content
stringlengths 1
17.8k
| category
stringclasses 5
values | label
int64 0
4
|
---|---|---|
.https://www.youtube.com/watch?v=IIhWNE4aspw&feature=youtu.beTreni ya kwanza yenye mabehewa 22 na Tani zaidi ya Elfu Moja za mahindi yaliyouzwa na Tanzania kwa Serikali ya Zimbabwe imeondoka kuelekea Harare, huku ikielezwa kuwa, Tani zaidi zitaendelea kusafirishwa. | Biashara | 1 |
CHAMA cha Wamiliki wa Benki Tanzania (TBA) kimesema uamuzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuwataka kutoa huduma ya kubadilisha fedha za kigeni umekuwa na manufaa makubwa ya kiuchumi kwao.Mwenyekiti wa TBA ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema, tangu benki za biashara zianze kutoa huduma hiyo, amana zao zimeongezeka.Alisema hali hiyo inafanya benki hizo kuendelea kuimarika kiuchumi katika kuwahudumia wateja wao lakini pia haithiri maduka ya kubadilisha fedha za kigeni yaliyoko mtaani. Alisema maduka hayo bado ni muhimu kwa kuwa matawi ya benki hayapo kila mahali.Kwenye mkutano wa Rais John Magufuli na wafanyabiashara uliofanyika Ikulu Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Gavana wa Benki Kuu, Profesa Florens Luoga, alisema kupitia benki hizo, kwa siku wanakusanya zaidi ya Dola za Marekani milioni 10.Alisema katika kipindi cha wiki tatu sasa benki haziendi BoT kuomba fedha za kigeni na badala yake BoT sasa ina uwezo wa kununua fedha hizo kutoka kwa benki hizo na kuongeza kuwa benki hizo kwa sasa zina uwezo mkubwa wa kuhudumia sekta binafsi.Profesa Luoga alisema ni muhimu benki hizo kuwa ndiyo mkondo maalumu wa shughuli zote za kibenki nchini baada ya BoT kuchukua hatua ya kudhibiti uendeshaji wa biashara ya fedha za kigeni.Mwezi Februari mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji wa TBA, Tusekelege Joune, alilieza gazeti hili kuwa benki za biashara zilikuwa zikitoa huduma hiyo ya kubadilisha fedha za kigeni kama sehemu ya huduma ambazo wanaruhusiwa kisheria.Alisema hatua hiyo ya benki za biashara kutoa huduma ya kubadilisha fedha za kigeni itasaidia kujua mtiririko wa fedha hizo hapa nchini kwa kuwa kupitia benki, huduma itakuwa ikitolewa katika njia halali na za uwazi kwa kuwa mnunuzi na muuzaji watakuwa wakijulikana.Ikumbukwe kuwa Novemba 2018, Benki Kuu iliendesha operesheni maalumu dhidi ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni na kubaini baadhi ya maduka bubu kuendesha biashara hiyo bila kuwa na leseni, jambo ambalo ni kinyume na sheria.Kutokana na operesheni hiyo, maduka hayo yalifungwa kwa muda ili kupisha uchunguzi kwa lengo la kubaini maduka yaliyokuwa yakiendesha biashara hiyo kinyume na sheria ikiwemo biashara haramu ya utakasishaji fedha ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao. | Biashara | 1 |
YANGA leo inashuka dimbani kucheza nusu fainali dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa mashindano ya Kombe la Mapinduzi utakaochezwa kwenye Uwanja wa Amaan, Unguja, Zanzibar.Timu hizo zinakutana kwa mara ya kwanza msimu huu wa 2019/2020 na mchezo huo ambao utachezwa kuanzia saa 2:15 usiku unatarajiwa kuwa na ushindani kutokana na kikosi cha Yanga ambacho kinanolewa na Boniface Mkwasa kuwa na matokeo mazuri tangu aanze kukinoa.Hata Mtibwa Sugar inayofundishwa na Zuberi Katwila ni moja ya timu zenye kutandika kandanda safi ikiundwa na wachezaji chipukizi na katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara inashika nafasi ya saba ikiwa na pointi 22.Yanga ambayo ilikuwa kundi A katika mashindano hayo, imefuzu baada ya kuifunga Jamhuri kwa mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa juzi katika uwanja huo, wakati Mtibwa Sugar ambayo ilikuwa Kundi B ilifuzu baada ya kuifunga Chipukizi kwa penalti 4-2 katika uwanja wa Gombani, Pemba.Mabao ya Yanga yalifungwa na Adeyum Saleh na Mohammed Issa ‘Banka’, wakati penalti za Mtibwa Sugar zilifungwa na Omar Sultan, Abdulhalim Humud, Riffat Khamis na Dickson Job, baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya bao 1-1.Azam FC ambayo ni bingwa mtetezi, kesho itacheza dhidi ya Simba katika nusu fainali ya pili, huku wakiwa na kumbukumbu ya kuifunga katika fainali zilizopita kwa mabao 2-1 katika Uwanja wa Gombani, Pemba, hivyo mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.Simba ambayo ilikuwa kundi B, iliifunga Zimamoto juzi katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Gombani, Pemba kwa mabao 3-1 na Azam FC ambayo ipo Kundi A iliifunga Mlandege kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa juzi Uwanja wa Amaan.Mashindano haya ya 13 yalishirikisha timu nne za Zanzibar, ambazo zote zimeaga mashindano na timu nne za Tanzania Bara na yanachezwa kwa mtindo wa mtoano, ambapo bingwa anatarajiwa kuondoka na Sh milioni 15 pamoja na kombe. Timu ambazo zimeaga mashindano kutoka Kundi A ni Mlandege na Jamhuri, wakati zile za Kundi B ni Zimamoto na Chipukizi.Mashindano hayo maalum kwa ajili ya kusherehekea miaka 56 ya Mapinduzi, yalianza mwaka 2007 na hufanyika kila mwaka, ambapo Azam ndio bingwa mtetezi, baada ya kuifunga Simba 2-1 mwaka jana katika Uwanja wa Gombani, Pemba. Fainali za mashindano hayo zitafanyika Januari 13 katika Uwanja wa Amaan kuanzia saa 2:15 usiku | michezo | 2 |
WACHUNGAJI Josephat Katunzi wa Kanisa la EAGT-City Center la Mtongani Dar es Salaam na Julius Oisso wa Kanisa la Waadventisa Wasabato (SDA), Mtaa wa Kitunda Jimbo la Kusini Mashariki mwa Tanzania wamesema matumizi ya simu za mkononi yanahitaji umakini kwani yanaporomosha maadili nchini.Walisema hayo kwa nyakati tofauti kabla ya kuongoza Ibada ya Kumshukuru Mungu kwa matokeo mazuri ya mtihani wa mwisho uliowawezsha wanafunzi wa Shule Huria ya Brothers Academy (Brofoa) Banana-Ukonga, Ilala jijini Dar es Salaam kufaulu kwa kiwango kikubwa katika mafunzo ya QT shuleni hapo. Mmoja wa wachungaji hao, Katunzi alisema licha ya faida kadhaa za matumizi ya simu katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), bado simu za mkononi zinachangia kubomoa maadili ya jamii kwani vijana wengi hawazitumii kwa faida na kulipa Kanisa na taifa mzigo wa malezi ya vijana waliokengeuka nazo.“Malezi ya watoto wengi yameharibika. Simu za mkononi zimeondoa ibada na uwepo wa Mungu katika familia nyingi na kuchangia watoto wengi kuharibikiwa katika masomo na maisha yao,” alisema Mchungaji Katunzi. “Kanisa na Taifa tunahitaji nguvu ya pamoja kuhakikisha teknolojia hii, badala ya kubomoa vizazi vyetu, inavijenga,” Mchungaji alisema. Aliipongeza Brothers Academy kwa mafanikio katika utoaji elimu unaowawezesha wanafunzi wake kufaulu kwa wingi akisema hayo ni matokeo pia ya kumtanguliza Mungu mbele.Mchungaji Oisso alisema: “Kuporomoka kwa madili kunachangiwa na mambo mengi ikiwamo teknolojia kwa kuwa licha ya dini na wazazi kutimiza majukumu yao, mitandao ya kijamii inafichua na kuweka wazi kila kitu kwa watoto na vijana hata mambo machafu.” Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto alipongeza matokeo mazuri na ufaulu wa wanafunzi wa Brothers Academy. Alisema manispaa iko nao bega kwa bega kuhakikisha matamanio ya Rais John Magufuli ya vijana kupata haki ya elimu bora, yanatimia.“Taasisi kama Brothers Academy zinaonesha kuwa msaada kwa taifa kwani wapo wanafunzi wengi waliokosa fursa kwa sababu mbalimbali hivyo, shule hizi zinawapa nafasi nyingine kuweka mambo sawa,” anasema Kumbilamoto. Mmoja wa wanafunzi waliofaulu shuleni hapo, Restituta Fredrick alisema msimamo wake wa kukataa kumiliki simu hadi atakapokamilisha masomo, ni moja ya mambo yaliyomwezesha kufanya vizuri zaidi katika mitihani yake. Mwalimu na Mkurugenzi wa Brothers Academy, Robert Rwezaula aliyataja mambo yanayochangia mafanikio ya elimu shuleni hapo kuwa ni uwepo wa walimu wa kutosha wenye elimu ya shahada na shahada ya uzamili, uwepo wa maabara ya masomo ya sayansi na kuzingatia mitaala ya wizara na taasisi zake. | Kitaifa | 0 |
Hatua hiyo pia imesababisha idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa pia kushuka kwa asilimia 84 hadi kufikia Sh milioni 1.8 kutoka milioni 11.6. Akizungumza jana kuhusu taarifa ya soko katika mauzo yaliyofanyika wiki iliyopita, Meneja Miradi na Biashara wa DSE, Patrick Mususa alitaja kampuni tatu zilizoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kuwa ni Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) asilimia 39.72, benki ya CRDB asilimia 26.18 na Kampuni ya Saruji Tanga (TCCL) asilimia 24.39.Mususa alisema idadi ya mtaji wa soko la hisa la Dar es Salaam imeshuka pia kutoka Sh trilioni 21 hadi Sh trilioni 20.2 katika mnada wa mauzo ya hisa uliofanyika wiki hii. Alisema idadi ya mtaji wa kampuni ya ndani pia imeshuka kutoka Sh trilioni 9.8 hadi kufikia Sh trilioni 9.6.Akizungumzia mabadiliko ya bei za hisa, alisema kampuni moja imejitokeza kuongoza katika ongezeko la bei ya hisa wiki iliyopita ambayo ni kampuni ya Nation Media (NMD) kwa asilimia 7.14.Kwa upande wa viashiria vya sekta, Mususa alisema kiashiria cha sekta ya viwanda kimeshuka kwa pointi 9.3 kikiwa kimechangiwa na punguzo la bei ya hisa kwenye kaunta za Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) kwa asilimia 0.62 na TCCL kwa asilimia 0.37. | Biashara | 1 |
Rai hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri MKuu(Uwekezaji na Uwezeshwaji), Dk Mary Nagu wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF).Alisema ukosefu wa rasilimali watu wenye ubora ni kikwazo kikubwa kwa wawekezaji wanaokuja kuwekeza nchini.Waziri Nagu alisema baadhi ya wawekezaji wanakosa wataalamu wenye ujuzi stahiki wa kuwasaidia katika kuendeleza sekta husika ambayo imewekezwa.Alisema serikali kwa upande wake imeimarisha mazingira ya uwekezaji kwa kuimarisha miundombinu ya kiuchumi, kusimamia sheria za nchi na kulinda amani na utulivu, ikiwa ni kama njia mojawapo ya kuweka mazingira bora ya uwekezaji.Aliongeza kwa sasa serikali inaandaa sera ya taifa ya maendeleo ya sekta binafsi kwa kushirikiana na TPSF kwa lengo la kuhakikisha kuwa watanzania wananufaika na biashara.Alisema pia serikali katika kuhakikisha hilo linafanyika, itatumia Mabaraza ya Biashara ya Mikoa na Wilaya kubaini mahitaji ya sekta binafsi na kufanya tathmini ya gharama za kufanya biashara kwenye miko na wilaya.“Sasa katika kuhakikisha kuwa hili linafanikiwa kirahisi, uzoefu utakaopatikana utatuwezesha kuchukua hatua za kupunguza muda wa gharama za kufanya biashara na kuwekeza hapa nchini,” alisema Dk Nagu.Aliongeza; “kwa sasa kampeni ya kutumia Bidhaa za Huduma za Tanzania imeanza kupata mafanikio makubwa kwa kuwa tayari watanzania wameanza kutengeneza bidhaa zenye ubora na zinazohimili ushindani”.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TPSF, Reginald Mengi alisema kuwa katika mkutano huo wa mwaka wanajadili masuala mbalimbali kuhusu maendeleo na changamoto. | Biashara | 1 |
['.'] | michezo | 2 |
RAIS John Magufuli ameagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha inatafuta mbinu mbadala za kukusanya kodi na kuacha mara moja tabia ya kuwakadiria wafanyabiashara viwango vikubwa vya kodi.Aidha, amewaonya wafanyabiashara wadogo maarufu machinga kuacha kutumiwa na wafanyabiashara wakubwa ambao wamebuni njia mbadala za kukwepa kulipa kodi kwani hivi sasa machinga hao wanakuwa na biashara kubwa na hawana risiti za TRA wala mashine.Rais Magufuli ameyasema hayo jana wakati alipozungumza na wananchi wa eneo la Kimnyaki , Kata ya Kimnyaki wilayani Arumeru mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji wenye thamani ya Sh bilioni 520 fedha zilizotolewa kama mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).Ameagiza TRA kufanya tathimini za kwanini watu hawalipi kodi kwani mamlaka hiyo ndio imechangia kwa kiasi kikubwa watu kukwepa kodi kutokana na kukadiria viwango vikubwa vya ulipaji wa kodi.Amesema ni afadhali TRA ikaliangalia jambo hilo kwa makini ikiwemo kuweka viwango vidogo vitakavyowawezesha wananchi kulipa kodi kwani kuna baadhi ya maeneo bado hawajaanza kukusanya kodi.“Nyie TRA nani aliwaambia muweke mazingira yasiyorithisha kwa wananchi kulipa kodi, kuna wafanyakazi wengine mnakwenda na polisi kudai kodi mkiulizwa kwanini mnafanya haya mnasema hapa kazi tu kwani mimi niliwatuma muwatishe watu? “…Nasema hapana nyie TRA ndio mmeweka mazingira magumu yanayotoa mianya kwa wafanyabiashara kukwepa kodi kwanini mnawakadiria makadirio makubwa wafanyabiashara ? alihoji.Aliwaagiza kukaa chini na kufanyia tathmini suala hilo ili wananchi waone umhimu wa kulipa kodi.“Na naagiza TRA mkae na Waziri wa fedha pamoja na wafanyabiashara myaangalie haya mambo,”“Mnakadiria gharama kubwa sana kwa wafanyabiashara ili mpewe rushwa halafu mnasema hapa kazi tu nani amewatuma kufanya haya? Na nasema wafanyakazi wa TRA wenye tabia ya kuomba rushwa katika utawala wangu hawana nafasi,” alisisitiza.Pamoja na hayo, Dk Magufuli, alitoa rai kwa wafanyabiashara wadogo kaucha kutumiwa na wafanyabiashara wakubwa ambao wamebuni njia mbadala za kukwepa kulipa kodi kwani hivi sasa machinga hao wanakuwa na biashara kubwa na hawana risisti za TRA wala mashine .“Nashangaa siku hizi mmetumia mwanya wa ruhusa yangu ya nyie machinga kufanya biashara kama mtaji kwa wafanyabiashara wakubwa, sasa naomba msikubali kutumiwa na wafanyabiashara ili kukwepa kodi msitumie vibaya fursa hii niliyowapa nawaomba sana,” alisisitiza.Akizungumzia suala la madini ya tanzanite, Rais Magufuli alisema haiwezekani nchi ya Tanzania ikawa maskini wakati inazalisha madini hayo ndio maana aliamua kujenga ukuta.“Baada ya ujenzi wa ukuta kukamilika kuna nchi moja (hakutaja jina) ilipiga kelele kweli kweli kwani ilikuwa ikizalisha ajira ya watu 15,000 kila siku kutokana na madini hayo ya tanzanite wakati nchi hiyo haichimbi huku Tanzania ikinufaika na madini hayo kwa asilimia sita hadi saba tu,” alisema.Kuhusu Korosho Alisema baadhi ya viongozi wanahusika kuwalangua wakulima kwani walikuwa wakinunua korosho hizo shambani wakati zikitoa maua kwa kilo moja Sh 200 wakati hata mashamba hawana.Rais huyo alieleza kuwa serikali imeingilia kati suala hilo la uuzwaji wa korosho kwa wakulima na hivi sasa mtu anayetaka kuuza korosho lazima aonyeshe shamba lake lipo wapi na si kumnyonya mkulima wa zao hilo.“Hili suala la korosho baadhi ya viongozi wakubwa wanahusika na nilipowagusa walipiga kelele, sasa nasema serikali imeamua kununua zao hili na ukitaka kuuza korosho onyesha shamba kwanza,” alibainisha''.Aliongeza kuwa “Mnajua hii nchi ukiwa unasimamia mambo yaende sawa wanakuita kila jina na mimi nakubali mniite mnavyotaka lakini nasema hivi nilichaguliwa na wananchi maskini na sitakubali waonewe na wale wezi nitawakamata tuu ili mpige kelele vizuri” | Kitaifa | 0 |
Mashine ya kwanza itatumika na wafanyakazi pekee wa Kampuni ya Pacific International Lines (PIL) ambayo watatumia kuweka fedha kwenye akaunti zao moja kwa moja bila kulazimika kufika kwenye ofisi au kuhudumiwa na wafanyakazi wa benki hiyo. Baadaye mashine za aina hiyo zitawekwa maeneo mengine kwa ajili ya kutumiwa na wateja wote wa benki hiyo.Ufunguzi wa mashine hiyo ulifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni ukihusisha mwakilishi wa benki hiyo ambaye ni Mkuu wa Huduma za matawi , Eugine Massawe pamoja na Meneja Mkuu wa kampuni ya PIL, Kevin Stone.Akizungumzia mashine hiyo iliyopo kwenye jengo la Maktaba Dar es Salaam, Massawe alisema ni mwendelezo wa mkakati wa benki hiyo kurahisisha huduma zaidi za kifedha kwa wateja wake.“Mashine hii itawawezesha wateja wetu kuweka pesa moja kwa moja kwenye akaunti zao wao wenyewe,’’ alisema.Massawe alisema kwa kuanzia mashine hiyo itaanza kupokea noti za Dola ya Marekani kwa kiasi chochote.“Ifahamike kwamba mashine hii ina uwezo mkubwa wa kutambua fedha bandia au zile zisizofaa kwa kuwa imewekewa mfumo bora kabisa wa kiusalama,” alisema.Aliongeza kuwa mashine hiyo inamwezesha mtumiaji kupata risiti ya muamala atakaoufanya na kumhakikishia mafanikio ya muamala husika.Alisema Exim itabaki kuwa benki pekee yenye kubuni huduma zinazokidhi matakwa ya wateja kulingana na mabadiliko ya kimahitaji katika huduma za kibenki.Alisema huduma hiyo imewekwa jirani na makao makuu ya benki hiyo kuwawezesha watumiaji wa huduma hiyo kupata msaada kwa urahisi kutoka kwa wafanyakazi wa benki pale wanapohitaji.“Itakapofikia kipindi ambacho wateja wetu watakuwa tayari wamejenga uelewa wa kutosha kuhusiana na matumizi sahihi ya mashine hii tutakuwa tayari kuongeza mashine nyingine katika maeneo mbalimbali ili waweze kufurahia huduma hii zaidi,’’ alisema. | Biashara | 1 |
MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amedai kuwa yeye ndiye aliyewafanya watu wengi kwenye wilaya yake wampende msanii wa muziki kutoka WCB, Harmonize.Kwani amekuwa akitumia nyimbo zake kwenye matukio mbalimbali ya kijamii. Jokate ameeleza hayo juzi wakati wa futari iliyoandaliwa na Harmonize wilayani Kisarawe, ambayo ililenga msanii huyo kufuturisha mashabiki wake waliopo wilayani humo.“Mimi ndio nimefanya watu wengi wilayani kwangu wampende Harmonize, sasa hivi wimbo ambao tunaupenda ni Kainama na Kwangaru, na sio unafiki sisi nyimbo zake tunazitwanga sana, maana yake ukiingia field lazima upige muziki kidogo. Sisi Kwangwaru, Kainama na hii Never Give Up tunaisikiliza kwa sababu inaamsha.” alisema Jokate.Kwa upande mwingine, Jokate amemshauri Harmonize aoe na pia amekaribisha ndani ya wilaya yake kwenda kuwekeza, kwani fursa zinapatikana kwa wingi.“Mimi nilitaka niseme aoe lakini nakumbuka mimi mwenyewe sijaolewa, Namshauri mimi awekeze Kisarawe kuna ardhi ya kutosha,” alisema Jokate. | michezo | 2 |
Meneja wa Urasimishaji wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (Mkurabita), Makame Juma Pande, alisema wakulima watakaonufaika na mpango huo wa kupatiwa hati za kimila ni wa Ruhembe, Kitete Msindazi, Kihelezo na Kidogobasi katika wilaya ya Kilosa.Vijiji vingine ni Mgombera, Katulukila, Sonjo, Sole, Mkula na Msola Ujamaa vya wilaya ya Kilombero.Chini ya mpango huo, vijiji 40 katika wilaya za Kilosa na Kilombero vitapatiwa hati miliki za vijiji, ambapo pia hati zaidi ya 5,000 zitatolewa kwa wakulima wadogo wa miwa.Kwa upande wake, Mratibu wa Mkurabita Wilaya ya Kilosa, Symphoroza Mollel, alisema mpango huo utawezesha wakulima kupata mikopo kwa ajili ya kuendeleza kilimo hicho kwa kutumia hati hizo za kimila. | Biashara | 1 |
Waziri wa Madini Angellah Kairuki leo Alhamisi asubuhi ametembelea Kituo cha Umahiri cha Bariadi kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.Ametoa pongezi kwa Mkandarasi SUMA-JKT kwa kazi iliyofanyika ya ujenzi wa kituo hicho na kumtaka mkandarasi huyo kuzingatia muda wa kukamilisha ujenzi na ubora.Aidha, amemweleza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka kuwa Wizara itaangalia namna ya kuusaidia mkoa huo katika uendelezaji wa madini ya Nikel na chumvi yanayopatikana mkoani humo.Aidha, amempongeza Rais John Magufuli kwa kuridhia kuondoa tozo tisa kati ya 16 zilizokuwa zikitozwa na Taasisi mbalimbali katika Sekta ya Madini.Amesema uwepo wa kituo hicho mkoani humo, utawezesha wachimbaji wadogo wa madini kuchimba kwa tija. Pia, ametoa rai kwa wananchi walio tayari kuwekeza katika Sekta ya Madini kuwekeza mkoani humo pamoja na maeneo mengine nchini.Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa huo Anthony Mtaka, ameishukuru Wizara kwa kuuchagua mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa ambayo vituo hivyo vya umahiri vinajengwa. | Kitaifa | 0 |
['Rais wa zamani wa TTF Jamal Malinzi', 'Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na aliyekuwa Katibu wa shirikisho hilo, Selestine Mwesigwa kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini.', 'Malinzi ametakiwa kulipa faini ya Shilingi 500,000 na Mwesigwa Shilingi milioni moja. Wote wamekubali kulipa kiasi hicho cha fedha.', 'Mahakama hiyo imetoa hukumu hiyo leo Jumatano baada ya kuwatia hatiani .', 'Wakati Malinzi akitiwa hatiani kwa shtaka moja la kutengeneza nyaraka za uongo, Mwesigwa alitiwa hatiani kwa kutumia nyaraka hizo.', 'Mahakama hiyo imewaachia huru washtakiwa wawili katika kesi hiyo ambao ni aliyekuwa mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga na Frola Rauya ambaye alikuwa karani.', 'Katika shtaka hilo Malinzi anadaiwa kutengeneza nyaraka hizo zinazoeleza kuhusu kikao cha kamati tendaji ya TFF kwa kubadili watia saini badala ya Edagar Masoud aliwekwa Mwanga.', 'Washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka 20 yakiwemo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha ambazo ni Dola 173,335 za Marekani.'] | michezo | 2 |
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amesema jana kwa mwenendo huo ni matarajio ya Serikali kuwa msamaha wa kodi katika mwaka wa fedha 2015/2016 utakuwa ni Sh bilioni 752.141 sawa na asilimia 0.84 ya Pato la Taifa.Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo Peneza (Chadema) aliyetaka kufahamu lini Serikali itatekeleza ahadi yake ya kupunguza misamaha ya kodi kufikia asilimia ya Pato la Taifa.Dk Kijaji alitaja hatua zilizochukuliwa na serikali katika kupunguza misamaha ya kodi kuwa ni pamoja na kurekebisha upeo wa misamaha inayotolewa chini ya Kituo cha Uwekezaji (TIC) na sekta ya madini ambazo zimesaidia kupunguza misamaha hadi kufikia asilimia 1.9 ya Pato la Taifa katika mwaka wa fedha 2014/2015.Mwaka 2009/2010 serikali iliamua kupitia upya sheria zinazohusu misamaha ya kodi ili kuondoa misamaha ambayo haikuwa na tija kwa taifa. Alisema katika mapitio hayo, serikali ilibaini kuwa takriban asilimia 60 hadi 64 ya misamaha yote ya kodi ilikuwa inatokana na VAT.Baada ya kubaini hilo, serikali ilifanyia maboresho Sheria ya VAT, sura ya 148 na kuondoa misamaha ambayo haikuwa na tija kwa taifa.Juhudi za kupunguza misamaha ya kodi zilianza kufanyika mwaka 2010/2011 baada ya kubaini kwa wastani misamaha ilikuwa imefikia takriban asilimia 3.2 ya Pato la Taifa kwa mwaka katika kipindi cha mwaka 2006/2007 hadi 2009/2010.Katika swali la nyongeza, Peneza alitaka kufahamu lini serikali itapeleka bungeni marekebisho ya sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004 inayotoa misamaha ya kodi kwa mishahara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar(SMZ) pamoja na majaji. | Biashara | 1 |
Hayo yameelezwa na Katibu wa chama hicho, Mohammed Ali Hilali ‘Tedy’ alipokutana na mwandishi wa habari hizi jana ambae alitaka kujua mwelekeo mzima wa chama hicho kuhusu ligi.Tedy alisema kikao hicho kitafanyika katika ukumbi wa VIP Amaan asubuhi, na kitakuwa chini ya Mwenyekiti wake Rais wa ZFA, Ravia Idarous Faina.Alisema ni wajibu wa kamati hiyo kukutana maana kuna ligi zinaendelea na nyingine zinakaribia kumalizika. Aidha alisema kuwa kikao hicho pia kitasikiliza malalamiko mawili moja likiwa la timu ya Negro dhidi ya African Boys na lingine la Timu ya Miembeni City dhidi ya Chuoni.“Tunakutana katika kikao cha kawaida cha kamati ya utendaji ambapo mambo mbali mbali yatajadiliwa yanayohusu chama chetu,” alisema.Alisema kuwa mbali na hayo pia kikao hicho kitatumika kujadili waamuzi wawili waliosimamishwa na kutoa maamuzi ya muda watakaotumikia adhabu hiyo.Aliwataja waamuzi hao watakaojadiliwa ni Mohammed Kassim na Abeid Juma wakidaiwa kushindwa kuzitafsiri sheria za mpira wa miguu siku walipochezesha mechi ya Miembeni City na Chuoni. | michezo | 2 |
KINARA wa upachikaji wa mabao kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL), Salim Ayee amesema angekuwa anachezea timu kubwa za Simba na Yanga angejumuishwa kwenye kikosi cha Taifa Stars.Mchezaji huyo anayeichezea timu ya Mwadui ya Shinyanga, mpaka sasa amepachika mabao 14 na kuongoza orodha ya wachezaji waliofunga mabao mengi akiwapiku Heritier Makambo wa Yanga na Meddie Kagere wa Simba ambao kila mmoja amefunga mabao 12.Hata hivyo, pamoja na kuwa kinara wa ufungaji kwenye ligi kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike hakumjumisha mshambuliaji huyo chipukizi kwenye kikosi chake.Akizungumza na gazeti hili jana, Ayee anayotokea Tanzania visiwani alisema angekuwa anacheza Simba au Yanga angeweza kuitwa Taifa Stars.“Naamini ningekuwa nacheza timu kubwa kati ya Simba na Yanga au hata Azam ningeitwa, inawezekana wana vigezo vikubwa wanavyoangalia au kuna wanaofanya vizuri zaidi yangu,” amesema Ayee.Ayee alisema anashangaa pamoja na kuongoza kwa kufumania nyavu kwa miezi miwili ameshindwa kupewa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi. | michezo | 2 |
KABLA ya mechi za jana za michuano ya Mataifa ya Afrika, Afcon 2019, mshambuliaji wa Uganda Emmanuel Okwi alikuwa miongoni mwa wanaoongoza katika kuwania kiatu cha dhahabu. Okwi na timu yake wako Kundi A wakiwa na wenyeji Misri, Zimbabwe na Congo DR. Mshambuliaji huyo amefunga mabao mwili mpaka sasa wakichuana na Mickael Pote wa Benin na Michael Olunga wa Kenya. Okwi aliliambia gazeti hili kuwa lengo lake ni kuweka historia kwa kuibuka mfungaji bora wa michuano hii.“Najua ushindani mkali, washambuliaji wapo wengi lakini nitajitahidi kufunga kila mechi ili nipate kiatu cha dhahabu,” alisema. Uganda inamaliza mechi ya makundi leo dhidi ya wenyeji Misri, katika mchezo unaotarajia kuwa mkali na wa kusisimua. Uganda, The Cranes, ipo kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele hatua ya mtoano endapo itashinda au kupata sare ya aina yoyote katika mchezo wake huo wa mwisho.Baadhi ya wenye bao moja moja ni Mbwana Samatta na Simon Msuva wa Tanzania, Adam Traore wa Mali, Mohamed Salah, Mohamed Trezguet wa Misri na Andre Ayew wa Ghana | michezo | 2 |
SHIRIKISHO la Wachimbaji Madini Tanzania limempongeza Rais John Magufuli kwa kuwaboreshea mazingira ya kazi na biashara ya madini kwa wachimbaji wadogo.Rais wa shirikisho hilo, John Mabina amesema, Rais Magufuli na serikali yake wamefanya vizuri kwa kuandaa na kufanikisha Muswada uliopitishwa bungeni mwishoni mwa wiki ambao unatoa unafuu kwa wachimbaji wadogo wa madini.“Kwa kweli tumefurahi sana na kwa kuonesha furaha yetu tumeandaa maandamano Jumamosi hii kumpongeza Rais kwa kutujali sisi wachimbaji wadogo wa madini hapa nchini,” amesema.Juzi Bunge lilipitisha Muswada wa Sheria ambao pamoja na mambo mengine unaondoa kodi ya zuio la asilimia tano inayotozwa kwenye bei ya kuuzia madini kwa wachimbaji wadogo na kurekebisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa kutoa msamaha kwenye madini ya metali na vito yatakayouzwa katika masoko ya ndani ya nchi.Mabina amesema maandamano hayo yatafanyika nchi nzima katika mikoa yote kuonesha kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli katika kuboresha mazingira ya biashara kwa wafanyabiashara hao ambao ni wachimbaji wadogo wa madini.Aidha, alisema kwa punguzo hilo sasa wachimbaji wa madini wadogo wamebaki na tozo moja la asilimia sita la ‘loyalty’ pekee, jambo ambalo linatoa unafuu mkubwa kwao.“Rais wetu ni msikivu amesikia kilio chetu na kutupa unafuu sisi wachimbaji wa madini na sisi tunampongeza sana kwa moto wake huo,” amesema Mabina.Alisema baada ya unafuu huo wachimbaji wadogo sasa wataingia kuuza madini yao katika masoko rasmi yaliyowekwa na serikali. Marekebisho hayo ya Muswada yanakusudia kuanzisha vituo vya ununuzi wa madini katika maeneo ambako masoko ya madini hayakuwepo na kuweka utaratibu wa uingizaji madini nchini.Akizungumzia hatua hiyo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana aliishauri serikali kuandaa masoko hayo rasmi haraka ili serikali ikusanye mapato yake.Alisema maboresho ya Muswada huo yanaonesha wazi kuwa Rais Magufuli anatekeleza kwa vitendo ahadi zake na pia anatekeleza kwa wakati.“Haijapita wiki tatu tangu Rais azungumze na wafanyabiashara wa Sekta ya Madini na wao kumueleza changamoto zao, lakini tumeona Muswada umeenda bungeni na kupitishwa ni dalili kuwa Rais anatenda tena kwa wakati,” amesema Dk Bana. | Kitaifa | 0 |
