na gesi kwa vijana na kwa kuanzia, mwaka jana walikwenda vijana 50, mwaka huu 60.Waziri Yousfi alisema ushirikiano huo wa kiuchumi hautaishia katika miradi hiyo pekee bali itakuwa na wigo mpana zaidi.Alisema katika nchi yake yenye wananchi milioni 38 asilimia 98 wanapata umeme majumbani huku idadi kubwa ikitumia gesi kupikia.Alisema nchi yake imevutiwa kushirikiana na Tanzania katika uwekezaji kutokana na ushirikiano wa kisiasa uliopo kwa miaka mingi baina ya nchi hizo mbili, kuwapo rasilimali nyingi na utulivu wa kisiasa.Alisema nchi yake inatarajia kufaidika na uzoefu wa masuala ya madini ambayo Tanzania inayo huku zikibadilishana uzoefu katika masuala ya kiuchumi. | Biashara | 1 |
Timu hiyo ya Ligi Kuu iliongoza baada ya bao la Willian katika dakika ya 62 na ilionekana kuibuka na ushindi. Kross ya Christensen ndani ya eneo la hatari liliiadhibu Chelsea baada ya Lionel Messi kuunasa mpira na kuifungia Barca bao la kusawazisha ugenini.Alipoulizwa kuhusu bao hilo, bosi huyo wa Chelsea, Conte alisema: "Nadhani kiwango cha Christensen kilikuwa kizuri, tunazungumzia mchezaji ambaye ndio kwanza ana umri wa miaka 21 hapa”."Inafurahisha kwamba alikuwa tayari kucheza mechi hii akiwa amepevuka kiakili, nina furaha sana, alikuwa miongoni mwa wachezaji bora usiku huu (juzi)."Ni ngumu kuchagua mchezaji mmoja au mwingine lakini nadhani Christensen alicheza mechi hii kwa kiwango kikubwa, nimefurahishwa na kiwango chake”.Wakati Barcelona ikitawala mchezo, Chelsea ndio iliyotengeneza nafasi nzuri, ambapo mashuti ya Willian yaligonga mwamba mara mbili katika kipindi cha kwanza na Eden Hazard alishindwa kufunga baada ya kushindwa kujiweka pazuri."Nadhani tulikuwa karibu kwenye kucheza mchezo sahihi,” alisema Conte."Nadhani tumeadhibiwa na kosa moja, lakini kama mnavyojua kucheza dhidi ya aina hii ya wachezaji Messi, kama [Andres] Iniesta, [Luis] Suarez, kama utafanya kocha litakugharimu”."Unapocheza dhidi ya Barcelona, tunajua kwamba kama unataka kucheza dhidi yao hatua kwa hatua, mnachanganyikiwa, unapoteza mechi sio kwa 1-0 au 2-0 lakini kama kilichotekea Hispania 4-0, 5-0 au 6-0. | michezo | 2 |
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amewataka wakazi mkoani hapa kuitumia kwa manufaa ziara ya Rais John Magufuli ili kuuwezesha mkoa kunufaika nayo.Akizungumza na waandishi wa habari juu ya ziara ya Rais, Chalamila alisema ni wakati kwa wakazi wa mkoani hapa kujitokeza kwa wingi katika maeneo atakayopita Rais Magufuli huku pia akihadharisha watu kutotumia fursa hiyo kuonesha mabango yenye maneno ya uchonganishi yanayoweza kuvuruga amani ya mkoa.Alisema serikali mkoani hapa haijakataza kuonesha mabango ya kero za wananchi kwa Rais, lakini ni muhimu ujumbe wa kwenye mabango ubebe ukweli wenye lengo la kuujenga mkoa na si uchonganishi.“Hatujakataza mabango hata kidogo, tunachosisitiza sisi ni watu waje na mabango yenye hoja za kweli. Wananchi wa Mbeya waitumie ziara ya Rais kuufanya Mkoa uneemeke kwa matunda mazuri baada ya ujio wake na si kuibua vilio baada ya ziara hiyo. “Niwasihi pia wananchi tushikamane kwa pamoja katika ziara hii tangu Rais atakapowasili mkoani kwetu.Tujitokeze kwa wingi kila atakakopita na pia kule atakakofanya mikutano pamoja na shughuli nyingine zilizopangwa,” alisisitiza Chalamila. Akizungumzia ratiba ya ziara ya Rais Magufuli ambaye aliwasili jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, Chalamila alisema leo, pamoja na mambo mengine, Rais atafanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya CCM maarufu kama Rwanda Nzovwe jijini hapa.Alisema kesho