content
stringlengths
1
17.8k
category
stringclasses
5 values
label
int64
0
4
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari (TPA) nchini, Madeni Kipande alisema hayo juzi alipokuwa akijibu swali juu ya hatua iliyofikiwa katika mchakato wa ujenzi huo wakati wa mkutano na wadau wa bandari uliofanyika hapa.Alisema mchakato unakwenda vizuri kwani wawekezaji hao wanaendelea kujaza zabuni zao na kuziwasilisha TPA ili kuruhusu kazi ya kumpata mwekezaji atakayetekeleza mradi huo kuendelea.“Zabuni zinaendelea kujazwa hadi mwisho wa mwezi huu wa Novemba ili kuruhusu zoezi la kuzichambua liweze kufanywa mapema mwezi ujao”, alisema na kuongeza.“Awali Kampuni 22 za kimataifa ndizo zilionesha nia ya kutaka kuwekeza kwenye ujenzi wa Bandari ya Mwambani lakini baadaye Serikali ikaona kwamba 16 ndizo zina uwezo mzuri wa kufanya kazi hiyo,” alibainisha.Aidha, Madeni aliwataka watendaji wa mamlaka hiyo mkoani Tanga kuendelea kujituma na kukubaliana na mabadiliko chanya yenye lengo la kuiwezesha Bandari ya sasa ya Tanga kufanya kazi kibiashara zaidi kama ya Dar es Salaam.
Biashara
1
SIMBA imeendeleza rekodi ya ushindi baada ya kuifunga KMC mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam jana.Simba iliingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Lipuli FC katika uwanja huo kwenye mchezo wa ligi kuu wakati KMC walifungwa na Polisi Tanzania kwa mabao 2-1 katika Uwanja wa Ushirika Moshi, Kilimanjaro.Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zote zikimliki mpira hasa sehemu ya katikati huku zikishambuliana kwa zamu na hadi kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliyokuwa imepata bao Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Simba kupata bao dakika ya 46 likifungwa na Deo Kanda kwa shuti kali lililojaa wavuni akiunganisha mpira wa pasi ya Hassan Dilunga.Baada ya bao la Dilunga Simba waliendelea kumiliki mpira huku wakipigiana pasi fupi na kuelekea kwenye lango la wapinzani wao na dakika ya 80 Clatous Chama nusura afunge bao lakini mpira ulitoka nje na dakika ya 86 Deo Kanda pia alishindwa kufunga bao akiwa na kipa wa KMC, Jonathan Nahimana. Kuonesha kwamba wana kiu ya mabao mengi, dakika ya 90 Gerson Fraga alifunga bao la pili akiunganisha mpira uliopigwa na Francis Kahata Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 31 katika michezo 12, ikiizidi pointi saba Kagera Sugar wanaoshika nafasi ya pili wakiwa wamecheza mechi moja zaidi, wakati Yanga ni ya tatu kwa pointi 21 katika mechi 10 ilizocheza.Kikosi cha KMC kilikuwa; Jonathan Nahimana, Kelvin Kijiri, Ally Ramadhani, Abdallah Mfuko, Ismail Gambo, Jean Baptiste Mugiraneza, Abdul Hilal/Rayman Mgungira dakika 87, Kenny Ally, Ramadhan Kapera, Hassan Kabunda/Rehani Kibingu dakika ya 71 na Bonphace Maganga/Serge Alen dakika ya 60.Simba ni Aishi Manula, Haruna Shamte, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Kennedy Juma, Pascal Wawa, Gerson Fraga, Deo Kanda, Muzamiru Yassin, Meddie Kagere, Ibrahim Ajib/ Clatous Chama dakika ya 63 na Hassan Dilunga/Francis Kahata dakika ya 68.Ligi kuu inatarajiwa kuendelea leo ambapo Polisi Tanzania itaikaribisha Azam FC katika Uwanja wa Ushirika Moshi, Kilimanjaro na kesho Yanga itacheza na Biashara United katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
michezo
2
Mwanasiasa Boris Johnson (55) amechaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza akichukua nafasi ya Theresa May aliyejiuzulu mwezi Juni mwaka huu.Johnson ambaye ni kiongozi wa Conservative ameshinda kwa kura 92,153, akimshinda mpinzani wake Jeremy Hunt aliyepata kura 46,656.Kiongozi huyo ambaye pia amewahi kuwa Meya wa London, amesema, atamaliza mgogoro wa Brexit na kumshinda kiongozi wa kambi ya upinzani Jeremy Corbyn.“Nitaiunganisha hii nchi na kuhakikisha sakata la Brexit limefikia mwisho ifikapo Oktoba 31, ili tuanze kunufaika na fursa zote zinazotokana na uamuzi huo,” ameeleza.Johnson anatarajia kuanza kazi rasmi kesho Jumatano.
Kitaifa
0
OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imesema mwezi ujao kibali kingine cha kuajiri walimu kitapatikana kukabili upungufu mkubwa wa wanataaluma hao nchini.Aidha, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mwita Waitara alisema jana bungeni, uhamisho wa walimu umesimamishwa kutengeneza mizania ya idadi ya walimu katika maeneo mbalimbali. Waitara aliagiza wakurugenzi na makatibu tawala wa halmashauri kuhakikisha shule zote nchini zinakuwa na walimu wa jinsi zote.Akijibu swali serikali inavyokabili upungufu wa walimu maeneo mbalimbali, alisema kibali wanachotarajia kupata Mei na Juni, ni baada ya kile cha kuajiri walimu 8,500 mwaka huu. Miongoni mwa waliouliza maswali ni Mbunge wa Viti Maalumu, Felister Bura (CCM) aliyesema Mkoa wa Dodoma una upungufu wa walimu wa Sayansi 527 akitaka kufahamu ni lini serikali italeta walimu wa kutosha shuleni.Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga (Chadema) alisema halmashauri ya Kilombero ina upungufu wa walimu 1018 na upo pia uhaba wa walimu wa kike katika baadhi ya shule. Waziri Waitara alisema zipo shule zenye walimu wa kike pekee na suala la kuchanganya jinsi liko ndani ya uwezo wa wakurugenzi wa halmashauri walifanyie kazi miezi miwili.Kuhusu uhamisho, alisema wapo watu ambao wamekuwa wakiomba uhamisho kwa sababu ya kukimbia maeneo yenye mazingira magumu. Kutokana na hali hiyo, uhamisho wote ukiwamo wa ugonjwa na kufuata wenza umezuiwa sasa.
Kitaifa
0
HATIMA ya aliyekuwa rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange ‘Kaburu’ kupata dhamana, imegonga mwamba baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kuwasilisha kusudio la kukata rufaa. DPP ameweka kusudio la kukata rufaa kupinga uamuzi uliotolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhusu kuondoa mashitaka ya utakatishaji fedha yaliyokuwa yanawakabili.Hatua hiyo imekuja wakati washitakiwa hao walipopandishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kukamilisha masharti ya dhamana ili waweze kuachiwa kwa dhamana na kuanza kujitetea. Hata hivyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon akisaidiana na Wakili kutoka Takukuru, Leornad Swai alidai, kuwa DPP amewasilisha kusudio la kukata rufaa kutokana na uamuzi wa mahakama hiyo uliotolewa juzi wa kuyaondoa mashitaka mawili ya utakatishaji fedha baada ya mahakama kuona kuwa hawana kesi ya kujibu kwenye mashitaka hayo. Hata hivyo, Wakili wa utetezi, Nehemia Nkoko, alidai hoja zilizowasilishwa za kukata rufaa zinasimamia katika mashitaka hayo mawili yaliyoondolewa ya utakatishaji na kwamba hawajaweka kusudio la kupinga dhamana.Nkoko aliiomba mahakama iwapatie dhamana wateja wake kwani upande wa mashitaka jana walipoulizwa kama wanapingamizi lolote juu ya washitakiwa kupewa dhamana baada ya kuondolewa mashitaka hayo ya utakatishaji, walisema hawana pingamizi lolote. Akitoa uamuzi, Hakimu Simba alisema sheria inawapa nafasi upande wa mashitaka kusikilizwa na kupeleka maombi yao. Hata hivyo, aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 23 mwaka huu kwa ajili ya kuwasilisha hoja za kukata rufaa. Kutokana na hali hiyo, washitakiwa Kaburu na Aveva wamerudishwa rumande. Juzi, mahakama hiyo iliondoa mashitaka mawili kati ya tisa yaliyokuwa yakiwakabili washitakiwa hao kwa kuonekana kuwa hawana kesi ya kujibu baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao. Washitakiwa hao pamoja na mwenzao Zacharia Hansppope walikutwa na kesi ya kujibu katika mashitaka saba ambayo ni kughushi, kula njama, matumizi mabaya ya madaraka, kutoa nyaraka za uongo, na kutoa maelezo ya uongo ambayo upande wa mashitaka umeweza kuthibitisha mashitaka.
michezo
2
Mkuu wa wilaya hiyo, Chande Nalicho aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kudorora kwa zao hilo ofisini kwake mjini Namtumbo.Nalicho alieleza kuwa uzalishaji wa tumbaku katika wilaya hiyo umeshuka kwa kiwango kikubwa kutoka wastani wa tani 1,000,000 kwa mwaka katika miaka mitano iliyopita hadi kufikia tani 900,000 mwaka 2014, jambo linalotishia kushuka kwa uchumi wa wilaya hiyo.Alisema tabia ya wizi na kubambikia madeni wakulima inayofanywa na viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika kumewafanya wakulima wengi kukatishwa tamaa hivyo kuamua kupunguza uzalishaji wa tumbaku na kuanza kulima mazao mengine wanayoona kuwa yatasaidia kuwainua kiuchumi badala ya tumbaku zao ambalo kwa sasa linakabiliwa na tatizo la bei.Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya , hata kiasi cha tani 900,000 zilizopatikana msimu huu zimetokana na juhudi kubwa za viongozi wa serikali kupita kwa wakulima kuhamasisha kilimo hicho,hata hivyo bado wengi wao wameonesha hawako tayari kulima tumbaku na kuna wakulima ambao wana shehena kubwa ya tumbaku majumbani wakipinga kuuza kwa bei ndogo iliyotangazwa na makampuni yanayonunua zao hilo.Akizungumzia kukamatwa kwa baadhi ya viongozi 18 wa vyama vya msingi vya ushirika, Nalicho alimpongeza Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kwa kuingilia kati suala hilo na kusema kuwa linaweza kurudisha morali ya wakulima kuendelea tena na uzalishaji wa tumbaku.
Biashara
1
Biashara
1
NAHODHA wa African Lyon, Jabir Aziz ‘Stima’ amesema licha ya kuwa kwenye nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara watahakikisha wanapambana kuepuka kushuka daraja.Akizungumza jana alisema nafasi waliyopo sio nzuri kwasababu wamekuwa na michezo migumu ambayo waliamini wangeweza kupata matokeo mazuri lakini haikuwa kama walivyotarajia.“Bado tuna nafasi ya kupigana ili tujinasue kwenye hatari ya kushuka daraja licha ya kucheza michezo kadhaa ya mzunguko wa pili, hivyo tuna kila sababu ya kuanza kubadili matokeo mabaya kuwa matokeo mazuri,” alisema Stima.Alisema licha ya timu yao kuwa na pointi 21 katika mechi ambazo wamecheza bado anaamini uwepo wa wachezaji vijana na wakongwe utasaidia timu hiyo kubaki ligi kuu licha ya kupata matokeo mabaya katika mechi zilizopita.Kulingana na kanuni timu mbili za mwisho katika msimamo wa ligi kuu zitashuka daraja na timu zitakazoshika nafasi ya 17 na 18 zitacheza na timu za daraja la kwanza zitakazo shika nafasi ya pili kwa kila kundi ili kupata timu mbili zitakazopanda Ligi Kuu.
michezo
2
KAMPUNI ya Vodacom imezindua huduma ya kwanza ambayo inaruhusu wateja wa M-PESA kukamilisha miamala wakati hawana fedha za kutosha katika akaunti zao za M-PESA.Uvumbuzi huu wa kibunifu uitwao M-Pesa Songesha umezinduliwa jana katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam. Akizungumzia huduma hiyo, Mkurugenzi wa M-Commerce, Epimack Mbeteni alisema, “Dhamira yetu ya kuleta mifumo bunifu ya kifedha kwa kutumia simu za mkononi ilitufanya kutazama kwa makini vikwazo vya mara kwa mara vinavyowazuia wateja wetu kukamilisha miamala yao kwa sababu ya upungufu wa fedha katika akaunti zao.Uchunguzi huo umefanya kuja na ufumbuzi wa kibunifu wa wateja wetu kuweza kukamilisha miamala ya M-Pesa ambayo ingeshindikana kukamilika kwa sababu ya upungufu wa fedha,” alisema. Mbeteni alisema watumiaji wa M-Pesa wanaweza kufikia huduma ya Songesha kwa kupiga namba za huduma ya M-Pesa, kisha kuchagua huduma za kifedha na kujiunga na huduma hiyo ya M-Pesa Songesha. Baada ya mteja kujiunga na Songesha, atapata ujumbe wa kiwango ambacho anastahili na ataweza kutumia kiwango hicho kukamilisha miamala yake.Kiasi hicho kitarejeshwa pale ambapo mteja atapokea fedha katika akaunti yake ya M-Pesa. “Kiwango hicho kina riba ya asilimia moja kwa siku 18 na wateja wetu wanaweza kufanya miamala kwa kutumia huduma hii kadri watakavyo ikiwa ni ndani ya kikomo cha kiwango chao.Tumeungana na Benki ya TPB kuwezesha huduma hii na ili kuamua kiwango mteja anachostahili, benki itatumia taratibu zilizowekwa kulingana na miamala ya mteja husika katika matumizi yake ya M-Pesa,” alisema . Kwa upande wake, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Moses Manyatta alisema, “Lengo letu kama benki ni kuhamasisha huduma jumuishi za kifedha huku tukiwahamasisha Watanzania kujenga tabia ya kujiwekea akiba na kujipatia mikopo kwa urahisi.”
Kitaifa
0
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kwa kushirikiana na Kamati ya Hamasa ya Taifa Stars amewaomba Watanzania kuichangia timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, fedha kwa ajili ya kuwapa motisha wachezaji.Timu ya taifa kwa iko Misri ikijiandaa na fainali za Mataifa ya Afrika zinazotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki hii, Tanzania ikitarajiwa kufungua dimba na Senegal Jumapili.Akizungumza jana Dar es Salaam Waziri Mwakyembe alisema timu ina matumaini ya kufanya vizuri hivyo kuna kila sababu kwa watu wote kuchangia kiasi chochote cha fedha ili kuwatia moyo na kuwapa hamasa wachezaji.“Timu haina matatizo kule Misri ila tumeona kuna vita kubwa ya ndani na nje ya uwanja kwenye mashindano yale kutoka kwa makundi mengine yakiahidiwa kupewa bilioni kadhaa kwa ajili ya hamasa, yote hayo ni kuvurugana kisaikolojia nasi tumeona kuna haja ya kuchangia vijana wetu wawe na motisha,” alisema.Alisema kilele cha uchangiaji kitahitimishwa Alhamisi ya wiki hii katika hafla ya harambee itakayofanyika hoteli ya Serena.Pia, alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kumpatia cheti cha shukrani baada ya kufanikiwa kuhamasisha vizuri katika mchezo wa mwisho wa kufuzu fainali hizo dhidi ya Uganda.Mwakyembe alisema watu wanaweza kuchangia kupitia akaunti hizi 0111010009781 NBC yenye jina la BMT, 01J1019956700 CRDB yenye jina la TFF, TTCL 0735414043.Mwenyekiti wa Kamati ya ushindi ya Taifa Stars, Makonda alisema kwa kuwa timu ni mali ya Watanzania sasa ni wakati wao kuichangia ili watakapoanza mashindano wacheze kwa juhudi.Alisema Kamati ya Hamasa ilifanya mazungumzo na kampuni 41 zilizoahidi kuchangia na kuyahimiza kuanza kuweka fedha katika akaunti hizo zilizotangazwa.Makonda aliwahimiza Watanzania wote kwa imani zao kuiombea Taifa Stars ili ifanye vizuri katika michezo hiyo, baada ya kufanya maandalizi mazuri ya mwezi mmoja na kucheza mechi mbili za kirafiki.“Watanzania wote siku ya Jumamosi tuelekeze nguvu zetu kuiombea timu, kama ni maandalizi yapo, nguvu ya fedha ipo, kinachohitajika ni maombi ili Mungu aweze kutusikia na kufanya vizuri,” alisema. Stars ipo kundi moja na Kenya, Senegal na Algeria
michezo
2
WANACHAMA wa Chakula Salama (Slow Food) Mkoa wa Arusha, wamesema uwekezaji uliofanywa kwenye shamba la Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda ni kielelezo tosha kuwa Watanzania wana uwezo wa kutoka pale walipo kwa kutumia raslimali zinazowazunguka.Wamesema hayo wakati wa kikao cha pamoja baada ya ziara ya mafunzo katika shamba la Waziri Mkuu Mstaafu Pinda lililopo eneo la Zinje (Zuzu) nje kidogo ya Jiji la Dodoma.Akizungumza kwa niaba ya ya kundi hilo, Kiongozi wa msafara huo, Rose Machange alisema hajawahi kuona uwekezaji mkubwa uliofanywa katika eneo moja kama huo.“Hatujawahi kuona sehemu nyingine yenye vitu vingi vya pamoja ni uwekezaji wa mfano, Watanzania lazima tujifunze kupitia hili,” alisema. Kundi hilo lilijionea ufugaji wa kuku wa asili, ufugaji nyuki, kilimo cha mboga na matunda.Alisema kiongozi huyo alisema kwa kuona shamba la Pinda wamebaini kuwa Tanzania ina raslimali nyingi ambazo zikitumika ipasavyo zitaweza kuondolea wananchi umaskini.Mratibu wa Slow Food mkoa wa Dodoma, Amandus Chitopela alisema ziara hizo za kimafunzo zimelenga kujifunza masuala mbalimbali yanayolenga kuboresha ulimaji wa vyakula na matunda ya asili.Alisema pamoja na wanachama wa Arusha kufanya ziara hiyo nao wa Dodoma watapata nafasi za kutembelea mikoa mingine ili kuhakikisha kwamba Kilimo cha vyakula vingi vya asili kinaendele akuhsamiri kwa manufaa ya wananchi na jamii.“Tunafikiria kuwa na maonesho ya vyakula vya asili kwa siku za usoni,” alisema. Hata hivyo, Chitopelo alisema mwamko kwa wajasiriamali wa Dodoma kujiunga katika chama hicho bado ni mdogo licha ya kuwa kiingilio ni kidogo cha Sh 25,000 .“Kwa Dodoma kuna kikundi kimoja chenye wanachama 20 lengo ni kuhakikisha vyakula vya asili kama uwele, karanga, mlenda, mboga nyingine za majani za aina mbalimbali na matunda ya asili vinaendelea kuwepo” alisema.Chitopela alisema kikundi Cha Dodoma kinachojulikana Ndigwa Convivium, kila mwaka kimekuwa kikiandaa mpango kazi kulingana na malengo ya Slow Food International.Aidha wanasaidia shule ambazo zina bustani kwa kuwapa elimu kwenye filosofia ya slow food ambapo miongoni mwa shule hizo ni Marie de Matius ambayo ina bustani ya mboga na matunda.Alisema wanachama wamekuwa wakitembelea nchi mbalimbali kujifunza na kuona jinsi gani nchi nyingine zinaendesha kilimo cha mbogamboga na matunda ya asili.Alisema kihistoria, vuguvugu la vyakula vya asili , Slow Food duniani,lilianzishwa na Carlos Petrini wa Italia mwaka 1989 ili kukabiliana na vyakula vya haraka (fast food) ambavyo vimeonekana kuwa na madhara kwa jamii.