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ameagiza minada ya mifugo baada ya serikali kushinda kesi ifanyike nje ya hifadhi ili kuondoa dhana ya kuwa wahifadhi wanajiuzia wenyewe.Pia, amewaonya askari wanyamapori wenye tabia ya kuvizia mifugo ikiwa mpakani kati ya kijiji na hifadhi na kisha kuwasukumia ndani ya hifadhi ili waikamate na kusema si sawa.Kanyasu ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na viongozi wa vijiji 15 vilivyopo na vinavyozunguka Pori la Akiba la Mkungunero lililopo wilayani Kondoa mkoani hapa.Amesema mifugo inayokamatwa katika hifadhi na kutakiwa kupigwa mdana, ipigwe mnada nje ya hifadhi ili kuondoa dhana ya kuwa wahifadhi wanajiuzia wenyewe.Kanyasu alisema kuwa kabla ya minada hiyo kufanyika ni lazima itangazwe katika vijiji ili kuwajulisha wananchi na kutoa fursa ya wao kushiriki katika minada hiyo.Pia, alisema hatua ya minada kufanyika nje ya hifadhi, kutaondoa tatizo la vibali vya kuingia kwenye hifadhi wakati wa minada kwani wananchi wanalazimika kuwa na vibali na kwa wale ambao huingia bila vibali hukamatwa kwa makosa ya kuingia hifadhini kinyume cha taratibu."Minada hii ikifanyika nje ya hifadhi, hata tuhuma na malalamiko mengi yatapungua kama vile tuhuma za rushwa na malalamiko ya kuwa wahifadhi ndio wamekuwa wakishiriki kuwatafuta wanunuzi wa mifugo kwa makubaliano ya kulipwa mara baada ya mnada."Aliongeza: " Pia kumekuwapo na malalamiko ya wale ambao mifugo yao imetaifishwa kuwa hawajui siku inayofanyika minada hiyo na badala yake wanaopewa taarifa ni wafanyabiashara wakubwa pekee jambo ambalo linaibua chuku dhidi ya wahifadhi."Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikengwe, Ismail Hamis alisema licha ya huo utaratibu mpya wa kufanyia minada nje ya hifadhi, anaiomba serikali iangalie upya sheria ya kutaifisha mifugo kwani imesababisha wafugaji wengi kuwa maskini.Alisema ni vyema mifugo ikikamatwa ndani ya hifadhi, waruhusiwe kulipa fidia kwa sababu mifugo hiyo ndio imekuwa tegemeo lao kwa kuwasaidia kusomesha watoto wao.Kwa upande wake, Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Mabula Misungwi aliahidi kutekeleza agizo hilo na kusisitiza kuwa watafanya utaratibu wa kuwajulisha wananchi wa maeneo ambayo mifugo imekamatwa. Misungwi pia aliwataka watumishi hao kujiepusha na rushwa pindi wanapokamata mifugo kutoka kwa wafugaji. | Kitaifa | 0 |
VYAMA vya siasa nchini vimetakiwa kutekeleza matakwa ya sheria ya msajili wa vyama vya siasa ambayo inavitaka vyama hivyo kuzingatia uwepo wa Muungano katika katiba za vyama vyao ikiwa ni moja ya tunu ya taifa.Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu ya miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Mohamed Ali Ahmed alisema muungano ndiyo utambulisho wa taifa la Tanzania. Alisema sheria ya vyama vya siasa imetambua umuhimu wa kuwepo kwa muungano katika katiba za vyama hivyo kwa ajili ya kupata viongozi ambao watafahamu umuhimu wa muungano.Alisema marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2019 kifungu cha 6 (5) unavitaka vyama vya siasa vyenye usajili nchini katika maandalizi ya katiba zao na sera kuzingatia suala la muungano kama kipaumbele cha kwanza. Aidha katika marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2019 pia umevitaka vyama vilivyopata usajili kuyatambua Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 kuwa ndiyo yaliyowakomboa wananchi wa Zanzibar na wazalendo kushika hatamu ya kuongoza dola. ‘’Katika marekebisho ya sheria ya msajili wa vyama vya siasa suala la kuyaenzi Mapinduzi ya Zanzibar limetambuliwa rasmi kwa lengo la wanachama na wananchi kwa ujumla kuyatambua kwa mujibu wa sheria,’’alisema.Mambo mengine ya msingi ambayo yametakiwa kutambuliwa na kuingizwa katika katiba na sera za vyama vya siasa ni mwenge wa uhuru, demokrasia na utawala bora. Akifafanua zaidi kuhusu Mwenge wa Uhuru, alisema upo kwa ajili ya kujenga umoja na mshikamano wa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ndiyo maana hutembezwa nchini kote. Alisema Mwenge wa Uhuru hata muundo wake umewekwa alama ya Adamu na Hawa ambayo ni nembo rasmi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukionesha ushirikiano wa pamoja. | Kitaifa | 0 |
TIMU ya Soka ya Kiluvya United imesema itawafunga mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho la Soka nchini(TFF), Mtibwa Sugar wakati timu hizo zitakapokutana kwenye hatua ya awali ya michuano hiyo Desemba 21.Akizungumza na gazeti hili jana, Mwenyekiti wa timu hiyo, Edward Mgogo alisema wapo kwenye maandalizi makubwa kuhakikisha wanawatoa mabingwa hao watetezi na kuanza safari ya kusaka ubingwa wa michuano hiyo.“Tutawashangaza wengi msimu huu licha ya kuanza na mabingwa watetezi, lakini tutajitahidi kwa hali na mali kuhakikisha tunafanya vizuri na kutimiza mipango tuliojiwekea kwenye mashindano haya ya kombe la TFF,” alisema Mgogo.Alisema hata hivyo, mchezo wao dhidi ya Mtibwa hautakuwa rahisi kwani wanacheza na timu ambayo msimu uliopita ilitwaa kombe hilo na kuongeza kuwa tayari wako kwenye maandalizi mazito ya kuhakikisha wanaitoa timu hiyo. “Tumepangwa kucheza na Mtibwa Sugar ambao ni mabingwa wa msimu uliopita wa mashindano haya; sio mchezo rahisi hata kidogo lakini tumedhamiria kuwashangaza kwa kuwatoa mashindanoni,” alisema Mgogo.Mgogo aliwaomba wadau wote wa soka wa mkoa wa Pwani kushirikiana na uongozi wa klabu ya Kiluvya kuhakikisha wanaiunga mkono timu yao na kuiondosha Mtibwa Sugar kwenye mashindano hayo.Mtibwa Sugar walishinda Kombe la TFF baada ya kuifunga timu ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa fainali msimu uliopita na kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF). | michezo | 2 |
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Airtel wa Huduma kwa Wateja, Adriana Lyamba wakati wanachuo hao walipofanya ziara ya mafunzo kwenye duka la kisasa la Airtel Expo lililopo ofisi kuu za Airtel, Morocco Dar es Salaam jana.Ziara hiyo imewezeshwa na kampuni hiyo ya simu kama sehemu ya kutanua wigo wa kutoa huduma zenye ubora za kibunifu kwa wateja wake.Wakiwa hapo wanachuo hao walijifunza mambo mengi juu ya kampuni hiyo inavyofanya kazi kuanzia huduma zake hadi bidhaa zinazouzwa ikiwemo modemu iliyozinduliwa hivi karibuni maarufu kama modemu ya maajabu.Wanafunzi hao pia wamejionea jinsi duka la Airtel Expo linavyohudumia wateja wengi kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu ya kidigitali.Aidha, akizungumza na wanachuo hao, Lyamba amewapongeza wanafunzi hao kwa dhamira yao ya kutaka kujifunza katika ulimwengu wa teknolojia na kuwakaribisha wengine kuhudhuria | Biashara | 1 |
YANGA juzi iliendeleza wimbi la ushindi kwa kuikandamiza African Lyon kwa bao 1-0 lakini taarifa ikufi kie kuwa benchi la ufundi la timu hiyo limeeleza kuwa moto huo waliouwasha hautazima na kwamba watahakikisha wanazoa pointi tatu katika kila mechi iliyo mbele yao.Yanga ilipata ushindi huo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha na kuifanya izidi kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu kwa jumla ya pointi 47 dhidi ya Azam wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 40 na mabingwa watetezi Simba wanaoshika nafasi ya tatu kwa pointi 30. Kocha msaidizi wa wanajangwani hao, Noel Mwandila alianza kwa kuelezea ugumu wa mchezo wao dhidi ya Lyon hasa ukichanganya changamoto ya uwanja waliokuwa wakichezea lakini anafurahi kwa kuwa walikabiliana na vikwazo hivyo na mwisho kupata pointi tatu muhimu.“Haukuwa mchezo rahisi, Lyon walikuwa sawa na walicheza vizuri ingawa tulipambana na kuwazidi na kuibuka na ushindi. Awali pia kulikuwa na changmoto ya ubora wa uwanja lakini wachezaji wakapambana kuendana na hali halisi na kufanikiwa kucheza vizuri kwa kiasi kikubwa. “Yote kwa yote tumefurahi kuondoka na pointi tatu, bado kuna safari ndefu lakini hatutaangalia wanaotufukuzia (Azam na Simba) kwa sasa.Shida yetu ni kuhakikisha tunashinda na kuondoka na pointi tatu katika kila mechi… “Tukifanikiwa hapo, tutakuwa tumekaribia lengo letu na tutakuwa sehemu salama zaidi, kila mchezo uliopo mbele yetu tunauchukulia kwa umakini mkubwa na tutahitaji ushindi na pointi tatu pia, tunachohitaji hicho tu kwa sasa,” alisema Mwandila. Baada ya ushindi huo, Yanga sasa imecheza jumla ya mechi 17 bilakupoteza zaidi ya kutoa sare michezo miwili pekee. Mmoja dhidi ya Simba waliotoka suluhu na mwingine dhidi ya Ndanda uliotoka sare ya bao 1-1. | michezo | 2 |
Mabao ya Yanga yalifungwa na kiungo Pius Buswita dakika ya 82 akiunganisha pasi ya Amisi Tambwe, kabla Tambwe hajafunga bao la pili kwa pasi ya Buswita. Baada ya mabao hayo, Reha walionekana kukubali matokeo na Yanga wakaanza kucheza kwa uhuru uwanjani, wakigongeana pasi za kuwaburudisha mashabiki wao.Katika mchezo huo, Reha walionekana kuwa wagumu karibu muda wote wa mchezo na hasa kipindi cha kwanza ambapo walicheza kwa kujihami zaidi wakifanya mashambulizi ya kushtukiza lakini Yanga waling’amua janja hiyo na kubadili maarifa kipindi cha pili na kushambulia kwa nguvu zaidi.Reha ambayo ilikuwa chini ya kocha Ivo Mapunda, kipa wa zamani wa Yanga na timu ya taifa ilikuwa ngumu kufungika, na kipa wake Idrissa Ramadhani alikuwa nyota kwa kudaka kwa ustadi.Mabadiliko ya kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa ya kumpumzisha Emmanuel Martin na kumuingiza Said Mussa aliyekuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kilichoshiriki fainali za Afrika nchini Gabon Mei mwaka huu, yalifufua matumaini.Said aliongeza nguvu safu ya ushambuliaji wa Yanga akishirikiana na Yussuf Mhilu, Tambwe na Buswita na kupatikana mabao mawili ya haraka haraka. Kikosi cha Yanga: Youth Rostand, Juma Abdul, Gadiel Michael, Nadir Haroub, Andrew Vincent, Papy Tshishimbi, Yusuph Mhilu, Raphael Daud, Amis Tambwe, Pius Buswita na Emmanuel Martin/Said Mussa dk 69.Reha FC: Idrisa Ramadhan, Brian Khiza, Japhary Athuman, Abdul Hassan, Ambele Daud, Zuberi Makame, Rajabu Mohamed, Silvanus Sostenes/Mohamed Abdallah dk58, Bazo Sentumbi/ Mohammed Hassan dk 64, Salum Athuman na Idrisa Omary. | michezo | 2 |
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma imeanza kutekeleza mkakati wa kufufua kilimo cha pamba ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuwa na uchumi wa viwanda.Kauli hiyo ilitolewa na Ofisa Kilimo Wilaya Kasulu, Faida Misango wakati akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2019, wakati mwenge huo ulipotembelea na kukagua shamba la mfano la mkulima wa kijiji cha Makere, Malegesi Mchunga.Misango alisema kuwa baada ya kilimo cha pamba kufa kwa muda mrefu walianza mkakati wa kufufua zao hilo mwaka 2016 ambapo walianza na wakulima 81 na kwamba kwa miaka hii miwili tayari wakulima 1,620 wameanza kulima pamba kwenye mashamba yenye ukubwa wa ekari 2,310.Ofisa kilimo huyo wa Wilaya ya Kasulu alisema kuwa hadi sasa tayari kata 14 na vijiji 21 vimeanza kutekeleza mpango huo wa kufufua kilimo cha zao la pamba wilayani Kasulu.Akizungumza baada ya kutembelea na kukagua shamba hilo la mfano la mkulima wa pamba katika kijiji cha Makere wilaya Kasulu, kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru, Mzee Alli Mkongea alisema kuwa kilimo cha mazao ya biashara yanayotoa malighafi za viwandani ndiyo mpango wa serikali katika kusimamia viwanda.Alisema kuwa mpango huo unatoa uhakika wa upatikanaji wa masoko kwa wakulima hivyo kusaidia kuongeza uchumi wa wakulima wadogo wadogo.Moja wa wananchi wa kijiji cha Makere, Mchunga ambaye alikuwa mkulima wa pamba miaka mingi iliyopita na kuacha, amesema kuwa ameamua kurudia kulima pamba baada ya serikali kuweka mazingira mazuri ya kilimo na soko.Mchunga alisema msimu uliopita alianza kulima tena pamba msimu uliopita na msimu huu tayari ameshalima ekari nne ambazo ana uhakika wa kuingiza milioni 4.1 kama hatapatwa na majanga ya hali ya hewa au wadudu waharibifu. | Biashara | 1 |
Katika kipindi cha zaidi ya miongo mitano, mdada huyo amecheza zaidi ya filamu 150, zikiwemo zile kali kama Mr India, Chandni, ChaalBaaz na Sadma.Alikuwa akichukuliwa kama mmoja wa wanawake wachache wa Kihindi ambao wamepata mafanikio makubwa katika filamu bila kuwategemea mashujaa wakiume.Tangu akiwa na umri wa miaka minne, alikuwa akicheza filamu huko Tamil, Telugu, Malayalam, Kannada na Hindi.Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi alitwiti kuwa ameshtushwa na kifo hicho cha nyota huyo wa filamu nchini India, wakati Rais wa India, Ram Nath Kovind aliandika kuwa “Mshtuko”. Meya wa London, Sadiq Khan alitoa salamu za rambirambi kwa nyota huyo, akiandika katika Twitter:"Kwa kweli nilifurahia sana nilipokutana na nyota wa Bollywood Sri Devi wakati nilipotembelea India hivi karibuni."Ni huzuni kubwa kusikia taarifa za kifo cha msanii nyota kama huyo mwenye kipaji cha hali ya juu, katika uigizaji na utengenezaji wa filamu.”Msanii huyo alikuwa Umoja wa Falme za Kiarabu, ambako alikuwa akihudhuria sherehe za harusi za binamu yake, Mohit Marwah.Mume wa Sridevi, Boney Kapoor na mtoto wao wa kike, Khushi walikuwa pamoja naye wakati akiaga dunia Jumamosi, taarifa hizo zilisema. Shemeji yake, Sanjay Kapoor alisema kifo hicho kilitokea kama majira ya saa 5:00 usiku. | michezo | 2 |
RAIS John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na wakuu wa mikoa na makatibu Tawala wote wa Tanzania Bara, Ikulu Jijini Dar es Salaam.Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa ilisema Rais Magufuli na viongozi hao wa mikoa walikutana jana na wamezungumza masuala mbalimbali yanayohusu utendaji kazi wa serikali mikoani, hususani usimamizi wa shughuli za maendeleo na utoaji wa huduma kwa wananchi.Kikao hicho kilihudhuriwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo. | Kitaifa | 0 |
['Barcelona huenda ikamjumuisha mshambulizi wa kimataifa wa Ufaransa wa miaka 28, Antoine Griezmann katika mkataba wa kumsajili tena mshambuliaji nyota wa Brazil Neymar, 27, kutoka Paris Saint-Germain msimu ujao. (Le10Sport - in French)', 'Chelsea inamatumaini kuwa mlinzi wake Fikayo Tomori, 21, na mshambuliaji Tammy Abraham, 22, watasaini mkataba mpya wiki chache zijazo. ', "Wachezaji hao wawili wamejumuishwa katika kikosi England cha kufuzu kwa kintang'anyuro cha Euro 2020 baadae mwezi huu. (Standard)", 'Chelsea pia inakaribia kufanya mazungumzo ya wazi ya mkataba na mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil wa miaka 31- Willian, ambaye mkataba wake wa sasa unakamilika mwisho wa msimu huu. (Express)', 'Manchester City haina mpango wa kumsaini kiungo wa kati wa Norway aliye na umri wa miaka 20 Martin Odegaard, ambaye yuko Real Sociedad kwa mkopo kugoka Real Madrid. (Manchester Evening News)', 'Kocha wa Everton Marco Silva amesema mchezaji wa safu ya mashambulizi ya England ya wachezaji wa chini ya miaka-19 -Anthony Gordon, 18, anakaribia kujiunga na kikosi cha kwanza cha timu hiyo. (Liverpool Echo)', "Manchester United inafuatilia kwa karibu mchezo wa mshambuliaji wa Klabu ya Leon wa miaka 20 Mmexico Jose Juan Macias, ambaye amebatizwa jina la 'Javier Hernandez wa baadae'. (Marca via Express)", 'West Ham inamnyatia kiungo wa kati wa miaka 20 raia wa Bolivia, Daniel Camacho, ambaye anachezea klabu ya nyumbani ya Aurora. (Diez via Sport Witness)', 'Real Madrid inapania kumuajiri meneja wa zamani wa Chelsea Antonio Conte kama kocha wao mpya baada ya kumfuta kazi Julen LuLutetiu mwaka jana lakini uamuzi huo ukabatilishwa kufuatia ushauri wa nahodha Sergio Ramos.(Fichajes.net via Mail)', 'Manchester United inamsaka mshambuliaji wa Urusi wa miaka 20 Aleksandr Sobolev, nayechezea klabu ya PFC Krylia Sovetov Samara inayoshiriki Ligi Kuu ya Urusi. (Mirror)', 'Kocha wa Anderlecht, Vincent Kompany anamlenga mlinzi wa Wales Ashley Williams,35, mkataba wake na Bristol City utakapokamilika mwezi Januari. (Sun)', 'Kiongo wa safu ya mashambulizi ya Croatia, Mario Mandzukic, 33, anayelengwa na Manchester United nu miongoni mwa wachezaji watatu watakaouzwa na Juventus mwezi January. (Calciomercato - in Italian)', 'Mlinzi wa zamani wa Tottenham na Arsenal Sol Campbell na mshambuliaji wa zamani wa Celtic na Barcelona Henrik Larsson wamehojiwa kuchukua wadhifa wa meneja wa Southend. (Sky Sports)', 'Stakabadhi iliyovujishwa umefichua kiwango cha faini Real Madrid inayowatoza Inawatoza wachezaji wake kwa kukiuka sheria kama vile kuchelewa kufika kwa mazoezi nakutumia simu wakiwa katika basi la timu au chumba cha kubadilisha mavazi. (Marca)', 'Kocha wa zamani wa England Fabio Capello amefichua kuwa alijaribu kumsajili nyota wa Barcelona Lionel Messi kwa mkopo kipindi akiinoa timu ya Juventus. (Sky Sports Italia via Mail)', 'Kocha wa Arsenal Unai Emery amegoma kukanusha uwezekano wa kiungo Mesut Ozil kuihama klabu hiyo mwezi Januari. (Sun) ', 'Kiungo nyota wa Tottenham Christian Eriksen bado anaamini mipango yake ya kuhamia Real Madrid inaweza kufanikiwa, na wakala wake mwishoni mwa wiki hii anatarajiwa kwenda Uhispania kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Madrid. (Star)', 'Mchezaji wa Callum Wilson, 27, wa Bournemouth yupo katika rada ya usajili wa klabu ya Manchester United ambao wanatafuta kwa nguvu zote mshambuliaji wa kusajili katika dirisha dogo la mwezi Januari. (Sky Sports)', 'Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Lukas Podolski ametoa kauli ya kebehi kwa wapinzani wake wa zamani Tottenham kwa kusema kuwa Serge Gnabry inabidi awe mchezaji bora wa mwezi wa Arsenal. ', 'Gnabry ambaye amewahi kuichea Arsenal alifunga goli nne peke yake wakaqti Bayern ikiidondoshea Spurs goli 7-2 wiki hii. '] | michezo | 2 |
KATIKA kutatua migogoro ya ardhi, Jiji la Dodoma limeanzisha programu maalumu ya kutoa viwanja vya makazi bure kwa wananchi waliojenga kwenye maeneo yaliyotengwa kwa shughuli za umma, ili kuwezesha kuondoka katika maeneo hayo.Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, aliliambia Baraza la Madiwani jana kuwa programu hiyo itasaidia kutatua changamoto ya migogoro ya ardhi ambayo wameirithi kutoka iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu(CDA). “Mpaka sasa, tumetenga viwanja vipya 1,170 katika eneo la Kata ya Ipagala kwa wananchi ambavyo vitakuwa na maeneo ya wazi, barabara za mitaani na ardhi kwa ajili ya kujenga taasisi za umma, lengo ni kuwaondoa katika maeneo yaliyokuwa kwa matumizi ya umma,” alisema.Akifafanua zaidi, Kunambi alisema wananchi ambao watakuwa kwenye mpango huo wa kupewa viwanja bure kwa ajili ya makazi, watatakiwa kulipa ada ya kisheria kwa Jiji na kuwa mamlaka zitathibitisha majina ya wananchi hao. Aidha, Kunambi alisema Jiji pia limeanza kupima viwanja vipya vya makazi maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dodoma katika maeneo ya Hombolo, Iyumbu, Kikombo na Nzuguni. “Wananchi wa Dodoma kwa sasa anaweza kumiliki kiwanja cha makazi kwa Sh 900,000 ikiwa ni gharama ya chini,” alisema.Kunambi alisema Jiji limekuwa na mafaniko makubwa katika upimaji na upangaji wa miji wa kipindi cha mwaka mmoja na miezi minne na kuwa mpaka sasa mamlaka hiyo imepima viwanja kwa matumizi mbalimbali 100,000 katika maeneo mbalimbali ya jiji. Naye, Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde alilipongeza Jiji la Dodoma kwa mafanikio na mikakati iliyofanya na kusisitiza kuwa kwa sasa migogoro ya ardhi imepungua. Mavunde alitumia fursa hiyo kuwataka watendaji wa Jiji kutembelea na kusikiliza kero za wananchi ili waweze kutatua changamoto hizo ikiwamo ile ya migogoro ya ardhi. | Kitaifa | 0 |
Pia Lwandamina alisema jana Dar es Salaam wiki moja inamtosha kuandaa kikosi chake kwa msimu mpya wa ligi na Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambayo imepangwa kuanza Agosti 26 mwaka huu.Programu ya Lwandamina ilianza kwa mazoezi ya wachezaji kutanua misuli ya miili kwa wiki moja katika Gym City Mall. Juzi wachezaji waliingia hatua ya pili ya mazoezi ya uwanjani kufundishwa vitu mbalimbali ikiwemo mbinu na mifumo.Alisema kitu alichopanga kuanza nacho ni kutengeneza mfumo wa uchezaji ambao ni muhimu kuipa timu matokeo mazuri. Alisema ataiunganisha timu kiuchezaji kwani baadhi ya wachezaji ni wageni hivyo wanatakiwa kuelewana na msimu uliopita.Yanga leo wanaenda Morogoro kupiga kambi ya wiki moja kujiandaa dhidi ya Simba mechi ya Ngao ya Jamii Agosti 23. Katika kujiimarisha zaidi jana wamemsajili kipa wa Serengeti boys, Ramadhan Kabwili ambaye ataungana na makipa wengine wawili.Watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United Agosti 6 Uwanja wa Taifa. Msemaji wa Yanga, Dismas Ten alisema Lwandamina amepania kuweka rekodi hivyo anahitaji mazingira yaliyotulia. Simba wako Afrika Kusini kujiandaa na msimu tangu wiki iliyopita. | michezo | 2 |
SERIKALI imeziomba taasisi za elimu za makanisa nchini kuunga mkono juhudi za kujenga Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (TVET) nchini ili kuziba pengo la uhaba wa vyuo hivyo na kusaidia vijana wanaomaliza kidato cha nne kujifunza ufundi ili wajiajiri.Akifungua mkutano wa wakuu wa shule za sekondari chini ya mwamvuli wa Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) jijini Dodoma jana, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo alisema mafunzo hayo ya ufundi yanahitajika ili kukidhi kiu ya wahitimu kidato cha nne nchini. “Jitihada zaidi zinahitajika kukabiliana na ongezeko la uhitaji wa elimu hususani ufundi stadi, jambo linaloweza kusaidia kuingia kwa urahisi uchumi wa kati na viwanda,” alisema.Alisema mahitaji ni makubwa zaidi kwa vijana wanaohitimu shule za serikali na binafsi ili wajiendeleza katika fani za ufundi na kujiajiri. Dk Akwilapo alisema hitaji hilo la vyuo vya ufundi sasa ni kubwa kuliko kipindi chochote kwani wanaohitimu kidato cha nne wanazidi.Alipongeza taasisi hizo kwa kutoa mchango katika kuboresha utoaji wa elimu tangu ngazi ya elimu ya awali, msingi, sekondari, ufundi, mafunzo ya ualimu na elimu ya juu ambapo kwa sasa zina vituo 1,224 vya kutolea elimu nchini. Aliwapongeza kwa kuunga mkono serikali kutoa elimu kwani takwimu zinaonesha mwaka 1961 kulikuwa na shule 3,238 na mwaka huu shule za msingi zilizosajiliwa ni kama 17,704. Alisema katika elimu ya sekondari, wakati wa Uhuru mwaka 1961, zilikuwa shule 41 na sasa zipo 4,963 na kati ya hizo, 1,266 ni za binafsi. | Kitaifa | 0 |
KOCHA wa Yanga, Charles Mkwasa, amesema siku zilizosalia zinatosha kuiandaa timu yake kabla ya kuikabili Simba kwenye mechi ya Ligi Kuu Jumamosi wiki hii katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Mkwasa alisema juzi kuwa, siku hizo zinatosha kuiandaa timu yake kisaikolojia na mbinu zitakazowafanya kuibuka na ushindi kwenye mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.Kauli hiyo ya Mkwasa imekuja baada ya kuifunga Biashara United bao 1-0 katika mechi ya ligi hiyo juzi na kushika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 24. Alisema anachanga karata zake kupitia mbinu hizo, lengo likiwa ni kuwang’oa wapinzani wao hao kwenye usukani wa ligi na kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa.“Siku tatu kama kocha nadhani zinatosha kuwaandaa na kuwajenga wachezaji wangu kisaikolojia, mbinu tutakazoingia nazo kwenye mechi inayokuja dhidi ya Simba, tunahitaji sana ubingwa, naamini kwa kikosi nilichonacho najua hakuna linaloshindikana tunaenda kujipanga,” alisema.Mkwasa alisema kinachozidi kumtia nguvu kuelekea kwenye mchezo huo ni uwezo unaoneshwa na wachezaji wake kwa kupata ushindi michezo miwili mfululizo na maingizo mapya ya wachezaji waliosajiliwa kipindi hiki cha dirisha dogo lilofunguliwa Desemba 16 na likitarajiwa kufungwa Januari 15.Mkwasa alisema pamoja na tofauti waliyo nayo dhidi ya Simba, sio kigezo cha kubariki Simba kujihakikishia kutetea ubingwa na kwamba kwenye mchezo wa soka chochote kinawezekana.Alisema mchezo uliopita dhidi ya Biashara wachezaji wake hawakucheza kwa ubora aliotarajia kwa vile walichoka kutokana na ratiba ya mechi za ligi hiyo kuwa ngumu kwao kwani walipumzika siku moja wakitoka safari ya Nyanda za Juu Kusini kucheza michezo miwili ya ligi dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons.Aidha, Mkwasa amempongeza mchezaji Tariq Kiakala kwa kuanza na mguu mzuri kwa kitendo cha kuifungia timu hiyo bao pekee kwenye mechi dhidi ya Biashara. | michezo | 2 |
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa ACB, John Lwande alisema kupitia akaunti hiyo, wateja pia watarahisishiwa kufikia malengo kwa kuwa na utaratibu wa kujiwekea akiba.Alisema mteja anayejiunga na huduma hii atafungua kwa Sh 50,000, kiasi ambacho ataweza kupata faida ikiwa ni asilimia tatu ambayo itahesabiwa kila mwezi kutokana na amana yake.Lwande alisema mbali na faida hiyo, pia mteja wa ACB Golden Account atapata faida ya ziada (bonus) ya asilimia 2 kwa mwaka iwapo atakuwa hajatoa fedha au ametoa mara moja katika kipindi cha robo mwaka.Lakini pia mteja hatokuwa na gharama za uendeshaji wa akaunti za kila mwezi na pia anaweza kupata mkopo hadi asilimia 80 ya kiasi alichonacho kwenye akaunti yake, kwani amana zake ndizo zinazotumika kama dhamana ya mkopo.Naye Meneja Uendeshaji wa ACB, Juliana Swai alisema benki yake imefanya utafiti na kubaini kuwapo kwa mahitaji ya akaunti ya aina hiyo ambayo yanalenga makundi yote ya jamii. | Biashara | 1 |
Okwi, ambaye wiki iliyopita alitangazwa na Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kuwa mchezaji wa mwezi Agosti na kuzawadiwa Sh milioni moja na wadhamini wa Ligi hiyo, Vodacom, alifunga bao moja kila kipindi na la tatu likafungwa na John Bocco.Alifunga bao la kwanza katika dakika ya saba baada ya kupiga mkwaju mkali uliomgonga beki na kujaa wavuni baada ya kupokea pasi ya Shiza Kichuya aliyegongeana naye vizuri. Mshambuliaji huyo mhenga raia wa Uganda aliongeza bao la pili dakika ya 67 baada ya kuchukua mpira na kutisha kama anapiga kisha akaachia mkwaju mkali na kufunga.Dakika tano baadaye, dakika ya 72, Bocco alimchambua beki wa Mwadui FC na kufunga bao safi la tatu kwa Simba na la kwanza kwake katika ligi msimu huu. Bocco alifunga bao hilo dakika mbili tu baada ya Okwi kupiga mpira wa adhabu uliotoka sentimeta chache nje.Kwa ushindi huo, Simba sasa imefikisha pointi saba sawa na Azam FC iliyokuwa ya pili kwenye msimamo nyuma ya Mtibwa Sugar inayoongoza kwa pointi tisa hadi jana. Simba imeiengua Azam FC katika nafasi ya pili kwa kuwa ina magoli 10 ya kufunga na haijafungwa bao katika mechi tatu ilizocheza dhidi ya Azam, Mwadui na Ruvu Shooting ambayo ilifungua nayo dimba na kuishinda 7-0.Pamoja na kufungwa, Mwadui FC walitoa upinzani kwa Simba na mara kadhaa walifanikiwa kuonesha makali yao. Mwadui FC ndio walikuwa wa kwanza kufika langoni mwa Simba lakini shuti lililopigwa na mchezaji lilipita juu. Timu zote zilishambuliana kwa zamu hadi dakika ya 16, Okwi alipopiga mkwaju wa faulo lakini mpira ukapita juu.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Simba wakionekana kupania kupata bao la pili kujihakikishia ushindi. Dakika ya 48, Okwi aliambaa vizuri na mpira pembeni na kutoa krosi nzuri lakini Ndeule akaokoa. Okwi alirudi tena dakika tatu baadaye akiwa amebaki na kipa Massawe akapiga juu.Katika dakika ya 54, Simba waligongeana vizuri lakini Bocco aliyekuwa wa mwisho kumalizia akaachia mkwaju ukatolewa kona iliyochongwa na Kichuya ikaokolewa. Dakika mbili kabla ya hapo, Mwadui walimpima kipa wa Simba, Aishi Manula akaruka juu kudaka krosi ya Ndeule.Mwadui walijaribu bahati yao tena dakika ya 56 na kupata kona lakini Manula akada kwa ustadi na dakika ya 58, Mbonde aliruka na kuondosha mpira hatarini. Katika kuongeza nguvu, Simba ilifanya mabadiliko dakika ya 60 kwa kumwingiza Mwinyi Kazimoto na kumtoa Gyan | michezo | 2 |
