content
stringlengths 1
17.8k
| category
stringclasses 5
values | label
int64 0
4
|
---|---|---|
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Ilala inawashikilia watu watatu akiwamo mmiliki wa Kampuni ya Motrax, Chandulal Ladwa kwa tuhuma za kutoa rushwa ya Sh200,000.Mtuhumiwa huyo alitoa rushwa kwa wakili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Goodluck Mwangomango ili ampe upendeleo kwenye kikao cha kujadili marejeo ya mikataba ya miradi ya chama hicho.Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ilala, Christopher Myava aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwa Mei 29, mwaka huu, saa 4 asubuhi, maeneo ya Sea View Upanga kwenye mgahawa wa Central Park, Ladwa ambaye ni mpangaji wa maeneo ya biashara ya CCM alitoa kiasi hicho ili apewe upendeleo kwenye kikao cha kufanya marejeo ya mikataba.Alisema mtuhumiwa alifikishwa mahakamani jana chini ya Kifungu cha 15 (1), (b) cha Sheria ya Takukuru Na.11/2007 ili kujibu tuhuma hizo. Alisema CCM wanaendelea kufanya uhakiki wa mali zote za chama ikiwa ni agizo la Rais John Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho Taifa. Alisema kiwanja ambacho mtuhumiwa amepanga ni mali ya CCM hivyo mtuhumiwa aliomba kukutana na wakili huyo wa CCM ili apate kipaumbele cha kupatiwa tena eneo alilopanga maeneo ya Oysterbay.Wakati huo huo, maofisa wawili wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (Dawasa), Selaman Ally na Issa Khalifan wanashikiliwa na Takukuru kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Sh 150,000.Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ilala Myava alisema tukio hilo lilitokea Aprili 24, mwaka huu, saa saba mchana, maeneo ya Tabata Kisukuru baada ya kuomba rushwa kutoka kwa mtoa taarifa ili wamrekebishie ankara ya maji na kumrejeshea huduma hiyo. Myava alisisitiza wananchi kutoa taarifa na ushirikiano kwa Takukuru ili kutokomeza vitendo vya rushwa nchini. Pia alitoa rai kwa viongozi wa vyama vya siasa kutoa taarifa za watu wanaofanya ubadhirifu wa mali za vyama hivyo ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa. | Kitaifa | 0 |
KUFUATIA kuwepo kwa taarifa zilizoenea za kusimamishwa kwa baadhi ya benki katika biashara ya kubadilisha fedha, Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imebainisha kuwa ilichokifanya ni kuzisimamisha ushiriki katika soko la jumla la fedha za kigeni na si kubadili fedha reja reja.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na benki hiyo kupitia Idara ya uhusiano wa Umma na Itifaki, ilisema kuwa benki za Barclays , Exim, UBA, BancABC na Azania zimesimamishwa kushiriki katika Soko la jumla la fedha za kigeni kati ya benki za kibiashara (IFEM), kwa kuvunja kanuni na taratibu kama inavyowataka kufanya.Hatua inatajwa kuchukuliwa baada ya benki hizo, kushindwa kutoa taarifa kwa Benki Kuu ya Tanzania juu ya miamala yote ya kifedha inayofanyika. Taarifa hiyo ilifafanua kuwa soko la fedha za kigeni kati ya mabenki (IFEM), lina kanuni na taratibu zake, ambazo zinaeleza kinagaubaga namna washiriki wote wanavyotakiwa kufanya biashara hiyo na kwamba washiriki wote katika soko hilo, wanatakiwa kutoa taarifa BOT kuhusu miamala waliyofanya kwa siku.Hata hivyo, inaeleza kuwa washiriki wa IFEM ambao watavunja kanuni na taratibu za soko hilo, hufungiwa kushiriki katika kuuza na kununua kwenye soko hilo kwa kipindi maalum. “Hivyo kwa benki hizo tano, kufungiwa kwake kunahusu tu ushiriki katika soko la fedha za kigeni kati ya mabenki na sio biashra rejareja ya fedha,” ilisema taarifa hiyo na kusema kuwa benki hizo zinaruhusiwa kuuza fedha za kigeni kwa wateja wake au kununua kutoka kwao.Soko la jumla la fedha za kigeni kati ya benki za kibiashara (IFEM), linawezesha benki za biashara na taasisi za fedha kuuza na kununua (kubadilishana) dola za kimarekani na shilingi kati yao. Taarifa hiyo ilieleza kuwa soko hilo, husaidia kuamua kiwango rasmi cha kubadilisha dola dhidi ya shilingi kwa siku husika. Benki Kuu ya Tanzania pia inashiriki kuuza na kununua fedha za kigeni pale inapolazimu, wakati mwingine huingilia soko ili kuhakikisha hakuna mabadiliko makubwa. | Kitaifa | 0 |
WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amechukizwa na kukemea utendaji kazi wa watendaji wa wilaya ya Kongwa wa kufanya kazi kwa maigizo.Pia, ameagiza Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Nelson Milanzi kujieleza kwa maandishi kwa kushindwa kuwajibika katika utekelezaji wa miradi ya elimu na kutaka maelezo hayo kufika kwa Katibu Mkuu Tamisemi ifikapo Ijumaa.Jafo ambaye juzi alitembelea miradi kadhaa katika wilaya ya Kongwa na kukuta shughuli za ujenzi katika shule mbili za sekondari ukiwa kwenye hatua ya msingi ikiwa ni miezi sita tangu kutolewa kwa fedha.Akiwa katika shule ya Sekondari ya Kongwa, Jafo alimuagiza Mkurugenzi wa halmashauri ya Kongwa kumpigia simu Ofisa Elimu Milanzi ambaye yuko Mtwara kwenye mashindano ya Umiseta kurejea kwenye kituo chake cha kazi, kujieleza kimaandishi na kurejesha fedha za safari alizopewa kwa siku ambazo alitakiwa kuwepo kwenye mashindano.“Mpigieni simu arudi, na akifika aandike barua ya kujieleza kwa katibu mkuu kwanini ameshindwa kutimiza wajibu, nimetoa nafasi hii kwa sababu napenda kutenda haki, pengine kuna jambo nyuma ya ukuta,” alisema. “Nataka tumsikilize na yeye pengine kwenye ofisi yenu mnakwamishana mwenyewe apime, akishajieleza Katibu Mkuu atapima maelezo yake na kuamua ama kumbakisha au akapangiwe kazi zingine maana anaweza kurudi kufundisha, kuwa afisa elimu kata,” alisisitiza.Hatua ya Jafo ilitokana na maelezo yaliyotolewa kwa nyakati tofauti na Mkuu wa Wilaya, Deo Ndejembi na Mkurugenzi, Dk Omary Nkulo waliodai kuchelewa kujengwa kwa majengo katika shule ya Sekondari Kongwa na Sejeli kutokana na kuwapo kwa mvutano wa ama watumie mfumo wa Force Account au watumie mkandarasi.Maelezo kama hayo pia yalitolewa wakati Jafo akikagua mradi wa shule ya Sekondari ya Sejeli ambako ujenzi wake pia uko katika ngazi ya msingi. Akiwa kwenye shule ya Sejeli, Jafo alisema: “ Hapa nikuambie ni uzembe hakuna sababu yoyote, hata hii kazi kwa kiasi kikubwa imeanza kufanyika leo (juzi) na kwa sababu Jafo amekuja anaweza kutembelea shule.Kama tunaenda kanisani na misikitini nani anaweza kusimama na kusema naongopa anyoshe mkono hapa, hata machinjio ya kuku pia yametelekezwa.” Alisema fedha kwa ajili ya shule hizo zilitolewa na kupokewa tangu Januari, mwaka huu, lakini hakuna kitu kilichofanyika wakati maeneo mengine waliyopelekewa fedha kama hizo wamemaliza mabweni na wamajiandaa kupokea wanafunzi wa kidato cha tano.“Hapa kazi sijaridhika na mnamuangusha Spika (Job Ndugai) ambaye ametafuta fedha kwa ajili ya wananchi wake, kwa kweli sijaona sababu ya msingi, nendeni Bahi ina watumishi kama ninyi, lakini wanajenga mabweni, madarasa, hospitali ya wilaya na mambo yanaenda vizuri ila hapa sijaridhika,” alisema. | Kitaifa | 0 |
WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imeanza operesheni maalum kubaini wamiliki hewa wa viwanja zaidi ya 9,000, vilivyoandikishwa kumilikiwa na watumishi wa wizara hiyo kwa njia isiyokuwa halali.Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ilibainisha kuwepo kwa idadi kubwa ya viwanja, vinavyomilikiwa na wafanyakazi hao kwa majina bandia au anuani za uongo. Alisema watumishi hao wamejimilikisha isivyo halali ili waje kuviuza kwa wananchi kwa njia za udanganyifu na kuwa wapo watumishi, ambao wamepima viwanja vya wananchi mara mbili mbili na kuwasababishia kero wananchi hao. Aliongeza kuwa idadi kubwa ya viwanja hivyo havijalipiwa kodi na pia havijaendelezwa kwa kuwa vimeachwa kwa muda mrefu bila ya shughuli za kibinadamu kufanyika hali inayowaathiri wakazi wengine wa maeneo hayo.Alisema,“wizara imejipanga kunasa viwanja vyote ambavyo umiliki wake una mashaka na vitachukuliwa na kurejeshwa serikalini hivyo basi wananchi mnaombwa kutoa ushirikiano stahiki ili operesheni hii iwe na tija.” Akizungumzia kuhusu athari zaidi za kutoendelezwa kwa viwanja hivyo, alisema kuwa ni sawa na kuwadhurumu haki wananchi wengine kumiliki ardhi na kuongeza kuwa kwa kutokuendelezwa huko, kunasababisha uwepo wa nyoka, uchafu au hata uharifu kwa wananchi waishio maeneo husika au jirani.Aliwataka wananchi waishio jirani na maeneo yasiyoendelezwa kwa zaidi ya miaka 10 bila ya kuwaona wamiliki wake kutoa taarifa ili yaanze kuchunguzwa. Kwa upande wa Wilaya ya Kinondoni, viwanja hivyo na idadi yake ni Mbweni Mpiji viwanja 3,544, Mbweni JKT viwanja 1,424, Mivumoni viwanja 1,508 na Bunju viwanja 4,868. Kwa upande wa Temeke ni maeneo ya Tuangoma yenye viwanja 3,384 na Kizota ikiwa na viwanja 2,362.Kwa upande wa Wilaya ya Kigamboni, maeneo yenye viwanja vya aina hiyo ni Mtoni Kijichi, viwanja 1,776, Mwongozo viwanja 2,754 na Vijibweni viwanja 38. Maeneo mengine ni Kibada viwanja 6,223 na Gezaulole viwanja 1,128, wakati Wilaya ya Ilala eneo la Buyuni Chanika viwanja 7,570 na Mwanagati viwanja 2,164. Waziri Lukuvi aliwataka watu wenye taarifa za watu wanaomiliki viwanja visivyoendelezwa kwa muda mrefu kwenye maeneo hayo, kumpigia simu yake ya mkononi namba 0755 333334 huku akiwahakikishia usalama wao kuwa hawatajulikana kuwa ndio wametoa taarifa hizo. | Kitaifa | 0 |
KATIBU Mkuu Kiongozi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Balozi John Kijazi amezindua vikundi kazi vya baraza hilo kwa lengo la kujenga na kuimarisha mahusiano kati ya sekta za umma na binafsi katika kuibua changamoto na kuzijadili kwa mustakabali wa maendeleo ya Tanzania.Akizungumza baada ya uzinduzi wa vikundi kazi hivyo jijini Dar es Salaam juzi, Balozi Kijazi alisema madhumuni ya kuunda vikundi kazi hivyo vilivyowajumuisha wataalamu katika sekta mbalimbali, vitawezesha majadiliano juu ya changamoto zijadiliwe kwa kina zaidi kabla ya kupelekwa katika ngazi ya Baraza.“Jumla ya vikundi kazi vinne nimevizindua leo (juzi) ikiwa ni pamoja na Kikundi kazi cha Mazingira ya Biashara, Viwanda, Misitu na Kilimo vitavyokwenda kuibua changamoto na kuleta mapendekezo yatakayosaidia kuboresha sera na miongozo iliyopo,” alisema Balozi Kijazi.Alisema ushirikiano kati ya sekta binafsi na ya umma, unahitajika ili kuweza kubaini changamoto na kuzijadili na kuja na mapendekezo yatakayoleta tija katika mustakabali wa kujenga uchumi wa Taifa.“Serikali itapokea mapendekezo yote yatakayowakilishwa na timu za wataalamu kutoka katika vikundi kazi hizi na tutayafanyia kazi mapendekezo yote, zaidi kwa mengine yanayoweza kuchukuliwa na maamuzi kwa ngazi yenu endeleeni lengo ni kupanga majadiliano katika ngazi ya taifa,” alisema Balozi Kijazi.Alisisitiza kuwa mijadala ya vikundi kazi hivyo vifanyiwe kazi kwa uhuru na usawa kwa kutohofia cheo cha mtu au mali, bali wote wawe kitu kimoja ili majadiliano yaweze kuleta tija na mapendekezo yatakayofanya mazingira ya biashara kuboresheka zaidi.“Vikundi kazi hizi vikapitiwe Sera, Miongozo na Sheria zilizopo ili waje na mapendekezo yatakayoboresha mazingiria ya biashara kuwa rafiki kwa wawekezaji na wafanyabiashara nchini,” alisema.Alisema kumekuwa na malalamiko mengi juu ya tozo, mamlaka za udhibiti na kero mbalimbali katika uanzishaji wa biashara nchini, hivyo ni muhimu vikundi kazi hivyo vikatoa mapendekezo katika maeneo hayo ili yafanyiwe kazi. “Uongozi wa awamu ya tano umefanikiwa kupunguza baadhi ya changamoto ikiwemo utitiri wa kodi kwa wafanyabiashara, hivyo ni matumaini yangu tutakwenda kumaliza kabisa changamoto zilizopo na kupelekea nchi yetu kupiga hatua kiuchumi,” alisema Balozi Kijazi.Pia, Balozi Kijazi alisema kikosi kazi cha kilimo kisimamie utekelezaji wa nguzo kumi za kilimo kwanza na pia kufanya mapitio ya Mpango wa Awamu ya Pili wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP- II) na kuleta mapendekezo ya utekelezaji wake. “Lengo letu ni kutizama azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025, vikundi kazi hivi ndiyo vitatupa mwanga wa kufikia malengo kwa kuja na mapendekezo yenye tija na utekelezaji ufanywe maendeleo yapate kuonekana,” alisema Balozi Kijazi. | Kitaifa | 0 |
SIMBA itacheza nusu fainali dhidi ya Azam FC katika mchezo wa mashindano ya Mapinduzi yanayochezwa visiwani Zanzibar kesho kutwa.Mchezo huo utachezwa katika Uwanja wa Amaan, Unguja baada ya jana kuifunga Zimamoto kwa mabao 3-1 katika Uwanja wa Gombani, Pemba. Azam FC ambaye ni bingwa mtetezi wa mashindano hayo, anakutana na Simba ambayo katika fainali zilizopita waliifunga kwa mabao 2-1 katika Uwanja wa Gombani Pemba, hivyo mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.Simba ambayo ipo Kundi B iliifunga Zimamoto jana kwa mabao 3-1 inakutana na Azam FC ambayo ipo Kundi A ambayo iliitoa Mlandege kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa juzi Uwanja wa Amaan kwa bao la Obrey Chirwa dakika ya 57.Simba ilianza kupata bao la kwanza dakika ya nne likifungwa na John Bocco na dakika tano baadaye iliongeza bao la pili lililofungwa Sharaf Shiboub katika dakika ya tisa akiunganisha kona iliyopigwa na Ibrahim Ajibu, lakini dakika ya 28 Zimamoto walipata bao la kwanza lililofungwa na Ibrahim Ahmada na timu hizo kwenda mapumziko zikiwa 2-1.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na katika dakika ya 53 Ibrahim Ajib aliifungia Simba bao la tatu baada ya kuwazidi mbio walinzi wa Zimamoto, bao lililodumu hadi dakika 90 kipyenga cha mwisho kilipopulizwa.Kwa mara ya kwanza Simba ilimchezesha Louis Mequissone raia wa Msumbiji iliyemsajili juzi katika dirisha dogo ambaye aliingia dakika ya 78 kuchukua nafasi ya Hassan Dilunga.Baada ya mchezo huo, nahodha wa Simba, John Bocco, alisema wanakwenda kuangalia makosa yao na kuyafanyika kazi na mchezo wao dhidi ya Azam FC utakuwa wa ushindani na wao watahitaji kushinda mchezo huo ili kuwapa raha mashabiki.“Azam FC ina wachezaji wazuri kama ilivyo Simba hivyo mchezo huo tumeuchukulia kwa uzito mkubwa na tunakwenda kujiandaa ili tuweze kushinda,” alisema Bocco.Mtibwa Sugar ambayo ipo Kundi B inatarajiwa kucheza nusu fainali kesho na mshindi wa mchezo wa Yanga dhidi ya Jamhuri ambao ulichezwa jana usiku. Mtibwa Sugar iliifunga Chipukizi kwa penalti 4-2 baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya bao 1-1 mchezo uliochezwa Uwanja wa Gombani, Pemba, ambapo kipa Said Mohammed ‘Ndunda’ aliokoa penalti mbili.Chipukizi ilitangulia kufunga bao dakika ya tano lililofungwa na Suleiman Nassor na Haroun Chanongo kuisawazishia Mtibwa Sugar dakika ya 63. Shujaa wa Mtibwa alikuwa Nduda ambaye aliokoa penalti za Jumaa Kassim na Abdallah Mohamed, huku penalti za Mtibwa Sugar zikifungwa na Omar Sultan, Abdulhalim Humud, Riffat Khamis na Dickson Job na zile za Chipukizi zilifungwa na Salim Abui na Abdallah Khalisan.Mashindano hayo ya 13 yanashirikisha timu nne za Zanzibar na timu nne za Tanzania Bara na mecho zitachezwa kwa mtindo wa mtoano, ambapo bingwa anatarajiwa kuondoka na Sh milioni 15 pamoja na kombe. Fainali za mashindano hayo zitafanyika Januari 13 katika Uwanja wa Amaan majira ya saa 2:15 usiku. | michezo | 2 |
SERIKALI imejizatiti kuongeza uwekezaji katika kilimo cha miwa ukienda sanjari na ujenzi wa viwanda vya sukari, kupunguza nakisi iliyopo.Akizungumza na Habarileo hivi karibuni, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema upo mkakati wa makusudi kuhakikisha viwanda vilivyopo vinaongeza uzalishaji wa sukari na kuongeza uwekezaji katika kilimo cha miwa.Mwaka jana, Rais John Magufuli alipokutana na wafanyabiashara jijini Dar es Salaam, aliwataka kuwekeza zaidi katika viwanda vya sukari, kukabili nakisi inayosababisha nchi kuagiza sukari kutoka nje.Rais Magufuli alisema mahitaji ya sukari ni tani 590,000 kwa mwaka huku tani 455,000 zikiwa ni sukari ya kula na 135,000 ya viwandani. Upo upungufu wa tani 125,000 wa sukari ya kula na tani 135,000 ya viwandani.Alitaja Kampuni ya Sukari ya Kilombero kwamba ina mkakati mkubwa wa miaka mitatu wa kuongeza uzalishaji wa miwa mara mbili.“Sasa wanazalisha zaidi ya tani 130,000 na wamesema wana uwezo wa kuzalisha hadi tani 250. Wanataka kupanua mashamba na wazalishaji wa nje wa miwa waongeze uzalishaji,” alisema.Viwanda vya Kagera na Mtibwa pia vinatajwa kuwa na mpango wa kupanua uzalishaji wa miwa. Kwa upande wa TPC Moshi, Hasunga alisema wanashindwa kufanya upanuzi kwa sababu ya eneo kuwa dogo.Waziri Hasunga alitaja miradi mipya ambayo serikali inaiwekea mkazo ni Mkulazi 1 na Mkulazi 2 mkoani Morogoro.Mmoja una uwezo wa kuzalisha tani 50,000 za sukari na mwingine tani 200,000 hadi 250,000.Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kupitia kampuni yake ya Mkulazi Holding na Jeshi la Magereza, ndiyo imeanzisha kiwanda katika Gereza la Mbigiri mkoani Morogoro.“Kwa sasa hivi wameshapanda miwa maeneo mengi na walioko nje wamepata miwa mingi, kinachosubiriwa sasa ni viwanda vitakavyosindika hiyo miwa,” alisemaAlitaja kampuni nyingine ya miwa ya Morogoro, ambayo pia imewekeza katika kilimo cha miwa kwa wingi ianze uzalishaji . Ingawa alisema siyo mzalishaji mkubwa, lakini alisema itachangia uzalishaji wa sukari. | Biashara | 1 |
Baadhi ya wakazi wa maeneo ya Dar es Salaam na Bagamoyo watakosa maji kwa kipindi cha saa kadhaa kutokana kupasuka kwa bomba la maji eneo la Mtamboni,Ruvu mkoa wa Pwani kupasuka.Haya yameelezwa na kitengo cha mawasiliano cha Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) kwenye taarifa maalumu kwa vyombo vya habari.Taarifa hiyo inaeleza kuwa bomba hilo la maji lililopasuka jioni ya Jumapili, Januari 20, lilipelekea mamlaka hiyo kuuzima mtambo wa Ruvu Chini.Baadhi ya maeneo yatakayoathirika na suala hili ni pamoja na Bunju, Tegeta, Mbweni, Wazo, Sinza, Masaki, Magomeni, Tabata na mengineyo.Kazi ya marekebisho ya bomba hilo imeanza na inatarajiwa kukamilia Jumatatu, January 21 majira ya saa 12 jioni, na maji kuanza kupatikana katika maeneo hayo. | Kitaifa | 0 |
WAGONJWA 400 wa mabusha na matende wamefanyiwa upasuaji wa ugonjwa huo katika Wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke tangu kuanzishwa kwa kampeni hiyo, hatua iliyotokana na elimu mbalimbali inayoendelea kutolewa kwa wananchi.Hayo yalibainishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam jana, Dk Grace Maghembe wakati wa semina iliyoendana na uzinduzi rasmi wa kampeni ya utoaji dawa za kingatiba za magonjwa ya mabusha na matende inayotarajiwa kuanza leo katika wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam.Katika uzinduzi huo ambao mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Dk Maghembe alisema wagonjwa hao wamepatikana tangu kuanza kwa kampeni hiyo miaka mitano iliyopita ambapo mbali na wagonjwa hao, asilimia 80 ya wananchi wamepatiwa dawa za kingatiba. “Tunawaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika unywaji wa dawa za kuzuia mabusha na matende ili kusaidia kulinda afya zao, ikumbukwe kuwa tiba ni bora kuliko kinga hivyo ni vyema wananchi wajitokeze kwa wingi kushiriki kampeni hiyo” alisema Dk Maghembe.Pia alisema kampeni ya unywaji wa dawa kinga hizo utahusisha watu wa jinsi zote kuanzia umri wa miaka mitano na kuendelea na kuwasisitiza wanawake kujitokeza kwa wingi kunywa dawa hizo kwa kuwa magonjwa hayo huwapata watu wa jinsia zote.Alisema ili kufanikisha suala hilo, vituo 923 vya huduma ya kudumu na 671 vya huduma za kuhama pamoja na mikoba 252 kwa kata na mitaa yote ya Jiji la Dar es Salaam vitatoa huduma hiyo, lengo ni kufikia asilimia 90 ya wananchi kwa mwaka huu pekee. Kwa upande wake, Makonda aliwataka wananchi hao kujitokeza kwa wingi kunywa dawa hizo ili kufanikisha kutokomeza magonjwa hayo katika Mkoa wa Dar es Salaam.Alisema kufanyika kwa kampeni hiyo kumelenga kutokomeza kabisa ugonjwa huo na malengo kwa mwaka huu ni kufikia asilimia mia huku akiahidi kuanzisha kampeni dhidi ya ugonjwa tezi dume kwa wananchi wa Jiji hilo. Alisema kuanzishwa kwa uchunguzi na tiba ya ugonjwa huo katika hatua ya kaya hadi kaya, kumelenga kutokomeza ugonjwa huo ambao siku za hivi karibuni umeonekana kuwakumba wananchi wengi nchini, wakiwemo wakazi wa Jiji la Dar es Salaam. | Kitaifa | 0 |
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa kesho Jumatatu atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano ya kitaifa ya Umoja wa Shule za Sekondari Tanzania (Umisseta) yatakayofanyika mjini Mtwara.Michezo hiyo itakayoshirikisha takribani washiriki 3,304 kutoka mikoa 26 ya Tanzania Bara na miwili Zanzibar, itafanyika hadi Juni 21 na kufungwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Prof Joyce Ndalichako.Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Idara ya Elimu (Tamisemi), Leonard Thadeo alisema jana kwa njia ya simu kuwa kila kitu kimekamilika na tayari yeye na timu yake wako Mtwara kwa ajili ya michezo hiyo.Alithibitisha kuwa Majaliwa ndiye atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa michezo hiyo mwaka huu, ambayo itashirikisha michezo ya soka, netiboli, riadha, mpira wa kikapu, mpira wa wavu, mpira wa mikono kwaya pamoja na ngoma.Aidha, Thadeo alisema kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ndiye atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Umoja wa Michezo ya Shule za Msingi (Umitashumta) utakaofanyika Juni 25 wakati wachezaji wataanza kuwasili siku mbili kabla.Alisema kuwa michezo ya Umitashumta yenyewe itashirikisha mikoa 26 ya Tanzania Bara tu na inatarajia kufungwa Julai 3 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jafo.Thadeo aliongeza kuwa lengo lao kubwa la kwanza ni kuwawezesha wanafunzi kucheza michezo, ambayo ni sehemu ya elimu na wale wanaohusika na kuendeleza vipaji wanatakiwa kuwaendeleza watoto hao.Alisema mfano shule za michezo na mashirikishi au vyama vya michezo kama Chaneta (Netiboli), TFF (Soka), TBF (Kikapu) Taha (Mpira wa Mikono), Tava (Wavu) na RT (Riadha), ndizo zenye majukumu ya kuwaendeleza vipaji vya watoto hao | michezo | 2 |
LEO, Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kwa michezo mitatu katika viwanja tofauti ukiwemo ule utakaowakutanisha mabingwa mara 27 wa ligi hiyo, Yanga SC ambao watawaalika Mbao FC katika Uwanja wa Taifa.Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa Mei 22 mwaka jana katika uwanja huo huo ambapo Yanga walitoka na ushindi wa bao 1-0 lilofungwa dakika ya 22 na Thaban Kamusoko kwa mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja wavuni.Yanga ina matokeo mazuri tangu kuanza msimu huu ambapo katika michezo yake mitano imeshinda minne na sare moja huku Mbao wakiwa wamecheza michezo minane wameshinda minne, sare mbili na kufungwa miwili.Kabla ya mechi za jana, Mbao walikuwa wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 14, Yanga walikuwa nafasi ya nne na pointi zao 13.Mbao wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya matokeo mbaya kwenye mechi zao mbili mfululizo za ugenini, walitoka sare ya 1-1 na Coastal Union, Mkwakwani na kufungwa 1-0 na Ruvu Shooting wakati Yanga ambao mechi zao zote wamecheza kwenye uwanja huo wakiwa na rekodi nzuri ya ushindi mara nne na sare moja.Yanga ndio wanaonekana kuwa wakali zaidi katika kufumania nyavu za wapinzani wao ambapo wamefunga mabao tisa na kufungwa manne tofauti na Mbao ambao wamefunga sita na kufungwa idadi sawa na Yanga.Mechi zingine zitakazochezwa leo ni kati ya Biashara United itakayokuwa nyumnbani kwenye Uwanja wa Karume, Mara kuwakaribisha wachimba madini wa Mwadui FC ambao wanaburuza mkia, nao Maafande wa JKT Tanzania watakabiliana na Alliance ambao wanashika nafasi yapili kutoka mkiani mwa msimamo. | michezo | 2 |
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeingia katika ushirikiano na kampuni ya Samsung Mobile pamoja na kampuni ya usambazaji ya Yellow box kuzindua ingizo jipya la simu za kisasa aina ya Samsung A series.Airtel na Samsung imeingia ubia huo huku ikizindua OFA maalumu kupitia Samsung A10 na A2 core inayolenga kuwafaidisha wateja wake katika msimu huu wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jana, Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, alisema Airtel imeingia kwenye ushirikiano mpya na Samsung Mobile pamoja na Yellow Box kwa kuzindua simu za kisasa kwa lengo la kuongeza watumiaji zaidi wa huduma za intaneti kutokana na uhitaji wa wateja wetu”.“Kwenye ulimwengu wa kidijiti kwa jinsi ambavyo teknolojia inakua, Airtel tunaona ni vyema pia wateja wetu ambao ni muhimu sana kwenye ukuaji wa biashara zetu kuendana na ukuaji huo. Katika msimu huu wa Saba Saba tunawaletea smartphone mpya kabisa za Samsung A series zenye ofa kabambe kupitia A10 na A2 core,” alisema Mmbando.Mmbando alisema hiyo ni fursa ya kipekee kwa wateja wa Airtel kujipatia simu mpya aina ya Samsung A series ikiwemo hii ya A10 na A2 core na kujipatia ofa ya bando ya 36GB kwa muda wa miezi 12 bure. Simu za Samsung A series na A10 na A2 core zitapatikana pia kwenye maduka yote ya Airtel Money Branch, maduka ya Airtel nchi nzima na katika maonesho ya Sabasaba.Naye Meneja Biashara wa Samsung Mobile, Suleiman Mohammed alisema ushirikiano baina ya Samsung na Airtel ni muhimu sana, kwani utakuza watumiaji wa simu za kisasa nchini. | Kitaifa | 0 |