ataendelea na ziara katika Wilaya ya Rungwe na Kyela ambapo atasalimiana na wananchi katika miji ya Kiwira, Tukuyu na kufungua Kiwanda cha Maparachichi, kuweka mawe ya msingi katika majengo mbalimbali mapya ikiwemo mabweni katika Chuo cha Ualimu Mpuguso wilayani Rungwe na kisha atakwenda wilayani Kyela ambako atazindua barabara ya Lami ya Kikusya-Matema na kufanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya John Mwakangale wilayani humo.Alisema keshokutwa, Rais Magufuli atakuwa katika Viwanja vya Sokoine jijini hapa katika ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Mbeya, Julius Nyaisonga ambapo alitoa wito kwa watakaohudhuria sherehe hizo kuingia uwanjani kabla ya saa nne asubuhi na kwamba kila atakayeingia uwanjani humo atakaguliwa kwa ajili ya usalama. | Kitaifa | 0 |
KOCHA Mkuu wa Azam FC, Ettiene Ndayiragije amesema wako tayari kuwakabili Simba katika mchezo wa ngao ya jamii mwishoni mwa wiki hii akiamini utakuwa wenye ushindani kwa sababu timu zote zinawakilisha kimataifa. Azam FC tayari imewasili Dar es Salaam ikitokea Ethiopia ilipopoteza kwa bao 1-0 mchezo wa awali wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Fasil Kenema ya huko. Akizungumzia mchezo huo katika taarifa yake iliyotumwa na msemaji wao, Jaffar Maganga, Ndayiragije alisema wanahitaji kucheza kwa nidhamu kubwa kutokana na kuwa na jukumu kubwa la kujipanga na mchezo wa marudiano dhidi ya Waethiopia. “Mchezo wetu dhidi ya Simba ni mchezo mzuri kwa sababu timu zote zinawakilisha nchi, kutakuwa na ushindani wa hali ya juu, tunahitaji kuwa na nidhamu hasa ikitegemewa kuwa kuna mchezo wa kimataifa mbele yetu,”alisema. Ndayiragije alisema anakiamini kikosi chake kitafanya vizuri katika mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi na kuwahimiza mashabiki wajitokeze kwa wingi kupata burudani nzuri. Simba inawakilisha nchi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na ilicheza mechi yake ya kwanza ugenini dhidi ya UD Song ya Msumbiji na kutoka nayo suluhu ambapo mchezo wa marudiano ni Agosti 25. Akizungumzia kikosi chake, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu alisema wachezaji wake walifanya mazoezi jana asubuhi na jioni walitarajiwa kuingia kambini Mbweni. Mara ya mwisho Simba na Azam zilikutana kwenye Ligi Kuu msimu uliopita ambapo mechi ya kwanza Simba ilishinda mabao 3-1 na mechi ya pili zilitoka suluhu. Mechi ya ngao ya jamii msimu uliopita Simba ilicheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1. | michezo | 2 |
Jafo ameyasema hayo leo katika kata ya Kiluvya iliyoko wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, katika ziara ya kukabidhi vifaa vya kufanyia kazi kwa wanufaika wa mradi wa kuwezesha vijana kiuchumi (YEE).Kata nyingine ambazo wanufaika walikabidhiwa vifaa ni pamoja na Malumbo na Kurui.Mradi wa YEE ulioanza mwaka 2015 hadi 2018, umedhaminiwa na Jumuiya ya Ulaya (EU) na kuendeshwa na Shirika la Plan International Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na unatekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara.Kuhusu viwanda, Jafo alisema ametoa agizo kwa kila mkoa kuhakikisha unaunda viwanda 100 vinavyoanzia na mtaji wa Sh milioni 2.5 hadi 10 ili viweze kutoa fursa kubwa ya ajira kwa vijana na jamii kwa ujumla.Ametoa mfano kuwa wanufaika wa mradi huo kuwa wapo mafundi cherehani, mafundi wa kuchomelea, wapishi na wapambaji na hata mafundi umeme ambao kwa pamoja wakitumia vizuri taaluma zao wanaweza kufikia mbali na kupunguza wimbi la vijana wanaokabiliwa na tatizo la ajira.Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja mradi wa YEE, Simon Ndembeka alisema kwa wilaya ya Kisarawe mradi huo umetekelezwa katika kata tano, tayari vikundi 37 viliundwa na sasa wanakabidhiwa vifaa vya kuanzia kazi kulingana na fani walizosomea. | Biashara | 1 |