YANGA imeendeleza wimbi la ushindi kwenye Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, baada ya jana kuifunga Ruvu Shooting mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 44 baada ya kucheza michezo 16. Azam inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 40 kwa michezo 16 na Simba inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 27 baada ya kucheza michezo 12.Shujaa wa Yanga kwenye mchezo wa jana alikuwa mshambuliaji Heritier Makambo aliyefunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Ibrahim Ajib dakika za nyongeza za mchezo huo.Yanga walitangulia kufunga kwa bao la Amis Tambwe dakika ya 11 akimalizia mpira hafifu uliopigwa na Heritier Makambo aliyepata krosi nzuri ya Paul Godfrey. Ruvu Shooting walisawazisha kupitia kwa Fully Zulu Maganga dakika ya 31.Feisal Salum aliifungia Yanga bao la pili dakika ya 78 kwa shuti kali nje ya eneo la penalti na kumshinda kipa wa Ruvu, Abdallah Rashid. Said Dilunga aliifungia Ruvu Shooting bao la penalti dakika ya 83 baada ya Amis Tambwe kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.Huku ikidhaniwa mchezo huo ungemalizika kwa sare, Heritier Makambo alifunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Ibrahim Ajib baada ya beki Paul Godfrey kufanyiwa madhambi nje kidogo ya eneo la hatari. | michezo | 2 |
Huku TIPER ikiwa na mpango wa kupanua hifadhi ya mafuta kufikia mita za ujazo 315,000 za mafuta ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Charles Mwijage alisema hayo jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Kisangi (CCM) aliyetaka kufahamu serikali imepata faida gani kutokana na uwekezaji katika kampuni hiyo.Pia alihoji kwa nini mpaka sasa hakuna uendelezaji mkubwa katika eneo la TIPER, na lini uboreshaji wa mazingira ya TIPER utakamilika.Akijibu swali hilo, Mwijage alisema serikali inaendelea kunufaika na uwekezaji wa TIPER kwa kupata hifadhi kubwa ya mafuta kwa ajili ya soko la ndani na nje kwa kuweza kupata gawio la Sh bilioni 4.4 kwa kipindi cha miaka mitano.Alisema hifadhi ya TIPER ina uwezo wa kuhifadhi mita za ujazo 141,000 za mafuta yaliyosafishwa, huku ikifanya ukarabati wa matangi yenye mita za ujazo wa 72,000 na kufanya hifadhi hiyo kuwa na jumla ya mita za ujazo 213,000 za mafuta ukarabati utakapokamilika.Mwijage alisema kwa sasa kampuni hiyo ipo katika mpango wa kupata fedha kwa ukarabati, ikiwa ni pamoja na kupanua hifadhi hiyo mpaka kufikia uwezo wa mita za ujazo 315,000 ifikapo mwisho wa mwaka huu.“kampuni hiyo inaendelea kuboresha mazingira ya eneo hilo hatua kwa hatua kwa kuodnoa miundombinu iliyochakaa na kurejesha ama kujenga miundombinu mipya pale inapobidi huku shughuli zote zikiendeshwa kwa kuzingatia usalama wa afya za wafanyakazi na mazingira,” alisema. | Biashara | 1 |
SIMBA ina watu bwana! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kuhitimisha tamasha lake la Simba day kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.Mbali na mashabiki waliojaa ndani na nje ya uwanja wa Taifa, lakini kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wa kikosi hicho ilikuwa burudani tosha kwa mashabiki wake waliojazana uwanjani hapo wakiongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Meddie Kagere ndio shujaa wa jana baada ya kufunga mabao yote matatu katika mechi hiyo iliyokuwa ya kasi muda wote.Mkongwe huyo aliendeleza makali yake kwa kuandika bao la kuongoza katika dakika ya tatu ya mchezo baada ya mabeki wa Dynamos kujichanganya kabla Power Dynamo haijasawazisha kwa kichwa kupitia kwa Jimmy Dlingai. Simba walitala mpira katika dakika takriban 20 za kipindi cha kwanza kabla wapinzani wao kubadilika na kushambuliana kwa zamu.Kagere ambaye msimu uliopita aliondoka na kiatu cha dhahabu kwenye Ligi Kuu Bara alifunga bao la pili katika dakika ya 59 akiunganisha krosi safi ya Deo Kanda. Mnyarwanda huyo alifunga bao la tatu katika dakika ya 74 akiunganisha mpira wa kona wa Miraji Athumani. Kocha wa Simba, Patrick Aussems alijaribu kutumia wachezaji wake karibu wote na hawakumuangusha kwani wote waliopewa nafasi iwe wapya ama wa zamani walionyesha kiwango kikubwa.Tamasha hilo lilianza mapema saa tano asubihi na ilipofika saa tisa alasiri iliamuliwa mashabiki wasiingie tena baada ya uwanja kujaa, hivyo kuishia nje. Shughuli rasmi ilianza saa 11 kasoro jioni baada ya msemaji wa Simba, Haji Manara kuingia kwa mlango wa pembeni wanapokaa mashabiki wa Simba akiwa na mabaunsa wawili ambapo alizungumza uwanja kusalimia mashabiki kabla ya kuanza kutambulisha benchi la ufundi na baadae wachezaji.Katika utambulisho huo pia msemaji huyo mwenye maneno mengi alimtambulisha mwekezaji wa timu hiyo Mohamed ‘Mo’ Dewji ambaye aliingia kwa shangwe kubwa pia na kuzunguka uwanja kusalimia mashabiki kabla ya kusalimia benchi la ufundi na wachezaji kisha akamalizia kwa kupiga mpira pasi mbili tatu. Kikosi cha Simba: Beno Kakolanya, Mohammed Hussein, Shomari Kapombe/ Hamis Ndemla, Wilker Da Silva, Paschal Wawa, Mzamiru Yassin, Deo Kanda/ Rashid Juma, Sharaf Shiboub/ Gerson Vieira, Meddie Kagere, Clatous Chama, Francis Kahata/ Miraji Athumani. | michezo | 2 |
BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) limesema litavifutia usajili vyama vyote vya michezo vilivyoshindwa kukidhi vigezo na sifa zilizowekwa kuendesha shughuli zao.Mwenyekiti wa BMT, Leodegar Tenga amesema jijini Dar es Salaam kuwa, sifa za vyama vya kitaifa ni pamoja na kuwa na ofisi inayotambulika, akaunti ya benki na mipango yao ya maendeleo.Amewaeleza waandishi wa habari kuwa, endapo chama kitakosa vitu hivyo, kitapoteza sifa ya kuwa cha kitaifa kinachotambulika.“Huwezi kuwa na chama cha kitaifa hakina ofisi, akaunti ya benki, hakina mipango wala hakitoi taarifa zozote za matumizi na mahesabu, wanatakiwa wafanye kazi zao kwa mujibu wa katiba,” amesema.Tenga aliyewahi kuwa Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) alizungumzia mikakati yao katika maendeleo ya kimichezo kuwa ni kufanya tathmini ya hali halisi ya michezo nchini.Pia, alisema wataendelea kufanya mapitio ya sera na sheria ya michezo iliyoundwa na BMT ili iendane na hali halisi, kufanya mikutano na wadau, kutoa mafunzo ya utawala bora, kuhamasisha ujenzi wa miundombinu na kuhakikisha vyama vya michezo vinaheshimu katiba zao.Aidha, Tenga alizungumzia umuhimu wa vyama vya michezo kushiriki katika shughuli za kijamii kama kusaidia kampeni za kitaifa za chanjo kwa watoto, kupambana na Ukimwi, kutokomeza malaria na kupiga vita dawa za kulevya.Aligusia pia suala la migogoro katika vyama mbalimbali vya michezo na mashirikisho na kuvitaka kuzingatia katiba zao kutafuta haki na kutatua changamoto hiyo.“Migogoro ni sumu ya maendeleo ya michezo kwa hiyo ni wajibu wetu tuondokane nayo ili kuwavutia mashabiki, wadhamini na washirika wengine tunaowahitaji kwa maendeleo ya michezo,” alisema. | michezo | 2 |
MAKALA haya yatazungumzia kidogo matatizo yanayojitokeza katika utumiaji wa lugha ya Kiswahili. Tukumbuke kuwa lugha ni chombo chetu cha mawasiliano na tunapaswa kuipiga msasa mara kwa mara kadiri inavyowezekana.Yapo makosa mengi na mengine yameshawahi kuzungumziwa lakini leo tutayataja machache hata kama tutakuwa tunarudia, kwa lengo la kuweka msisitizo tu. Katika makala haya tutazungumzia zaidi makosa ya mara kwa mara ambayo tukiyaacha yanaweza kuleta mkanganyiko kwa watumiaji wa lugha hii.Yapo maneno mengi ambayo hukosewa mara kwa mara, yapo yanayochanganywa matumizi, na yapo ambayo waandishi huyatumia bila kujua. Mfano wa makosa hayo ni yale ya kuchanganya umoja na wingi kwa baadhi ya msamiati.Makosa ya aina hii hujitokeza, kwa maneno yaliyo katika mfumo wa wingi katika uundaji wake, wengi wetu huyalazimisha yawe na mfumo wa umoja. Tuangalie maneno kama vile madhumuni, madhehebu, mafao, maadhura n.k.Umbo la maneno haya ni la wingi na hayapaswi kuingizwa katika umoja. Hivyo si sahihi kutumia neno ‘dhumuni’, ‘dhehebu’, ‘fao’, ‘adhura’ n.k. Aidha, yapo maneno yenye mfumo wa umoja ambayo baadhi yetu tunayabebesha wingi kwa lazima.Kwa mfano: neno ‘saa’ ‘dawa’, ‘shule’ ‘uamuzi’. Haya ni baadhi tu. Pia, kuna makosa mengine ya mara kwa mara ambayo baadhi ya waandishi huongeza kiambishi cha awali ‘ma’ katika maneno kuonesha msisitizo au wingi, kama vile mashirikiano, mashule, makampuni, mahusiano na kadhalika. Matumizi sahihi ya maneno haya ni ushirikiano, shule, kampuni na uhusiano.Aidha, kuna ukataji wa maneno usioleta maana iliyokusudiwa. kwa mfano, unapiga simu toka wapi badala ya unapiga simu kutoka wapi, tafsiri sisisi kutoka katika lugha nyingine kwa mfano, mwisho wa siku badala ya “hatimaye” au “mwishowe”.Kuna makosa yanayokuzwa na waandishi, haya mara nyingi huwa yanabebwa kutoka katika jamii ya wazungumzaji ambao ni wamiliki wa lugha yao, kuna maneno ambayo huwa ni simo au yaliyotoholewa bila kufuata misingi ya lugha.Makosa haya huwa yanarekebishika lakini athari zake huwa katika taarifa ambazo labda zimehifadhiwa kwa maana ya kurekodiwa au kuandikwa. Makosa hayo huonekana dhahiri wakati wa kurejea kipindi kirefu kilichopita tangu matumizi ya msamiati huo. Matumizi potofu: Kizazi cha sasa kimeibua dhana ya mfanano wa matendo, na matendo hasi zaidi, kuna upotoshaji ambao umekithiri katika jamii na kunyang’anya msamiati kwa waandishi kwa hofu kwamba akiliandika atamaanisha maana mbaya.Yaani msamiati wa kawaida umeingia shubiri, ni vigumu kwetu waandishi kutumia maneno kama kutia, kukazana, kusimika, denda, ingiza, chomeka, chomoa, jicho, ndogo, kulamba, mzigo, mate, kugonga au kugongwa. Makosa ya kiuandishi, Jamii ya wasomaji hufanya marejeo mengi kutoka katika maandiko, hivyo inapandwa mbegu ambayo hatuijui ukubwa wake na athari zake.Uundaji wa msamiati kama live, prodyuza, tyuni, nimekumisi, inaweza ikawa na nguvu badala ya mubashara, mtozi, kurahani, na nimekuhamu. Kuna maneno mengine ya Kiingereza ambayo watu wamejenga imani kwamba hayana msamiati wake katika Kiswahili, kama birthdaysiku ya kuzaliwa, surprisekushitukiza, booking- wekesho, appointment- miadi weekend-mwisho wa wiki/ juma. Tanzania ina makabila mengi sana. Inakadiriwa kuwa yapo makabila zaidi ya 120, makabila haya yana athari kubwa katika lugha ya Kiswahili.Unaweza kutambua asili ya mtu kwa lafudhi yake. Isivyo bahati ni kwamba hakuna tena kabila la Waswahili ambalo labda lingepewa jukumu la kuwa waandishi kutokana na lafudhi murua ya Kiswahili. Waandishi tumejikuta tukitumia lafudhi za makabila yetu, baadhi ya maneno ya Kiswahili yanayokinzana sana na makabila yetu.Kuna makabila hawana /r/ katika matamshi yao, unapomlazimisha kutamka neno lenye r anatamka l, wengine hawana z na badala yape hutumia s, wengine f badala ya v. Lakini pia kuna kushadidia neno kwa kuongeza ga kama kulimaga, kulaga, kusimikaga, kukimbiaga, na kadhalika. Haya ni matatizo ya lafudhi na siyo lahaja. Matatizo yaliyo katika lahaja yanatatulika kiurahisi kwa kuwa kila lahaja ina namna ya kumeza msamiati wake na hakuna makosa ya kuubadilisha msamiati tofauti na lafudhi ambayo hujenga msamiati mpya potofu unaokaribiana na msamiati sanifu.Kwa mfano: luga, singo, langi, ledio, kasa, hombi, akuna, ongera, n.k. Makosa ya kurithi, pamoja na kwamba sisi ni mahiri katika lugha ya Kiswahili na ndio maana tumepewa jukumu la kuwa waandishi, kuna makosa mengi sana ya kurithi ambayo tumeyapata na tumeyapokea, mengine kwa kulazimishwa na wanaojiita wakongwe katika tasnia na mengine yapo kwa kuwa tumeyakuta. Maneno kama vile pelekea, sintofahamu na kadhalika. Aidha, ni dhahiri kwamba upo msamiati wa kimahalia. Misamiati ya aina hii inatokana na dhana na hii inaweza kuwa inazaliwa kila siku kutokana na mazingira ya maisha tunayoishi. Hivi leo, nchi hii ina maeneo mengi sana yanayojulikana kama chekereni.Chekereni limetokana na maneno ya Kiingereza kwa maana ya check rail yaani kuwa mwangalifu/angalia reli. Mfano mwingine ni neno mlimani kwa maana ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Neno Mlimani likitamkwa peke yake kwa maana ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam halina ubishi kuwa linafahamika lakini kuna vyuo vikuu vingapi nchini ambavyo havinasibishwi na mlimani. Uundaji wa maneno kwa namna hii huwa yana historia yake na hupata mashiko makubwa katika matumizi. Ufumbuzi ni kwamba tukiwa waandishi tunapaswa kujifunza mara kwa mara, kununua machapisho, kufanya rejea, kuwasiliana na Baraza pale kunapotokea mgongano katika matumizi ya Kiswahili fasaha. | Kitaifa | 0 |
Kauli hiyo ya Serikali ilitolewa jana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa anafungua mkutano wa kila mwaka wa wadau wa korosho uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Mipango, mjini Dodoma.Alisema nia ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha vikwazo vyote vilivyokuwa vinawakabili wakulima wa zao hilo vinaondolewa ili kuwawezesha kupata tija zaidi kutokana na zao lao.“Mheshimiwa waziri wa kilimo mifugo na uvuvi, hebu sema lile tuliloazimia kuhusu pembejeo kuanzia msimu wa mwaka huu… tunataka wajumbe wa mkutano huu muhimu wajue nini sisi kama serikali tumekubaliana”, alisema Majaliwa huku akimwinua waziri huyo kutoa kauli ya serikali kwa niaba yake.Alisema lengo la Serikali ni kuona mashamba yaliyotelekezwa na yenye mikorosho iliyozeeka yanafufuliwa ili kuongeza uzalishaji na kukuza uchumi wa wakulima na nchi kujipatia kipato cha kutosha.“Mikorosho asilimia 25 iliyopo sasa ni ile iliyozeeka ambayo haizalishi kiasi cha kuridhisha…lakini pia kuna mashamba yaliyotelekezwa kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukosa mitaji kwa ajili ya kununua pembejeo,hivyo basi kwa hatua hii tunatarajia yatafufuliwa”, alisema Majaliwa huku akishangiliwa na wadau hao.Awali akitoa taarifa kwa mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Nchini (CBT), Anna Abdallah, alisema bodi hiyo imenunua tani 18,000 za pembejeo aina ya Salfa ambayo inatumika kudhibiti na kutibu ugonjwa wa ubwiriunga unaowasumbua wakulima wa zao hilo.Alisema kiasi hicho ni sawa na asilimia 95 ya pembejeo zote zilizoagizwa kwa msimu huu wa kilimo, ambapo pembejeo nyingine ni pamoja na dawa za maji za kunyunyizia na mabomba ya kupulizia na jumla ya Sh bilioni 43.5 zitatumika katika kununua, kusambaza na malipo ya mawakala.“Mwaka huu tutafikisha pembejeo za ruzuku hadi wilayani badala ya ule mfumo wa miaka yote wa kuwa na vituo vichache…na tayari tumeshapokea pembejeo zote tunasubiri muda muafaka tuanze kusambaza kwa wakulima,” alisema Anna.Akitoa taarifa za mapato yatokanayo na mazao ya biashara, Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ushirika, Dk Charles Tizeba alisema korosho imeongoza kwa kuliingizia taifa fedha za kigeni kutokana na mauzo ya zao hilo nje ya nchi katika msimu uliopita.Tizeba alisema jumla ya dola za kimarekani milioni 300.46 (sh bilioni 630.9)n zilipatikana kutokana na mauzo hayo na hivyo kuongoza na kufuatiwa na zao la tumbaku, katika msimu huo tani 260,000 zilikusanywa na kuuzwa kwa mnada kwa wanunuzi wa ndani na nje ya nchi.Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa amewaonya watendaji wa serikali na viongozi wa vyama vya ushirika wanaoshirikiana na wafanyabiashara wasio waaminifu kununua korosho nje ya mfumo wa ununuzi wa stakabadhi ghalani (kangomba) na kwamba ikibainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.Alisema serikali kuanzia msimu uliopita imefanya mazungumzo na wanunuzi wakubwa kutoka nchi mbalimbali ili kuja nchini kununua korosho badala ya kutegemea wafanyabiashara kutoka India pekee kama ilivyozoeleka na matokeo ni kupanda kwa bei ambapo ilifikia hadi Sh 4,000 kwa kilo. | Biashara | 1 |
Awamu ya kwanza ya mradi huo ilizinduliwa Mei 2015, ukiwa na lengo la kuwawezesha vijana kwa kuwapatia mbinu mbalimbali za biashara na vifaa vitakavyowawezesha kukuza biashara zao.Mavunde alisema: “Nchi yetu ya Tanzania imebarikiwa kwa kuwa na rasilimali zikiunganishwa pamoja na fursa zinazoletwa na miradi kama hii ya Airtel Fursa ni wazi vijana wenye malengo dhahiri ya kujiendeleza wataweza kuboresha maisha yao.’ Aidha aliwaasa vijana kutumia fursa hiyo kufanya kazi kwa bidii.Katika uzinduzi huo, Naibu Waziri huyo alisema Serikali chini ya wizara yake ataendelea kushirikiana na Airtel na kufanya kazi kwa kuweka mazingira bora yatakayochochea vijana kupata fursa ya kuchangia kuendeleza uchumi.Akizungumza kumkaribisha Naibu Waziri, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Sunil Colaso, alisisitiza dhamira ya kampuni yake kuwawezesha vijana na kutambua mchango walio nao katika kuendesha uchumi wa Tanzania.Mradi huu wa Airtel Fursa unadhihirisha dhamira yetu ya kuwawezesha vijana wa kitanzania wenye malengo ya kuinua maisha yao na kutimiza ndoto zao, alisema Colaso.Alisema msimu wa kwanza wa Airtel Fursa umetoa matokeo mazuri na umefanikiwa kugusa maisha ya maelfu ya vijana wengi kutoka katika mikoa mbalimbali nchini.Aidha alisema katika msimu huu wa pili watawekeza takribani Sh bilioni moja ili kuweza kuwafikia vijana wengi zaidi ambao wako tayari kutumia fursa na vipaji vyao.Katika msimu wa kwanza wa Airtel Fursa vijana zaidi ya 2,500 wenye umri kati ya miaka 18 hadi 24 walipatiwa mafunzo ya biashara na wengine 13 wafanyabiashara chipukizi wanaofanya vizuri zaidi kupokea vifaa vilivyowasaidia kuboresha biashara zao na kutengeneza fursa zaidi kwa jamii inayowazunguka Airtel Fursa ni mradi endelevu unaowalenga vijana nchi nzima kwa kuwapatia vifaa, mafunzo ya biashara na mafunzo mbalimbali kupitia mtandao ili kufikia malengo yao.Kutuma maombi vijana wameshauriwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15626 ikiwa na Jina, umri, aina ya biashara unayoifanya, mahali na namba za simu. | Biashara | 1 |
MWANACHUO wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Anna Mwaisumo (23) na mpenzi wake, Samson Kisuguta (28), wamefi kishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka manne likiwemo la kulawiti na kuchapisha picha za ngono kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp.Mwaisomo ambaye makazi yake ni kwenye Hosteli za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) huku Kisuguta akiishi mkazi wa Msasani na mfanyabiashara, walifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Salim Ally. Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono akisaidiana na Janeth Magohe alidai washitakiwa hao walitenda makosa hayo kati ya mwaka 2017 na mwaka huu maeneo ya Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam.Magohe alidai katika mashitaka ya kwanza kuwa, washitakiwa wote kwa pamoja katika tarehe na mahali kusikofahamika mwaka jana, ndani ya jiji hilo, walikula njama kutenda kosa la kulawiti, kuchapisha picha za ngono na kulazimisha kupata fedha ili kutochapisha picha hizo. Alidai katika mashitaka ya pili kuwa, Desemba 10, mwaka jana maeneo ya nyumba ya kulala wageni ya Morgan maeneo ya Msasani wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Kisuguta alimlawiti kinyume cha maumbile mwanafunzi anaesoma katika moja ya vyuo hapa nchini.Katika mashitaka ya tatu, inadaiwa Oktoba 7, mwaka huu ndani ya jiji hilo, Mwaisomo pamoja na Kisuguta walichapisha picha za ngono kupitia ukurasa wa WhatsApp kinyume cha sheria. Pia alidai Novemba 13, mwaka huu, ndani ya jiji hilo, washitakiwa hao walimlazimisha mlalamikaji huyo kutoa fedha taslimu Sh 250,000 ili wasichapishe picha hizo. Washitakiwa hao walikana mashitaka na upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika hivyo waliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.Hakimu Ally alitaja masharti ya dhamana kuwa kila mshitakiwa atatakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho kutoa serikali za mitaa watakaosaini bondi ya Sh 500,000 kila mmoja. Hata hivyo, washitakiwa hao walikosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza masharti hayo na kurudishwa rumande hadi Januari 3, mwaka huu kesi itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.Inadaiwa kuwa Mwaisumo alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mlalamikaji huyo wakati wakisoma sekondari ya juu na baada ya kuchaguliwa kujiunga na vyuo tofauti hawakuwa na mahusiano mazuri.Inadaiwa baadaye mwanamke huyo (Mwaisumo) alimtafuta mlalamikaji na kutaka waonane ndipo walikutania kwenye nyumba ya kulala wageni, lakini baadaye wakati wakiwa huko, mwanamke huyo alitoka na kuingia tena na mwanamume mwingine ambaye ni Kisuguta. Hata hivyo, baada ya Kisuguta kuingia chumbani, alimlawiti kinyume cha maumbile mlalamikaji huku wakichukua video na baadaye walitumia picha hizo kulazimisha kupewa fedha na mlalamikaji ili wasizichapishe kwenye mitandao ya kijamii. | Kitaifa | 0 |
MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Dk Tito Mwinuka amezindua rasmi ofi si mpya ya Dodoma na kubainisha kuwa makao makuu ya shirika hilo sasa yamehamia rasmi Dodoma.Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokewa katika ofisi za Tanesco, Dk Mwinuka alisema kuanzia sasa shughuli zote zitafanyika kuanzia Dodoma na huduma zote za kiofisi zitaendelea kama kawaida katika kanda saba, mikoa 29 ya Kitanesco na Wilayani.Alisema uwepo wa serikali Dodoma huku makao makuu ya Shirika hilo yakiwa Jijini Dar es Salaam ufanisi wa kazi unaweza kuwa si mzuri. “Tukiwa Dodoma ufanisi wetu utakuwa ni mzuri, natumaini tutatoa huduma bora zaidi kwa wananchi,” alisema.Alisema ujio wa serikali Dodoma utasababisha ujenzi wa majengo mengi yakiwemo ya serikali na huduma ya umeme itahitajika sana. Dk Mwinuka alisema katika awamu ya kwanza, watumishi 30 wameshafika Dodoma kutoka makao makuu Dar es Salaam. “Tutajenga jengo jipya hapa Dodoma ambalo litawapokea watu wote watahaohamia Dodoma,” alisema.Alisema jengo hilo jipya litajengwa na bajeti yake itatengwa mwaka ujao wa fedha na sasa kinachofanyika ni matayarisho ya mwanzo fedha zitakapokuja. Wakati huo huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano, January Makamba jana alikagua eneo litakapojengwa ofisi za wizara hizo huku akibainisha kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itakuwa na ofisi zake kwenye makao makuu ya serikali. Akizungumza katika mji wa serikali eneo la Mtumba alisema ofisi yake ina ekari nane kwa ajili ya ujenzi wa ofisi.Alisema wataanza na ujenzi wa jengo dogo la muda ili likikamilika watumishi wahamie. “Rais ametoa fedha kwa kila Wizara, tuko kwenye mchakato kwa kumpata mjenzi, ikiwemo wakala wa serikali na vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo Suma JKT,” alisema.Alisema Ofisi ya Makamu wa Rais ni ofisi ya pili kubwa kiserikali lazima waoneshe dhamira ya kuhamia haraka Dodoma na kutakuwa na mpango wa kupendezesha mazingira katika mji wa serikali.“Sisi tunasimamia Muungano ushiriki wa Zanzibar utakuwepo na kutokana na hilo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imepata ekari 10 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi zake. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Joseph Malongo alisema michoro ya jengo hilo imetayarishwa na Wakala wa Majengo (TBA) na jengo la chini litakuwa na mita za mraba 1,050. | Kitaifa | 0 |
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ametoa siku 18 kwa uongozi wa Jiji la Dodoma kuhakikisha kituo cha afya cha Mkonze kinakamilika kwa asilimia 100.Jafo alitoa agizo hilo jana alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Mkonze ambacho ni miongoni mwa vituo vya kutolea huduma za afya 352, ambavyo viko kwenye mpango wa kuboresha huduma za afya katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Katika mpango huo kunafanyika ujenzi wa majengo sita ambayo ni chumba cha upasuaji, wodi ya mama na mtoto, maabara, nyumba ya mganga, chumba cha kufulia na kichomea taka.Kutokana na kukuta kituo hakijakamilika Jafo alisema: “ Nimetoa maelekezo ifikapo Juni 30 mwaka huu kituo kile kiwe kimekamilika kwa asilimia 100. Nataka siku hizi chache zilizobakia Jiji la Dodoma lihakikishe linakamilisha kile kituo na mimi mwenyewe nitarudi tena kuangalia kama kituo kimekamilika.”Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi pamoja na kushukuru hatua ya serikali ya kutoa Sh milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho, jiji liliamua kujenga kituo chenye hadhi ya Sh milioni 500.“Kwa vile Dodoma ni makao makuu ya nchi, sisi tuliona tujiongeze na tujenge kituo cha afya chenye hadhi ya Sh milioni 500 na kwa vile fedha za ziada takribani milioni 100 hazikuwa kwenye bajeti ya mwaka 2018/2019 tuliomba mapitio ya bajeti na Kamati ya fedha imesharuhusu fedha hizo zitumika. Kunambi alisema kituo hicho kitakamilika kwa muda ulioelezwa kwa sababu fedha ipo.Katika hatua nyingine, Jafo ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kikuyu- Chidachi-Kinyambwe-Itega yenye urefu wa kilometa 6 inayojengwa kwa lami kwa thamani ya Sh bilioni 9 na Kampuni ya STECLO. Kwa upande wa barabara ya urefu wa kilometa 1.85 ya Martin Luther-Swaswa inajoyengwa kwa tahamani ya Sh bilioni 1.3, Jafo alimuagiza mkandarasi SKOL kuhakikisha anapeleka vifaa vingine ili kazi ya barabara ile ukamilike. “Tumekuta amepaki scaveter pembeni kwa sababu ya kuharibika, tunataka wakandarasi ambao wanapewa kazi wawe na uwezo wa vifaa, hivyo nataka mkandarasi yule kazi yake iendelee,” alisema. | Kitaifa | 0 |
Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Ineke Bussemaker alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Saba wa Mwaka na Mkutano wa Wanahisa wa benki hiyo.Alisema benki hiyo inaendelea kukua ambapo hadi sasa imefikisha wateja milioni 1.9 ambayo ni sawa na asilimia 40 ya Watanzania ambao wanatumia benki hiyo kwa kuweka amana zao katika akaunti.Kadhalika alisema benki hiyo imekuwa ikiwawezesha wajasiriamali wadogo nchini katika kuimarisha kazi zao ili kuweza kukua na kushindana katika soko ambapo wamefikiwa wajasiriamali 60,000.Ineke alisema fedha za benki hiyo ziko imara na kwamba wataanza tena kutoa mikopo kwa kampuni kubwa na hata kwa watu binafsi walioko kazini. Alisema kwa mujibu wa mikopo inayotolewa na benki hiyo asilimia tatu ndiyo inakuwa hailipiki wakati uwiano wa soko ni zaidi ya asilimia sita hadi saba.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya NMB, Profesa Joseph Semboja akizungumza aliushukuru uongozi wa benki hiyo kufikia mafanikio mengine kwa mwaka huu pamoja na kuwashukuru wanahisa kwa kuendelea kuwa wavumilivu na kuiamini taasisi hiyo.Alisema wanahisa wa benki hiyo wataweza kupata gawio la Sh bilioni 104 kwa hisa ambalo linatafsiriwa kuwa na faida ya Sh bilioni 52 zilizotengwa nje ya faida ya mwaka 2014.Profesa Semboja alisema benki hiyo imekuwa ikitoa huduma mbalimbali kwa watu binafsi na hata kwa wajasiriamali wadogowadogo na wafanyabiashara wakubwa. | Biashara | 1 |