MWANAMUZIKI wa kizazi kipya nchini, Ali Kiba amekuwa mdhamini rasmi wa klabu ya soka ya Coastal Union ya Tanga inayoshiriki Ligi Kuu Bara.Kiba amekuwa mdhamini wa klabu hiyo kupitia kinywaji chake cha Mo Faya.Msanii huyo mkubwa nchini, amesajiliwa na Coastal Uniona hivyo ataonekana akiichezea katika msimu mpya wa Ligi Kuu 2018/19 unaotarajiwa kuanza Agosti 22 mwaka huu.Kiba alizungumzia udhamini wake huo katika kipindi cha Nyundo ya Baruan cha runinga ya Azam kinachotarajiwa kurushwa kesho.“Nimeamua kuwa mdhamini ili kuisaidia Coastal Union kurudi katika ubora wake,” alisema katika sehemu ya mahojiano yake kwenye tangazo la kipindi hicho kinachorushwa kila Alhamisi kwenye Azam Sports HD 2.Coastal ni miongoni mwa timu zilizopanda Ligi Kuu msimu huu ingawa timu hiyo si ngeni kwani imekuwa ikipanda na kushuka daraja mara kwa mara.Kiba kabla ya kuvuma kwenye muziki alikuwa mshambuliaji mahiri kwenye kikosi cha Ashanti United ya Ilala. | michezo | 2 |
MABONDIA Watanzania wametakiwa kujiaandaa vyema kabla ya kwenda kushiriki kwenye mashindano makubwa.Rai hiyo imetolewa baada ya mabondia wa Tanzania, Swedi Mohamed na Suleiman Said kupigwa kwa Knockout (KO) katika mapambano ya utangulizi kabla ya pambano la marudiano kati ya Andy Ruiz na Anthony Joshua lililofanyika nchini Saudi Arabia juzi.Akizungumzia mapambano hayo Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Kamisheni ya Ngumi za kulipwa nchini Tanzania (TPBRC), Yahya Poli alisema mabondia ni vema kujiandaa kabla ya kukubali pambano kuepuka fedheha ya kupata kipigo.“Kupigwa katika ndondi ni kitu cha kawaida lakini tunaangalia umepigwa pigwaje, hivyo nawashauri mabondia kujiandaa vema kabla ya kukubali pambano kwani kufanya hivyo kunawajengea heshima,” alisema Poli.Swedi Mohamed alichapwa na Ivan ‘Hopey’ Price wa Uingereza katika raundi ya tatu kwenye pambalo la uzito wa Super Bantam na Suleiman Said alipigwa hadi akakaa raundi ya kwanza na Mmarekani Diego Pacheco katika uzito wa kati Katika usiku huo wa masumbwi Anthony Joshua alifanikiwa kurejesha mataji yake ya WBA, WBO, IBO na IBF baada ya kumshinda kwa pointi za majaji, 118-110 mara mbili na 119-109, Andy Ruiz.Joshua alipokonywa mataji yake ya WBA, WBO na IBF baada ya kupigwa na Ruiz kwa Knockout (KO) raundi ya saba katika pambano lililofanyika Juni mwaka huu ukumbi Madison Square, New York, Marekani.Ikumbukwe juzi bondia mwingine, Mtanzania, Bruno Tarimo ‘Vifua Viwili’ alifanikiwa kutwaa taji la IBF International uzito wa Super Feather baada ya kumshinda kwa pointi mwenyeji, Nathaniel May ukumbi wa ICC Exhibition Centre mjini Sydney, Australia.Bondia huyo mzaliwa wa Rombo, mkoani Kilimanjaro alimzidi mpinzani wake kwenye pambano hilo la raundi 10 na haikuwa ajabu kutangazwa mshindi jana.Hilo lilikuwa pambano la 28 kwa Tarimo tangu ajiunge na ngumi za kulipwa Desemba 25, mwaka 2013 akiwa ameshinda mara 25, mara tano kwa KO, amepigwa mara mbili zote kwa KO na droo moja. | michezo | 2 |
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa chuo hicho, Profesa Mathew Luhanga, katika hotuba yake iliyosomwa na Profesa Eliuter Mageni katika mahafali ya 48 ya chuo hicho mwishoni mwa wiki.Alisema kwamba ufugaji wa nyuki ni eneo linalokua kwa kasi hapa nchini hivyo chuo hicho kinajipanga kutoa mchango wake kwa jamii katika eneo hilo.“Tayari elimu ya awali juu ya bidhaa za nyuki imeanza kutolewa kwa baadhi ya wanafunzi ndani ya chuo,” alisema Profesa Luhanga na kuongeza mitaala imezingatia utoaji wa mafunzo ya ujasiriamali ambayo dhamira yake ni kufanya utafiti, kutoa huduma za ushauri na mbinu za kutafuta masoko na mitaji kwa wajasiriamali.Katika mahafali hayo, ambayo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda aliyewakilishwa na Naibu wake, Gregory Teu, jumla ya wahitimu 2,272 katika ngazi za astashahada, stashahada na shahada ya uzamili walitunukiwa.Aidha, kulikuwa na wahitimu waliomaliza mafunzo ya lugha ya Kifaransa daraja la kwanza na wanane wa daraja la pili.Katika mahafali hayo, ambayo Desemba 14 yataendelea kwenye Kampasi ya Mwanza, Mkuu wa Chuo, Profesa Emmanuel Mjema aliiomba Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara kutoa ushirikiano katika kukiendeleza chuo kimuundombinu. | Biashara | 1 |
CHAMA cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimevishauri vyuo vikuu nchini kuona umuhimu wa kufundisha masuala ya mazingira, madini na mafuta katika mitaala yao, ili kuijengea jamii uelewa mpana katika maeneo hayo.Rais wa TLS, Dk Rugemeleza Nshala alisema hayo Dar es Salaam jana na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo, itasaidia kudhibiti mianya ya wizi kwa rasilimali hizo, huku jamii ikipata manufaa katika nyanja mbalimbali.Akizungumza kuhusu mafunzo ya rasilimali zinazokwisha, kwa mawakili wa serikali, binafsi, wadau wa mazingira na madini kutoka serikalini yaliyofadhiliwa na nchi ya Canada, Dk Nshala alisema uelewa kuhusu masuala ya madini ni mdogo kwa sababu vyuo vingi hapo awali vilikuwa havifundishi masuala hayo na kuhamasisha kwa sasa kubadilika na kufundisha. Alisema kwa sasa nchi ina miradi mingi ya uchimbaji mafuta na madini, hivyo ni vyema kuwajengea uwezo wa kielimu wananchi wake ili kuhakikisha nchi inanufaika na rasilimali zake.“Ni vyema kufanya jitihada za kuwajengea uwezo wa kielimu kuhusu masuala ya madini, mafuta na mazingira wananchi wetu ili waweze kufahamu haki zao na sheria zilizopo,” alisema Nshala na kuwataka wanafunzi pia kuona umuhimu wa kujikita katika maeneo hayo kwa manufaa ya baadae. Alisema ipo haja sasa kwa vyuo vingi hapa nchini kuanza kutoa elimu hiyo ili pengo la uelewa mdogo wa masuala ya mazingira na madini likazibwa.Nshala alisema Watanzania wanaoishi maeneo ya madini wakifahamu sheria, kupigania haki zao, majukumu ya serikali za vijiji yakatekelezwa itasaidia rasilimali zilizopo kutumika kwa manufaa ya jamii.Kwa upande wake, Mshiriki ambaye ni Mwanasheria kutoka Baraza la Mazingira (NEMC), Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Naomi Joshua, alisema mabadiliko ya sheria ya mazingira ya mwaka 2017 yamechagiza uwezo wa shughuli za kimazingira hasa katika sekta ya madini. Alisema NEMC imekuwa ikijitahidi kufuatilia miradi mbalimbali na kuangalia athari za kimazingira na namna ya utekelezaji kabla ya kuanzisha kwa mradi.“Wanaokwenda kinyume tumekuwa tukiwachukulia hatua na tutahakikisha utekelezaji wa miradi unafanyika bila kuathiri mazingira,” alisema Naomi. Alisema mafunzo hayo ana imani yatawasaidia wanasheria wengi kufahamu mambo mbalimbali kuhusu mazingira, madini na mafuta kabla na baada ya kusaini mikataba ya uchimbaji madini. Mwanasheria wa Serikali, Godfrey Nyamsenda alisema, ni vyema kulinda na kuangalia masuala ya mazingira kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho. | Kitaifa | 0 |
MBUNIFU wa teknolojia ya umwagiliaji wa shamba kwa kutumia simu janja, Ramadhani Bakari kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, amebuni mfumo wa umwagiliaji unaomwezesha mkulima kumwagilia kwa kutumia simu ya mkononi akiwa ndani au nje ya nchi.Bakari ambaye ni Mhitimu wa Stashahada ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), chuoni hapo alisema hayo alipokuwa akizungumza na Habari Leo na kuongeza kuwa ametumia simu janja yenye ‘application’ ambayo inawasiliana na mfumo maalum.Alisema mfumo huo unaunganishwa na pampu ya maji, mabomba na kifaa cha kieletroniki ambacho ndicho kinachosaidia mfumo kufanya kazi kupitia simu ya mkononi.“Unakwenda kwenye simu na ku download application inayoitwa Blwnk, ukiifungua utakutana na kitufe kinaitwa washa ukibonyeza tu hapo unakuwa unafanya mawasiliano na mfumo wako popote ulipo kwa kuwa unajiwasha na shamba linaanza kupata maji,” alisema.Alisema lengo la kubuni teknolojia hiyo ni kupunguza changamoto ya umwagiliaji kwa wakulima kwani wamekuwa wakiajiri watu au kutumia nguvu kazi kubwa mashambani. Pia kuzuia upotevu wa maji unaweza kufanywa na wafanyakazi wazembe.Alisema utafiti huo upo katika hatua ya kujifunzia, Ulianza mwaka jana, na kwamba ukiendelezwa teknolojia hiyo inaweza kufanya kazi hadi kumwagilia eka 10. Naye Mkuu wa Idara ya Masomo ya Elimu ya Juu chuoni hapo, Dk. Philip Daninga alisema chuo kinafundisha Tehama ili wanafunzi waweze kujiajiri pale wanapomaliza masomo yao pasipo kutegemea kuajiriwa kwani ajira zimekuwa ni changamoto.Dk. Daninga alisema ulimwengu wa sasa unategemea Tehama hivyo chuo kinahakikisha kozi zinazofundishwa zinamsaidia mwanafunzi akimaliza aweze kuzifanyia kazi kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kuwa mbunifu anayeweza kuangalia mazingira yanayomzunguka na kubuni kitu.Dk. Daninga alisema kijana anapokuwa mbunifu inakuwa rahisi hata kupata ajira hivyo kama chuo wamekuwa wakihusisha mitaala kwa namna ambayo mwanafunzi anapomaliza masomo yake anakuwa na uwezo wa kujiajiri. | Kitaifa | 0 |
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewakumbusha wananchi kudai risiti sahihi kila wanapofanya manunuzi ya bidhaa, la sivyo haitasita kuwatoza faini na hata kuwashitaki mahakamani.Meneja wa TRA Mkoa wa Mwanza, Ernest Dundee alisisitiza hilo alipozungumza na HabariLeo jijini hapa juzi kuhusu wajibu wa mnunuzi wa bidhaa katika kuwezesha upatikanaji wa kodi za serikali.“Kutodai risiti sahihi wakati wa manunuzi ya bidhaa ni kushiriki kukwepa kodi, ndio maana sasa tumeanza kutoza faini ya Sh 30,000 hadi Sh milioni 1.5 kwa mtu anayebainika kukwepa wajibu huo wa kisheria,”alisema.Kwa upande mwingine, mfanyabiashara anayebainika kufanya mauzo bila kutoa risiti sahihi hutozwa faini ya Sh milioni tatu hadi milioni 4.5 na kushitakiwa mahakamani anaporudia kukwepa kodi kwa mbinu hiyo.Hatua hizo za TRA ni sehemu ya kusimamia utekelezaji wa matumizi ya mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFDs) wakati wa mauzo na manunuzi ya bidhaa mbalimbali.Dundee ametaja faida kuu za kutoa na kudai risiti kila yanapofanyika manunuzi ya bidhaa kuwa ni kutunza kumbukumbu za msingi za kuthibitisha bidhaa au mali na uzalendo wa kushiriki katika kuwezesha upatikanaji wa kodi halali za serikali.Faida nyingine ni kuongeza uwajibikaji ambapo kwa mfano, kumbukumbu husaidia TRA kufanya makadirio sahihi ya kodi na mlipakodi kupata haki stahiki ya kikodi ikiwemo ya unafuu unaotokana na sheria za kodi.Aidha, mfanyabiashara huweza kufanya manunuzi sahihi ya kuendeleza biashara kutokana na kumbukumbu alizonazo ikiwa ni pamoja na kuboresha biashara, kuomba mkopo wa fedha na kuweka mipango endelevu.Kutoa risiti pia kunamsaidia mfanyabiashara kuimarisha na kujiongezea fursa za kibiashara ikiwemo kupata zabuni mbalimbali kutoka kwa wateja wakubwa ambao ni serikali na taasisi zake, kampuni, mashirika yasiyo ya serikali (NGOs) na wafanyabiashara wakubwa.Makisio ya mapato ya serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 ni Sh trilioni 32.9 zikiwamo trilioni 18 zinazotarajiwa kukusanywa na TRA kutokana na kodi mbalimbali. | Biashara | 1 |
OFISI ya Waziri Mkuu inayoshughulikia Sera, Bunge, Vijana, Kazi na Ajira mkoani Lindi imetoa mikopo yenye thamani ya Sh milioni 200 kwa vikundi vya uzalishaji mali vya vijana tujiajiri 53 kwa nyakati tofauti.Vijana hao wanatoka vikundi vya uzalishaji vilivyoko katika halmashauri sita za wilaya za Kilwa, Liwale, Nachingwea, Lindi, Ruangwa na Manispaa ya Lindi mkoani humo. Ofisa Maendeleo ya Vijana, Ofisi ya Waziri Mkuu inayoshughulikia Sera, Bunge, Vijana, Kazi na Ajira kutoka makao makuu mkoani Dar es Salaam, Atupokile Mhalila alisema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofauti na vikundi mbalimbali vya uzalishaji.Mhalila alisema mikopo hiyo imegawanyika katika sehemu kuu mbili, kwanza kuanzisha miradi na pili kuendeleza vijana wanaounda makundi hayo. Mhalila alisema lengo kuu ni kuwanyanyua vijana kiuchumi kwa kuanzisha miradi ya uzalishaji mali ili iwawezeshe kujiajiri wenyewe na kupata kipato kwa kuanzisha viwanda vidogo. Alisema kila kikundi kinakuwa na vijana kumi na hupewa mkopo baada ya kuomba mradi wanaotaka kuufanya na kuutekeleza.Ofisa Maendeleo ya Jamii katika Manispaa ya Lindi, Iddi Maketa alisema kuwa wizara ya nchi, ofisi ya waziri mkuu inayoshughulikia sera, kazi, bunge, ajira na vijana ilitoa mikopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kiasi cha Sh milioni 90 kwa vipindi tofauti, navyo ni 2014/15, 2016/17 na 2018. Alisema vikundi vya hapa mjini vinajishughulisha kuongezea thamani mbao kwa kutengeneza samani za viti, vitanda na aluminium kwa madirisha, ya vioo na uchomoleaji wa milango ya vyuma pamoja na madirisha yake.Abdul Said kutoka kikundi cha Mshikamano cha kata ya Wailes mjini hapa aliishukuru serikali kwa kuwapa mkopo wa Sh 3,000,000 na uliwawezesha wanachama watano. Alisema walitumia fedha hizo kununua mashine za kuchomea na vifaa vinginevyo vya mradi wao wa kikundi hicho na kutoa ushauri kwa serikali badala ya kutoa fedha za mkopo wakopeshe vifaa vya kufanyia kazi siyo kutoa mkopo wa fedha. | Kitaifa | 0 |
USHINDI wa Azam FC wa mabao 2-0 dhidi ya Lipuli katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa juzi, ni salamu kwa Yanga kuwa wako tayari kupambana kuelekea katika mchezo utakaowakutanisha kesho.Azam FC ilishinda mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kufuatia Uwanja wao wa Azam Complex, kuwa katika matengenezo ambao mabao yalifungwa na Shaban Chilunda na Joseph Mahundi.Wakati wanalambalamba hao wa Chamazi wakifurahia ushindi huo, Yanga walikula kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar hivyo huenda mchezo wa kesho ukawa mgumu kwao.Akizungumzia ushindi katika mchezo huo , Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche alisema walifanikiwa kujua mapungufu ya Lipuli ndio maana walipata matokeo mazuri.“Nashukuru Mungu wachezaji walipewa maagizo nini cha kufanya, mchezo ulikuwa mgumu mwanzo mwisho ila tulipata pointi tatu kwa sababu tulitumia mapungufu yao kuwaadhibu,” alisema.Naye Kocha wa Lipuli, Julio Ellieza alisema kilichowagharimu wakafungwa ni kwa sababu walifanya makosa na walipambana kwa uwezo wao ila bahati haikuwa yao.“Tumefanya makosa wametuadhibu, tulipambana kadiri ya uwezo wetu lakini imeshindikana, naamini makosa yaliyojitokeza tutaenda kuyafanyia kazi ili tufanye vizuri katika michezo inayokuja,” alisema. | michezo | 2 |
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya jumla ya bilioni 42.8/- Machi, mwaka huu, tangu mfumo mpya wa Stempu za Kodi za Kieletroniki (ETS) uanze kutumika.Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Charles Kichere wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, leo mchana (Jumanne).Ameeleza kuwa makusanyo hayo ni ongezeko la bilioni 3.5/- (sawa na asilimia tisa) ukilinganishwa na bilioni 39.3/- zilizokusanywa Machi, 2018.Ameongeza kuwa, hadi kufikia Aprili 30, itakuwa mwisho wa matumizi ya stempu za karatasi, kwenye bidhaa zote za sigara, pombe kali, mvinyo, bia na aina zote za vileo zenye stempu zisizo za kielektroniki na zile zisizo na stempu kabisa.“Baada ya Aprili 30, bidhaa hizo hazitaruhusiwa kuwepo sokoni bila kubandikwa stempu za kodi za kielektroniki,” aliongeza.Habari kamili itachapishwa kwenye gazeti la HabariLeo Jumatano | Kitaifa | 0 |
.Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu nchini Kenya (KFCB), – Dkt Ezekiel Mutua ameipongeza kampuni ya Google kwa kuuondoa kwenye mitandao ya kijamii wimbo wa Tarimbo, ulioimbwa na kundi la Ethic Entertainment la nchini humo. | Burudani | 4 |
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mohamed Ahmada katika hafla ya uzinduzi wa mtandao wenye kasi wa 4G pamoja na huduma za kibenki kwa njia ya simu kutoka kampuni ya Zantel.Alisema pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na sekta za mawasiliano na fedha, lakini bado ipo changamoto kubwa ya kuyafikia maeneo mengi yanayohitaji kuboreshewa huduma hasa upatikanaji wa huduma hizo vijijini.“Nafurahi kuona kuwa Zantel na Benki ya watu wa Zanzibar imeanza vizuri katika hili katika kuhakikisha mnakuwa mstari wa mbele kuisaidia Serikali kuweza kuleta maendeleo kwa wananchi wake,” alisema Ahmada.Alisema serikali itaendelea kuhakikisha huduma za kifedha kwa pamoja na mawasiliano zinawafikia Wazanzibari wote kwa urahisi kabisa.Alisema katika kuhakikisha hilo linafanyika Serikali ya Zanzibar imeendelea kufanya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu hasa barabara, njia za mawasiliano na utengenezaji wa sera zilizo stahiki pamoja na kupigana na umasikini na ukosefu wa elimu kwa wananchi wa Zanzibar.Kuhusu huduma ya kibenki, alisema mteja wa Zantel atajipatia huduma mbalimbali za kibenki kwa njia ya simu kama vile kuweka na kutoa fedha, kulipia ankara za huduma mbalimbali kama vile maji, umeme au kununua vocha za simu, na hata kupata mikopo ya benki ambapo huduma hizo zote zinazingatia kanuni na misingi ya Kiislamu.Alitoa mwito kwa wananchi wa Pemba kuchangamkia fursa hizo adimu kutoka Zantel ambao wanashirikiana na Benki ya Watu wa Zanzibar ili kuendelea kujipatia maendeleo.Aitoa rai kwa uongozi wa Zantel na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kuhakikisha kuwa wananchi wa Pemba wanapata huduma hizo kwa wakati na kwa viwango vya hali ya juu.Naye Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin alisema uzinduzi wa huduma hizo mpya ni moja kati ya jitihada zinazofanywa na kampuni hiyo katika kutoa huduma zenye ubora nchini ili kutimiza mahitaji mbalimbali ya wateja wao. | Biashara | 1 |
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imesema haikusudii kuiondoa Kampuni ya Fastjet kufanya kazi zake nchini, badala yake inatakiwa kufuata masharti ya sheria za uendeshaji wa shughuli za usafiri wa anga ili kuepusha madhara, ikiwamo ajali.Kuhusu Mwenyekiti Mtendaji wa Fastjet, Lawrence Masha kujichagua kuwa Meneja Uwajibikaji, imeelezwa kuwa, kwa mujibu wa sheria, Meneja Uwajibikaji anapaswa kuwa na utaalamu wa masuala ya ndege na matengenezo.Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari, Dar es Salaam jana kutokana na kusambaa kwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mamlaka hiyo inalenga kuwaondoa Fastjet na kuipendelea ATCL.Taarifa hizo zilisambazwa kwenye mtandao wa Jamii Forums, pamoja na mazungumzo ya Mwenyekiti huyo Mtendaji wa Kampuni ya Fastjet, Masha kupitia kipindi cha Amka na BBC cha Shirika la Utangazaji la Uingereza. Johari alisema TCAA haiipendelei Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) na kuionya Fastjet kuwa isipokuwa makini katika kipindi hiki cha notisi ya siku 28, itakufa endapo hawatafanyia kazi upungufu wao. Aidha, imekiri kupokea barua pepe kutoka kwenye Kampuni ya Fastjet kuomba kuleta ndege mbili zenye usajili wa Afrika Kusini, andiko kuhusu uwezo wao kifedha kufanya biashara hiyo na barua ya kumtaja Meneja Uwajibikaji.Johari alisema wanataka kila shirika la ndege kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na kwamba hawana lengo la kuua mashirika hayo, kwa sababu wanataka ushindani wa kibiashara. Alieleza kuwa kazi ya kurusha ndege angani ikiwa na abiria ni hatarishi, hivyo ili kuhakikisha usalama wa abiria kuruka na kufika salama, inahitaji fedha pamoja na meneja uwajibikaji ambaye ana uelewa wa uendeshaji wa ndege, matengenezo na uzoefu wa menejimenti.Alisema Desemba 2008 iliifungia ATCL mpaka Januari 6, 2009 ndio ilikamilisha taratibu za kisheria na kuruhusiwa kuendelea na biashara hiyo, hivyo kitendo wanachokifanya ni kwa sababu sheria imewapa mamlaka hayo. Mkurugenzi huyo alisema Desemba 17, mwaka huu walitoa taarifa kwamba Fastjet imepoteza sifa kwa mujibu wa sheria pamoja na mabadiliko baada ya Waingereza kujitoa kuwekeza fedha katika kampuni hiyo.Alifafanua kuwa baada ya kuuzwa kwa hisa na wazawa kuchukua kampuni hiyo, kwa mujibu wa sheria inawataka ndani ya siku 14 kueleza kilichojiri ikiwemo uwezo wa kifedha kwa sasa, kumtaja Meneja Uwajibikaji baada ya aliyekuwepo kujitoa. “Fastjet mpaka sasa bado inadaiwa na mamlaka hii Dola za Marekani 156,000, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) inawadai shilingi bilioni 2.1, Kampuni ya Swissport inadai shilingi bilioni 2.1, Kampuni ya EYACO ya Mwanza inadai shilingi bilioni 1.1 na Kampuni ya Maendeleo ya Uwanja wa Ndege Kilimanjaro (KADCO) inadai shilingi milioni 286.Kwa mujibu wa kifungu cha 10 (1) (cha sheria ya mamlaka ya anga) kinaelekeza kwamba madeni yote yanayodaiwa kwa shirika yalipwe ndipo usajili ufutwe,” alisisitiza. Johari alieleza baada ya kutoa notisi hiyo, Fastjet iliwalipa TCAA Sh milioni 760 na Dola za Marekani 54,000 huku watoa huduma wengine wakiwa wanawadai, na kwamba ni matakwa ya sheria kulipa madeni hayo hivyo walizuia ndege zao ambazo zilitakiwa kurudishwa kwa mtu aliyezikodisha ili kufidia madeni.Kwa mujibu wake, hawakuizuia Fastjet kuingiza ndege nchini kwa sababu wanachotaka ni ushindani kwenye mashirika ya ndege na kwamba hivi karibuni kampuni hiyo ilitangaza kuleta ndege mbili aina ya Boeing 737- 500. Alisema katika maelezo yao wameeleza kuwa wataleta ndege hizo na mojawapo ni ile waliyoizuia kufanya kazi zake, pia waliandika maelezo ya fedha za kuendesha biashara kwa mujibu wa kifungu cha 25 (1) cha udhibiti uchumi cha Sheria ya Mamlaka ya Usimamizi wa Anga, na kupeleka barua ya kumchagua Masha kuwa Meneja Uwajibikaji.Akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu Masha kujichagua kuwa Meneja Uwajibikaji, Johari alisema kwa mujibu wa sheria, Meneja Uwajibikaji anapaswa kuwa na utaalamu wa masuala ya ndege na matengenezo na kwamba watapitia maelezo yake kuona kama anastahili au la. Pia alisema watapitia andiko kuhusu masuala ya fedha na kama hawatakidhi vigezo vyote vya kisheria hawatawasaidia kwa sababu wanaweza kusababisha ajali.Alisisitiza kuwa kabla ya mzawa kuchukua kampuni hiyo alishauriwa ni vitu gani anatakiwa kufanya na serikali inamsaidia mwekezaji kwa kumtaka afuate sheria na taratibu zilizowekwa. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye alisema TCAA inafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria, na sio lengo la kuondoa kampuni binafsi kufanya kazi hizo. Simbeye alisema mwaka 2015 sekta binafsi walivyokutana na Rais John Magufuli moja ya maelekezo aliyoyatoa ni sekta binafsi kuwekeza kwa wingi kwa kufuata sheria na kulipa kodi. Aliongeza kuwa ni lazima wawekezaji wazawa kufuata sheria kwa sababu hakuna nchi inayofanya uwekezaji bila kufuata sheria. Jana, vyombo vya habari hasa magazeti yalimkariri Masha mwenye asilimia 68 ya hisa za Fastjet Tanzania, akiiomba TCAA imruhusu kuingiza ndege kisha kulipa madeni baada ya kufanya biashara. Alisema madeni hayo aliyakuta baada ya kununua hisa za kampuni hiyo ya usafiri wa anga. | Kitaifa | 0 |
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga amesema udanganyifu ni tatizo kubwa linalokabili mfuko huo na kwamba hadi sasa wameweza kuokoa Sh bilioni 4 ambazo zingeliwa na wajanja kwa udanganyifu. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga kwenye kikao cha mfuko huo na wahariri, kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam juzi. Mbinu zinazotumika katika udanganyifu huo ni baadhi ya watoa huduma kuongeza gharama za matibabu kwa wenye kadi za NHIF, au kutumia kadi za NHIF kujipatia fedha katika maduka ya dawa au kuchelewesha kuwapatia huduma wenye kadi za NHIF ili baadaye kufanya udanganyifu. Ili kupambana na udanganyifu huo, Konga alisema kwanza wameanzisha kitengo cha kupambana na udanganyifu (fraud) na kina wataalamu mbalimbali, wakiwamo madaktari. Pili, wameamua kushirikisha taasisi za uchunguzi kupambana na udanganyifu huo, kama vile Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Polisi na vyombo vya usalama.Tatu, aliviomba vyombo vya habari kusaidia kuweka wazi tatizo hilo kwa jamii ili wananchi na watoa huduma waepukane nalo. Kuhusu idadi ya wanachama walio nao, Konga alisema NHIF imejipanga kuongeza wanachama kutoka asilimia 32 ya sasa hadi kufikia asilimia 70 mwaka 2020 na baadaye kuwezesha Watanzania wote kunufaika na bima ya afya.Aidha, alisema mfuko huo umetoa mikopo mingi ya vifaa tiba, dawa, vitendanishi na ukarabati wa majengo. Alizungumzia pia suala la utafiti, ambapo alisema NHIF inaendelea kufanya utafiti ili kuongeza vifurushi, huduma na vituo vinavyohitajika. Pia, alisema wanafanya utafiti wa programu mpya ya Tehama, itakayowezesha wateja kujua aina ya dawa, matibabu na gharama zake. Alisema NHIF imeingia mkataba na vituo 7,000 nchini vya kutolea huduma na vingi ni vya serikali. Aidha, wahariri hao walisimama kwa dakika moja, kukumbuka kifo cha aliyewahi kuwa Meneja Mawasiliano wa mfuko huo, Rehani Athumani kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwa miaka mingi kwa mfuko huo. | Kitaifa | 0 |
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kuanzia saa 2:00 usiku.Ni mchezo mgumu na muhimu kwa timu zote kushinda kwani atakayepata matokeo mazuri ndiye atakayesonga mbele hatua ya nusu fainali. Azam Complex inapewa nafasi ya kusonga mbele kutokana na sababu zifuatazo.Mara nyingi inapocheza kwenye uwanja wa nyumbani hupata matokeo mazuri lakini pia, timu hiyo bado ipo kwenye kiwango bora kwani ipo kwenye mbio za ubingwa wa ligi.Kadhalika, Mtibwa Sugar ina nafasi kutokana na kwamba ni timu isiyotabirika kwani mwanzoni mwa msimu huu raundi ya kwanza walionekana wako vizuri kiasi cha kuzitisha timu kubwa ingawa baadaye walikuja kuanguka na kushuka.Ikumbukwe kuwa katika mchezo wa raundi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.Hivyo, yeyote ana nafasi kutokana na namna atakavyojiandaa.Katika mechi sita tofauti kwa kujumuisha ligi na FA kwa timu zote, kati ya hizo kwa upande wa Azam imeshinda nne na kupata sare mbili huku Mtibwa kwa idadi hiyo ya mechi, ikishinda mchezo mmoja pekee, ikifungwa nne na kupata sare moja.Kwa kutizama matokeo hayo inaonesha ni jinsi gani Azam wako vizuri kuliko Mtibwa ingawa hata hivyo, dakika 90 ndizo zinazoweza kutoa mshindi. Mchezo mwingine utakaochezwa leo ni Tanzania Prisons wakiikaribisha JKT Tanzania kwenye uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.Prisons wana nafasi ya kusonga mbele kwa maana kama wataweza kutumia uwanja wa nyumbani vizuri lakini pia, ni miongoni mwa timu zilizoonesha kiwango bora msimu huu ikiwa inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.Hata JKT ina nafasi ya kufanya vizuri kwani ina kocha mzoefu wa ligi, Bakari Shime ambaye aliiongoza timu hiyo kupanda Ligi Kuu msimu huu ikiwa ni miongoni mwa timu zilizotikisa Daraja la Kwanza msimu huu. | michezo | 2 |