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewaaga watalii 1,000 waliokuja nchini kutoka Israel na kuwataka wakawe mabalozi wazuri wa Tanzania nchini mwao.Mwito huo ulitolewa jana mkoani hapa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) wakati akiaga kundi la kwanza la watalii 274 ambao ni kati ya watalii 1,000 waliowasili nchini Aprili 20 mwaka huu kutembelea maeneo ya vivutio kwenye Ukanda wa Kaskazini.Watalii hao wameondoka kwa nyakati tofauti na kwa makundi tofauti kuanzia juzi usiku hadi jana usiku.Waziri Mkuu aliwaomba watalii hao wapange muda wao na watafute fursa nyingine ya kuja Tanzania kutembelea mbuga nyingine za ukanda wa Kusini pamoja fukwe nzuri za Zanzibar.“Tumefarijika sana na ujio wenu na tunaamini mtaenda kutangaza mazuri mliyoyaona kwa wengine. Tunazo mbuga nyingine za Rubondo, Katavi, Ngorongoro, Ruaha, Selous, fukwe nzuri za Zanzibar na mlima Kilimanjaro,” alisema Waziri Majaliwa.Pia amewashukuru mawakala wa utalii nchini na Mkurugenzi wa kampuni Wakala wa Utalii ya Another World kutoka Israel, Carmel Shlomo kwa kuamua kuitangaza Tanzania kama kivutio namba moja cha utalii barani Afrika.Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla aliwashukuru watalii hao kwa kuamua kuitembelea Tanzania licha ya kuwa wangeweza kwenda maeneo mengine yaliyo jirani na Israel.Pia alizishukuru kampuni za utalii za Tanzania na Israeli kwa kushirikiana kuleta watalii wengi kiasi hicho. Alizitaja kampuni hizo kuwa ni Excellent Guides, Mauly Tours and Safaris, Matembezi, Leopard Tours and Safaris, African Queen Adventures na TAWISA zote za kutoka Tanzania.Kamuni za kutoka Israeli ni Another World, My Trip, Camel na Kampuni ya Safari. Kwa upande wao, baadhi ya watalii kutoka Israel walisema wamevutiwa na waliyoyaona hapa nchini na wameahidi kurudi tena ili watembelee vivutio vingine zaidi.Naomi Peer Moscovich na mabinti zake, Dana na Lihi walisema wamevutiwa na wingi wa wanyama waliowaona lakini pia wameguswa na ukarimu wa watu waliokutana nao.“Tunaondoka na neno moja kubwa nalo ni kwamba hatutaisahau Tanzania (we say Unforgettable Tanzania) na tutarudi tena hivi karibuni,” alisema Dana Peer Moscovich ambaye ni dada yake Lihi. | Biashara | 1 |
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa tahadhari ya kimbunga kilichopewa jina la Kenneth kutokea katika Bahari ya Hindi.Kimbunga hicho kitaathiri huduma baharini kwa asilimia 100 na athari nchi kavu, huku kikisababisha ongezeko la mvua nchini na upepo mkali.Aidha, kimbunga hicho ambacho mpaka jana asubuhi kilikuwa kilometa 600 kutoka Pwani ya Tanzania na Msumbiji, kimekuwa kikiendelea kusogea maeneo ya Pwani ya nchi, huku kikiwa na upepo wa kasi ya kilometa 100 kwa saa.Kimbunga hicho kitaathiri maeneo mbalimbali karibu na Bahari ya Hindi hasa mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma na maeneo mengine ya karibu na mikoa hiyo kwa umbali wa kilometa 500.Akitoa tahadhari hiyo jana Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Pascal Waniha (pichani) alisema inaonesha mpaka kufikia leo, kimbunga hicho kitakuwa kilometa 200 toka mpaka wa Msumbiji na Tanzania, kikiwa na upepo wa kasi ya kilometa 100 kwa saa na kuendelea kusogea mpaka Ijumaa.Kwa mujibu wa mifumo ya hali ya hewa, inaelezwa kuwa jana kimbunga hicho kilisogea zaidi kwa kilometa 450 na kufikia usiku wa kuamkia leo kitafika kilometa 250 na kufikia kilometa 150 na upepo wa kasi ya kilometa 150 kwa saa.Dk Waniha ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi TMA, alisema katika saa 24 zilizopita, mgandamizo mdogo wa hewa uliendelea kuimarika kwa kasi hadi kufikia kiwango cha kimbunga kamili na kuwa umbali wa kilometa 700 mashariki mwa Mkoa wa Mtwara.