Biashara
1
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula amepiga marufuku wananchi wanaoshitakiana katika mabaraza ya ardhi, kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia usafiri wa kwenda eneo lenye mgogoro.Alisema hayo wakati wa akizindua Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki.Dk Mabula alisema kutoa pesa ya kugharamia usafiri kwa mmoja wa wanaoshitakiana katika Mabaraza ya Ardhi kwenda eneo la tukio, kunaweza kuleta ushawishi kwa wajumbe wake, hasa kwa yule aliyetoa kiasi kikubwa cha pesa.Alisema ni lazima wakati wa kwenda eneo lenye mgogoro kwa wanaoshitakiana katika Mabaraza ya Ardhi, Mkurugenzi wa Halmashauri husika aratibu zoezi hilo huku ratiba nzima ikiwasilishwa kwa Mkuu wa Wilaya katika kipindi cha mwezi mmoja.‘’Jamaa anatoa shilingi laki mbili anayelalamika, hana kitu, unategemea hapo haki itatendekaje, ni marufuku kabisa na taratibu zote za kwenda barazani zipitie kwa DC na ratiba ijulikane mapema,’’ amesema Dk Mabula.Akizindua Baraza la Ardhi na Nyumba katika wilaya ya Ulanga, Naibu Waziri huyo alisema serikali imezindua baraza hilo ili kupeleka huduma karibu na kurahisisha usikilizaji kesi za ardhi kwa wananchi, ambao baadhi ya maeneo wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kupata huduma hiyo.Amebainisha kuwa sasa wananchi wa Ulanga, watapata haki kwa wakati na kwa umbali mdogo.Amewaasa wananchi wa wilaya ya Ulanga, kulitumia vyema Baraza la Ardhi na Nyumba lililozinduliwa na wafuate taratibu zote za utatuzi wa migogoro ya ardhi na kuachana na migogoro ya kifamilia, kwa kutumia Mabaraza ya Vijiji na Kata kushughulikia migogoro hiyo.Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba nchini, Stela Tulo alisema uzinduzi wa Baraza la Ardhi katika Wilaya ya Ulanga, limejibu kiu ya muda mrefu ya wananchi wa wilaya hiyo kupata huduma karibu, ambapo huko nyuma walisafiri umbali mrefu hadi Kilombero kupata huduma.Kwa mujibu wa Stela, kuzinduliwa kwa Baraza la Ulanga sasa kunaufanya mkoa wa Morogoro kuwa na Mabaraza ya Ardhi na Nyumba Manne.Kwamba baraza hilo sasa linaongeza idadi ya mabaraza yanayofanya kazi nchini kufikia 54 kati ya 97 yaliyoidhinishwa
Kitaifa
0
['Everton wako tayari kuipa changamoto Arsenal kumuwania mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, ambaye anauzwa na klabu yake ya Crystal Palace kwa kitita cha pauni milioni 80. (Evening Standard)', 'Manchester United, Everton na Paris St-Germain imefanya mazungumzo na Juventus kuhusu kumsajili Blaise Matuidi. (Le Parisien)', 'Manchester United wanaongeza jitihadi kumpata kiungo wa Lazio, mzaliwa wa Serbia Sergej Milinkovic-Savic. (Mirror)', 'Inter Milan wanamtaka mchezaji wa Man United Lukaku.', 'Livepool inamtaka beki wa kushoto wa Augsburg Philipp Max, 25, (Sport)', 'Tottenham na West Ham wanamtolea macho Diego Llorente, 25 wa Real Sociedad. (El Mundo Deportivo)', 'Wolverhampton Wanderers wanataka kumsajili mshambuliaji wa Italia na AC Milan Patrick Cutrone mwenye thamani ya takriban pauni milioni 20. (Express & Star)', 'Tottenham imempa mkataba mpya wa mwaka mmoja mshambuliaji Fernando Llorente. (Mail) ', "'Arsenal kuwasajili wachezaji maarufu na ghali zaidi'", 'De Ligt safarini kukamilisha usajili na Juventus ', 'Crystal Palace imetangaza dau la pauni la milioni 8 kumpata kiungo wa Everton James McCarthy. (Sky Sports)', 'Kocha wa Chelsea, Frank Lampard amemaliza matumaini ya Everton kwa kumsajili Kurt Zouma ambaye aliutumia msimu uliopita akiwa Goodison Park kwa mkopo. (Mirror) ', 'Mshambuliaji wa Manchester City Edin Dzeko, 33, huenda akaondoka Roma baada ya miaka mitatu, huku Inter Milan ikiwa na mpango wa kupata saini ya mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni 15.(Sportitalia)', 'Mchezaji wa Chelsea, 18, Ethan Ampadu amefanya vipimo vya kiafya kabla ya kuhamia RB Leipzig ya Ujerumani. . (Sky Sports)', 'Klabu ya Brugge ya Ubelgiji ina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Brighton na timu ya taifa ya Afrika Kusini Percy Tau, aliyecheza michuano ya kombe la mataifa Afrika. (Argus)', 'Derby County inataka kumsajili mlinda mlango wa Watford Daniel Bachmann, 25, kwa mkopo. (Derby Telegraph)']
michezo
2
TIMU ya Taifa ya soka ya wanawake chini ya umri wa miaka 17, imeifunga timu ya Burundi kwa mabao 5-1 katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 2020 nchini India uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana.Katika mchezo huo wa hatua za awali kufuzu Kombe la Dunia Tanzania ilianza kupata bao dakika ya tisa likifungwa na Aisha Masaka na lingine alifunga dakika ya 12,Joyce Meshack alifunga bao la tatu dakika ya 35 na Protasia Mbunda akafunga bao la nne na kuifanya kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 4-0.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Tanzania ikizidisha mashambulizi na dakika ya 59 Aisha Masaka akafunga bao la tano ambalo lilikuwa la tatu kwake kwa mchezo huo lakini ikiwa ni ya ‘hat trick’ ya sita kwake tangu aanze kucheza mpira.Dakika ya 72 Burundi walipata bao la kufuta machozi lililofungwa na Lydia Karenzo kutokana na mabeki kuzembea kuondoa mpira eneo la hatari na kumpiga tobo kipa wa Tanzania na kuingia wavuni.Baada ya mchezo kumalizika makocha wa timu zote walizungumzia mchezo huo ambapo Kocha wa Tanzania, Bakari Shime aliwashukuru wachezaji kwa kufanya kile alichowatuma na kuwapongeza Watanzania kwa kuwaunga mkono.“Nimefurahi kupata ushindi leo ila kazi ndio imeanza kwani tunakwenda kuruadiana Januari 25 Bujumbura na lolote linaweza kutokea hatuwezi kusema tumewatoa,” alisema Shime.Naye kocha wa Burundi Daniella Niyibimenya alilalamikia uwanja pamoja na joto lakini alikiri timu yake kufanya makosa kadhaa ambayo yalisababisha kufungwa.“Uwanja haukuwa rafiki kwetu kwani tumezoea nyasi bandia, pia joto lilikuwa kali lakini tulifanya makosa ambayo yalitugharimu na nitakwenda kuyafanyia kazi ili mchezo ujao tushinde,” alisema Daniella.Daniella ni kama vile hakutarajia kipigo hicho ukizingatia mara ya mwisho walipocheza na Tanzania katika mashindano ya Cecafa yaliyofanyika nchini Uganda walitoka sare ya mabao 3-3.
michezo
2
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Klabu ya Azam leo inatarajiwa kwenda Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano dhidi ya Triangle United FC.Azam watakuwa na kibarua kigumu katika mchezo huo wa ugenini unaotarajiwa kupigwa Septemba 28, kwani wanahitaji kupata ushindi wa zaidi ya mabao 2-0 ili wasonge mbele baada ya kufungwa 1-0 katika mchezo wa awali uliopigwa wiki iliyopita Azam Complex, Chamazi. Akizungumza na gazeti hili jana, kocha msaidizi wa mabaingwa hao wa Ligi Kuu Bara msimu wa mwaka 2013/14. Iddy Nas sor ‘Cheche’ alisema kuwa timu itasafiri leo asubuhi na wachezaji ambao hawapo katika kikosi cha Taifa Stars.Alisema kuwa kwa wachezaji ambao wapo katika kikosi cha Taifa Stars watasafiri kesho pamoja na kocha Etiene Ndayiragije baada ya mechi dhidi ya Sudan itakayochezwa leo. Alifafanua kuwa wanakwenda Zimbabwe wakiwa na imani kubwa ya kupindua matokeo baada ya kuyafanyia kazi makosa yaliyojitokeza katika mechi ya kwanza na kuwafanya wapoteze mchezo. “Timu inatarajia kusafiri kesho kwa wachezaji ambao hawapo katika timu ya taifa na wachezaji ambao wapo na majukumu ya timu ya taifa hao watasafiri Jumatatu baada mechi ya Jumapili.“Tunaamini tutapata matokeo mazuri ambayo yatatufanya tusonge mbele, nasema hivyo kwa sababu mapungufu yaliyojitokeza katika mechi ya kwanza tumeyafanyia kazi na pia kufanyia kazi mapungufu tuliyoyaona kwa wenzetu,” alisema Cheche.
michezo
2
UJENZI wa mabweni mengi ya wasichana pamoja na sekondari nyingi nchini ni kati ya sababu zilizochangia serikali kuwachukua wanafunzi wa kike wote waliofaulu kujiunga na kidato cha tano mwaka huu. Juzi Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), ilitangaza kuwachukua wanafunzi wote wa kike wenye sifa za kujiunga na kidato cha tano na elimu ya ufundi. Tukio hilo ambalo ni mara ya kwanza kuwahi kutokea nchini, limesababisha wanafunzi 108,644 sawa na asilimia 98.31 ya wanafunzi 110,505 wenye sifa waliotangazwa kuchaguliwa mwaka huu kujiunga na kidato cha tano. HabariLeo imezungumza na Naibu Katibu Mkuu Tamisemi anayeshughulikia elimu, Tixon Nzunda ambaye alibainisha kuwa sababu kubwa ya mafanikio hayo ni ujenzi wa mabweni ya wasichana pamoja na sekondari za kutwa nyingi sehemu mbalimbali za nchi. Nzunda alibainisha kuwa serikali imepeleka zaidi ya Sh bilioni 29 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na mabweni mikoa mbalimbali nchini kipindi cha kuanzia Januari mwaka huu. Alisema, kumekuwa na ongezeko kubwa la ujenzi wa mabweni kwa wanafunzi wa sekondari ambapo mengi ni mabweni ya wasichana, hali ambayo imechangia kuchukuliwa kwa wasichana hao wote kwenye matokeo ya kidato cha tano mwaka huu. Alisema,”mabweni mengi yamejengwa pamoja na shule za sekondari za kutwa, hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kuchukuliwa kwa wasichana wote waliofaulu kidato cha tano mwaka huu. Lakini pia ifahamike kuwa kuna sera ya kuwawezesha wasichana kupata elimu ya juu zaidi ila hiyo sio sababu kubwa ya wao kuchukuliwa kwa maana ya hatujawapendelea wao tu na kuwaacha wanafunzi wa kiume”.Alisema wanafunzi wa kiume walioachwa ambao ni 1,861 watachukuliwa wote kwenye udahili wa awamu ya pili. Alisema Tamisemi kupitia mikoa mbalimbali imefanikiwa kujenga madarasa takribani 2,093 nchi nzima kwa gharama ya Sh bilioni 29.9. Kwa upande wa shule za msingi imejenga madarasa 2,897 kwa gharama ya Sh bilioni 35 huku akibainisha kuwa miundombinu ya kuwawezesha wanafunzi wa shule za msingi kusoma vema ili kujiunga kwa wingi sekondari inazidi kuboreshwa. Juzi Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo alibainisha kuwa wanafunzi 108,644 sawa na asilimia 98.31, ya wanafunzi 110,505 wenye sifa, wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo mbalimbali vya ufundi nchini.Jafo alifafanua kuwa jumla ya wanafunzi 69,356 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano ambapo katika chaguo hilo, idadi ya wasichana ni 31,809 na wavulana 37,547 sawa na asilimia 62.76 ya wanafunzi 110,505 ya waliokuwa na sifa. “Waliojiunga na shule za wanafunzi wenye ufaulu mzuri zaidi (vipaji maalumu) ni 1,462 ambapo wasichana ni 646 na wavulana 816. #Miongoni mwao wanafunzi sita ni wenye mahitaji maalumu ambao wasichana ni watatu na wavulana watatu,” alisema. Aliongeza kwamba wanafunzi wenye mahitaji maalumu waliochaguliwa ni 157 ikiwa wasichana ni 74 na wavulana ni 86 wakati wanafunzi waliochaguliwa ambao waliosoma chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ni 174, ikiwa ni wasichana 74 na wavulana 100. Aidha, Jafo alisema wanafunzi 1,046 ikiwa ni wasichana 257 na wavulana 789 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vinne vya Elimu ya Ufundi ambavyo ni Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo cha Usimamizi wa Maendeleo ya Maji (WDMI) na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST). Jafo pia alisema wanafunzi 32,619 ikiwa ni wasichana 11,665 na wavulana 20,954 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vingine vya elimu ya ufundi vinavyosimamiwa na NACTE. Akichanganua waliochaguliwa na idadi yao kwenye mabano kuwa ni waliochaguliwa vyuo vya afya kwa astashahada 345 na stashahada ni 1,477, vyuo vya walimu ni 4,472 wa astashahada na 4,146 wa stashahada. Jafo alisema Vyuo vya Ardhi ni wanafunzi 464, Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (2,850), Chuo cha taifa cha Utalii (450), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (1,500), Chuo cha Mipango-Dodoma (2,200), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (1,864), Vyuo vya Uvuvi-FETA(575), vyuo vya mafunzo ya kilimo-MATI (921), Taasisi ya Uhasibu Arusha-IAA(1,295). Vyuo vya Maendeleo ya jamii-CDTI (1,573), Taasisi ya Uhasibu Tanzania- TIA(5,254), Vyuo vya Mafunzi ya Mifugo-LITA (1,281), Vyuo vya utumishi wa Umma-TPSC( 3,955) na Chuo cha Elimu ya Biashara-CBE( 3,620).Aidha, Jafo ameagiza wanafunzi wote waliopangiwa kujiunga kidato cha tano wanapaswa kuripoti katika shule walizochaguliwa ndani ya siku 14 kuanzia Julai 8 mwaka huu na baada ya muda huo kupita nafasi itachukuliwa na wanafuzni mwingine aliyekosa nafasi. “ Mabadiliko ya shule yataruhusiwa baada ya kukamilika kwa muhula wa kwanza wa masomo na utaratibu huo utafanyika kwa kuzingatia uwepo wa nafasi kwenye shule kwa idhini ya maafisa elimu wa mikoa husika,” alisema.
Kitaifa
0
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Hotelini, Majumbani, Huduma za Jamii na Ushauri (CHODAWU), Said Wamba, amewataka wadau wa sekta ya utalii katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wawe na usawa wa kimaslahi pamoja na sheria bora za kazi kwa wafanyakazi wa sekta hizo, ili kuongeza mapato katika sekta ya utalii.Wamba aliyasema hayo wakati akizungumza katika kongamano la wadau wa utalii kutoka nchi za EAC katika kuangalia namna ambavyo wafanyakazi waliopo katika sekta ya utalii wanaweza kunufaika na sekta hiyo.Alisema kumekuwepo na changamoto zilizofanana katika sekta ya utalii katika nchi zote za jumuiya ambapo wadau hao kwa pamoja wataweza kujadili namna ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi katika ubora na staha za kazi kwa nchi hizo.Kongamano hilo lililoandaliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi wa Hoteli na Kilimo Duniani (IUF) ni la kwanza katika nchi za jumuiya hiyo katika kuangalia namna ya kuboresha sekta ya utalii kwa nchi hizo, pamoja na kuhakikisha maslahi yanakuwa sawa kwa nchi zote huku wafanyakazi katika sekta hiyo wakinufaika moja kwa moja kupitia sekta ya utalii.“Changamoto iliyopo kwa wafanyakazi katika sekta hii ni wengi wao kutokuwa na ujuzi wa kazi zao, hivyo kusababisha kulipwa mishahara duni. Ni wajibu wa wadau katika sekta hiyo kuhakikisha wafanyakazi wanapatiwa mafunzo yatakayoweza kuwajengea mazingira bora na hatimaye kuweza kulipwa mishahara bora,” alisema.Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Kanda ya Afrika Mashariki, Wellington Chibebe alisema, lengo la mkutano huo ni kuhakikisha waajiri, wafanyakazi wote kwa ujumla wanapata haki sawa katika nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki ili wote kwa pamoja waweze kuwa na sauti moja ya kuboresha sekta ya utalii.Mwenyekiti wa CHODAWU Taifa, Cosmas Chikoti, aliwataka waajiri katika sekta hiyo kuwapa fursa wafanyakazi wake ya kujiendeleza kitaaluma na kusomea lugha zaidi ya Kiswahili na Kingereza, ili kuwezesha kumudu ushindani na kuweza kupata wageni wengi zaidi.
Kitaifa
0
Simba haipo kwenye michuano ya Kombe la FA, kwa hiyo kocha wake amekuwa na muda wa kutosha kukiandaa kikosi chake kuelekea mchezo huo wa raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika CAF.Lechantre amesema, anatambua ugumu uliopo kwenye mchezo huo, hivyo anahitaji muda wa kutosha kukiandaa kikosi chake ili kuweza kuwadhibiti wapinzani wao na hatimaye kuvuka hatua inayofuata.“Haipendezi kuondolewa mapema kwenye michuano ya FA, lakini kwa hatua tuliyofikia CAF, naamini muda huu utatusaidia kujipanga vizuri na kutengeneza mikakati mbadala itakayotusaidia kuwatoa Al Masry na kusonga mbele raundi ya pili,” amesema Lechantre.Mfaransa huyo alisema kwa sasa amepanga kufanya mazoezi mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni ili kuongeza pumzi itakayowasaidia kucheza kwa muda mrefu na kasi, mbinu ambazo hutumiwa sana na timu za kiarabu.Ukitoa pambano la Ligi Kuu dhidi ya Mbao FC, Simba haitakuwa na mchezo mwingine zaidi ya kusubiri pambano hilo la kimataifa, ambalo litapigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kabla ya kurudiana nchini Misri.Wapinzani wa Simba, Yanga wapo katika michuano mitatu tofauti na wamekuwa na malalamiko makubwa na Bodi ya Ligi kutokana na ratiba kuwabana na kukosa muda wa kutosha kujiandaa na mpambano wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rolles ambayo watacheza nayo kwenye raundi ya pili ya michuano hiyo.
michezo
2
WAKATI Watanzania wakitarajia kuungana na wenzao kusherehekea Sikukuu ya Idd el Fitri leo au kesho, Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakar Zuberi amelishauri Jeshi la Polisi kukamata magari yatakayobeba vijana kuwapeleka ufukweni kusherehekea sikukuu hiyo. Ushauri huo ulitolewa jana na Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa kwa niaba ya Mufti, akitolea taarifa ya swala ya Iddi, ambayo alisema kitaifa itaswaliwa katika mkoa wa Tanga katika Msikiti Mkuu wa Tanga uliopo Barabara ya Tisa na Kumi Ngamiani.Aliomba Jeshi la Polisi kuzuia magari, ambayo yataonekana yamewabeba vijana wa kike na kiume kwenda beach kusherehekea sikukuu hiyo kwa kuwa kitendo hicho sio salama kwao.“Kinachotokea ni pamoja na maambukizo ya magonjwa kama Ukimwi na ukosefu wa maadili, tunashuhudia vijana wetu hasa watoto wa kike na kiume wanakodi mabasi na kwenda beach, jambo hilo sio salama, wazazi tusiwaruhusu mabinti zetu kutoka na wavulana ni uharibifu unaotokea baada ya hapo,” alisema.Aliwaasa pia wazazi kuwapeleka watoto kusherehekea siku hiyo sehemu ambazo ni salama kwa watoto wao. Pia alitoa mwito kwa waislamu na watu wengine siku hiyo ya Iddi washerehekee kwa namna ambayo inampendeza Mungu. “Siku ya Iddi ni siku adhimu, mtu akisherehekea kinyume cha utaratibu wa Mungu anajitafutia laana yeye mwenyewe, mwenye kumuasi Mungu katika siku kama hii ni kama amemuasi Mungu siku ya kiama,” alisema. Aidha, alitoa mwito kwa watu kutorudi kwenye matendo ambayo hayampendezi Mungu kama vile zinaa, unywaji pombe hasa katika siku hiyo. Inatarajiwa muandamo wa mwezi unatarajiwa kuoenakana kesho swala hiyo itafuatiwa na baraza la Iddi saa nane mchana katika hoteli ya Tanga Beach Resort, waislamu wanatarajiwa kuwepo pale Tanga kwa ajili ya swala hiyo,” alieleza.
Kitaifa
0
Rais John Magufuli amesema kikokotoo cha mafao kilichokuwa kikitumika kwa kila mfuko wa jamii, kabla ya mifuko yote kuunganishwa kiendelee katika kipindi hiki cha mpito hadi mwaka 2023, ambapo wanachama 58,000 ndio watastaafu katika kipindi hicho.Amesema hayo katika mkutano wake na wawakilishi kutoka Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), vyama shiriki, watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PSSSF na NSSF pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) kuzungumzia kikokotoo cha mafao ya wastaafu."Katika kipindi hiki cha mpito, vikokotoo husika vitumike kwenye mifuko husika, ili kwamba mifuko ijiimarishe kwenye kipindi hiki na wastaafu pia wasipate shida katika kupata stahiki zao," aliongeza.Rais Magufuli pia ametoa maagizo kwa mifuko hiyo ya jamii kuboresha daftari la wastaafu, ili kuondoa wastaafu hewa na wanaotambulika zaidi ya mara moja.Vile vile amewaagiza kupunguza matumizi ya ovyo, na kuepuka kufanya uwekezaji usio na tija kwa kutumia fedha hizo za mafao ya wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji wa mifuko.Rais Magufuli ameeleza kuwa hadi kufikia mwezi Machi 2017, serikali ilikuwa imelipa deni lake lote la shilingi trilioni 1.2/- iliyokuwa ikidaiwa na mifuko ya jamii.
Kitaifa
0
MAMBO matano ya kufahamu kuhusu timu mbili zinazopambana leo katika fainali ya Michuano ya Mataifa ya Afrika, Afcon 2019, Algeria na Senegal itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.ALGERIA Nahodha na winga Riyad Mahrez kutoka Manchester City ndiye mchezaji pekee wa Algeria anayewakilisha Ligi Kuu ya England. Mchezaji mwingine wa Algeria anayecheza soka England, ni kiungo Adlene Guedioura, lakini yeye yuko katika klabu ya Ligi Daraja la pili ya Nottingham Forest.Timu hiyo ina wachezaji saba wanaosakata soka nchini Ufaransa, wakiwemo mabeki Ramy Bensebaini na Mehdi Zeffane kutoka klabu ya Rennes, na watatu wengine kutoka Italia na Saudi Arabia.Guedioura ndiye mchezaji mkongwe zaidi katika kikosi hicho cha timu ya taifa ya Algeria akiwa na umri wa miaka 33 na Hicham Boudaoui, ndiye mchezaji pekee katika kikosi hicho anayecheza soka nchini mwao na ana umri wa miaka 19 tu. FAINALI TATU Algeria imecheza fainali mbili zilizopita za Mataifa ya Afrika na zote ikikutana dhidi ya Nigeria. na walifungwa 3-0 jijini Lagos mwaka 1980 na kushinda bao 1-0 huko Algiers miaka 10 baadae.Timu nyingi za mataifa ya Afrika zinachagua majina ya wanyama kuwa majina yao ya utani na Algeria ni miongoni mwao baada ya kuchagua jina la Mbweha na kujulikana na Mbweha wa Jangwani.SENEGAL Nahodha na beki wake Cheikhou Kouyate (Crystal Palace), kiungo Idrissa Gueye (Everton) na mshambuliaji nyota Sadio Mane (Liverpool) wanacheza katika Ligi Kuu ya England. Kikosi cha Senegal kina wachezaji wanane wanaocheza soka nchini Ufaransa, akiwemo kipa Abdoulaye Diallo na washambuliaji Mbaye Niang na Ismaila Sarr kutoka Rennes.Mabeki Saliou Ciss kutoka klabu ya Daraja la Pili Ufaransa ya Valenciennes ndiye mchezaji mkongwe zaidi katika kikosi hicho akiwa na umri wa miaka 30 na mshambuliaji Krepin Diatta kutoka klabu ya Brugge ndiye chipukizi zaidi akiwa na miaka 20.Hii ni fainali ya pili ya Senegal baada ya ile ya kwanza, ambapo walifungwa kwa penalti na Cameroon mwaka 2002 baada ya kutoka suluhu licha ya kuongezewa muda huko Bamako. Timu yao ya taifa inajulikana kwa jina la utani kama Simba wa Teranga. Teranga ina maana ya ukarimu lugha maarufu sana kwa nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
michezo
2
MBUNGE wa Viti Maalumu, Amina Mollel (CCM) ameomba muongozo bungeni akitaka serikali itoe ufafanuzi wa hali ya ugonjwa wa homa ya dengue ambao umeendelea kuwa tishio na kuua wananchi Dar es Salaam.Mollel ameomba muongozo huo baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, ambapo alidai kuwa ugonjwa huo umekuwa ni tishio kwa sasa jijini Dar es Salaam huku wengi wa waliougua wakiripotiwa kufariki dunia, lakini serikali imekaa kimya.“Mheshimiwa naomba nizungumzie tatizo lililopo jijini Dar es Salaam, hasa ugonjwa wa dengue, ugonjwa huu umekuwa tishio kwa sasa jijini humo na taarifa zilizopo ni wagonjwa wengi waliougua wamefariki dunia na hakuna taarifa rasmi ya serikali kuhusu hilo,” amesema Amina.Amesema wagonjwa wanaokwenda hospitalini kwa ajili ya kupimwa wamekuwa wakitozwa fedha hadi Sh 50,000 na wengi wao wameshindwa kupimwa kutokana na ukosefu wa fedha.“Naibu Spika, serikali imekuwa kimya juu ya ugonjwa huu na wanapokwenda hospitali wanaambiwa kipimo ni shilingi 50,000 kwa hiyo watu wengi wanakwepa kupima sababu ya hiyo hiyo fedha. Kwa hiyo Mheshimiwa Naibu Spika naomba ikikupendeza kutumia Kanuni ya 49 (1) (2) ili tuweze angalau tupate taarifa ama majibu kutoka kwa serikali,” amesema Amina.Akijibu hoja hiyo, Naibu Spika Dk Tulia Ackson amesema serikali imeshatolea ufafanuzi jambo hilo kupitia taarifa zikiwemo zilizotolewa kwa vyombo vya habari.“Waheshimiwa wabunge ugonjwa alioutaja Mheshimiwa Amina Mollel wa dengue nadhani serikali imeshatoa kauli mbalimbali katika vyombo mbalimbali.“Kwa maana hiyo matumizi ya kanuni ya 49 mimi naweza kusema kwamba kwa sababu hii inahusu kauli za mawaziri, serikali ikiona kuna taarifa za ziada ambayo haijatoa mpaka sasa yenyewe itaomba kibali ili iweze kutoa kauli hiyo hapa bungeni kwa kutumia kanuni hiyo lakini kiti hakiwezi kutoa muongozo kwa sababu imeshatoa maelezo ya ugonjwa huo,” alisema Dk Ackson.