MCHUNGAJI wa Kanisa la Gospel Revival Center (GRC), lililopo Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam, Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ amewataka Watanzania kumpa muda Rais John Magufuli katika kazi yake ya kuliunganisha taifa na kuleta maendeleo na kwamba watahoji utendaji wake mara baada ya kutoka madarakani.Amesema kuwa demokrasia ipo nchini na kwamba endapo serikali itaruhusu kufanyika kwa maandamano ya mara kwa mara hakutakuwa na nchi ya amani kama ilivyo sasa.Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mchungaji Lusekelo amesema kutokana na miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa nchini, Tanzania itakuwa miongoni mwa nchi ambazo wananchi wake watakuwa na maisha mazuri.Alisema Rais Magufuli amesaidia kuipeleka nchi mahali salama katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio ya ujambazi nchini.Alisema kuwa baada ya kuingia madarakani, hakuna udini, ukanda wala ukabila na badala yake watoto wa masikini wanasomeshwa kupitia kodi za matajiri ambazo wanalipa kutokana na biashara mbalimbali.‘’Sio kwamba najipendekeza kwa kutaka Ukuu wa Wilaya au Mkoa lakini nataka kuwaambia kuwa siwezi kuona aibu kusema mema anayoyafanya kiongozi wowote kwani hata katika maandiko matakatifu yanatuelekeza kuwa ni mwiko kumsema vibaya mkuu wa nchi yako,’’ alisema Lusekelo.Aliongeza kuwa ni lazima apewe nafasi afanye kazi kwa mujibu wa sheria, katiba, mila na desturi za Kitanzania na kwamba watamhoji utendaji wake baada ya kukamilisha uongozi wake kama wanavyofanya kwa viongozi waliopita.Alifafanua, Rais amehakikisha kunakuwapo muungano imara wa Tanganyika na Zanzibar ambao haupaswi kufanyiwa biashara wala kugusa misingi yake, na badala yake kama kuna maboresho wanapaswa kuzungumza kwa hekima.Pia alisema yapo mabadiliko makubwa yanaendelea kufanyika nchini ikiwemo masuala ya usafiri wa anga kwa kusaidia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kuwa na ndege nane na kutumia fedha za ndani kununua zao la korosho.‘’Tungepata Magufuli kama 30 hivi nchi ingenyooka lakini tunapaswa kusema asante kwa kiongozi huyu kwa sababu ndiye ambaye Mungu ametuletea. Mnaweza msione matokeo ya uongozi huu kwa saa lakini baadaye mtasema asante Yesu,’’ alisisitiza mchungaji huyo.Akijibu maswali ya waandishi kuhusu demokrasia nchini, Lusekelo alisema kuwa kwa mara ya kwanza alishuhudia Watanzania milioni sita wakiwapigia kura wapinzani na kwamba wapo wabunge na madiwani wengi kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF) na vyama vingine.Alieleza uwepo wa wawakilishi hao wa vyama vingi inamaanisha kuwa demokrasia ipo na hivyo ni lazima kuwepo wakati wa kusema na kunyamaza na wakati wa kusema na kutekeleza mambo mbalimbali. | Kitaifa | 0 |
Waziri Mwakyembe ametoa ojnyo hilo mjini Kigoma wakati anafunga mafunzo ya ngazi ya chini (Grass Root) ya ualimu wa mpira wa miguu kwa walimu kutoka shule za msingi na sekondari, ikiwa ni programu ya kuibua vipaji kuanzia ngazi za chini.Alisema amekuwa akipitia video zilizofungwa katika uwanja huo na kuona baadhi ya watu wakionekana kunyunyuzia dawa kwa maana ya kuroga ili kupata ushindi na kusema kuwa vitendo hivyo lazima vikomeshwe na adhabu kali zitatolewa.Waziri huyo wa michezo alisema kuwa sambamba na viongozi wa klabu na wapenzi wao pia serikali itachukua hatua kali kwa viongozi wa vyama vya soka watakaojihusisha na vitendo hivyo ikiwemo kusafiri na waganga nje ya nchi kwa nia ya kupata ushindi.Aidha Waziri huyo alisema kuwa serikali inasikitishwa na kilio cha gharama kubwa ya kuingiza vifaa nchini kinachotolewa na uongozi wa TFF na kwamba ameamua kulisimamia jambo hilo kwa kulifikisha kwa Waziri wa Fedha ili kuona namna ya kusaidia kuondoa kodi katika uingizaji wa vifaa vya michezo nchini.Alisema, vifaa ni muhimu katika mazoezi na maandalizi ya michezo na kwamba kilio cha muda mrefu katika hilo lazima kipatiwe ufumbuzi sasa kwa kulifikisha jambo hilo kwa Waziri wa Fedha na kumshauri namna ya kulishughulikia. | michezo | 2 |
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amekuwa mbogo kwa watendaji wanaochelewesha ugawaji na usambazaji vitambulisho vya wajasiriamali katika maeneo yao mkoani humo. Dk Mahenge alisema hayo baada ya kutembelea halmashauri mbalimbali, kukagua namna vitambulisho hivyo vilivyotolewa kwa wajasiriamali na Rais John Magufuli Desemba 10, mwaka jana vinavyosambazwa kwa wajasiriamali wadogo. Hali ya usambazaji au ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali katika halmashauri hizo mkoani humo, haujashika kasi kubwa, hivyo aliwataka watendaji hao kuongeza kasi ili kufikia lengo la kukamilisha vitambulisho hivyo. Mkuu wa Mkoa alifanya ziara katika halmashauri za Chamwino, Kongwa, Kondoa na ziara bado inaendelea katika maeneo mengine ili kuhakikisha usambazaji wa vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo unakamilika mapema. Akiwa katika ziara wilayani Kondoa, Dk Mahenge aliwataka watendaji kuharakisha usambazaji wa vitambulisho hivyo kwa wananchi na viongozi wanatakiwa kuhamasisha wananchi kuvichukua. Alitawaka watendaji kuongeza kasi kugawa vitambulisho lakini kusimamia na kuhakikisha kwamba wajasiriamali wasio na vitambulisho hivyo hawaruhusiwi kufanya biashara au shughuli zozote. akiwa wilaya ya Chamwino, Dk Mahenge alimtaka Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Athuman Masasi kuharahakisha usambazaji wa vitambulisho hivyo vya wajasiriamali, badala ya kufanya kazi bila kuwa na vitambulisho. Mkuuu wa Mkoa wa Dodoma alikabidhiwa na Rais Magufuli vitambulisho vya wajasiriamali 25,000, ambavyo alivigawa katika halmashauri zake kwa uwiano wa wingi wa idadi ya watu katika wilaya hiyo. Katika mgawanyo huo, Jiji lilipata vitambulisho 5,000, Chamwino 4,000, Kongwa 3,750, Mpwapwa 3,500, Bahi na Chemba zote zilipata vitambulisho 2,750 kila moja, Kondoa Mji 2,500 na Kondoa Vijijini 750. Vitambulisho vilivyogawiwa Dodoma ni sehemu ya vitambulisho vya wajasiriamali 670,000 nchini alivyovigawa Rais Magufuli kwa wakuu wa mikoa Desemba 10, mwaka jana. Vitambulisho hivyo jijini Dodoma vinatolewa katika jengo la bima, Chamwino katika jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya, Bahi katika jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya, Kondoa katika jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya, Kongwa katika jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya, Mpwapwa katika engo la ofisi ya mkuu wa wilaya na Chemba katika jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya. | Kitaifa | 0 |
SIMBA, leo inatarajiwa kukabidhiwa taji lake la Ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya mechi dhidi ya Biashara United itakayofanyika kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Mechi hiyo ni ya 37 kwa Simba ambayo imeshatangaza ubingwa tangu wiki iliyopita ilipoifunga Singida United mabao 2-0 na kufikisha pointi 91 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa Karume Musoma, Simba ilichomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Biashara hivyo ni kazi kwao kuendeleza ubabe dhidi ya timu hiyo ngeni kwenye Ligi Kuu au Biashara kupindua matokeo ili kujiweka salama zaidi kubaki msimu ujao.Ugumu wa mechi ya leo unatokana na Simba kutana kukabidhiwa kombe lake kwa heshima kwani msimu uliopita ilikabidhiwa kwa kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja huohuo wa Taifa, hivyo haitakubali kurudia kosa, huku Biashara ikitaka ushindi kujiweka vizuri zaidi kubaki msimu ujao.Biashara wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa wanashika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi hiyo baada ya kufikisha pointi 43 na kumbukumbu ya kutoka kuibuka na ushindi kwenye mchezo ulipita kwa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting.Kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema kubeba ubingwa haimaanishi kwamba kazi imeisha hivyo wanahitaji ushindi katika michezo yote iliyosalia ili watwae ubingwa na pointi nyingi. Katika hatua nyingine kocha huyo amezungumzia mechi dhidi ya Sevilla waliyofungwa mabao 5-4 juzi akisema alilazimika kufanya mabadiliko ya wachezaji kwa lengo lakuwapa wachezaji fursa kutengeneza historia ya kucheza na timu kubwa.Alisema kila mchezaji alikuwa anahitaji kucheza na timu hiyo kubwa inayocheza ligi kubwa hivyo aliona ni busara kila mmoja acheze kwa kuwa ushindi haukuwa kipaumbele chao zaidi ya kuwapa wachezaji fursa wapate changamoto ya kujifunza. Kocha huyo amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya mashabiki waliojitokeza kuisapoti timu hiyo kulitupia lawama benchi la ufundi kwa kufanya mabadiliko yaliyopelekea kikosi hicho kupoteza mchezo. | michezo | 2 |
['Tunisia iliishinda Ghana kupitia mikwaju ya penlati na kutinga robo fainali michuano ya Afcon dhidi ya Madagascar.', 'Mlinda lango Farouk Ben Mustapha ndiye aliyekuwa shujaa baada ya kuingia na kuokoa mkwaju wa penalti wa Caleb Ekuban.', 'Tunisia ilikuwa imekaribia kushinda ilipofikia dakika ya 90 kabla ya beki wa ziada Rami Bedoui kujifunga kupitia kichwa dakika za lala salama alipogusa mpira kwa mara ya kwanza.', 'Wakati huohuo Wilfried Zaha alifunga goli la ushindi na kuisaidia Ivory Coast kuilaza Mali 1-0 ili kutinga robo fainali ya michuano ya Afcon.', 'Mshambuliaji huyo wa Crystal Palace ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Arsenal aliufukuza mpira wa adhabu uliopigwa na Sylvain Gbohouo na kuupata kabla ya kipa Djigui Diarra. ', 'Mali ilikuwa imepoteza nafasi chungu nzima kupitia Moussa Marega na Moussa Djenopo, wote wakikosa nafasi nzuri baada ya pasi safi. ', 'Ivory Coast sasa itacheza dhidi ya Algeria katika mechi ya robo fainali siku ya Alhamisi. ', 'Ndovu hao wameibuka washindi wa komnbe hilo mara mbili mwaka 1992 na 2015 lakini walisonga mbele katika raundi ya muondoani wakiwa katika nafasi ya pili baada ya kushindwa 1-0 na Morocco. ', 'Tunisia ilikuwa inaongoza kupitia goli la mshambuliaji wa IsmailiaTaha Yassine Khenissi aliyepata krosi nzuri kutoka kwa Wajdi Kechrida.', 'Mshambuliaji wa Leeds Ekuban ndiye mchezaji wa pekee aliyekosa mkwaju wake katika penalti hizo huku Ferjan Sassi akifunga goli la ushindi. ', 'Tunisia sasa itakabiliana na Madagascar iliopo katika nafasi ya 108 duniani siku ya Alhamisi licha ya kutoshinda mechi hata moja katika dakika 90. ', 'Mwewe hao walitoka sare mechi zao zote tatu kabla ya mikwaju hiyo ya penalti dhidi ya Ghana. ', 'The Black Stars walitawala kipindi cha mwanzo cha mchezo huku shambulio la kichwa la Nuhu Kassim likigonga mwamba wa goli. ', 'Walipata bao la kwanza lakini likakataliwa . Thomas Partey alimpigia pasi Jordan Ayew ambaye naye alitoa pasi murua kwa nduguye Andre na kufunga kupitia kisigino. ', 'Refa aliamuru kwamba Partey alikuwa ameunawa huku refa wa kutumia Video VAR akitarajiwa katika mechi za robo fainali, lakini kiungo huyo wa Atletico alikuwa ameuzuia mpira huo kwa kifua. ', 'Tunisia ilitawala mechi wakati Wahbi Khazri ambaye alikuwa na jeraha alipoingia kunako dakika ya 68. ', 'Muda mfupi baadaye kona yake iligonga mwamba wa goli kupitia kichwa cha Khenissi. ', 'Hatahivyo bahati ya Tunisia ilisimama wakati Khazri alimpigia pasi ya kisigino Kechrida ambaye krosi yake ilifagiliwa hadi wavuni na Khenissi. ', 'Shambulio la kiungo wa Ghana Mubarak Wakaso lilipanguliwa kabla ya kuchangia katika bao la kusawazisha. ', 'Beki Bedoui aliingia katika nafasi ya Khenissi katika dakika ya mwisho ili kuongeza ulinzi-lakini alifunga mkwaju wa adhabu wa Wakaso hadi wavuni mwa goli la Tunisia. ', 'Pande zote mbili zilikuwa na fursa dakika za lala salama -lakini zilishindwa kuzitumia hivyobasi mechi ikaishia kuamuliwa kupitia mikwaju ya penalti.'] | michezo | 2 |
KOCHA wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Emanuel Amunike ametangaza kikosi cha wachezaji 25 kitakachocheza na Uganda katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon 2019) mchezo utakaochezwa Septemba 8 kwenye Uwanja wa Namboole Kampala, Uganda.Akizungumza jana, Amunike alisema timu hiyo itaingia kambini Agosti 27 na kwa kushirikiana na wasaidizi wake kocha Emeka Amadi na Hemed Morocco watajitahidi kufanya kile ambacho Watanzania wanatarajia. “Najua Watanzania wana imani na sisi na mimi ni sehemu ya Tanzania kwa sababu ninakula chakula cha hapa na ninakunywa maji ya hapa, hivyo tutajitahidi kuhakikisha timu inafanya vizuri ila siwezi kusema tutafanya maajabu,” alisema Amunike.Kikosi kilichoitwa ni makipa Aishi Manula (Simba), Mohammed Adbulrahman (JKU) na Benno Kakolanya (Yanga). Walinzi ni Shomari Kapombe (Simba), Hassan Kessy (Nkana FC Zambia), Gadiel Michael (Yanga), Kelvin Yondan (Yanga), Abdi Banda (Baroko FC Afrika Kusini), Aggrey Morris (Azam FC) na Andrew Vicent (Yanga).Viungo wakabaji ni Himid Mao (Petrojet Misri), Mudathir Yahya (Azam FC), Jonas Mkude (Simba) na Erasto Nyoni (Simba) Viungo washambuliaji ni Simon Msuva (Al Jadida Morocco), Shiza Ramadhani (Simba) Rashid Mandawa (DBF Botswana), Hassan Dilunga (Simba), Feisal Salum (Yanga) na Farid Mussa (Tenerife Hispania) Washambuliaji ni Mbwana Samatta (Genk KRC Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (Al Hilal Sudan), Shaban Idd (Tenerife- Hispania), Yahya Zayd (Azam FC) na John Bocco (Simba) Kwa sasa Uganda Cranes inaongoza Kundi L ikiwa na pointi tatu baada ya kuifunga Cape Verde bao 1-0 na Tanzania na Lesotho zina pointi moja baada ya kutoka sare ya bao 1-1 nyumbani. Amunike amesema kwamba katika kukinoa kikosi hicho, atasaidiwa na Mnigeria mwenzake, Emeka Amadi pamoja na Mzalendo, Hemed Suleiman ‘Morocco’. | michezo | 2 |
Aidha kampuni hiyo iliyopo chini ya Kampuni ya Toyota Tanzania Limited imeamua kupunguza bei ya pikipiki zake aina ya Yamaha kwa lengo la kuwavutia vijana wengi na kuunga mkono jitihada za serikali za kuongeza ajira kwa vijana kupitia biashara ya bodaboda ambayo imesaidia vijana wengi kujiajiri na kuepuka kujitumbukiza kwenye matukio ya uhalifu.Meneja wa kampuni hiyo tawi la Arusha, Meetal Shah alisema kampuni yake imefikia hatua hiyo ikiwa ni sehemu ya kuchangia ajira kwa vijana kupitia biashara ya bodaboda.“Tunachokifanya ni kuwaunganisha wateja wa pikipiki wasio na fedha taslimu na benki ambazo zimekubali kuwakopesha kwa riba nafuu na sisi kama Kampuni ya City Motors tutawapatia pikipiki na benki ndiyo itakayotulipa sisi, ’’alisema Shah.Kwa upande wa waendesha pikipiki, John Jumanne (39) mkazi wa Sombetini aliyepatiwa pikipiki aina ya Yamaha kupitia mpango huo, ameishukuru kampuni hiyo ya City Motors kwa kueleza kuwa kabla ya hapo alikuwa akiendesha pikipiki ya mtu kwa makubaliano ya kumlipa Sh 7,000 kwa siku na hivyo kujikuta akibakiwa na fedha kidogo ambazo hazitoshelezi kutunza familia yake. | Biashara | 1 |
MSIMU mpya wa Coke Studio Africa umezinduliwa rasmi Tanzania katika hafla iliyofanyika klabu ya burudani ya Lifepark Mwenge mwishoni mwa wiki iliyopita.Mkurungezi Mkuu wa Coca-Cola Kwanza, Basil Gadzios amekiri kufurahishwa na vipaji na uwezo wa wasanii Watanzania watakaoshiriki kwenye msimu huu mpya. Tanzania itawakilishwa na wasanii tano watakaotumbuiza katika msimu wa sita wa Coke Studio.Mkurugenzi wa mauzo na masoko wa Coca-Cola Kwanza, Josephine Msalilwa, aliwatambulisha wasanii watakaowakilisha kwenye msimu huo ni Faustina Charles’ Nandy’, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Rajabu Abdul ‘Harmonize’, Juma Jux na Mimi Mars.Amesema wasanii hao wataungana na wasanii wengine 20 kutoka nchi mbalimbali za Afrika na kutimiza idadi ya wasanii 25.“Nchi nyingine msanii huchukuliwa mmoja lakini kwa Tanzania imekuwa tofauti kidogo, hii yote inaonesha ni namna gani muziki Watanzania yaani bongo fleva umekuwa ukikubalika na wasanii wake kupendwa,” amesema.Kwa upande wao wasanii akiwemo Rayvanny alishukuru kuwa mmoja wa wasanii watakaotumbuiza katika msimu huu huku akieleza hii ni mara yake ya pili.Nandy amesema “kushiriki Coke Studio kunakusaidia kukutana na wasanii kutoka Afrika wenye vipaji lukuki... nafasi hii kwa msanii yeyote ni kitu cha kujivunia sana na pia inasaidia kutengeneza kazi tofauti na kufanya jina au brand ya msanii kuimarika na nguvu katika soko la muziki Afrika na dunia nzima.”Jux amesema Coke Studio ni kitu kikubwa, na hakuwahi kutarajia kukutana na msanii mkubwa kama Skales kutoka Nigeria ambaye ameurudia wimbo wa Ninogeshe na kumuelezea kuwa ni msanii ambaye ana ushirikiano mzuri. | michezo | 2 |
Mabao hayo yalifungwa kipindi cha pili na Zablon Raymond na Frank Wanchope yameifanya Mnadani FC kucheza na Itezi FC ya Mbeya kutafuta mshindi wa tatu baada ya kufungwa na Goms United ya Dar es Dar es Salaam pia.Fainali inatarajiwa kuchezwa kesho kwenye Uwanja wa Bandari, Dar es Salaam, mchezo ambao ni wa kulipa kisasi kwani Goms imepania kufuta uteja kwa Misosi ambayo iliwafunga kwa penalti 5-4 na kutwaa ubingwa wa Ndondo mkoa wa Dar es Salaam mwaka jana.Akizungumza baada ya mechi hiyo juzi, kocha wa Goms United, Shaban Kazumba alisema wamejiandaa kulipa kisasi kwa sababu msimu uliopita walipoteza mchezo katika mazingira ambayo wanajuta hadi leo hivyo kila mtu anajua mashabiki wanataka nini.“Tulianza kufunga bao lakini Misosi walisawazisha tukalazimika kuingia kwenye mikwaju ya penalti tukafungwa hali ambayo iliwasononesha mashabiki wetu,” alisema Kazumba.Michuano ya Ndondo Super Cup ilianza mwishoni mwa wiki iliyopita kwa mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Bandari, Temeke | michezo | 2 |
JIJI la Dodoma limetenga maeneo matatu kwa ajili ya kuwaweka wafanyabiashara wadogo wanaopanga biashara zao barabarani. Ofisa Masoko wa Jiji la Dodoma, James Yunu akizungumza na gazeti hili alisema maeneo hayo yaliyotengwa ni pamoja na pembeni ya soko la sabasaba ambalo ndio stendi kubwa ya mabasi yanayozunguka maeneo mbalimbali ya jiji.“Maeneo mengine ambayo jiji limetenga ni pamoja na soko la Bonanza karibu na Chang’ombe na eneo la karibu na Soko la Dk Rehema Nchimbi,”alisema. Alisema mkakati huo wa soko unawalenga wafanyabiashara ndogo 150 waliojiandikisha awali, hata kama idadi yao inazidi kuongezeka kutokana na watu wengi kuhamia jijini humo.Yunu alisema mkakati huo ambao umewekwa na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi unalenga kuhamisha wafanyabiashara ndogo wanaopanga bidhaa zao barabarani.Kunambi alitoa agizo hilo kwa ofisa biashara huyo kuhakikisha ndani ya muda mfupi wafanyabiashara ndogo waliozagaa pembeni ya barabara wanaondolewa. Lengo la kuwaondoa ni kuhakikisha jiji linakuwa safi, linakuwa katika mpango mzuri wa namna ya kufanya biashara yaliyotengwa kwa ajili ya wafanyabiashara hao wadogo.“Pia wanalenga kuhakikisha kwamba mazingira ya jiji, ikiwemo mitaa na barabara zinatunzwa vizuri kwa ajili ya matumizi ya watu mbalimbali wala si kwa ajili ya biashara,”alisema.Alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara ndogo jijini hapa kufanya biashara pembeni ya barabara, hivyo kuzuia magari na wapita njia, jambo ambalo linaleta kero kwa wapitaji.Kutokana na serikali kuhamia Dodoma, jiji hilo limekuwa katika mkakati mahususi wa kupanga jiji lake na kuacha maeneo ya barabara na yasiyotakiwa kufanya shughuli zozote. Jiji la Dodoma lilishafanya mpango mwingine mara baada ya kuwaondoa wafanyabiashara katika maeneo ya Jamatini ambao walikwenda Makole na eneo la Sabasaba. | Kitaifa | 0 |
MARAIS Dk John Magufuli na Profesa Arthur Peter Mutharika wa Malawi wamekubaliana kwa pamoja kukuza uchumi wa nchi zao.Akiwa nchini humo, Rais Magufuli jana alifungua msimu wa soko la tumbaku na kusema nchi za Afrika zina haja ya kufanya mapinduzi kwenye sekta ya kilimo, kwa kuanzisha viwanda vya usindikaji vitakavyoongeza thamani mazao na kuokoa uharibifu wa asilimia 40, ya mazao yanayovunwa na kukosa mahali pa kuhifadhia. Kauli hiyo ya Rais Magufuli aliitoa jana mjini Lilongwe nchini humo, ikiwa ni siku ya pili na ya mwisho ya ziara yake aliyoifanya kutokana na mwaliko wa Rais wa Malawi, Profesa Arthur Peter Mutharika.Akizungumza kabla ya kufungua rasmi msimu huo, Rais Magufuli alisema uchumi wa Bara la Afrika kwa asilimia kubwa unategemea sekta ya kilimo na kwamba nusu ya watu wake wameajiriwa kwenye sekta hiyo huku pia nchi hizo zikitegemea kilimo kwa usalama wa chakula, lakini bado kinatekelezwa kwa njia duni. Alisema nchini Malawi asilimia 80 ya wananchi wake wanategemea kilimo kupata ajira huku asilimia 60 ya fedha za kigeni zinatoka kwenye mazao na asilimia 37 ya Pato la Taifa hilo hutegemea kilimo hivyo kuna haja ya kufanya mapinduzi makubwa kwenye sekta hiyo kwa kufungua zaidi viwanda vya usindikaji ili kuongeza thamani mazao.Rais Magufuli pia alitoa mfano kwa Tanzania akisema kilimo kinategemewa kwa asilimia 100 kwenye usalama wa chakula, lakini pia asilimia 70 ya wananchi wanategemea ajira huku malighafi za viwandani ikitegemewa kwa asilimia 60. Aidha, kilimo kina mchango kwenye fedha za kigeni ambako asilimia 25 za fedha hizo hutokana na mazao ya kilimo, huku pia pato la nchi likitegemea kilimo kwa asilimia 30 na kusema hiyo inathibitisha kuwa kilimo barani Afrika ni sekta muhimu ya kukuza uchumi inayohitaji kufanyiwa mapinduzi makubwa.Akizungumzia zao la tumbaku, Rais Magufuli alisema zao hilo sio tu muhimu nchini Malawi, bali pia Tanzania kwani ni miongoni mwa mazao yanayoingiza fedha nyingi za kigeni na kutolea mfano kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo, kuanzia 2014 zaidi za Sh bilioni 1.33 zimetokana na zao hilo. Kwa upande wa Malawi, alisema kwa msimu uliopita nchi hiyo imepokea dola za Marekani milioni 300 kwa mauzo ya tumbaku na fedha hizo zingeweza kuongezeka maradufu iwapo wangekuwa na viwanda vya kusindika zao hilo.“Msimu uliopita nimeambiwa ulipata dola milioni 300 kwa mauzo ya tumbaku, sasa kama tungekuwa na viwanda vya usindikaji ina maana tungepata fedha nyingi zaidi, kuliko kuuza malighafi, tunahitaji mageuzi kwenye kilimo na nyie nasikia mmeanza, ni vizuri hongereni,” alisema Rais Magufuli. Kuhusu changamoto za kilimo, Rais Magufuli alisema bado Afrika inakabiliwa na matumizi madogo ya pembejeo, mbinu za zamani za kilimo na matumizi madogo ya mbolea na zana za kisasa hivyo tija haiongezeki.Alisema mbali na changamoto hiyo, pia kuna ukosefu wa maghafa ya kutosha ya kuhifadhi mazao baada ya kuvunwa, takwimu zikionesha asilimia 40 ya mazao yaliyovunwa huharibika kwa kukosa maghala ya kuhifadhia. Aidha, Rais Magufuli alitaja changamoto nyingine kwenye kilimo kuwa ni ukosefu wa masoko ya mazao kwa sababu kilimo cha Afrika kwa asilimia kubwa kinategemea masoko ya kimataifa ambayo bei zake hazitabiriki na wakati mwingine hazina faida kwa mkulima. | Kitaifa | 0 |
KAZI ya kutandaza mabomba ya gesi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwa Mkoa wa Lindi inatarajia kuanza mwisho wa mwezi huu.Hayo yamebainishwa bungeni na Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kuteuliwa, Salma Kikwete (CCM), aliyetaka kujua ni lini wananchi wa Lindi watafikishiwa huduma ya gesi nyumbani.“Katika swali la msingi, inaonesha utekelezaji mradi ya usambazaji wa gesi nyumbani kwa mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara, lakini sijasikia kuhusu Mkoa wa Lindi, je ni lini wananchi wa Lindi watafikiwa na huduma hiyo?” amehoji Salma.Amesema kwa upande wa Mkoa wa Lindi kazi ya kutandaza mabomba ya kusambaza gesi nyumbani itaanza mwisho wa Mei.Hivi karibuni, Dk Kalemani ameagiza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuhakikisha inaongeza kasi ya kusambaza gesi ya kupikia ili angalau robo ya nyumba za Jiji la Dar es Salaam ziwe zimefikiwa na huduma hiyo ndani ya miaka mitatu ijayo.Awali, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema kwa sasa TPDC inaendelea na utekelezaji wa mradi kwa kuagiza na kujenga miundombinu ya usambazaji wa gesi asilia majumbani, viwandani na katika taasisi mbalimbali kwa mikoa ya Mtwara, pwani na Dar es Salaam. Mgalu alikuwa akijibu swali la msingi la Mbunge Newala Vijijini, Rashidi Akbar (CCM) aliyeuliza:“Takwimu zilizopo zinaonesha kuwa gesi kutoka Mtwara na Songosongo inatumika kwa asilimia sita tu, je, kwanini kiwanda cha saruji cha Dangote na Mtwara Cement mkoani Mtwara havijapatiwa umeme wa gesi asilia hadi leo.Pia aliuliza, je, kwa nini wananchi wa Mtwara wasiunganishiwe gesi asilia kwenye nyumba zao?Akijibu maswali hayo, Mgalu alisema awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza gesi asilia mkoani Mtwara imeshaanza ambapo kwa sasa kazi ya ununuzi wa mambomba, mita za kupima gesi pamoja na vifaa vya kupunguza mgandamizo wa gesi inaendelea.“Inategemea zaidi kata 120 za awali zitaunganishiwa mabomba ya gesi mkoani Mtwara kwa matumizi ya nyumbani ifikapo Juni mwaka 2019,” alisema Mgalu.Kuhusu viwanda vya Dangote na kiwanda cha saruji cha Mtwara kuunganishiwa umeme, Mgalu alisema kwa sasa kiwanda cha saruji cha Dangote kimeunganishiwa na miundombinu ya gesi asilia ambapo awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa kuwezesha matumizi ya gesi asilia kuzalisha umeme kwa ajili ya kiwanda cha Dangote ilikamilika na kuanza kufanya kazi Agosti, 2018.“Hadi kufika Aprili mwaka 2019, Kiwanda cha Dangote kiemanza kutumia wastani wa futi za ujazo milioni 5 kwa siku kwa kuzalisha umeme,” amesema.Amesema awamu ya pili ya mradi ilikamilika Desemba 2018 na sasa Kiwanda cha Dangote kinatumia gesi ya wastani wa futi za ujazo milioni 15 hadi 20 kwa siku kwa ajili ya uzalishaji wa saruji. “Jumla ya gharama za mradi ni Shilingi bilioni 8.2,” amesema Mgalu. | Kitaifa | 0 |