“Mifumo ya hali ya hewa inaonesha kimbunga cha Kenneth kilichopo eneo la Kaskazini Magharibi mwa Kisiwa cha Madagascar kinaambatana na mvua kubwa na upepo mkali katika eneo hilo,” alisema na kubainisha kuwa vipindi vya upepo mkali unaofikia zaidi ya kasi ya kilometa 80 kwa saa, vinatarajiwa kujitokeza katika Ukanda wa Pwani ya Kusini katika mikoa ya Lindi na Mtwara na iliyo karibu.“Kimbunga hiki kitaendelea kutawala mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa nchini hivyo kusababisha ongezeko la mvua zinazoambatana na ngurumo za radi pamoja na upepo mkali kadri kinavyokaribia maeneo ya ukanda wa Pwani,” alisema mkurugenzi huyo wa TMA.Alisema kimbunga hicho kitakapoingia nchi kavu kikiwa na nguvu inayotarajiwa, kitakuwa na madhara makubwa kwa maisha ya watu na mali zao, ambayo ni mafuriko, uharibifu wa mali na makazi, kuezuliwa mapaa kutokana na upepo mkali, uharibifu wa mazao shambani na miundombinu kutokana na mafuriko na upepo mkali.Madhara mengine ni kuongezeka kwa kina cha maji ya bahari katika kipindi kifupi, kuathirika kwa shughuli za usafirishaji kwa anga, kwenye maji na nchi kavu mkoani Mtwara na maeneo jirani ya umbali wa kilometa 500.“TMA inaendelea kufuatilia mwenendo wa kujengeka kwa kimbunga hicho kusini magharibi mwa Bahari ya Hindi pamoja na mwenendo wa mifumo mingine ya hali ya hewa kwa ujumla na kutoa mrejesho kila inapobidi ili kuchukua tahadhari zaidi,” alisema Dk Waniha.Alisema kama hiyo iliwahi kutokea mwaka 1952 katika Mkoa wa Lindi, lakini mpaka kinafika hakikuwa na madhara makubwa. Mwezi uliopita, Kimbunga Idai kilizikumba nchi za kusini mwa Afrika za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe na kusababisha vifo vya watu wapatao 1,000. Serikali ya Tanzania ilituma msaada wa chakula, dawa na vifaa tiba kusaidia watu walioathiriwa na kimbunga hicho.Mkoani Mtwara, Mwandishi Wetu, Sijawa Omary anaripoti kuwa Meneja wa Kanda ya Kusini wa TMA, Daudi Amasi amewataka wakazi waishio mabondeni mkoani humo kuchukua tahadhari juu ya tukio hilo.Alisema kimbunga hicho kitakuwa na upepo mkali, mvua kubwa itakayoambatana na radi, kuchafuka kwa bahari, mawimbi ya bahari na bahari inaweza kujaa hali ambayo inaweza kuathiri wananchi wanaoishi kando ya bahari.Akizungumza na waandishi wa habari jana, Amasi alisema tahadhari kubwa inapaswa ichukuliwe kwa wakazi wa mabondeni kuhama huku maeneo yenye mifereji yakisafishwa na kuondolewa takataka ili kuruhusu maji kupita kwa urahisi.Alisema tukio hilo litaanza saa tatu hadi saa tano asubuhi, na saa tano hadi saa sita, mvua itaongezeka na saa sita mvua itazidi mpaka saa tisa alasiri ambako mvua zitaanza kupungua na kisha kuondoka kuelekea nchini Msumbiji.Alisema mamlaka hiyo inaendelea kufuatilia ili kuona kama kinaweza kuongezeka nguvu na kuleta madhara makubwa kwa wakazi wa mabondeni ikiwemo kuezuliwa nyumba zao kutokaka na upepo mkali.Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa alisema wataalamu wameona ujio wa kimbunga Kenneth kikiwa na uelekeo wa Mkoa wa Mtwara ambacho kinaweza kuleta madhara makubwa.“Ni vizuri kuchukua tahadhari mapema kuliko kuchukua hatua za kuokoa wakati hatujui nini kitakachotokea..... watalaamu wanasema kuwa kimbunga hiki kina uelekeo wa Mtwara na kitakuja na mvua, upepo, radi,” alisema. | Kitaifa | 0 |