Kitaifa
0
['Kiungo wa Manchester United na Uskochi Scott McTominay, 22, ametaka watu wamvumilie kocha Ole Gunnar Solskjaer. (Mirror)', 'Solskjaer amethibitisha kuwa Manchester United itaingia sokoni kutafuta mshambuliaji na kiungo mchezeshaji ili kuboresha nguvu ya mashambulizi ya klabu hiyo ambayo imeshindwa kufunga zaidi ya goli moja kwenye michezo 17 kati ya 20 iliyopita. (Telegraph)', 'Arsenal wanataka kumtoa kwa mkopo kiungo Mjerumani Mesut Ozil, 30, mwezi Januari, hata kama itawalazimu kutoa ruzuku ya mshara wake kwa timu atakayoenda. (Mirror)', 'Kocha wa Inter Milan Antonio Conte anawekeza nguvu zake katika kumsajili kiungo wa kimataifa wa Serbia kutoka klabu ya i Manchester United Nemanja Matic, 31. (Calciomercato)', 'Manchester United wanatarajiwa kujaribu tena kumsajili msahambuliaji wa timu ya taifa ya Croatia na klabu ya Juventus Mario Mandzukic, 33, ambaye alikuwa kwenye mipango yao kwenye dirisha la usajili lililopita. Juve wanatarajiwa kutaka ada ya uhamisho ya pauni milioni 9, huku Mandzukic akitarajiwa kukataa ofa yoyote ya mshahara chini ya kiwango anacholipwa sasa cha pauni milioni 4.5 kwa mawaka. (Goal.com)', 'Mandzukic amevunja mazungumzo na klabu ya Al Rayyan na sasa hatajiunga na timu hiyo kutokea nchini Qatar. (Goal.com)', 'Klabu ya PSV Eindhoven ya Uholanzi inataka kumsajili kwa mkopo kiungo wa Manchester United na timu ya taifa ya Uholanzi ya chini ya miaka 21Tahith Chong. (Sun)', 'Mshambuliaji wa klabu ya Napoli na timu ya taifa ya Ubelgiji Dries Mertens, 32, anajianda kuondoka kwenye klabu hiyo kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu. (Calciomercato)', 'Kocha wa Arsenal Unai Emery amekanusha kuwa ana matatizo ya lugha na hivyo kushindwa kuelewanan na wachezaji wake - japo anasema Kingereza chake ni kizuri kwa alama sita kati ya 10. (Mirror)', 'Kiungo wa zamani wa Arsenal Emmanuel Petit amemuonya Emery dhidi ya kubadili kikosi mara kwa mara. (Sun)', 'Kocha wa Stoke ambaye yupo kwenye wakati mgumu Nathan Jones amesisitiza kuwa bado anaimani na uwezo wake na anaamini yeye ndio mtu sahihi wa kuinoa kalabu hiyo. (Stoke Sentinel)', 'Kocha wa klabu ya Celtic ya Uskochi Neil Lennon amesisitiza kuwa mkuu wa usajili wa klabu hiyo Nick Hammond yupo kibaruani kumpatia machaguo ya kukiboresha kikosi chake kuelekea dirisha la usajili la mwezi Januari. (Star)']
michezo
2
Takriban asilimia 90 ya korosho ghafi yote inayozalishwa nchini huuzwa nchi za Vietnam pamoja na India. Haya yamesemwa leo, Jumapili na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Alfred Francis katika maadhimisho ya siku maalumu ya mazao ya mkakati kwenye Maonyesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa (Sabasaba).Francis ameeleza kuwa hii ni kutokana na ukosekanaji wa miundombinu ya kubangua korosho hizo nchini. “Kama tutawekeza kwenye miundombinu bora ya kubangua korosho ghafi zetu, tutanufaika zaidi ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa fursa za ajira, pamoja na mapato,” ameeleza. Ameongeza tena kuwa korosho hizi zikibanguliwa nchini, zipo bidhaa nyingine zitapatikana kutokana na maganda hayo ya korosho ikiwa ni pamoja na kutengenezea juisi, mvinyo, maziwa ya korosho na mengineyo.“Ubanguaji wa korosho nchini utasaidia pia kuongeza thamani ya mazao yetu nchini na kuongeza wigo wa masoko,” amesema.
Kitaifa
0
['Manchester United inafikiria kumuongezea dau kiungo wa Ureno Bruno Fernandes, 25, kabla ya Ijumaa ambayo ndiyo siku ya mwisho ya dirisha la usajili. (Guardian)', 'Ingawa Fernandes amejumuishwa katika kikosi cha Sporting kitakachominyana na Maritimo Jumanne jioni, hali inayoonesha kuwa uhamisho huo unaweza kuwa mgumu kukamilika. (Express)', 'United imeamua kumpa nafasi nyingine Alexis Sanchez mwenye umri wa miaka 31, kuonyesha uwezo wake na itamrejesha kutoka Inter Milan mwezi Juni. (Star)', 'Mashetani wekundu United hata hivyo wanaonyesha dalili ya kutotaka kufanya usajili katika dirisha hili la Januari hasa baada ya kupata mikingamo kwenye kuwanasa Fernandes na Edson Cavani wa PSG ambaye anaripotiwa kwenda klabu nyengine. (Independent)', 'Klabu ya Arsenal inatarajiwa kufanya mazungumzo na mshambuliaji wa Barcelona Pierre-Emerick Aubameyang, mwenye umri wa miaka 30. (Telegraph)', 'Arsenal imebadili vigezo walivyoweka katika mkataba wa Pablo Mari, 26 baada ya ripoti ya uchunguzi wa afya yake, na kuweka wingu jeusi juu ya uhamisho huo. (Mail)', 'Usajili wa Mari umeshindikana na beki huyo yupo njini kurudi Brazil. (ESPN)', 'Atletico Madrid inakaribia kufikia makubaliano na Cavani. (ESPN)', 'Chelsea inamfuatilia mshambuliaji wa AC Milan Krzysztof Piatek mwenye umri wa miaka 24, ambaye anawaniwa na Tottenham wakati wakijipanga kupata mbadala wa Cavani. (Telegraph)', 'Raia wa Uholanzi Steven Bergwijn, 22 amekanusha kukataa kucheza katika timu ya PSV Eindhoven siku ya Jumapili na kuwa yupo kwenye mazungumzo na Tottenham. (Sky Sports)', 'Ingawa Bergwin aliitaka PSV kumruhusu ajiunge Spurs kabla ya dirisha la usajili halijafungwa. (90min)', 'Kiungo wa Denmark Christian Eriksen, 27, anatarajiwa kuthibitishwa kuwa mchezaji wa Inter Milan siku ya Jumanne baada ya kupita vipimo vya afya usiku wa Jumatatu. (Mail)', 'Manchester United, Arsenal na Tottenham wanavutiwa kumsajili mchezaji wa Ujerumani Emre Can mwenye umri wa miaka 26 akitokea Juventus.(Metro)', 'Borussia Dortmund wanawania pia kumsainisha Can ambaye ni kiungo wa kati wa zamani wa Liverpool. (Bild - in German)', 'Mchezaji wa Tottenham Danny Rose, 29 na Kyle Walker-Peters mwennye umri wa miaka 22 wanatarajia kuondoka Spurs kwa mkopo kabla ya siku ya mwisho ya usajili. (Standard)', 'Saints wamejipanga kumsajili Walker-Peters kwa mkopo, huku wakiendelea na majadiliano kuhusu mkataba wake kama utajumuisha malipo ya paundi milioni 12 kuwa sehemu ya mkataba wake . (Mail)', 'Aston Villa imewasilisha dau la usajili la pauni milioni 4.2 kwa mchezaji wa zamani wa Chelsea na Liverpool, Daniel Sturridge, 30 kutoka klabu ya Uturuki ya Trabzonspor. (Talksport)', 'West Ham wanajipanga kumsajili mchezaji wa Tottenham na Argentina Juan Foyth, 22. ', 'Klabu hiyo pia iko kwenye mazungumzo na Slavia Prague juu ya kiungo wa kiungo Tomas Soucek, 24. (Guardian)']
michezo
2
ZAIDI ya tani tatu za ufuta uliochanganywa na uwele umekamatwa katika kijiji cha Miguruwe, wilayani Kilwa mkoani Lindi . Kukamatwa huko kumetokana na wapokeaji wa ufuta huo katika Chama cha Msingi cha Ushirika (amcos), Zinga, kushtukia magunia ya ufuta wakati wakifanya ukaguzi wa awali kwa kutumia fito maalumu (bamboo).Mwenyekiti wa Amcos hiyo, Mshamu Mpwate alisema ufuta huo ulifikishwa jioni ya Juni 24, mwaka huu na mfanyabiashara aliyejitambulisha kwa jina moja la Cheche, ulifanyiwa ukaguzi Juni 25, mwaka huu kwa kuwa wao jioni huwa hawafanyikazi na ulipokaguliwa gunia la kwanza ulionekana kuwa una uchafu lakini walipokagua magunia hadi kumi wakajiuliza aina ya uchafu unaonekana katika maguni hayo.Alisema wamekuwa wakisisitiza ukaguzi wa awali kutokana na agizo la Mkuu wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai aliyetaka uongozi na vyama vya msingi kuhakikisha ubora wa ufuta ili soko lisiharibiwe na kwamba ilibainika kuwa ufuta huo umechanganywa na uwele baada ya ukaguzi wa kina na wananchi wanaojua nafaka ya uwele kuthibitisha.Mwenyekiti huyo alisema kwamba huenda jambo hilo limefanyika kwa makusudi kwa kuwa kijiji hicho wala tarafa hiyo hailimi uwele na kwamba katika miaka yake miwili ya uongozi hajawahi kukumbana na tatizo la aina hiyo kwenye misimu ya mauzo ya ufuta. Mkuu wa wilaya Ngubiagai akizungumza na waandishi wa habari alisema kwamba serikali inamsaka mfanyabiashara huyo ambaye ametoroka baada ya ujanja wake kubainika na kuongeza kuwa ufuta huo kwa sasa upo chini ya uangalizi wa serikali ya kijiji, utachambuliwa na kisha kuuzwa na fedha zake kutumika kwa maendeleo ya kijiji.Alivitaka vyama vya msingi kuwa imara , kukagua na kujiridhisha kabla ya mnada na pia wakati wa kuusafirisha baada ya kuufungasha pamoja na kuwataka viongozi wa vijiji ,kata na maofisa tarafa kutembelea na kukagua mara kwa mara uendeshaji wa biashara ya ufuta ili kubaini changamoto kwa haraka na kuzichukulia hatua.Mkuu huyo wa wilaya aliendelea kusema kwamba kupatikana kwa ufuta huo uliochanganywa unatoa somo kwa vyama vyote vya msingi kuwa na uangalifu mkubwa ili ufuta wa Kilwa uendelee kuwa bora na kuwataka wafanyabiashara kufuata utaratibu uliowekwa na mkoa ili kuhakikisha kwamba shughuli za uuzaji ufuta unaneemesha wakulima na kuondoa manung’uniko ya kucheleweshewa malipo yao.
Kitaifa
0
RAIS wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Leah Ulaya, amesema migomo na maandamano ya wafanyakazi katika kudai stahiki zao si suluhisho la mwisho kupata haki zao.Ulaya alisema hayo jana kwenye mkutano wa Shirikisho la Vyama vya Walimu vya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (FEATU), unaofanyika jijini hapa. Alisema migomo na maandamano, siyo njia sahihi ya kupigania haki na sio utaratibu, utakaohitimisha upatikanaji wa stahili kama vyeo na mishahara dhidi ya waajiri, bali ni vurugu ambazo mwisho zitapatiwa suluhisho katika meza ya mazungumzo kwa pande zote.Alisema alijifunza kwa migomo ya walimu iliyofanyika nchini Kenya hivi karibuni, ambayo ilichukua muda mrefu na mwisho wa siku walimu hawakupata suluhisho la madai yao. Badala yake, mwajiri aliwaambia hawakuwa kazini hivyo hana mshahara wa kuwalipa.“Wenzetu wa Kenya walikuwa na madai mbalimbali ya stahiki zao wakagoma kwa takribani mwezi mmoja, matokeo yake mwajiri ambaye ni serikali akawaambia sina pesa za kuwalipa kutokana na kutofanyakazi kwa muda mrefu, mambo haya si suluhisho la kufikia waliyoyataka, njia nzuri ni meza ya mazungumzo,” alisema.Rais huyo wa CWT alisema uzoefu alioupata kupitia vikao vya shirikisho la FEATU, umemsaidia kuona Tanzania kuna mafanikio kwa madai ya stahiki za kupanda madaraja, baada ya kukaa mezani na mwajiri na kuweka mkataba wa maridhiano na baadaye serikali, ambaye ni mwajiri mkuu kutekeleza madai hayo.“Umoja wetu wa FEATU kwa Afrika Mashariki uko bega kwa bega na Shirikisho la Kimataifa la Elimu la Afrika (EIA) na Chama cha Walimu cha Denmark (DLF) ambao ni wafadhili wa FEATU pamoja na Shirika la Kazi Duniani (ILO),” alisema.Mratibu wa FEATU ambalo makao yake makuu yapo Arusha, Anthon Mtavangu alisema shirikisho hilo limeshapeleka maombi ya kupewa fursa ya kushiriki katika masuala ya elimu.Aidha, Mtavangu alitaja madhumuni ya shirikisho hilo kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa ni kuunga mkono juhudi za jumuiya hiyo na mifumo na michakato ya sera za elimu, kusaidia kutunza, kuthamini na kuunga mkono lugha ya Kiswahili ndani ya shirikisho lenyewe na ndani ya jumuiya. Alisema madhumuni jingine ni kutetea maendeleo na viwango bora katika sekta ya elimu na mambo ya walimu. Alitaja nchi sita zinazounda shirikisho la FEATU kuwa ni Tanzania, Uganda, Zanzibar, Rwanda, Burundi na Kenya.
Kitaifa
0
['Mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 26, hatosaini kuongeza mkataba wake hivi sasa na anataka kujiunga na Real Madrid haraka iwezekanavyo. (Marca)', 'Paris St-Germain inamtaka kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen mwenye umri wa miaka 27, kama mchezaji atakayeichukua nafasi ya mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil Neymar, anayekaribia kurudi Barcelona. (Le Parisien)', 'Bayer Leverkusen inataka kumsaini beki wa kati wa Tottenham na timu ya taifa ya Ubelgiji Jan Vertonghen, aliye na miaka 32, kabla ya kuwadia Jumatatu muda wa mwisho wa dirisha la uhamisho Ulaya. (Kicker)', 'Beki kamili wa Manchester United na timu ya taifa ya Italia Matteo Darmian, mwenye umri wa miaka 29, yupo katika majadiliano kurudi katika ligi ya Serie A na klabu ya Parma. (La Gazzetta dello Sport kupitia Football Italia)', 'Mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal na timu ya taifa ya Misri Mohamed Elneny, aliye na miaka 27, yupo katika mazungumzo na timu ya Uturuki Besiktas kuhusu uhamisho wa msimu mzima kwa mkopo (Sky Sports)', 'Meneja wa Gunners Unai Emery anasema beki kamili mwenye umri wa miaka 33 Nacho Monreal, aliyehusishwa na uhamisho kwenda Real Sociedad, huenda akaondoka katika klabu hiyo kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho Ulaya. (Mirror)', 'Bosi wa Tottenham Mauricio Pochettino anasua sua kumuita mlinzi wa timu ya taifa ya Ivory Coast Serge Aurier kwa Derby ya London kaskazini siku ya Jumapili huko Arsenal wakati mchezaji huyo wa miaka 26 akiwa anaweza kuondoka kabla ya kufungwa dirisha la uhamisho Ulaya Jumatatu. (Evening Standard)', 'Manchester United ilijitoa katika mkataba wa msimu wa joto ya mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala, mwenye umri wa miaka 25, kutokana na matakwa ya malipo ya mchezaji huyo wa Argentina ya thamani ya £18m kwa mwaka. (Mail)', 'Aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku, mwenye umri wa miaka 26, amepunguza uzito wa mwili baada ya kufuata muongozo wa lishe chini ya meneja Antonio Conte tangu raia huyo wa Ubelgiji kujiunga na Inter Milan. (Mail)', 'Mlinzi wa Barcelona Gerard Pique anatumai kuwa Harry Maguire ataweza kuisaidia klabu yake ya zamani Manchester United kushinda taji la ligi kuu ya England. (Express)', 'Mchezaji wa kiungo cha kati wa Aston Villa Aaron Tshibola amejiunga na timu ya Ubelgiji Waasland-Beveren kwa mkataba wa miaka mitatu. (Birmingham Mail)', 'Arsenal dhidi ya Tottenham inajitayarisha kuipiku Liverpool dhidi ya Everton katika mchezo mkali wa Derby katika ligi kuu ya England. (Sun)', 'Kipa wa Paris St-Germain Alphonse Areola, mwenye umri wa miaka 26, amekubali kujiunga na Real Madrid. (RMC Sport)', 'Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Chile Alexis Sanchez, mwenye umri wa miaka 30, ametuma ujumbe kwa wachezaji wenzake wa Manchester United katika Instagram kabla ya kujiunga na Inter Milan kwa mkopo. (Manchester Evening News)', 'Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer yupo tayari kusubiri hadi msimu ujao w ajoto kushinikiza kiungo cha ushambilizi , huku mchezaji wa kiungo cha mbele wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 19, akisalia kuwa mchezaji anayemlenga pakuu. (Evening Standard)', 'Barcelona na Paris St-Germain zimekubali malipo ya uhamisho wa mchezaji wa miaka 27 wa timu ya taifa ya Brazil Neymar, lakini majadiliano yanaendelea kuhusu makubaliano ya mkataba huo. PSG inataka mchezaji wa kiungo cha mbele wa Ufaransa Ousmane Dembele, mwenye umri wa miaka 22, kuwa sehemu ya mpangilio huo. (Mirror)', 'Hatahivyo, Ajenti wa Dembele anasema mchezaji huyo hatoondoka Nou Camp, hatua ambayo huenda ikachangia kupromoka kwa pendekezo la uhamisho wa Neymar kwenda Barcelona. (Daily Mail)', 'Mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea raia wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, mwenye umri wa miaka 25, amekubali makubaliano ya kujiunga upya na Monaco kwa mkopo - huku kukipangiwa malipo ya £31.8m ka mkataba wa kudumu.(RMC Sport, kupitia Sun)', 'Mlinzi wa Arsenal Nacho Monreal, mwenye umri wa miaka 33, c huenda akarudi katika klabu alikotoka Uhispania kaba ya kufungwa dirisha la uhamisho Ulaya Jumatatu, huku Real Sociedad ikiwa na hamu kubwa ya kumsajili mchezaji huyo wa zamani wa Osasuna na Malaga. (Evening Standard)', 'Mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya England Sam Greenwood, mwenye umri wa miaka 17, ametambuliwa na timu bingwa ya Italia AC Milan na Juventus kama mchezaji anayelengwa baada ya kuridhisha maajenti katika mshindano ya ubingwa wa Ulaya wa timu za wachezaji walio chini ya umri wamiaka 17 mapema msimu huu wa joto. (Sun)']
michezo
2
Mizania ya benki hiyo ya nchini na yenye matawi visiwani Comoro, inaonesha kukua kwa asilimia 18 kutoka Sh bilioni 967 na kuvuka Sh trilioni moja mpaka Sh trilioni 1.14.Amana za wateja zimekua kwa asilimia 11 kutoka Sh bilioni 723 mpaka Sh bilioni 804, suala lililotokana na uamuzi wa benki hiyo kujikita zaidi katika amana zenye gharama nafuu.Makusanyo ya mikopo nayo yamekua kwa asilimia 23 kutoka Sh bilioni 455 mpaka Sh bilioni 559, fedha zikitawanywa katika sekta zote za kiuchumi na fedha za wanahisa kukua kwa asilimia 43 kutoka Sh bilioni 109.4 mpaka Sh bilioni 157.Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Ofisa Mkuu wa Fedha, Selemani Ponda alisema matokeo hayo mazuri yametokana na utendaji mzuri wa kibenki unaoenda sambamba na kukua kwa benki hiyo.“Mwaka jana tuliweza kutekeleza kikamilifu mikakati yetu ya ukuaji wa benki kupitia uwekaji msisitizo katika amana zenye gharama ya chini na uboreshaji wa shughuli zetu zilizowatoshereza wateja wetu,” alisema Selemani na kuongeza:“Kutokana na mikakati hiyo, pato litokanalo na tozo mbalimbali limepanda kwa kiasi kikubwa kwa asilimia 33 kutoka Sh bilioni 22.8 mwaka jana mpaka Sh bilioni 30.4.”Kwa upande wa biashara za kimataifa zimeonesha kufanya vizuri na kuongezeka kwa faida ya asilimia 26 kabla ya kodi kila mwaka kwa Benki ya Exim Comoro mpaka Sh bilioni tatu hivyo kuchangia asilimia 15 ya faida katika benki.“Kutokana na utendaji mzuri wa Benki ya Exim nchini Comoro kwa mwaka 2013, tawi limeweza kutoa gawio la kiasi cha Sh bilioni mbili litakalopokelewa na benki mama ya Exim Tanzania katika mwaka 2014,” aliongeza Selemani.Katika mwaka, pato la riba ya jumla imekuwa kwa asilimia moja kutoka Sh bilioni 45 mpaka Sh bilioni 45.4. Pato litokanalo na fedha za kigeni limekua kwa asilimia 73 kutoka Sh bilioni nne mpaka Sh bilioni 6.9 wakati huo huo pato la ada na kamisheni likikua kwa asilimia 24 kutoka Sh bilioni 17.7 mpaka Shi bilioni 22.“Mwenendo wa kiutendaji wa benki yetu unaonesha mafanikio katika nyanja zote za kibiashara. Pato letu la jumla la uendeshaji limeongezeka kwa asilimia 12 kutoka Sh bilioni 67.7 mpaka Sh bilioni 75.8,” alisema Ofisa huyo mkuu wa fedha.Alisema kuwa gharama za jumla za uendeshaji zimeweza kukua mpaka asilimia 17.8 kutoka Sh bilioni 45.5 mpaka Sh bilioni 53.6 ongezeko hilo likitokana na uanzishwaji wa matawi mapya na motisha kwa wafanyakazi katika jitihada za kuongeza upatikanaji wetu kijeografia na kuiimarisha benki kwa ujumla.