Alisema kuanzishwa safari mpya katika Bara la Afrika na Marekani, na kuimarika kwa hali ya kisiasa, kunachangia kampuni hiyo kupata faida zaidi ya hasara.Kwa mujibu wa mtendaji huyo, KQ ilipata hasara ya Dola milioni 61 katika kipindi cha miezi tisa iliyopita tangu Aprili hadi Desemba 2017.“Hasara hiyo imesababishwa na mambo mbalimbali kama vile mapungufu ya wakurugenzi wetu, kutotulia kwa baadhi ya nchi za Kiafrika na kuwepo kwa chaguzi mbili za Kenya mwaka jana,” amesema Sebastian Mikosz.Mikosz ametaja sababu nyingine za kampuni kupata hasara hiyo kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa bei ya mafuta kwa asilimia 14.Amesema, kuongezeka kwa bei ya mafuta ni changamoto kubwa katika kutafuta faida, hivyo kampuni kuishia kupata hasara na kupunguza kasi ya uendeshaji wa kampuni.“Hali ya kisiasa nchini imetulia na kutuhakikishia biashara yetu kuendelea vizuri baada ya Rais Uhuru Kenyatta kukutana na kufanya mazungumzo na Raila Odinga Machi 9 mwaka huu hatua ambayo tunaamini itaimarisha uchumi wa nchi,” amesema Mikosz.Kutokana na hali hiyo, Mikosz alisema anaamini mwaka 2018 utakuwa mzuri kwa KQ kwa kuwa mwezi Oktoba 2018 safari za moja kwa moja kwenda New York na Mauritius na safari zingine za moja kwa moja kwenda Cape Town, Afrika Kusini zitaanza.Mikosz amekiri kuwa si rahisi faida kuonekana ndani ya mwaka huu. “Hali nzuri ya kifedha itaanza kuonekana mwaka 2019 kutokana na ongezeko la mapato hadi asilimia 10 kwa safari za Nairobi hadi New York pekee,” aliongeza Mikosz. | Biashara | 1 |
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi amewaasa watumishi wa ofisi hiyo wanaotarajia kustaafu hivi karibuni, kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi hadi siku zao za kuhitimisha utumishi wao katika ofisi hiyo zitakapofika.Akizungumza katika hafla ya kuhitimisha mafunzo ya kujiandaa kustaafu yaliyoandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea nchini kote, aliwaeleza umuhimu wa kuendelea kuwajibika kulingana na taratibu na kanuni zinazoongoza utendaji kazi wa kila siku.“Hatutarajii kuona kati yenu hata mmoja wenu akianza kuchelewa kazini au kuanza kuzembea katika kutekeleza majukumu yake kwa kuwa anatarajia kustaafu mwaka huu,” alisisitiza, Maimuna.Akifafanua amesema kila mtumishi wa umma anayetarajia kustaafu anapaswa kuhakikisha kuwa anaendelea kuonesha mfano bora katika sehemu yake ya kazi kwa kutekeleza yale anayotakiwa kwa weledi na kwa wakati akizingatia maslahi ya nchi.Aliwaasa watumishi hao kutumia vizuri elimu waliyopatiwa kupitia mafunzo ya kuwaandaa kustaafu yaliyoandaliwa na ofisi hiyo ili hatimaye wanapostaafu waweze kuanzisha na kuendeleza shughuli za uzalishaji katika maeneo yao.Mkufunzi kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni, Ziada Sadick amesema kuwa chuo hicho kinapongeza ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuandaa mafunzo hayo kwa watumishi wake wanaotarajia kustaafu hivi karibuni.Aliongeza kuwa mafunzo haya yanawapa uwezo watumishi hao katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza zikawakabili baada ya kustaafu.Katika mafunzo hayo watumishi wanaotarajia kustaafu waliweza kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuanzisha miradi ya uzalishaji, mbinu za kukabiliana na msongo wa mawazo na mada nyingine mbalimbali. Mafunzo hayo yalishirikisha watumishi takribani ishirini wa kada mbalimbali. | Kitaifa | 0 |
Rais John Magufuli, leo Jumanne ameongoza mamia ya waombolezaji kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni za IPP Dkt. Reginald Mengi.Shughuli hiyo imefanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali. Akihutubia kwa niaba ya Rais, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi ameeleza kuwa kifo cha Mengi ni pengo kubwa kwa taifa na kwamba Tanzania imempoteza mzalendo wa kweli.“Kwa niaba ya serikali natoa pole nyingi kwa uongozi na watumishi wote wa makampuni ya IPP kwa kuondokewa na kiongozi na mtu muhimu sana katika utekelezaji wa majukumu yenu na yetu,” alisema. Kwa upande wake Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe amesema taifa limempoteza mlezi wa Timu ya Taifa ya Vijana wa chini ya miaka 17 Serengeti Boys.“Mengi ameondoka na amemgusa kila mmoja na mimi nawez kuelewa, majuzi timu yake ya Serengeti Boys aliyokuwa anailea iliposhindwa katika mashindano hakukata tamaa” aliongeza.Baadhi ya viongozi waliohudhuria ni pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Hamis Juma, Katibu Mkuu Kiongozi, Dk John Kijazi, pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda. Mwili wa Dk Mengi utasafirishwa kesho, Jumatano, kuelekea Machame mkoani Kilimanjaro kwaajili ya mazishi. | Kitaifa | 0 |
SERIKALI imesisitiza kuwa hali na mwenendo wa biashara nchini inakwenda vizuri, jambo linaloiwezesha kutekeleza miradi ya maendeleo, kulipa wafanyakazi mishahara, lakini pia kuwa na mazingira mazuri ya kuongeza idadi ya biashara zinazoanzishwa.Aidha, imeendelea kuweka msimamo wake wa kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye taulo za kike isipokuwa inapunguza kodi ya Corporate Income Tax kutoka asilimia 30 hadi 25 kwa viwanda vinavyozalisha taulo hizo nchini kwa muda wa miaka miwili.Hayo yamebainishwa kwa nyakati tofauti na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango na Naibu Waziri wake, Dk Ashatu Kijaji wakati wakijibu hoja za wabunge takribani 236 waliochangia katika mjadala wa kupitisha Bajeti ya Serikali Kuu kwa mwaka wa fedha 2019/20, bungeni jana.Dk Kijaji amesema hali ya mwenendo wa biashara nchini ni nzuri na inazidi kuimarika tofauti na madai ya wabunge waliochangia huku wengine wakitumia takwimu zisizo sahihi kuhusu hoja kwamba hali ya biashara ni mbaya nchini.Alisema alishawahi kueleza awali kuwa takwimu zinazowasilishwa bungeni humo kuwa biashara zinakufa nchini si sahihi na kuweka bayana takwimu halisi zinazoonesha kuwa biashara zinazofungwa ni 16,252 wakati zilizofunguliwa ni 147,817.Alielezea sababu za biashara kufungwa ambazo zinawakabili wafanyabiashara dunia nzima kuwa ni mfanyabiashara kubadili biashara, kuzidiwa na ushindani kwa biashara husika, kushindwa kufanya biashara na mzigo mkubwa wa madeni ya kodi na benki.“Zipo tafiti duniani zinazoonesha zaidi ya asilimia 50 ya biashara za kati na ndogo hufa kabla ya kusherehekea mwaka wa kwanza wa uanzishwaji wake, na hili si kwa Tanzania tu bali dunia nzima,” alisema.Alisema pamoja na ukweli huo, kupitia biashara zinazoendelea nchini serikali imekuwa ikiingiza mapato mengi na hivyo kutekeleza shughuli zake za kawaida ikiwemo kulipa mishahara kwa watumishi wake, lakini pia kuendeleza miradi ya maendeleo.“Serikali inalipa Sh bilioni 580 kila mwezi na kuwalipa watumishi wake kila tarehe 22 lakini pia ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka Sh bilioni 70 hadi zaidi ya Sh trilioni moja kwa mwezi. Sasa jamani hiyo hali mbaya ya biashara inatoka wapi?” alihoji.Aidha, amesema kwa sasa takribani asilimia 85 ya fedha zinazoenda kwenye miradi ni fedha za ndani. “Je, hizi fedha sasa zinatoka wapi kama biashara imekufa Tanzania?” alihoji.Alisema jambo la msingi kwa wizara ni kuendelea kuhakikisha mazingira na mwenendo wa biashara nchini yanaimarika ikiwemo kudhibiti mianya yote ya rushwa na watumishi wasio waaminifu wanaoikosesha serikali mapato.Alisema anafahamu kuwa amenyooshewa vidole na kudaiwa kuwa amekuwa akifurahia biashara kufa, tuhuma zinazotokana na msimamo wake wa kuhakikisha kuwa pamoja na biashara kuendelea kushamiri nchini, lakini taratibu na sheria za nchi zinafuatwa.Dk Kijaji alisema kutokana na jitihada za wizara hiyo ya fedha kuanzia Mei mwaka 2017 hadi Aprili 2019 watumishi zaidi ya 30 wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) walisimamishwa kazi kwa utovu wa nidhamu. | Biashara | 1 |
SHILINGI milioni 334 zimetumiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kununua gari la kubeba taka na makontena 20 ya kuweka taka.Kauli hiyo imetolewa jana na Fundi Mkuu wa Manispaa ya Tabora, Gaitan Mkweng’e wakati wa mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo wa bajeti.Amesema gari jimpya lililonunuliwa China litasaidia kukusanya na kuondoa taka maeneo mbalimbali.Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora, Bosco Nduguru amesema uzalishaji wa tani kwa siku katika manispaa hiyo ni tani 120 lakini kabla ya ununuzi wa gari hilo walikusanya tani 70 kwa siku.Alisema gari hilo litafanya wawe na uwezo kumalizia sehemu ya taka ambayo ilikuwa inabaki kwa siku.Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira katika Manispaa hiyo, William Mpangala alisema ununuzi wa gari hilo jipya utasaidia kuongeza uwezo wao kwani kila tarafa itakuwa na gari lake la ukusanyaji wa taka.Diwani wa Kata ya Cheyo, Hamisi Kitumbo alisema ununuzi wa gari lingine utawezesha wakazi wa halmashauri hiyo kuishi katika mazingira safi na salama.Alisema hatua hiyo itapunguza uwezekano wa magonjwa ya mlipuko yanayotokana na mrundikano wa uchafu maeneo yasiyo rasmi yanayotupwa taka. | Kitaifa | 0 |
KIWANGO cha ufaulu kwa wahitimu wa darasa la saba mkoani Morogoro kimeongezeka mwaka huu, ambapo wahitimu 37,111 wamefaulu sawa na asilimia 77.38. Mwaka jana asilimia 70.78 ya wahitimu, ndio waliofaulu, hivyo mwaka huu kuna ongezeko la ufaulu la asilimia 6.6.Hayo yalisemwa jana na Katibu Tawala Msaidizi upande wa Uchumi, Ernest Mkongo kwenye kikao cha uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga kidato cha kwanza Januari mwakani, kilichofanyika mjini hapa. Mkongo alisema kuwa hali ya ufaulu kwa kipindi cha mwaka 2018 imepanda, ukilinganisha na mwaka jana, ambapo ilikuwa ni asilimia 70.78 pekee.Alisema kuwa wanafunzi waliofanya mitihani ya darasa la saba Mkoa wa Morogoro ni 47,961, ambapo waliofanulu ni 37,111, ambao ni sawa na asilimia 77 ambapo lengo la mkoa ni kufikia asilimia 82. ‘’Kwa kuwa hatujafikia lengo la asilimia 82 tulilojiwekea upo umuhimu wa kuweka nguvu kazi ya pamoja na mikakati ili kuweza kufikia malengo hayo,’’ alisema Mkongo.Alisema kuwa kati ya watahiniwa 48,301 waliosajiliwa kufanya mitihani, watahiniwa 340 sawa na asilimia 0.7 hawakufanya mitihani huo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro, ugonjwa na vifo.Aliziagiza halmashauri zote tisa mkoani Morogoro, kutathimini matokeo hayo na kisha kuibua changamoto na kuzitafutia mikakati ya ufumbuzi na shule ambazo hazikufaulisha hata mwanafunzi mmoja na zenye watahiniwa wachache, zifanyiwe ukaguzi ili kubaini sababu za msingi zilizosababisha hali hiyo.Alipongeza Halmashauri ya Ulanga, Manispaa ya Morogoro na Malinyi kwa kufanya vizuri na kuzitaka Halmashauri za Wilaya ya Kilosa, Gairo na Morogoro kuongeza juhudi.Alitoa agizo kwa shule ambazo hazikufaulisha mwanafunzi hata mmoja, kuhakikisha ifikapo mwaka 2019 shule hizo zinafaulisha walau wanafunzi asilimia 50 ya watahiniwa wake. Katibu tawala huyo alimpongeza mwanafunzi, Innocent Seleli wa Shule ya Msingi Carmel iliyopo Manispaa ya Morogoro, kwa kuwa mwanafunzi bora wa mkoa na pia kuwa mwanafunzi kumi bora kitaifa.Ofisa Elimu Mkoa wa Morogoro, Joyce Baravuga alisema anapongeza shule na wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao na hivyo kupelekea mkoa kuwa miongoni wa waliochangia ufaulu wa kitaifa kupanda.Alisema kuwa mbali na ufaulu kupanda kwa mwaka huu, alizihimiza halmashauri zote kufanya tathimini ya mitihani kila mwaka na kubuni mbinu sahihi zinazolenga kuboresha taaluma kulingana na mazingira yao, hasa kurekebisha utendaji wa kazi, unaolenga kuinua taalumu kuanzia ngazi ya wilaya hadi shule. | Kitaifa | 0 |
TIMU ya soka ya taifa, Taifa Stars leo inatarajiwa kuanza mazoezi kujifua na mechi ya kirafi ki ya Fifa dhidi ya Rwanda na ile ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani, Chan dhidi ya Sudan.Stars inatarajiwa kucheza na Rwanda Oktoba 14 katika mechi ya kirafiki ya kalenda ya Fifa na siku nne baadaye itacheza na Sudan. Kocha mMsaidizi wa Stars, Juma Mgunda alisema timu hiyo itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Stars ina kazi ya kupindua matokeo katika mechi dhidi ya Sudan baada ya kukubali kufungwa bao 1-0 nyumbani.Mshindi wa mechi hiyo atafuzu fainali za Chan mwakani zitakazofanyika Cameroon. Mgunda alisema wachezaji 29 walitarajia kuanza kuripoti kambini tangu jana.“Mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Rwanda tunategemea yataanza kesho ( leo) Uwanja wa Uhuru ,wachezaji wote walioitwa watakuwa wamewasili kambini kulingana na ratiba ilivyowataka isipokuwa wale wa kutoka nje ya nchi tunatarajia kuungana nao siku tatu zijazo,”alisema Mgunda.Mgunda alisema anaamini kambi hiyo itakuwa na mafanikio makubwa ya kupata ushindi katika mchezo huo licha ya kusaliwa na siku chache kabla ya kukutana na Rwanda. Alisema katika mchezo huo wanahitaji zaidi ushindi kurudisha moyo kwa watanzania baada ya kupoteza mchezo uliopita nyumbani. | michezo | 2 |
Meneja Mwendeshaji wa Kampuni ya Shamy, Khamis Mwinjuma Simba akizungumza mjini hapa alisema kwamba kampuni yake kupitia Bodi ya Utalii ya Sweden wamepata kibali na leseni ya kuanzishwa kwa branchi ya kampuni hiyo yenye makao makuu yake mjini Zanzibar , mtaa wa Malindi.Kampuni hiyo ambayo tangu kuanzishwa kwake ina miaka minne sasa ilifanya uzinduzi wa branchi yake hivi karibuni, kazi iliyofanywa na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dora Msechu wakati akizindua mgahawa wa Mtanzania, Issa Kapande wiki iliyopita.Simba alisema kwamba tangu kuanzishwa kwake wamepata maendeleo makubwa hasa katika kukabiliana na changamoto za soko na kwamba kwa kuanzishwa kwa tawi hilo wanaangalia kufikia nchi 30 za Ulaya zinazotumia viza ya Ulaya.Alisema kuwa na ofisi nchini Sweden kumeamsha mori wa kuongeza mafanikio ya kampuni ili kusaidia juhudi za Wizara ya Utalii Zanzibar katika kuhakikisha kwamba sekta ya Utalii inaendesha uchumi wa Zanzibar.Alisema wizara kama wizara imefanya juhudi kubwa kuhakikisha utalii unakua na kuleta mafanikio kwa Zanzibar na hivyo ni wajibu wao kama Shamy Tours kuhakikisha kwamba wanatoa fursa walizowezeshwa na wizara hiyo kutanua shughuli zao ili kuihakikishia mapato serikali kwa kuingiza wageni wengi zaidi.“Tumepata faida kubwa kama Shamy Tours kutoka kamisheni ya utalii hasa usajili, kupewa hati za uendeshaji na vipeperushi na machapisho mbalimbali na hasa chapisho la Karibu Zanzibar linalohusu Zanzibar,” alisema Simba na kuongeza kuwa kwa kusaidiwa huko wameweza kusonga mbele na katika miaka minne kwa kushirikiana na Issa Kapande, Mtanzania mbaye amefungua mgahawa wa Kitanzania nchini Sweden, wameweza kuanzisha branchi nchini Sweden.Alisema pamoja na kuzindua ofisi yao, wameitumia siku ya ufunguzi wa mgahawa wa Issa Kapande kukutana na wadau mbalimbali wa masuala ya utalii nchini Sweden na kuwapatia zawadi halisi za Kitanzania kuwapa ushawishi wa kuja nchini.Baadhi ya zawadi hizo ni vinyago vya kimakonde taswira za Wamasai na vipeperushi mbalimbali. Alisema kuwapo kwa Shammy Tours nchini Sweden kutakuza biashara ya utalii.Alisema mipango ya kuanzisha ofisi nchini Sweden ilianza zamani wakati Issa Kapande akifanya shughuli zake katika Hoteli ya African House miaka sita iliyopita na kushika kasi katika miaka miwili iliyopita ambapo Issa Kapande alifika Zanzibar mara mbili kukamilisha ushirikiano uliozaa ofisi hiyo ya Sweden.Alisema pamoja na kujitangaza katika nchi zaidi ya 30 za Ulaya kupitia ofisi hiyo ya Sweden Shamy Tours inatarajia kushiriki katika maonesho ya utalii Afrika Kusini yatakayofanyika Mei mwaka huu, Urusi Juni mwaka huu na London, Uingereza Novemba mwaka huu.Alisema ushiriki wao ni sehemu ya kutafuta masoko na kuitangaza Tanzania, nchi ya visiwa vya Zanzibar, mlima Kilimanjaro na mbuga ya Serengeti. | Biashara | 1 |
KLABU ya Yanga leo itakuwa na mchezo wa majaribio dhidi ya timu ya Daraja la Kwanza Mawezi maalumu kwa ajili ya kumuaga mchezaji wao Nadir Haroub ‘Canavaro’.Canavaro aliyeitumikia Yanga zaidi ya miaka 10, amestaafishwa msimu huu na kupewa nafasi ya Meneja kwenye kikosi hicho na sasa jezi yake namba 23 huenda akaikabidhi kwa mchezaji mwingine leo.Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro. Sherehe zitaanza mchana timu ya wanawake Yanga Princess itakapochuana na Moro Kombaini chini ya mwigizaji Wema Sepetu.Yanga wanatarajia kutumia mchezo si tu kwa ajili ya burudani bali kuwachezesha wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.Baadhi ya wachezaji tangu wamesajiliwa hawajawahi kucheza mchezo wowote hivyo, Kocha Mwinyi Zahera anatarajiwa kuwatazama na kutengeneza muunguniko mzuri wa kikosi chake za kwanza.Waliosajiliwa ni Mrisho Ngassa, Haritier Makambo, kipa Klaus Kindoki, Feisal Abdallah ‘Fei toto’, Mohamed Issa ‘Banka’ na Deus Kaseke ambaye yeye pekee tayari alishacheza katika mchezo wa kimataifa dhidi ya Gormahia waliyofungwa 3-2.Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga Dismas Ten amesema kutakuwa na burudani kutoka kwa Richi Mavoko, Afande Sele, Gigys Money na Msaga Sumu. | michezo | 2 |
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amewataka watumishi wa wizara hiyo kufanya kazi kwa uaminifu katika kutekeleza kazi zao badala ya kufanya kazi kwa kutaka kujinufaisha kwa kisingizio cha ukosefu wa fedha. Kauli hiyo aliitoa wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kilichofanyika jijini hapa juzi. Alisema tatizo la upungufu wa fedha linatakiwa lisitumike kama kichaka kwa baadhi yao kufanya ubadhirifu kwa kutaka kujinufaisha wao binafsi. “Katika kipindi hiki serikali inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kiuchumi hivyo kumekuwepo na matatizo ya kifedha, hivyo matatizo hayo yanatakiwa yasitumike kama kichaka kwa watumishi kukosa uaminifu,” alisema. Alisema, watumishi wa serikali wanatakiwa kuepuka kutumia vibaya madaraka yao, kuacha kufanya kazi kwa upendeleo na kufanya kazi kwa kuendeleza maslahi yao binafsi. Waziri Lugola ambaye ni Mbunge wa Mwibara alibainisha kuwa katika mwaka huu wa fedha unaoishia Juni 30, kutokana na kuwepo kwa fedha katika bajeti ya wizara ndio maana baadhi ya stahiki za watumishi hao zimelipwa. Aliwataka wajumbe wa mabaraza ya wafanyakazi katika kila chombo na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo, kujadili kwa uhuru na uwazi changamoto zilizojitokeza katika utendaji wao na njia mbadala za utatuzi changamoto hizo. “Upungufu na udhaifu unatakiwa kusemwa wazi kwa uhuru ili ufahamike na kutafutiwa mbinu za kutatuliwa,” alisema Lugola. Pia aliwataka watumishi wa wizara hiyo kuzingatia sheria na kanuni na kufanya kazi kwa nidhamu katika kutimiza majukumu yao, kwani serikali inaendelea kuboresha mazingira bora kwa watumishi wa umma. Lugola pia alikemea vitendo vya baadhi ya wajumbe wa baraza hilo kuwakilishwa na watu ambao hawakuchaguliwa wakati baraza hilo linatakiwa kuwa na wajumbe waliochaguliwa na wafanyakazi wenzao. “Hapa ni kama nimeuziwa mbuzi kwenye gunia. Nimefungua kikao cha makundi mawili kwa pamoja. Kundi la wajumbe wanaowawakilisha wafanyakazi na watu ambao wanawawakilisha wajumbe ambao walipaswa kuwawakilisha wafanyakazi,” alisema. Naye, Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Ramadhani Kailima, alisema kikao hicho kina kazi muhimu ya kujadili bajeti na changamoto za watumishi na kuishauri wizara hatua za kukabiliana na changamoto hizo. Kailima ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, alisema changamoto zote kutoka kwa wawakilishi wa wafanyakazi zitapokewa na kutekelezwa. “Baraza la wafanyakazi wa wizara ni chombo huru. Nawaomba wawakilishi wa watumishi wote waeleze changamoto zao kwa uwazi na tutazifanyia kazi,” alieleza Waziri Lugola. | Kitaifa | 0 |
SERA ya Uchumi wa Kati kupitia ujenzi wa viwanda, umepata msukumo baada ya Kampuni ya IPP kuingia ubia wa kuanzisha kiwanda cha kuunganisha magari kutoka Jamhuri ya Korea maarufu kama Korea Kusini, kinachotarajiwa kuzalisha magari 1,000 kwa mwaka.IPP imeingia ubia huo na Kampuni ya Youngsan wenye uwekezaji wa kiasi cha zaidi Sh bilioni 22, sambamba na kutoa ajira za moja kwa moja kwa wananchi 500, idadi inayotarajiwa kuongezeka kadri ya muda unavyokwenda. Ujenzi wa kiwanda hicho kinachotarajiwa kujengwa eneo la Kurasini, utaanza mwanzoni mwaka ujao na uzalishaji rasmi unatarajiwa kuanza kati ya Septemba na Oktoba mwaka huo.Makubaliano ya uanzishwaji wa kiwanda hicho yalifikiwa jijini Dar es Salaam kati ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Song Geum-young ambao kwa pamoja walisema kuanzishwa kwa kiwanda hicho, kumelenga kuunga mkono juhudi za maendeleo nchini.Akizungumzia hatua hiyo, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi alisema kuanzishwa kwa kiwanda hicho, ilikuwa moja ya ndoto zake kama hatua ya kuitikia mwito wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli, inayosisitiza kasi ya ujenzi wa viwanda nchini.“Hakuna kinachoshindikana ukiwa na nia, hata Rais wetu anapambana katika mambo ambayo wengi waliona yanashindikana, amenunua ndege na kufanya mengine mengi..hii ni hatua kubwa katika kukuza maendeleo yetu,” alisema Mengi.Alisema kiwanda hicho kikianza kazi, kitatoa ajira kwa Watanzania, pia kitasaidia kuongeza mzunguko wa biashara katika Afrika Mashariki na Kati na kuiingizia mapato serikali kupitia kodi mbalimbali.Aidha, alisema mipango yake ya baadaye ni kuhakikisha wanajenga kiwanda chenye uwezo wa kutengeneza magari kuanzia mwanzo hadi inapokamilika kutoka katika hatua hiyo ya uunganishaji, jambo alilosema litazidi kuitangaza Tanzania.Magari yanayotarajiwa kuunganishwa kupitia kiwanda hicho ni mabasi, malori na magari madogo, ambapo kwa mujibu wa Balozi wa Jamhuri ya Korea, magari hayo ni ya kisasa. Alisema Jamhuri ya Korea imepiga hatua kubwa katika uzalishaji wa magari na kwamba anaamini kuwa kuanzishwa kwa kiwanda hicho nchini, kutasaidia kuleta mapinduzi katika sekta ya viwanda na kuleta tija kimaendeleo. | Kitaifa | 0 |
WIZARA ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafi rishaji imesema meli ya mv Maendeleo haitauzwa, kwa sababu huduma zake zinahitajika za kusafi risha abiria na mizigo katika ukanda wa Unguja na Pemba.Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Mohamed Ah- mada (pichani), wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Kiwani Pemba, Mussa Ali Mussa aliyetaka kujua lini meli hiyo itafanyiwa matengenezo baada ya kushindwa kufanya kazi kwa muda mrefu sasa. Ahmada alisema jumla ya dola za Marekani milioni 1.3 zinahitajika kwa ajili ya kuifanyia matengenezo meli hiyo ikiwemo kuisafirisha na kuipeleka Chelezoni Mombasa.Alisema hadi sasa jumla ya Dola za Marekani 500,000 tu zimepatikana kwa ajili ya kuifanyia matengenezo meli hiyo. Alisema meli hiyo haiwezi kufanyiwa matengenezo nchini, kwa hivyo lazima ipelekwe Mombasa. “Meli ya mv Maendeleo inahitaji Dola za Marekani milioni 1.3 kwa ajili ya matengenezo makubwa na kuiepeleka chelezoni ili iweze kufanya kazi zake za kutoa huduma za usafirishaji abiria na mizigo katika ukanda wa Unguja na Pemba,’’ alisema.Mapema, Ahmada alisema serikali haina nia ya kuiuza meli hiyo ambapo utafiti umebaini kwamba bado ina tija kubwa kwa serikali. Kwa mfano alisema wapo wafanyabiashara tayari wameonesha nia ya kuikodi meli hiyo kwa ajili ya shughuli zao za kibiashara.‘’Mwenyekiti napenda kuwajulisha Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwamba seri- kali haipo tayari kuiuza meli hiyo kwa sababu bado ina tija na faida kubwa za huduma za usafiri kwa wananchi wetu wa Unguja na Pemba,”alisema. Shirika la Meli za Zanzibar linamiliki meli tatu ikiwemo ya mv Mapinduzi 11 pamoja na Maendeleo na meli nyengine ni ya mv Ukombozi inayotoa huduma za mafuta. | Kitaifa | 0 |
[' Cameroon au Ivory Coast haitashiriki katika kombe la dunia 2022 nchini Qatar baada ya timu hizo kuwekwa katika kundi moja katika raundi ya pili ya michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia.', 'The indomitable lions ya Cameroon imeiwakilisha Africa mara saba katika kombe la dunia, huku Ivory Coast ikishiriki katika kombe hilo mara tatu. ', 'Makundi mengine mawili yanashirikisha timu mbili ambazo zimeiwakilisha Afrika katika kombe la dunia. ', 'Ghana na Afrika Kusini zitakutana katika kundi G pamoja na Zimbabwe na Ethiopia huku Misri na Angola pia zikikutana katika kundi F pamoja na Gabon na Libya. ', 'Misri ilikuwa miongoni mwa wawakilishi watano wa Afrika katika kombe la dunia pamoja na Morocco, Nigeria, Senegal na Tunisia - na zote zinaamini kwamba zina fursa nzuri ya kufika katika raundi ya tatu na ya mwisho mnamo mwezi Novemba 2021. ', 'Katika kundi B, Tunisia itakutana na Zambia, Mauritania na Equitorial Guinea huku Nigeria ikikutana na Cape Verde, Jamhuri ya Afrika ya kati na Liberia katika kundi C. ', 'Kundi H Senegal itakabiliana na Congo, Namibia na Togo huku Morocco ikichuana na Sudan, na Guinea pamoja na Guinea Bissau katika kundi I. ', 'Raundi ya kwanza ya mechi hizo za kimakundi itaanza Oktoba 2020 na kukamilika Oktoba 2021 kabla ya kufanyika kwa michuano ya muondoano Novemba 2021. ', 'Ni washindi wa makundi hayo 10 pekee watakaosonga mbele katika mechi za muoandoano ambapo awamu mbili zitaamua wawakilishi watano wa kombe la dunia kutoka Afrika. ', 'Mechi za kufuzu zilitarajiwa kuanza mwezi Machi lakini shirikisho la CAF likaahirisha michuano ya Afcon kutoka mwezi Juni hadi Januari. ', 'Raundi ya kwanza ya mechi za kufuzu kwa kombe la dunia za Afrika ziliyafanya mataifa yanayoorodheshwa chini kushindana katika awamu mbili huku mshindi akisonga mbele na kujiunga na mataifa mengine 26 ambayo yataendelea katika raundi ya pili.'] | michezo | 2 |
BAO pekee lililofungwa na mshambuliaji David Molinga, lilitosha kuipandisha Yanga hadi nafasi ya nne ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaa, jana na kumalizika kwa 1-0 Molinga alifunga bao hilo dakika ya 51, akipokea pasi iliyopigwa na Ditram Nchimbi na kufikisha idadi ya mabao sita katika orodha ya wafungaji ambapo anayeongoza ni Meddie Kagere wa Simba kwa mabao 12. Matokeo hayo yameifanya Yanga kutoka kwenye nafasi ya sita na kupanda hadi ya nne ikiwa na pointi 31, katika michezo 16 waliyocheza sawa na Namungo FC ambayo inashika nafasi ya tatu zikitofautina kwa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa na idadi ya michezo. Yanga inazizidi pointi moja moja, Kagera Sugar, Coastal Union na Polisi Tanzania ambazo zote zimecheza mechi 18 na wanazidiwa pointi 16 na vinara, Simba ambao pia ndio mabingwa watetezi. Yanga walilipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 katika mchezo wa raundi ya pili ya ligi kuu msimu uliopita uliochezwa Aprili mwaka jana Morogoro na msimu huu kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi hatua ya nusu fainali kwa mikwaju ya penalti 4-2. Ukosefu wa umakini kwenye safu ya ushambuliaji ya Mtibwa Sugar kumewafanya washindwe kusawazisha bao hilo kwani walitengeneza nafasi ambazo hakuweza kuzitumia. Pia washambuliaji wa Yanga wangeweza kupata mabao zaidi endapo wangetulia kwani walikosa nafasi za wazi za kuwapa mabao na sifa zimuendee kiungo mkongwe, Abduhalim Humud ‘Gaucho’ aliyemdhibiti kiungo Bernard Morrison.Kikosi cha Yanga: Metacha Mnata, Juma Abdul, Jaffar Mohamed, Lamine Moro, Said Juma ‘Makapu’, Papy Kabamba Tshishimbi, Patrick Sibomana/Ditram Nchimbi dakika ya 46, Haruna Niyonzima, David Molinga/ Yikpe Gislain dakika ya 68, Mapinduzi Balama na Bernard Morrison/Abdulaziz Makame dakika ya 85. Mtibwa Sugar: Shaaban Kado, Kibwana Shomari, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Cassian Ponera, Henry Shindika, Abdulhalim Humud ‘Gaucho’, Ismail Mhesa/Juma Luizio dakika ya 56, Ally Makarani, Riphat Msuya/ Haroun Chanongo dakika ya 81, Awadh Juma na Salum Kihimbwa/Omary Hassan dakika ya 73. Michezo mingine iliyochezwa jana, Azam FC ikiwa Uwanja wa Samora, Iringa ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbeya City, na kubaki katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 37, Simba ikiwa kileleni kwa pointi 47 na Mbeya City bado ipo kwenye hali mbaya kwani ipo katika nafasi ya 18 ikiwa na pointi 14.Katika mchezo wa JKT Tanzania na Polisi Tanzania ambao ulisitishwa juzi dakika ya 53 kufuatia Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kujaa maji na kuahirishwa wakiwa hawajafungana umemaliziwa jana na Polisi Tanzania kushinda bao 1-0. Tanzania Prisons ikicheza katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC ambapo kwa matokeo hayo, Tanzania Prisons imefikisha pointi 21 katika nafasi ya 12 na KMC imefikisha pointi 17 katika nafasi ya 17. | michezo | 2 |
Nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Kundi la Navy Kenzo linaloongozwa na Emmanuel Mkono “Nahreel na Haika pamoja na rapa, Joh Makini walifunika kwa kuwakosha watu juzi usiku kwenye Tamasha la Utamaduni la Afrika Mashariki (JAMAFEST).Katika tamasha hilo linaloendelea kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wengi walipanda jukwaani kutumbuiza lakini walioongoza kwa kushangiliwa zaidi ni hao ikionesha dhahiri kundi kubwa la vijana lililohudhuria lilivutiwa zaidi na muziki wao.Ukizungumzia upande wa Bongo Fleva, Kundi la Navy Kenzo lilikuwa ndio la kwanza kupanda jukwaani na kuwanyanyua baadhi ya watu waliokuwa wamekaa mbali na kusogea karibu wakionekana kuimba na kucheza na hata walipomaliza bado watu walitamani aendelee kubaki kuwapa burudani.Alifuata Joh Makini na muziki wa kufoka huku vijana wengi na hata wamama waliokuwepo wakionekana kufurahia burudani aliyotoa kuonesha namna anavyokubalika. Ukiachilia mbali msanii huyo, Juma Jux alipanda jukwaani na kuimba kidogo kisha kumtambulisha mpenzi wake mpya Mchina ambaye amekuwa akizunguka naye, hali iliyowavutia mashabiki wengi waliokuwepo na kuanza kuimba shemeji, shemeji, shemeji na kisha kuanza kuimba muziki wake wa taratibu.Wengine waliotumbuiza ni pamoja na kwaya ya Kinondoni Revival, Kundi la Utamaduni Zanzibar, Kundi la Utamaduni Arusha, Bendi ya muziki kutoka Rwanda na vikundi mbalimbali kutoka Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya, ambavyo vilitumbuiza katika tamasha hilo la tatu kufanyika baada ya mengine kufanyika Uganda na Rwanda. | michezo | 2 |
TIMU ya Soka ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes jana ilitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya timu ya taifa ya Kenya kwenye mechi ya michuano ya Kombe la Chalenji kwa nchi za ukanda wa Baraza la Vyama Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).Mechi hiyo iliyofanyika Uwanja wa Jinja, Uganda ilikuwa na kasi kutokana na ubora wa vikosi vyote viwili. Timu zote hizo zilishinda idadi kubwa ya mabao katika mechi zake za kwanza, Tanzania ikiifunga Ethiopia mabao 4-0 na Kenya ikiifunga Zanzibar 5-0. Mabao ya Ngorongoro katika mechi ya jana yalipatikana kupitia kwa wachezaji Andrew Sichimba dakika ya 37 akifikisha bao lake la nne baada ya mchezo uliopita kufunga hattrick na Abdul Seleman alifunga dakika ya 56.Wafungaji wa Kenya walikuwa Otieno Odhiambo dakika ya 26 na Otieno Patrick dakika ya 52. Kwa matokeo hayo katika kundi B Kenya wanaongoza kundi kwa wastani wa mabao wakiwa na pointi nne sawa na Ngorongoro iliyo nafasi ya pili. Michezo mwingine wa kundi hilo ulitarajiwa kupigwa jana jioni kati ya Zanzibar dhidi ya Ethiopia kwenye Uwanja huo,mechi ambayo kila timu ilikuwa imepania kupata ushindi kukwepa kushika mkia kwenye kundi hilo ambalo lina ushindani mkali. | michezo | 2 |
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara, Simba wanashuka dimbani leo kuivaa Lipuli FC kwenye uwanja wa Samora, Iringa.Timu zote mbili hakuna aliyewahi kumfunga mwenzake tangu Lipuli ipande Ligi Kuu msimu uliopita. Wamekutana katika mechi tatu na zote wametoka sare. Mchezo wa leo ambao wekundu hao wako ugenini wakiwa moto huenda wakatengeneza rekodi nyingine mpya kwa kuhakikisha wanashinda ingawa mchezo unaweza kuwa mgumu kwa vile hata wenyeji wamepania kushinda.Ukitizama mechi tano zilizopita za Simba imeshinda zote na mchezo wa mwisho imeifunga Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa kwa mabao 3-1. Wekundu hao wako moto kutokana na kasi yao na ushindi katika michezo iliyopita.Mpaka sasa wamecheza michezo 18, wameshinda 14, sare tatu na kupoteza mchezo mmoja wakiwa wanashika nafasi ya tatu na pointi 45, nyuma ya Azam yenye pointi 50 katika michezo 25 sawa na vinara Yanga wanaoongoza kwa pointi 61. Lipuli katika michezo mitano iliyopita imeshinda mmoja, imepoteza miwili na kupata sare mbili ikiwa inashika nafasi ya tano na pointi 38 katika michezo 27.Yeyote anaweza kuibuka Na Yasinta Amos in Arusha MWANARIADHA Failuna Abdi ameshinda katika mashindano ya riadha ya Semi Marathon International de safi 2019 yaliyofanyika Casablanca, Morocco mwishoni mwa wiki iliyopita. Katika mbio hizo za wanawake waliokimbia kilometa 21, Failuna aliongoza kwa kutumia saa 1: 10 :50 akiwaacha wanariadha kutoka Ethiopia waliomfuata kwa nafasi ya pili na ya tatu, Asnakesh Awoke Mengesha aliyetumia saa 1:10:57 huku Hiwoti Ayalew Yemer akimaliza kwa saa 1:11:50.Kwa upande wa wanaume mwanariadha kutoka Kenya, Bernard Kipkorir Ng’eno aliongoza kwa saa 1:1:06 akifuatiwa na Gizachew Hailu Negasa kutoka Ethiopia 1:01:33 Mwanariadha Faraja Damas kutoka Tanzania (JKT) alishika nafasi ya sita baada ya kutumia saa 1: 02 :20.Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Wilhelm Gidabuday alisema mwanariadha Failuna amewashinda Wakenya na Waethiopia wote, hivyo RT inafurahi kuona Mtanzania ameweka changamoto na kuwashinda wenzake wa Afrika Mashariki ambao wamezoea kushinda. NAIROBI, Kenya KUPOTEZA muda, majeruhi, kulazimisha kufanya mabadiliko na kuoneshwa kwa kadi nyekundu ni mambo yaliyojitokeza wakati Gor Mahia ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Hussein Dey kwenye Uwanja wa Kasarani jijini hapa juzi.Mchezo huo wa tatu wa Gor Mahia katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ulifanyika kwenye uwanja huo na kuifanya timu hiyo kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali. Francis Kahata na Jacques Tuyisenge walifunga mabao hayo na kuwapatia wenyeji pointi zote tatu katika mchezo huo mkali. Timu ya Algeria ilibidi kufanya mabadiliko baada ya baadhi ya wachezaji wake kupata majeraha akiwemo nahodha wao, Ahmed Gasmi na kiungo Hocine Orfi walitolewa uwanjani na nafasi zao kuzibwa mara moja na wachezaji wa akiba.Gasmi alionekana kuumia zaidi, na alikimbizwa katika hospitali ya Aga Khan akidaiwa kupata maumivu ya kichwa. Kutokana na ushindi huo, Gor Mahia imerejea kileleni mwa msimamo wa Kundi D ikiwa na pointi sita. Gor Mahia wakati wakielekea mwishoni mwa mchezo huo, ilibidi kugangamala ili kuhakikisha wanaondoka na pointi zote tatu, huku Waalgeria wakichanganyikiwa baada ya kulazimika kufanya mabadiliko mapema mara mbili pamoja na mchezaji wao mmoja kutolewa kwa kadi nyekundu.Timu hiyo ya Algeria ya Hussein Dey imepoteza pointi na kuifanya kuwa katika nafasi ya pili wakiwa na pointi nne, ikitegemea mechi kati ya Petro Atletico na Zamalek ya Misri huko Alexandria. Timu hizo zilifungana 1-1.Ilikuwa siku mbaya kwa Hussein Dey, wakati wachezaji wake wawili wakubwa walipoumia. Nahodha Ahmed Gasmi na kiungo Hocine Orfi walitolewa nje katika dakika ya 30 na 37 na nafasi zao kuchukuliwa kwa haraka na Hocine Laribi na Aberouf Choiuter. Simba, Lipuli zawania rekodi GWIJI LA HABARI TANZANIA EO Yanga yamkumbuka Urungu UK.23 na ushindi katika mchezo huo kutegemea na walivyojiandaa ingawa Simba inapewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na ubora kiufundi. Wekundu hao wako vizuri katika safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Meddie Kagere mwenye mabao 11 kwenye ligi.Ni wazi kuwa atapambana kuifungia timu yake ili kuwafikia wanaoongoza ambao ni Heritier Makambo wa Yanga mwenye mabao 12 sawa na Said Aiyee wa Mwadui. Simba imefunga mabao 38 ikiwa na pungufu tofauti na Lipuli iliyoko mbele michezo tisa, ikiwa imefunga mabao 23. Wekundu hao wapo vizuri pia, katika safu ya ulinzi wamefungwa mabao sita pekee katika mechi 18 walizocheza.Kocha wa Simba, Patrick Aussems alisema Lipuli sio timu ya kubeza na wanajua ni kwa namna gani mchezo utakuwa mgumu, lakini muhimu kwao ni kupambana kupata pointi tatu. “Tunawaheshimu wapinzani wetu tukijua wapo kwenye uwanja wao wa nyumbani wamejipanga kupata matokeo na sisi pia, tunataka pointi tatu,” alisema. Kocha wa Lipuli, Selemani Matola alisema hawajawahi kuifunga Simba, hivyo wanataka awamu hii kuweka rekodi mpya ya kupata pointi tatu kwenye uwanja wao dhidi ya mabingwa hao watetezi. | michezo | 2 |
SHIRIKISHO la soka Tanzania, TFF lipo kwenye mchakato wa mabadiliko ya Katiba yake ambapo sasa kutakuwa na ukomo wa vipindi vitatu kugombea nafasi mbalimbali. Mbali na hilo, lakini pia katiba hiyo inataka wajumbe wa mkutano mkuu kupungua kutoka 130 mpaka 87 na kupunguza wajumbe wa kamati ya Utendaji kutoka 22 mpaka 13.Akizungumza na wadau wa soka Dar es Salaam jana kuhusu miaka miwili ya uongozi wake, Rais wa TFF, Wallace Karia alisema mabadiliko hayo yatafanyika kwa maagizo ya Shirikisho la soka la kimataifa, Fifa.“Maagizo haya yaliletwa na Fifa Tangu mwaka 2014, lakini mabadiliko yaliyokuwa yafanyike mwaka 2016 yalikwama mimi nikiwa mmoja wa waliyoyakataa kwa sababu utaratibu haukufuatwa,” alisema.“Sasa kugombea itakuwa na ukomo wa miaka minne minne kwa vipindi vitatu, maana yake ukigombea ukapata na kuwa madarakani kwa miaka 12, basi hutakiwi kugombea tena, hiyo ipo hata Fifa na Caf, sasa hatutamuona Infantino (Gianni, rais wa Fifa) akakaa madarakani kama ilivyokuwa kwa Blatter (Sepp, rais wa zamani wa Fifa) au Ahmad (Rais wa Caf) akakaa kama mzee wetu Hayatou (Issa, rais wa zamani wa Caf),” alisema.Kuhusu wajumbe wa mkutano mkuu, Karia alisema watapunguzwa na sasa kila mkoa utatoa wajumbe wawili badala ya wanne kama ilivyokuwa awali. “Sasa katika mikoa yote watakuja Mwenyekiti, na mjumbe wa mkutano mkuu, wawakilishi wa klabu tutaangalia namna ya kuwashirikisha kwenye shughuli za Shirikisho na makatibu wao watakuwa na kazi ya kusimamia shughuli zote za soka kwenye mikoa yao na watawezeshwa, wajumbe watakaokuja watatu kwenye mkutano mkuu ni kutoka vyama shiriki,” alisema.Kuhusu mikoa kugawanywa katika kanda, Karia alisema zitapunguzwa kutoka 13 zilizokuwa awali mpaka sita. “Na sasa wajumbe wa kamati ya utendaji kutoka kwenye kanda watakuwa sita, kisha watakaoungana na wengine wanne ambapo sasa katiba itamruhusu Rais kuwateua badala ya watatu kama awali, ila kwenye hao wanne, mmoja itabidi awe mwanamke hapo na wale sita watakaochaguliwa na mkutano mkuu watakuwa 10 kati ya hao 10 Rais atachagua makamu wake humo ambaye atapitishwa na mkutano mkuu,” alisema.Alisema, mjumbe mmoja atasimamia mikoa mitano na ili ataruhusiwa kugombea nafasi ya kamati ya utendaji kama atapitishwa na mkoa wake.“Mkoa utasimamisha mtu mmoja tu hakuna kusimamisha watu wengi, kwa hiyo mfano kanda ya kwanza ni Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Pwani na Morogoro hapo kila mkoa utaleta mgombea wake watapigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu.”Alisema yeye na wasaidizi wake kwa nyaati tofauti watafanya ziara kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuelezea mabadiliko hayo ili yafahamike kwa wadau wa soka. “Sisi kamati ya utendaji tumeyapitia tukapeleka Fifa wakaturudishia sasa tunasubiri kwenye mkutano mkuu Desemba wajumbe nao wakapitishe,” alisema. | michezo | 2 |
CHUO cha Bandari kiko katika mchakato wa kupitia upya mitaala ya kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho, ili kuendana na mahitaji ya sasa ya soko na mabadiliko ya teknolojia.Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Chuo hicho, Dk Joseph Kakeneno alipozungumza na HabariLeo kwenye maonesho vya vyuo vya ufundi yanayoendelea katika uwanja wa Jamhuri jijini hapa. Alisema chuo kimeamua kupitia upya mitaala baada ya kufanya utafiti wa kina kuangalia kama mitaala ya sasa inakidhi hali ya sasa hasa baada ya kuwapo kwa ongezeko la teknolojia na mahitaji ya soko ya sasa.“Matokeo ya utafiti tulioufanya yametufanya tuone haja kufanya mapitio ya mitaala yetu kwa kozi tunazotoa ili kuwa na mitaala ambayo itaendana na hali ya sasa, mahitaji ya soko na mabadiliko ya teknolojia.”Alisema pia mapitio ya mitaala yanalenga kukabiliana na ongezeko la mabadiliko katika soko, lakini pia kufikia uchumi wa viwanda kwa kuzingatia umuhimu wa bandari katika suala zima la kuinua uchumi wa nchi. Dk Kakeneno alisema mapitio ya mitaala hiyo yanatarajia kukamilika mwezi ujao na kuwa baada ya hapo wataiwasilisha Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ili kupata ithibati mpya.Dk Kakeneno alisisitiza juu ya haja ya wale ambao wanatarajia kozi mbalimbali kufanya hivyo ili kuweza kupata ujuzi katika masuala ya bandari ili kuweza kuendana na mabadiliko ya fani hiyo ili kuwe na ufanisi. “ Ili kuwapa fursa waombaji wa kozi mbalimbali bila kuharibu ratiba zao, Chuo cha Bandari kinatoa mafunzo wakati wa asubuhi na jioni ambayo ni fursa kwa wale ambao wako kazini.”Akizungumzia mikakati ya kujipanua zaidi, Dk Kakeneno alisema Chuo cha Bandari kina mkakati wa kuanzisha vituo vya mafunzo katika bandari zingine za Mtwara, Kigoma, Tanga na Kyela. Chuo cha Bandari kimekuwa kikidahili wanafunzi wapya kupitia mfumo wa kidijitali ujulikanao kama “Student’s Information Management System (SIMS) ambao unatoa nafasi kutumia njia ya mtandao kutuma maombi. | Kitaifa | 0 |
['Manchester United wameongeza dau la £30m juu ya thamani ya kiungo wa Ufaransa Paul Pogba, 26, na sasa wanataka dau la £180m kumuuza mchezaji huyo waliyemnunua kwa dau la £89m in 2016.(Star)', 'Juventus wamesitisha hamu yao ya kutaka kumsajili Pogba, wakitoa fursa kwa Real Madrid kumsaini mchezaji huyo wa Ufaransa. (Mail)', "Manchester United huenda ikamsajili beki wa Monaco na Ufaransa 19 Benoit Badiashile,ambaye pia anawaniwa na Wolves - iwapo watamkosa beki a leicester na Uingereza Harry Maguire, 26. (L'Equipe, via Express)", 'Inter Milan huenda wakalazimika kulipa takriban £90m ili kuweza kuwa na fursa ya kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji na Man United Romelu Lukaku, 26, msimu huu (Telegraph)', 'Arsenal itataka kulipwa dau la £8.8m ili kumuuza nahodha wake na beki wa Ufaransa Laurent Koscielny, 33 ambaye anataka kuondoka katika klabu hiyo na alikataa kuondoka na wenzake kuelekea Marekani kwa mechi za maandilizi ya msimu ujao. (London Evening Standard)', 'Arsenal imeimarisha hamu yake ya kumsaini beki wa Benfica na Ureno Ruben Dias, 22, kufautia maamuzi ya hivi karibuni yaKoscielny . (Mail)', 'West Ham infanya mazungumzo na Eintracht Frankfurt over a deal to sign 25-year-old French striker Sebastian Haller for around £40m. (Sky Sports)', 'Mshambulaji wa Manchester United na Jamhuri ya Ireland Mipo Odubeko, 16, ambaye aliifungia magoli 35 shule yake ya mafunzo ya soka msimu uliopita amekataa kuongeza kandarasi mpya.. (Mail)', 'Juventus imekubali dau la £63m kumnunua beki wa Ajax na Uholanzi Matthijs de Ligt mwenye umri wa miaka 19. (De Telegraaf - in Dutch)', 'West Ham wametaka kulipwa kitita cha £10m ili kumsajiuli kiungo wa kati wa Equatorial Guinea Pedro Obiang, 27, licha ya klabu za Itali kama vile Bologna na Sassuolo kuonyesha hamu ya kumnunua mchezaji huyo. (Sun)', 'Tottenham inatarajiwa kuwasilisha ombi la kumsajili kiungo wa kati wa Leeds na Uingereza Kalvin Phillips, ambaye klabu hiyo ya York Shire inasema ana thamani ya £30m. (Mirror)', 'Manchester United bado ina hamu ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Newcastle na Uingereza Sean Longstaff kutoka Newcastle licha ya klabu hiyo kutokubaliana juu thamani ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Sky Sports)', 'Lakini bei ya Newcastle ya £50m inaweza kuilazimu United kumaliza hamu yao.. (ESPN)', 'Barcelona inakaribia kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa na Atletico Madrid Antoine Griezmann kutoka Atletico Madrid kwa dau la £107m . (Mirror)', 'Duru kutoka Barcelona zimekana ripoti kwamba tayari klabu hiyo imetoa dau hilo (Sport)', 'Mshambuliaji Gareth Bale, 29, alishiriki mazoezi na wenzake wa Real Madrid nchini Canada huku akiendelea kujilazimisha katika mipango ya mkufunzi Zinedine Zidane. (Mail)', 'Newcastle inajiandaa kumteua mkufunzi wa Sheffield Wednesday Steve Bruce kuwa kocha wake na wanatumai ataweza kujiunga na timu hiyo katika maandalizi ya msimu ujao ziarani China. (Telegraph)', 'Newcastle inajadiliana kuhusu fidia ya takriban £5m na klabu ya Sheffield Wednesday ili kumsajili Bruce. (Times)', 'Manchester United na Manchester City zimepigwa jeki katika harakati za kumsajili Bruno Fernandes huku klabu yake ya Sporting Lisbon ikikaribia kumsajili mchezaji atakayechukua mahala pake.. (Mirror)', 'Manchester United imeanza majadiliano na Roma kuhusu kumuuza mshambuliaji wake mwenye umri wa miaka 26 Romelu Lukaku. (Goal.com)', 'Mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Inter Milan Piero Ausilio amesafiri kuelekea mjini London ili kukutana Manchester United ili kuona iwapo dau watakaloliwakilisha kumsajili Lukaku litafanikiwa kumnunua (Guardian)', 'Ajenti wa beki wa Tottenham Toby Alderweireld amefanya mazungumzo na Roma kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 mwenye thamani ya £22.5m. (Calciomercato)', 'Mchezaji wa Real Madrid na Jamhuri ya Dominican Mariano Diaz, 25, hana hamu ya kujiunga na Arsenal msimu huu. (AS, via Mirror)', "Paris St-Germain wanatarajiwa kuimarisha hamu yao ya kutaka kumsajili mchezaji wa Everton Idrissa Gueye kwa dau la £27m kwa kiungo huyo wa Senegalr. (L'Equipe, via Sun)", "Arsenal ina hamu ya kumsajili mchezaji wa Real Madrid's Dani Ceballos kwa mkopo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 pia amekuwa akifanya mazungumzo na klabu ya Tottenham. (Sky Sports)", 'Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anatarajiwa kuzuia jaribio la Steven Gerrard kumrudisha winga Ryan Kent katika klabu ya Rangers msimu huu. Mchezaji hyo mwenye umri wa miaka 22 alihudumu msimu uliopita kwa mkopo na klabu hiyo ya Uskochi.. (Express)', 'Ajenti wa winga wa PSV Eindhoven Steven Bergwijn, 21, ameiambia klabu ya Bayern Munich kwamba mteja wao anayekumbwa na uvumi wa kuhamia klabu ya Manchester United yuko tayari kuhamia Ujerumani. (Express)', 'Manchester United wamefutilia mbali hamu yao inayoripotiwa ya kumsaini mchezaji wa Southampton na Gabon Mario Lemina, 25, ambaye amehusishwa na Arsenal. (Manchester Evening News)', 'Mshambuliaji wa Bournemouth na Uingereza Callum Wilson, 27 - anayelengwa na West Ham - anatarajia kutia saini mkataba mpya wa miaka minne na The Cherries. (Talksport)', 'Bournemouth inajiandaa kumruhusu mchezaji mwenye umri wa miaka 25 winga wa Uskochi Ryan Fraser, ambaye amehusishwa na uhamisho wa Arsenal, kuondoka kwa dau la bila malipo mwisho wa msimu ujao badala ya kumuuza msimu huu. (Express)', 'Mchezaji wa zamani wa Uingereza Peter Crouch, 38, hajaamua iwapo atastaafu baada ya kandarasi yake na Burnley kuisha msimu huu . (Talksport)', 'Wachezaji wanaolengwa na Newcastle Joelinton, mchezaji wa Hoffenheim ,22 raia wa Brazil pia ananyatiwa na Wolves. (Newcastle Chronicle)', 'Winga wa Crystal Palace 26 Wilfried Zaha, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Arsenal hakushirikishwa katika picha za jezi mpya ya ugenini ya klabu hiyo. (Express)'] | michezo | 2 |
VIONGOZI wa dini nchini wamezindua mkakati wa Mfumo wa Uchumi wa Soko Jamii unaolenga kuchochea kasi ya Tanzania kuelekea katika uchumi wa kati unaoendeshwa na viwanda vinavyojengwa.Uzinduzi huo ulifanyika jana jijini Dar es Salaam ukiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Mahusiano ya Dini Mbalimbali, Askofu Steven Munga kwa niaba ya Wakristo, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa kushirikiana na Kaimu Mufti wa Tanzania, Shehe Ali Muhidin Mkoyogore kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata).Viongozi hao wa dini walisema katika uzinduzi huo mfumo wa uchumi wa soko jamii kwa Tanzania unalenga kuongeza ukuaji wa uchumi shirikishi na endelevu na kuhakikisha ustawi wa baadaye wa nchi.Muhtasari wa Mfumo wa Uchumi wa Jamii wa Soko Jamii kwa Tanzania: Kuelekea Maendeleo Shirikishi na Endelevu ya Kiuchumi unataja tunu za mfumo huo ni ufahamu, hekima, uwajibikaji, taifa kwanza, jumuiya, utu wa binadamu, uadilifu, vijana, tathmini ya sera za maendeleo, uwazi na umoja.Munga ambaye ni Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, alisema umefika wakati Watanzania kumuunga Mkono Rais John Magufuli kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kuongeza tija na kukuza uchumi.“Sasa tuhame kutoka kwenye maneno kwenda kwenye vitendo…dosari zilizopo katika mkakati huu kutegemea mazingira tofauti ya utekelezaji, zinaweza kurekebishwa ili kufikia malengo ya mradi, kila mmoja atimize wajibu wake,” alisema Askofu Munga. Shehe Mkoyogore alisema, “mfumo huu tuusome kwa makini na kuufanyia kazi sawa sawa.”Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine cha Tanzania (Saut), Ntui Ponsian alisema mfumo huu unahitaji jamii kuwa na taarifa sahihi za kutosha kufanya uamuzi kwa maslahi ya taifa huku watu wakiwa waaminifu. “Mfumo huu pia utazalisha walipa kodi wengi kupitia ajira mbalimbali na biashara na watu watakwenda katika kilimo shambani kwa vile wanajua wana uhakika wa soko na kupata fedha,” alisema. Alisema ili matamanio ya Rais Magufuli kuacha Tanzania ikiwa na mabilionea 100 yatimie,viongozi wa dini wanatamani hayo ndiyo yafanyike huku kukiwa hakuna Mtanzania anayeachwa nyuma kiuchumi.Shehe wa Mkoa wa Mwanza, Hassan Kabeke, alisema uzinduzi wa kitabu hicho utawasaidia viongozi wa dini kuelewa wajibu wao kwani baadhi wanadhani kimakosa suala la uchumi linaihusu serikali pekee. Katibu Mkuu wa TEC, Padri Dk Charles Kitima alisema, “Uchumi wa Soko Jamii ni mfumo unaolenga utu wa mtu bila kunyanyasa wengine; kumfaa binadamu na siyo kumwangamiza; ni mfumo unaolenga kutunza mazingira na siyo kuyaharibu na yote yanakuwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vijavyo.”Alisema licha ya jukumu lao kubwa kuwaweka binadamu karibu na Mungu, wanatambua wajibu wao kuwafanya binadamu kushiriki uchumi shirikishi wa uzalishaji mali wawe na maisha bora na maendeleo. Padri Kitima alisema Watanzania wanapaswa kushirikishwa na kuelewa zaidi umuhimu wa uzalishaji na uendeshaji biashara adilifu katikati ya uchumi ili Mtanzania ampende Mungu na pia maendeleo ya kweli. Awali katika mazungumzo na wanahabari, Dk Kitima alisema wanataka kuwajenga watu wawe na ushindani na uzalishaji shirikishi katika uchumi hata kupitia Watanzania kumiliki kampuni mbalimbali na kubwa hata kupitia hisa ndiyo maana wanahimiza watu wafundishwe kuzalisha kiadilifu na kulipa kodi. | Kitaifa | 0 |
TIMU ya taifa ya Tanzania, Serengeti Boys jana ilijiweka katika nafasi fi nyu katika mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Uganda kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Uganda waliandika bao lao la kwanza katika dakika ya 15 lililofungwa na Kawooya Andrew akiunganisha wavuni krosi ya Najibu Viga huku lile la pili likifungwa na Asaba Ivan katika dakika ya 27 Najib Yiga.Serengeti Boys iliendelea kulala, Yiga aliifungia Uganda bao la tatu na la ushindi na kuifanya Serengeti kushika mkia katika Kundi A na kuacha simanzi kwa wapenzi wa soka nchini. Serengeti Boys inasubiri mchezo wa mwisho dhidi ya Senegal huku Nigeria ikisonga mbele baada ya kushinda mchezo wake wa awali kwenye uwanja huo na kufikisha pointi sita baada ya kushinda ule wa ufunguzi dhidi ya Tanzania. | michezo | 2 |
JUMLA ya watoto 2,345 wenye umri chini ya miaka mitano wamepatiwa chanjo ya Surua Rubella katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida kati ya Januari na Machi, mwaka huu.Mratibu wa chanjo katika halmashauri hiyo, Emmanuel Mawa alieleza kuwa idadi hiyo ya watoto waliochanjwa ni sawa na asilimia 89 ya malengo ya kuwapatia huduma hiyo watoto 2,648. Aidha, alieleza kuwa katika kipindi hicho halmashauri ililenga kufikia jumla ya watoto 2,648 kwenye chanjo ya Penta, lakini walifanikiwa kuwachanja watoto 2,571 ambayo ni sawa na asilimia 97.Alifafanua kuwa licha ya mafanikio hayo, bado kuna baadhi ya wazazi na walezi kutojitokeza kuwapeleka watoto wao kwenye chanjo za aina mbalimbali, hali inayosababisha malengo yanayowekwa na halmashauri kwenye utoaji wa huduma hiyo, kutofikiwa kwa asilimia 100. “Kwa mfano, chanjo ya Surua Rubella tumefikia asilimia 97.Mtu anaweza kudhani kuwa idadi ya asilimia tatu iliyosalia ni ndogo lakini kwa malengo tuliyojiwekea ya kufikia watoto 2,648 na kuchanja 2,345 tu, hapo ni kuzungumzia watoto zaidi ya 300 ambao hawakupata huduma hiyo,” alisema.Uchunguzi wa kina uliofanywa na mwandishi wa habari hizi kuhusu kutofikiwa malengo ya chanjo katika halmashari hiyo, umebaini kuwa moja ya sababu ni imani potofu juu ya chanjo zitolewazo na serikali; dhana ambayo imeenea maeneo mengi ya mkoa huo. Imebainika kuwa baadhi ya wazazi na walezi wanaamini kuwa chanjo kwa watoto huathiri mfumo wa uzazi kwa kundi hilo na kwamba mara baada ya kupatiwa huduma hiyo mtoto huwa tasa au mgumba kwa maisha yake yote.Uchunguzi huo unaonesha kuwa licha ya serikali kuhakikisha inatimiza wajibu wake katika kutoa huduma ya afya kwa watoto wote kwa mujibu wa Sera ya Afya ya mwaka 2007 na kutumia gharama kubwa ili kundi hilo lipate huduma hiyo bila malipo, baadhi ya wazazi hasa wa maeneo ya vijijini bado wanakwamisha juhudi hizo kutokana na imani potofu.Akizindua kampeni ya chanjo katika kituo cha afya Sokoine Manispaa ya Singida, Mkuu wa Wilaya ya Singida, Paskasi Muragili alikemea imani hizo potofu, akisema chanjo zinazotolewa zimefanyiwa utafiti wa kitaalamu na kuonekana kuwa hazina madhara yoyote kwa mtoto. Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kuwa watoto wachanga milioni 22 hawapati chanjo inayostahili, ambapo zaidi ya milioni 1.5 walio na umri chini ya miaka tano hufariki dunia kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuiwa kupitia chanjo, huku wataalamu wakisema chanjo ina tiba ya kuaminika na kwamba inaweza kuzuia vifo kati ya milioni mbili na milioni tatu kila mwaka. | Kitaifa | 0 |
["Kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba yuko tayari kuondoka katika klabu hiyo katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari , huku klabu ya Real Madrid ikiwa na matumaini ya kuanzisha mazungumzo ya kupunguza bei ya Man United ya £126.4m ili kumuuza mchezaji huyo wa Ufaransa huku akiingia miezi 12 ya mwisho katika kandarasi yake. (L'Equipe via AS)", 'Tottenham imeendeleza hamu yake ya kutaka kumnunua mchezaji wa Ajax Donny van de Beek , lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 na raia wa Uholanzi anataka kuhamia Real Madrid, ambao wanajiandaa kutoa dau la £46.2m (De Telegraaf via FourFourTwo)', 'Manchester City na Chelsea wamekuwa na mazungumzo na wawakilishi wa mchezaji wa Barcelona Ousmanne Dembele mwenye umri wa miaka 22 (Eldesmarque via Sun)', 'Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard anaweza kupata zaidi ya £150m kutumia baada ya marufuku ya uhamisho ya klabu hiyo kupunguzwa huku ikiwalenga winga wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 27, pamoja na beki wa kushoto wa Leicester City na Uingereza Ben Chilwell, 22.. (Mail)', 'Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, ambaye amesalia na miezi 18 katika kandarasi yake amejiondoa katika mazungumzo ya kumuongezea kandarasi na yuko tayari kuondoka msimu ujao.. (Mirror)', 'Mkufunzi wa Leicester City Brendan Rodgers anatumai kwamba mkataba mpya aliotia saini utawashinikiza wachezaji nyota kusalia katika klabu. (Times - subscription required)', 'Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anasema kwamba klabu hiyo ingekuwa imemuuza kiungo wa kati wa wales Harry Wilson, ambaye yupo katika mkopo katika klabu ya Bournemouth, iwapo haiamini kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 atasalia katika klabu hiyo. (Guardian)', 'Kocha wa Leicester Brendan Rodgers', 'Klopp anasema kwamba Liverpool inaweza kumsaini mshambuliaji mwenye umri wa miaka 19 raia wa England Rhian Brewster ambaye ataondoka kwa mkopo mwezi Januari.. (Liverpool Echo)', 'Mkufunzi wa wa England Gareth Southgate alisagfiri hadi Itali ili kumtazama beki wa Man United aliyepo kwa mkopo katika klabu ya Roma Chris Smalling, 30, akiichezea klabu yake dhidi ya Inter Milan. (Mail)', 'Crystal Palace imewasiliana na AC Milan kuhusu uwezekano wa kumsaini mshambuliaji wa zamni wa Liverpool Fabio Borini kwa mkopo. (Evening Standard)', 'Mkufunzi wa Napoli manager Carlo Ancelotti na mkufunzi wa zamani w a Tottenham Mauricio Pochettino ni miongoni mwa wale wanaotarajiwa Marco Silva Everton. ', 'Mshambuliaji wa Brazil Gabriel Barbosa, 23, ambaye alifunga magoli 43 katika mechi 56 akiwa kwa mkopo katika klabu ya Flamengo kutoka Inter Milan, akisema kwamba angependelea kuichezea (Mail)', 'Atletico Madrid in mpango kumnunua mshambuliaji wa Paris St-Germain Edinson Cavani baada ya mchezaji huyo wa Uruguay 32 kutochezeshwa mara kwa mara katika klbau hiyo ya Paris. (ESPN)', 'Leicester imeanza mazungumzo na kocha Brendan Rodgers kuhusu mkataba mpya ili kuiwekea ukuta nia ya Arsenal kumnasa kocha huyo. (Telegraph)', 'Kocha wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino hatakuwa kocha wa Bayern Munich.(Bild)', 'Kocha wa zamani wa Juventus Massimiliano Allegri amesema hatarejea kuwa meneja mpaka kipindi cha majira ya joto lakini anafanya mafunzo ya kiingereza kutokana na kuhusishwa na timu za ligi kuu ya England. (ESPN)', 'Manchester United bado wana matumaini ya kumsajili kiungo wa Tottenham Christian Eriksen, 27, mwezi Januari baada ya mchezaji huyo kuwakataa.(Mirror)', 'Mshambuliaji wa Red Bull Salzburg na timu ya taifa ya Norway Erling Braut Haaland, 19, anaweza kuuzwa kwa kitita cha pauni milioni 17 mwezi Januari kwa mujibu wa mkataba wake.(Manchester Evening News via Bild)', 'Chelsea wana mpango wa kumsajili mshambualiaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 27, kipindi kijacho cha majira ya joto.(Independent)', 'Unaweza pia kusoma', 'Mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud, 33, hataiacha klabu hiyo mwezi Januari huku vilabu vinavyomtaka vikiamua kusubiri mpaka mchezaji huyo atakapopatikana kwa uhamisho wa bure. (Sun)', 'Borussia Dortmund wana mpango wa kumbakisha mshambuliaji Jadon Sancho, 19 mpaka mwishoni mwa msimu.(Telegraph)', 'Kocha wa zamani wa Leicester Nigel Pearson amehojiwa kwa ajili ya nafasi ya ukocha katika klabu ya Watford. (Times)', "Kocha wa zamani wa West Ham, Newcastle na West Brom Alan Pardew amesema anapenda kuifundisha Everton lakini amesema kocha wa zamani wa Everton David Moyes 'anafaa kwa nafasi hiyo'.(Mail)", 'Wakala wa mshambuliaji wa Barcelona KOusamne Dembele,22, amekutana na uongozi wa Chelsea na Manchester City. (El Desmarque - in Spanish)', 'West Ham watajaribu kumuuza mlinda mlango Roberto mwezi Januari na kutengana na mkurugenzi wa michezo aliyemuingiza kwenye klabu hiyo.(Guardian)', 'Mshambuliaji wa miaka 17 Ansu Fati ametia saini mkataba mpya wenye kipengele ambacho kitamfanya anunuliwe kwa Pauni milioni 337.5. (FC Barcelona)'] | michezo | 2 |
Walisema, wakulima wengi hawana uelewa wa kutosha kuhusu thamani ya fedha hizo za kigeni na ndiyo sababu wanapohitaji kuzitumia inakuwa vigumu kwao, jambo linalowalazimu kuwatafuta watu waliosoma ambao nao huhitaji fedha ili kuwasaidia.Hali hiyo, inatokana na wakulima wengi kutofahamu mabadiliko ya fedha za kigeni zinazolipwa na makampuni yanayonunua tumbaku na mazao mengine ya wakulima yanayozalishwa kwa wingi katika wilaya hiyo.Mmoja wa wakulima wa kijiji cha Matepwende, Abdallah Ngonyani alisema, makampuni kutumia fedha za kigeni, hususan Dola kuwalipa wakulima ni sawa na kuwaibia kwa kuwa wakulima wengi wanaoishi maeneo ya mashambani huwa hawaji na kiwango cha kubadilisha fedha cha wakati huo.Mbali na hilo alisema huchukua muda mrefu hadi kufika mjini kufuata huduma za kibenki. Ni kwa msingi huo aliiomba Serikali kuanzia msimu huu wa 2015/2016 ikomeshe hali hiyo kwani inawarudisha nyuma wakulima wengi.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Ali Mpenye alisema, tayari ofisi yake imeshawaandikia barua watendaji wa vijiji na kata kuwajulisha kwamba hakuna anayeruhusiwa kununua mazao kutoka kwa wakulimakwa kutumia fedha za kigeni. | Biashara | 1 |
JUZI ilikuwa mwisho kwa mashabiki wa Batista na mchezo wa mieleka kwa ujumla kumshuhudia tena ulingoni nguli huyo akipambana baada ya kutangaza rasmi kustaafu kushiriki mchezo huo wa mapigano.Batista alitangaza azimio lake hilo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram ikiwa ni dakika chache tangu atoke ulingoni kupigana na kushindwa pambano dhidi ya Triple katika Wrestle- Mania 35. Batista, 50 ambaye pia ni muigizaji wa filamu amestaafu akiwa chini ya World Wrestling Entertainment (WWE) akiwa amehudumu katika mchezo huo kwa miaka 20.“Kwa mashabiki wote wa WWE kutoka moyoni kabisa nawashukuru kwa kunipa nafasi ya kuwaburudisha kwa muda wote huo. Leo (juzi) nimefunga rasmi hadithi ya kitabu changu cha mieleka. Nimestaafu rasmi, nitaukumbuka sana ulingo lakini hakuna jinsi nashukuru kwa yote,” ilieleza sehemu ya andiko lake hilo. | michezo | 2 |
Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade alisema hayo Dar es Salaam jana wakati akipokea msaada wa magari mawili kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo nchini Japan (JICA) kwa lengo la kuratibu shughuli za ulinzi katika mpaka wa Tanzania na Uganda na Tanzania na Rwanda.Magari hayo yana thamani ya zaidi ya Sh milioni 90 na yatatumika katika shughuli za kuangalia mipaka ya Uganda, Rwanda na Burundi ili kuzuia mali za magendo.Alisema kwenye mpaka wa Tanzania na Uganda na hata Tanzania na Kenya, wamekuwa wakikamata mali hizo za magendo, huku wengine wakipita usiku na kutokana na kukosekana kwa vifaa vya kuonea jambo hilo lilikuwa likiendelea.“Katika programu hii tutafanya operesheni za pamoja na nchi hizo na hata kama kutatokea kuwepo kwa tatizo la uadilifu watatambuliwa na kukomesha vitendo hivyo,” alisema Bade.Bade alisema kwa mamlaka hiyo kupata magari hayo pamoja na vifaa vingine vya mawasiliano vitawasaidia kufanya operesheni usiku na mchana katika kukomesha mali hizo za magendo.Alisema mbali na msada huo wa vifaa, lakini pia JICA imekua ikisaidia mamlaka hiyo, ikwemo kujenga jengo la Mapato la Tanzania na Kenya na Rwanda (Kisumo) ambayo kwa pamoja yamekamilika.Alisema katika chuo cha kodi, JICA imeshiriki kutoa mafunzo na pia imeendelea kusaini mikataba mingine ya kuendelea kutoa mafunzo pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama katika mali ya mageno inayopita baharini.Ofisa Mkuu kutoka JICA, Nagase Toshio alisema tangu mwaka 2007, JICA imekuwa ikisaidia kuweka mazingira bora ya biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki na kujenga uwezo wa kusimamia vyema mipaka.Alisema Tanzania ikiwa ni njia kwa nchi nyingi za Afrika Mashariki, jambo muhimu ni kuimarisha biashara na kulinda jamii kutojihusisha na bidhaa hatari. | Biashara | 1 |
NICHOLAS Musonye ametangaza kuachia ngazi hivi karibuni kama Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka la Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) baada ya miongo miwili ya kulitumikia baraza hilo.Katika mahojiano maalumu na gazeti moja la Kenya juzi jijini Kigali, kiongozi huyo wa muda mrefu wa Cecafa alieleza mipango yake ya kupata shahada ya udaktari wa falsafa (PhD).Pia Musonye alithibitisha kuwa na nia kubwa ya kutaka kujitosa katika siasa. “Nimepata uzoefu mkubwa, ninajulikana na ninajuana na watu wengi duniani kote katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, na ninataka kufaidi matunda hayo na watu wangu wa Kakamega wakati nitakapokuwa nawatumikia kama gavana. Nategemea watanipatia nafasi hiyo, alisema Musonye.“Nina marafiki ambao waliomba nigombee Nairobi lakini nitafikiria kuhusu hilo na kulitangaza hadharani haraka.” Mwandishi huyo wa zamani wa Nation alijiunga na uongozi wa soka mwaka 2000 wakati alipochaguliwa kuwa katibu wa Cecafa wakati wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Soka, Fifa, uliofanyika Buenos Aires, Argentina.“Sasa ni miaka 20 tangu wakati huo. Kwa kweli mambo mengi yametokea.” “Kutoka mashindano madogo na hadi sasa tumeweza kuandaa mashindano yenye hadhi kama yale ya Kombe la Chalenji, na Kombe la Kagame.“Timu zetu zimepata udhamini na makampuni mbalimbali kama Tusker, MTN, SuperSport, GTV, Serengeti Breweries na Azam TV. Pia tunapata dola milioni moja kila mwaka kuendesha mashindano ya watoto na wanawake, na nusu ya fedha hizo kwa ajili ya kuendeshea ofisi yetu.”“Tumewaendeleza wachezaji mbalimbali kama akina Mariga (Mcdonald), Dennis Oliech, Victor Wanyama, Michael Olunga, Dennis Onyango na vipaji vingine wakiwemo nusu ya wachezaji wa sasa wa timu ya taifa walioshindana katika Michuano ya Mataifa Afrika, Afcon 2019.”“Naondoka Cecafa ikiwa katika hali nzuri na ninawaomba wale watakaoichukua kutoka kwangu waendelee kuandaa mashindano na kuviibua vipaji. Licha ya kazi ngumu iliyopo, kiwango cha soka katika ukanda huu ndio kilikuwa cha chini katika Afcon 2019 nchini Misri.”“Tuna mashindano ya klabu na yale ya Chalenji nchini Uganda Desemba mwaka huu na ninazitaka timu za taifa kujisajili na kushiriki mashindano hayo.” Cecafa ilianzishwa mwaka 1927 na makao makuu yake yakiwa jijini Nairobi, Kenya, Cecafa ina wanachama 12, ambao ni Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan, Sudan Kusini, Tanzania, Uganda na Zanzibar. | michezo | 2 |
['Ghana, Senegal na Ivory Coast zote zilishindwa kufuzu kwa kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN) 2020 siku ya Jumapili', 'Ghana ilishindwa kulipiza bao moja iliyofungwa katika mkondo wa kwanza dhidi ya Burkina Faso, na kutoka sare tasa mjini Ouagadougou.', 'Hii inamanisha kuwa Black Stars hawatashiriki fainali za mashindao hayo ya Cameroon 2020 ambayo yanachezwa na wachezaji wa Afrika katika mataifa waliozaliwa.', 'Senegal, pia ni timu kubwa iliyoondolewa katika fainali hizo baada ya kushindwa na Guinea kupitia mikwaju ya penati.', 'Senegal ilienda Conakry ikiwa kifua mbele kwa bao 1-0 lakini Guinea ilijitutumua katika mechi yao ya nyumbani na kujipatia ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Mamadouba Bangoura.', 'Baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mechi zote, wenyeji walifuzu kupitia mikwaju ya penalti 3-1.', 'Ivory Coast ilishindwa kufuzu katika fainali hizo licha ya kushinda mechi yao ya nyumbani dhidi ya Niger 1-0. ', 'Timu hiyo ilishindwa mabao 2-0 na Niger katika mkondo wa kwanza kumaanisha waliondolewa kupitia wingi wa mabao 2-1 .', 'Siku ya Jumapili pia, Zimbabwe ilijikatia tiketi ya kushiriki mashindano hayo ya Cameroon mwaka 2020 baada ya kutoka sare tasa dhidi ya Lesotho lakini ikafuzu kwa wingi wa mabao 3-1.', 'DR Congo iliichapa Jamhuri ya Afrika ya Kati mabao 4-1 mjini Kinshasa ushindi ambao uliwapatia jumla ya mabao 6-1 huku nao Congo Brazzaville wakifuzu kwa bao 1-0 la nyumbani dhidi ya Equatorial Guinea na kunyakua jumla ya mabao 3-2.', 'Katika eneo la kaskazini,Tunisia ilijikatia tiketi ya mashindano hayo baada ya kupata ushindi wa jumla wa mabao 3-1 dhidi ya Libya.', 'Mali pia itashiriki mashindano hayo baada ya Cameroon, baada ya kuinyuka Mauritania jumla ya mabao2-0. ', 'Nigeria iliathiriwa zaidi katika mashindano hayo baada ya kushindwa na Togo siku ya Jumamosi huku bingwa watetezi Morocco wakipata ushindi dhidi ya Algeria. ', 'Timu zilizofuzu kwa mashindano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani, (CHAN) yatakayoandaliwa na Cameroon:'] | michezo | 2 |
RAIS John Magufuli amewataka Watanzania likiwemo Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kufanya biashara na Wakenya kwa kuwauzia unga wa mahindi.Alitoa kauli hiyo Ikulu, Dar es Salaam jana wakati akishuhudia makabidhiano ya fedha taslimu Sh milioni 170 za Tanzania, Sh 171,600 za Kenya na Dola za Marekani 77,500 zilizoibwa na majambazi mwezi Mei mwaka 2004 baada ya kuvamia Benki ya NBC Tawi la Moshi pamoja na kilogramu 35.34 za dhahabu zilizotoroshwa kutoka Tanzania na kukamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya, Februari mwaka jana.Baada ya makabidhiano hayo, Magufuli alisema miongoni mwa mambo waliyozungumza na Rais Uhuru Kenyatta alipomtembelea nyumbani kwake Chato mkoani Geita mwanzoni mwa mwezi huu ni pamoja na Tanzania kuizuia Kenya unga wa mahindi.Alisema baada ya mazungumzo hayo alizungumza na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo, ili viwanda vya jeshi hilo viwe miongoni mwa vitakavyosaga unga na kuwauzia Wakenya. Rais Magufuli aliwataka Wakenya wawe huru kufanya biashara na Watanzania katika kuhakiksha wanapata kiasi cha unga wanachohitaji.“Rais Kenyatta pia aliniambia Kenya inataka kununua gesi kutoka Tanzania, kwa hiyo Waziri wa Nishati mjiandae kwa hilo lakini pia wanahitaji makaa ya mawe,”alieleza Rais Magufuli.Mmoja wa Maofisa wanaohusika na kilimo wa Kenya alimweleza Rais Magufuli kuwa katika kipindi cha mwaka huu nchi yao imekumbwa na changamoto ya hali mbaya ya hewa kwa kupata kiasi kidogo cha mvua hali iliyosababisha kuwepo kwa uhaba wa chakula hususani mahindi.Alisema kwa wastani Kenya inatumia magunia milioni 4.3 ya mahindi kwa mwezi na miongoni mwa hayo magunia milioni 1.5 husagwa unga.Alisema kipindi cha kuanzia Agosti hadi Novemba mwaka huu watakuwa na changamoto ya uhaba wa chakula. Naye Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, aliwahakikishia Wakenya kuwa Wizara yake iko tayari kutoa ushirikiano ili biashara hiyo iweze kufanyika bila vikwazo kwa kuwa Tanzania ina akiba ya kutosha ya mahindi.Waziri wa Madini, Doto Biteko, alisema kuwa Wakenya ni miongoni mwa watu wanaofanya biashara ya kununua madini hapa nchini.Alisema kuna makampuni matatu ya Kenya yanayonunua dhahabu mkoani Geita. Biashara ya madini Rais Magufuli alisema hatua mbalimbali zilizochukuliwa na serikali yake katika kudhibiti utoroshaji wa madini ikiwemo kufanya mabadiliko ya sheria, kuanzishwa kwa masoko 28 ya madini, kupunguza kodi, kujenga ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite huko Mirerani, kumesaidia kuongeza mapato ya serikali yatokanayo na madini.Alisema katika mwaka 2017/18, serikali ilipanga kukusanya Sh bilioni 191 lakini ilivuka lengo kwa kukusanya Sh bilioni 301, mwaka 2018/19 ilipanga kukusanya Sh bilioni 310 lakini ilikusanya Sh bilioni 335 na katika mwaka 2019/20 wanatarajia kukusanya Sh bilioni 470 au zaidi.Baada ya kauli hiyo ya Rais, Waziri Biteko alisema tangu masoko ya madini yaaanzishwe maeneo mbalimbali nchini, soko la dhahabu la Chunya lilikuwa linapata kilo 12 tu kwa mwaka lakini tangu soko hilo lifunguliwe mwezi Machi mwaka huu, kiwango hicho kimeongezeka hadi kufikia kilo 270.“Mkoani Geita zaidi ya kilo 736 za dhahabu zinauzwa na jumla ya Sh bilioni 137.6 zimefanyiwa biashara katika masoko yote nchini na serikali imepata mrabaha wa Sh bilioni 7.7,”alieleza Biteko.Kuhusu leseni za uchimbaji alisema kuwa hivi hivi karibuni wanatarajia kutoa leseni mbili kwa ajili ya uchimbaji mkubwa wa madini ambao mtaji wake unafikia Dola za Marekani milioni 100, lakini pia wameshatoa leseni 32 za uchimbaji wa kati, leseni 2,675 za uchimbaji mdogo na leseni za utafiti wa madini 105. | Kitaifa | 0 |
Nyamohanga aliyasema hayo kwenye sherehe za uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini unaofadhiliwa na REA, uliofanyika katika kata ya Shishiyu wilayani Maswa mkoani Simiyu.Alisema kuwa Mradi wa REA Awamu ya Pili, utaviwezesha vijiji vilivyounganishwa na umeme 3,734, kati ya vijiji 15,180 ambayo ni asilimia 24.6 kufikia vijiji 5,234, ambayo ni asilimia 34.5 ifikapo mwezi Juni mwaka huu.Aliongeza kuwa mradi wa REA Awamu ya Pili wa miaka miwili, ulioanza mwaka 2013, lengo lake lilikuwa ni kuhakikisha kuwa vijiji vyote Tanzania vinapatiwa umeme hivyo kuboresha maisha ya wananchi na kukuza uchumi wa nchi.Akielezea mchango wa mradi wa usambazaji wa umeme vijijini, unaotekelezwa na REA katika kuboresha maisha ya wananchi Nyamohanga, alisema kuwa awali wananchi wote walikuwa wakilipa Sh 467,000 kama gharama ya kuunganishiwa umeme, ambayo ilikuwa ni kubwa, hivyo kufanya wananchi wachache wenye uwezo kuwa na nishati ya umeme huku kundi kubwa la wasio na uwezo kuishi gizani.Alisema katika Awamu ya Kwanza ya REA, gharama za uunganishaji wa umeme zilishuka kutoka Sh 467,000 hadi Sh 177,000 na kuongeza kuwa katika kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na uwezo wa kuunganishiwa umeme, Serikali iliamua kubeba gharama zote kupitia REA Awamu ya Pili na wananchi kutakiwa kuchangia Sh 27,000 tu kama Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).Alieleza kuwa mara baada ya kumalizika kwa Awamu ya Pili ya REA, viongozi wataainisha vijiji ambavyo havijapata umeme REA Awamu ya Pili, ambapo vitajumuishwa katika mradi wa REA Awamu ya Tatu.Nyamohanga alieleza michango mingine kuwa ni kufungua fursa za ajira na uwekezaji kwa vijana, ufaulu kuongozeka kwa shule za sekondari na kuboreshwa kwa huduma za afya.“Kwa mfano kwa shughuli za kiuchumi bei ya kusaga debe la mahindi ilikuwa ni Sh 1,000 itashuka hadi Sh 500 kutokana na kwamba mashine za kusaga zitakuwa zinatumia umeme badala ya dizeli kama zamani,” alisema Nyamohanga.Wakati huohuo, Meneja wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda ya Ziwa, Joyce Ngahyoma akielezea jinsi ya kuunganishwa na huduma ya umeme kwa wananchi wa vijiji vilivyopitiwa na mradi wa REA Awamu ya Pili, alisema kuwa wananchi wanaoishi mita 30 karibu na miundombinu ya umeme, wataunganishiwa kwa Sh 27,000 na kuwataka kuchangamkia fursa hiyo kwa kuboresha makazi yao.Alisema kwa wananchi wenye nyumba zenye vyumba viwili na vioski, hawahitaji kufunga mfumo wa umeme kwenye nyumba zao (wiring), badala yake watashauriwa kununua kifaa maalumu kijulikanacho kama “UMETA” (Umeme Tayari), kinachoweza kutumika kama mfumo kwa kuwa na uwezo wa kuunganisha taa mbili na vifaa vingine kama vile jiko, friji na pasi. | Biashara | 1 |
UKIFUNGUA kitabu cha Klabu ya Barcelona inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) na kukisoma kwa miaka ya hivi karibuni utagundua ya kwamba mashabiki wa timu hiyo wanaamini kama mchezaji wao, Lionel Messi akikosekana kwenye mechi yoyote hasa ya watani wao wajadi dhidi ya Real Madridi dabi ya El Classical basi hawawezi kupata ushindi.Hii inatokana na namna mchezaji huyo alivyojijengea ufalme wake wa kucheza soka la kiwango cha juu na wakati mwingine anakuwa msaada na mkombozi mkubwa kwa kuamua matokeo muhimu pale timu inapokuwa imepotea na kushindwa kupata ushindi kwenye mechi muhimu ambao unaweza kuisaidia timu kuivusha kwenye nafasi moja hadi hatua nyingine muhimu.Kwa kujua hilo basi na kutoa huko barani Ulaya na kukusogeza kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL), hapa tunaangalia kwenye timu ya Simba miongoni mwa timu vigogo kwenye ligi hiyo namna walivyopata kuwa na wachezaji walijenga ufalme na umaarufu kulingana na kiwango chao kilichowakosha mashabiki na wao kuendelea kuamini bila wao huwezi kuwaeleza chochote.Mashabiki hao imefikia wakati kama wachezaji hao watakosekana kwenye michezo hasa ya watani wa jadi hawawezi kupata matokeo chanya. Makala haya yanaanga- zia kuanzia miaka ya 2000 hadi tulipofikia sasa ni nyota gani walitikisa kwa nyakati tofauti ndani ya timu hiyo na walipata kuisumbua timu hiyo na viongozi wake kwa nyakati tofauti kutokana na umaarufu waliojijengea.JUMA KASEJAUkitaja jina la Kaseja ambaye kwa sasa anaitumikia timu ya KMC, kila mtu atakuwa anamfahamu hususani mashabiki wa Simba, ni miongoni mwa walindamlango waliopata kutokea kwenye timu hiyo, alikuwa anadaka mpira kwa uhodari mkubwa hasa kwenye masuala ya matuta huwezi kumtoa kutokana kuwa na uwezo mkubwa wa kumsoma mchezaji anapoenda kupiga penalti. Mlindamlango huyo aliidakia Simba kwa mafanikio makubwa, ikiwemo kuchukua mataji ya Ligi Kuu Bara na kushiriki kwenye michuano ya kimataifa yaani Ligi ya Mabingwa Afrika Caf na Shirikisho.Lakini kupitia umaarufu wake alikuwa anaisumbua timu hiyo kwa nyakati tofauti na kupeleka kutia presha kubwa kwa mashabiki hasa unapokaribia mchezo wa watani wa Jadi kati ya Simba na Yanga.HENRY JOSEPH ‘SHINDIKA’Shindika (Fundi ) jina hilo lilitokana na uwezo mkubwa wa kumiliki sehemu ya kiungo ingawa mchezaji huyu kwa nyakati tofauti alikuwa anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji alikuwa miongoni mwa wachezaji hatari waliopata kutokea kwenye timu hiyo na walikuwa wanaulazimisha mpira kufanya kile akili yake inachokifikiria. Mchezaji huyo kwa sasa anaichezea timu ya Mtibwa Sugar kutokana na uimara wake wakati anakipiga katika kikosi cha wekundu nguli alipata unahodha kwenye kikosi hicho na timu ya soka ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kutokana na uwezo wake wa kuficha mpira na kutoa pasi kwa wakati sahihi.HARUNA MOSHI ‘BOBAN’BOBAN ambaye alikuwa anakipiga kwenye klabu ya Yanga kuanzia katikati ya msimu wa 2018 /19 na kufanikiwa kuifikisha timu hiyo kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo huku Simba akifanikiwa na kutetea ubingwa huo kwa mara ya pili kwa tofauti ya pointi sita. Wakati akiwa Simba enzi zake alikuwa anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji alikuwa anakinukisha vilivyo kwa kuwatesa wapinzani wake hasa eneo la kutoa pasi za mwisho na zenye macho ambazo zilikuwa zinaifanya safu ya ushambuliaji kuwa hatari kwa kupachika mabao.Kutokana na uwezo wa kumiliki mpira na kutoa pasi zenye macho kiliwafanya mashabiki wa timu hiyo kumuamini nyota huyo kwenye kila mchezo na kwamba akikosekana kikosi hicho akiwezi kupata ushindi. Ingawa Bobani alikuwa ana utovu wa nidhamu nje ya Uwanja kwa kufanya makosa lakini pindi alipokuwa anaingia uwanjani alikuwa anafanya kazi yake ipasavyo tena kwa kutimiza majuku yake kama mchezaji.JONAS MKUDEMkude kwa miaka ya hivi karibuni mashabiki wa Simba huwezi kuwaeleza chochote kupitia kwa kiungo wao huyo, ambaye ni zao la timu hiyo aliyelelewa hapo na kuanza kucheza , nafasi ya kiungo wa kati kwani mashabiki wa kikosi hicho wanaamini kwamba mchezaji huyo kama atakosekana kwenye mchezo dhidi ya watani wao Yanga hawezi kupata matokeo chanya kama hatakosekana.Ugonjwa wa mashabiki kumuelewa mchezaji huyo umewafanya nao viongozi wa timu hizo kuingia kwenye mkumbo huo wakiendelea kuamini hivyo. Ndiyo maana hata sakata linaloendelea kwa sasa kuhusu usajili limekuja juu hadi bosi wa timu hiyo Mohamedi Dewji MO kulazimika kutoa ufafanuzi na kuwatoa mashabiki wasiwasi kwani kiungo huyo bado anaendelea kulazimisha ndani ya kikosi hicho.EMMANUEL OKWINi mchezaji raia wa Uganda anayecheza kwenye nafasi ya ushambuliaji ni miongoni mwa nyota ambao huwezi kushindwa kuwataja pale unapozungumzia mafanikio ya Simba kwa siku za hivi karibuni.Mchezaji huyo amekuwa lulu hapo Msimbazi kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kuwachambua wachezaji wa timu pinzani na kuwa na macho ya kuona lango kisha kutumbukiza mpira wavuni. Tangu mchezaji huyo ajiunge na kikosi hicho msimu wa mwaka 2009 amejizolea umaarufu mkubwa na kuwa kipenzi cha mashabiki na hata kuwagawa baadhi ya viongozi ambao kwa namna moja hama nyingine walikuwa wanaegemea upande fulani, lakini sasa ameanza kufunikwa na Meddie Kagere.MEDDIE KAGEREBora usimchezeshe Okwi, lakini wapenzi wa Simba kwa siku za hivi karibuni wanaweza wasikuelewe endapo Kagere atakuwa nje ya uwanja na timu hiyo ikapata sare au kufungwa. Kagere amebeba nyoyo za wapenzi wa Simba na licha ya msimu huu kuwa wa kwanza kwake kuichezea timu hiyo lakini ametoa mchango mkubwa kuiwezesha timu hiyo kutetea taji lake baada ya kufunga mabao 23 na kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2018/2019. | michezo | 2 |
WIZARA ya Biashara na Viwanda imesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inatekeleza sera ya biashara huria, hivyo haina sababu ya kuingilia kati bei za bidhaa za vyakula zinazozalishwa nchini ikiwemo mikate.Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Hassan Mohamed Hafidh wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Kijitoupele, Ali Suleiman aliyetaka kujua kwa nini serikali haiingilii kati bei ya mikate ambayo imekuwa ikipanda kiholela.Hafidh alisema kutokana na mabadiliko ya dunia na sera za biashara, serikali imetangaza rasmi kujitoa katika suala la kupanga bei za bidhaa zinazozalishwa nchini na nje.Alisema katika mabadiliko hayo, serikali kwa ujumla imeondoa tume ya bei ambayo ilikuwa ikifanya kazi ya kupanga bei za bidhaa zinazozalishwa nchini.Kuhusu kupanda kwa bei ya mikate maarufu ya boflo, Hafidh aliwataka wafanyabiashara na wazalishaji wa mikate hiyo kuongeza ubora wa bidhaa hiyo.Alisema mikate ya boflo inayozalishwa Pemba inao ubora wa hali ya juu tofauti na inayozalishwa Unguja ambayo hairidhishi.‘’Serikali haipo tayari kuingilia kati masuala ya bei ya bidhaa zinazozalishwa nchini ikiwemo mikate ya boflo lakini sisi tunachosisitiza zaidi ni ubora | Biashara | 1 |
MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) imewataka wazalishaji wanaotakiwa kutumia stempu za kodi za kieletroniki (ETS) kuendelea kutumia stampu hizo zilizopo kisheria ili waweze kufahamu bidhaa zao halisi zinazoingia sokoni ili kulinda viwanda na walaji wao.Kamishna Mkuu wa TRA, Dk Edwin Mhede Mhede ameyasema jana alipotembelea Kiwanda cha Uzalishaji wa Bia cha Tanzania (TBL) mkoani Mbeya ili kujione namna stempu za kodi za kieletroniki zinazofanya kazi katika kiwanda hicho.Alisema ETS inasaidia kukusanya taarifa sahihi si kwa matumizi ya kukadiria kodi pekee bali inamsaidia pia mzalishaji kujua kiasi alichozalisha na kwa muda gani lakini pia itamsaidia kuona kama kuna changamoto yoyote kuifanyia kazi mapema kitu ambacho ni muhimu sana katika shughuli za uzalishaji. “Ujumbe wangu kwa wazalishaji wengine ni kwamba waendelee kutumia stampu za kodi za kielektroniki kama ambavyo tumeelekezwa na sheria na taratibu za kodi kwa kuwa inasaidia kuongeza ufanisi katika uzalishaji na kuweka taarifa sahihi za uzalishaji huku zikilinda walaji kwa kupata bidhaa halisi,” alisema.Kwa upande wake Meneja wa TBL mkoa Mbeya, Godwin Fabian alisema kiwanda chake kinaamini kwamba ETS ni msaada mkubwa kwa wazalishaji kwa kuwa inawezesha kugundua bidhaa zisizo halali na zinazoingia sokoni bila kufuata taratibu za uzalishaji na lakini pia inasaidia katoka ulipaji sahihi wa kodi. “Ujumbe wangu kwa wazalishaji wengine waone ni kitu kizuri na wasiogope kutumia stempu za kodi kieletroniki kwa kuwa kama bidhaa zote zitawekwa stempu hizi itasaidia kufahamu bidhaa zisizo halali zinazoingia sokoni na hivyo mfumo huu utasaidia kukabiliana nazo,” alisema Meneja huyo.Kwa mujibu wa TRA, Matumizi ya Stempu za Kielektroniki za Kodi kwa bidhaa zinazotozwa Ushuru wa Bidhaa yalianzishwa kuchukua nafasi ya matumizi stempu za karatasi ambazo matumizi yake yalihusishwa na vitendo vya ukwepaji kodi pamoja na bidhaa bandia kwa kiasi kikubwa.