HOMA ya ugonjwa wa dengue imeendelea kutikisa mikoa ya Dar es Salaam na Tanga ambapo mpaka sasa watu zaidi ya 2,900 wamethibitika kuugua ugonjwa huo, katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Mei mwaka huu.Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto jana, wagonjwa wawili walipoteza maisha kwa dengue iliyoendelea kuitesa Dar es Salaam na Tanga.Ili kuepukana na madhara, serikali imesema wananchi wanaweza kujikinga na ugonjwa huo kwa njia mbalimbali ikiwemo kufukia madimbwi ya maji yaliyotuama au kunyunyizia dawa ya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi, kuondoa vitu vinavyoweza kuweka mazalia ya mbu, vifuu vya nazi, makopo na magurudumu ya magari.Njia nyingine za kujikinga na dengue ni kufyeka vichaka karibu na makazi, kufunika mashimo ya maji taka, kutumia dawa za kufukuza mbu, kuvaa nguo ndefu, kutumia vyandarua vyenye viuatilifu na kuweka nyavu madirishani na milangoni.Hata hivyo, serikali imesema idadi ya wanaougua ugonjwa huo imeendelea kupungua ikilinganishwa na wiki mbili zilizopita ambapo kwa wastani wagonjwa walioripotiwa kwa wiki walikuwa 525 ikilinganishwa na wagonjwa 420 kwa wiki kwa sasa na juhudi za kuudhibiti zaidi zinaendelea.“Wananchi zipuuzeni taarifa za kwenye mitandao ya kijamii zikiwemo video zinazosadikiwa kuwa ni za miaka ya nyuma zenye taarifa za upotoshaji ambazo zilitolewa ufafanuzi,” ilisema wizara.Pamoja na kwamba ugonjwa huo umeendelea kutishia maisha ya watu, wizara imesema homa ya dengue siyo ugonjwa mpya kwa kuwa hujitokeza nyakati za mvua sehemu mbalimbali duniani. Ilisema mwaka 2016 watu milioni 390 waliugua ugonjwa huo ikilinganishwa na watu milioni 216 waliougua malaria katika mwaka huo 2016.Wiki moja na nusu iliyopita, Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Kambi, alisema idadi ya wagonjwa waliothibitishwa kuwa na virusi vya homa hiyo au kuwahi kuugua ilikuwa 1,901 kipindi kuanzia Januari hadi Mei 15 mwaka huu.Alisema serikali inaendelea kuimarisha upatikanaji wa vipimo vya homa hiyo katika vituo vyake vya kutolea huduma katika maeneo yaliyoathirika.Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yudas Ndungile, alisema taratibu za kupata mashine ya kupulizia dawa kutokea angani ili kuua mbu hao makazi ya watu jijini zinaendelea.Serikali imeendelea kusisitiza kuwa ugonjwa huo unaombukizwa na mbu aina ya Aedes hauna tiba wala chanjo ya moja kwa moja mpaka sasa na tiba pekee kwa sasa ni panado pamoja na kunywa maji mengi. Mbu wa madoadoa meupe ya kung’aa hupendelea kuuma asubuhi, mchana na jioni. | Kitaifa | 0 |
Wadau wengine ni Wakala wa usafirishaji mizigo bandarini (TAFFA), Wakala wa vipimo (WMA), Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Maliasili na Utalii, Kampuni ya Kuhudumia Kontena Bandarini (TICS) na Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (TAZARA).Wengine ni Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Shirika la Viwango nchini (TBS), Wakala wa Barabara (Tanroads), Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Kitengo cha afya cha bandari na Chama cha wamiliki wa Malori nchini (Tatoa).Mwinjaka, alisema, "Kila mmoja atawajibika, ikitokea mwenzetu mmoja hawajibiki ipasavyo atajibu kwanini hafanyi kazi yake ipasavyo."Mwanjaka alisema eneo maalumu limeshapatikana kwa ajili ya benki ambapo kwa sasa CRDB na NMB tayari zimepewa eneo lakini pia benki za kimataifa.Alisema pia nchi nyingine ambazo zinachukulia mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam, zinatafutiwa eneo kwa ajili ya kufanyia kazi zingine za msingi wakiwa bandarini hapo."Kusaini makubaliano haya haina maana itakuwa mwisho wa kutekeleza majukumu mengine yaliyopo, kila mmoja atawajibika pale yatakapojitokeza na kwa pamoja yatashughulikiwa," alisema Mwanjaka.Kwa upande wake, Rais wa TAFFA, Steven Ngatunga alisema, makubaliano hayo yabane pande zote mbili Serikali na wateja ikiwa mmoja kati yao atabainika kuchelewesha mzigo apigwe faini."Yeyote atakayethibitika kuchelewesha, apigwe faini, siyo ikandamize upande mmoja hapo tutaweza kwenda sawa," alisema. Alisema kwa sasa kupanda kwa bidhaa mbalimbali kunasababishwa na gharama zilizopo bandarini."Mtu anapandisha bei pale Kariakoo kwa ajili afidie pesa yake, mzigo unafikia lakini uzembe unatokea upande mmoja anayetozwa ni huyu mteja," alisema. | Biashara | 1 |
SERIKALI imesema vyuo vya elimu ya juu nchini, havifanyi vizuri katika eneo la machapisho kwa kutokuwa nayo ya kutosha, jambo ambalo husababisha kushuka katika upangaji wa nafasi za vyuo vikuu kitaifa na kimataifa.Imeeleza katika eneo la taaluma, vyuo hivyo viko vizuri, lakini mara nyingi havishiki nafasi nzuri, huku wakitakiwa kuongeza machapisho. Aidha, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimesema wanataaluma wake wasiokuwa na machapisho kwa takriban miaka saba, wanaangalia uwezekano wa kupelekwa kufundisha shule za sekondari nchini.Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema hayo jijini Dar es Salaam wakati akifunga Wiki ya Tano ya Utafiti, iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kampasi ya Mlimani (UDSM). Kuhusu machapisho, Profesa Ndalichako alisema vyuo vya elimu ya juu vya ndani ya nchi, vinatakiwa kubadilika kwamba pamoja na kufanya tafiti, lakini waongeze machapisho yakipelekwa kitaifa na kimataifa.Alisema kila mwaka, kuna taasisi zinazopanga nafasi ya vyuo vikuu kitaifa na kimataifa katika ubora wake. Lakini, vyuo vya ndani vimekuwa haviko katika nafasi nzuri, hali hiyo ikisababishwa kuwa na machapisho na majarida yanayotambulika kitaifa na kimataifa. Aidha, alivitaka vyuo vya elimu ya juu nchini, kuiga kile kilichofanywa na UDSM kwa kutenga fedha kufanya tafiti na wao kuanza kutenga fedha za utafiti kwa kuwa wanalipwa fedha nyingi zikiwemo ada na mishahara.“Kupanga ni kuchagua, chagueni kufanya tafiti, utafiti unalipa iwapo mtawekeza kwa kiwango kinachostahili,” alisema Profesa Ndalichako na kupongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa wiki hiyo ya utafiti.Alisema wiki hiyo inatoa fursa kwa wadau, kupata jukwaa na aina za tafiti zilizofanyika kwa kuwa ni eneo ambalo limekuwa likiwashirikisha watunga sera na umma kwa ujumla. Alisema serikali imeendelea kutoa ruzuku kwa ajili ya ubunifu na ugunduzi, na wizara inaandaa mwongozo wa kutambua na kuthamini utafiti, kwa kuwa ni jambo ambalo limekuwa likiongeza mchango wa maendeleo nchini. | Kitaifa | 0 |
UCHAGUZI mdogo wa kujaza nafasi za uongozi Yanga umekuwa kizungumkuti baada ya Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kushindwa kutangaza tarehe ya kufanyika kwake.Awali, uchaguzi huo ulikuwa ufanyike Januari 13, mwaka huu, ukasogezwe mbele wagombea wakiwa katika hatua ya kujinadi kutokana na baadhi ya wanachama kufungua kesi mahakamani ya kupinga kufanyika. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Malangwe Mchungahela alifanya mazungumzo na waliofungua kesi na kukubaliana kuzifuta huku akisema wakati wowote atatangaza tena tarehe ya kuendelea pale walipoishia lakini mambo yanaonekana kukwama baada ya kushindwa mpaka sasa ikiwa inakaribia wiki ya pili.Akizungumza Dar es Salaam, Mchungahela alisema wanachosubiri ni wanachama hao kumalizia ufutaji wa kesi hizo na anaamini mambo yatakuwa mazuri. “Hatujakwama, tunaendelea kuzungumza nao ili kumaliza utaratibu wa kesi na wakati wowote tutatangaza pale tulipoishia wagombea wataendelea kujinadi na kufanya uchaguzi,”alisema. Alisema uchaguzi huo utafanyika kwa ushirikiano na Kamati ya uchaguzi ya Yanga kama walivyokubaliana. Nafasi zinazotakiwa kujazwa wazi ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wanne. | michezo | 2 |
SERIKALI kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imewaagiza maofisa elimu mikoa na wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kushughulikia nyongeza ya mishahara ya walimu waliopandishwa madaraja nchini ili waanze kulipwa stahiki zao kuanzia mwezi Agosti mwaka huu.Agizo hilo lilitolewa jana jijini hapa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tamisemi, Tixon Nzunda wakati wa ziara yake ya siku mbili ya kikazi baada ya kuitembelea Shule za Msingi Bukumbi na Kigongo zilizopo wilayani Misungwi.Aliagiza walimu hao waongezewe mishahara yao kuanzia mwezi ujao. Shule za Msingi Kigongo na Bukumbi ni kati ya zinazotekeleza Mradi wa Fursa kwa watoto tangu mwaka 2014 hadi 2018 kwa ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Children in Crossfire(CIC) linalohusika na malezi na makuzi ya awali ya watoto kwa kushirikiana na Shirika la Uchumi wa Nyumbani (TAHEA). Nzunda alitoa agizo hilo kutokana na malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya walimu wa shule hizo waliopandishwa madaraja waliodai kutoongezewa mishahara yao zaidi ya miezi mitano sasa.“Wakurugenzi hakikisheni kila mwezi mnaingia kwenye mfumo kuangalia kwa sababu viongozi wanaweza kutengeneza mazingira ya rushwa ndipo stahiki zao zishughulikiwe,” alisema.Alisema katika kushughulikia stahiki za walimu au watumishi wengine wa umma, serikali kamwe haitawavumilia baadhi ya watendaji walioko serikalini ambao wamekuwa vinara katika kuwakandamiza watumishi wenzao wasifanikiwe na wasipate stahiki zao na kusisitiza uongozi wa aina hiyo haufai. “Tunataka viongozi wanaowezesha wanaowaongoza kufanikiwa.Hivyo nawaagiza nyie ambao mnawaongoza hawa walimu kushughulikia nyongeza yao ya mishahara,” alisema na kuagiza wamjulishe yeye kama tatizo ni kuthibitisha madai ya walimu ili awasiliane na Katibu Mkuu wake kwa ufumbuzi. | Kitaifa | 0 |
WIZARA ya Miundombinu imeelekeza watoa huduma ya usafiri wa pikipiki maarufu bodaboda kutumia mfumo wa kisasa wa abiria kutolipa fedha taslimu Julai 1, mwaka huu.Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya kuhakikisha matumizi ya fedha taslimu katika huduma zote yanakoma ifikapo mwaka 2024.Uamuzi wa kuanza na pikipiki umefikiwa baada ya baraza la mawaziri kuidhinisha mkakati wa taifa wa usafiri wa pikipiki kibiashara.Waziri wa usafirishaji, de Dieu Uwihanganye, amesema mkakati huo utaondoa ulipaji nauli kwa abiria na wamiliki wa vyombo vya usafiri.Alisema mkakati huo utasaidia upatikanaji wa huduma za usafiri na kuimarisha usimamizi wake, hivyo kufikia Julai lazima wenye pikipiki kujisajili katika mifumo ya YegoMoto au Pascal Technology Ltd, ambazo ni kampuni zinazowezesha ulipaji kwa kuwekewa meta.Serikali pia iko katika mchakato wa kupanga gharama mpya za nauli kwa kilometa kwa usafiri wa taxi-moto, gharama watakayokubaliana baada ya majadiliano na wadau.“Meta zitasaidia mambo mengi, kwani itasaidia polisi kufuatilia watakaokiuka sheria za usalama barabarani na kuwatoza faini halali,” alisema.Nchini hapa kuna leseni za biashara za pikipiki 25,000 na inakadiriwa 20,000 hawajasajiliwa, lakini wanatoa huduma na mpaka sasa pikipiki 7,000 zinatumia malipo bila fedha taslimu.Mkakati huo ni kuwezesha malengo ya nchi kufikia uchumi wa kutotumia fedha taslimu mwaka 2024.Alisema mkakati huo utasaidia pikipiki kuhakikisha usalama wa barabarani,usalama wao, kwani ajali nyingi husababishwa na pikipiki, hivyo mfumo huo utasaidia kufuatilia pikipiki zitakazoibiwa kwa kutumia GPS. Takwimu zinaonesha ajali 145 zimetokea Januari mpaka Machi mwaka huu na asilimia 50 zimesababishwa na pikipiki na vifo vya watu 108, asilimia 38 vimesababishwa na pikipiki.Rais wa Shirikisho la Vyama vya Waendesha Pikipiki Rwanda (FERWACOTAMO), Daniel Ngarambe alisema watafanya kazi na wenye pikipiki, wasimamizi na wawekezaji, kwani kuna changamoto ya mtandao hivyo, ni vema kufanyiwa kazi mapema huduma ikamilike | Biashara | 1 |
KUTOKANA na kuwepo kwa matendo ya unyanyasaji na ukatili kwa watoto Shirika lisilo la Kiserikali la Compassion International Tanzania limeiomba serikali ione uwezekano wa kuweka somo la ulinzi wa mtoto kwenye mitaala ya elimu.Hayo yalielezwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo Tanzania, Agness Hotay wakati akitoa salamu kwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya shirika hilo tangu lianze kuhudumia watoto wahitaji nchini.Alisema kuwa shirika hilo lilianzishwa kwa malengo ya kuwasaidia watoto wenye uhitaji wanaotoka katika familia ambazo hazina uwezo kwa lengo la kuwafanya watoto hao waweze kuishi maisha yenye furaha.Akitoa salamu, mkurugenzi huyo alisema kuwa shirika lina wajibu wa kuhakikisha kuwa kila mtoto bila kujali jinsi, dini au kabila ana uthibitisho kuwa anapendwa, analindwa na kujulikana.Alisema uwakili wa shirika ni pamoja na kumtetea mtoto na kusimamia stahiki za mtoto husika ili kuhakikisha kuwa anafikia ndoto anazotarajia.Alisema kuwa tangu kuanza kwa shirika hilo nchini Tanzania na kutimiza miaka 20 sasa limefikia vijana 135,750 ambapo hadi sasa vijana 99,671 bado wapo kwenye huduma na 36,133 wameshamaliza na kutoka kwenye mpango wa kuhudumiwa na Compassion Tanzania.“Kupitia makanisa ambayo ni washirika wenza na Compassion International Tanzania yameweza kutoa ajira zaidi ya 1,300 hivyo kushiriki katika kuondoa uhaba wa ajira kwa kutengeneza ajira na kuongoza pato la Taifa.“Shirika limeweza kuwezesha makanisa kutengeneza miundombinu, kuhamasisha ujenzi wa madarasa, uchimbaji wa visima, ujenzi wa vyoo vya kisasa na jiko, uanzishwaji wa karakana za mafunzo mbalimbali, uanzishwaji wa VICOBA na ujalismali,” alisema Hotay.Kwa upande wake, Naibu Waziri- Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia wenye Ulemavu, Stella Ikupa, alisema maadhimisho hayo yawatake vijana kutumia fursa zilizopo kujipatia maendeleo.Mbali na hilo, aliwasihi viongozi wa dini kutoa elimu kwa watoto wenye ulemavu ili jamii iweze kuwapa haki sawa na watu wengine.“Naomba niwasisitize viongozi wa dini kutoa elimu ya uelewa kwa jamii ili wasiwachukulie watoto wenye ulemavu sehemu ya mkosi hata ifike hatua hata kwenye mahusiano mtu mwenye ulemavu asikose kuoa au kuolewa kwa kigezo cha kuwa na ulemavu,” alisema Ikupa.Ikupa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, alisema kitendo cha shirika hilo kujitolea kuwahudumia watoto wenye uhitaji ni sehemu ya kulifanya taifa kuwa na watu ambao wamelelewa katika maadili mazuri na wenye kufanya kazi kwa uadilifu. | Kitaifa | 0 |
MKUU wa Mkoa wa Mara, Adam Malima ametoa siku tatu kwa viongozi wa Wilaya ya Tarime kubaini zilipo fedha za huduma zilizotolewa na Mgodi wa Acacia North Mara kwa miaka mitatu kiasi cha Sh bilioni 9.5.Malima alitoa agizo hilo kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Charles Kabeho, maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Kamati ya Ulinzi na Usalama kwenda kuchunguza miradi iliyotekelezwa na Halmashauri ya Tarime Vijijini.Inadaiwa kuwa baadhi ya watumishi na madiwani wa halmashauri hiyo na viongozi wa serikali wamehusika katika kuhujumu fedha hizo hivyo hatua zaidi za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika.Malima amesema hayo katika kikao cha kumtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kabeho kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Tarime na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa wilaya hiyo na watumishi wa halmashauri za Tarime Mjini na Tarime Vijijini, madiwani wote wa halmashauri hizo wakiongozwa na wenyeviti wao, Moses Yomami (Tarime Vijijini), Khamis Nyanswi (Tarime Mjini).Pia walikuwapo wakurugenzi watendaji wa halmashauri hizo, Kamati za Ulinzi na Usalama Mkoa na Wilaya, Kamanda wa Polisi Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Samwel Kiboye ‘Namba Tatu’ na viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa dini.Malima alionesha kuwapo kwa vitendo vya hujuma katika halmashauri hiyo ya Tarime Vijijini katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita ambako halmashauri zote mbili zinaongozwa na Chadema.Alisema katika shughuli za maendeleo hakuna itikadi za vyama, na kwamba Halmashauri ya Tarime Vijijini katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita wamepokea Sh bilioni 9.5, akizitaja kuwa ni Agosti 10, 2015 walipokea Sh bilioni 1.1, Januari 18, 2016 (Sh 1.6), Julai 29, 2017 (Sh bilioni 1.334), Februari 7, 2017 (Sh bilioni 1.770), Julai 27, 2017 (Sh bilioni 1.477), Julai 18, 2018 (Sh bilioni 1.253) na Septemba 8, 2018 (Sh bilioni 1.435).Alisema mwezi uliopita walitaka kupewa tena Sh bilioni 1.5, lakini amezizuia kwanza hadi fedha hizo za awali Sh bilioni 9.5 za huduma zilitolewa na Mgodi wa Acacia North Mara, kwa ajili ya miradi ya mandeleo, kujulikana matumizi yake kwani kuna harufu ya ufisadi katika fedha hizo.Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Kiboye alimpongeza Rais Magufuli kwa kusikia kilio cha watu wa Tarime na kumteua Kabeho kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime na kuahidi chama hicho kitampa ushirikiano kwa maendeleo ya wana-Tarime na kuwaonya wahujumu halmashauri kwamba dawa yao inachemka na mwisho wao umefika. | Kitaifa | 0 |
WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema ana hakika timu hiyo itarejea na ushindi kutoka Cape Verde.Stars ilisafiri alfajiri ya jana kwenda Praia kucheza na wenyeji wao Cape Verde kesho mechi ya kuwania kufuzu fainali za michuano ya Kombe la Mataifa Afrika iliyopangwa kufanyika Cameroon mwakani.Stars na Cape Verde zipo kundi moja na Uganda na Lesotho na tayari kila timu imecheza mechi mbili huku Uganda ikiongoza msimamo wa kuwa na pointi nne, ikifuatiwa na Tanzania yenye pointi mbili.Akizungumza kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam saa chache kabla timu hiyo haijaondoka, Mwakyembe alisema ameamua kuacha usingizi wake na kwenda kuwasindikiza kutokana na kuwa ana uhakika wa asilimia zote kuwa watarudi na ushindi hivyo wasimuangushe.Kwa upande wa serikali, kiongozi aliyeambatana na Stars ni Mkurugenzi wa Michezo, Yusuf Singo. Mwakyembe aliwataka wachezaji hao kutambua kuwa serikali pamoja na watanzania kwa ujumla wapo nyuma yao hivyo wasiwaangushe na pia kama alivyofanya kuwasindikiza hivyohivyo anatarajia kufanya pia wakati watakaporudi hivyo wanapaswa kuhakikisha wanapata ushindi ili awapokee kwa furaha.Aliwasisitiza kuhakikisha wanakabiliana na wapinzani wao kwa kujiamini na kujituma licha ya kuwa ugenini wakijua fika kuwa wanapigania taifa lao ambalo limepoteza heshima kwenye michuano hiyo kwa miaka 38 sasa tangu kushiriki fainali ikiwa ni mara ya kwanza na mwisho.“Nyie ndio tumaini la Tanzania kuturejeshea heshima iliyopotea kwa zaidi ya miaka 38 haijapata kutokea ni muda mrefu mno, sasa tumechoka, nina uhakika tuna kikosi kizuri sana, benchi la ufundi zuri sana lenye weledi wa kila aina…“Sisi kazi yetu kubwa kuwatia moyo na kuwaombea kwa Mungu mfike salama na vilevile tarehe 12 muoneshe mchezo wa kujiamini, kujituma kupigania taifa lenu mimi nina uhakika moyo wangu hauna dukuduku kabisa najiandaa kuwapokea mkirudi,” alisema Mwakyembe. | michezo | 2 |
KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema amewajenga wachezaji wake kisaikolojia kukabiliana na mbinu za fi tina zinazotumiwa na timu nyingi za Kiarabu wakiwa kwao kujinufaisha kupata matokeo chanya.Aidha, Zahera alisema wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na malengo mawili makubwa, kwanza kujilinda kuzuia wasifungwe na kuhakikisha wanapata ushindi wa mabao mawili ili kusonga mbele kufutia kupoteza mchezo wao wa mkondo wa kwanza kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.Zahera alisema amechukua hatua hiyo kwa kuwa ana uzoefu wa kutosha na soka la kiafrika, hasa kwa timu nyingi zinazotoka kwenye ukanda wa kaskazini mwa Afrika kwani wamekuwa na utamaduni wa kutumia mbinu chafu za kuwadhoofisha wachezaji kabla ya kuingia kwenye mchezo. Zahera amefichua kauli hiyo ikiwa ni maandalizi ya mwisho kuelekea kwenye mchezo wao wa marudiano dhidi ya Pyramids unaotarajiwa kupigwa kesho jioni kwenye Uwanja wa 30 June, Cairo nchini Misri. Zahera anajua mchezo huo utakuwa mgumu kwao kwa kuwa kikosi cha wapinzani wao kimesheheni wachezaji wakubwa na wanatumia akili katika kucheza hivyo watazidisha umakini kwa kutowaruhusu kupata nafasi ya kupata mwanya wa kuwafunga. Alisema kitu pekee kinachozidi kumpatia matumaini ya kwenda kuchomoza na ushindi ni kwamba kwenye mazoezi yaliyopita waliyofanya wachezaji wake walikuwa wanafundishwa mbinu ya kufunga na kujilinda na walicheza kwa kujiamini na walionesha maelewano mazuri. | michezo | 2 |
UTALII unachangia asilimia 25 ya pato la ndani Zanzibar na asilimia 80 ya fedha za kigeni, jambo ambalo wataalamu wanasema lisingewezekana bila kuwepo kwa matumizi bora ya teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama).Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Dk Mzee Suleiman Mndewa amesema hayo na kuongeza kwamba licha ya watalii kupata taarifa za utalii wakiwa kwao, pia wanapata fursa ya kuendelea kuwasiliana na jamaa zao wakiwa Zanzibar.“Kwa kuwa ni kisiwa, Zanzibar inahitaji mifumo mizuri ya mawasiliano ili kuwavutia watalii wengi zaidi. Ni jambo lisilopingika kwamba watalii wanahitaji sana kuwasiliana na ndugu zao kwa kipindi chote wanapokuwa hapa,” amesema.Aliongeza pia kwamba uimara wa mifumo ya mawasiliano ni muhimu pia kwa watalii wanaotoka ndani ya Jamhuri ya Muungano, akitolea mfano wa boti zinazokwenda Zanzibar kila siku zikitokea Dar es Salaam.“Kwa kifupi, kila boti inabeba takribani watu 400, kila abiria anayekuja hapa anahitaji kuwasiliana na ndugu zake aliowaacha nyumbani. Hii ndio maana tunaamini kwamba suala la kuimarisha mifumo ya mawasiliano linahitaji kuwekewa mkazo,” amesema.Aliongeza kwamba tehama licha ya kuwa na mchango mkubwa kwenye utalii pia ina mchango mkubwa sana kwenye sekta nyingine za kiuchumi ikiwemo kilimo na uvuvi.“Kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano kwenye kilimo, kwa mfano, unaweza kutengeneza mfumo ambao utakuambia muda muafaka wa kufanya jambo fulani la kuhudumia mazao kama muda wa kumwagila…,” alisema.Akitolea mfano wa uvuvi, Dk Mzee amesema kwamba mfumo huo pia unaweza kumwongoza mvuvi kujua ni sehemu gani kuna samaki wengi na wapi anaweza kupata soko la samaki, hivyo kuifanya kazi yake kuwa ya uhakika na yenye tija. | Biashara | 1 |
MGOMBEA nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji katika klabu ya Yanga, Athanas Kazige amesema anataka kutumia fani yake kuiwezesha kiuchumi klabu hiyo. Uchaguzi wa Yanga umepangwa kufanyika Mei 5 na sasa wagombea wanajipigia kampeni ili kuwania nafasi wanazogombea.Akizungumza jana na gazeti hili Dar es Salaam, alisema anaona faraja kuitumikia klabu hiyo kwa kutumia mitandao ya kijamii kuiwezesha kiuchumi. “Mimi nikipata nafasi ya kuwa mjumbe nitashirikiana na viongozi waliopo kutengeneza mfumo wa kuandika na watu wakisoma habari, makala kwa kulipa ili klabu iweze kupata fedha,”alisema Kazige.Aliongeza kuwa yeye ni mwanahabari, hivyo atahakikisha anashirikiana na viongozi watakao chaguliwa kufufua gazeti la Yanga Imara. “Ukweli hivi sasa wanachama nimeona kwamba kuna upungufu huo, hivyo nitashirikiana na Ofisa Habari wa Yanga ili kuongeza mapato ya klabu kupitia gazeti na mitandao ya kijamii,” alisema Kazige ambaye anagombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji katika uchaguzi huo.Aidha, Kazige alisema kuwa mabadiliko ya mfumo ili klabu hiyo iweze kujitegemea ni muhimu kwa sasa. “Naomba wanachama wenzangu mchague viongozi wenye uwezo wa kuleta mabadiliko katika klabu yetu, na mimi naahidi kuwa nitatumia taaluma yangu kuisaidia Yanga kiuchumi kwani habari kwa sasa ni fedha,”alisema Kazige ambaye ni mwandishi wa habari mwandamizi nchini. | michezo | 2 |
SERIKALI imesema hadi Desemba 31, mwaka huu, Watanzania wote wenye sifa za kupata vitambulisho vya Taifa watakamilisha usajili wa kuchukua alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki, kazi inayoendelea kufanywa sasa.Sambamba na hilo, serikali imesema itanunua mashine mpya za uzalishaji wa vitambulisho vya taifa zenye uwezo mkubwa zaidi kwa lengo la kuharakisha upatikanaji vitambulisho hivyo.Hayo yalibainishwa jana bungeni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni wakati akijibu swali la mbunge wa Buyuni, Christopher Chiza (CCM). Mbunge huyo alihoji serikali ina mpango gani wa kuharakisha zoezi la kutoa vitambulisho vya taifa wavitumie kwa shughuli za maendeleo.Akijibu swali hilo, Masauni alisema serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), inaendelea kukamilisha usajili kwa watu wote wenye sifa ikitarajiwa kukamilisha kazi ya uchukuaji alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki Desemba 31, mwaka huu.Alisema hadi sasa vitambulisho milioni tano vya taifa vimeshatolewa na kwamba vingine milioni 13 vipo hatua za mwisho kutolewa na kwamba hadi ifikapo Desemba mwaka huu, lengo lao ni kutoa jumla ya vitambulisho milioni 24.4. “Wananchi waendelee kuwa watulivu na wale waliokamilisha uchukuaji alama za vidole, saini na picha na hawajapata vitambulisho, huenda ndio hivyo milioni 13 vilivyo hatua za mwisho kutolewa,”alisema Naibu Waziri Masauni.Aidha alisema katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bila kukwama ikiwemo wale wanaojisajili kibiashara Brela, NIDA imefungua dawati maalum la usajili katika ofisi hizo. Alisema usajili huo unafanywa kwa kuzingatia sifa bila kuathiri masharti ya kisheria na kanuni.Akijibu swali kuhusu utaratibu gani umewekwa na serikali wa kuwapa vitambulisho wananchi wanaokaa mipakani bila kuathiri malengo ya utoaji vitambulisho hivyo, Waziri Masauni alisema utaratibu wa kuwapa vitambulisho hautofautiani na ule wa kawaida uliopo. | Kitaifa | 0 |