Biashara
1
KAMATI ya Uchaguzi ya klabu ya Simba imeweka wazi mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Novemba 3, mwaka huu.Akizungumza na vyombo vya habari jana Mwenyekiti wa kamati hiyo, Boniface Lyamwile amesema Kamati imeona Septemba 3 ndio siku sahihi ya kufanya uchaguzi, hivyo wanatarajia uwe wa haki na huru kwa kufuata katiba mpya ya Simba na kanuni za uchaguzi za TFF.‘’Katiba ya Simba imeeleza nafasi sita zinazogombewa, ya kwanza ya Mwenyekiti na mjumbe wake ambao wanatakiwa kuwa na kiwango cha elimu kuanzia Shahada ya kwanza, ya pili wajumbe wanne wenye kiwango cha elimu kuanzia kidato cha nne pia awepo angalau mwanamke mmoja,’’ amesema.Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Steven Ally alielezea mchakato mzima kuelekea uchaguzi huo.‘’Kuanzia kesho (leo) mpaka Septemba 10 uchukuaji waa fomu, mgombea awe na nyaraka za malipo yaliyofanyika kwenye akaunti ya klabu, Septemba 11-15 kurudisha fomu, Septemba 16-18 usaili utaanza rasmi kwa wagombea na kamati itabandika wagombea waliokidhi vigezo’’.Ally amesema wanachama wenye pingamizi wawasilishe kuanzia Septemba 21-23 saa 3 asubuhi mpaka 10 jioni Makao Makuu ya klabu.Septemba 24-26 ni kipindi cha kupitia pingamizi, Septemba 27-29 kufanya mahojiano na waliowekewa pingamizi na kutolewa maamuzi ambaye hajaridhika atakata rufaa kwenye kamati ya rufaa TFF.‘’Oktoba 2, mwaka huu tutatangaza majina ya wagombea waliokidhi vigezo na Oktoba 3 kampeni kwa wagombea zitaanza rasmi huku Novemba 3 mwaka huu uchaguzi utaanza rasmi na siku hiyo hiyo kama mchakato utaenda kama ulivyopangwa watatangazwa washindi wa nafasi hizo,’’ amesema Ally.Ada ya fomu kwa mwenyekiti ni Sh 500,000 na kwa wajumbe wote ni Sh 300,000. Sehemu ya kuchukua na kurudisha fomu ni makao makuu ya klabu kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 10 jioni.Alisema Ally. Pia Ofisa habari wa klabu hiyo, Haji Manara aliwaomba wanachama wa Simba kuwa watulivu na kuwa makini katika uteuzi wa watu makini kwa kuzingatia vigezo vinavyohitajika na kusisitiza kuwa wao kama wajumbe wa uchaguzi hawatohusika katika kufanya kampeni yoyote."Kesho (leo) zoezi la kuchukua fomu litaanza rasmi kwa ajili ya kutoa wajumbe wanane ndani ya bodi ya wakurugenzi wa klabu. Tuwe makini katika uteuzi huo kupata watu watakaotupeleka mbele, sina shaka mwekezaji ataleta watu wake madhubuti na sisi tusijiangushe wenyewe,’’ alisema Haji.
michezo
2
MSANII nguli wa bongo fl eva, Nassib Abdull ‘Diamond Platnumz’ amesema anatarajia kutoa msaada kwa ajili ya wakazi wa mtaa aliozaliwa wa Tandale Dar es Salaam ambapo anakaridia kutumia zaidi ya Sh milioni 465. Msanii huyo aliliambia gazeti hili kuwa atatoa bima za afya kwa kaya 250, ambapo kila kaya ni Sh 1,501,200 kwa bima ya NHIF. Kwa maana hiyo kwa kaya 250 atatumia zaidi Sh milioni 375. Pia atatoa mitaji ya biashara kwa akina mama ambapo ina karidiwa atatumia zaidi ya Sh milioni 20 kwa akina mama 100.“Nitagawa Sh laki moja mpaka Sh laki mbili kwa akina mama wa Tandale,”alisema Diamond. Alisema atatoa pikipiki 20 kwa ajili ya vijana ili wajikwamue kiuchumi ambapo inakadiriwa atatumia zaidi ya Sh milioni 50. Muimbaji huyo ambaye ni rais wa kundi la WCB, alisema atakarabati shule za Tandale pamoja na kuweka matangi ya maji ambapo inakadiriwa atatumia zaidi ya Sh milioni 50. Alisema ili kuhakikisha anatekeleza ahadi hiyo leo ataambatana na viongozi mbalimbali wa serikali na kampuni mbalimbali kuwakabidhi msaada huo
michezo
2
WAPINZANI wa Yanga, Pyramids wanaotarajiwa kumenyana kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika wametoka suluhu dhidi ya Smouha FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu nchini Misri uliochezwa Uwanja wa June. Yanga wanatarajia kuumana na Pyramids kwenye mchezo huo wa kwanza ambao wanajangwani hao wanahitaji ushindi wa mabao mengi Oktoba 27 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi. Timu hizo zinataraja kukutana Novemba 3 katika mchezo wa marudiano wa play-off kwa ajili ya kusaka nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Matokeo hayo yana wafanya Pyramids kushika nafasi ya pili kwa hazina ya pointi nane kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiwa nyuma ya vinara wa ligi hiyo Al Ahly inayoongoza kwa pointi tisa baada ya kucheza michezo mitatu. Pyramids hadi sasa kwenye ligi hiyo wamefanikiwa kushinda mechi mbili dhidi ya ENPPI wanaoshika mkia kwa kuwa na pointi moja, dhidi ya Tanta wanaoshika nafasi ya 11 kwenye msimamo huo huku wakitoka sare mechi mbili dhidi ya Smouha na Tala ‘ea EL-Gaish.Matokeo hayo Pyramids bado yanatengeneza uwiano mdogo dhidi ya Yanga wanaoshika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kucheza mechi tatu na kushinda moja, kufungwa moja na kutoka sare moja. Yanga wanatarajiwa kuondoka kesho kwenda Mwanza kuanza maandalizi ya kuwakabili wapinzani wao hao kabla ya mchezo huo.
michezo
2
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imesema taasisi na mashirika mengi ya serikali yanatumia huduma za Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) chini ya kiwango wakati serikali imewekeza kwa kiwango kikubwa katika kuinua shirika hilo.Kutokana na madai hayo, PIC imeagiza watendaji wa shirika hilo kubadilika na kwenda kwa kasi zaidi katika utendaji wake ili kaulimbiu ya “Rudi Nyumbani Kumenoga” iwe na ufanisi zaidi kwa jamii.Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Raphael Chegeni ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea shirika hilo kuona uwekezaji pamoja na utendaji kazi wake.Kuhusu uwekezaji huo, Dk Chegeni amesema kamati imebaini taasisi na mashirika ya serikali hazitumii vizuri huduma za TTCL bila maelezo ya kutosha namna linavyoweza kuendelea kulitumia shirika.“Taasisi nyingi zinatumia TTCL chini ya kiwango, ilhali serikali imewekeza kwa kiwango kikubwa,” amesema Dk Chegeni na kuongeza kuwa inatakiwa uwekezaji uliofanywa ulete manufaa hapa nchini.Taasisi za serikali zilizounganishwa na mtandao wa Mkongo wa Mawasiliano zitakuwa zinawasiliana kwa huduma iliyoboreshwa zaidi yenye uhakika na iliyoboreshwa katika sekta hiyo ya mawasiliano.Aidha, alisema uwekezaji unaofanywa nchini unagharamiwa na serikali, na isiwe ni kwa shirika ili kurahisisha katika kufanya hesabu.Alisema TTCL ilitoa gawio serikalini la Sh bilioni 1.5 kwa kipindi cha mwaka jana, huku likiazimia kufikia gawio la Sh bilioni mbili kwa mwaka huu.Alisema ni muhimu kwa mashirika na taasisi za serikali kutoa gawio serikalini na kutofanya kazi chini ya kiwango, badala yake kubadilika na kujiboresha zaidi. “Kama ilivyo kauli ya rudi nyumbani kumenoga, ni vyema ikajulikana TTCL ndio chaguo la kwanza, hivyo vyema likabadilika na kuenda kwa kasi zaidi ili kuendelea kuwa wabunifu,” alisema Dk Chegeni.Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Omar Nundu amesema shirika hilo linaendelea kujiimarisha kwa kufanya miradi mbalimbali iliyokuwepo kabla ya mabadiliko na hata ambayo inaendelea kuibuliwa na shirika.“Kazi kubwa imefanyika ya kulibadilisha shirika na tumeanzisha miradi kadha wa kadha ikiwemo pia T-Pesa na hata wakala jambo lililowezesha hisa za soko kuongezeka kutoka asilimia 0.84 kwa kipindi cha mwaka jana na kufikia asilimia mbili,” amesema Nundu.Amesema ipo miradi mbalimbali iliyoanzishwa na shirika hilo na ambayo inaendelea kuanzishwa ambayo miongoni mwake ipo ambayo waasisi wake ni wao peke yao ambayo itajulikana kadri itakavyotakiwa.
Biashara
1
MREMBO wa vyuo vikuu nchini ya El Salvador, Mariselo De Montecristo ameahidi kujitolea kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania nje ya nchi kwa kuwa bado havijulikani nje ya nchi.Mrembo huyo aliyasema hayo alipokuwa katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire iliyopo mkoani Manyara na kupokelewa na mkuu wa idara ya Utalii ya Hifadhi hiyo, Neema Philipo.Alisema aliposhuka tu katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro, KIA, alijiona yuko katika nchi yenye hali tofauti kimazingira na kila alipokuwa akipata taarifa ya vivutio mbalimbali kutoka kwa muongoza watalii, Denis Meela pale KIA na Tarangire, alijuwa wazi kuwa nchi hii ina vivutio vingi, lakini havijatangazwa nje ya nchi.Montecristo ambaye aliambatana na mama yake mzazi na rafiki yake wa kiume alisema ni mara yake ya kwanza kuja nchini, lakini aliahidi kuwa Balozi mzuri wa kutangaza vivutio katika mji wa Califonia nchini Marekani anakoishi na kufanya kazi.‘’Ni mara yangu ya kwanza kuja hapa Tanzania na nimefurahishwa sana na vivutio vya kitalii nilivyoviona hapa Tarangire na nitakuwa Balozi wa kutangaza vivutio katika mji wa Calfonia ili watalii wengi waweze kuja kutembelea hifadhi hii,’’ alisema.‘’Zawadi za kitamaduni nilizopewa na uongozi wa Tarangire na akina mama wa kimasai ni kichocheo kikubwa kwangu kuutangaza utalii wa Tanzania nje ya nchi, “alisema mrembo huyo.Mkuu wa Idara ya Utalii katika Hifadhi ya Tarangire, Neema alisema kuja kwa mrembo huyo kutautangaza utalii nje kwani ameahidi kufanya hivyo baada ya kujionea mwenye vivutio kibao katika hifadhi ya Tarangire ukiachilia mbali wanyama.Neema alisema ameahidi kutembelea hifadhi mbalimbali hapa nchini ikiwemo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na kupiga picha, lengo ni kuutangaza utalii nje ya nchi.Muongoza Watalii Meela alisema kuwa mrembo huyo amevutiwa sana na vivutio vingi vya hapa nchini na alipokuwa akimpa taarifa za vivutio hivyo alisema angependa kwenda kila sehemu ya vivutio hivyo.Meela amesema, mrembo huyo ameahidi mambo mengi, ikiwemo kuutangaza utalii nje hasa Calfonia anakoishi na ameahidi kuwahimiza warembo wengi zaidi wa nchi mbalimbali kuja nchini kutalii.
michezo
2
['Usakaji wa mshambuliaji katika klabu ya Aston Villa ulikuwa mgumu hali ya kwamba mkufunzi wa klabu hiyo Dean Smith alilazimika kukubali kwamba jeraha la mshambuliaji wa pekee Wesly lilikuwa limemaliza msimu wa mchezaji huyo hivyobasi shinikizo ya kutafuta mchezaji atakayechukua nafasi yake ilifaa kuanza. ', 'Kulingana na mtandao wa Birmingham Live ulionukuliwa na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, wakati mmoja Villa ilishiriki mechi bila mshambuliaji mwafaka katika mechi za ligi na zile za kuwania makombe. ', 'Ni hapa ambapo jina la Mbwana Samatta lilichipuka kama mshambuliaji ambaye angefunga magoli yaliohitajika na Villa ili kuweza kusalia katika ligi ya premia. ', 'Pia unaweza kutazama:', 'Huku dau la £8.5m likikubalika ili kumnunua mchezaji huyo, hii ilikuwa bei ya chini ukitazama thamani ya washambuliaji kipindi hiki hususan wakati wa dirisha dogo la uhamisho la mwezi Januari ambapo wengi hawataki kuondoka katika klabu zao. ', 'Kwanini watafutaji wa wachezaji Villa walimchagua Mbawana Samatta?', 'Lakini kwanini maskauti wa klabu ya Villa walifikiria kuhusu Mbwana Samatta kama mtu ambaye angeleta mafanikio na kuisaidia Villa kusalia katika Ligi. ', 'Ripoti moja inasema kwamba , Samatta ambaya kwa sasa ana umri wa miaka 27 anaelekea kilele chake , huku akionekana kuwa na mchango mkubwa wa kuisaidia Villa kusalia katika ligi. ', 'Mchezaji huyo mwenye urefu wa futi 5 ana uwezo wa kucheza kwa kutumia maguu yote mawili , ana kasi na kwamba ameimarika sana katika kipndi cha miaka miwili iliopita. ', 'Amecheza mara 28 katika mashindano yote kufikia sasa msimu huu , akifunga mara 10 na kutoa pasi mbili zilizozsababisha magoli. ', 'Mwaka uliopita alicheza mara 51 na kufunga magoi 32 mbali na kutoa pasi sita zilizosababisha magoli - hatua iliomfanya kushinda taji la mfungaji bora. ', 'Ripoti ya watafutaji wa wachezaji katika klabu hiyo pia ilionyesha kwamba , Samatta ni aina ya mchezaji ambaye yuko tayari kufunga katika lango la upinzani. ', 'Walidai kwamba Samatta ndio mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa katika ligi ya Ubelgiji kwa sasa , akiwa na sifa ambayo ni vigumu kwa upinzani kumzuia.', 'Kulingana na The Citizen Tanzania Ripoti hiyo inasema kwamba Samatta ni mchezaji hatari anapopewa fursa ya kufunga na kuchangia magoli ndani na nje ya lango la upinzani. ', "'Uwezo wake wa kuruka juu ni salaha yake kuu'", 'Ana uwezo wa kufunga kwa njia tofauti. Uwezo wake wa kuruka angani ndio silaha yake kubwa hatua iliowafanya mabeki wa Liverpool akiwemo Vigil Van Dijk kushindwa kumkabili. ', 'Amefunga magoli matatu kupitia kichwa msimu huu rekodi iliopitwa na mchezaji mmoja pekee. ', 'Msimu uliopita alifunga jumla ya magoli saba kupitia kichwa na rekodi hiyo ilipitwa na mchezaji mmoja pekee aliyefunga magoli manane. ', 'Uwezo wake wa kuruka juu utaisaidia sana timu ya Smith wakati wa mipira ya adhabu mbali na kwamba umbo lake linamruhusu kuzuia mipira kabla ya kutoa pasi, ijapokuwa ni mahiri sana wa kumaliza anapopata pasi murua karibu na lango la upinzani. ', 'Ilipendekezwa kwamba wakati Wesley atakaporudi, uwezekano wa yeye kushirikiana na Samatta utawaburudisha mashabiki wa Aston Villa iwapo kocha huyo atawachezesha pamoja. ', 'Wote wana nguvu na uwezo wa kuwakabili mabeki hatua ambayo itatoa fursa kwa Jack Grealish na wengine kuonesha umahiri wao.']
michezo
2
Mwenyekiti wa chama hicho, Otieno Igogo alimwambia mwandishi wa habari hizi, kwamba kiwango cha Sh milioni 14 cha sasa ni kidogo, kitafanya wafanyabiashara wengi kuacha biashara au kubuni mbinu za kukwepa kifaa hicho.“Sisi tunadhani nia njema ya Serikali kuongeza idadi ya walipa kodi itakwama kama kiwango cha Sh milioni 14 hakitapitiwa upya kwani wafanyabiashara wengi wadogo mtaji wao ni mdogo kuweza kumudu kununua na kutumia mashine hizo,” alisema.Alitoa mfano kwamba kupitia Sheria ya Mapato ya sasa, mfanyabiashara anaruhusiwa kupata faida ya asilimia 30 kwa mwaka kama kiwango cha juu, kwa hiyo kama mauzo yake ni Sh milioni, akitoa faida, anabaki na Sh milioni 9.8.“Ukichukua pesa hiyo na kuigawanya kwa miezi kumi na miwili basi utaona kwamba mtaji wa mfanyabiashara huyu mdogo ni Sh 816,000 ambao ni karibu kabisa na bei ya juu ya kifaa cha EFD,” alisema Igogo.Alihoji pia mkataba uliotiwa saini kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kampuni nne za Italia na Bulgaria, zinazotengeneza vifaa hivyo.Alisema makataba huo unawanyima wafanyabiashara haki ya kufanya matengenezo au kununua vitu kama karatasi, wino kutoka kwa wauzaji wengine, isipokuwa mtandao huo uliopewa baraka na TRA.Alidai karatasi za kutumia kwenye mashine, zinauzwa Sh 16,000 na wasambazaji rasmi walioidhinishwa na TRA. Kaimu Kamishina Mkuu wa TRA, Rished Bade alikanusha bei ya karatasi kuwa kubwa.Aidha alisema wafanyabiashara hawalazimishwi kulipa gharama za matengenezo kwani ndani ya mwaka mmoja huduma hiyo hutolewa bure.“Lakini suala la kima cha chini kuongezwa kutoka Sh milioni 14 mpaka Sh milioni 20, basi siyo letu TRA bali Serikali,” alisema. Bade alisisitiza kwamba jukumu la TRA ni kukusanya kodi na siyo mambo ya sera wala utungaji sheria.
Biashara
1
OFISA Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Hamis Lissu amewataka walimu wakuu na wakuu wa vyuo kuhakikisha wanafuata miongozo ya elimu, ikiwemo ya kutowafukuza shule wanafunzi bila bodi kukaa na kutochapa wanafunzi bila kupimwa afya zao.Akizungumza kwenye mahafali ya 11 ya Chuo cha Walimu Ebonite Dar es Salaam jana, Lissu alisema wapo baadhi ya walimu wakuu na wakuu wa vyuo ambao wanatumia vibaya madaraka yao kwa kuwafukuza wanafunzi bila kusubiri maamuzi ya bodi ambayo ndio yenye mamlaka. Alisema serikali imeweka miongozo mbalimbali ikiwemo huo wa kukataza wanafunzi kufukuzwa hata kama amefanya kosa kubwa, bodi ndiyo yenye maamuzi na nguvu ya kumfukuza mwanafunzi na badala yake wakuu wa shule na vyuo wanapaswa kumsimamisha shule hadi maamuzi yatakapotoka.“Kufanya maamuzi kama haya mwanafunzi anaweza kukata rufaa na tunaweza kumrudisha chuoni au shuleni hata kama alimpiga mwalimu au kumtukana, kwa sababu taratibu za kumfukuza hazikuzingatiwa halafu baadaye mtasema tumewadharau lakini sivyo,”alisema. Katika muongozo wa elimu unaelekeza kuwa anayepaswa kutoa adhabu ya kiboko ni mwalimu mkuu pekee au walimu watakaopewa mamlaka ya kuchapa viboko vinene pekee.Lissu alifafanua kabla ya kuadhibiwa kwa mwanafunzi yafaa kupimwa afya zao ili kuepusha kesi mbalimbali, kwani wapo wanafunzi ambao hata akichapwa kiboko kimoja anaweza kuanguka na kupoteza maisha. Alisisitiza walimu wanapaswa kuzingatia miongozo hiyo na sio kuwachapa wanafunzi kama mbwa koko na kuwasababishia ulemavu. Aidha, alisema mwaka jana shule saba za mkoa huo zilichafua taswira ya elimu baada ya kuvujisha mtihani na kusababisha wanafunzi 801 kufutiwa matokeo yao.“Walimu mnapaswa kujiamini katika ufundishaji na sio kuamini katika mitihani feki ambayo haimjengi mwanafunzi kwani wenzenu wana kesi mahakamani na wengine wamekimbia nchini kwa sababu ya kufanya udanganyifu,”alieleza. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya ushauri wa chuo hicho, Thadeous Njuu alisema wanakumbana na changamoto ya upungufu wa wanafunzi kwa sababu udahili wa kozi ya ualimu hivi sasa ni daraja la tatu ya 25.Njuu alisema zamani walikuwa wanapata wanafunzi wengi kutokana na kuchukua wanafunzi wenye daraja la nne ya 28 na wanafanya kazi vizuri hivyo serikali ione haja ya kulegeza masharti ili wapate wanafunzi wengi. “Bado tunachangamoto ya kodi ya majengo ambayo kwa mwezi ni zaidi ya shilingi milioni nane, hivyo uendeshaji wa chuo hiki unakuwa mgumu kwani wanafunzi tulipokea ni wachache na mahitaji ya kodi ni mengi hivyo tunamuomba rais akutane na wamiliki wa vyuo na shule binafsi ili kujadiliana kuboresha elimu,”alifafanua.Naye, Mkuu wa chuo hicho, Mwinjuma Mirambo alisema walimu 130 ndio ambao wamehitimu kozi ya astashahada na stashahada ya elimu ya awali na elimu msingi. Mirambo alisema walipoanza kutoa mafunzo ya ualimu mwaka 2007, walikuwa wanatoa mafunzo ya ualimu daraja la 3A na baadaye walianza mafunzo ya elimu ya awali kwa nadharia na vitendo. Alieleza kuwa mwaka 2015, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ilikipandisha hadhi chuo hicho na kuwa kama taasisi.
Kitaifa
0
MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege (TAA) imesema Jengo la Tatu la Abiria (Terminal III) la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), litaanza kutumiwa na ndege kwa majaribio kuanzia Julai 17 hadi Julai 29, mwaka huu kabla ya kuzinduliwa Agosti, mwaka huu.Katika hatua nyingine; Shirika la Reli nchini (TRC) limesema mataluma yote yanayotumika katika ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), yanazalishwa nchini na kwamba kiwanda kinachozalisha mataluma hayo cha Soga mkoani Pwani kimeongeza uzalishaji kutoka mataruma 1,080 hadi 1,500 kwa siku.Kuhusu Terminal III kuanza kufanyiwa majaribio, Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Julius Ndyamukama alisema ujenzi wa uwanja huo umekamilika na Julai 17 hadi 29, mwaka huu wataanza kurusha ndege kwa majaribio. Alisema uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuwa na ndege 22 za safari za kimataifa.Alikuwa akitoa taarifa kwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliofanya ziara kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo uwanja huo.Ndyamukama alisema baada ya kuanza kutumika kwa jengo hilo jipya, jengo la zamani maarufu kama Terminal II litaanza kutumika kwa ndege za abiria wa ndani. Kuhusu mataruma ya reli ya SGR, Mkurugenzi Mkuu waTRC, Masanja Kadogosa alisema kuna maneno ya uzushi yanayodai kuwa mataluma yanatoka nje ya nchi, jambo ambalo si la kweli.Kadogosa aliwaeleza pia wajumbe hao kuwa mwezi ujao, wanatarajia kuingiza treni za mizigo tatu zenye uwezo wa kubeba tani 10, 000, ambapo treni moja ina uwezo wa kubeba malori 500 ya tani 20. Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo alisema miradi wa SGR ni moja ya miradi mikubwa iliyopo katika mkoa huo na kazi yao ni kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo.