| Biashara | 1 |
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora imesema, asali ni kipaumbele chake cha kwanza katika uwekezaji na kuna hamasa kubwa kuchangia ujenzi wa kiwanda cha zao hilo la nyuki.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Martha Luleka ametoa msimamo huo wakati anazungumza na timu kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) iliyokwenda Sikonge kuzifahamu fursa zilizopo za biashara na uwekezaji.“Mimi nataka nikubaliane na na falsafa ya Simiyu, Simiyu wao wamesema hivi, one product one district (Wilaya moja bidhaa moja). Hatuwezi kwamba Kaliua wanataka watengeneze kiwanda cha tumbaku na sisi nae tunataka tutengeneze kiwanda, why (kwa nini), unnessesary competition (ushindani usio na umuhimu), tuwaache wanaotaka kutengeneza kiwanda cha tumbaku, mimi siwajui akina nani, sisi huku tumejikita mazao mengine. Tutalima tumbaku, tutaenda kuwapelekea kama kikianza kiwanda wapi sijui, Urambo, tutapeleka, eeh, na wenyewe wajikite waboreshe na sisi tutawapelekea zao hili (asali). Kwa hiyo huko kwenye ushindani wa tumbaku na kiwanda hicho mimi naomba nisiwepo huko” amesema ofisini kwake.Kwa mujibu wa Luleka, watu na taasisi mbalimbali wamehamasika sana kuchangia ujenzi wa kiwanda cha asali Sikonge, na kwamba, tayari kuna eneo, na yanaandaliwa malipo ya fidia kwa wananchi yatakayotokana na mapato ya ndani.“Upembuzi yakinifu unaendelea kufanyika, lakini kwenye suala la funding (upatikanaji wa fedha) tunataka hata kujiuliza tumchukue nani kwa jinsi watu walivyopata hamasa ya kuja kuwekeza hapa, niwataje tu kwa kifupi. Kupita kwa barabara hii ya lami tayari Tanroads (Wakala wa Barabara Tanzania) walishatuwekea milioni 500 ya kuja kuwekeza kwenye kiwanda cha asali kwa sababu waliuliza sisi tunataka tuwagawie gawio katika mradi mmoja ambao utaambatana na kupita kwa barabara, sisi tumechagua kiwanda cha asali...“Juzi katika mazungumzo na Benki ya Wakulima wale nao wanasema wanangojea upembuzi yakinifu ukiwa tayari tuwapelekee wapo tayari. Na nadhani kuna mmoja nitakuwa nimemsahau na yeye ana hamasha ya kuja kuwekeza kwenye asali hiyo kwa hiyo suala la funding ya kiwanda au uwekezaji katika hilo uko bayana kwa kweli tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo” amesema Luleka.Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge mkoani ipo kwenye mchakato wa kujenga kiwanda cha asali na imekaribisha wawekezaji wa viwanda vya bidhaa zinazotokana na zao hilo la nyuki.Luleka amesema, kiwanda hicho kitaongeza thamani na matumizi ya asali inayozalishwa kwa wingi wilayani humo. Amesema, kuna warina asali zaidi ya 6500 wilayani Sikonge wanaozalisha tani 2,000 na kama watawezeshwa na mnyororo wa ongezeko la thamani wataweza kuzalisha tani 6,000 hadi 7,000.“Kwa hiyo mwekezaji asiwe na wasiwasi kwamba pengine malighafi itashuka hapana, sana sana itaongezeka kwa sasa wanafanya tu kwa mazoea yao ya kupata mapato kama ilivyokuwa awali lakini ikija kiwanda kikakaa sawa tutakuwa na warina asali wakubwa” amesema Luleka. | Biashara | 1 |
WANAWAKE watatu na mwanamume mmoja wameuawa mkoani Shinyanga, kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za miili yao katika matukio tofauti, yanayohusu wivu wa mapenzi na kugombea mali.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Richard Abwao alisema katika tukio la kwanza mkazi wa kitongoji cha Mhida Kijiji cha Busagi Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama, Zainabu Shija (28) ameuawa katika tukio linalohusishwa na wivu wa mapenzi.Abwalo alisema Zainabu aliuawa hivi karibuni na mtu aliyefahamika kwa jina moja la Emmanuel, akishirikiana na wenzake wawili kwa kumkata mapanga na kitu chenye ncha kali usoni na kichwani. “Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi baada ya marehemu kukataa kurudi kwa mtuhumiwa ambaye alimfukuza kutokana na kutopata mtoto kwa muda mrefu, lakini alipoolewa na mwanamume mwingine alipata mtoto,” alisema Abwao.Kamanda huyo alisema katika tukio jingine, wanandoa wakazi wa Masengwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Nyamizi Mserengeti (40) na muwewe, Manyara Nderema (48) wameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni baada ya kuvamiwa usiku wakiwa wamelala.Kamanda Abwao alisema chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa kifamilia kuhusu mashamba yanayomilikiwa na Nderemo, ambayo aliyanunua kutoka kwenye familia yao. Kamanda huyo alisema watuhumiwa sita wamekamatwa kuhusu tukio hilo, wanne kati yao wilayani Nzega mkoani Tabora wakijaribu kutoroka.Katika tukio la tatu, Kamanda Abwao alisema Ester Samweli (35) mkazi wa Ndembezi Manispaa ya Shinyanga, ameuawa kwa kupigwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya wananchi kujichukulia sheria mkononi.Alisema chanzo cha tukio hilo ni marehemu kutuhumiwa kuiba mafungu sita ya mboga aina ya chainizi na mahindi mabichi matatu katika soko la Kitangili. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. Kamanda Abwao alisema juhudi za kuwatafuta waliohusika na matukio hayo, zinaendelea na uchunguzi ukikamilika, watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili. | Kitaifa | 0 |
WANACHAMA wa Yanga wamekubali kufuta kesi Mahakamani ili kuruhusu kuendelea kwa mchakato wa uchaguzi mdogo kufanyika kujaza nafasi zilizowachwa wazi.Uchaguzi huo uliokuwa ufanyike mwishoni mwa wiki iliyopita, ulisimamishwa baada ya baadhi ya wanachama wa klabu hiyo kutoka baadhi ya mikoa kufungua kesi Mahakamani kuzuia usifanyike.Akizungumzia hayo Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Malangwe Mchungahela amesema baada ya kufuatilia walijiridhisha kesi hizo zilijikita kwenye malalamiko makuu matatu huku pia, baadhi yao wakibainika si wanachama hai wa klabu hiyo.Ametaja malalamiko ya wanachama hao ni kutaka kujua uhalali wa wale wenye kadi za zamani za CRDB na Benki ya Posta na ufafanuzi wa kukataliwa majina katika baadhi ya matawi kuingizwa kwenye reja za wanachama.Pia, kuwepo sintofahamu ya Mwenyekiti wa Yanga hivyo kusababisha baadhi ya wanachama wenye sifa za uongozi kuwa na mashaka ya kujitokeza.“Kamati ya Uchaguzi licha ya kuchambua yote hayo imebaini kuwa walalamikaji wote kasoro mmoja sio wanachama hai wa Yanga, nimepeleka ujumbe kwao kuwa uwanachama wao una hitilafu ya kikatiba hivyo, hawakuwa na sifa,”amesema.Alisema Katiba ya Yanga, TFF na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) na Duniani (Fifa) haziruhusu wanachama wao kupeleka kesi Mahakamani, huku akisema utaratibu huo hauna tija mbali ya kuiondolea klabu sifa ya kuheshimu taratibu.“Malalamiko yao yote yatatatuliwa kwa taratibu zilizo ndani ya shirikisho, hivyo hawana budi kuondoa kesi hizo Mahakamani mara moja,”alisema na kuongeza kuwa walalamikaji wote wamewaelewa na wamekubali kuondoa kesi hizo.Amesema Kamati ya Uchaguzi itawasiliana na vyombo vingine na kuyafanyia kazi malalamiko hayo ndani ya siku saba kuanzia juzi na baada ya hapo, itatangaza tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi huo mdogo.Aliwataka wanachama wa klabu hiyo kutambua kwamba viongozi watakaochaguliwa hawatakuwa na kipindi cha zaidi ya miaka miwili kabla ya mchakato wa Uchaguzi Mkuu kuanza.Kabla ya kusimamishwa kwa uchaguzi huo, tayari baadhi ya wagombea walianza kampeni za kujinadi.Nafasi zinazotakiwa kujazwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wanne | michezo | 2 |
LICHA ya Simba kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City juzi, Kocha wake, Patrick Aussems amesema hajaridhishwa na maamuzi ya mchezo huo.Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, wekundu hao walitangulia kufungwa kipindi cha kwanza, kisha wao kusawazisha na kupata bao la ushindi kipindi cha pili.Akizungumza baada ya mchezo huo, Aussems amesema tangu wapate penalti mbili katika moja ya mchezo uliopita dhidi ya KMC ambazo zililalamikiwa, waamuzi wamekuwa hawatoi tena nafasi hizo kwenye sehemu walikostahili.“Leo (juzi) sina furaha na maamuzi kwa sababu kuna sehemu hatukutendewa haki,”alisema na kuongeza kuwa jambo la muhimu wanashukuru kwasababu wamepata pointi tatu.Kocha huyo aliwapongeza wachezaji wake kwa kuendelea kucheza kwa kujitolea akisema wamekuwa mashujaa wasiokata tamaa.“Wachezaji wameendelea kuonyesha kiwango bora, wanacheza kwa kujitoa bila kukata tamaa, najivunia ubora wao wa hali ya juu,”alisema Aussems.Simba inatarajia kucheza mchezo mwingine leo dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa huko Mbeya.Kwa upande wake, Kocha wa Mbeya City Ramadhan Nswanzirimo naye pia, ametoa lawama hasa kwa kocha msaidizi namba moja wa mchezo huo akisema hakuwa sahihi katika baadhi ya maamuzi.Alisema sio kwamba Simba haikustahili kushinda isipokuwa faulo wanazopewa nyingine sio sahihi kwao kwasababu inawatengeneza nafasi ya kufunga.“Sijafurahishwa kwasababu hatukustahili kupoteza mchezo ila waamuzi ndio wenye kuamua matokeo ya mchezo, walitoa faulo kwa Simba ambayo haikustahili,”amesema huku akiongeza anawapongeza wekundu hao kwa kushinda.Nswanzirimo alisema kinachoonekana mpira wa sasa unaendeshwa kwa pesa hivyo, timu yenye pesa ndio iliyoshinda. | michezo | 2 |
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza, lengo la hatua hiyo ni kuzifanya shughuli hizo zitoe ajira zaidi kwa vijana.Mahiza aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akimkaribisha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani, alipofanya ziara iliyolenga kukagua shughuli za Mamlaka ya Bandari (TPA) Tanga.Shughuli kuu inayofanywa kwenye bandari hizo 19 zisizo rasmi zaidi alisema ni ushushaji wa mizigo mbalimbali kutoka mjini Zanzibar, Mombasa na Brazil ambako bidhaa kama nguo na sukari hununuliwa kwa nusu ya bei iliyoko sokoni hapa nchini.Alisema kutokana na changamoto ya uwepo wa bandari hizo bubu katika wilaya za Pangani, Muheza, Tanga na , uongozi wa mkoa umeamua kubuni mpango ambao utatumia tatizo hilo kama fursa ya kuongeza ajira kwa vijana na serikali kupata mapato.“Hali ya ulinzi na usalama iko vizuri lakini changamoto iliyopo ni uwepo wa bandari bubu nyingi ambazo hutumika kukwepa kodi kutokana na wafanyabiashara kuingiza bidhaa mbalimbali ikiwemo sukari kutoka nchini Brazil, hatua ambayo inaathiri sana ushindani katika soko kwa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini,” alisema Mahiza.Aliongeza: “Baada ya kuona bandari bubu hizi ni changamoto, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huu imeona kuzifunga halitakuwa suluhisho, badala yake imekuja na wazo ambalo tumeanza kulifanyia kazi.”Akizungumzia sukari ya magendo inayoingizwa nchini kupitia bandari bubu ya Kigombe ambayo ilikamatwa mwezi uliopita, mkuu huyo alisema tayari wamekamilisha taarifa za uchunguzi na wahusika watachukuliwa hatua.“Mheshimiwa Waziri, tunaunga mkono agizo la Rais wetu la kupiga marufuku uingizwaji wa sukari kutoka nje ya nchi na kwa upande wetu kimkoa tayari unazo taarifa za vyombo vinavyohusika na biashara hiyo,” alisema.Alisema mkoa umeshajua vyombo vinavyohusika kuingiza sukari ya magendo ni vya akina nani, wanaishi wapi na maeneo yote ikiwemo nyumba wanakohifadhia hiyo sukari kutoka Brazil.“Changamoto tuliyonayo kwa sasa, tumebaini kwamba sukari hii inahusishwa na watu wazito wakiwemo viongozi wa kisiasa na kiserikali ambao wanazo kinga zao kisheria,” alisema.Mkuu huyo alimweleza waziri kwamba pamoja na changamoto ya wasambazaji hao hivi sasa mkoa unaendelea kuelimisha wananchi katika wilaya zote zenye bandari bubu ili kuwawezesha wakazi kutumia haki na wajibu wao kisheria kuhusu tatizo hilo.Waziri Ngonyani alisema dhana hiyo ya kushushia mizigo katika bandari bubu itakuwa na maana endapo tu uongozi wa mkoa utajiridhisha kwamba hapatakuwepo na namna yoyote ile ya ukwepaji wa kodi ya serikali. | Biashara | 1 |
UONGOZI wa timu ya Biashara United umeanzisha Wiki ya Biashara inayojulikana kama Biashara Family Week iliyoanza juzi na kilele chake kinatarajiwa kuwa Jumapili ya wiki hii kwa mchezo wa kimataifa dhidi ya Tusker ya Kenya. Mwenyekiti wa klabu hiyo, Sulemani Mataso alisema jana lengo la kuanzisha tamasha hilo ni kurudisha fadhila kwa mashabiki wa timu hiyo walioisapoti timu hadi kubakia kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara. Alisema kupitia tamasha hilo, watatangaza kikosi watakachokuwa nacho msimu ujao wa ligi na kutambulisha wachezaji waliosajiliwa.“Pamoja na kurejesha shukrani kwa mashabiki, lakini pia kupitia mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa, timu itapata maandalizi mazuri kwa ajili ya Ligi Kuu,” alisema Mataso. Alisema kupitia wiki hiyo wanachama na wakereketwa wa timu hiyo, wanafanya shughuli za kijamii ikiwemo kufanya usafi kwenye vituo vya Afya, na kutoa misaada kadhaa.Biashara inakuwa miongoni mwa timu zilizofuata nyayo za Simba kuwa na wiki yake ambapo wachezaji, wanachama na mashabiki wake hufanya shughuli za kijamii kisha kuadhimisha kwa mechi ya kirafiki ya kimataifa ambapo hutambulisha kikosi kipya, wengine waliofanya hivyo ni Ndanda miaka ya nyuma na mwaka huu, Yanga imefanya hivyo mwishoni mwa wiki. | michezo | 2 |
Rais John Magufuli amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila kuhakikisha serikali inagharamia matibabu ya mtoto aliyelawitiwa mkoani Mbeya.Mama wa mtoto huyo mwenye umri wa miaka 9, aliyejitambulisha kwa jina la Swaumu, alimwambia Rais Magufuli jana, Ijumaa kuwa mwanaye ana hali mbaya kiafya ikiwa ni pamoja na kutokwa na haja kubwa mfululizo, baada ya kulawitiwa na mwanaume wa miaka 53.Mama huyo alieleza kuwa hatahivyo amekuwa hapati ushirikiano wa kutosha kutoka kwenye vyombo vya dola. Akizungumza leo, Jumamosi katika viwanja vya Sabasaba, alipokuwa akifungua barabara ya Mbeya-Lwanjilo-Chunya na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Chunya- Makongolosi, Rais Magufuli amesema amefatilia kesi hiyo na mwanaume huyo amehukumiwa kifungo cha maisha.“Nilituma watu wangu waende gerezani kuangalia kama mtuhumiwa huyo yupo, na ni kweli walimkuta na wakampiga picha wakaniletea, na ninampongeza Hakimu Mkazi Michael Mteite, aliyetolea hukumu kesi hiyo,” alisema.Aliongeza kuwa jina la Hakimu huyo Mteite lipelekwe kwenye mapendekezo kwa Jaji Mkuu, kwa majina yatakayoteuliwa Ujaji, ili naye awe Jaji. | Kitaifa | 0 |
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Halima Bulengo (CCM). Mbunge Halima alitaka kujua kwa nini vituo vya reli vikubwa kama Morogoro, Dodoma, Tabora na Mwanza havijawekezwa huduma muhimu kama maduka na hoteli.Ngonyani alisema serikali inashangaa kwa nini wafanyabiashara hawachangamkii kuwekeza katika vituo vya reli ambayo ni fursa muhimu kwa biashara. “Hata hivyo wizara itawashauri TRL kuwahamasisha wafanyabiashara kuwekeza biashara na huduma kwa ajili ya wasafiri katika vituo hivyo,” alisema.Akijibu swali la Mbunge Halima aliyehoji serikali ina mkakati gani kuboresha huduma za maji, vyoo na sehemu za kukaa wakati wa mvua ili kuwaondolea adha akinamama na watoto.Ngonyani alisema TRL ina stesheni 124 katika mtandao wake wa reli, na tayari imeshaanza ukarabati wa stesheni za reli ambapo pamoja na mambo mengine imezingatia uboreshaji wa mifumo ya maji, vyoo na sehemu za kukaa abiria wakati wa mvua kwa kutumia vyanzo vya ndani vya mapato.Alisema stesheni zilizokishwa karabatiwa ni Kigoma, Kaliua, Pugu, Malindi na Mwanza ambacho ukarabati wake bado unaendelea. Ngonyani alisema kampuni inatambua changamoto ya ukosefu wa baadhi ya huduma katika stesheni za reli kutokana na kuwa na miuondombinu chakavu. | Biashara | 1 |
KOCHA wa JKT Tanzania, Bakari Shime amesema mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere amekuwa wa kwanza kuharibu rekodi yao kwa msimu huu baada ya kufunga mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga juzi.Akizungumza jana, Shime alisema huu ni mchezo wa 11 wakicheza na walikuwa hawajafungwa ila Kagere ameharibu rekodi yao, kwani bao la kwanza kufunga liliwatoa mchezoni na kupoteza umakini.“Kagere alifunga bao la kwanza dakika ya 13 ambalo lilikuwa jepesi na aliongeza la pili dakika ya 39 akimalizia mpira uliotemwa na kipa Abdulrahman Mohamed na kufanikiwa kuharibu rekodi yetu kwani tangu ligi ianze hatujaruhusu bao kipindi cha kwanza,” alisema Shime.Pia Shime amesema wanajiandaa na mechi dhidi ya Mbeya City itakayochezwa Uwanja wa Sokoine Mbeya, Novemba 8 na kuhakikisha wanafanya vizuri baada ya makosa waliyofanya katika mechi dhidi ya Simba.Simba kwa sasa imefikisha pointi 26 nyuma ya Azam FC wenye pointi 27 na JKT wamefikisha pointi 18 baada ya kucheza mechi 12 na kushika nafasi ya saba. | michezo | 2 |
MSHAMBULIAJI wa Aston Villa na timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta amesema wamejikisia vibaya kupoteza mchezo huo wa Ligi Kuu England dhidi ya Bournemouth. Samatta ambaye alicheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya England na kufunga bao lakini walifungwa mabao 2-1 na Bournemouth katika Uwanja wa Vitality alisema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo huo. “Tumesikitishwa, hatukupata kile tulichokihitaji. Wakati wote ukipoteza mchezo kunakuwa na wakati mgumu, amesema Samatta. “Sijazoea vizuri mazingira ya England, nitazoea haraka kwa sababu ninatokea ligi ya Ubelgiji, japo ushindani hapa ni mkubwa kwa hiyo inanibidi nielewe kila kitu na nikielewa nitakuwa na wakati mzuri zaidi wa kuisaidia timu,”aliongeza. Samatta alifunga bao kwa kichwa dakika ya 70 akiunganisha mpira uliopigwa na mshambuliaji David Keinan kisha kuwababatiza walinzi wa Bournemouth. Kwa bao hilo, Samatta ameingia kwenye kitabu cha historia kwa kucheza katika ligi hiyo na kufunga bao ukiwa ni mchezo wake wa kwanza tangu asajiliwe akitokea KRC Genk ya Ubelgiji. Aston Villa inashika nafasi ya 17, ikiwa na pointi 25, nyuma ya West ham yenye 24 na Watford yenye 23, huku Norwich ikiburuza mkia kwa pointi 18. | michezo | 2 |
Uamuzi huo umefikiwa baada ya kubainika kwamba ni vyama vichache ambavyo kwa sasa vina uwezo wa kulipa lakini kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika vingine havina uwezo.Awali baada ya Mkuu wa mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila alishauri kuahirishwa kwa malipo hayo wakati alipokuwa akizungumza na wajumbe wa RCC.Alisema hayo baada ya Ofisa ushirika wa mkoa wa Lindi, Saidi Munjai kusema kwamba upo waraka kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kwenda katika halmashauri za wilaya na manispaa, unaosema kwamba kuna baadhi ya vyama vya msingi havitaweza kulipa malipo ya pili kwa sasa.Alisema endapo baadhi ya vyama vya msingi vikishindwa kulipa malipo kutasababisha mkoa huo kutotawalika ikiwa baadhi ya wakulima watakosa malipo.Wajumbe wa kikao hicho waliridhia kwa pamoja kuwa kwanza malipo hayo yasimamishwe ili kuangalia vyama vyote vya ushirika vitazamwe uwezo wa kulipa ili isitokee vurugu kama zilizotokea mwaka jana.Katika vurugu za mwaka jana baadhi ya viongozi wa wilaya ya Liwale walikuwa na wakati mgumu kwa kuharibiwa mali zao na nyumba kuchomwa moto. | Biashara | 1 |
Akizungumza katika uzinduzi, Ofisa Mkuu wa Biashara wa Airtel , Arindam Chakrabarty alisema, ofa hiyo inajulikana ‘Kamata tano zaidi’.“Lengo letu ni kutoa huduma nafuu, zenye ubora, tija na zinazokidhi mahitaji ya mawasiliano kwa wateja wetu nchini kote. Nina imani ‘Kamata Tano Zaidi’ italeta uhuru wa kuwawezesha wateja wetu kuwasiliana na familia zao,marafiki na hasa kuongeza ufanisi katika biashara zao popote pale walipo . “Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano, alisema, ‘nyongeza mara tano’ itapatikana kwenye aina zote za manunuzi ya muda wa maongezi yatakayonunuliwa kwenye mfumo wa Airtel Money.Alisema muda wa maongezi utakaonunuliwa utajumlisha muda wa maongezi wa kawaida pamoja na vifurushi vyote vya Yatosha au Yatosha Noma. | Biashara | 1 |
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Taifa ya Kenya, Harambee Stars, Sebastien Migne amesema Tanzania, Taifa Stars sio timu rahisi.Kenya na Tanzania zipo Misri zikijiandaa kushiriki fainali za michuano ya Kombe la Mataifa Afrika, Afcon, zinazotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki hii. Tanzania na Kenya zimepangwa kundi C kwenye fainali hizo pamoja na Senegal na Algeria.Akizungumza na Cafonline Migne alisema: “Senegal ni timu namba moja Afrika, Algeria pia sio rahisi, soka nchini mwao iko juu wakiwa na wachezaji wazuri… Tanzania pia itakuwa mechi nzuri, sio timu rahisi.” Tanzania imefuzu fainali hizo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39 na itarusha kete yake ya kwanza mwishoni mwa wiki hii dhidi ya Senegal.“Tanzania iliifunga Uganda 3-0 kufuzu na hilo linaonesha kiwango chao, itakuwa mechi tatu nzuri na tutajaribu tuwezavyo kuweka taswira nzuri kwenye soka ya Kenya,” alisema.“Tunahitaji kuendelea kuota, tunahitaji kuthibitisha ndoto, tuna bahati kushiriki kwenye michuano hii na tulikuwa tukihitaji.” Aidha, kocha huyo alisema, kikosi chake kipo Misri kushindana na si kuongeza idadi. Kenya ilifuzu fainali hizo baada ya kumaliza ya pili kwenye kundi G nyuma ya Ghana. Hii ni mara ya pili kwa Kenya kupangwa kundi moja na Senegal kwenye michuano hiyo. Wawili hao walikutana kwenye michuano ya mwaka 1990 na mechi iliisha kwa suluhu. | michezo | 2 |
SERIKALI imevitaka vyuo kushindana kwa kutoa wahitimu wenye maarifa, waliopikwa na kuiva vizuri. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo alisema hayo juzi katika mahafali ya 11 ya Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo yaliyofanyika viwanja vya Magufuli chuoni hapo.Alisema ni vyema kutoa wataalamu waliopikwa vizuri waweze kulitumikia taifa kwa weledi kuinua mapato. Jafo alisema pia serikali itaendelea kutoa kipaumbele cha ajira kwa wahitimu wanaotoka chuoni hapo.“Tulishatoa maelekezo wahitimu wanaotoka Hombolo wapewe fursa na kipaumbele cha ajira katika halmashauri wakiwemo watendaji wa vijiji, kata, wahasibu, utawala na kada nyingine,” alisema na aliwataka wahitimu hao kwenda kufanya kazi kwa weledi na uaminifu ili waweze kutangaza sifa njema ya chuo hicho.“Wengi wenu mnakwenda kuajiriwa katika halmashauri, mkazitendee haki kwa kufanya kazi kwa bidii kukuza uwajibikaji… nimekuwa nikipokea sifa nyingi za wahitimu wa chuo hiki wanapofanya kazi nchini,” alisema.Alisema sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma ziwe muongozo katika utendaji kazi wao wa kila siku wakafanye kazi kwa umakini mkubwa kuongeza wataalamu wenye weledi maendeleo ya taifa yaweze kufikiwa.Alizitaka halmashauri kutumia mfumo ulioboreshwa wa fursa ulioandaliwa na chuo hicho. Alisema mfumo huo utazisaidia halmashauri kupambana na vikwazo vya maendeleo na kutumia fursa zinazopatikana maeneo yao. Mkuu wa chuo hicho, Dk Mpamila Madale alisema kinatoa mafunzo ya muda mfupi, mrefu na kufanya tafiti na kuwa sasa chuo kina wanafunzi 7436 na ongezeko lao limesababisha uhaba wa madarasa ambapo mwaka huu wamejenga darasa moja la wanafunzi 504 kwa kutumia mapato ya ndani na ujenzi huo umetumia force account.Rais wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo, Amani Kiswabi alitaka serikali kuboresha barabara kutoka Ihumwa hadi chuoni hapo ili iweze kupitika kwa urahisi. Alisema chuo hicho kina upungufu wa madarasa na mabweni. Wanafunzi walihitimu Astashahada ya Utawala Serikali za Mitaa, Uhasibu na Fedha Serikali za Mitaa, Ugavi na manunuzi, menejimenti ya rasilimali watu, utunzaji kumbukumbu na nyaraka na Astashahada ya maendeleo ya jamii.Wengine wamehitimu Shahada ya Utawala Serikali za Mitaa, Uhasibu na Fedha Serikali za Mitaa, Menejimenti ya Rasilimali watu, Maendeleo ya jamii, Ugavi na manunuzi na Stashahada ya Utunzaji wa Kumbukumbu 2019. | michezo | 2 |