BAADA ya ya kuondolewa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, mshambuliaji tegemeo wa Yanga, Mkongomani, Heritier Makambo amewatuliza mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia watulie, sasa makali yao watayatoa katika Ligi Kuu Tanzania Bara.Kauli hiyo aliitoa baada ya timu hiyo kutua nchini ikitokea Rwanda, ambako ilifungwa bao 1-0 katika mchezo wa kukamilisha ratiba kwa Yanga katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Afrika.Kipigo hicho kiliisaidia Rayon kutinga hatua ya robo fainali ya mashindano hayo na kuipiku Gor Mahia ya Kenya, ambayo kabla ya mchezo wake wa mwisho dhidi ya wawakilishi wa Tunisia, ilikuwa katika nafasi ya pili katika kundi lao.Katika mchezo huo, Makambo alitoka katika dakika ya 69 na nafasi yake kuchukuliwa na Yusuph Mhilu baada ya kupata majeraha katika mchezo huo uliojaa upinzani mkubwa.“Tunajua mashabiki wetu wanataka ushindi katika kila mechi, hivyo hilo tunalifanyia kazi kuhakikisha tunawapa furaha ili waendelee kutusapoti katika ligi, ambayo tumepanga kufanya vizuri msimu huu,” alisema Makambo.Aidha, Kocha Mkuu wa Yanga, Zahera Mwinyi alisema majeraha ya Makambo hayana madhara makubwa, hivyo wanatarajia kuendelea kumchezesha katikamechi zijazo za Ligi Kuu.“Aliumia kwa sababu ya uwanja haukuwa mzuri kutokana na mvua, ambayo ilianza kunyesha tangu tunaanza mechi, ataendelea na mazoezi ambayo nimemuachia programu Kocha Noel Mwandila ambaye yeye ndiye atawasimamia wachezaji wote kwa kipindi hiki, ambacho mimi sitakuwa na timu,” alisema Zahera ambaye ameenda kwao DR Congo kwa majukumu ya timu yao ya taifa.Yanga imemaliza mashindano hayo ikiwa na pointi nne baada ya kushinda mechi moja na kutoka sare moja, huku ikifungwa mechi zingine nne katika kundi lake. | michezo | 2 |
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Adolf Mkenda amebainisha kuwa wizara yake imeingia mkataba na Kampuni ya Suma JKT kwa ajili ya ujenzi wa ofi si za wizara hiyo katika mji wa kiserikali Ihumwa nje kidogo ya Jiji la Dodoma.Mkanda aliyabainisha hao alipozungumza na waandishi wa habari jijini hapa wakati wa kutia saini mkataba huo. Alisema kwa mujibu wa mkataba ulioingiwa pande hizo mbili, Suma JKT wanatarajia kukamilisha ujenzi wa ofisi hiyo ndani ya mwezi mmoja ili wizara hiyo kuhamia rasmi katika ofisi hizo mpya.“Tumeshaingia makubaliano na wenzetu wa Suma JKT ambao ndio watatujengea ofisi zetu, na mkataba unawataka kukamilisha kazi hiyo ndani ya mwezi mmoja ili sisi tuweze kuingia kwenye ofisi hizo mpya,” alisema.Profesa Mkenda alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa agizo la Rais kutaka Dodoma kuwa makao makuu na wizara zote kuhamia jijini hapa wizara imeingia mkataba wa muda mfupi na SUMA JKT ili kukamilisha majengo ya ofisi.Aidha, alisema kuwa kwa kipindi ambacho watumishi wa serikali kupitia wizara hiyo ambao wamehamia Dodoma kwa sasa wanafanya kazi katika ofisi ambazo zipo barabara ya polisi na wengine wakiwa katika majengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).