YANGA imeendeleza wimbi la ushindi dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya baad aya kuifunga 2-0 katika mchezo wa Kombe la FA, hatua ya 32 bora katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam jana. Hii ni mara ya pili kwa Yanga kuifunga Tanzania Prisons msimu huu, ambapo kwa mara ya kwanza waliifunga 1-0 na kuwa timu ya kwanza kuifunga timu hiyo katika ligi msimu huu. Kwa ushindi huo, Yanga sasa imetinga hatua ya 16 bora sawa na watani zao Simba, ambao juzi waliifunga Mwadui ya Shinyanga kwa mabao 3-1 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja huo wa Uhuru. Ushindi huo wa Simba ulikuwa ni sawa na kulipa kisasi kwa Mwadui, ambayo hadi sasa ndio timu pekee iliyoifunga Simba katika Ligi Kuu, Tanzania Bara. Mabao ya Yanga yalifungwa na wachezaji wapya wa timu hiyo, Bernard Morrison na Yikpe Gislain na kuiwezesha Yanga kuibuka na ushindi huo wa mabao 2-0. Morrison ndiye alikuwa wa kwanza kuifungia Yanga bao pale alipofunga kwa penalti, katika dakika ya 11, baada ya beki wa Tanzania Prison, Michael Ismail kunawa mpira wa krosi katika eneo la hatari, uliopigwa na Juma Abdul. Mpaka mapumziko, Yanga ilikuwa mbele kwa goli 1-0, licha ya wapizani wao kuonesha uimara wa hali ya juu katika muda wote wa mchezo. Mshambuliaji mwingine mpya, Yikpe alifunga bao katika dakika ya 63 kwa mpira wa kichwa baada ya kutumia vyema pasi ya Haruna Niyonzima, ambaye aling’ara katika mchezo wa jana. Pamoja na matokeo hayo, kivutio kikubwa katika mchezo huo, alikuwa ni mshambuliaji mpya wa Yanga, Morrison ambaye licha ya kufunga goli, alionesha kiwango cha hali ya juu, huku akiuchezea mpira kwa namna anavyotaka.Haikua siku nzuri kwa mshambuliaji David Molinga, ambaye aliumia kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na mfungaji wa bao la pili, Yikpe. Dakika za mwishoni, Deus Kaseke alitoka na nafasi yake kuchuliwa na Patrick Sibomana, wakati Feisal Salum aliingia kuchukua nafasi ya Morrison. Kwa upande wa wapinzani wao, waliongeza nguvu kwa kumtoa Salum Kimenya na kuingia Samson Bangula ambaye hata hivyo hakuleta matokeo chanya kwa timu yake. | michezo | 2 |
Akizungumzia mfumo huo alisema mfumo huo utatumika kutoa mizigo bandarini, katika viwanja vya ndege na mipakani na wenye kuhusisha wadau mbalimbali.“Awali Idara ya Forodha ilikuwa ikitumia mfumo wa asycuda kwa ajili ya kutolea mzigo ambapo umekuwa na changamoto nyingi zilizokuwa zikisababisha ucheleweshwaji wa kutoa mizigo bandarini,” alisema Silaa na kuongeza kuwa mfumo huo ni wa Watanzania na katika kuutekekeza umegharimu dola za Kimarekani milioni 11.6.Alisema katika mfumo wa awali ulipaji wa mizigo ilikuwa lazima kwenda benki ambapo ulijumuisha pia mifumo mingine midogomidogo ambayo imekuwa ikisababisha usumbufu haswa wakati wa kuandaa ripoti.Silaa ambaye pia ni Mkurugenzi wa mfumo huo, alisema baada ya kuona mfumo wa awali ulikuwa na changamoto mbalimbali ndipo idara hiyo ilianza mchakato wa kutafuta mzabuni atakayefanya upembuzi juu ya mfumo huo wenye kukidhi matakwa ya Watanzania.Alisema faida za mfumo huo ni kurahisisha taratibu na kupunguza gharama na muda wa kutoa mizigo kutoka siku tisa hadi tano, kuwa na taratibu za wazi zenye kuleta manufaa katika utoaji wa mizigo na kuunganisha vitengo vya ndani vya TRA.Kuhusu kama mfumo huo utaweza kubaini mizigo haramu alisema mfumo huo utaweka wazi hatua kwa hatua ya mzigo tangu kuingia hadi kuondoka na kwamba nanikafanya nini hali ambayo itarahisisha kubaini watakaohusika na kitendo chochote chenye kutiliwa shaka.“Katika mfumo huu nyaraka za kughushiwa zitapunguzwa, utazingatia uadilifu kwa wanaoutumia kwani utatoa taarifa kila wakati unapotumiwa, kufahamu mzigo ulikocheleweshwa na ni nani aliyehusika, kuondoa uongo na kuondoa kufahamiana wakati wa kufuatilia nyaraka,’ alisema.Kwa upande wake, Vileth Kazimoto wa kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TRA, alisema chini ya mfumo huo zipo changamoto wanazotarajiwa kukumbana nazo, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa uelewa mdogo wa taaluma hiyo kwa wafanyakazi wengi wa TRA. | Biashara | 1 |
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally amekitangaza kijiji cha Nzali kuwa kituo cha uhamasishaji Mkoa wa Dodoma.Alisema hayo katika kijiji cha Nzali kata ya Chilonwa Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 42 tangu kuzaliwa kwa CCM na kubainisha kuwa maadhimisho hayo yatadumu kwa mwezi mzima.Kauli ya Dk Bashiru imekuja wakati wa maadhimisho hayo ambapo zaidi ya vikundi 30 vya ngoma vilijitokeza kwenye uzinduzi wake vikiimba nyimbo za hamasa pamoja na kuelezea miradi inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano.Amesema wakati huu ambapo nchi iko katika vita ya kiuchumi kila kitu kinahitaji hamasa.“Tunahitaji kufufua hamasa za kisiasa kwa nyimbo, na sasa tunatakiwa kuwepo na vikundi vya hamasa, tunataka sanaa inayohamasisha kushiriki vita vya kiuchumi” alisema.Alisema yeye pamoja na msemaji wa chama hicho Humprey Polepole watafika kijijini hapo kujifunza watu wanavyojitolea kuwa na hamasa.“Msiishie kukisifia tu chama kikosoeni kwa adabu” alisema.Katibu Mpya Idara ya Oganaizesheni CCM Pereira Ame Silima, amesema tangu aingie kwenye siasa na kuzunguka maeneo mbalimbali nchini hajawahi kuona hamasa kubwa katika aliyoikuta katika kijiji cha Nzali.“Sijawahi kuona hamasa kubwa kama hii niliyokuta kijiji hiki, lazima nikiri hilo. Hapa kuna hamasa kubwa wasanii wanaimba na kupiga ngoma na kueleza umma kazi zinazofanywa na serikali yao” alisema. | Kitaifa | 0 |
WAKATI nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kila moja ikionesha kuridhika na kuwa tayari kuiunga mkono Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika kampeni za kujiunga na jumuiya hiyo, wadau wengine wa maendeleo nao hawako nyuma.Wasomi, wachumi na wanadiplomasia ni miongoni mwa wanaoiunga mkono DRC kutaka iwe nchi ya saba mwanachama wa EAC, baada ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini, wakisema taifa hilo kubwa.Tayari Rais Felix Tshisekedi wa DRC ameshawasilisha ombi kwa Mwenyekiti wa EAC, Rais Paul Kagame wa Rwanda juu ya dhamira ya nchi yake kutaka kujiunga na jumuiya hiyo ambayo kwa sasa ina takribani watu milioni 170.Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kwa Umma katika Sekretarieti ya EAC, Owora Richard Othieno, ombi hilo litajadiliwa katika kikao cha wakuu wa nchi wanachama Novemba 30, mwaka huu jijini Arusha na kwamba kama kutakuwa na ulazima wa kujadili mapema, mwenyekiti anaweza kuitisha kikao wakati wowote kutokana na unyeti wake.Mhadhiri azungumza Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Razack Lokina alisema DRC kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki itasaidia kutanua soko la bidhaa za ukanda huo na kukuza uchumi wa nchi kutokana na nchi hiyo kuwa na idadi kubwa ya watu.Alibainisha kuwa kwa ushirikiano huo pia kutawezesha maeneo mengi zaidi ya nchi hiyo kutumia bandari ya Dar es Salaam kuingiza bidhaa katika nchi hiyo yenye idadi kubwa ya watu kwani baadhi ya mikoa kutumia bandari inarahisisha ufanyaji biashara.Profesa huyo alibainisha kuwa lakini jambo la msingi ni kuhakikisha nchi hiyo inakuwa na amani kwani hakuna eneo lisilo na amani kunaweza kufanyika biashara.Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara Afrika Mashariki (EABC), Peter Mathuki, anasema ombi la DRC linakuja katika wakati mwafaka na linapaswa kuungwa mkono.Mathuki ambaye pia ni Mbunge wa zamani wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), alisema EAC imara itakuwa na nguvu ya kiuchumi na hivyo kuchuana na pande nyingine za dunia.Alisema ukubwa wa DRC ni mtaji tosha, kwani ndiyo nchi ya pili kwa ukubwa Afrika na ya kwanza kusini mwa Jangwa la Sahara. Inatajwa kuwa ya 11 duniani, ikiwa na mtaji wa watu milioni 81 ambao wakichanganya na milioni 170 kutoka nchi wanachama wa sasa wa EAC, ukanda utakuwa na `soko’ la watu milioni 250.Mbali ya ukubwa na mtaji wa watu, DRC ni nchi tajiri kwelikweli, huku asilimia 80 ya ardhi yake ikifaa kwa kilimo. Ina hazina ya asilimia 10 ya shaba ya dunia nzima.Asilimia 30 ya cobalt ya dunia nzima, dhahabu, almasi, platinum, bauxite, risasi, madini ya fedha, zink, uranium na inazalisha asilimia 80 ya madini ya coltan yanayotumika kutengeneza simu, sumaku, iPods, na injini za ‘Jet’.Inaelezwa kuwa, nchini DRC kuna aina 1,100 za madini. Ina Mto Kongo ambao ni mto wa pili kwa ukubwa duniani, ukiwa na maporomoko yanayoweza kuzalisha umeme unaoweza kusambazwa Afrika na Ulaya kwa pamoja. Ina pia utajiri wa mafuta ambayo bado kuchimbwa, misitu, wanyama, vivutio vya utalii vilivyopo Ituri na milima ya Virunga pamoja na mito na mabonde yenye unyevu na rutuba, maziwa na kadhalika.Mdau mwingine, Patience Mutesi ambaye ni Mkurugenzi Mkazi wa taasisi ya TradeMark East Africa nchini Rwanda naye amesifu, akisema ni fursa nzuri kwa ukuaji wa EAC kibiashara.Alisema kwa sasa, tayari DRC ni soko la karibu nusu ya bidhaa zote zinazozalishwa katika nchi za EAC na kwamba, yenyewe pia itafungua milango ya bidhaa zake kwa nchi nyingine wanachama.Takwimu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Uganda inaonesha kuwa, nchi iliuza DRC bidhaa zenye thamani za Dola za Marekani milioni 398 mwaka 2018 na kwamba inakusudia kuongeza na kufikia bidhaa za Dola bilioni 2 ifikapo mwaka 2020. Wakati Uganda ikiuza kiasi kikubwa ch bidhaa, yenyewe iliagiza bidhaa zenye thamani ya Dola milioni 2.5 tu kutoka DRC.Kwa upande wa Rwanda, iliuza bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 456.8 mwaka 2018 na iliagiza bidhaa za dola milioni 11.2 tu kutoka DRC, kwa mujibu wa takwimu za Benki Kuu ya Rwanda. Tanzania ilipeleka DRC bidhaa zenye thamani ya dola za Marekani milioni 153 mwaka 2017 na iliingiza bidhaa zenye thamani ya dola milioni moja tu kwa ajili ya bidhaa za matumizi ya ndani ya nchi, kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania. Kenya, kwa mujibu wa Shirika la Takwimu la Taifa Kenya, nchi ilipeleka DRC bidhaa zenye thamani ya dola milioni 150 mwaka 2018, huku ikiingiza bidhaa za dola milioni 12.Mchambuzi wa sera kutoka Nairobi, Kenya, Jeremiah Owiti amekaririwa akisema kuwa, DRC ni nchi muhimu kwa ustawi wa ukanda wowote unaotaka maendeleo ya kweli kiuchumi, kutokana na nchi hiyo kuwa na mtaji wa watu, ardhi nzuri ya kilimo, utajiri mkubwa wa madini duniani na kadhalika.“Kama mchakato wa kuipa uanachama utaharakishwa, kasi ya ukuaji wa kiuchumi itapata msukumo mpya zaidi hivyo kuzidi kuifungua Afrika Mashariki,” alisema Owiti.Mchumi UN Kaimu Mkurugenzi wa Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa (ECA) katika Kanda ya Afrika Mashariki, Andrew Molde, ameungana na wadau wengine kuelezea umuhimu wa DRC kiuchumi endapo itapokelewa ndani ya EAC.Kwa mujibu wa Rais Tshisekedi, anataka kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa sababu za maendeleo ya kiuchumi na usalama wa eneo hilo la Afrika, akiamini wakijiunga EAC huenda usalama ukaimarika kwa nguvu za pamoja kutoka nchi wanachama, hivyo kuelekeza nguvu katika maendeleo kwa ujumla.Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli ameweka hadharani dhamira yake ya kuiunga mkono DRC baada ya Rais Tshisekedi kutaka kuungwa mkono alipokuwa ziarani Tanzania wiki iliyopita.Tshisekedi amekutana pia na marais wa Kenya (Uhuru Kenyatta), Uganda (Yoweri Museveni), Rwanda (Paul Kagame ambaye pia ni Mwenyekiti wa sasa wa EAC) na Pierre Nkurunziza wa Burundi, ili pamoja na mambo mengine, akiomba maombi ya nchi yake yaungwe mkono.Wakati DRC ikiwasilisha ombi la kujiunga EAC, baadhi ya nchi zimewahi kufanya hivyo, lakini zikakwama miongoni mwao ikiwa Sudan. Nchi ya Somalia pia imekuwa ikipigania kujiunga, lakini haijabahatika. | Kitaifa | 0 |
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajia kuwa mgeni rasmi katika tamasha la Urithi Wetu litahitimishwa keshokutwa Jumamosi kwenye viwanja vya Rock City Mall jijini hapa.Akizungumza juzi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela alisema tamasha hilo ni kubwa na lengo ni kutambua utamaduni wetu na sanaa zetu. Alisema tamasha hilo litaanza leo na kufika tamati Novemba 2 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Majaliwa.Alisema katika tamasha hilo kutakuwa na michezo mbalimbali kama mieleka ya asili, muziki na ngoma. Alisema anawaomba wakazi wa mkoani wa Mwanza kujitokeza kwa wingi kuhudhuria tamasha hilo. | michezo | 2 |
MAMLAKA ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA) imesema inaendelea kuvutia uwekezaji kwenye viwanda vinavyotumia teknolojia ya kisasa, ili kukuza na kuendeleza wajasiriamali waitumie kukuza uchumi.Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji wa EPZA, James Maziku alipozungumzia uwekezaji wa kiwanda cha kutengeneza kadi za kielekroniki cha DZ Cards Afrika, kilichopo katika Eneo Maalum la Uwekezaji la Benjamin William Mkapa jijini Dar es Salaam.Uwekezaji katika kiwanda hiki pekee kilichopo Afrika katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara ni zaidi ya Sh bilioni 11.Baadhi ya viwanda vilivyopo katika maeneo maalumu ya uwekezaji wa EPZ ni pamoja na viwanda vya nguo, vinavyochakata nafaka, vya kutengenezea vifungashio, vifaa vya ujenzi na vya bidhaa za ngozi.Maziku alisema kuongezeka kwa mahitaji ya kadi za kielekroniki na kukuza uchumi usiotumia fedha taslimu, ndio imefanya kiwanda cha DZ Cards Afrika kupanua masoko ili kusambaza bidhaa zake katika bara lote la Afrika.“Ongezeko la mahitaji ya kadi za kielekroniki na kukuza matumizi Uchumi usiotumia pesa taslimu ndio imetoa msukumo mkubwa kwa wawekezaji wa kiwanda cha DZ Cards Afrika kupanua masoko zaidi,” alisema Maziku.Kiwanda cha DZ Cards Afrika kilianza uzalishaji miaka minne iliyopita na tangu wakati huo, kimepata wastani wa mauzo ya dola za Marekani milioni 2.9 (zaidi ya Sh bilioni 6.67).Kiwanda hiki huzalisha kadi zenye viwango vya kimataifa zinazotumika katika kufanya miamala katika sekta mbali mbali za uchumi. Baadhi ya kadi hizo ni Mastercard na Visacard.Maziku alisema kiwanda cha DZ Cards Afrika, kitakuwa na uwezo wa kuajiri zaidi ya watu 400 wakati uzalishaji ukiwa katika kiwango cha juu. Kwa sasa kinaajiri watu takribani 100. | Biashara | 1 |
WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imewaonya wafanyabiashara na wafugaji watakaojaribu kutorosha mazao ya mifugo zikiwemo ngozi kwa njia ya panya na kuikosesha serikali mapato, kuwa watachukuliwa hatua kali kisheria.Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Elisante Ole Gabriel alitoa onyo hilo hivi karibuni wakati alipotembelea Kiwanda cha Ngozi cha ACE kilichopo Mtaa wa Viwanda Kihonda katika Manispaa ya Morogoro.Profesa Ole Gabriel alisema azma ya serikali ni kuona viwanda vyote vya ndani vinaendelea kuzalisha kwa tija kwa kutumia malighafi zinazopatikana nchini kwa lengo la kuwanufaisha Watanzania katika masuala ya kupata ajira.Pia aliwataka wawekezaji wa viwanda vya ngozi kuangalia mahitaji ya soko ikiwamo kuboresha zaidi utengenezaji wa ngozi ili wenye viwanda vidogo vya kutengeneza viatu, mabegi, mikanda na bidhaa nyingine zitokanazo na mazao ya ngozi kupata soko kubwa likiwemo la nchi za kusini mwa Afrika zenye idadi kubwa ya watu.Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Ngozi cha ACE, Onorato Garavagilia, alisema kwa sasa kinasindika ngozi vipande 4,000 kwa siku za wanyama wakubwa na vipande 7,000 vya ngozi za wanyama wadogo.Alisema hadi kufikia Septemba mwaka huu, kiwanda kinatarajia kuingiza mitambo mipya ya kisasa ambayo itakuwa na uwezo wa kutengeneza ngozi hadi kwa kiwango cha daraja la mwisho kwa ajili ya watumiaji wa viwanda vidogo vya kutengeneza viatu na bidhaa nyingine za mazao ya ngozi.“Kwa sasa hatuna tatizo la soko, tunalo China na India pia nchi za Ulaya, kinachohitajika ni kwetu ni kupokea malighafi za ngozi zenye ubora kutoka wa wateja wetu ili uzalishaji uwe na ubora zaidi,” alisema.Baadhi ya wadau wa sekta ya ngozi akiwemo Meneja Uzalishaji wa zamani wa Kiwanda cha Morogoro Tanneries, Kenneth Boma, alisema ubora wa ngozi inahitajika zaidi.Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Mazao ya Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Gabriel Bura alisema wameanza kuwapatia mafunzo wachunaji ngozi wa Mkoa wa Morogoro hususani wa Manispaa ya Morogoro na hadi sasa uchunaji wa ngozi wenye matatizo umepungua kwa asilimia 80 hadi sasa. | Kitaifa | 0 |
MABINGWA wa kihistoria wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara Yanga leo wana kazi ya kuhakikisha wanasaka ushindi dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa ligi utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Huo utakuwa mchezo wa tatu wa ligi tangu kuanza kwa msimu huu wa mwaka 2019/20 Yanga ikicheza kwenye uwanja huo ambapo katika miwili iliyopita imepoteza mmoja na kupata sare moja. Lakini kwa Coastal utakuwa ni mchezo wa nne baada ya kucheza michezo mitatu na kati ya hiyo, ikishinda mmoja, sare moja na kupoteza mmoja. Mara ya mwisho timu hizo zilikutana msimu uliopita Februari 2019 kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga na zilitoka sare ya bao 1-1. Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Dar es Salaam Yanga ilishinda bao 1-0.Mchezo wa leo huenda ukawa mgumu na wenye presha hasa kwa wenyeji Yanga wanaohitaji ushindi angalau kuwatuliza mashabiki wao baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Polisi Tanzania katikati ya wiki hii. Sare hiyo haikuwafurahisha mashabiki wao hasa ikizingatiwa kuwa mchezo wa kwanza walipoteza kwa bao 1-0 mbele ya Ruvu Shooting hivyo, iwapo watashindwa kupata matokeo mazuri tena leo hali itakuwa ngumu kwa Kocha Mkuu Mwinyi Zahera. Timu zote mbili zina washambuliaji wazuri wenye madhara langoni, ukimtazama David Molinga aliyefunga mabao mawili katika mchezo uliopita anataka kuendelea kufunga ili kuendelea kudhihirisha ubora wake na kwa upande wa Coastal hatari zaidi ni Ayoub Lyanga.Safu ya ulinzi ya Yanga bado haijakaa vizuri sana kwa sababu katika mechi mbili wamefungwa mabao manne na kushinda matatu huku Coastal ikionekana kuwa vizuri baada ya kucheza michezo mitatu kufungwa mawili na kufunga mabao matatu. | michezo | 2 |
MKAZI wa Boko, Abubakar Hamisi (46) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mkataba wa mauziano ya kiwanja kati yake na aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Takukuru, Godfrey Gugai, uliandikwa Sh milioni 60 lakini walipewa Sh milioni 80 ili kupata ahuweni ya kodi.Hamisi ni shahidi wa 20 katika kesi ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zilizozidi kipato, inayomkabili Gugai na wenzake. Akiongozwa na Wakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Awamu Mbagwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba shahidi huyo akizungumza jana alidai kuwa Gugai ni jirani yake na amewahi kufanya naye biashara.Alidai walifanya makubaliano baina ya familia na Gugai ya kuuziana kiwanja namba 64 kilichopo kitalu C cha Boko Ununio Dar es Salaam, kwa Sh milioni 80 na malipo yalifanyika kwa fedha taslimu. Alidai baada ya familia kufanya makubaliano na Gugai, Mwanasheria wake alienda kuandaa mkataba na walipofika nyumbani kwake jioni aliwapa na kuusoma kisha akawakabidhi fedha. Shahidi huyo aliendelea kudai kuwa katika mkataba huo uliandikwa Sh milioni 60 tofauti na makubaliano lakini walikabidhiwa fedha taslimu Sh milioni 80.Aliendelea kudai katika mkataba huo uliofanyika nyumbani kwake akiwa na mwanasheria uliandikwa hivyo ili kuweza kupata ahuweni ya kodi. Baada ya maelezo hayo, shahidi huyo aliiomba mahakama kupokea mkataba wa mauziano ya kiwanja kama kielelezo baada ya kuutambua kwa majina na saini. Hata hivyo, upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Semi Malimi ulipinga kupokewa kwa mkataba huo wakidai kuwa ni nakala na sio nyaraka halisi ya mkataba.Alidai nyaraka yoyote inayotolewa mahakamani lazima iwe halisi kwa mujibu wa sheria kifungu 67 (1) na kama ni nakala yapo mazingira yanayoruhusu ipokewe. Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 11, mwaka huu atakapotoa uamuzi kama kielelezo hicho kipokewe au la. Gugai na mwenzake watatu wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo, makosa 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo hilo linamkabili Gugai. | Kitaifa | 0 |
Kauli hiyo ameitoa wakati wa ufunguzi wa duka kubwa la kampuni hiyo mjini Dodoma baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa ili liweze kuwa la kisasa linalokidhi mahitaji ya mji mkuu.Mkuu huyo wa mkoa wa Dodoma pamoja na kuwapongeza kwa kuboresha utoaji wa huduma za mawasiliano kwa watumiaji nchini, amewataka wakazi wa Dodoma kutumia nyenzo hiyo muhimu katika kuunganisha jamii na kuendesha shughuli za kibiashara na kiuchumi .“Serikali inaunga mkono juhudi zinazofanywa na Airtel na tunawaomba waendelee kuwekeza zaidi katika kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasiliano nchini. Tuko tayari kushirikiana Airtel katika kuhakikisha tunaweka mazingira bora ya kuendesha biashara ili kuwawezesha wananchi wetu kufaidika na huduma hizi za mawasiliano na hatimaye kuwa maisha bora,” alisema Dk Nchimbi.Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa wateja Adriana Lyamba alisema:”Leo tunazindua rasmi duka hili lenye muundo mpya lililopo katika barabara ya Mkuu hapa Dodoma ikiwa ni moja kati ya mikakati yetu ya kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma zetu na kupunguza msururu wa wateja wanaoingia dukani hapa kupata huduma mbalimbali. “ alisema.Aidha alisisitiza kwamba kupitia duka hilo wateja watapata huduma za pesa mkononi za Airtel Money ,intaneti na kuweza kununua muda wa maongezi pamoja bidhaa zikiwemo simu za mkononi na vifaa vya huduma za mawasiliano na huduma nyingine nyingi.Lyamba pia alisema Airtel imeendelea kuboresha maduka yake nchini ambapo hivi karibuni imezindua maduka yake mapya katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza Mbeya na Mtwara.Maduka mengine yaliyopo Morogoro, Bukoba na Zanzibar yanategemewa kuzinduliwa kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Septemba. | Biashara | 1 |
WAENDESHA bodaboda nchini wametakiwa kutochukua sheria mkononi inapotokea watu wamesababisha ajali wakiendesha barabarani.Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni alisema hayo mjini hapa jana wakati akijibu swali la Nyongeza la Mbunge wa Kuteuliwa, Salma Kikwete (CCM). Salma alitaka kujua serikali inachukua hatua gani kuelimisha waendesha bodaboda ambao wamekuwa wakichukua hatua za papo kwa hapo na kupiga watu waliosababisha tatizo au ajali.Salma alisema pamoja na bodaboda kuleta faida nyingi zikiwemo ajira, usafiri na maendeleo, kumekuwa na changamoto za kuchukua hatua mikononi mara watu wanaposababisha ajali. Masauni alisema waendesha bodaboda hawatakiwi kuchukua hatua wanaposababisha vifo ili waepuke kuingia katika mkono wa sheria wakipelekwa mahakamani na kufungwa.Masauni pia alijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Chwaka, Bhagwanji Maganlal Meisuria (CCM) aliyeuliza serikali ina mkakati gani kukomesha vitendo vya bodaboda kupora mali za abiria zikiwemo simu na mikoba ajalini.Masauni alisema waendesha pikipiki na bajaji wanaopora mikoba na simu za raia au abiria si wema bali wahalifu kama wahalifu wengine na hivyo Polisi wanatakiwa kuwashughulikia. Mbunge wa Musoma Mjini, Vedasto Manyinyi (CCM) alihoji lini serikali itatekeleza mkakati wa kupunguza tatizo la waendesha bodaboda kusababisha ajali za mara kwa mara na wizi. Masauni alisema vipo vyanzo vikuu vitatu vinavyosababisha ajali za barabarani nchini.Alivitaja vyanzo hivyo kuwa ni makosa ya binadamu ambayo huchangia kwa asilimia 76, ubovu wa magari asilimia 16 na mazingira ya barabara ambayo huchangia asilimia nane.Alisema makosa ya binadamu ni uendeshaji wa kizembe/ hatari, mwendo kasi, ulevi, uzembe wa wapanda pikipiki, wapanda baiskeli na watembea kwa miguu na sababu nyingine. Polisi inatoa elimu kwa waendesha boda namna nzuri ya utumiaji pikipiki ikiwemo kuvaa kofia ngumu, kukagua leseni kupunguza waendeshaji wasio na leseni wanaoweza kusababisha ajali. | Kitaifa | 0 |
Alisema asilimia 81 ya mabomba yameshawasili eneo la mradi kutoka China. Idadi ya mabomba inayohitajika ni 440 hali ambayo alisema inamfariji kuwa mradi huo utakamilika kwa wakati. Aliongeza kuwa mabomba zaidi ya nusu (kilometa 265 ) yameshaunganishwa kati ya kilometa 542 ambazo ndio umbali wa Mtwara hadi Dar es Salaam.Mtaro ambao umechimbwa hadi sasa ni kilometa 114 kazi ambayo Pinda alisema inaendelea vizuri na inasimamiwa na wataalamu wazuri kutoka Afrika Kusini na nchini. Kuhusu ubora wa mabomba, Pinda alihakikishiwa na mtaalamu mwelekezi anayesimamia mradi huo kuwa yana ubora wa hali ya juu.“Hili la ubora linatuhakikishia tusiwe na wasiwasi, kwani hawa wataalamu wamekwenda hadi China, kukagua utengenezaji wa mabomba haya na kuridhika na ubora wao,” alisema Pinda.Aliongeza kuwa uhai wa mabomba hayo chini ya ardhi ni miaka 30, na yakifanyiwa matengenezo yana uwezo wa kudumu miaka 50 hadi 70. Jambo ambalo linaonesha mradi utadumu kwa miaka mingi.Awali akimpa maelezo Waziri Mkuu, Mhandisi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Baltazar Mroso alisema kati ya kazi zinazofanywa ni kuweka zege kwenye mabomba yatakayotandazwa baharini umbali wa kilometa 25.Alisema asilimia 85 ya kazi ya kutandaza mabomba inafanywa na Watanzania, hivyo mradi umesaidia kuongeza ajira nchini.Pinda alikagua kiwanda cha kusiliba mabomba baharini na ya maeneo ya ardhi oevu kwa saruji, alitembelea maeneo wanayochimba mtaro wa mabomba, alikagua eneo linapoibukia bomba la baharini litokalo Songosongo na sehemu mabomba yanakopindwa. | Biashara | 1 |