WAWAKILISHI pekee wa Afrika Mashariki katika Ligi ya Mabingwa wa Afrika, Simba SC wamewatanguliza mashushushu nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili kuwachunguza wapinzani wao AS Vita Club watakayokutana nao Jumamosi katika mchezo wa Kundi D.Simba inaongoza katika kundi lake, inatarajia kuondoka kesho Alhamisi kwenda Kongo tayari kucheza dhidi ya AS Vita iliyopo katika nafasi ya tatu ya msimamo wa kundi hilo.Katika mchezo wa kwanza dhidi ya klabu ya Algeria ya JS Saoura, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa Jumamosi jioni huku AS Vita ikifungwa 2-0 katika mchezo uliofuata dhidi ya Al Alhly ya Misri huko Alexandria.Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana kuhusu mikakati yao kuelekea kwenye mchezo ujao Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Crescentius Magori alisema mipango ya maandalizi inaenda vizuri ingawa hawataki kuweka wazi mipango yao kutokana na Wakongo wengi kuishi nchini.Alisema wanaofia mipango na mikakati yao kufichuliwa, lakini alisisitiza kuwa tayari Simba imetuma watu wake `wapelezi’ kuifuatilia AS Vita na kuiandalia Simba sehemu ya kufikia na mambo mengine.“Hadi sasa tumetuma watu kuanza kufanya maandalizi ya awali kuelekea kwenye mchezo wetu na wapinzani wetu ili kuhakikisha mipango yetu ya kuvuna ushindi inaenda sawa, tunajua timu za Kongo zinajua fitina kwenye soka na ndio maana hatuwki mipango yetu yote hadharani, “amesema Magori.Amesema idadi ya kikosi kinachoondoka kuelekea kwenye mchezo huo kitawekwa wazi na kocha wa kikosi hicho Patrick Aussems muda wowote baada ya kufanya mazoezi ya jana ya kujiweka fiti kwa mchezo .Hadi sasa gharama za kusafiri mashabiki kwenda kuishangilia timu hiyo kwenye mchezo huo imeshawekwa wazi tiketi ya ndege kwenda na kurudi kwa Kenya Airways kwa Alhamisi ni dola za Marekani 760 sawa na Sh. 1,748,563 kwa siku ya Ijumaa ni dola 850 sawa na Sh. 1,955,757 wakatoi malazi ni dola 70 sawa na Sh. 161,074 wakati viza ni dola 50, sawa Sh 115,052. | michezo | 2 |
BAADA ya ubanguaji wa korosho mkoani hapa kuanza kwa kasi ndogo, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, imetoa rasimu ya mikataba kwa wamiliki wa viwanda wabangue.Akizungumza na wamiliki wa viwanda hivyo Mtwara hivi karibuni, Waziri wa Viwanda na Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda alisema ubanguaji wa korosho kwa kiasi kikubwa unategemea viwanda na wamiliki hao.Alisema katika kupanua viwanda, kutoa ajira na kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja nchini, serikali haina budi kushirikiana na wamiliki hao katika ubanguaji korosho, kwani ndio wanaajiri wafanyakazi na watendaji katika viwanda vyao. Alisema katika kutekeleza ubanguaji, serikali kwa kushirikiana na wadau wa zao la korosho wametengeneza rasimu ya mikataba na kuwataka wamiliki wa viwanda kupitia na kuhakikisha korosho zote zinabanguliwa nchini.“Kama kuna eneo linalotakiwa maboresho hadi kufikia kesho (leo) kwa pamoja tuhakikishe tunakaa chini na kuchukua mapendekezo haya ya rasimu kwani lengo ni kuhakikisha ubanguaji wa korosho unafanikiwa,” alisema Kakunda.Alisema uwezo wa viwanda vilivyopo nchini ni kubangua tani 50,000 za korosho kwa mwaka hali inayoashiria mwelekeo mzuri kama watashirikiana na wamiliki wa viwanda hivyo. Viwanda vilivyo chini ya serikali ni 13 ambapo kati yake, vinavyofanya kazi ni vitano na saba havifanyi kazi na vinahitaji marekebisho, 23 vikitarajiwa kuhusishwa katika ubanguaji huo.Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alisema lengo la wizara hiyo ni kuhakikisha viwanda vyote nchini, vikiwamo vya watu binafsi na vya serikali vinafanya kazi ambapo serikali baada ya kununua korosho hizo, matarajio yake sasa ni kuzisambaza kwa wamiliki wa viwanda hivyo.“Lengo la serikali ni kuona viwanda vikifanya kazi na kukuza pato na uchumi wa nchi kwa jumla lakini pia kutengeneza ajira nyingi kwa Watanzania kupitia viwanda hivyo na kuongeza wigo wa kulipa kodi na kuongezeka kiwango cha ulipaji kodi wa nchi,” alisema Hasunga | Kitaifa | 0 |
WAZIRI wa Madini, Dotto Biteko amebaini madudu yanayofanywa na maofisa wake mjini hapa, jambo ambalo lilimfanya Katibu Mkuu kumsimamisha kazi papo hapo, Ofisa Madini, Ashen Daniel ili kupisha uchunguzi.Moja ya madudu ambayo yanafanywa na wafanyakazi wa Ofisi ya Madini Mkoa wa Dodoma ni kutokujaza uzito wa madini (dhahabu), unaopatikana baada ya uchenjuaji na kuruhusu uuzaji wa madini hayo kwa watu wasio na vibali, jambo linalosababisha upotevu wa mapato ya serikali. Biteko alibaini hayo juzi jioni, alipofanya ukaguzi wa kushtukiza katika moja ya vituo vya uchenjuaji madini, eneo la Kizota jijini hapa.Tukio hilo limekuja siku chache baada ya Rais John Magufuli kukutana na wadau wa sekta ya madini nchini na kupokea kero na maoni yao juu ya wizi wa madini, unaofanywa na wachimbaji na maofisa wa serikali wanaohusika na ukaguzi. Akizungumza katika ziara hiyo, Biteko alisema Ofisa Madini, Daniel ameshindwa kujaza kwa makusudi gramu za dhahabu zinazopatikana baada ya kuchenjuliwa, jambo ambalo ni dhahiri linaashiria kufanya hujuma ili wazifanyie utaratibu mwingine wa kuliibia Taifa kwa kujaza uzito tofauti na uliopo, kinyume cha utendaji wa kazi.Alisema ofisa huyo atakuwa mfano kwa wengine wote, wanaofanya kazi kwa kuiibia serikali hawatakuwa katika mikono salama kutokana na kwamba atakwenda nao sambamba na hili zoezi ni endelevu. “Tumekuwa tukipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuwa vituo vya uchenjuaji madini nchini kumekuwa kukifanyika udanganyifu mkubwa na mbaya zaidi unafanywa na maofisa wetu kwa kupima uzito wa madini, lakini hawaandiki kiasi halisi walichokipata,” alisema Biteko.Aidha, alisema watafanya ukaguzi katika maeneo yote ya uchenjuaji na lengo ni kuhakikisha wezi wote wa madini, wanaondoka ili kuiacha sekta hiyo ikiwa salama. Mbali na hilo, Biteko aliagiza kupitia kwa Katibu Mkuu kuwa Tume ya Madini ifanye ukaguzi katika maeneo yote ya uchenjuaji, kujua ni kilo ngapi za kaboni zilipelekwa na madini kiasi gani yalipatikana.Aidha, aliwaonya wachimbaji wa madini kuwa ujanja wanaoufanya katika maeneo ya uchenjuaji wa kuiibia serikali, anazo taarifa zao na hatua stahiki zitaanza kuchukuliwa na ofisi yake. Mapema Daniel akihojiwa na waziri, alisema ni kweli amepima madini, lakini hakujaza kutokana na changamoto mbalimbali, ambazo pia alishindwa kuziainisha mbele ya waziri na kusababisha kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi uendelee kuhusu kitendo hicho anachofanya.Alisema ofisa huyo atakuwa mfano kwa maofisa wengine kutokana na utendaji mbovu wa kazi ya madini, jambo linalosababisha upotevu mwingi wa madini ambayo yanauzwa bila kujulikana sehemu wanayopeleka. Aidha, Biteko alimwagiza Ofisa Madini Mkoa wa Dodoma, Jonas Mwano kuwasilisha taarifa zote za ukaguzi wa madini za miezi sita kwa kwa Kamishna wa Madini kwa ukaguzi.“Naomba Ofisa Madini ujitathmini sana sana katika hili, nasema kabla mimi sijafikiwa lazima mimi niwafikie ninyi mapema, naomba ripoti ya miezi sita ya ukaguzi wa madini uiwasilishe kwa Kamishna wa Madini,” aliagiza. Alimwagiza Ofisa Madini wa Mkoa kupeleka kazi zake zote za madini za miezi sita, ambazo zimefanywa zikiwemo za kuchenjua na uuzaji unaofanywa na wanunuzi wa madini mbalimbali, ambao wamebainika walikuwa wakifanya kazi hiyo bila ya kuwa na leseni, lakini waliruhusiwa kufanya kazi hiyo.Mbali na hilo, Katibu Mkuu wa wizara, Profesa Simon Msanjila amemsimamisha ofisa huyo kwa muda usiojulikana ili kupisha uchunguzi uendelee kutokana na vitendo wanavyofanya katika ofisi hizo, ikiwemo kutofuatilia watu wanaonunua madini bila kuwa na leseni. “Kuanzia leo nakusimamisha kazi ili uache watu wafanye uchunguzi kubaini ukweli wa mambo,” alisema Profesa Msanjila. Katika hatua nyingine, waziri huyo alishtukiza katika moja ya madalali wanaonunua na kuuza madini mkoani Dodoma aliyepo Kizota na kubaini udanganyifu katika taarifa zake za ununuzi na uuzaji wa madini. | Kitaifa | 0 |
UNAPOZUNGUMZIA soka ukanda wa Kaskazini, unajumuisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara, ambayo kiujumla ilipoteza mwelekeo katika gurudumu la ushiriki wa soka katika ngazi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.Mkoa wa Kilimanjaro umetegua kitendawili hicho baada ya Polisi Tanzania kufanikiwa kuingia Ligi Kuu, mikoa ya Arusha na Manyara imekuwa ikiendelea kukosa timu katika daraja hilo la juu licha ya kuwa na timu zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, ambazo ni Arusha FC na Arusha United. Katika mapinduzi makubwa yaliyofanyika ni timu ya Polisi Tanzania yenye maskani yake mjini Moshi mkoani Kilimanjaro ilipambana kuhakikisha inarudisha heshima ya mkoa iliyopotea kwa miaka 27 kwa kukosa timu inayoshiriki kucheza Ligi Kuu soka Tanzania Bara baada ya Ushirika kushuka na kupotea kabisa mwaka 1992.KUTINGA LIGI KUUMei 4 mwaka huu, ilikuwa shangwe kubwa katika mji wa Moshi baada ya maafande wa Polisi Tanzania kufanikiwa azma yao ya kutinga kucheza Ligi Kuu msimu ujao wa mwaka 2019/2020 pale walipoichakaza Boma FC kwa mabao 2-1 mchezo uliopigwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Ushirika.Mabao ya ushindi yaliwekwa nyavuni na mchezaji Patrick Madadi dakika 13 na 34 huku Boma ikifunga kupitia kwa Ramadhan Abdallah dakika ya 90. Ushindi huo uliiwezesha Polisi Tanzania kumaliza ligi hiyo ikiwa kileleni kwa kujikusanyia jumla ya pointi 47 nyuma ya wapinzani wao Pamba FC kwa pointi 42 sawa na Geita Gold, ambazo zitaenda kuchuana katika hatua ya mwisho ya nchujo kusaka nafasi ya kucheza Ligi Kuu kuungana na Polisi.POLISI TANZANIANi baada ya agizo la Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lililoelekeza kila taasisi au kampuni kuwa na timu moja katika mchuano ya Ligi Kuu ndipo Jeshi la Polisi nchini likaamua kuja na timu moja ambayo italiwakilisha. Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Frank Geofrey alisema katika kutekeleza hilo, Jeshi la Polisi lilivunja timu zake zote na kuziunganisha pamoja na kuita Polisi Tanzania, ikitekeleza agizo la kila taasisi kuwa na timu moja.“Baada ya hapo tuliamua kuja Mkoa wa Kilimanjaro na hii ni kutokana na kuwa timu ni ya Makao Makuu, hivyo ikaelekezwa iletwe Moshi kama maskani yake na ikizingatiwa Moshi ndio chimbuko la askari wote, huduma zote tungezipata tukiwa hapa,” alisema Geofrey. Alisema baada ya mabadiliko hayo sasa kuwa Polisi Tanzania, timu hiyo haikufanya vizuri katika msimu wake wa kwanza wa mwaka 2017/2018 na ikajipanga tena kwa msimu wa mwaka 2018 /2019 na hii ni kutokana na kuimarisha uongozi na kufanikiwa kutimiza malengo yao.MIKAKATI MIKUBWANaye Mtendaji Mkuu wa timu ya Polisi, Robert Munisi alisema mzunguko wa kwanza hawakufanya vizuri, hali iliyosababisha kubadilisha benchi zima la ufundi, ambalo liliongozwa na kocha Mbwana Makata pamoja na uongozi mzima uliosababusha kupanda daraja. “Mikakati ni kuwa mipango yetu ni kuhakikisha mwaka wa kwanza lazima tunapambana kubaki Ligi Kuu mwaka wa pili kubaki na mwaka wa tatu kuwania ubingwa wa ligi,” alisema Munisi.Naye Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania, Mbwana Makata alisema azma yao ya kupanda Ligi Kuu ilitimia ikizingatiwa aliichukua timu ikiwa katika nafasi ya saba hivyo walipambana kwa ushirikiano wa pamoja na uongozi wa timu, mashabiki wote wa mkoa Kilimanjaro.“Mkataba wangu umeshaisha baada ya kuipandisha timu vinginevyo tunaweza kukaa mezani na kuzungumza kuhusu mkataba mwingine, kama nikisaini tena mkataba tunaweza tena fanya usajili uliokuwa bora ili kuweza kuleta ushindani,”aliongeza Makata. “Nawashukuru wote kwani haikuwa kazi rahisi Ligi Daraja la Kwanza inahitaji mpira wa matokeo zaidi utumie nafasi na ucheze kwa majukumu zaidi na sisi kila mechi ilikuwa ni fainali zaidi,” alisema Makata.CHAMA CHA SOKA KRFAMwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Kilimanjaro (KRFA), Goodluck Moshi alisema kupanda kwa timu hiyo ni mafanikio kwa wana Kilimanajro, kwani ni takribani miaka 27 mkoa ulikosa timu ya Ligi Kuu hivyo hivi sasa wapenzi wa soka waendelee kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika ligi hiyo.“Hivi sasa tunajipanga kuhakikisha tunakutana na uongozi wa Chuo cha Ushirika ili kukaa na Mkuu wa Mkoa na Manispaa kwa pamoja kuangalia namna ya kuuboresha uwanja huo wa Majengo ili kuona namna gani uwanja utafanyiwa marekebisho ili uwe katika hadhi ya kuchezewa michezo ya Ligi Kuu.Alieleza kuwa hivi sasa kama KRFA itaendelea kushirikiana na wananchi kwa ujumla kuhakikisha timu haishuki na kuongeza juhudi zaidi kupata timu itakayo cheza Ligi Daraja la Kwanza ili kuongeza msisimko wa Ligi Kuu.Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwira aliipongeza timu hiyo ya Polisi Tanzania na kusema kama mkoa utaendelea kushirikiana nao kama ilivyokuwa katika michuano ya Daraja la Kwanza. “Tutashirikiana kwa pamoja kuhakikisha Uwanja wa Ushirika na viwanja vingine vinaboreshwa ili kusiwe na kukwama na tunawaomba wafanyabiashara mbalimbali mkoani Kilimanjaro kuiunga mkono timu kwa kila namna ili iendelee kufanya vizuri Ligi Kuu,” alisema Mghwira.MASHABIKI WANENAMashabiki mbalimbali mkoani Kilimnajro waliipongeza timu hiyo na kusema kwa hatua hiyo kubwa ya kuingia Ligi Kuu huku wakiutaka uongozi wa timu hiyo uweke mikakati na mipango mipya . Mmoja wa mashabiki, Daudi Enyimba alieleza kuwa timu hiyo iungwe mkono ili iweze kufanya vizuri Ligi Kuu na kuweka mipango itakayowawezesha kuleta mapinduzi makubwa pia iweze kuangalia katika suala la usajili na mshikamano waliouonesha uendelee.Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza ilipangwa katika makundi mawili A na B, ambapo Kundi A lilijumuisha timu za Namungo, Mlale, Mbeya Kwanza, Njombe Mji, Friends Rangers, Reha, Majimaji FC, Mufindi United, Ashanti United, Dar City na Kiluvya United. Kundi B lina timu za Polisi Tanzania, Pamba FC, Geita Gold, Boma FC, Mashujaa FC, Arusha United, Rhino Rangers, Dodoma, Green Warriors, Transit Camp, Arusha FC na Mgambo Shooting.WADHAMINI SOKAKlabu za soka zinahitaji fedha nyingi ili kujiendesha, na mkoa wa Kilimanjaro licha ya kuwa na wafanyabiashara wengi waliozagaa nchi nzima, lakini wamekuwa wagumu kusaidia timu zao na kusababisha kukabiliwa na ukata. Tuliona huko nyuma timu ya Ushirika ya Moshi ilishindwa kuendelea katika Ligi Kuu kutokana na kushindwa kudhaminiwa na kusababisha kupotea kabisa katika ligi hiyo. Wafanyabiashara wa Mkoa wa Kilimanjaro wanatakiwa kubadilika sasa na kuisaidia timu yao ya Polisi Tanzania kama wanataka timu hiyo iendelee kuwepo katika Ligi Kuu Tanzania Bara. | michezo | 2 |
Wanariadha hao ni Said Makula, Sara Ramadhani na Stephano Huche ambao watakimbia mbio ndefu (Marathon), Failuna Matanga meta 10,000, Ally Ghulam atakimbia meta 100 na 200 huku Antony Mwanga akikimbia Miruko na mitupo.Awali wanariadha 9 walitarajiwa kuiwakilisha nchi lakini wawili kati yao Magdalena Shauri na Emanuel Giniki waliitwa katika ajira jeshini na mwanariadha mmoja ambaye ni Agustino Sulle aliondolewa kambini kutokana na utovu wa nidhamu na hivyo sasa kubaki idadi ya wanariadha sita pekee.Akizungumza jana katika kambi ya timu hiyo iliyopo Kata ya Kiranyi Wilaya ya Arusha DC, Katibu wa Riadha Tanzania (RT), Wilhelm Gidabuday alisema kuwa kambi ilianza rasmi Februari 8 Arusha."Kambi ilianza ikitegemewa kuwa na wanariadha 15 lakini changamoto zilizojitokeza ni kwa wanariadha wa JKT kukosa ruhusa ya kuendelea na kambi na hao wanariadha ndio walikuwa vinara chini ya udhamini wa DSTV baada ya wao kuondolewa kambini wadhamini hao sasa wamesitisha udhamini kwa muda mpaka pale watakapokutana na uongozi wa RT ili kuona namna gani DSTV wataendelea kudhamini ilihali walengwa hawako kambini," alisema Gidabuday.Aidha alifafanua kuwa kambi hiyo mpaka sasa imewezeshwa na DSTV na aliwaomba radhi kwa changamoto zingine zilizojitokeza ikiwemo ruhusa kwa wanariadha wa JKT ni jambo ambalo halikuwa ndani ya uwezo wa RT lakini pamoja na yote Shirikisho linawashukuru wadhamini kwa kusaidia mpaka wanariadha wanatarajiwa kuondoka."Changamoto zilizojitokeza zimetupatia hasara kubwa ya uaminifu ndani na nje maana usajili wa wanariadha wa Madola, mashindano ya Dunia ya nusu Marathon Hispania pamoja na London Marathon ambapo Simbu ndiye alikuwa muwakilishi pekee nchini Tanzania," aliongeza.Gidabuday.Wanariadha hao wabatarajiwa kuondoka Arusha Jumapili ya wiki hii kuelekea Dar es Salaam ambapo watakabidhiwa bendera kabla ya kuelekea Australia wakiambatana na makocha wawili: Zacharia Barie na Luiza John. | michezo | 2 |
WADAU wa maendeleo na wahisani wanaosaidia miradi ya afya nchini wamepongeza maboresho makubwa yaliyofanywa na serikali nchini katika kuimarisha utoaji huduma, upatikanaji wa vifaa na dawa za kutosha hali inayochangia kupunguza vifo ikiwemo vifo vya wanawake wajawazito na watoto.Kauli hiyo ya wadau wa maendeleo imetolewa mjini Kigoma wakati wa hafla ya kufungwa kwa mradi wa miaka 13 wa afya ua uzazi, mama na mtoto uliokuwa ukilenga kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wakati wa kujifungua ambapo mradi huo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma za afya mkoani humo na kuwezesha kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto.Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Engender Health Tanzania, Prudence Masako alisema kuwa pamoja na uboreshaji wa maeneo ya utoaji huduma uliofanywa kwa pamoja baina ya serikali na wadau, uhakika wa upatikanaji wa madawa na vifaa tiba lakini uboreshaji wa miundo mbinu ya barabara umekuwa na mchango mkubwa katika kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto mkoani Kigoma.Masako alisema kuwa dhana ya ujenzi wa uboreshaji wa vituo vya afya maeneo ya mbali na hospitali za wilaya na mkoa inatokana na miundo mbinu duni ambapo mama wajawazito na watoto walikuwa wakifia njiani hali ambayo kwa sasa ni tofauti ambapo mgonjwa anayehitaji rufaa anaweza kusafirishwa kwa haraka kwenda hospitali ya wilaya na mkoa kwa matibabu ya kitaalam zaidi.Mratibu wa Shirika la Bloomberg Philanthropies, ambao ndiyo wafadhili wa mradi huo, Dk Godson Maro alisema kuwa mradi umekuwa na mafanikio makubwa na hiyo inatokana na ushirikiano mkubwa ambao serikali imetoa katika utekelezaji wake kuanzia ngazi za zahanati hadi kwa waziri wa afya ambaye amesaidia sana mradi kutekelezwa hadi kufikia mafanikio yaliyopo sasa.Dk Maro alisema kuwa katika utekelezaji wa mradi huo kwa miaka 13 mkoani Kigoma jumla ya vituo vya utoaji huduma 100 vimeboreshwa kwa majengo, uwekaji wa vifaa tiba na elimu kwa watoa huduma 400 ambapo takwimu hizo zinaonyesha kuwa jumla ya vituo afya 13 vimepandishwa hadhi na kuweza kutoa huduma za dharula za upasuaji kwa mama wajawazito.Mratibu wa Miradi ya Afya ya Uzazi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamad Makuwani alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa na kuwa serikali imetekeleza ujenzi wa vyumba vya upasuaji wa dharula kwenye vituo vya afya nchi nzima lengo ikiwa kusaidia kuokoa vifo vya wanawake na watoto wakati wa kujifungua. | Kitaifa | 0 |
SERIKALI inajiandaa kuwasilisha bungeni muswada wa sheria kuhusu uwekezaji ili kuwe na sheria moja inayosimamia uwekezaji kwa lengo la kuweka mazingira rafiki ya kufanya biashara.Waziri wa Nchi katika Ofi si ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati anafungua kongamano la wafanyabiashara wanawake lililoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) lenye lengo la kusikiliza kero za wafanyabiashara wanawake nchini.Amesema, sheria itakayotungwa itapunguza utitiri wa vikwazo vinavyotokana na kutokuwa na mfumo rafiki kwenye uwekezaji.Waziri Kairuki ameyasema, hayo baada ya kusikiliza baadhi ya kero za wafanyabiashara wanawake.Aidha aliwataka wajenge umoja, wajiamini na kufanya kazi kwa bidii ili kuinua vipato vyao pamoja na kujenga uchumi wa nchi.Akielezea dhumuni la kuwakutanisha wafanyabiashara hao, Mwakilishi wa Wanawake Wazalishaji wa Bodi ya TPSF, Fatma Abdallah alisema taasisi hiyo imewakutanisha wanawake ili kuibua fursa mbalimbali za kiuwekezaji, lakini pia kujadili changamoto wanazozipata.Rais wa Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VOWET), Maida Waziri alisema kuwa kuna changamoto kubwa kwa wajasiriamali wanawake hasa kwenye urasimishaji wa biashara zao, lakini ni vyema serikali ikaangalia zaidi sera na sheria zilizo rafiki ili kupunguza hatari ya kuwakatisha tamaa wafanyabiashara.Maida pia aliiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kutoa fursa kwa wajasiriamali kwenye vyuo mbalimbali ili waweze kuelimishwa juu ya mazingira na jinsi ya kuwekeza.“Kuna changamoto ya elimu, lakini TPSF na Taasisi ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) ina jukumu la kutoa mafunzo lakini pia serikali kupitia vyuo mbalimbali vya ufundi na biashara vinaweza kutoa msaada wa bure kwa wafanyabiashara wenye lengo la kuwainua,” alisema Rais huyo.Kwa upande wa Mwakilishi wa Chama cha Wachonga Vinyago cha Tanzania (TANCRAFT), Louise Mushi alieleza kuwa, wajasiriamali wengi wanawake wanakabiliwa na miundombinu ya kufanyia kazi sambamba na mazingira bora ya kufanya biashara kwenye maeneo ya mipaka.Mwakilishi wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA), Leilla Jumbe alisema kuwa changamoto kubwa inayowakabili wanawake wengi ni mitaji na kwamba inatokana na wanawake wange kutokuwa na mali au ardhi kwa ajili ya kuweka dhamana. | Biashara | 1 |