Kitaifa
0
["Real Madrid wana mpango wa kuanzisha ''operesheni 200'' wakiwa na mpango wa kuwauza Gareth Bale, 30 na James Rodriguez, kwa ajili ya kuuwezesha kifedha mpango wao wa kumnunua kiungo Paul Pogba. (Marca, via Sun)", 'Neymar amefungua milango kwa United wakati akiwa na shauku ya kuondoka Paris Saint-Germain. (Mundo Deportivo, via Sun)', 'Kocha mkuu wa Newcastle Steve Bruce kutumia zaidi ya pauni milioni 90 katika dirisha la usajili. (Sky Sports)', "Bruce 'alikuwa chaguo la 11' kwa ajili ya kazi hiyo ndani ya Newcastle. (Daily Mail)", "'Arsenal kuwasajili wachezaji maarufu na ghali zaidi'", 'De Ligt safarini kukamilisha usajili na Juventus ', "Hoffenheim wamethibitisha kuwa mshambuliaji Joelinton, 22, yuko kwenye ''mazungumzo ya kina'' na klabu hiyo na Newcastle United wana matumaini ya kuvunja rekodi kumnasa mchezaji huyo mwenye asili ya Brazil. (Chronicle Live)", "Kocha wa Leicester Brendan Rodgers amesifu utaalamu wa Harry Maguire, 26, na kukubali kuwa alikuwa ''ametulia'' kuhusu nia ya Manchester United kumnasa mlinzi huyo wa kati .(Independent)", 'Liverpool haina mpango kabisa wa kumuuza golikipa Simon Mignolet, 31 kwa mkopo kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Liverpool Echo)', "Manchester United iko kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya kiungo wa Roma Nicolo Zaniolo. (Mirror)", 'Mshambulizi Romelu Lukaku, 26, ana mpango wa kuondoka Manchester United na kuhamia Inter Milan. (Times - subscription required)', "Unai Emery amesisitiza kuwa Arsenal wanafanya kazi kupata wachezaji ''watatu au wanne kabla ya kuanza msimu mpya. (Independent)", 'Kiungo Granit Xhaka yuko kwenye nafasi ya kuwa nahodha wa Arsenal akichukua nafasi ya Koscielny. (Telegraph)', 'Wadau wa klabu ya Juventus wamempa wakala wa Matthijs de Ligt mapokezi makubwa wakati alipoambatana na mchezaji huyo, mwenye miaka 19 kwa ajili ya vipimo siku ya Jumatano. (Metro)', 'Mchakato wa Arsenal kumpata mlinzi wa kikosi cha Celtic, raia wa Scotland Kieran Tierney huenda ukapata upinzani kumnasa mchezaji huyo. . (Scotsman)\ue028', 'Arsenal imepewa angalizo kuwa haitaweza kufikia dau la Crystal Palace kwa ajili ya mshambuliaji Wilfred Zaha. (Mirror)', 'Pep Guardiola amefungua milango kwa Leroy Sane, 23, kuondoka Manchester City kwa kumwambia winga huyo anaweza kufanya hivyo kama hana furaha. (Mirror)', 'Burnley wana nia ya kumuuza golikipa wa kimataifa Tom Heaton wa England, kwa pauni milioni 12. (Birmingham Mail)', "Ashley Cole amesababisha minong'ono kuwa yuko mbioni kuingia kwenye jopo la makocha wa Chelsea, baada ya kuweka picha yake akiwa uwanja wa ndege akielekea Japan. (Mirror)"]
michezo
2
MABINGWA wa Ligi Kuu nchini, Simba wanatarajiwa kucheza mechi maalumu ya kirafi ki dhidi ya Sevilla ya Hispania Mei 23 mwaka huu.Awali waandaaji wa mechi hiyo kampuni ya SportPesa walikuwa kwenye kigugumizi cha nani acheze na Sevilla kati ya Simba na Yanga lakini jana Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa katibu wake mkuu, Kidao Wilfred walikata mzizi wa fitina na kuitangaza Simba kupata nafasi hiyo kwa vigezo walivyoweka. Kidao aliwaambia waandishi wa habari kuwa timu iliyofanya vizuri kwenye michuano ya SportPesa iliyofanyika nchini ndiyo itakayopata nafasi hiyo na hivyo wameiteua Simba kwa vile ilifika nusu fainali.“Timu ya Tanzania ambayo ilifanya vizuri katika mashindano ya Sportpesa yaliyopita ni Simba na ilifika nusu fainali hivyo ni rasmi sasa Simba itacheza na Sevilla ni jambo la kujivunia,” alisema Kidao. Awali Sportpesa ikishirikiana na serikali ilipeleka ombi kwa bodi ya ligi ya Tanzania kuomba nafasi ya kuandaa mechi ya Simba na Yanga ili mshindi wa mchezo huo acheze na Sevilla lakini ilishindika na ndipo ilipokabidhi jukumu hilo kwa TFF.Pia klabu hizo zimegomea kuunda timu ya kombaini ambayo itacheza na Sevilla baada ya nafasi ya kuandaa mechi kukosekana. Mbali na kuishia nusu fainali kwenye michuano ya SportPesa iliyoshirikisha pia timu kutoka Kenya, Simba pia imekuwa na msimu mzuri kwenye michuano ya kimataifa baada ya kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa na kung’olewa na TP Mazembe ya Congo DR. Msemaji wa Simba, Haji Manara alisema jana ni heshima kubwa kwao kucheza dhidi ya Sevilla iliyowahi kuwa bingwa wa Europa kwa misimu mitatu mfululizo.
michezo
2
Mazrui alitoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara ya kukagua mashamba ya miwa Mahonda Wilaya ya Kaskazini Unguja ambayo yameteketea kwa moto na watu wasiojulikana ambapo inadaiwa ni matukio ya hujuma.'Vitendo vya hujuma vinaijengea taswira mbaya Zanzibar katika sekta ya uwekezaji...tukiendelea na hujuma hizi hakuna mwekezaji atakayekuja kuwekeza Zanzibar,” alisema Mazrui.Alisema kitendo cha kutia moto ekari 18 za miwa, ambazo zilikuwa zivunwe hivi karibuni kwa ajili ya uzalishaji wa sukari kwa majaribio, zimerudisha nyuma juhudi hizo za kuimarisha sekta ya viwanda na uwekezaji.Alisema tabia kama hizo haziwezi kuachiwa, kwani zitarudisha nyuma maendeleo katika sekta ya viwanda, ambapo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa sasa ipo katika hatua za mwisho kutayarisha sera ya viwanda.Mshauri Mkuu wa kiwanda cha Sukari cha Mahonda, Dk Hamza Husein Sabri alisema lengo la kiwanda kuanza kuzalisha sukari mwezi ujao kwa majaribio.Alisema kiwanda kimeingia hasara ya Sh milioni 750, ambapo tani 500 za miwa zimeathirika zikiwa tayari kwa ajili ya uzalishaji wa sukari kwa majaribio.“Kitendo cha hujuma katika kiwanda cha sukari cha Mahonda zimerudisha nyuma maendeleo ya sekta ya uzalishaji wa sukari nchini...tulitegemea kuzalisha sukari mwezi ujao,” alisema.Kiwanda cha sukari cha Mahonda kilijengwa mwaka 1971 kwa msaada wa serikali ya watu wa China, ambapo waliimarisha mashamba ya miwa kwa ajili ya uzalishaji wa sukari.Baada ya kukaa zaidi ya miaka 15 bila ya uzalishaji wa sukari, mwekezaji mpya ameanza kazi ya kufufua mashine na mitambo kwa ajili ya kuzalisha sukari na kuimarisha mashamba ya miwa.
Biashara
1
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mifugo, Profesa Elisante ole Gabriel amezitaka taasisi za fedha nchini kuchangamkia soko la usindikaji wa maziwa linalohitaji uwekezaji wa kimkakati kutokana na kiasi kidogo cha maziwa kusindikwa. Gabriel ametoa rai hiyo katika kongamano la 10 la Wiki ya Maziwa kitaifa nchini. Alisema kiwango cha maziwa kwa mwaka ni lita bilioni 2.7 wakati kiwango cha maziwa kinachosindikwa ni lita milioni 56 hatua inayomnyima mapato mazuri mfugaji nchini. “Nitoe mwito kwa taasisi za fedha kuchukua fursa hii muhimu kwa kuwekeza kwa nguvu kwenye mnyororo wa thamani ili kuyapa thamani maziwa yetu. Ipo fursa kubwa ambayo itawasaidia wafugaji na taasisi zenu kupata faidi,” alisema Gabriel. Kongamano hilo la wadau kutoka mikoa mbalimbali nje ya nchi linajadili namna ya kuongeza uzalishaji bora wa maziwa nchini. Pia linajadili kukabiliana na changamoto za upatikanaji mbegu bora za uhamilishaji, malisho ya mifugo, masoko ya maziwa na uhaba wa viwanda vya usindikaji wa maziwa nchini. Mwenyekiti wa Bodi ya Maziwa nchini, Lucas Malunde alisema viwanda zaidi vinahitajika kuongeza kiwango cha maziwa yaliyosindikwa kumpa faida mfugaji na mtumiaji wa maziwa. Alisema kiwango cha matumizi ya maziwa kwa mtu mmoja hapa nchini kipo chini kiasi cha lita 49 kwa mwaka wakati lengo ni kumwezesha mtu kutumia lita 200 za maziwa kwa mwaka. Ofisa Utafiti wa benki ya NMB, Mboka Mwanitu alisema wametenga Sh bilioni 500 kwa tasnia ya maziwa kwa ujumla. Alisema wapo wajasiriamali walionufaika kwa kuchukua mkopo wa Sh bilioni 30 kutokana na kuongezeka mahitaji ya maziwa nchini. Alisema mikopo yao imelenga kupata mbegu bora za ng’ombe, vituo bora vya kukusanyia maziwa, vifaa vya kisasa vya usindikaji maziwa, malisho na huduma za chanjo na matibabu.
Kitaifa
0
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi wakati akifunga mafunzo ya wajasiriamali wa Mkoa wa Dodoma yaliyoendeshwa na kampuni ya Mjasiriamali Kwanza Enterprises kwa udhamini wa Benki ya Akiba Commercial (ACB).Alisema wanawake wengi wamekuwa wakijitahidi kufanya biashara lakini wanashindwa kuwa na mipango mizuri ya fedha wanazopata kwani asilimia kubwa ya fedha hizo hutumika kununua nguo.“Kila nguo inapotoka unayo, wako wengi watanunua si lazima ununue wewe, kila siku unahangaika na khanga mpya achana na hayo fikiria maendeleo ya biashara kwanza,” alisema.Pia alisema wengi wamekuwa wakitumia fedha za mtaji wa biashara kununua vocha za simu na kuzungumza bila mpangilio bila kufahamu kuwa fedha wanazotoa mara nyingi huwa hazirudi.Aidha aliwataka wajasiriamali hao kutosita kukopa katika taasisi za kifedha ili waweze kuinua mitaji yao na kujiimarisha kibiashara kwani hata wafanyabiashara wakuba wamekuwa wakitumia taasisi za fedha kupata mikopo kwa ajili ya kuendesha biashara zao.Mkurugenzi wa Mjasiriamali Kwanza Enterprises, Dk Didas Lunyungu alisema washiriki wanawake wamekuwa wakihudhuria kwa wingi kwenye mafunzo hayo kwenye mikoa mingi ambapo wamekuwa wakipita kupata mafunzo hayo.Wajasiariamali zaidi ya 800 wa mkoa wa Dodoma walihudhuria mafunzo hayo ambapo miongoni mwa mambo waliyofundishwa ni pamoja na ufugaji wa kisasa, kupika vyakula mbalimbali na utengenezaji wa sabuni za usafi na utengenezaji wa batiki na vikoi.
Biashara
1
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesaini makubaliano ya ushirikiano na Ubalozi wa Norway na kupewa dola za Marekani milioni 2.2 (sawa na Sh bilioni 4.6) kwa ajili ya kutekeleza mkakati wa kipindi cha miaka sita ikiwemo kuujengea umma uwezo juu ya haki za binadamu.Aidha, mkakati huo ni pamoja na kufanya uchechemuzi kwa lengo la kuboresha sheria, kupanua ushiriki wa wananchi, kukuza na kudumisha demokrasia na kuchochea mabadiliko ya Katiba. Makubaliano hayo yalifikiwa jana jijini Dar es Salaam, baina ya Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga na Balozi wa Norway nchini, Elisabeth Jacobsen.Akizungumza, Henga alisema mkakati mwingine ni pamoja na kudumisha haki za kijamii pamoja na haki za kiuchumi na kuhakikisha haki ya kila mwananchi kuishi katika mazingira safi na salama yanazingatiwa na kuchochea maboresho ya sheria na sera zinazosimamia haki za wanawake na watoto na wenye ulemavu.Alisema malengo hayo yanayoanzia mwaka huu hadi 2024 yatawezesha kituo hicho kujipima baada ya muda fulani na pia kuipima jamii na nchi kwa ujumla kuona ni kwa kiwango gani wamepiga hatua katika kulinda, kutetea na kudumisha utawala wa sheria.“Pia kupitia mkakati huu tunaweza kuona namna bora ya kupendekeza ili kutatua changamoto katika jamii hususani katika kujenga uwezo wa kujua haki zinazowahusu,” alisema Henga. Aliongeza kuwa mchango uliotolewa na Norway ni kwa ajili ya Watanzania wote kwani wamejikita katika kumfikia kila mmoja kuweza kuelewa haki zake na kulinda kusimamia haki.Alimshukuru Balozi Elisabeth kwa mchango huo na kuridhishwa na utendaji kazi wao hadi kufanya kuamua kufadhili mpango mkakati huo. Makubaliano hayo yanaongeza nguvu kwa kituo katika utetezi za haki, hasa kwa kuzingatia kwamba changamoto ya ukiukwaji wa haki za binadamu ipo nchini.Aidha alitoa mwito kwa Watanzania na wadau wengine kwa ujumla wenye lengo la kuimarisha ulinzi wa haki za binadamu kuendelea kusimamia haki za binadamu na kuunga mkono juhudi za utetezi wa haki za binadamu kwa lengo la kujenga jamii yenye haki na usawa.Kwa upande wake Balozi, Elisabeth alisema ili kufikia uchumi wa kati nchini, jitihada mbalimbali zinahitajika ikiwemo pia kuimarishwa kwa uelewa juu ya haki za binadamu zikiwemo za wanawake, watoto na hata walemavu. Alisema LHRC ni kituo ambacho kimekuwa kikijikita kutetea haki za binadamu, kikihimiza uwajibikaji nchini katika ngazi mbalimbali na hata pia kutetea utawala wa sheria.
Kitaifa
0
Rais John Magufuli amesema, anataka atakapoondoka madarakani aache mabilionea Watanzania angalau 50 wenye kulipa kodi.Amewahakikishia Watanzania wote kuwa taifa linakwenda katika mwelekeo mzuri, hasa baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuchukua hatua madhubuti ya kuimarisha huduma za uchumi na kijamii, kama vile afya, elimu, maji, nishati na miundombinu ya usafiri.Amesema hayo wakati anazungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Africa Media Group (AMGL), yenye vituo vinne vya televisheni ikiwemo Channel Ten na vituo viwili vya redio ikiwemo Magic FM, ambavyo kwa sasa vinamilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).Wakati anazungumza na wananchi katika mtaa wa Zanaki baada ya ziara hiyo Rais Magufuli alisema pamoja na mafanikiko hayo, serikali itaendelea kupambana na dhuluma na matumizi mabaya ya raslimali za taifa.Alitoa wito kwa watanzania wote, kuiunga mkono serikakli kwa kuhakikisha wanatanguliza maslahi ya taifa.Akiwa ndani ya jengo la AMGL, Rais ambaye ni Mwwenyekiti wa Taifa wa CCM, alijionea mitambo, chumba cha habari na studio za kurushia matangazo za Kituo cha Redio cha Magic FM na Kituo cha Televisheni cha Channel Ten.Pia alizungumza na wafanyakazi ambao walimweleza changamoto mbalimbali, ikiwemo uhaba na uchakavu wa vitendea kazi, maslahi madogo na uchakavu wa jengo la matangazo. Rais Magufuli aliahidi kutoa Sh milioni 200 ndani ya siku mbili kwa ajili ya kununulia vitendea kazi vya kituo hicho.Aliwataka wafanyakazi hao wa AMGL, kumpelekea jina la jengo lolote la CCM lenye hadhi nzuri ili kuhamishia kituo hicho. Aidha, Rais alivitaka vyombo vya habari nchini kufanya kazi kwa maslahi ya taifa na kwa kuzingatia sheria na maadili ya kazi hiyo.Alisema vyombo vya habari nchini, vimekuwa na mchango mkubwa katika kuibua mambo mbalimbali, ambayo yameisaidia serikali katika kuyafuatilia na kuyafanyia kazi.Alisema vyombo vya habari vya Tanzania, ndivyo vinavyotakiwa kuongoza maisha ya Watanzania kwa kupanua uelewa wa wananchi katika mambo mbalimbali, ikiwemo kutoa elimu ya kilimo na ufugaji kwa kuwa asilimia 75 ya watanzania ni wakulima.Alisema hivi sasa nchini kuna vyombo vya habari zaidi ya 170 vilivyosajiliwa, hivyo havina budi kufanya kazi zao kwa maslahi mapana ya Taifa, kwa kuwa vyombo vya nje mara nyingi hutoa taarifa hasi kuhusu Afrika ikiwemo matukio ya vita.Baada ya kutoka AMGL, Rais Magufuli alikagua Mradi wa Ukarabati mkubwa wa Jengo la Kitega uchumi la CCM (SUKITA), lililopo mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, ambalo litakamilika mwezi Juni mwaka huu.Rais alimalizia ziara yake kwa kutembelea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, iliyopo mtaa huo wa Lumumba na kuzungumza na wafanyakazi.
Kitaifa
0
Alisema hayo jijini Arusha wakati wa kikao chake na Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara ambazo zimeamua kufanya kazi kwa pamoja ili kudhibiti utoroshaji wa madini ya tanzanite na kufuatilia kwa karibu shughuli za uchimbaji na biashara ya madini hayo ili yanufaishe taifa.Alisema tanzanite hiyo ghafi yenye uzito wa gramu 2,015.59, ilikuwa ikitoroshwa na raia wa India, Jain Anurag aliyekuwa akitaka kwenda mji wa Jaipur kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Qatar wiki iliyopita.Alisema madini yaliyokamatwa yameshataifishwa kama ambavyo sheria na kanuni za madini zinavyoelekeza na kwamba ukamataji dhidi ya watorosha madini hufanywa na Wizara ya Nishati na Madini kupitia Wakala wake wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) kwa kushirikiana na taasisi nyingine kama Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Idara ya Uhamiaji.Aidha, amesema Serikali itafuta leseni za wafanyabiashara wa madini watakaobainika kutorosha rasilimali hiyo nje ya nchi ikiwemo kuwakamata wachimbaji na wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi stahiki kwa serikali.Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla ametoa saa 24 kwa raia wa kigeni wote wanaojihusisha na biashara ya madini ya tanzanite na madini mengine kinyume cha sheria, kuondoka nchini mara moja na watakaokaidi agizo hilo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Biashara
1
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe ameagiza kuitishwa kwa Baraza la Dharura la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga ili kujadili taarifa ya tume iliyoundwa na Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) iliyochunguza tuhuma za ubadhirifu na upotevu wa kiasi cha Sh bilioni 2.9.Fedha hizo ni za miradi mbalimbali ya maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga na zinazodaiwa kutumika kinyume cha utaratibu na nyingine kutoingizwa benki. Jana, Tamisemi kupitia Waziri wake, Selemani Jafo alitangaza kuchukuliwa hatua kwa wahusika wote wa kadhia hiyo. Dk Kebwe alitoa agizo hilo kwa Katibu Tawala wa Mkoa, Clifford Tandari mbele ya waandishi wa habari juzi.Aliagiza timu kutoka Sekretarieti ya Mkoa kuondoka mara moja na kwenda Ulanga kwa ajili ya kushughulikia jambo hilo na kuagiza pia kikao cha Dharura cha Baraza la Madiwani kinapaswa kuketi Januari 7, mwakani. Pia aliagiza aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga, Rajab Siriwa ambaye katika kupisha uchunguzi wa tume hiyo alihamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, arudishwe mara moja Ulanga kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo na baraza hilo limsimamishe kazi kuanzia Januari hiyo.
Kitaifa
0
RAIS wa Rwanda, Paul Kagame amewataka wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuendeleza ushirikiano ili kujiletea maendeleo alipokuwa akikabidhiwa kiti cha jumuiya hiyo katika mkutano wa 20 wa wakuu nchi hizo jijini hapa jana.Rais Kagame alikabidhiwa uenyekiti na Rais Yoweri Museveni wa Uganda. Kabla ya Rais Museveni kutangaza kumkabidhi kijiti mwenyekiti huyo mpya, wakuu wa nchi wa jumuiya hiyo walishiriki kikao cha awali kilichochukua saa kadhaa na baadaye waliingia tena kwenye kikao cha kukabidhiana madaraka. Baada ya Rwanda kukabidhiwa uenyekiti, Rais Kagame aliendelea kuendesha kikao hicho huku akimtaka mwenyekiti wa zamani, Rais Museveni.Akihutubia Rais Museveni alisema kuwa sekta ya ujasiriamali inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo utozaji wa riba kubwa katika bidhaa zao, ukosefu wa nguvu kazi za kutosha, gharama kubwa za usafiri na kusisitiza kuwa EAC imejitahidi kupunguza gharama za usafiri kwa kujenga reli ili kurahisha usafiri. Pia aliishauri Jumuiya hiyo kupunguza gharama kubwa za umeme ili wananchi waweze kunufaika na nishati hiyo.Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Liberata Mfumukeko alisema EAC imekuwa kwa kiasi kikubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya afya, miundombinu na kusisitiza kuwa Jumuiya hiyo itaendelea kuhakikisha kila mwananchi ananufaika nayo. Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyabiashara wa EAC, Nicolas Nesbert alisema mipaka ya Jumuiya hiyo isiwe na vikwazo vya biashara ili kukuza sekta binafsi kwa ajili ya kukuza uchumi katika kila nchi mwanachama kwani wapo hapo kwa ajili ya kuzalisha ajira. Alisisitiza kuwa wafanyabiashara wanataka kufanya biashara zenye tija hivyo ni vyema kuondoa urasimu ili kuwezesha wafanyabiashara kufanya biashara zao sambamba na kutengeneza ajira.Naye Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya, Alhaji Kirunde Kivejinja alisema Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo limetekeleza maagizo yote ya wakuu wa nchi ikiwemo kuongeza nafasi ya Naibu Katibu Mkuu. Pia katika kikao hicho Jaji Sauda Mjasiri kutoka nchini Tanzania alikula kiapo mbele ya wakuu hao wa nchi kuwa Jaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) na anakuwa Jaji wa pili mwanamke kwenye mahakama hiyo. Viongozi hao pia walitoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mashindano ya insha ya Jumuiya hiyo katika shule za msingi na sekondari.Michael Msafiri kutoka Tanzania anayesoma Kibaha Sekondari aliibuka mshindi wa kwanza akifuatiwa na Rwanda, Burundi, Kenya na Uganda kwa mwaka 2017. Wakati washindi wa mwaka 2018; wa kwanza ni Innocent Shirima kutoka nchini Tanzania kutoka shule ya sekondari Moshi alikabidhiwa cheti na fedha huku washindi wengine wakitoka nchini Rwanda, Uganda, Burundi na Kenya. Baada ya makabidhiano ya zawadi hizo kuisha, Rais Kagame alimshukuru Rais John Magufuli kwa kuandaa mkutano huo nchini Tanzania na kumshukuru Mwenyekiti wa awali Rais Yoweri Museveni kwa kuendesha vikao hivyo kama mwenyekiti kwa kipindi cha miaka miwili.