WAKATI serikali ikiendelea na ujenzi wa reli ya kisasa kati ya Dar es Salaam na Mwanza yenye urefu wa kilometa 1,219 na pia kukarabati ile ya zamani maarufu kama `Reli ya Kati’, Shirika la Reli Tanzania (TRL), limetangaza kugeukia ujenzi wa reli za mijini, ikianza na Dar es Salaam na Dodoma.Lengo la reli hizo, limetajwa kuwa ni kuondoa msongamano katika maeneo ya mijini, lakini pia kuziunga sehemu zenye shughuli kuu za kiuchumi kama viwanda, ili kuweza kusafirisha bidhaa kwa urahisi.Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa alipokuwa anazungumzia mikakati mbalimbali ya kuimarisha usafiri wa reli nchini. Alisema kwa Dar es Salaam, mbali ya kuimarisha safari za sasa za ndani ya Dar es Salaam na maeneo jirani kama Pugu, zitajengwa pia reli mpya kati ya Mbezi na Bagamoyo, nyingine itakwenda Mbagala, lakini itakuwepo pia ya kwenda Uwanja wa Ndege.“Mpango huu wa kuwa na mtandao mpana wa reli za mijini unalenga kukabiliana na foleni, hasa ikizingatiwa katika miji na majiji kunakuwa na watu wengi, hivyo kukwamisha katika shughuli zao na foleni.“Ndiyo maana tunaangalia uwezekano wa kuwa na mtandao wa reli, tukianza na Dar es Salaam na Dodoma. Haya mambo yapo katika mipango kwa muda mrefu, ila kwa sasa tunakwenda kutenda. Ni suala la muda tu,” alisema Kadogosa ambaye ofisi yake inajiandaa kufyatua jingo la ghorofa saba eneo la Ihumwa, jirani na mji mkuu wa kiserikali wa Dodoma.Aliongeza kuwa reli hizo zitasaidia pia usafirishaji wa bidhaa kutoka viwandani, kwani zitakuwepo pia zitakazoungwa na viwanda ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na malighafi. Tayari Dar es Salaam kuna safari za treni za ndani ya jiji, ya Tazara- Pugu-Mwakanga, ya Stesheni ya Dar es Salaam-Pugu na Stesheni ya Dar es Salaam-Ubungo, ambazo zimetajwa kusaidia wakazi wake kutumia muda mfupi wa safari tofauti na mabasi ya abiria.Aidha, kwa kutumia usafiri wa treni, abiria wengi wamekuwa wakisafirishwa kwa wakati mmoja. Mathalani, kwa safari moja, treni kati ya Stesheni-Pugu husafirisha zaidi ya abiria 2,000 kutokana na mabehewa yake kati ya 19 na 23. Behewa moja hubeba abiria kati ya 80 na 120 na safari huchukua kati ya nusu saa na saa moja, wakati kwa safari kama hiyo kwa basi, abiria huweza kutumia hata saa 3-4. | Kitaifa | 0 |
Mshambuliaji Elius Maguli anayekipiga klabu ya Dhofar inayoshiriki Ligi Kuu Oman ndiye aliyefunga bao hilo dakika ya 18 kwa shuti. Taifa Stars sasa itamenyana na Zambia katika mechi ya nusu fainali baada ya Zambia kuitoa Botswana juzi katika robo fainali nyingine.Baada ya kufungwa bao hilo, Afrika Kusini walibadilika na kufanya mashambulizi mengi katika lango la Tanzania, lakini washambuliaji wao walikosa umakini na kushindwa kufunga. Taifa Stars walirudi nyuma na kujihami huku wakitumia mashambulizi ya kushtukiza, hadi mapumziko hakukuwa na mabadiliko.Kipindi cha pili, Afrika Kusini waliingia kwa kasi na kulishambulia zaidi lango la Tanzania, lakini washambuliaji wake walipoteza nafasi nyingi. Kocha Salum Mayanga alifanya mabadiliko, dakika ya 49 kwa kumtoa Thomas Ulimwengu na kumuingiza Simon Msuva aliyeonekana kukaa na mpira na kuwasumbua mabeki wa Afrika Kusini.Afrika Kusini walilisakama lango la Taifa Stars mara kwa mara lakini safu ya ulinzi chini ya nahodha Himid Mao na Erasto Nyoni ilihimili. Kocha wa Stars, Salum Mayanga aliwapongeza wachezaji wake kwa kuonesha juhudi kubwa uwanjani hata kupata matokeo hayo mazuri.Alisema wataendelea kucheza kwa nidhamu nusu fainali ili kutimiza lengo lao la kufika fainali na kutwaa ubingwa wa COSAFA. Maguli alichaguliwa mchezaji bora wa mechi hiyo na kukabidhiwa tuzo maalumu. Aliwashukuru mashabiki wa Tanzania waliojitokeza uwanjani hapo kuwashangilia. | michezo | 2 |
Lulu aliye nje kwa dhamana atapanda kizimbani mahakamani hapo baada ya kusomewa maelezo ya awali karibu miaka miwili na nusu iliyopita. Msanii huyo anakabiliwa na kesi hiyo akidaiwa kumuua Kanumba bila kukusudia kinyume cha Kifungu cha 195 cha Kanuni za Adhabu.Inadaiwa Lulu alimuua Kanumba bila ya kukusudia Aprili 7, 2012 nyumbani kwa marehemu huyo Sinza Vatican, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya kesi za mauaji ya bila kukusudia iliyotolewa na Mahakama Kuu Dar es Salaam jana, kesi hiyo itasikilizwa siku hizo na Jaji Sam Rumanyika. Kesi hiyo inaanza kusikilizwa baada ya kupangiwa Jaji kufuatia upelelezi kukamilika.Mara ya kwanza Lulu alipandishwa kizimbani Aprili 11, 2012 mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam wakati huo, Augustina Mbando ambapo alisomewa mashitaka ya mauaji.Hata hivyo, Februari 18, 2014 akisomewa maelezo ya awali Lulu alikiri mahakamani kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Kanumba na pia kusema kulikuwepo ugomvi baina yao siku ya tukio la kifo cha mwigizaji huyo.Lulu aliachiwa kwa dhamana Januari 29, 2013 baada ya kesi hiyo kubadilishwa hati ya mashitaka kutoka kwenye kesi ya mauaji kwenda mauaji ya bila kukusudia ambapo badiliko hilo lilimpa nafasi ya kupata dhamana.Katika kesi ya msingi namba 125 ya mwaka 2012, inadaiwa Aprili 7, 2012 Sinza Vatican Lulu alimuua Kanumba bila kukusudia. Lulu alipelekwa rumande gereza la Segerea hadi mashitaka yalipobadilishwa akapata dhamana. | michezo | 2 |
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula ametengua uteuzi wa nafasi ya Ofi sa Ardhi Mteule wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Paul Misuzi na wakuu wa idara za ardhi wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma na Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji.Hatua hiyo imekuja baada ya watendaji hao, kushindwa kutekeleza maagizo waliyopewa ikiwemo kushindwa kukusanya mapato ya serikali. Waziri huyo alichukua hatua hiyo katika kikao cha pamoja na watumishi wa idara ya ardhi wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma na Manispaa ya Kigoma Ujiji, kilichofanyika mjini Kigoma.Alisema kuwa watendaji hao, licha ya kushindwa kutekeleza maagizo ya serikali yaliyotolewa kwao, pia wameshindwa kuthibitisha uwezo wao wa kusimamia majukumu yaliyopo chini yao. Misuzi ni Afisa ardhi Mteule pekee kwa mkoa Kigoma, ambaye kitaaluma na kiutumishi, kwa mujibu wa taratibu za serikali, alikuwa na uwezo wa kusaini nyaraka kwa ajili ya mchakato wa utoaji wa hati za umiliki wa viwanja na majengo akiwa ameletwa mkoa Kigoma kwa mchakato maalum baada ya mkoa huo kutokuwa na Afisa Ardhi Mteule kwa muda mrefu.Pamoja na sifa hiyo na nafasi nyeti ya mtumishi huyo, naibu waziri huyo alisema kuwa Misuzi alishindwa kutekeleza mpango wa utoaji hati kwa waombaji, waliokuwa wakitaka kupatiwa hatimiliki za viwanja na majengo, licha ya kuwepo kwa maombi mengi kutoka kwa wananchi. Wengine waliotenguliwa katika sakata hilo ni Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, Brown Nziku na Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Halmashauri ya Wilaya Kigoma, Emanuel Maghembe.Viongozi hao wanadaiwa kwa miaka miwili tangu mwaka 2017, Naibu Waziri alipotoa maagizo, wameshindwa kufanyia kazi maagizo yaliyotolewa na kuandika taarifa zenye visingizio lukuki, ambavyo vinathibitisha kuwa uwezo wao wa kiutendaji ni wa chini. Jambo moja kubwa ambalo lilimuudhi naibu waziri huyo ni kitendo cha watendaji hao waandamizi wa idara ya ardhi, kushindwa kusimamia makusanyo ya fedha za serikali kupitia kodi za ardhi wakati suala hilo liko kwenye uwezo wao.Kwa mwaka wa fedha 2018/2019, walipanga kukusanya Sh bilioni 1.1, lakini kilichokusanywa ni Sh milioni 337. Naibu Waziri alisema kuwa watendaji hao, wameshindwa kutekeleza agizo la kuingiza kwenye mfumo wa malipo ya serikali ya ukusanyaji maduhuli viwanja vyote, ambavyo vimesharasimishwa kutokana na idadi ndogo ya viwanja ambavyo vimeingizwa kwenye mfumo huo, huku watendaji hao wakiwa hawajui takwimu za kiasi cha viwanja, ambavyo kiuhalisia vinapaswa kuingizwe kwenye mfumo huo.Kutokana na hali hiyo, naibu waziri alisema watendaji hao wamevuliwa hadhi na nyadhifa zao na watabaki kuwa watumishi na watendaji wa kawaida wa idara ya ardhi kwenye maeneo yao ; na nafasi zao zitatafutiwa watumishi wengine wa kuziongoza. Awali, Afisa Ardhi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Brown Nziku akitoa taarifa kwa naibu waziri alisema kuwa hadi kufikia Desemba 2018, viwanja 15,529 vimeingizwa kwenye mfumo wa ukadiriaji wa kodi ya ardhi huku viwanja 43,000 vikiwa vimefanyiwa michoro na kupangwa. | Kitaifa | 0 |
IKIWA zimebaki siku tatu, kuanza kwa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki, Jiji la Dar es Salaam limeweka mikakati mbalimbali kwa ajili ya kutekeleza agizo hilo katika mitaa mbalimbali.Aidha, uongozi wa mkoa, umeahidi kuwa kazi ya kutokomeza mifuko hiyo, haitakuwa ya nguvu wala usumbufu wowote na tayari vikosi kazi vimeshaundwa.Akizungumza jijini Dar es Salaam, katika mkutano wa viongozi mbalimbali wa jiji hilo, Katibu Tawala wa Mkoa, Abubakar Kunenge amesema mkakati huo una maeneo manne yakilenga katika kusimamia sheria na kanuni ambazo zitasaidia katika kutokomezwa kwa mifuko hiyo ambayo ina madhara makubwa.Alisema katika kutekeleza mkakati huo, elimu kwa umma ni jambo litakalozingatiwa, usimamizi na uratibu, eneo ambalo mifuko hiyo itawekwa pamoja na usimamizi na pamoja na kufanya kazi na wadau mbalimbali.“Dar es Salaam inaendelea kutoa taarifa ya maelekezo kwa wananchi, pia tunaendelea kutayarisha mabango ambapo mpaka sasa yameshatayarishwa saba pamoja na manispaa mbalimbali,” alisema Kunenge na kuongeza kuwa magari yanaendelea kupita mitaani kuelimisha wananchi.Alisema elimu ni suala endelevu kwa wananchi na kwa kiwango kikubwa wameonesha utayari wa kuacha matumizi ya mifuko hiyo, hivyo agizo hilo ambalo lilitolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa litafanikiwa kwa kiwango kikubwa.Alisema katika eneo la usimamizi tayari vikosi kazi mbalimbali vimeundwa kwa ajili ya kuwajibika na kuripoti kuhusu suala zima la utekelezwaji wa udhibiti wa mifuko hiyo na wakuu wa wilaya watapita katika maeneo yao kuona yaliyopangwa na utekelezaji wake.“Wananchi wameelezwa mahali pa kuweka mifuko hiyo, kuna vituo mbalimbali vya kukusanya vipatavyo 137 na katika vituo hivyo, mifuko haitakiwi kukaa kwa muda mrefu,” alisema Kunenge na kufafanua kuwa katika vituo hivyo vitakuwa vimefungwa kuepuka upepo lakini pia kutakuwa na walinzi kuepusha wananchi kufika na kuchukua mifuko tena.Alisema katika maeneo mbalimbali watu wameshatenga maeneo kuanzia ngazi ya mtaa kwa ajili ya kukusanya mifuko hiyo na kwamba kazi ya kuondoa mifuko pamoja na kupiga faini haitegemewi kuwa ni chanzo cha ufisadi na taarifa zitatolewa mara kwa mara.Awali Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema kazi ya kuzuia matumizi ya mifuko hiyo haitakuwa ya kutumia nguvu wala usumbufu wowote.“Jiji hili ndilo linalozalisha na kutumia mifuko hiyo kwa kiwango kikubwa, tukiweza kupiga hatua kwa asilimia 60 itakuwa ni hatua kubwa imefanyika,” alisema. | Kitaifa | 0 |
WAKATI michuano ya soka ya Ligi ya Mabingwa Afrika Mashariki na Kati, (Kombe la Kagame) ikianza leo kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Baraza la vyama vya soka ukanda huo, Cecafa, Nicholaus Musonye amesema viongozi wa vyama wanachama wanahujumu.Akizungumza na waandishi wa habari jana Musonye alisema wamejiandaa vizuri kufanikisha michuano hiyo inayoanza leo na kumalizika Julai 13 lakini hakusita kuweka wazi dukuduku lake kuwa viongozi wa vyama wanachama ndio wanaohujumu mashindano hayo kwa kuweka nguvu kwenye mashindano yenye fedha nyingi na kuacha kusapoti kazi ya kukuza michezo katika ukanda wao hali inayofanya kudorora.“Kuna mashindano yanayoendeshwa kwenye nchi zetu na viongozi wa vyama wanayakumbatia kwa sababu yana pesa nyingi na kusahau jukumu letu kama Cecafa la kuandaa mashindano ambayo ndiyo chimbuko la kuendeleza soka kwenye ukanda wetu, mimi nilikuwa Nairobi lakini sikwenda kuangalia,” alisema Musonye na kukataa kutaja amelenga mashindano gani.Pia Musonye alisema yeye amehudumu kwa muda mrefu kwenye Cecafa kama Katibu Mkuu lakini akitakiwa kuondoka ili waweke mtu mwingine yeye yupo tayari.“Kesho (leo) tutafungua mashindano rasmi na naamini tutafanya michuano bora na yenye wachezaji bora wanaoweza kupambana kwani kila timu hasa zile zinazoshiriki mashindano ya kombe la Shirikisho Afrika zimeleta timu nzima,” alisema Musonye.Aidha Musonye aliziombea timu zilizojitoa kwenye mashindano hayo kwa madai ya kujiandaa na michezo ya kombe la Shirikisho Afrika kufika mbali na hata kutwaa ubingwa kwani hakupenda kuzitamkia maneno mabaya kwa wakati huu.Yanga na St George ya Ethiopia ndizo zilizojitoa kwenye michuano hiyo zikidai kutaka muda wa kujiandaa zaidi na michuano ya Afrika.Kaimu Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani alisema wamejiandaa ipasavyo kukamilisha michuano hiyo ya Kombe la Kagame.Michuano hiyo inazinduliwa leo ambapo mechi ya ufunguzi itakuwa saa nane mchana kati ya JKU ya Zanzibar dhidi ya Vipers ya Uganda kabla Azam FC haijacheza na Kator ya Sudan Kusini na saa kumi jioni na saa moja usiku utachezwa mchezo wa Kundi C kati ya Singida United na APR ya Rwanda. Mechi zote zitachezwa uwanja wa Azam Complex Chamazi. | michezo | 2 |
SERIKALI imezitaka halmashauri zote zinazojenga hospitali za wilaya mkoani Lindi, zimalize kwa wakati uliopangwa bila kutoa sababu na kusababisha ujenzi wa hospitali hizo kuchelewa zaidi.Hayo yalibainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo mwishoni mwa wiki wakati alipokagua Hospitali ya Wilaya ya Lindi inayojengwa katika kata ya Kiwalala. Ujenzi wa hospitali hiyo unagharimu Sh bilioni 1.5 zilizotolewa na serikali kuu.Waziri Jafo alisema katika halmashauri nyingi tayari fedha za ujenzi wa hospitali hizo za wilaya zimeshatolewa, hivyo ni vyema ujenzi wake ukamilike mapema bila sababu zisizo za msingi. Alisema amekuwa akipokea sababu nyingi kutoka kwa wakurugenzi kuhusu kutokamilika kwa wakati kwa ujenzi wa hospitali hizo, jambo ambalo kuanzia sasa hatolikubali tena.“Unasikia mkurugenzi anakuambia njia ilikuwa haipitiki, mara maji shida, hizi ni baadhi ya sababu nyingi tu ambazo hazina athari ya kusababisha mradi usiishe kwa wakati unaotakiwa,”alisisitiza. Alisema ni lazima majengo saba ya hospitali mkoani humo yakamilike haraka hadi kufikia Juni 30, mwaka huu, ili wananchi wapate huduma safi na ya karibu ya afya.“Sitamvumilia mkurugenzi yeyote yule anitolee sababu za ujenzi wa hospitali uchelewe kukamilika, mimi sitamuelewa kabisa,’’ alisema. Pamoja na hayo, Waziri Jafo alionesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi unaoendelea katika hospitali hiyo ya Lindi ambao umefikia katika hatua ya kuezeka bati. Aliimpongeza Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye kwa kazi aliyoifanya ya kufuatilia hospitali hiyo mpaka kujengwa hapo Kiwalala wilayani Lindi.Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya, Dismas Masulubu alisema serikali kuu ilishatoa Sh bilioni 1.5 na mpaka sasa zimeshatumika Sh milioni 950. Alisema ujenzi wa hospitali hiyo ulianza Januari na unatakiwa ukamilike Juni 30, mwaka huu ambapo majengo saba, kati ya 22 ya hospitali hiyo yanayotakiwa kujengwa mwaka huu.Dk Masulubu alisema majengo hayo saba yanahusisha pia jengo la wazazi, mapokezi, maabara, x-ray, kufulia nguo, upasuaji na jengo la watoto wachanga. Diwani wa Kiwalala, Mohamedi Chilumba alisema tangu kuanzishwa wilaya ya Lindi mwaka 1983 haijawahi kuwa na hospitali ya wilaya. | Kitaifa | 0 |
['Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars hii leo imeandikisha sare 1-1 na timu ya taifa ya Burundi Intamba Murugamba katika mechi za kufuzu kwa kombe la dunia nchini Qatar 2022.', 'Licha ya kutawala kipindi cha kwanza cha mchezo Tanzania ilishindwa kuona lango la wenyeji wao huku washambuliaji hodari Mbwana Samatta anayeichezea klabu ya Genk nchini Ubelgiji na Simon Msuva wakishindwa kuwika katika lango la Burundi.', 'Kipa wa Burundi Jonathan alikataa katakata kufungwa na wachezaji hao wawili kupitia uokoaji wa hali ya juu.', 'Udhaifu wa Burundi ulionekana katika utoaji pasi sawala lililopelekea kipindi cha kwanza kukamilika kwa sare tasa.', 'Burundi hatahivyo ilitawala kipindi cha pili cha mchezo mbele ya mashabiki wao baada ya kocha wake Olivier Niyungeko kufanya baadhi ya mabadiliko miongoni mwa wachezaji wake.', 'Mbwana Samatta alikosa bao la wazi akiwa amesalia na kipa wa Burundi aliyepangua shambulizi lake na kuisaidia pakubwa Intamba Murugamba.', 'Hatahivyo kunako dakika ya 81 ni Burundi ndio ilioanza kuona lango la wageni wao kupitia mchezaji Cedric Hamissi anayechezea soka yake nchini Tanzania ambaye alipokea pasi muruwa kutoka kwa Mohamed Amissiwari aliyeingia katia nafasi ya Bienvenue kanakimana.', 'Hatahivyo Tanzania waliimarisha mashambulizi yao kunako dakika hizo za lala salama na haikuchukua muda mrefu wakati Simon Msuva aliposawazisha dakika tatu baadaye.', 'Mechi ya marudio iutachezwa nchini Tanzania wikendi ijayo tarehe 8 mwezi Septemba.', 'Mshindi wa mechi hiyo atafuzu kwa raundi ya pili ya michuano hiyo.'] | michezo | 2 |
AZAM FC jana ilikata tiketi ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam baada ya kuifunga Kagera Sugar kwa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba,Kagera.Katika mchezo huo bao pekee lililoifanya Azam kusonga mbele liliwekwa kimiani na Joseph Mahundi dakika ya 79 baada ya kuwatambuka mabeki wa Kagera na kuachia shuti hafifu lilomshinda mlinda mlango wa Kagera Jeremia Kisubi. Azam sasa inaungana na timu za Lipuli FC na KMC kufika hatua hiyo. Robo fainali ya mwisho inatarajiwa kuchezwa leo kati ya Yanga na Alliance.Na baada ya kupata ushindi huo Azam wanatarajiwa kukutana na KMC, kwenye hatua inayofuata ya nusu fainali. Mchezo wa jana ulianza kwa kasi kubwa huku kila timu ikicheza kwa umakini mkubwa wakihofia kuruhusu bao la mapema kwenye lango lao lakini mpaka mapumziko hakukuwa na timu iliyoliona lango la mwenzake.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kila timu ikifanya mabadiliko wakiwa na matarajio ya kubadilisha mchezo ili wapate matokeo mazuri . Azam ililazimika kumaliza mechi pungufu baada ya mlinda mlango wake Razak Abarola kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mchezaji wa Kagera Sugar nje kidogo ya eneo la hatari. | michezo | 2 |
SAKATA la askari polisi wanane wanaodaiwa kujihusisha na kashfa ya utoroshaji dhahabu jijini Mwanza, limetua rasmi kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Boaz.Askari hao ambao Januari 4, mwaka huu, waliwakamata watu waliotaka kutorosha kilo 323.6 za dhahabu yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 30 na fedha taslimu Sh milioni 305, walitaka wapewe Sh bilioni 1 kutoka kwa watuhumiwa hao. Baada ya mpango wao huo kukwama kutokana na mamlaka za nchi kuingilia kati na watuhumiwa kutiwa mbaroni na askari wenzao, kinachoendelea kwa sasa ni uchunguzi wa suala hilo ili watuhumiwa waweze kufikishwa mahakamani.DCI Boaz, katika mahojiano maalumu na gazeti hili jana, alisema ofisi yake itakamilisha upelelezi wa jambo hilo hivi karibuni. Alisema kuwa upelelezi unaoendelea, utawasaidia kujua ni makosa ya aina gani watuhumiwa hao wanane, wanakabiliwa nayo ili mashitaka dhidi yao yaweze kufunguliwa. Alisema kwa kuwa watuhumiwa hao ni askari, watapelekwa kwanza kwenye Mahakama ya Kijeshi kwa ajili ya mashitaka ya kinidhamu na kama kutakuwa na jinai yoyote dhidi yao, ndipo watakapopelekwa kwenye Mahakama za Kiraia.Wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam juzi, akiwemo Waziri wa Madini, Doto Biteko, makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu, katibu tawala mmoja na makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Rais John Magufuli aliwaeleza Watanzania mpango mzima ulivyokuwa. Kwa mujibu wa Rais Magufuli, askari hao baada ya kuwakamata watuhumiwa, waliwafikisha Kituo Kikuu cha Polisi Mwanza, lakini hawakushushwa kwenye gari, badala yake walichokifanya ni kuwataka watuhumiwa wawepe Sh bilioni 1.Baada ya majadiliano yao, watuhumiwa katika mkupuo wa kwanza, waliwapatia askari hao Sh milioni 300, mkupuo wa pili wakawapa Sh milioni 400 na kuahidi kumaliza mkupuo wa tatu wa Sh milioni 300 watakapofika wilayani Sengerema. Wakiwa njiani kuelekea Sengerema, ndipo walipokutana na kizuizi cha polisi njiani na watuhumiwa wote wakiwemo askari hao wanane wakatiwa mbaroni. Kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na jeshi hilo, Rais Magufuli alimpongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro kwa kazi nzuri iliyofanyika.Ili kufanikisha kazi hiyo ya kufuatilia utoroshaji wa dhahabu na madini mengine nchini, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamanda Ahmed Msangi, alisema kuwa msingi wao mkubwa wa kufanikisha kazi hiyo ni wananchi. Alisema Jeshi la Polisi litafanya kazi kwa karibu na wananchi, ikiwemo kuwapatia elimu ili wananchi hao waweze kushirikiana na jeshi hilo, kwa kutoa taarifa kuhusu utoroshaji huo. | Kitaifa | 0 |
AGIZO la Rais John Magufuli la kumtaka Msajili wa Hazina kuyabana mashirika ya umma ili kulipa gawio kwa serikali, hatimaye ofisi hiyo imevuka lengo kwa kukusanya Sh bilioni 633.39 hadi kufikia Juni mwaka huu, sawa na asilimia 106.Fedha hizo zinatokana na makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi kutoka katika taasisi, mashirika na kampuni ambazo serikali ina hisa.Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka amesema wamevuka lengo ambalo waliliweka la kukusanya Sh bilioni 597.77 mwaka huu.“Kwa mwaka 2019 tulijiwekea lengo la kukusanya Sh bilioni 597.77 lakini hadi Juni 21, mwaka huu, tulikuwa tumeshavuka lengo kwa sababu tumekusanya zaidi ya Sh bilioni 633, sawa na asilimia 106 hadi sasa na bado tunaendelea kukusanya,”alisema Mbuttuka.Akizungumzia idadi ya mashirika na taasisi hizo zinazotoa gawio, Mbuttuka alisema zimeongezeka kutoka 13 mwaka 2015 hadi kufika 28 mwaka 2018 na kwamba uchangiaji wa mapato umeongezeka.Akifafanua mgawanyiko wa taasisi hizo na aina ya uchangiaji unaotolewa, Mbuttuka alisema taasisi hizo zimegawanyika katika sehemu kuu tatu: Sehemu ya kwanza ni gawio linalotoka katika mashirika ambayo serikali inamiliki kwa kiasi kikubwa na kampuni ambazo serikali ina hisa chache na kwamba gawio hilo hulipwa kwa mujibu wa Sheria ya Msajili wa Hazina ya Madaraka.Sehemu ya pili ni michango ya asilimia 15 ya mapato ghafi kutoka katika taasisi za serikali, ambao unalipwa kwa mujibu wa Kifungu cha 47 cha Sheria ya Fedha Namba 15 ya mwaka 2015 iliyorekebisha Sura ya Msajili wa Hazina Sura ya 370.Sehemu ya tatu ni makusanyo mengineyo ambayo yanajumuisha marejesho ya ziada, marejesho ya mikopo na riba kutokana na serikali kukopesha mashirika (on-lending) na makusanyo ya Mtambo wa Kuhakiki Mawasiliano ya Simu (TTMS).Alisema makusanyo yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na kuimarika kwa utendaji wa mashirika pamoja na jitihada za Ofisi ya Msajili wa Hazina katika kufuatilia mapato husika.Pamoja na kuimarika kwa makusanyo na utendaji wa mashirika, Mbuttuka alisema kumekuwa na baadhi ya mashirika hayafanyi vizuri na kwamba, jitihada zimefanyika ikiwa ni pamoja na kuimarisha utendaji wa bodi za wakurugenzi na menejimenti.Aidha amezielekeza taasisi hizo, zijikite katika majukumu ya msingi ya uanzishwaji wake kwa kuwa amebaini baadhi ya mashirikia hayo yamekuwa yakitoka nje ya kazi za msingi ambazo zimesababisha athari zisizo za lazima.Pia hatua kadhaa zimechukuliwa, ikiwemo kuongeza mitaji kwa mashirika stahiki baada ya uchambuzi na kujiridhisha na uhitaji huo na mfano halisi ni Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Benki ya Rasilimali nchini (TIB).Alisema hatua nyingine zilizochukuliwa ni kupunguza, kuunganisha na kuhamisha majukumu yanayofanana baina ya taasisi na mashirika ya umma ili kuongeza tija na kupunguza mzigo kwa mashirika hayo.“Tutaendelea kuboresha na kuyapitia mashirika yote yanayotuhusu ili tuone jinsi ya kuyaboresha na yale yasiyoweza tutatafuta njia nyingine ambazo tumeanza kufanya kama ni kuyaunganisha, lengo ni kupata matokeo bora zaidi, lakini kubwa ni kuhakikisha utawala bora unazingatiwa na watumishi wote,” alisisitiza Mbuttuka.Mara kadhaa Rais Magufuli amekuwa anamuagiza Msajili wa Hazina, kuzibana kampuni za umma zisizolipa gawio serikalini.Mara ya mwisho ilikuwa hivi karibuni wakati akipokea gawio la Sh bilioni 2.1 kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL). | Biashara | 1 |
MKOA wa Pwani umewalipa wakulima wa zao la korosho Sh bilioni 60.6 kwa msimu wa mwaka 2018/19.Pia korosho tani 46 za daraja la kwanza ziliuzwa kwa Sh 2,571 na daraja la pili ziliuzwa tani 109 kwa Sh 2,075 ambapo hadi Desemba jumla ya tani 765 zimeuzwa.Akizungumza katika Kikao cha Ushauri cha Mkoa (RCC) kilichofanyika mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Mkoa, Evarist Ndikilo alisema kwa wakulima ambao hawajalipwa serikali inaendelea na uhakiki ili kuwalipa walengwa.“Korosho itakayolipwa ni ile itakayokuwa imepelekwa kwenye ghala kuu lakini zile zilizo kwenye vyama vya msingi vya ushirika watalipwa huko huko,” alisema Ndikilo.Alisema hadi sasa kuna tani zaidi ya 6,000 ziko kwenye vyama vya ushirika vya msingi (Amcos) na korosho nyingine ziliharibika kutokana hali ya mvua na ukosefu wa magunia.“Korosho nyingi ziko kwenye Amcos na hazina ubora unaotakiwa na iliamuliwa korosho zipimwe ubora kabla ya kupelekwa ghala | Biashara | 1 |