“Pamoja na kuwa kwa sasa tunafanya kazi bila kuwa na majengo ya kutosha lakini kazi zinafanyika vizuri na kwa ushirikiano mzuri huku tukiwa tunasubiria kupata ofisi ya uhakika ambayo itajengwa na Suma JKT katika mji wa kiserikali Ihumwa jijini hapa.Aliongeza: “Ninaamini kuwa iwapo tutakaa katika jengo moja la ofisi na watumishi kufanya kazi kwa pamoja tutafanikiwa kufanya kazi kwa ushirikiano mzuri zaidi na wenye tija kwa manufaa ya taifa na jamii kwa ujumla.”Aidha, Profesa Mkenda alisema kuwa mkataba huo wa muda mfupi ni ujenzi wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa jengo la awali. “Mkataba huu wa muda mfupi imelenga kukamilisha awamu ya kwanza ya mradi wa ujenzi wa ofisi ambapo litajengwa jengo kwa ajili ya ofisi na baadaye awamu ya pili ya ujenzi jengo kubwa la ghorofa ambalo wakurugenzi wote na viongozi watahamia hapo.” Hivi karibuni serikali imetoa takribani Sh bilioni 1 kwa kila wizara ili kuhakikisha inajenga jengo la wizara katika mji wa serikali uliopo Ihumwa nje kidogo ya jiji la Dodoma. | Kitaifa | 0 |
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa anatamani wilaya hiyo iwe kitovu cha utalii nchini Tanzania.Amesema, Bagamoyo ina vivuto vingi vya utalii vinavyohitaji uwekezaji mkubwa zikiwemo hoteli.“Yaani hiyo ndiyo ndoto yangu. Ndoto yangu kubwa sana ipo kwenye kuifanya Bagamoyo kuwa kitivo cha utalii”amesema ofisini kwake mjini Bagamoyo.Amesema fukwe za Bagamoyo bado hazijawekezwa kikamilifu, na kwamba, maeneo ya kihistoria wilayani humo ni fursa nzuri kwa uwekezaji.Zainabu ameyasema hayo wakati akizungumza na timu ya wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maonesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani 2019 na kongamano hilo.“Maeneo ambayo naweza kusema hayajaguswa kikamilifu ni kwenye maeneo ya fukwe ambako tunaweza tukawa na hoteli za kitalii kwa sababu kwa ujumla Bagamoyo ina vivutio vingi sana vya kitalii ambavyo vinahitaji uwekezaji mkubwa” amesema.Zainabu amesema fursa ya utalii kwenye fukwe za Bagamoyo inahitaji uwepo wa hoteli na kwamba hata kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadani hakuna hoteli za kutosha.“Lakini pia fukwe zetu za bahari bai hazijaendelezwa, zinahitaji kuendelezwa. Lakini pia kwenye sekta ya uvuvi na kwenyewe pia, uchumi wa Bagamoyo unategemea sana uvuvi”amesema. Amesema Serikali imetoa shilingi bil 1.6/- kwa ajili ya ujenzi wa soko la kisasa la samaki hivyo kuna fursa ya kuwekeza kwa kujenga kiwanda cha samaki.“Kwa hiyo nawakaribisha wawekezaji wanaopenda kuja kuwekeza Bagamoyo, ardhi bado tunayo nzuri kabisa yenye rutuba katika maeneo mbalimbali. Tunavyo viwanda zaidi ya sitini vikubwa, vidogo na vya kati. Na vile vidogo kabisa sijavitaja kabisa hapo”amesema. | Biashara | 1 |
WAZIRI wa Nchi Ofi si ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ametoa siku sita kwa uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, kumpa taarifa ya kina kwa nini hawajachukua Sh bilioni 50.9 zilizotengwa kwa ajili ya mradi wa kituo cha mabasi cha Mbezi Luisi.Jafo aliyasema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema iwapo uongozi huo utashindwa kutoa maelezo ya kina, fedha za mradi huo zitapelekwa kwenye halmashauri nyingine zikafanye shughuli za maendeleo.Alisema mradi huo wa kituo cha mabasi cha Mbezi Luisi umetengewa fedha nyingi ambayo ni Sh bilioni 50.9, lakini anashangazwa ni kwa nini mpaka sasa unasuasua. Awali mradi huo ulipangwa kuanza Julai mwaka 2017 lakini mpaka sasa haujaanza.HabariLeo ilimtafuta Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana kuhusu suala hilo alisema, “Kuna mambo ya ndani ambayo yanakwamisha, ila mchakato bado unaendelea, tutampelekea taarifa kumjulisha hili, kuna mambo ya ndani ambayo sitaweza kuyaweka wazi.”Aidha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam, Paul Makonda hakuweza kupatikana kuzungumzia kusuasua kwa ujenzi wa kituo cha mabasi cha Mbezi Luisi, kutokana na simu yake kuita bila kupokewa, hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi haukujibiwa. | Kitaifa | 0 |