Kitaifa
0
KIKAO kilichokuwa kikisubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa riadha kati ya uongozi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) na Serikali kinatarajia kufanyika kesho jijini Dar es Salaam.Kikao hicho kinatokana na agizo la Mkurugenzi wa Michezo, Dk Yussuf Singo, kuliagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kukiandaa ili kujadili matatizo mbalimbali yaliyobuka hivi karibuni ndani ya shirikisho hilo la riadha nchini.Hivi karibuni Singo alikiri kuwapo na matatizo ndani ya RT ambayo yanasababisha viongozi wa juu kulumbana mara kwa mara ndani ya vyombo vya habari. Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Neema Msitha, jana alisema kikao hicho na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, kitafanyika jijini Dar es Salaam kesho Ijumaa, Novemba Mosi.“Hicho kikao kitafanyika Novemba Mosi, lakini mahali nitakujulisha mara itakapojulikana,” alisema Neema kwa ufupi wakati akijibu swali la mwandishi wa habari hizi aliyetaka kujua siku ya kikao hicho.Rais wa RT, Anthony Mtaka, alisema hivi karibuni kuwa, hakuna mgogoro RT, lakini katibu wake, Wilhelm Gidabuday, alisisitiza kuwa upo na anataka wote wapatiwe nafasi sawa bila kujali wadhifa wa mtu ili kila mmoja atoe dukuduku lake.
michezo
2
TIMU ya taifa ya soka ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars na ile ya Zanzibar, Zanzibar Heroes zinatarajiwa kushuka dimbani leo kwenye mechi mbili tofauti kusaka ushindi katika mchezo wa mwisho wa makundi ya michuano ya Kombe la Chalenji Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.Kilimanjaro Stars itachuana na Sudan huku Zanzibar Heroes ikitarajiwa kucheza na Kenya katika michezo itakayochezwa kwenye Uwanja wa KCCA, Kampala Uganda.Ukiachilia mbali Kenya iliyokwisha kufuzu kwa pointi sita, Tanzania yenye pointi tatu, Zanzibar na Sudan zenye pointi moja, kila mmoja anaweza kuungana naye endapo zitashinda mechi zao za hatua ya makundi.Kocha wa Kilimanjaro Stars, Juma Mgunda, alisema wataingia kwa tahadhari na umakini mkubwa kwani wanajua hautakuwa mchezo rahisi kwa sababu wanahitaji ushindi na Sudan itakuwa inahitaji kushinda ili ifikishe pointi nne.“Vijana wako salama na wapo tayari kwa mchezo wa kesho (leo) na tunajua utakuwa mgumu kwa sababu utatoa maamuzi ya nani atasonga mbele kikubwa ni kuwa makini tusirudie makosa,”alisema Mgunda.Alisema amewapa wachezaji mbinu nzuri zitakazowapa matokeo na kurekebisha makosa yaliyoonekana katika michezo iliyopita.“Umakini unahitajika kuhakikisha hawarudii makosa, waendelee kutuombea ili tupate matokeo mazuri,”alisema.Naye kocha wa Zanzibar Heroes, Hemed Morocco alisema wapo tayari kwa mchezo na wanaamini watashinda na kufuzu nusu fainali. Katika michezo ya Kundi A iliyochezwa jana, Somalia iliifunga Burundi na kuondoka kwenye mashindano bila ushindi na Eritrea ikaifunga Djibouti kwa bao 1-0.
michezo
2
WATUMIAJI wa Usafi ri wa Mabasi wanatarajiwa kuanza kutumia rasmi mfumo wa ukataji wa tiketi kwa njia ya kielektroniki kuanzia Septemba Mosi mwaka huu baada ya Serikali kuazimia kuanzisha utaratibu unaotajwa kuwa na faida mbalimbali ikiwemo kuondoa usumbufu wanaoupata abiria.Hatua hiyo ilibainishwa katika mkutano wa wadau mbalimbali wa usafiri ulioitishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRAC) jana ambayo hapo awali ilijulikana kama (Sumatra), uliolenga kupata maoni mbalimbali ya wadau hayo kuhusiana na mfumo huo miezi michache kabla ya kuanza kutumika.Awali akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa (LATRAC), Gilliard Ngewe alisema kuanzishwa kwa mfumo huo pamoja na mambo mengine kumelenga kutatua changamoto mbalimbali zinazowakumba watoaji wa huduma pamoja na wananchi kwa kutoa majibu yanayostahili. Alisema mfumo huo huo maarufu kama E-Ticketing utakaotolewa na Ofisi ya ‘National Internet DATA Centre’ (NIDC) iliyopo chini ya Wizara ya Mawasiliano, umeanzishwa maalumu kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya huduma za usafiri ikiwa ni lengo la Serikali kuondoa hali hiyo iliyodumu kwa kipindi kirefu.Alisema kwa kipindi kirefu iliyokuwa Sumatra ilikuwa ikipambana katika kuhakikisha mifumo mbalimbali ya usafiri ukiwemo wa ufuatiliaji wa magari (VTS) unafanya kazi na kwamba ujio wa mfumo huo wa ukataji tiketi kwa njia ya kielektroniki unakuja kumaliza tatizo hilo. “Bila shaka mtakubaliana nami kuwa tangu kuanzishwa (VTS) ajali nyingi zimeweza kupungua hivyo kuletwa kwa mfumo wa ukataji wa tiketi kwa mfumo huo mpya kumelenga kuboresha huduma za usafiri,” alisema Ngewe.Aidha alisema faida ya mfumo huo ni pamoja na kumwezesha mmiliki wa basi kupata faida kutokana na mfumo huo kuwa na uwezo wa kuunganisha huduma za ukataji tiketi kutoka kwa abiria kwenda kwa mteja huku ukimuondolea usumbufu abiria kutoka eneo moja hadi kituoni kukata tiketi.Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Utafiti na Ujenzi kutoka Ofisi ya National Internet Data Centre, Khalifa Ali alisema kuletwa kwa mfumo huo pia kutaiwezesha Serikali kupata mapato yake kwa urahisi na kuondoa suala la ukadiliaji lililokuwa likifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) dhidi ya wenye mabasi.Aidha alisema mfumo huo unatarajiwa kuanza kufanya kazi kwa majaribio ifikapo Julai kwa kuyahusisha mabasi 18 yanayofanya kazi katika mikoa ya Dodoma na Dar es Salaam ili kujiridhisha na uwezo wake kabla ya kuanza kufanya kazi rasmi ifikapo Septemba Mosi mwaka huu.
Kitaifa
0
BAADHI ya wananchi wa kijiji cha Mtumba, kata ya Mtumba mkoani hapa, wameiomba serikali kuweka alama za barabarani ili kuepusha ajali za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikijitokeza na kukatisha maisha ya watu kutokana na mwendo kasi.Katika barabara ya Dodoma, Morogoro kumekuwa na ongezeko la magari kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa mji wa serikali unaoendelea kijijini hapo. Hatua hii imekuja kutokana na kugongwa hadi kufa mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi Mtumba anayejulikana kwa jina la Elia Meleto (37) wakati akijaribu kukatisha barabarani kuelekea katika kituo chake cha kazi.Kwa mujibu wa wananchi hao wamesema, magari mengi yanayotumika katika kubeba madini ya ujenzi katika kijiji hicho hayaangalii usalama wa wananchi na badala yake madereva wamekua wakilaumiwa kutumia ubabe wa matumizi ya barabara. Aidha, kutokana na ajali hiyo wananchi wameiomba serikali kuweka vibao vinavyoonesha mwendo unaohitajika kutokana na eneo hilo kuwa na makazi ya watu ikiwa ni pamoja na kuweka alama za barabarani (Zebra)hali itayosaidia kupunguza ajali. Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo, Mbaruku Masenha alisema alimuona mwalimu huyo akikatiza barabara ghafla gari lenye mwendo kasi likakatiza na kumgonga hali iliyosababisha umauti wake.“Nilikuwa nimesimama kando ya barabara na nilimwona mwalimu Eliya akiwa anakatiza barabara lakini ghafla gari lililokuwa limebeba madini ya ujenzi likakatiza huku likiwa na mwendo kasi na kumgonga, Hata hivyo, hakuweza hata kutapatapa maana alipoteza uhai wake palepale ,ni tukio linalonipagawisha maana kuna wakati najihisi kama ni ndoto hasa ukizingatia nilitoka kuongea nae muda huo huo,”alisema Mbaruku.Kwa upande wa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mtumba ambako marehemu alikuwa anafanyia kazi, Busuna Matoja alisema mwalimu huyo alikutwa na adha hiyo mapema alfajiri jana. Alisema mwalimu huyo alikuwa na kawaida ya kuamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kufanya mazoezi kisha kujiandaa kwenda shule kuwajibika lakini kwa bahati mbaya hali hiyo imekatisha ndoto zake . “Mwalimu alikuwa na kawaidia ya kuamka asubuhi anafanya mazoezi kabla ya kuelekea shuleni kuwajibika kufundisha,kwa kweli ameacha pengo ambalo sio rahisi kuzibika,”alisema Matoja.
Kitaifa
0
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally, amewataka Watanzania kutumia uwezo wa kuhifadhi vitabu vitakatifu kuongeza ubunifu katika nyanja ya sayansi na teknolojia na nyingine ili kuendeleza jamii kwa kuipatia maendeleo stahiki.Dk Bashiru alitoa mwito huo katika kata ya Pahi wilayani Kondoa mkoani Dodoma, wakati wa mashindano ya kuhifadhi Kurani yaliyowashirikisha wadau kutoka maeneo mbalimbali nchini.Alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa katika kuwekeza kwenye elimu kwa watoto, kwa kuwa watoto wakisoma si tu wanajengewa maarifa lakini pia wanaunganishwa na hivyo kuwa chachu ya kuweza kuisaidia jamii inayowazunguka.Mratibu na Mwandaaji wa mashindano hayo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Dk Ashatu Kijaji, alisema kuwa lengo la mashindano hayo ya kuibua vipaji vya watoto vya kusoma Kitabu Kitukufu cha Kurani ni kuwajengea uwezo wa kuwa na ujasiri katika kueleza wanayoyaamini yakiwemo mambo mazuri ambayo yanafanywa na serikali.Kwa upande wake, Naibu Spika Dk Tulia Ackson alisema kuwa kazi zinazofanywa na Dk Kijaji, ni za kupigiwa mfano hasa kwa wanawake na akawataka wazazi katika Wilaya ya Kondoa kumuunga mkono kwa kushiriki kikamilifu katika mikakati ya kuinua elimu katika eneo hilo.Aidha, aliwataka kuhakikisha wanawapeleka watoto katika makambi yaliyo na lengo la kuongeza ufaulu wa wanafunzi.Mgeni asmi katika mashindano hayo, Shehe wa Mkoa wa Dodoma, Mustapher Shabaan, aliwapongeza vijana walioshiriki mashindano hayo na kuonesha umahiri mkubwa wa kuhifadhi Kurani na kuwataka waumini wa Kiislamu kusoma na kukielewa kitabu hicho kitukufu.Alifafanua kuwa kitabu hicho kimejaa elimu na maarifa mengi yatakayowasaidia kuenenda vyema katika jamii na kupata thawabu kutoka kwa Mungu.
Kitaifa
0
Bella ambaye anatamba na wimbo wa ‘Lamba Lamba’ alisema jana hadi sasa ana wimbo ambao ameandikiwa na Nikki wa Pili, hivyo muda wowote atasikika akirapu.“Walijua Bella naimba muziki wa bolingo tu, hapana! Nina wimbo nimeandikiwa na Nikki wa Pili ambao nitachana mistari kwani napenda kufanya vitu ambavyo sijawahi kufanya, watu hawajui kama Bella anaweza kurapu,” amesema.“Napenda sana hip hop hata kama naimba, napenda sana kusikiliza watu wanaochana si Weusi tu nawasikiliza wasanii tofauti tofauti wanaorapu,” ameongeza.Bella amewahi kushirikishwa na wasanii wanaofanya vizuri katika muziki wa hip hop ambao ni Weusi na Fid Q, Joh Makini na Khaligraph Jones kutoka Kenya.
michezo
2
USHINDI wa Simba na JS Saoura ya Algeria juzi umezidi kuliweka Kundi D la Ligi ya Mabingwa wa Afrika katika uwazi zaidi na kuifanya kila inayoshiriki katika kundi hilo kuwa na nafasi ya kuweza kufuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo.Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya mabingwa wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika Al Alhly na kuwafanya mabingwa hao wa Tanzania kufikisha jumla ya pointi sita na kuwatoa AS Vita Club ya Congo katika nafasi ya pili baada ya timu hiyo kufungwa 1-0 na JS Saoura ya Algeria.JS Saoura ambayo ilifungwa na Simba kwa mabao 3-0 katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika Kundi D, kwa ushindi wake huo wa juzi, sasa imefikisha pointi tano na kukalia nafasi ya tatu huku AS Vita ikiburuza mkia ikiwa na pointi nne.AS Vita Club ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo iliifungwa katika mchezo wake wa kwanza na Al Alhly kwa mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa Alexandria kabla ya timu hiyo kutoka sare na JS Saoura ya Algeria.Kutokana na msimamo wa kundi hilo, timu yoyote hata AS Vita Club ambayo iko mkiani mwa msimamo wa ligi hiyo, inaweza kupenya na kutinga robo fainali kwani timu mbili za kwanza ndizo zitacheza hatua hiyo inayofuata.Kwa upande wa Simba, wenyewe mchezo unaofuata watakwenda Algeria kuifuata JS Saoura kabla ya kucheza mchezo wa mwisho dhidi ya AS Vita Club utakaofanyika jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa katika mchezo wa kufunga pazia.Al Alhly wenyewe watacheza dhidi ya AS Vita Club katika mchezo wao wa mwisho na timu itakayocheza vizuri mechi hizo zilizobaki, inaweza kucheza hatua ya robo fainali kwani kila moja ina uwezo wa kufikisha pointi nyingi zaidi ya mwingine itategemea atakavyocheza.MCHEZO WA SIMBAKatika mchezo huo wa Simba, bao pekee katika mchezo huo lilifungwa kwa shuti la mguu wa kulia na mchezaji wa kimataifa wa Rwanda, Meddie Kagere katika kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza timu hiyo kushindwa kutumia nafasi kibao ilizopata.Kocha wa Al Ahly, Martin Lasarte alimuingiza Nasser Maher ili kuimarisha safu yake ya ushambuliaji, dakika 20 kabla ya mchezo haujamalizika, lakini hilo halikuisaidia timu yake kuepukana na kipigo hicho, ambacho kilionekana kuwachanganya sana.Ushindi huo wa Simba ni sawa na kulipa kisasi baada ya timu hiyo yenye maskani yake Msimbazi kupokea kichapo cha `mbwa mwizi’ baada ya kufungwa mabao 5-0 na Al Alhly katika mchezo uliofanyika Misri siku kadhaa zilizopita.MECHI ZINGINETimu ya Horoya ilipanda hadi nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi B wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya FC Platinum katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Stade du 28 Septembre huko Conakry juzi.Ocansey Mandela na Yakubu Hudu ndio waliozifumania nyavu kwa vigogo hao wa Guinea ambao wamepaa pointi mbili zaidi ya timu iliyopo katika nafasi ya pili ya Orlando Pirates na pointi moja nyuma ya mabingwa watetezi Esperance de Tunis.Nayo Wydad Casablanca walijikuta wakilazimishwa suluhu dhidi ya Lobi Stars katika mchezo mwingine wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika Kundi A katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah nchini Morocco.Sare hiyo imeshuhudia vigogo wa Morocco, Wydad na wale wa Nigeria Lobi wakibaki katika nafasi ya pili na nne katika msimamo wa Kundi A.Club Africain na TP Mazembe wenyewe walitoka suluhu katika mchezo mwingine wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika wa Kundi C kwenye Uwanja wa Stade Olympique de Rades huko Tunisia.Sare hiyo imezifanya timu hiyo ya Tunisia ya Africain na vigogo vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mazembe zimebaki katika nafasi ya tatu na pili katika msimamo wa Kundi C.
michezo
2
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kuibuka maneno ya upendeleo kwa mtu aliyeshinda zabuni hiyo, ambaye hajatangazwa rasmi.Aidha, Jiji hilo limesema halijaingia mkataba wowote na Kampuni ya Max Malipo kama inavyodaiwa, bali halmashauri hiyo ilifanya mazungumzo ya awali ili kujua kama wakitumia huduma hiyo wanaweza kunufaika vipi na ukusanyaji wa mapato.Lakini, hivi sasa wananchi wanalipia kodi kwa kutumia mfumo wa utoaji wa risiti za kieletroniki, badala ya ule wa kuandika risiti kwa njia ya mkono.Hayo yalisemwa jana jijini hapa na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, ambaye ni Mwekahazina wa Jiji, Kessy Mpakata wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mikakati waliyoiweka kwa jiji la Arusha kwa ajili ya kupanga mji kwa kipindi cha miaka 100 ijayo.Alisema hawezi kuingilia mambo ya zabuni na kuamua nani apewe ruhusa ya kukusanya mapato, lakini amelazimika kusema hayo mara baada ya kutokea maneno mengi mitaani, yanayodai kuwa ametoa ruhusa ya kumpata mtu fulani zabuni wakati ni kinyume cha taratibu na sheria.Alisema Kamati ya Bodi ya Zabuni na Kamati ya Fedha, zimeshindwa kuafikiana, ndio maana suala hilo limepelekwa PPRA ili waweze kutangaza nani anastahili kupewa dhamana ya kukusanya mapato ndani ya jiji hilo.“Hakuna upendeleo kwenye zabuni badala yake kamati hizo zimeshindwa kuafikiana juu ya nani apewe zabuni ndio maana tumepeleka suala hilo PPRA ili watoe maamuzi lakini pia jiji halijaingia mkataba na Max Malipo bali linatafuta njia ya kudhibiti wizi wa mapato kwa kuanza kutoa risiti za mfumo wa kieletroniki badala ya njia ya kuandika kwa mkono ambapo awali kulikuwa na wizi mkubwa wa mapato ya Jiji hilo,” alisema.Kuhusu mfumo wa ulipaji kodi kwa njia za kielektroniki, alisema jiji hilo litaendelea kutoa risiti za kielektroniki mara baada ya mtu kulipa kodi za nyumba na badala ya kuandikiwa kwa mkono, kwani wamegundua kuwa jiji lilikuwa likiibiwa fedha nyingi na baadhi ya watumishi, kutokana na tabia ya kuandika mapato kwa mfano mwananchi analipa Sh 100,000 matokeo yake risiti anayopewa inaonesha kalipa kiasi hicho cha fedha, lakini kwenye nakala inayobaki kwenye (carbon paper ) inaonesha kuwa amelipa Sh 10,000.Mpakata aliongeza kuwa wahusika walioshinda zabuni mwaka jana wataendelea kukusanya mapato ndani ya jiji hilo hadi Desemba 31 na wale waliopaki vibaya, nao wamepewa muda hadi Desemba 31 na baada ya hapo PPRA itatoa jina la mzabuni aliyeshinda na kuondoa maaneno yaliyozuka hivi karibuni.