SERIKALI imetoa tahadhari kwa shule 108 za msingi, sekondari na za ufundi kwa kushindwa kukidhi matakwa ya wizara hiyo.Ripoti mpya ya Wizara ya Elimu inasema shule hizo zimebainika kutokidhi viwango vya usafi, matumizi mabaya ya ruzuku, kushindwa kutoa elimu na matumizi mabaya ya vifaa vya teknolojia ya mawasiliano.Hatua hiyo ni mikakati ya wizara kuhakikisha shule zinafuata vigezo vya kutoa elimu bora. Agosti mwaka huu, wizara ilisitisha huduma za shule 57 nchini lakini baadaye zilifunguliwa baada ya kukidhi matakwa ya wizara.Waziri wa Elimu, Eugene Mutimura, alisema serikali haitawavumilia viongozi wa shule zilizoshindwa kufikia viwango. “Kuna shule ambazo hazitafunguliwa Januari ikiwa watashindwa kukamilisha yale waliyoshauriwa wakati wa ukaguzi,” alisema.Aliongeza kuwa shule 31 zilikaguliwa kutokana na matumizi mabaya ya rasilimali za serikali, huku nyingine 17 zikitakiwa kupewa ushauri katika utoaji elimu. Takribani shule za msingi, sekondari na vyuo vya ufundi na taasisi za elimu ya juu 900 zilikaguliwa, hivyo hawatawaeleza nini wafanye bali kutimiza wajibu wao katika nyanja zote. | Kimataifa | 3 |
TANZANIA na Uganda zimeanzisha rasmi Jukwaa la Biashara baina ya nchi hizo, lengo likiwa kufungua milango zaidi ya biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).Mbali ya Tanzania na Uganda, nchi nyingine wanachama wa EAC, jumuiya yenye wakazi zaidi ya milioni 170 ni Kenya, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo hivi karibuni jijini Kampala, Waziri wa Nchi wa Uganda anayeshughulikia masuala ya EAC, Dk Philemon Mateke alisema jukwaa linatarajiwa kuwa `daraja’ muhimu katika sekta ya biashara baina ya Tanzania na Uganda.“Hatuna sababu za kutofanya biashara kwa uwazi na kisasa zaidi kwani nchi zote hizo zimetengeneza mazingira mazuri ya biashara. Nchi zote zina amani, miundombinu mizuri na kadhalika.Ni wakati wa kuchangamka kibiashara,” alisema Dk Mateke. Kutokana na kuzinduliwa kwa jukwaa hilo, alisema kwa siku mbili kuanzia Septemba 4 mwaka huu, wadau muhimu watakutana Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali yatakayoboresha ustawi wa biashara. Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Richard Kabonero alisema mkutano huo utafanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), ukiwa na kaulimbiu ‘Ukuzaji Biashara na Uwekezaji kwa Ukuaji na Maendeleo Endelevu’.Miongoni mwa washiriki watakuwa viongozi wa taasisi za kibiashara, watunga sera, wadau wa biashara na wengine, ili pamoja na mambo mengine kuchambua fursa zilizopo baina ya nchi hizo mbili na jinsi zinavyoweza kuleta neema kwa watu wa mataifa hayo.Alisema wakati wa mkutano, watazungumza pia na Rais Yoweri Museveni wa Uganda na mwenzake wa Tanzania, Dk John Magufuli juu ya masuala mbalimbali na changamoto za kibiashara baina ya nchi zao. Naye Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Aziz Mlima, alisema mikakati ya kukuza biashara baina ya nchi hizo mbili, ikiwa ni pamoja na kuondoa vikwazo mbalimbali inafanyiwa kazi ili kutengeneza mazingira bora ya biashara. | Kitaifa | 0 |
WAHADHIRI wa vyuo vya elimu ya juu wameunga mkono kauli ya Rais John Magufuli kwamba baadhi ya shahada zinazotolewa na vyuo vikuu sasa hazina hadhi bali wanafunzi wanamaliza vyuo ili kupata vyeti.Aidha wameshauri kufanyika kwa maboresho ya elimu na kuwe na msukumo wa kuwajali walimu kimaslahi lakini pia kuwaendeleza kitaaluma.Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, wasomi hao wamesema tatizo la shahada za ‘kudesa’ katika vyuo vikuu nchini ni kubwa na linahitaji ufumbuzi wa kudumu ili kuhakikisha nchi inapata wasomi wazuri wanaomaliza vyuo na vyeti vinavyolingana na elimu waliyoipata.Juzi Rais Magufuli akizindua Maktaba ya Kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) aliutaka uongozi wa chuo hicho kuhakikisha shahada wanazotoa zina viwango vya juu na si shahada za ‘kudesa’ na kuwataka wahadhiri kuwa wakali.Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dk Frank Tillya alisema walimu wanaowafundisha wanafunzi hao nao pia wanachangia kwa kiasi kikubwa kuporomoka kwa elimu ya vyuo vikuu."Walimu nao wanachangia kwa kiasi kikubwa, wengi hawana maadili kwa sababu kama una maadili huwezi kukubali kuona mwanafunzi anatoka hajui kitu, wanafunzi wengi wanatoka hawana kabisa quality (kiwango) ya shahada kwa sababu hawakufundishwa kufikiri," alisema.Alisema wanafunzi wengi wanafanya tu mitihani ili kufaulu, lakini elimu yao haiakisi hadhi ya shahada hata wanapomaliza vyuo, jambo ambalo linaleta changamoto katika kupata kazi kwani wanakuwa hawana uwezo wa kushindana."Hata ukiangalia 'interview' za kazi utabaini tatizo kubwa kwani vyeti wanavyokuja navyo vinakuwa na ufaulu mkubwa lakini wanapohojiwa unabaini kichwani hawana ujuzi unaofanana na ufaulu wao,” alisema.Dk Frank alisema ingawa Rais Magufuli hakueleza kwa kirefu ukubwa wa tatizo hilo, lakini ni suala linalohitaji mjadala wa kitaifa ili kulipatia ufumbuzi wa kudumu.Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana alisema shahada ya sasa haimfanyi mhitimu kupata uwezo wa kuchanganua mambo wala kufikiri kwa mapana."Hili ni tatizo la kitaifa sijui tumejikita zaidi katika elimu nyingine, kijana amehitimu chuo lakini ukimwambia akuandikie barua au mpe habari ya kurasa tatu mwambie aifupishe hawezi," alisema Dk Bana.Hata hivyo, Dk Bana alisema moja ya sababu ya kushinda kuimarika kwa kiwango cha elimu ni mfumo wa elimu ya juu ambao alisema hauvidhibiti vyuo kuzalisha elimu bora kwa kiwango cha kutosha.Aidha alisema baadhi ya walimu wanatekeleza wajibu tu lakini hawana moyo wa kuwasaidia wanafunzi kupata maarifa na wengine hawana sifa kabisa za ualimu ambapo alishauri kufanyike maboresho ya elimu ya juu.Alisema elimu ya vyuo vikuu inashuka hasa vyuo vinavyoanzishwa sasa na kwamba mwanafunzi anavyojibu mtihani wake na alama anazopewa na mwalimu wake havilingani na kwamba wanafunzi wanataka matokeo mazuri bila kuyasumbukia.Na aliyewahi kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Profesa Tolly Mbwete amesema uongozi wa vyuo uwe tayari kushughulikia tatizo hilo ili kuongeza ubora wa elimu nchini.Alisema tatizo hilo lipo katika vyuo vingi kwani wanafunzi wengi hawana bidii ya kujisomea ili kupata maarifa badala yake wanataka kuhitimu ili wapate vyeti safi vya kwenda kutafutia ajira. | Kitaifa | 0 |
BAADA ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa, Yanga wametamba kuifunga Pyramids katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.Yanga watashuka dimba CCM Kirumba Jumapili kuikaribisha Pyramids ya Misri katika mchezo wa ply-off wa kusaka nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.Timu hizo zinatarajia kurudiana Novemba 3 Misri. Kocha msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila (pichani) alisema kwa sasa akili na nguvu zao zote wanazielekeza katika mchezo huo wa Jumapili na wana matumaini makubwa ya kushinda, Alisema anawaomba wadau na wapenzi wa soka wa timu yao wajitokeze kwa wingi katika kuipa timu yao sapoti iweze kufanya vizuri zaidi na kurahisisha njia yao ya kufuzu.Akielezea kuhusu mchezo wao dhidi ya Mbao FC,Mwandila alisema mchezo huo ulikuwa ni mgumu sana, lakini timu yake ilicheza vyema kwa kupambana zaidi na kufanikiwa kuibuka na ushindi huo.Aliwapongeza wachezaji wake kwa kupambana na kuibuka na ushindi licha ya ugumu wa mchezo huo. Alisema wapinzani wao wa Mbao FC walipambana pia huku akiwa na matumaini ya timu yake kupambana Jumapili na kupata matokeo mazuri. Alisema ushindi wa Mbao FC ni kiashiria kuwa timu yake itaifunga timu ya Pyramid FC kutoka nchini Misri.Kwa upande wake nahodha wa timu ya Yanga Pappy Tshishimbi alisema wamejipanga kuhakikisha na wanapata ushindi katika mchezo wa Jumapili na ule wa marudiano nchini Misri ili kutinga makundi. | michezo | 2 |
KUPITIA Mfumo wa Mawasiliano ya Simu (TTMS) Serikali imepata zaidi ya Sh bilioni 93.6 fedha ambazo kama sio mfumo huo zingekuwa kwenye mifuko ya watu.Takwimu hizo zilitolewa Dar ea Salaam jana na Rais John Magufuli wakati akikabidhiwa rasmi mfumo huo ambao unasimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili kuthibiti mawasiliano pamoja na mapato ya huduma ya Mawasiliano ya simu hapa nchini. Rais Magufuli alisema:“Bila kuwa na mfumo huu huwezi kuhakiki mapato yatokanayo ya Mawasiliano ya simu, TRA hawakuweza kukusanya kodi iliyostahili, mtambo huu unahakiki mapato.”Mfumo huo ulikabidhiwa na Kampuni ya TMS na GBG kwa TCRA ambapo Rais Magufuli alisema sasa kila kitu kiko wazi katika sekta hiyo kwani hakuna fedha itakayopotea.Alisema kupitia mfumo huo kampuni za kutoa huduma ya mawasiliano pia zimenufaika kwa kupata Sh Bilioni 173.93 na mkandarasi Sh bilioni 53.52 na Sh bilioni 13.3 wamepata TCRA kupitia simu za kimataifa.Rais Magufuli aliipongeza TCRA kwa kazi wanayoifanya sasa kwani alipoingia madarakani hakupendezwa na utendaji kazi wao palikua na mchezo mbaya. “Palikua na mchezo mbaya sana, Tanzania tumeibiwa mno, tumechapwa ukweli, tumeliwa kweli, tumedhulumiwa vya kutosha,” alisema.Alisema 2015 alipoingia madarakani aliamua kuutafuta mkataba wa wakandarasi hao ambapo mkataba halisi ulifichwa na kuwa kipengele kilichohusu kukusanya fedha kwenye kampuni za mawasiliano kilifichwa hivyo ilibidi atumie vyombo vya ulinzi akaupata mkataba huo.“Nilichofanya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Simba nikatengua uteuzi wake nikamtoa kwanza tukapeleka mabadiliko kwenye Bunge na Spika na watu wake wakakiweka kipengele kilichokua kimefutwa kwa ujanja ujanja uliofanywa na baadhi ya viongozi waliokuepo serikali ni,” alisema Rais Magufuli.Alisema baadaye mkandarasi aliamriwa kurudi kukamilisha kipengele kilichofichwa kwenye mkataba na baada ya kutimiza sasa wamekabidhi kazi. Rais Magufuli alisema aliongeza mkataba wa miaka mitano zaidi kwa mkurugenzi Mkuu wa TCRA ili aendelee kufanyia kazi mfumo huo.Alisema takwimu za kidunia zimeonesha kuwa sekta ya Mawasiliano ni nyeti na muhimu na inakua kwa kazi duniani, zaidi ya watu bilioni tano wanatumia simu duniani kote na wanaotumia data ni milioni 3.9 na kwa Tanzania, wanaotumia simu ni zaidi ya watu milioni 42.“Biashara nyingi ya rejareja zinaendeshwa kwenye mitandao na kwa mwaka 2017 biashara hiyo iliyofanyika kwenye mitandao zilikua na thamani ya dola za Marekani trilioni 2.3 kupiku biashara za kwenye maduka makubwa na maduka ya kawaida,” alisema rais.Aidha alisema sekta ya mawasiliano imewezesha kupatikana kwa huduma ambazo awali hazikuwepo mathalani afya, elimu, usafiri wa teksi, kibenki ambapo zaidi ya watu milioni 20 wamejiunga na huduma za kibenki mitandao na pia ndio uliosaidia serikali kufingia simu hafifu milioni moja na kufahamu vifaa vyote vinavyotumia mtandao.Alisema sekta hiyo imetoa ajira zaidi ya milioni 28 za moja kwa moja na kufanya sekta hiyo kuitwa kisima kipya cha mafuta au mgodi wa madini. Hata hivyo, alisema sekta hiyo inachangamoto zake ambazo ni pamoja na uhalifu wa mtandao na kuathirika mila na desturi.“Kukabiliana na changamoto hizi serikali imekua ikianzisha mamlaka na mfumo mbali mbali kudhibiti na sisi tumeanzisha mamlaka kutunga sera, sheria na kuweka miundombinu pamoja na mfumo huu wa TTMS kufatilia takwimu za Mawasiliano,” alisema.Rais Magufuli pia alitoa mwito kuujengea uwezo mfumo huo na kuusimamia isitokee yaliyotokea katika mfumo wa kukusanya kodi wa TRA, EFD. “Wote tunajua yaliyotokea katika mfumo wa EFD, mtambo haukua Tanzania lakini sasa tumebadili uko hapa nchini nchini ya Wizara ya Fedha,” alisema.Rais aliagiza pia taasisi zote za serikali ambazo zinahusika na ukusanyaji mapato ya serikali kutengeneza mfumo wa kukusanya mapato na pia kuunganishwa na mfumo wa taifa. “Kati ya taasisi 667 ni taasisi 339 tu zimeunganishwa, Waziri wa fedha nataka uwaandikie barua nakala apewe Waziri Mkuu na mimi nipewe nakala yangu ili niweze kufuatilia,” alisema.Rais Magufuli pia aliwashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kumuombea na kuongeza kuwa vita ya uchumi inahitaji maombi na kuwa matatizo yaliyopo sasa serikali hii isipoyatatua hayatatatuliwa tena. Akizungumzia mfumo huo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba alisema kukamilika kwa mfumo kumewezesha kuonesha taarifa mbalimbali zinazopita katika Mawasiliano hapa nchini.Aidha, alisema Mfumo unaiwezesha TCRA kupata takwimu za Mawasiliano ya simu yanayofanyika ndani na nje, kuhakiki mapato ya watoa huduma, kupata takwimu zinazohusiana na huduma za mawasiliano ya sauti, data na ujumbe mfupi, kubaini Mawasiliano ya ulaghai, kutambua takwimu za fedha za mitandaoni na kusimamia ufanisi na ubora zaidi viwango vya mawasiliano kwenda kwa watoa huduma, kuwasililisha mapato ya Mawasiliano ya kimataifa.“Toka mwaka 2013 mfumo ulipoanza kufanya kazi mpaka Septemba 2018 serikali imepata chanzo kipya cha Mawasiliano yanayotokana na Mawasiliano ya kimataifa zinazoingia na kuishia hapa nchini na kiasi cha Sh bilioni 93 ziliwasilishwa serikalini,” alisema.Aidha alisema pato la kodi limeongezeka na kwamba simu za kimataifa zilikua zinaingia kiulaghai. Mfumo umewezesha kubaini watu wenye mfumo mingine ya ulaghai kuingiza simu za nje kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, sasa simu zinazoingia kwa njia za ulaghai ni asilimia kumi wakati awali zilikua zaidi ya asilimia 60.Malaba alisema sasa TRA na BOT zinapata taarifa ya kiasi cha fedha na kuwa awali zilikua Sh trilioni nane kwa mwezi na kwa mwaka jana kufikia Sh trilioni 11. Mkurugenzi huyo aliahidi wataendelea kuboresha mfumo huo kutanua wigo ili kuendelea kutoa huduma na kuongeza mapato kwa serikali ambapo aliahidi mamlaka hiyo kuutunza mfumo wa TTMS.Alisema chimbuko la kuanzishwa mfumo huo ni Bungeni baada ya malalamiko ya gharama za simu zinazoingia nchini kushuka kila kukicha hali ambayo ilipunguza mapato kwa watoa huduma na pia kodi kwa serikali na mchango katika uchumi.“Ilionekana hitaji la mfumo huu, TCRA ilisimamia manunuzi ya mfumo huu na Machi 22, 2013 kwa lengo la kutekeleza mradi ikiwa ni kujenga kuendesha na kuhamisha umiliki Octoba mosi 2013 mkataba wa miaka mitano Septemba 2018 mkataba huo umemaliza muda wake,” alisema.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema gharama ya kuunganisha mitandao imepungua kutoka Sh 30.58 iliyokuwepo mwaka 2015 hadi kufikoa Sh 10 kwa dakika kwa mwaka huu na itaendelea kupungua ifike Sh mbili mwaka 2022.Alisema ilani ya Chama cha Mapinduzi ilielekeza kulinda wananchi dhidi ya wizi wa mtandao ambapo wanaendelea kusajili kwa kutumia alama za vidole kuendelea kuzuia wizi huo. | Kitaifa | 0 |
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linaendelea kumshikilia Mwenyekiti wa Kijiji cha Bangata, wilayani Arumeru, Michael Silamoi kwa tuhuma za kumshambulia hadi kumsababishia kifo mmoja wa wanakijiji wa kijiji hicho.Mbali na Mwenyekiti huyo, wengine wanaoshikiliwa ni askari mgambo wawili wa kijiji hicho waliofahamika kwa majina ya Balozi Andrea na Wariael Obedi pamoja na mkazi mwingine aliyefahamika kama Onesmo Siyoi.Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO), Hassani Omary akizungumza na gazeti hili jana alithibitisha Mwenyekiti huyo na wenzake watatu kuendelea kushikiliwa na jeshi hilo kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa tangu kukamatwa kwao Januari 8, mwaka huu.“Ni kweli Mwenyekiti wa kijiji cha Bangata na wenzake watatu tunaendelea kuwashikilia kwa tuhuma za kumpiga hadi kusababisha kifo cha Stalei Samwel (29) kilichotokea Januari 3, na jalada la kesi hiyo tumeshalipeleka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi za kisheria,” alisema.Mkuu huyo wa Upelelezi wa Mkoa wa Arusha aliongeza kuwa watuhumiwa hao hawawezi kuachiwa kwa dhamana kutokana na kuwa wanatuhumiwa kwa mauaji na kinachosubiriwa ni taratibu zikamilike ili wafikishwe mahakamani kujibu tuhuma hizo zinazowakabili.Akizungumza na gazeti hili kijijini hapo, baba mzazi wa marehemu huyo, Samwel Lukumay (77), alisema kuwa kijana wake alikamatwa na mwenyekiti huyo akiwa na watuhumiwa hao wanaoshikiliwa na Polisi pamoja na mwenyekiti wa usalama wa kijiji hicho, Nuruel John ambaye alitoroka baadaye.Alisema kuwa kijana wake alifungiwa katika ofisi ya kijiji na kuanza kushambuliwa na watuhumiwa hao na kwamba chanzo cha tukio hilo ni mwanawe kudaiwa kumjeruhi mmoja wa wanakijiji.Alisema viongozi hao walimjeruhi mwanawe sehemu mbalimbali za mwili wake na kufikia kumnyoa nywele zake kwa kutumia panga, hali iliyosababisha hadi ngozi ya kichwa kutoka.Mzee huyo aliongeza kuwa baada ya viongozi hao kuona hali ya kijana wake ni mbaya walimpeleka katika Kituo cha Polisi Baraa wakidai kuwa alikuwa ni mwizi na kwamba alishambuliwa na wananchi wenye hasira kali jambo ambalo polisi walilitilia shaka na kutoa PF3 ili akapatiwe matibabu kutokana na hali yake aliyokuwa ambapo alifariki | Kitaifa | 0 |
KOCHA Msaidizi wa Taifa Stars Juma Mgunda amesema wanakwenda Sudan kupindua matokeo na kukata tiketi ya kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani zitakazofanyika Cameroon mwakani. Taifa Stars ikiwa kwenye nyumbani ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Sudan na kujiweka kwenye wakati mgumu wa kufuzu kwa mara ya pili kwenye fainali hizo ambapo mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa ni mwaka 2009. Mwaka 2009 ikiwa chini ya kocha Mbrazili Marcio Maximo Taifa Stars ilifuzu kwa mara ya kwanza fainali hizo kwa kuifunga Sudan ambapo kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 kabla ya kwenda kupata ushindi mwingine wa mabao 3-1, Kartoum. “ Nawaomba watanzania wawe na subira na watusamehe kwa matokeo tuliyopata, bado tuna nafasi kubwa kwenye mchezo wa marudiano kwa kusahihisha makosa tuliyofanya na kwenda kupindua matokeo ” alisema Mgunda.Mgunda, mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Tanzania na Coastal Union alisema kiuhalisia matokeo waliyopata sio mazuri hasa ukichukulia walikuwa kwenye uwanja wa nyumbani.“Tulitengeneza nafasi nyingi za kufunga kwa bahati mbaya hatukuweza kuzitumia. Usipotumia nafasi unazopata wenzako wakipata wanakuadhibu.“Nawaomba mashabiki wawasamehe wachezaji kwani na wao ni binadamu ila nina imani tunaenda kupindua matokeo kwenye mchezo wa marudiano,”alisema Mgunda ambae pia ni kocha wa Coastal Union ya Tanga. Taifa Stars itarudiana tena na Sudan mwezi ujao mchezo utakaopigwa Uganda kufuatia nchi ya Sudan kuwa kwenye machafuko ya kisiasa. Kabla ya kukutana na Sudan, Taifa Stars iliitoa timu ya taifa ya Kenya kwa mikwaju ya penalti, baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika michezo yote miwili. | michezo | 2 |
Ulipaji huo wa kodi utaiwezesha serikali kupata mapato na kuweza kutekeleza mipango yake kwa wakati kama ya kuboresha huduma za afya, elimu, miundombinu mbalimbali, ulinzi na usalama.Aliyasema hayo jana katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Manju Msambya wakati akifungua semina ya walipa kodi wakubwa na wa kati iliyofanyika jijini hapa.Kwa upande wake, Naibu Kamishna wa Walipa Kodi Wakubwa, Alfred Mregi alisema washiriki wa semina hiyo watapitia sheria mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya mwaka 2014.Alisema sheria mpya ya VAT imeboreshwa katika maeneo mbalimbali kwa kuyaangalia maeneo yenye mapungufu katika sheria wanayoitumia sasa kama watakavyoelezwa na wataalamu. | Biashara | 1 |
RAIS mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Kikwete ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amewataka wahitimu wa shahada za ualimu, kujiandaa kisaikolojia kufundisha shule za msingi, badala ya sekondari kama walivyotarajia.Alisema hayo juzi kwenye mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam cha Elimu Mkwawa (MUCE), Iringa baada ya kuwatunuku wahitimu shahada.Alisema, serikali hivi sasa inawapeleka walimu waliohitimu shahada za ualimu, kufundisha shule za msingi, jambo ambalo halikupokelewa vyema na walimu, wakidai kushushwa hadhi, kwa kuwa waliamini stahili yao ni sekondari. Tunaungana na wadau wa elimu, kumpongeza Dk Kikwete kwa kuwaasa walimu kujiandaa kufundisha shule za msingi, kwani mwelekeo wa serikali sasa ni mapinduzi ya viwanda na mapinduzi ya elimu.Ni matarajio yetu walimu waliohitimu juzi na waliohitimu zamani, sasa wameelewa vyema nia ya Serikali ya Awamu ya Tano kuboresha elimu ya msingi na kujenga msingi bora wa elimu ya juu. Ni vizuri wakauelewa na pia kuupokea vyema mpango huo wa serikali, unaolenga kuboresha elimu ya msingi na pia kuwahakikishia ajira kubwa wahitimu wa ualimu kutokana na shule za msingi, kuhitaji walimu zaidi wenye shahada.Kwa wasioelewa maana ya mpango huo ni vyema wakarejea kauli ya Rais mstaafu Kikwete kuhusu mabadiliko, ambayo mfumo wa elimu nchini umepitia tangu ukoloni hadi leo. Kimsingi, mpango huo umelenga kuboresha utoaji wa elimu ya msingi ili kwenda na wakati, teknolojia na utandawazi kuziba pia ombwe la walimu wa darasa la saba (UPE), kidato cha nne (Daraja C) na wa diploma walioostaafu au kufa.Kwa kuwa elimu yetu inapita katika vipindi na mfumo tofauti, ni vizuri wahitimu wa ualimu wakaelewa mantiki ya serikali kuamua walimu wenye shahada, wakafundishe shule za msingi ili kuboresha taaluma ili tushindane na nchi za nje. Wazazi, walimu, wadau wa elimu na wanafunzi ni mashahidi wa malalamiko kuhusu ubora wa elimu inayotolewa, kufuatia baadhi ya wahitimu kutokidhi matarajio ya viwango vya waajiri. Malalamiko hayo yakiwemo ya wahitimu shule za msingi kutojua vyema Kiingereza, yanaelekea kupata jibu sahihi, kwa hatua hizi za serikali kwa kuboresha sifa za walimu watakaofundisha.Ni muhimu basi kama Taifa, kila mmoja kwa nafasi yake, ashiriki mageuzi haya ya elimu kwa kushirikiana na serikali kuboresha mfumo mzima wa utoaji elimu ili ukidhi mahitaji ya soko. Serikali inatekeleza sera ya viwanda, ambayo inahitaji wasomi wenye weledi wa kuendesha viwanda na kufanya biashara. Hivyo, ni muhimu kwa vyuo vye elimu kubadili mitaala, kukidhi utoaji elimu bora, utakaokidhi matarajio hayo. | Kitaifa | 0 |
Promosheni hiyo itakayojulikana kama ‘Pata Patia na NMB’ itadumu kwa miezi sita, ina lengo la kuhamasisha wateja kujiwekea akiba katika akaunti zao na kuweza kujishindia fedha.Kaimu Mkuu Kitengo cha wateja binafsi, Boma Raballa alisema “NMB imeanzisha promosheni hii kwa lengo maalumu la kuhamasisha wateja wake kujiwekea akiba katika akaunti zao”.Alisema pia wateja wapya kujiunga na NMB kwa kufungua akaunti na kuweka akiba huku wakiwa na nafasi kubwa ya kujishindia fedha.Raballa alisema mteja anatakiwa kuweka kiasi kisichopungua Sh 50,000 na kuweza kujishindia kuanzia Sh 100,000 hadi Sh milioni tatu papo hapo.“Tunatarajia kuwafikia washindi 144 kwa miezi sita na tukimpata mshindi atapigiwa simu na ataelekezwa namna ya kushiriki promosheni hiyo,” alisema.Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa NMB, Rahma Mwapachu alisema “Tayari tumepata kibali kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha na tuna imani shindano hili litawanufaisha wengi na kufikia malengo yao waliyojiwekea”. | Biashara | 1 |
MABINGWA watetezi wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame), Azam FC watawakosa nyota watano katika michuano hiyo kutokana na sababu mbalimbali.Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii na Azam imepangwa kundi A pamoja na timu za JKU ya Zanzibar, Kator FC ya Sudan Kusini na Vipers kutoka Uganda.Ratiba inaonesha kuwa mabingwa hao watetezi ambao walilinyakua taji hilo mwaka 2015 mara ya mwisho kufanyika michuano hiyo, wataanza kucheza na Kator kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.Akizungumza na gazeti hili jana, Meneja wa Azam FC, Philip Alando, amesema, kikosi chao kinaendelea na mazoezi ya kujiandaa na michuano hiyo licha ya kuwakosa wachezaji wake watano wa kikosi hicho.Aliwataja wachezaji hao kuwa ni beki wao Yakub Mohammed, Daniel Amoah, Iddy Kipagwile, Salim Hoza na kiungo waliyemsajili hivi karibuni kutoka Singida United, Tafadzwa Kutinyu.Amesema, Kipagwile pamoja na Hoza wamepata likizo fupi baada ya wote wawili kufunga ndoa Ijumaa iliyopita, huku Amoah akiwa bado anasumbuliwa na majeraha na waliobakia wapo kwenye mapumziko ya kawaida na wanatarajiwa kurudi mwanzoni mwa mwezi ujao.“Timu inaendelea na mazoezi yake ya kuelekea michuano hiyo ambayo kwetu ni muhimu kama unavyojua sisi ndio mabingwa watetezi, baada ya kucheza mechi ya kirafiki na Green Warriors na kutoka sare ya kufungana bao 1-1, leo (jana) tutataendelea na mazoezi ya pamoja. | michezo | 2 |
TIMU ya soka ya vijana ya Tanzania imeiadhibu Zimbabwe kwa mabao 6-2 katika mchezo wa fainali za mashindano ya kwanza ya COPA Coca-Cola kwa vijana chini ya umri wa miaka 16 ya Mataifa ya Afrika na kutwaa ubingwa.Tanzania ilionesha kiwango cha juu na kuibuka mshindi katika mechi ya fainali iliyofanyika kwenye viwanja vya MPESA Foundation Academy mjini Thika, Kenya jana. Taarifa kutoka Kenya zinasema kwamba mshindi wa kiatu cha dhahabu, Paul Nyerere alifunga mabao 3 ‘hat trick’ katika kipindi cha kwanza wakati wa fainali hiyo. Nyerere ameibuka mfungaji bora baada ya kufikisha mabao 7 kwenye michuano hiyo.Mabao mengine yaliwekwa kimiani na Ndile Haruni, Rai Mohambi, Boniface Raphael na kuiwezesha Tanzania kutwaa taji la mabingwa wa Kombe la COPA Coca- Cola Afrika 2019.Akizungumza mara baada ya mashindo hayo kuisha, Kocha wa Tanzania, Alex Mtweve alisema, timu yake ilistahili taji hilo.“Tuliutawala mchezo tangu mwanzo na vijana wangu walionyesha ujuzi, kwa kweli tulikuja kwenye mashindano haya na lengo la kutwaa ubingwa, nashukuru vijana hawajaniangusha.”Mtweve aliongeza kuwa siri ya ushindi wake imekuwa ni kucheza mchezo wa kushtukiza na kushambulia kwa nguvu. Mlinzi wa timu ya Tanzania, Chuma Ramadhan alifanya kazi kubwa pia ya kuiwezesha timu yake kutawala mchezo baada ya kuokoa hatari kadhaa golini kwake na kuzuia penalti moja wakati wa mchezo huo wa fainali.Akizungumza baada ya mechi hiyo, Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt. Pindi Chama ambaye alishuhudia fainali hiyo alitumia nafasi hiyo kuwapongeza vijana hao na kuwatakia kila la heri. | michezo | 2 |
Miji hiyo ni Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Zanzibar na Mbeya na pia safari ya kimataifa kati ya Dar es Salaam na Johannesburg, Afrika Kusini.“Kwa mwaka mmoja sasa Fastjet imeona Watanzania wakisafiri kwa ajili ya mikutano ya kibiashara na kutembelea ndugu na jamaa hivyo kuepusha uchovu na muda mwingi wa kusafiri kwa saa nyingi kwa kutumia barabara,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Fastjet, Ed Winter.Kwa mujibu wa Winter, kampuni ilianza kwa safari mbili kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza na Kilimanjaro.Baada ya mahitaji ya safari za ndege kuongezeka, iliitikia mwito kuongeza safari mbili za nchini na moja ya kimataifa kwenda Johannesburg ndani ya mwaka mmoja. Winter alisema wana mpango wa kuongeza safari nyingine ya kimataifa kwenda Zambia ambayo ipo katika hatua nzuri.“Usafiri wa ndege wa bei nafuu ni muhimu sana kwa ajili kukuza uchumi wa Afrika,” alisema Winter. Kampuni hiyo ambayo nauli zake zinatajwa kuwa nafuu, zinaanzia Sh 32,000 na kwa safari za kimataifa, inaanzia Sh 160,000 lakini bila ada na kodi za Serikali.Wakati huo huo katika kusherehekea mwaka mmoja wa huduma zake, kampuni imetoa ofa maalumu leo ambako tiketi za safari kati ya Januari 6 na Machi 29 mwakani zitauzwa kwa bei ya chini ya Sh 32,000. | Biashara | 1 |
KAMPUNI ya teknolojia ya malipo ya kimataifa, Visa imetangaza ushirikiano wa mkakati na Halotel ili kuwezesha malipo ya Visa kwenye simu kwa kutuma codi ya QR kwa wateja wa Halotel nchini Tanzania. Huduma hiyo itakayotolewa mwanzoni mwa mwaka 2019 na hivyo kuwezesha wateja zaidi ya milioni moja wa HaloPesa kutumia Visa kwenye simu ili wafanye malipo ya biashara kwa salama na kuweka na kutoa fedha kwa mawakala wa Visa.Mteja yeyote wa HaloPesa ikiwa ni pamoja na wale ambao hawana akaunti ya benki, watafaidika na huduma hii. Lengo la huduma hii ni kuunganisha Watanzania zaidi kwenye mfumo wa malipo ya kimataifa, kuleta huduma ya malipo ya Visa ya usalama na urahisi kwa watumiaji na wafanyabiashara. “Tunafurahia ushirikiano huu na mojawapo wa kampuni maarufu ya simu ya Halotel. Ushirikiano wetu na Halotel utahakikisha kuwa Watanzania wanaweza kufanya malipo ya QR kwa kutumia Visa kwenye simu zao kwa wauzaji na wafanyabiashara zaidi ya 40,000. “Pia itasaidia kuongeza ushirikishaji wa kifedha kwa watumiaji ambao sasa wataweza kufaidika na kushiriki katika mfumo wa ecoVisa,” alisema Meneja Mkuu wa Visa wa Afrika Mashariki, Kevin Langley. Halotel ni kampuni ya simu inayokua kwa haraka zaidi nchini Tanzania ambayo ilianzishwa mwaka 2015. Ndani ya miaka mitatu, imepata wateja zaidi ya milioni nne na ambao zaidi ya milioni moja wanatumia huduma ya Halopesa. Pia kampuni inao wakala 40,000 kote nchini. “Tunajivunia kushirikiana na Visa katika mpango huu.Kwa ushirikiano huu, tutaweza kuwa na uwezo wa kuwaletea wateja wetu huduma za kimataifa za malipo za Visa na kuwawezesha wateja wetu kulipia na kulipwa kwa urahisi zaidi,” alisema Naibu Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Son. Kupitia ushirikiano, HaloPesa itawapa watumiaji fursa ya kufanya malipo kutumia codi ya QR ya Visa nchini Tanzania na kote duniani. | Biashara | 1 |
MWENYEKITI wa kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Ally Mchungahela ametangaza rasmi uchaguzi mkuu wa Klabu ya Yanga kwamba utafanyika Mei 5 mwaka huu.Uchaguzi huo umetangazwa kufanyika siku hiyo kutokana na agizo la Serikali kupitia Baraza la Michezo nchini (BMT), kuitaka TFF isimamie klabu hiyo ifanye uchaguzi wake ndani ya siku 30.Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya shirikisho hilo Karume Ilala jana, Mchungahela alisema wametoa taarifa ya kufanyika uchaguzi huo kwa lengo la kuwajulisha wapenzi na wanachama wa Yanga maendeleo ya mchakato wa uchaguzi yalipofikia na kwamba fomu za kuwania nafasi mbalimbali zitaanza kutolewa leo makao makuu ya Yanga.Alisema kwa wale waliochukua fomu awali kwa ajili ya uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi hawatachukua tena na badala yake watasubiri kupigiwa kura siku ya uchaguzi huo mkuu kwa vile walishafanyiwa usaili na kufanya kampeni. “Hakuna asiyefahamu uchaguzi wa Yanga ulipangwa kufanyika hapo awali lakini baadae ulishindwa kufanyika kwa sababu za kisheria na sasa uchaguzi utafanyika kwa tarehe tuliyopanga na si vinginevyo kwa ushirikiano wa wanayanga wenyewe chini ya uangalizi wa Shirikisho la soka nchini kwa sababu ni chombo kinachosimamia mpira,” alisema Mchungahela.Mchungahela alisema wao wana mamlaka ya mwisho kutangaza tarehe ya uchaguzi. Tarehe hiyo ni tofauti na ile iliyotangazwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Baraza la wadhamini la Yanga chini ya George Mkuchika kwamba Aprili 28 ndio uchaguzi ungefanyika.Mchungahela alisema tarehe hiyo iliyopangwa na baraza la wadhamini kutakuwa na fainali za Afcon kwa vijana zinazotarajiwa kuanza Aprili 14 nchini hivyo wengi watakuwa wakifuatilia fainali. Wajumbe Yanga waliohudhuria kwenye mkutano huo ni Omary Kaaya, Zayumba Hamis, Karume Benjani, Mwamedi Mtengulwa ambaye ni mbunge kutoka Rufiji na wakili Sam Mapande. Mchungahela alisema hadi sasa wameshapata daftari la leja linaloonesha orodha ya wanachama hai wa timu hiyo na kwamba hiyo ni ishara njema kwa wanachama. | michezo | 2 |
['Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer yupo tayari kusubiri hadi msimu ujao w ajoto kushinikiza kiungo cha ushambilizi , huku mchezaji wa kiungo cha mbele wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 19, akisalia kuwa mchezaji anayemlenga pakuu. (Evening Standard)', 'Barcelona na Paris St-Germain zimekubali malipo ya uhamisho wa mchezaji wa miaka 27 wa timu ya taifa ya Brazil Neymar, lakini majadiliano yanaendelea kuhusu makubaliano ya mkataba huo. PSG inataka mchezaji wa kiungo cha mbele wa Ufaransa Ousmane Dembele, mwenye umri wa miaka 22, kuwa sehemu ya mpangilio huo. (Mirror)', 'Hatahivyo, Ajenti wa Dembele anasema mchezaji huyo hatoondoka Nou Camp, hatua ambayo huenda ikachangia kupromoka kwa pendekezo la uhamisho wa Neymar kwenda Barcelona. (Daily Mail)', 'Mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea raia wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, mwenye umri wa miaka 25, amekubali makubaliano ya kujiunga upya na Monaco kwa mkopo - huku kukipangiwa malipo ya £31.8m ka mkataba wa kudumu.(RMC Sport, kupitia Sun)', 'Mlinzi wa Arsenal Nacho Monreal, mwenye umri wa miaka 33, c huenda akarudi katika klabu alikotoka Uhispania kaba ya kufungwa dirisha la uhamisho Ulaya Jumatatu, huku Real Sociedad ikiwa na hamu kubwa ya kumsajili mchezaji huyo wa zamani wa Osasuna na Malaga. (Evening Standard)', 'Mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya England Sam Greenwood, mwenye umri wa miaka 17, ametambuliwa na timu bingwa ya Italia AC Milan na Juventus kama mchezaji anayelengwa baada ya kuridhisha maajenti katika mshindano ya ubingwa wa Ulaya wa timu za wachezaji walio chini ya umri wamiaka 17 mapema msimu huu wa joto. (Sun)', 'Manchester United italipa kitita cha £300,000 cha malipo ya Alexis Sanchez ya £400,000 kwa wiki wakatimchezaji huyo wa kiiungo cha mbele wa Chile akiwa uhamishoni kwa mkopo huko Inter Milan. (Metro)', "Mchezaji wa kiungo cha mbele wa RB Leipzig na anayelengwa na Liverpool, Timo Werner, mwenye umri wa miaka 23, bado hajakata tamaa ya uhamisho kwenda ng'ambo katika siku za usoni licha ya mchezaji huyo wa kiungo cha mbele wa timu ya taifa ya Ujerumani kusaini mktaba mpya katika klabu hiyo kwenye ligi ya Bundesliga. (Mirror)", 'Kipa wa Bournemouth Asmir Begovic, mwenye umri wa miaka 32, huenda akaondoka baada ya kuipoteza nafasi yake kwa mchezaji wamiaka 21 wa England Aaron Ramsdale. (Sun)', 'Mshambuliaji wa Reading Sam Baldock, mwenye umri wa miaka 30, anavutia vilabu kadhaa katika ligi ya Ujerumani Bundesliga 2, huku mlinzi mwenye miaka 19 wa timu ya taifa ya England Tom Holmes akitarajiwa kujiunga na KSV Roeselare huko Ubelgiji kwa mkopo. (Get Reading)', 'Mchezaji wa kiungo cha kati wa Stoke City Giannelli Imbula, mwenye miaka 26, anakaribia kuhamia kwa mkopo kwenda klabu katika ligi ya Serie A. (Sport Italia)', 'Tottenham hawana uhakika na nia ya Christian Eriksen kutokana na kuvunjika kwa mahusiano kati ya mwenyekiti wao Daniel Levy na wakala wa kiungo huyo mwenye miaka 27 raia wa Denmark. (Guardian)', 'Meneja wa zamani wa Tottenham Harry Redknapp anaamini Eriksen anatakiwa kuanza kwenye mechi za Spurs licha ya kutokujulikana kwa hatma yake ya mbeleni. (Talksport)', 'Mshambuliaji wa Inter Milan Romelu Lukaku, 26 aliondoka Manchester United kwa sababu alichoshwa na klabu hiyo , kwa mujibu wa kocha wa Belgium Roberto Martinez. (Mirror).', 'Kaka yake Paul Pogba, Mathias mwenye umri wa miaka 29 ambaye ni mshambuliaji wa klabu ya Deportivo Manchego, amesema mdogo wake anayechezea Manchester United itapendeza zaidi kama atahamia Real Madrid. (AS)', 'Mshambuliaji wa Everton Cenk Tosun anataka kubaki katika klabu hiyo licha ya kuwepo kwa tetesi kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ana mpango wa kuhamia Eintracht Frankfurt. (Turkish Football)', 'Liverpool imesema kuwa haina mpango wa kumuuza mshambuliaji wake Bobby Duncan na imekataa kutumia mbinu za Fiorentina. (Liverpool Echo)', 'Mchezaji wa Brighton, Jurgen Locadia, 25 anaweza kusajiliwa kwa mkopo na Bundesliga side Hoffenheim. (Argus)', 'Olympiakos wako katika mazungumzo na klabu ya Leicester katika mpango mpya wa kumsajili mshambuliaji wa Foxes ambaye ni raia wa Algeria Rachid Ghezzal, 27. (Sky Sports)', 'Manchester City wapo katika mipango ya kumnasa mlinzi wa klabu ya Hearts Aaron Hickey kwa dau la paundi milioni 1.5 ili kumpata mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 ifikapo mwezi Januari. (Sun)', 'Kiungo wa klabu ya West Bromwich Albion, Rekeem Harper mwenye umri wa miaka 19 amepewa nafasi kubwa katika mipango ya kocha mkuu wa klabu hiyo Slaven Bilic katika msimu huu. (Express and Star)'] | michezo | 2 |
SIMBA sasa bado pointi tano tu kumfikia mpinzani wake mkubwa Yanga anayeongoza Ligi Kuu Soka ya Tanzania Bara baada ya jana kuifunga Biashara ya Mara kwa mabao 2-0.Ushindi kwenye mchezo huo uliochezwa mkoani Mara unaifanya Simba kufikisha pointi 69, pointi tano nyuma ya Yanga yenye pointi 74.Huo ni muendelezo wa mabingwa hao watetezi wa Tanzania Bara kucheza mechi zake za viporo vilivyotokana na ushiriki wa timu hiyo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba sasa imecheza mechi 27.Aidha, matokeo hayo yanazidi kuichimbia kaburi la kushuka daraja kwa Biashara ambapo inashika nafasi ya pili toka mwisho ikiwa na pointi 34 katika michezo 32.Mabao yote mawili ya Simba yalipatikana kipindi cha kwanza yakiwekwa kimiani na nahodha wa timu hiyo John Bocco na kumfanya kufikisha mabao 14 kwenye ligi hiyo mpaka sasa.Ilimchukua dakika 33 kwa nahodha huyo kuiandikia Simba bao la kuongoza akiunganisha kwa shuti kali la mguu wa kushoto pasi nzuri iliyopigwa na kiungo Mzamiru Yassin.Dakika tano kabla ya mapumziko Bocco tena aliifungia Simba bao la pili kwa kichwa akimalizia mpira wa krosi wa beki Asante Kwasi aliyecheza badala ya Mohamedi Hussein’Tshabalala’ Biashara ikicheza mbele ya mashabiki wake ilishindwa kutengeneza nafasi kipindi cha kwanza na kutoa nafasi kubwa ya Simba kutawala sehemu kubwa ya mchezo huo.Kipindi cha pili Simba walifanya mabadiliko kwa kumtoa John Bocco na kumuingiza Emmanuel dakika ya 58 na dakika ya 66 beki Paul Bukaba alipoteza nafasi ya wazi ya kufunga kwa shuti lake kuokolewa na kipa Nourdin Abalora na kuondoshwa na mabeki wa Biashara.Simba ilipata pigo dakika ya 71 kwa kiungo wake Mnyarwanda Haruna Niyonzima kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumchezea madhambi mchezaji wa Biashara.Haikuwa siku nzuri kwa mshambuliaji Meddie Kagere baada ya kupoteza nafasi ya wazi dakika ya 73 kwa shuti lake kutoka pembeni kidogo ya lango la biashara na dakika ya 74 alitolewa na kuingia Hassan Dilunga. | michezo | 2 |
Wakulima hao wa Kijiji cha Mgeta wilayani Morogoro, wananufaika kwa kupewa mbegu, kupaliliwa mashamba yao na kupewa elimu kwa ajili ya kuvuna mazao mengi zaidi ili waweze kujikimu.Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Chris Maongezi alisema pia wananchi hao wanasaidiwa kuuza mazao yao kwa urahisi, kutokana na kuwauzia wao.“Huu ni mradi maalumu ambao unasaidia familia takribani 6,500 kila upande uliotuzunguka, tunawasaidia wakimaliza kuvuna, tunayanunua mazao yao,” alisema Maongezi.Alisema pia shamba hilo limetoa ajira za kudumu kwa watu 250, huku wakati mavuno ajira ndani ya shamba hilo hufikia 400. Alisema ili familia ziweze kunufaika na mradi huo ni lazima zijiandikishe.Alisema kufanya hivyo, kunawasaidia wakulima kujikimu na kunufaika na kilimo wanachofanya | Biashara | 1 |
Huduma hiyo ambayo inatolewa kwa kushirikiana na Kampuni ya AFB, imelenga kubadilisha maisha ya wafanyabiashara wadogo ambao wanahitaji mikopo kuimarisha mitaji yao.Huduma hiyo itakayojulikana kama “Airtel Money Timiza” ni sehemu ya juhudi za Airtel ya kuungana na Serikali katika kuwezesha wananchi na wateja wa Airtel wote kujipatia mikopo ya haraka na ya muda mfupi kwa marejesho nafuu ya siku 7 hadi 28.Akizungumza wakati wa uzinduzi, Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipongeza huduma hiyo na kusema ni motisha kwa wafanyabiashara wadogo.Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso alisema: “Leo uzinduzi wa huduma yetu ya Airtel Money Timiza unadhihirisha dhamira ya dhati ya Airtel ya kutoa huduma iliyo bora na nafuu ili kugusa maisha ya kila siku ya wateja wetu hapa Tanzania .”Alisema ni matumaini yake kwamba huduma hiyo itaongeza kasi ya ukuzaji wa uchumi miongoni mwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na vikundi vya wanawake, wajasiriamali na watu binafsi.Kwa upande wake, Mwanzilishi wa AFB, Andrew Watkins-Ball alisema huduma hiyo ya mikopo ya Airtel Money Timiza ni ya kipekee tofauti na benki ambayo mara nyingi mteja hulazimika kuwa na historia ya uwekaji na utoaji katika benki hiyo.Alisema mikopo hiyo ya Airtel kwa kushirikiana na AFB, inatolewa kutokana na jinsi ambavyo mteja anatumia simu. | Biashara | 1 |
WATU 26 wakiwemo Watanzania watatu wamekufa katika shambulio la bomu lililofanyika katika hoteli mjini Kismayo, Somalia.Mwandishi wa habari maarufu mwenye uraia wa Canada na Somalia, Hodan Nalayeh na mumewe, Farid, ni miongoni mwa waliokufa katika shambulio hilo linalosadikiwa kufanywa na kundi la wapiganaji wa al shaabab katika hoteli ya Easey.Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), raia wengine waliokufa katika tukio hilo ni Wakenya watatu, Wamarekani wawili na Muingereza.Watu wengine 50 wamejeruhiwa katika shambulio hilo ambalo inadaiwa pia washambuliaji wanne waliuawa.Kuhusu vifo vya Watanzania, HabariLeo halikufanikiwa kupata msemaji upande wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuthibitisha taarifa hizo zilizoripotiwa na shirika la BBC.Mashuhuda wa tukio hilo walisema maofisa wa ngazi za juu wa kisiasa akiwemo mgombea urais katika uchaguzi ujao katika jimbo la Jubaland, ameuawa katika shambulio hilo la juzi usiku.Aidha, ofisa usalama, Abdi Dhuhul aliliambia Shirika la Habari la Ufaransa (AFP) kwamba waziri mmoja wa utawala wa eneo hilo pamoja na wakili ni miongoni mwa waliofariki katika shambulio.Wanasiasa wa eneo hilo pamoja na viongozi wengine walikuwa ndani ya hoteli hiyo wakijadili kuhusu uchaguzi unaotarajiwa kufanyika katika ukanda huo.Vikosi vya usalama katika mji huo ulio mwambao wa Kusini mwa Somalia, vilikabiliana na kundi hilo usiku kucha.Kwa saa kadhaa, vikosi vya usalama vilikabiliana na wapiganaji waliokuwa na silaha nzito hadi asubuhi.Walioshuhudia walisema walisikia milio ya risasi baada ya bomu lililokuwa ndani ya gari kulipuka. Miili ya watu iliondolewa kutoka kwenye hoteli hiyo wakati vikosi vya usalama vikiendelea na msako. | Kitaifa | 0 |
SERIKALI haina mpango wa kuvibadili vyuo vya Maendeleo ya Wananchi kuwa VETA. Hayo yamebainishwa jana mjini hapa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Willam Ole Nasha wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Rufiji, Mohamed Mchengerwa (CCM). Mchengerwa alisema katika swali: “Serikali imerejesha vyuo vilivyokuwa vya maendeleo kuwa chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya kusema hayo, alitaka kujua kama serikali haioni umuhimu wa kukibadili chuo cha Maendeleo Ikwiriri FDC kuwa VETA ili kubadili fikra za wananchi wa Rufiji, Kibiti na hatimaye kuleta mwamko wa elimu. Akijibu swali hilo, Waziri Ole Nasha alisema elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi hutolewa katika shule na vyuo katika kiwango na madaraja mbalimbali kulingana na malengo yake. Alisema ngazi ya shule za sekondari, elimu ya ufundi hutolewa kumuandaa mwanafunzi kujiunga na vyuo vya ufundi stadi na ufundi wa kati.“Vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi huandaa mafunzi mchundo na vyuo vya ufundi wa kati huandaa mafundi sanifu. Aidha, vyuo huandaa wahandisi katika fani mbalimbali zinazohusiana na ufundi.” Waziri Ole Nasha alisema vyuo vya Maendeleo ya Wananchi vilianzishwa kwa lengo la kumsaidia mwananchi kukabiliana na changamoto za kimaendeleo katika mazingira yake kwa kumpatia maarifa na stadi anuai Alisema kwa sasa serikali haina mpango wa kuvibadili vyuo vya Maendeleo ya Wananchi kuwa VETA na badala yake imejikita katika kuviboresha vyuo hivyo kwa kuvikarabati na kuviongezea vifaaa vya kujifunzia na kujifundishia ili viweze kutoa mafunzo bora zaidi. Waziri Ole Nasha alisema awamu ya kwanza ukarabati wa vyuo vya Maendeleo ya Wananchi 20 ipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji, na awamu ya pili inatarajiwa kuanza mapema Juni mwaka huu. “ Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Ikwiriri kilikuwa katika awamu ya kwanza na ukarabati umekamilika,” alisema. Aidha, Ole Nasha alisema katika mwaka wa fedha 2019/2020 Rufiji ni miongoni mwa wilaya zilizotengewa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya cha VETA. | Kitaifa | 0 |
Goms imefuzu fainali baada ya kuifunga Itezi ya Mbeya kwa mabao 3-2 na Misosi imefuzu baada ya kuifunga Mnadani ya Mwanza kwa mabao 2-0.Goms ambao ni washindi wa pili wa mashindano ya Ndondo mkoa wa Dar es Salaam walifungwa na Misosi FC katika mchezo wa fainali kwa penalti 5-4 baada ya kumalizika dakika 90 kwa sare ya bao 1-1.Akizungumza juzi kocha wa Goms United, Shaban Kazumba alisema wamejiandaa kulipa kisasi kwa sababu msimu uliopita walipoteza mchezo katika mazingira wanayoyayajutia mpaka leo.“Tulianza kufunga bao lakini Misosi walisawazisha tukalazimika kuingia kwenye mikwaju ya penalti tukafungwa hali ambayo iliwasonenesha mashabiki wetu,” alisema Kazumba.Michuano ya Ndondo Super Cup ilianza Jumamosi iliyopita kwa mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Bandari, Temeke na kushirikisha timu mabingwa wa mikoa wa Mwanza (Mnadani FC) na Itezi ambao ni bingwa wa Mbeya | michezo | 2 |
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge ameshauri wakuu wa mikoa nchini kuhamasisha matumizi ya mfumo wa anwani za makazi na postikodi.Pia ameiomba Ofisi ya Rais Tamisemi na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) kuwezesha suala la anuani ya makazi kufanikiwa. Hayo yamo katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi kwenye ufunguzi wa kikao cha wadau wa mfumo wa anwani za makazi na postikodi. Kikao hicho kililenga kujenga uelewa wa pamoja na kuhamasisha utekelezaji wa matumizi ya mfumo huo.Alisema wakuu wa mikoa kama watafanya jitihada za kuhamasisha matumizi ya mfumo huo, kutakuwepo na mafanikio na hivyo kurahisisha mawasiliano na utambuzi. Pia alishauri Tamisemi na Wizara ya ujenzi kuweka jitihada katika kuhamasisha, kujenga uelewa na uwezo katika utekelezaji wa matumizi ya mfumo, ikiwa ni pamoja na kuweka mifumo ambatanishi ya Tehama ili uwe na tija katika utoaji huduma hususani katika biashara mtandao.Pia alizitaka Wakala wa Barabara vijijini (Tarura), Wakala wa Barabara (Tanroads), Wakala wa Majengo (TBA), Shirika la Nyumba (NHC) na taasisi nyingine zote zenye majukumu ya kuweka miundombinu kuhakikisha mipango yao inakuwa na anwani ya makazi na postikodi kulingana na viwango vilivyopo. Aidha alizitaka taasisi mbalimbali zilizoko Dodoma kuanza mara moja kutumia anwani za makazi na postikodi katika kutoa huduma.Aidha, alizitaka Halmashauri zote kuweka mazingira ya kupatikana kwa urahisi na gharama nafuu nguzo zenye majina ya barabara, njia na vibao vyenye namba za nyumba ili endapo taasisi au wananchi watahitaji kwa ajili ya maeneo wapate bila usumbufu. Pia aliwataka watoa huduma, wafanyabiashara na wenye nyumba za biashara kuhakikisha maeneo yao ya huduma au biashara yanatumia anwani za makazi na postikodi katika huduma zao.“Tunatambua kuwa Dodoma ni mji wa kiserikali hivyo tunapaswa kuifanya kuwa na hadhi ya kiserikali, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa mifumo imara ya utoaji wa huduma. hatuna budi kuwa mfano kitaifa katika kutekeleza na kuutumia kwakuwa utaongeza tija na ufanisi,”alisema.Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Jim Yonazi alitaja baadhi ya changamoto zinazokabili mfumo huo kuwa ni ufinyu wa bajeti unaochangiwa na halmashauri kutotenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo. Pia mwamko mdogo wa taasisi na wananchi kushiriki katika kuchangia utekelezaji, barabara na mitaa mingi kutokuwa na majina yaliyorasimiwa na uharibifu wa muundombinu wa mfumo uliopo. | Kitaifa | 0 |
Maswi alitoa agizo hilo mjini Mbeya jana, wakati akizungumza na wafanyakazi wa Idara ya Madini mkoani Mbeya, ambako alipatiwa taarifa na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), kuhusu kampuni kubwa tatu zinazogoma kulipa maduhuli stahiki kwa Serikali, kwa madai ya kuwa na hati ya msamaha wa kodi katika baadhi ya maeneo.“Hili jambo mbona ni rahisi kwa kuwa sekta yetu hii ya madini inaendeshwa kwa kuzingatia sheria, na sheria inatamka wazi kuwa ni lazima kila mwekezaji wa madini alipe maduhuli kulingana na kiasi alichouza.“Kamishna wa Madini fuatilia hili na kama kweli kuna hizo hati…kwani zinatoka wapi? Si zimetoka serikalini basi zifutwe, hawa walipe malipo stahiki,” alisisitiza Maswi.Awali akiwasilisha ripoti ya ukaguzi wa TMAA katika Mkoa wa Mbeya, Ofisa Mfawidhi wa wakala huo mkoani hapa, Jumanne Abdallah, alisema ofisi yake imekuwa ikikabiliwa na wakati mgumu katika ukusanyaji wa maduhuli kutoka kampuni hizo za madini na kushindwa kukusanya malipo stahiki.Alisema kwa mujibu wa sheria hiyo, kampuni hizo zilitakiwa kulipa Sh milioni nne kwa mwezi kodi ya maduhuli, lakini kutokana na madai ya kuwa na hati hizo, zimekuwa zikilipa kila mwezi Sh milioni 3. | Biashara | 1 |
WATU watano wa familia moja wamekufa papo hapo baada ya kupigwa na radi ambayo pia iliwajeruhi watu watatu wa Kijiji cha Isongwa, Kata ya Mkole, Wilaya ya Sikonge, Tabora.Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Kamishina Msaidizi wa Polisi Emanuel Nley ilisema mvua kubwa iliyonyesha juzi usiku ikiambatana na radi ilisababisha vifo.Kamanda Nley alisema tukio hilo lilitokea saa nne usiku Aprili 22, mwaka huu watu hao wakiwa wamelala katika chumba kimoja kwao.Aliwataja waliokufa kwa radi hiyo kuwa ni Mhindi Petro (38) aliyeunguzwa kifuani na mguu wa kulia na Vailet Juma (16) aliyeungua usoni, ziwa la kushoto na mkono wa kulia.Wengine ni Grace Juma (13) aliyeunguzwa usoni, Kulwa Lukanya (12) mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Igalula aliyeungua tumboni na mkono wa kulia na Nyanzobe Juma (7) aliyeunguzwa usoni na mguu wa kulia.Majeruhi waliotibiwa Hospitali ya Wilaya ya Sikonge na kuruhusiwa ni Dotto Lukanya (12), mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Igalula ambaye aliunguzwa ubavu wa kushoto.Kamanda Nley aliwataja majeruhi wengine wa tukio hilo ni Pendo Machiya (11), mwanafunzi wa darasa la pili wa Shule ya Msingi Igalula aliyeunguzwa mguu wa kulia na Masanja Juma (11) aliyejeruhiwa mkono wake wa kushoto.Kamanda huyo alisema radi hiyo iliingilia dirishani chumba ambacho walikuwa wamelala wanafamilia hao wanane na kutokea ukutani upande wa pili na kusababisha ukuta kupasuka kutokana na kujengwa kwa miti na udongo.Alitoa pole kwa familia hiyo kutokana na tukio hilo na aliwataka watu waliobaki katika familia hiyo kuwa watulivu hasa katika kipindi hiki cha majozi ya kupotewa na ndugu na jamaa zao.Tukio hilo la vifo vinavyotokana na radi ni la pili kutokea kwa mwaka huu, kwani tukio kama hilo liliwahi kutokea miezi mitano iliyopita katika Wilaya ya Uyui baada ya radi kuua watu watatu wa familia | Kitaifa | 0 |