Biashara
1
TANZANIA leo imeandika historia kwa kuanza kutekeleza katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki, kama Sheria ya mwaka 2019 ya Usimamizi wa Mazingira Sura ya 191 pamoja na Kanuni za Usimamizi wa Mazingira za Kupiga marufuku inavyoeleza.Kuanza kutekelezwa kwake ni kwamba adhabu zinazohusu sheria hiyo zinaanza kutumika rasmi leo hivyo watakaokutwa wamebeba mifuko huyo kwa ajili ya matumizi au kusambaza, watakutana na mkono wa sheria. Sambamba na hilo, Shirika la Viwango Tanzania(TBS), limetoa onyo kwa wasambazaji na watengenezaji wa mifuko mbadala kwamba ni lazima wakaguliwe bidhaa wazalishazo au kusambaza kabla ya kuingia sokoni, ili kama mifuko hiyo mbadala itakidhi vigezo, ipewe leseni na idhini ya matumizi. Akizungumza na vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa TBS, Lazaro Msasalaga alisema kuanza rasmi kwa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki, kunawafanya sasa nao sheria yao ya kuwataka wazalishaji au wasambazaji mifuko mbadala kuidhinishwa na taasisi hiyo kuanza kufanyakazi.“Na sisi tunawatangazia wazalishaji na wasambazaji wa mifuko mbadala wawe ni wa ndani au wa nje ni lazima wapate leseni kutoka TBS za kuhakiki ubora wa mifuko hiyo na kuhakikisha malighafi iliyotengeneza haina hata chembe ya plastiki,wakikaidi adhabu ipo ya faini isiyozidi Milioni 50, kifungo cha miaka hadi miwili au vyote kwa pamoja,’alisisitiza Msasalaga. Alisema serikali imeanza kutekeleza rasmi leo katazo la mifuko hiyo ya plastiki na kutoa maelekezo ya mifuko inayoruhusiwa na kwamba katika kutekeleza agizo hilo taasisi mbalimbali zilipewa kazi za kufanya na wao walipewa majukumu matatu.Alisema jukumu la kwanza lilikuwa kusitisha uhuwishaji wa leseni za mifuko ya plastiki na vifungashio sambamba na kusitisha kutoa cheti cha ubora,kwa kampuni au taasisi zilizokuwa na vibali rasmi vya kufanya hivyo. Jukumu la pili lilikuwa ni kutopokea tena maombi mapya ya leseni za vifungashio hivyo vya plastiki na jukumu la tatu walilopewa TBS ni kuondoa kwenye matumizi kiwango cha ubora cha vifungashio vya mifuko ya plastiki. Msasalaga alisema baada ya kutekeleza majukumu hayo waliandaa viwango viwili vipya vya mifuko mbadala ambavyo ni kiwango namba TZS 2292 cha mwaka 2018 na kiwango namba TZS 2130,mwaka 2018. Viwango hivyo vinahusu mifuko mbadala ambayo ni pamoja na mifuko iliyotengenezwa kwa karatasi,vikapu na mengine kama hiyo ambayo baada ya matumizi yake huoza.“Hivi ndivyo viwango tunavyovitambua sasa na hakuna mzalishaji au msambazaji aliyefika kwetu kuomba leseni,awali kwenye mifuko ya plastiki tulitoa leseni kwa wasambazaji au wazalishaji zaidi ya 31, na wote sasa tumesitisha leseni zao kwa kuwa mifuko hiyo imepigwa marufuku,”alisema Msasalaga. Awali Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, ilitoa tangazo na maelekezo ya matumizi ya mifuko mbadala inayoruhusiwa na kutoa miongozo ya nini cha kufanya katika kutekeleza upigaji marufuku mifuko ya plastiki kwa kuwataka wananchi kuikusanya na kuipeleka kwenye maeneo yaliyobainishwa. Kadhalika, kuanzia leo katazo hilo limeanza kufanya kazi na kwamba wananchi watakaokutwa na mifuko hiyo adhabu yake ni faini ya Sh 30,000 hadi 200,000 au kifungo cha siku saba au vyote kwa pamoja. Aidha wauzaji wadogo watakaokutwa kuanzia leo wakiuza mifuko hiyo ya plastiki adhabu yao ni faini ya Sh 100,000 hadi 500,000 au vyote kwa pamoja na faini nyingine zimeainishwa kama zilivyotajwa awali. Kwa upande wao Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imesema tayari walishatoa taarifa inayokwenda kwenye vituo vyote vya Kimataifa, kuhusu mwisho wa matumizi ya mifuko ya plastiki na kuanza rasmi katazo hilo leo. Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha alisema tayari kupitia TAA taarifa za katazo hilo zimeshatolewa. “Hii taarifa inajulikana kitaalam kama ‘timatic pre-information’ ambayo inatumwa kwenye centre (vituo) zote duniani, ambapo kuna shirika la ndege ambalo linaleta abiria Tanzania itakuwa rahisi wao kupata taarifa ya katazo hilo na kuwafanya wasibebe mifuko hiyo,” alisema Rwegasha. Aliwataka wadau wote wanaofanya shughuli mbalimbali kwenye viwanja vya ndege kutoa ushirikiano mkubwa kuwaeleza abiria juu ya katazo hilo, na kuwaelekeza watumie mifuko mbadala, ambayo itakuwa ikipatikana kwenye maduka yaliyopo kwenye majengo ya Kwanza na Pili ya JNIA. Kwa upande wake, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limewaondolea hofu wadau wanaoendesha huduma mbalimbali kwenye Viwanja vya ndege, kuwa ipo mifuko, ambayo itaendelea kutumika kwa mujibu wa Kanuni namba tisa (9) ya sheria ya kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki ya mwaka 2019. Alisema mifuko hiyo baada ya kutumika inatakiwa ihifadhiwe sehemu maalumu na kupekekwa mahali itakapoteketezwa.Mwanasheria wa NEMC, Manchare Heche alisema kwa upande wa viwanja vya ndege ipo mifuko, ambayo itaendelea kutumika kwa mujibu wa Kanuni. Alisema kwa upande wa plastiki zinazofungia mizigo ya abiria wanaosafiri kutoka ndani na nje ya nchi kwa usafiri wa ndege itatakiwa kuondolewa abiria anapofika nchini, na zitakusanywa na kuhifadhiwa maeneo maalumu kabla ya kupelekwa eneo lililotengwa kwa ajili ya kuziteketeza. Heche alitoa angalizo kwa wale wote wanaohusika na ukamataji wa watumiaji wa mifuko hiyo, kutotumia nguvu ili kuepusha mikwaruzano na kutoelewana. Kadhalika aliwataka wadau hao kuhakikisha wanadai vitambulisho kwa wale wote watakaofika kwenye maeneo yao ya kazi kudai wanakagua endapo wanaendelea kuuza au kutumia mifuko ya plastiki.Aidha jana wakati ikiwa ni siku ya mwisho wa matumizi ya mifuko ya plastiki nchini, wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam walionekana wakifanya usafi kwa hiari katika maeneo yao kwa lengo la kuiondoa mitaani mifuko iliyozagaa ovyo. Aidha, tayari mifuko mbadala imeonekana kwa wauzaji wa bidhaa mbalimbali,huku ikiuzwa kwa viwango tofauti. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam jana, wakazi hao hususani wafanyabiashara wameonekana wakisafisha maeneo yao huku wasiokuwepo wakiitwa kwa ajili ya kuhakikisha mifuko ya plastiki haionekani. Akizungumza na gazeti hili, jana katika eneo la Mabibo, mfanyabiashara wa genge, Azura Mzava alisema ni kweli lazima kufanya usafi ili kuiondoa Mifuko ile iliyozagaa haswa ikizingatia kuwa ni siku ya mwisho kuonekana mitaani. “Mimi hapa kwenye genge langu wapo wafanyabiashara wengine hivyo imetulazimu kuitana kwa pamoja ili kuweza kuiondoa mifuko inayozagaa katika maeneo yetu jambo litakalotusaidia kuepuka kufikia katika vyombo vingine vya kisheria,” alisema Mzava na kuongeza kuwa ni vyema pia kupeana elimu wenyewe kwa wenyewe ili agizo hilo liweze kutekelezeka. Kwa upande wake, mfanyabiashara wa viungo kituo cha daladala, Ubungo, Sam Tarimo alisema yeye inamlazimu kuhakikisha Mifuko hiyo haionekaniki katika eneo lake ingawaje ipo hofu ya wananchi wasiokuwa na hekima ambao wanaikusanya na kwenda kutupa katika maeneo ya watu. Kuhusu mifuko mbadala, alisema wapo wajasiriamali wadogo ambao wameamua kuzunguka katika maeneo mbalimbali ya wafanyabiashara na kuuza mifuko hiyo kwa viwango tofauti. “Ipo Mifuko milaini inayouzwa shilingi 200, ipo ya shilingi 500 na hata mingine ya shilingi 1000 inategemea na hitaji la mteja kulingana na bidhaa alizonunua,” alisema Sam nakuongeza kuwa kwa mifuko ya kaki pia ipo inayouzwa na isiyouzwa. Habari hii imeandaliwa na Ikunda Erick na Lucy Lyatuu,Dar es Salaam.
Kitaifa
0
['Mkenya Eliud Kipchoge ameweka jina lake katika vitabu vya historia , akimaliza kilomita 42 za mbio za marathon kwa saa moja dakika 59 na sekunde 40 katika shindano la Ineos siku ya Jumamosi nchini Austria Vienna. ', 'Hatahivyo muda huo bora uliowekwa na bingwa huyo hautatambulika kama rekodi ya dunia.', 'Kulingana Shirika la Riadha duniani IAAF , kwa mbio yoyote kufikia sheria zake na hivyobasi kutambulika kama rekodi ya dunia kuna masharti yanayopaswa kufuatwa kulingana na chombo cha habari cha AFP.', 'Wakati wa jaribio la kwanza la mbio hizo za marathoni huko Monza nchini Itali miaka miwili iliopita, Kipchoge alipatiwa vinywaji huku wadhibiti mbio hizo wakibadilishwa mara kwa mara, hatua iliokiuka masharti ya IAAF. ', 'Siku ya Jumamosi , alipewa vinywaji kila baada ya kilomita 5 na hivyobasi kukiuka sheria hizo za shirikisho la riadha duniani. ', 'Mkimbiaji huyo mwenye umri wa miaka 34 tayari anashikilia rekodi ya dunia miongoni mwa wanaume katika umbali huo akiwa na muda wa saa mbili dakika moja na sekunde 39, ambao aliweka katika mbio za Berlin tarehe 16 mwezi Septemba 2018. ', 'Kulingana na AFP , barabara hiyo ilikuwa imeandaliwa hali ya kwamba ingemchukua Kipchoge sekunde 4.5 zaidi kulingana na uchanganuzi wa wataalam wa michezo katika chuo kikuu cha Vienna. ', 'Kwa jumla aliweza kushuka mita 26 na kupanda mita 12 , walisema wataalam hao. ', 'Mbio hizo za marathon zimekuwa na ushindani mkali katika kipindi cha miaka 16 iliopita kati ya wanariadha wa Kenya na wenzao wa Ethiopia. ', 'Mataifa hayo mawili ni washindani wakuu wa mbio ndefu uwanjani. ', 'Rekodi ya Kipchoge ilikaribia kuvunjwa na raia Muethiopia Kenenisa Bekele ambaye alikimbia saa 2 dakika moja na sekunde 41 ikiwa ni sekunde mbili pekee kabla ya kuivunja rekodi hiyo. ', 'Mbio hizo za Viena hazikuwa mashindano bali zililenga kuwapa motisha mamilioni ya watu duniani. Na Kipchoge amefanikiwa. ', 'Katika mahaojiano na vyombo vya habari , Kipchoge alisema kwamba mbio hizo za Vienna zililenga kuwapatia changamoto wanadamu katika maisha yao ya kila siku. ', 'Pia aliwashutumu wakosoaji wake. ', "Ninakimbia kuweka historia , ili kuuza #NoHumanLimited na kuwapa motosha zaidi ya watu bilioni 3 . Sio swala la fedha bali kubadilisha maisha ya watu'', alinukuliwa akisema."]
michezo
2
MCHEZAJI wa Azam FC, Salum Abubakari ‘Sureboy’ amesema pamoja na ligi ya safari hii kutawaliwa na upinzani mkali kwa kila timu wanayocheza nayo wamejipanga kuendeleza makali yao ya kufanya vizuri michezo inayokuja ili kutimiza lengo la kutwaa ubingwa msimu huu.Kauli hiyo ameitoa juzi baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi mkubwa wa mabao 4-0 dhidi ya Mbao FC ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara uliopigwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Chamazi Complex.Akizungumza baada ya kukamilika kwa mchezo huo juzi, Sure boy alisema anamshukuru Mungu kwa kumaliza salama na kuendeleza rekodi yao ya kufanya vizuri katika uwanja wa nyumbani.“Ligi ya safari hii ni ndefu, pamoja na kukabiliwa na upinzani mkubwa kwa kila timu tunayocheza nayo, lakini tumejipanga kuhakikisha tunaendeleza rekodi ya kufanya vizuri kila mchezo unakuja ili kuhakikisha tunatimiza malengo ya klabu ya kutwaa ubingwa msimu huu,” alisema.Nnahodha wa Mbao, David Mwassa amesema katika mchezo huo walitengeneza nafasi nyingi ambazo kama wangezitendea haki basi wangeibuka kifua mbele katika uwanja huo wa ugenini.“Azam wameshinda katika uwanja wao wa nyumbani, tunakubali matokeo, tunaenda kujipanga na mchezo ujao ili kuhakikisha makosa yaliyojitokeza leo (juzi) yasirudie tena, nakuhakikisha tunapata matokeo chanya ili kuendelea kushika nafasi za juu katika msimamo wa Ligi Kuu,” amesema.Katika mchezo huo kama Azam wangetumia vema nafasi walizopata basi wangeibuka na ushindi wa mabao mengi zaidi ya waliyoyapata.Kwa ushindi huo unawafanya Wanalambalamba hao kurejea usukani wa ligi kwa kufikisha pointi 39,baada ya kucheza michezo 15, pointi moja juu ya Yanga inayotarajiwa kucheza leo. Bingwa mtetezi Simba ni ya tatu ikiwa na pointi 27.
michezo
2
JESHI la Polisi nchini limesema linafuatilia kwa karibu maoni, yanayotolewa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kifo cha Mmiliki wa Kampuni za IPP, Dk Reginald Mengi ili kujiridhisha kama kweli kifo chake, kimetokana na mkono wa mtu au ni kifo cha kawaida.Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro alipofika nyumbani kwa Mengi jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki.IGP Sirro alisema Jeshi lake linafuatilia yote, yanayozungumzwa kwenye mitandao na kama itabainika kifo cha Dk Mengi, kimetokana na mkono wa mtu, sheria itachukua mkondo wake, kwa kuwa hakuna aliye juu ya sheria.Lakini, pia alisema wanafanya hivyo ili kujiridhisha wasije wakamuonea mtu yeyote kwa sababu ya mitandao.Aliwataka wananchi watulie, kwa kuwa yote yanayoelezwa mitandaoni wameyachukua kwa uzito wake. Alisema Jeshi hilo limefungua kadokezo kwa ajili ya kufuatilia hayo yote, yanayozungumzwa ili kuona kuna ukweli kiasi gani.“Jambo la msingi tumalize kwanza msiba, hayo yanayozungumzwa mitandaoni tunayafuatilia, tukiingiza mambo mengi wakati wa shida, tunaweza kupoteza mwelekeo, nilikuwa napitia na utaona kila mtu ana maoni yake, niwaombe tu wananchi watulie,”alisema IGP Sirro.Akimzungumzia Dk Mengi, IGP Sirro alisema alikuwa na tabia ya unyenyekevu, aliheshimu watu na alijishusha licha ya uwezo mkubwa aliokuwa nao, jambo ambalo ni nadara kuliona kwa matajiri wengi.Alisema taifa limempoteza mdau muhimu katika masuala ya ushauri.Kikwete Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, alisema kuwa taifa limepoteza mmoja wa raia wake makini, mchapakazi na mahiri.Lakini, alisema yeye binafsi amempoteza mtu ambaye kwake alikuwa kama rafiki, kaka na ndugu wa karibu.Kikwete alisema Dk Mengi ni mtu aliyeipenda nchi yake na maendeleo ya taifa lake, ameishi maisha yake na kufanya mambo mengi, lakini pia amekuwa mtu wa aina yake na alitumia utajiri wake kuwasaidia wengine walio na mahitaji mbalimbali.“Taarifa ya kifo chake kweli ilinistua kwa sababu ni jambo ambalo sikulitarajia, lakini kifo hakina taarifa. Tulizungumza kwa simu na kukubaliana kuwa yeye atakaporudi na mimi nitakaporudi kutoka safari, tungekutana kwa mazungumzo yetu ya kawaida, tumekuwa tukikutana kila mara na kuzungumza,”alieleza Kikwete.Aliwataka wanafamilia kuwa na moyo wa uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu walichonacho.Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Dk Ayoub Rioba, amesema miongoni mwa mambo makubwa ambayo Dk Mengi aliyafanya enzi za uhai wake, si tu kubadilisha maisha yake binafsi, bali na maisha ya watu wengine.Alisema Dk Mengi pia ameliachia taifa urithi mkubwa wa kitabu chake kinachoitwa “I CAN, I MUST, I WILL”, lakini pia amesaidia kuhamasisha vijana nchini kuwa na fikra chanya wakati wote pamoja na kujiamini kwamba wanaweza kubadilisha maisha yao na kusaidia wengine.DC mstaafu Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Baraka Konisaga, alisema kuwa siyo rahisi kupata mtu wa aina ya Dk Mengi na inaweza kupita miaka mingi kupata mtu wa aina hiyo.Alisema namna bora ya kumuenzi Dk Mengi ni kuendelea kuutumia ushauri wake katika mambo mbalimbali ili kuyaendeleza yale mazuri aliyoyaamini na kuyapigania enzi za uhai wake.Dk Mengi alifariki Dubai katika Falme za Kiarabu (UAE), usiku wa kuamkia juzi Alhamisi, Mei 2 baada ya kuugua kwa muda mfupi.Kwa mujibu wa Mwanasheria wake ambaye pia ni Msemaji wa Familia, Michael Ngalo mwili wa Mengi utawasili kesho kwa ndege ya Shirika la Ndege la Emirates saa 8:00 mchana.Alisema baada ya kupokelewa, utapelekwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo huku waombolezaji wakiendelea kuomboleza nyumbani kwa marehemu.Ngalo alisema Jumanne asubuhi mwili utapelekwa katika Viwanja vya Karimjee ili wananchi na viongozi mbalimbali, wakiwemo wafanyabiashara wenzake wapate nafasi ya kutoa heshima za mwisho kabla ya kupelekwa nyumbani kwake.Kwa mujibu wa Ngalo, Jumatano mwili utasafirishwa asubuhi kwenda Kilimanjaro kwa ndege na utapokelewa katika Uwanja cha Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kisha kupelekwa nyumbani kwake Machame katika kijiji cha Nkuu kwa maziko yatakayofanyika Alhamis asubuhi, Mei 9 yakitanguliwa na ibada itakayofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) la Kisereny.
Kitaifa
0
MWAKA 2019 Wizara ya Maji inaanza utekelezaji wa mkakati maalumu wa miaka miwili, lengo likiwa ni kufi kisha maji vijijini kwa asilimia 85. Wizara hiyo pia imedhamiria kuanzisha Wakala wa Maji Vijijini kwa lengo la kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maji.Hayo yamebainishwa jijini hapa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Kitila Mkumbo alipokuwa akizungumzia mikakati ya kufikisha huduma hiyo kwa wananchi. Alisema mkakati huo maalumu, utakaotekelezwa kuanzia mwaka 2019 hadi 2020, lengo lake ni kuharakisha upatikanaji wa maji kwa wananchi. Profesa Mkumbo alisema utekelezaji wa mkakati huo, unatarajiwa kufikisha maji mijini kwa asilimia 95 na vijijini kwa asilimia 85, kama ilivyoahidiwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/2020.Alisema mkakati huo utaongoza shughuli za wizara kwa kipindi cha miaka miwili iliyobaki kuelekea mwaka 2020. Profesa Mkumbo alisema kwa mwaka huu wizara yake imeendelea kusimamia miradi ya maji takribani 1,595 nchi nzima, ambapo utekelezaji wake umechangia upatikanaji wa maji mijini kwa asilimia 78 na vijijini asilimia 60. Akizungumzia makusanyo kutoka mamlaka za maji zilizopo nchini, Profesa Mkumbo alisema mwaka wa fedha 2018/2019, mamlaka hizo zimepanga kukusanya Sh bilioni 364.8.Alieleza katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza katika mwaka wa fedha 2018/19, mamlaka 33 zimeshakusanya Sh bilioni 91.2 ambazo ni sawa na asilimia 25. Profesa Mkumbo alizikumbusha mamlaka za maji, kuzingatia agizo la Rais John Magufuli la kuzitaka kuchangia katika gawio la serikali kuanzia mwaka huu wa fedha. “Nizikumbushe mamlaka kuhakikisha zinasimamia ipasavyo katika ukusanyaji wa mapato, ambapo baadhi ya fedha wanazitumika katika kuboresha miundombinu yao. Lakini kubwa wakumbuke kuwa kuanzia mwaka huu wa fedha wana wajibu wa kupeleka gawio serikalini,” alisema.Katika hatua nyingine, Profesa Mkumbo alisema serikali imedhamiria kuanzisha Wakala wa Maji Vijijini kwa lengo la kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maji. Alisema serikali ilishapeleka bungeni muswada wa kuanzisha Wakala wa Maji Vijijini na tayari umesomwa kwa mara ya kwanza katika unge lililopita. “Tumeshapeleka muswada bungeni ambao tayari umeshasomwa kwa mara ya kwanza, muswada huu ulienda sambamba na wa vyama vya siasa, naoana huo ndio unapigiwa kelele sana,” alisema.Alisema uanzishwaji wa Wakala wa Maji Vijijini, utaondoa changamoto ya upatikanaji wa maji vijijini, kwa kuwa na chombo mahususi cha kusimamia miradi hiyo. “Tuna changamoto kubwa sana kwa upande wa vijijini ambapo mpaka sasa tulikuwa tunafanya kazi na wenzetu wa halmashauri ambao wana majukumu mengi na zina vipaumbele vingi, tumeona kuna haja ya kuanzisha taasisi muhimu,” alisema. Alisisitiza kuwa Wizara ya Maji inaendelea kusimamia miradi nchi nzima ili kuhakikisha watu wanapata maji na kutekeleza azma ya kumtua mama ndoo ya maji kichwani.
Kitaifa
0
KUANZIA Julai mosi mwaka huu serikali inatarajia kutoa tamko rasmi, litakalolenga kuhakikisha kila dereva wa lori na basi nchini, anakuwa na mkataba wake wa ajira.Aidha, tamko hilo litalenga kuhakikisha wamiliki wa mabasi na malori hayo nchini, wanafuata na kutekeleza sheria za kazi na ajira. Hayo yalibainishwa bungeni Dodoma jana na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu, Anthony Mavunde wakati akijibu swali la Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka (Chadema).Katika swali lake la nyongeza, mbunge huyo alitaka kujua serikali inachukua hatua gani kushughulikia malalamiko ya madereva wa malori na mabasi, ambao takribani asilimia 90 hawana mikataba ya ajira. “Sisi wa kule mipakani ndio tuna hali mbaya kila siku tunasikia migogoro baina ya madereva hawa na wamiliki kuhusu mikataba, serikali ina mpango gani kuharakisha jambo hili?” Alihoji.Mavunde akijibu swali hilo, alisema katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), pamoja na ahadi ya Rais John Magufuli aliyoitoa mwaka 2015 wakati wa kampeni juu ya mikataba ya ajira, tayari wameanza kushughulikia suala hilo. Alifafanua kuwa awali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), katika kutatua tatizo hilo, iliweka masharti kwa wamiliki wa magari hayo wanaoenda kuomba leseni, lazima maombi yao yaambatanishwe na mikataba ya ajira kwa ajili ya madereva wao.“Hata hivyo, tuliona sharti hili bado lina walakini, sasa siku mbili zijazo yaani kuanzia Julai Mosi mwaka huu wizara itatema cheche kwani tutatoa tamko juu ya hatua gani zitachukuliwa kwa wamiliki wasiowapatia mikataba madereva wao lakini pia kuhakikisha kila dereva wa lori au basi anakuwa na mkataba wake wa ajira,” alisisitiza Mavunde. Alisema tamko hilo litatolewa kwa mtengamano wa wizara mbili, ikiwemo wizara hiyo ya ajira chini ya Jenista Mhagama na Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi chini ya Kangi Lugola.Awali, katika swali lake la msingi, Mwakajoka alitaka kujua ni lini serikali itasimamia na kuhakikisha madereva wa malori na mabasi, wanapata mikataba ya ajira ili kuboresha maslahi yao na kuongeza ufanisi katika utumishi wao kazini. Akijibu swali hilo, naibu waziri huyo alisema serikali kwa kushirikiana na viongozi wa Umoja na Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji nchini, waliufanyia marekebisho na kuuboresha mkataba wa ajira na madereva uliokuwepo.
Kitaifa
0
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene alisema hayo juzi wakati akizindua mtambo mahususi wa kusafisha mafuta ya alizeti katika kongamano la viwanda vidogo lililofanyika mjini hapa.Alisema kwa kipindi cha mwaka 2010 hadi 2012 wastani wa mauzo ya mafuta ya kula nje ya nchi ulikuwa dola za Kimarekani milioni 54.8. Alisema kwa kipindi hicho wastani wa uingizaji wa mafuta kutoka nje ya nchi ulikuwa dola za Kimarekani milioni 275.6.“Wazalishaji wetu wa ndani wangeweza kunufaika na soko la mafuta kwa kiasi hicho cha fedha endapo wangeweza kuzalisha na kusafisha mafuta kufikia kiwango cha ubora kinachokubalika kimataifa,” alisema.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wasindikaji wa Mafuta ya Alizeti Mkoa wa Dodoma, Ringo Iringo alisema kumekuwa na ongezeko la uzalishaji wa alizeti ambapo mwaka 2007 wakati chama hicho kikianzishwa kulikuwa na uzalishaji wa tani 87,000, mwaka 2011 uzalishaji uliongezeka na kufikia tani 787,000 na mwaka 2012 uzalishaji uliongezeka na kufikia tani milioni 2.6.
Biashara
1
['Napoli na Ajax ziko tayari kumpigania Jan Vertonghen, 32, na kuishawishi Tottenham kumuuza beki huyo raia wa Ubelgiji kabla ya kuruhusiwa kuondoka kwa uhamisho wa bure msimu wa joto. (Telegraph)', 'Marseille na Aston Villa ni miongoni mwa klabu zinazomfuatilia mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge, 30, ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Uturuki ya Trabzonspor. (Mail)', 'Real Madrid imewasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mane, 27. (Le10Sport)', 'Manchester United na Tottenham wanatarajiwa kukabiliwa kwa ushindani mkali wa kumnunua kiungo wa kati wa Lille Mfaransa Boubakary Soumare,20, huku ofa sita za kumnunua zikiripotiwa kupokelewa na klabu yake. (Mail)', 'Kiungo wa kati wa Uswizi Granit Xhaka, 27, atalazimika kusubiri mkufunzi wa Arsena Mikel Arteta kutafakari pendekezo lake la kuhamia Hertha, Berlin kwa mkopo mwezi huu wa Januari. (Independent)', 'Kocha wa Chelsea Frank Lampard amepuuzilia mbali tetesi kuwa anapania kumnunua mshambuliaji wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 27. (Star)', 'Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amedokeza kuwa kiungo wa kati wa England Adam Lallana, 31, huenda akaondoka katika klabu hiyo pindi mkataba wake utakapomalizika mwisho wa msimu huu. (Mirror)', 'Everton imekuwa ikimtaka Moise Kean, lakini haina mpango wa kumuuza mshambuliaji huyo wa Italia wa miaka 19, ajenti wake anasema. (La Repubblica via Star)', 'Kiungo wa kati wa Sporting Lisbon na Ureno Bruno Fernandes, 25, ambaye alikuwa akilengwa na Manchester United, amesema anakaribia kujiunga na Tottenham msimu wa joto kuliko klabu nyingine yoyote. (Express)', "Tottenham wanaongoza kinyang'anyiro cha usajili wa beki wa West Brom Nathan Ferguson, 19, ambaye pia nafuatiliwa na Crystal Palace. (Mirror)"]
michezo
2
KLABU ya Singida United imemleta kocha Mserbia, Dragon Popadic kwa mkataba wa miezi 10 kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho kinachoonelekana kufanya vibaya kwenye muendelezo wa papatupapatu za Ligi kuu Tanzania Bara (TPL) msimu huu ili kuhakikisha wanashika nafasi za juu katika msimamo.Kocha huyo amekubali kuchukua jukumu la kufundisha timu hiyo na kurithi mikoba ya Hemed Moroco aliyekuwa anakinoa kikosi hicho ambapo kwa sasa ana majukumu ya kitaifa ya maandalizi ya timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17.Kocha huyo aliyewahi kukinoa kikosi cha Simba na kutengeneza rokodi kubwa na miamba hao, ameungana na miamba hao wa Singida United kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho hususani katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye michuano ya SportPesa inayotarajiwa kufanyika mwezi huu, FA,na Ligi Kuu ya Tanzania Bara (TPL).Akizungumza Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa kikosi hicho, Festo Sanga alisema:“ Popadic atakuwa Kocha Mkuu kwa sasa akisaidiwa na Dusan ambaye pia ni raia wa Serbia, kwa kipindi cha miezi 10 ili kuhakikisha kikosi hicho kinafanya vema.”Aidha, Sanga amesema makocha waliokuwepo kikosini hapo Suleiman Jabir na Shadrack Nsajigwa, tayari wameshapewa taarifa na wamekabidhiwa majukumu mengine ndani ya kikosi hicho.Kikosi hicho kimekuwa na matokeo ya kusuasua katika muendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara tofauti na msimu uliopita, hivyo wa miliki wa timu hiyo wameamua kuwapa kazi Waserbia hao ili kurejesha makali ya kikosi hicho kilichofika fainali ya Azam FA Cup msimu uliopita.Timu hiyo inashika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kucheza michezo 20, wakishinda michezo sita kutoka sare michezo sita kupoteza michezo sita wakiwa na pointi 24, huku Yanga akiwa kinara wa Ligi hiyo kwa kujinyakulia pointi 50.
michezo
2
KOCHA wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes, Sebastien Desabre amesema kuwa atatumia ujuzi wake wote alionao kuhakikisha wanamzuia nyota wa Misri anayecheza soka England.The Cranes iko katika Kundi A pamoja na wenyeji Misri katika mashindano ya Mataifa ya Afrika, Afcon 2019, yatakayofanyika nchini humo kuanzia Juni 21 hadi Julai 9. Timu hiyo ya taifa ya Uganda imepangwa kukutana na Misri katika mchezo utakaofanyika Juni 30 jijini Cairo nchini humo.Uganda, ambao wanashiriki fainali hizo kwa mara ya pili mfululizo, mbali na wenyeji Misri ambao wametwaa taji hilo mara saba, wako pia na mabingwa mara mbili Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR) na Zimbabwe.Hata hivyo, kocha huyo wa The Cranes alisema kuwa sio kundi jepesi, lakini Uganda ina matumaini ya kusonga mbele katika mashindano hayo ambayo kwa mara ya kwanza yanashirikisha timu 24.Nahodha na kipa Denis Onyango na Faruku Miya ndio wachezaji wa Uganda wanaotajwa sana katika vyombo vya habari, huku wachezaji wa DRC Cedric Bakambu na Khama Billiat wa Zimbabwe nyota wengine wako katika orodha hiyo. Lakini kutoka Uganda, hadi Ulaya na kurudi tena Afrika, ni Mmisri Mohamed Salah ambaye amekuwa akitajwa kila mahali.
michezo
2
WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani ametoa miezi mitatu kwa mameneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wa wilaya kuwasilisha takwimu ya viwanda walivyoviunganishia umeme kwenye maeneo yao.Aamewaagiza kuhakikisha wanafanya jitihada za kupeleka umeme na kuunganishia kabla havijakamilika kwa kupeleka ankara stahiki kwa wenye viwanda, ili waweze kufanya malipo mapema ya maunganisho.Alisema kwa kufanya hivyo Tanesco watajiondoa kuonekana wao kuwa chanzo cha kukwamisha ufanyaji kazi wa viwanda.Dk Kalemani alisema hayo juzi wakati alipokutana na watendaji na watumishi wa Wizara ya Nishati, Tanesco na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kujadili mipango ya usambazaji umeme kwa mwaka 2019/20.Kuhusu suala la uunganishaji umeme kwa wateja wa muda mrefu, waziri huyo alitoa mwezi mmoja kwa Tanesco kuunganishia umeme wateja wote waliolipia umeme kwa muda mrefu na hawajaunganishwa na umeme.Kuhusu upelekaji umeme vijijini, Dk Kalemani alisema kila mtumishi wa wizara, Tanesco na REA lazima watambue lengo la serikali ni kupeleka umeme katika vijiji vyote ifikapo Juni 2021, hivyo ni lazima kila mmoja ahakikishe kuwa hilo linafanikiwa na bei ya kuunganisha umeme ni Sh 27,000 na Meneja asiyetaka kutekeleza hilo aachie ngazi.Mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Dk Hamisi Mwinyimvua, Menejimenti ya Tanesco, REA na Bodi ya REA, ulijadili kazi zilizofanyika katika mwaka 2018/19 na kujipanga katika utekelezaji wa majukumu kwa mwaka wa fedha wa 2019/20.Baadhi ya masuala yaliyojadiliwa kwa undani kwenye kikao hicho ni upelekaji umeme viwandani, kuimarisha hali ya umeme katika maeneo yaliyounganishwa na gridi, kuunganishia umeme kwenye tasisi za umma.Mengine ni kuunganishia umeme maeneo yaliyopitiwa na miundombinu ya umeme, bei ya kupeleka umeme vijijini, ununuzi vifaa vya umeme, utambuzi wa wateja wanaohitaji umeme viwandani na utambuzi wa wazalishaji wadogo wa umeme.Kwa upande wake, Naibu Waziri Mgalu alisisitiza kuhusu upelekaji umeme kwenye taasisi za umma kama vile shule, zahanati na visima vya maji kutokana na umuhimu wake kwa jamii zinazozunguka maeneo hayo na kuagiza kuwa suala hilo liwekewe mkakati maalumu.Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Innocent Luoga alimshukuru Waziri Kalemani kwa kufanya mkutano huo ambao unasaidia kuboresha utendaji kazi na kutoa wito kwa Tanesco kuendelea kutatua changamoto mbalimbali kama za kukatika umeme na kutounganishia umeme wateja ndani ya muda mfupi.
Biashara
1
TANZANIA kwa mara nyingine, imepata heshima ya kipekee kwenye sekta ya utalii, baada ya kuchaguliwa kuwa nchi pekee Afrika, itakayotembelewa na wataalamu wa mifumo ya kimtandao kutoka China.Wataalamu hao wanatoka mtandao wa Baidu, unaokadiriwa kuwa na watumiaji takribani milioni 700 nchini humo.Katika siku za hivi karibuni, mtandao huo umezindua mradi uitwao ‘Wonder Planet’ unaolenga kutembelea nchi saba, kwa lengo la kupiga picha na kuandika taarifa za vivutio vya nchi hizo duniani.“Tanzania imebahatika kuwa miongoni mwa nchi hizo saba na ndiyo nchi pekee kutoka Bara la Afrika. Hakika ni heshima kubwa sana kwetu na itatusaidia kenye kutangaza vivutio vyetu vya utalii”, amesema Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii, Jaji mstaafu Thomas Mihayo.Akizungumza na ugeni huo jijini Dar es Salaam, Jaji Mihayo amesema ugeni huo uliokuwa na wajumbe 11, uliingia nchini Agosti 22, mwaka huu.Katika ziara yao ya siku 10 nchini, timu hiyo ilitembelea mji wa kihistoria wa Bagamoyo, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Makumbusho ya Olduvai George, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Hifadhi ya Ziwa Manyara, Mji wa Mwanza na Zanzibar.“Lengo kuu la ziara ya wataalamu hawa ni kupiga picha jongevu na za mnato na kuandika taarifa za vivutio mbalimbali vya utalii katika maeneo waliyotembelea na kisha kuziweka katika mtandao wao wa Baidu ili kutangaza vivutio vyetu vya utalii na kuongeza idadi ya watalii kutoka China watakaotembelea nchi yetu,” alisema Jaji Mihayo.Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Utalii Duniani (UNWTO), China ndio soko kubwa la utalii duniani, ambapo mwaka 2018 takribani Wachina milioni 130 walisafiri nje ya nchi yao kama watalii.Pamoja na idadi hiyo kubwa ya Wachina, wanaosafiri duniani kama watalii, watalii 32,773 ndio waliotembelea Tanzania kwa mwaka huo kama watalii .Mwenyekiti huyo aliahidi kuongeza idadi hiyo kufikia watalii 100,000. Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Devota Mdachi alisema ziara hiyo ni matunda ya ziara ambazo wamekuwa wakizifanya nchini China, kuhakikisha wanaongeza idadi ya watalii.“Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, China ndiyo nchi inayoongoza duniani kwa wananchi wake kutumia fedha sana wanaposafiri nje ya nchi yao. Kwa sababu hiyo, soko la China ni muhimu sana kwetu na tuna kila sababu kuhakikisha tunaongeza mikakati zaidi ya kuvuna watalii wengi,” alisisitiza Mdachi.Kiongozi wa Msafara huo, Jin Xiaping aliisifu Tanzania kwa vivutio ilivyonavyo. Aliahidi kuhamasisha watalii zaidi kutoka China, kutembelea Tanzania. Xiaping alitaja maeneo waliyotembelea na kusema walitamani wakae zaidi kwa uzuri na vivutio vilivyopo nchini .Aliahidi kurudi tena akipata muda. “Tumezoea kuona wanyama kama simba na wengine katika sehemu maalumu za kuhifadhi wanyama wa porini (zoo), lakini tulipofika Serengeti wanyama hao simba, chui na wengineo walikuwa wakisogelea gari letu. Ilikuwa ni furaha sana kuwaona wanyama hawa kwa karibu zaidi na wakiwa kwenye maeneo yao ya halisi,” alisema kiongozi huyo huku akiwa na furaha.Nchi nyingine sita zitakazotembelewa wataalamu hao ni za mabara ya Amerika, Asia na Ulaya. Lakini, hawakuzitaja.
Biashara
1
KIUNGO wa Simba, Gerson Fraga, amethibitisha kuwa yeye ni Mbrazil halisi, baada ya jana kuweka nyavuni mabao yote mawili katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi Coastal Union uliochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa ushindi wa bao 2-0.Katika mchezo huo uliochezwa muda mchache baada ya mvua kunyesha Fraga alifunga bao la kwanza dakika ya saba, kwa mpira wa kichwa akiwa ndani ya eneo la goli akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo, Clatous Chama ambaye jana alikuwa mwiba kwa wapinzani wao.Fraga tena aliwainua mashabiki wa Simba dakika ya 78, baada ya kufunga bao la pili kwa mpira uliotemwa na kipa wa Coastal Union, Soud Dondola, shuti lililopigwa na kiungo Hassan Dilunga aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Ibrahim Ajib.Ufundi na utulivu kwa wachezaji ulikosekana katika mchezo huo, baada ya uwanja kuwa na maji maji, na kufanya timu zote mbili kucheza mipira ya juu hasa katika kipindi cha kwanza.Kwa matokeo hayo Simba inaendelea kuongoza ligi ikiwa na pointi 47, katika michezo 18 kwa pointi 11 zaidi ya Azam FC wanaofuatia katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 36 katika mechi 17 na Coastal Union inashika nafasi ya tano ikiwa na pointi 30, baada ya kucheza michezo 18.Mechi nyingine za ligi kuu leo, JKT Tanzania na Polisi Tanzania ilisitishwa dakika ya 53 kufuatia Uwanja wa Uhuru kujaa maji na mpaka mchezo unaahirishwa walikuwa hawajafungana na mchezo kati ya Tanzania Prisons na KMC haukufanyika kabisa sababu ya mvua kubwa.Kagera Sugar iliifunga Singida United kwa 3-0 katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mabao yoye yakifungwa na Kelvin Sabato na katika Uwanja wa Majaliwa Namungo FC iliibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Mbao FC, mabao mawili yakifungwa na Reliants Lusajo na Hashim Manyanya na Ndanda ikicheza nyumbani kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona iliifunga Alliance FC kwa bao 1-0 lililofungwa na Vitalis Mayanga, Biashara United iliifunga Mwadui FC kwa mabao 2-1 yakifungwa na Mpapi Nasibu na Ramadhan Chombo ‘Redondo’ lile la Mbao lilifungwa na Mussa Chamgenga na Ruvu Shooting ikaichapa Lipuli FC 3-1 na mabao yake yakifungwa na Graham Naftari, Rajab Zahir na Sadat Mohamed huku bao la Lipuli likifungwa na Daruweshi Saliboko.
michezo
2
Klabu hiyo yenye maskani yake Anfield inaweza kushika nafasi ya pili endapo jana itakuwa imeifunga West Ham jana baada ya kuifunga Porto 5-0 katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa hatua ya 16 bora. Salah mchezaji wa kimataifa wa Misri amefunga mabao 22 katika mechi 26 za ligi tangu alipotua Liverpool akitokea Roma kwa pauni milioni 34, Juni mwaka jana."Nimekuja hapa kutwaa mataji,’’alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea alitokea benchi mara tatu ikiwa ni dakika 30 wakati akiichezea the Blues ilipotwaa ubingwa msimu wa mwaka 2014-15, akimaliza msimu huo kwa kutolewa kwa mkopo kwenda timu ya Italia ya Fiorentina. Msimu uliofuata alitumika akiwa Roma kwa mkopo kabla hajajiunga na timu hiyo ya Serie A kwa ada ya pauni milioni 12 Agosti mwaka 2016. Salah amefanya makubwa tangu arejee katika Ligi Kuu na anatarajia juhudi zake zinaweza kuiwezesha Liverpool kutwaa taji la kwanza tangu mwaka 2012. "Naweza kuwaambia mashabiki tunafanya kazi kwa asilimia 100 na kujaribu kutwaa kitu fulani kwa ajili ya klabu yetu,’’ alisema mchezaji huyo. "Sasa ni muda mrefu tangu klabu iliposhinda taji la Ligi Kuu. Ni ndoto yangu kushinda taji la Ligi Kuu, lakini nataka kushinda na klabu hii.”
michezo
2
TIMU ya Taifa ya soka ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 inayojiandaa na fainali za Afrika za vijana inatarajia kwenda Dubai Machi 20 kwa ajili ya kambi ya wiki mbili.Akizungumza jana Kocha wa timu hiyo, Oscar Mirambo alisema timu hiyo ikiwa huko itacheza michezo ya kirafiki dhidi ya timu zitakazotangazwa baadae. “Tulikuwa twende Zanzibar lakini imeshindikana baada ya hotel tuliyokuwa tufikie kuwa na watalii wengi ila sasa tutakwenda Dubai na tukakaa huko kwa wiki na tukirudi tunaingia moja kwa moja kwenye fainali za Afrika,” alisema Mirambo.Pia Mirambo alisema licha ya wachezaji wake kufungwa michezo miwili kati ya mitatu waliyocheza tayari wameshasahau maana aliwaambia matokeo hayo hayawezi kubadilika zaidi itabaki historia hivyo wafikirie mbele. “Pamoja na kupoteza wachezaji walipata uzoefu na kuona utofauti wa soka la Afrika na Ulaya na sasa akili zao wameziweka katika fainali za Afrika na wanajua watanzania wanawategemea na ni wajibu wao kufanya vizuri ili wafuzu kucheza fainali za dunia,” alisema Mirambo.Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Kidao Wilfred alisema timu inahitaji michezo ya kirafiki ya kimataifa na watajitahidi kuhakikisha wanapata ili benchi la ufundi liweze kupima kile walichofundisha baada ya kutoka katika mashindano ya Uturuki.Fainali za Afrika zitakazofanyika hapa nchini kuanzia Aprili 14-28 katika Viwanja vya Taifa, Uhuru na Chamazi na tayari CAF imetaja waamuzi 29, wakiwemo wanawake watatu ambao watachezesha fainali hizo Mashindano yashirikisha timu kutoka Tanzania, Nigeria, Angola na Uganda ambazo zipo kundi A na kundi B litakuwa na timu za Guinea, Cameroon, Morocco na Senegal na timu zitakazofuzu nusu fainali zitawakilisha Afrika kwenye fainali za dunia kwa vijana wa umri huo.
michezo
2
Vilabu vilivyotimuliwa ni pamoja na Al Merreikh iliyokuwa nafasi ya pili kundi A klabu Bingwa Afrika ikiwa na pointi saba ikiongozwa na Etoile du Sahel ya Tunisia. Timu nyingine ni Al Hilal Omdurman iliyo katika nafasi ya mwisho kundi A Klabu Bingwa Afrika ikiwa na pointi nne.Timu nyingine ni Hilal El Obied Club iliyokuwa ikiongoza kundi C ikiwa na pointi 10 katika kombe la Shirikisho.
michezo
2
TAASISI inayojishughulisha na huduma za kuboresha afya pamoja na tohara kwa wanaume (Intra Health) imewafikia wanaume 305,715 mwaka huu na kuwafanyia tohara, jambo linalosaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi nchini. Aidha wanaume takriban 400,560 wanatarajiwa kufikiwa na kufanyiwa tohara hadi ifikapo mwaka 2019 katika mikoa saba na wilaya 33 nchini. Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Programu kutoka Intra Health Dk Pastory Sekule wakati akieleza kuhusu utekelezwaji wa Mradi wa Tohara Plus ukiwa na lengo la kuimarisha huduma za tohara na kuhakikisha wanaume wa miaka 10 hadi 29 wanafanyiwa tohara na kufikia asilimia 90 katika mwaka 2020.Aidha alisema taasisi pia inaelekeza nguvu kwa kufanya tohara kwa watoto wachanga kuanzia mwezi mmoja hadi miezi miwili na huduma hiyo iweze kuwa endelevu ni lazima wakubwa wawe tayari wamefanyiwa kitendo hicho. Alisema mradi wa Tohara Plus unatekelezwa katika mikoa saba na wilaya 33 na taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine wakiwemo Shirika la Tayoa na Afya Plus.Aliitaja mikoa inayoshiriki katika mradi huo pamoja na kiwango kiwango cha wanaume wasiofanyiwa to hara kwenye mabano kuwa ni pamoja na Simiyu asilimia (53), Shinyanga (52.5), Kagera (39), Kigoma (33.6), Geita (33), Mwanza (22.4) na Mara asilimia (9.5). Alisema mradi huo unafanyika katika mikoa ambayo kiwango cha maambukizi ya Ukimwi kiko juu huku wanaume wakiwa hawajafanyiwa tohara wakiwa na sababu mbalimbali.Hata hivyo, alisema kumekuwa na changamoto katika kuwafikia wanaume wenye umri mkubwa kuanzia miaka 20 na kuendelea huku wengine wakionesha kutokujua faida za tohara na wengine wakiona kama itakuwa kidonda kisichopona.“Ili kuwafikia watu wenye umri mkubwa wakati mwingine huduma inaweza kutolea usiku, wengine wakikataa kufanyiwa tohara na mhudumu wa kike lakini pia tunawahimiza wenzi wao waweze kuwaelimisha umuhimu wa tohara,” alisema Dk Sekule.Kuhusu watoto wachanga alisema wanalenga kuwafikia watoto 10,284, huku wakiongeza huduma iweze kutolewa kwa usahihi na kwa usalama zaidi ambapo wanahimiza tohara kufanyika pindi mtoto akianza huduma za chanjo nyingine. “Ikitokea tohara ikafanywa huondoa uwezekano wa maambukizi ya Ukimwi kwa asilimia 60, ingawaje sio kwamba ni tohara peke yake ndio inayopunguza maambukizi ya Ukimwi bali pia kuna uhitaji wa kutumia kondomu na hata kubadili tabia za mahusiano,” alisema.
Kitaifa
0
Alisema vitafunwa vingi vimekuwa vikiachwa wazi na kupata vumbi hata kuingiwa na wadudu mbalimbali, hali inayofanya kukata mitaji kutokana na kukosa soko.Alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akizungumza na wajasiriamali wanaotumia huduma za Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) alipotembelea vikundi vinavyojihusisha na mikopo katika benki hiyo mjini Dodoma.Alisema wapika vifafunwa na wauzaji wake walio wengi si waangalifu wanapopika vitafunwa hasa chapati,vitumbua, maandazi na bajia, kwani wamekuwa wakiacha bila hata kufunika hali inayotishia afya za walaji.“Mjitahidi kutumia vifungashio vizuri vitakavyovutia walaji hali itakayowafanya kuwa na wateja wengi na kukuza mitaji yenu. Siku hizi hata mahoteli makubwa wanatoa zabuni ya kutengenezewa vitafunwa sasa mteja akikukuta mchafu utakosa fursa na kubaki na imani za kulogwa,” alisema.Pia aliwataka wajasiriamali kutokata tamaa kwa sababu maisha ni hatua maana wengi huishia njiani kutokana na wanapoanza wanataka kupaa kimaisha kwa kila walichokihitaji na wanapona wanachelewa huamua kuacha kwa kisingizio cha biashara anayofanya haifai.Hata hivyo, Ofisa Mikopo Mwangalizi wa Benki ya Wanawake Tanzania, Tawi la Dodoma, Digna Damas aliwataka wajasiriamali hao kuwa waaminifu katika mikopo wanayochukua ili waendelee kufaidika kwa kukuza mitaji kutokana na aina yoyote ya biashara wanazofanya ili wajikwamue kiuchumi.
Biashara
1
['Manchester United inajiandaa kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, kwa Real Madrid au Juventus mwezi huu, lakini wanataka £150m. (Express)', 'Manchester United inapania kuwanunua viungo wa kati wa Aston Villa Jack Grealish, 24, na James Maddison, 23, kutoka Leicester. (Independent)', 'Wachezaji wengine wanolengwa na United ni kiungo wa kati wa Juventus na Ujerumani Emre Can, 25, na Sean Longstaff, 22, wa Newcastle. (ESPN)', 'Aston Villa ina mpango wa kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Michy Batshuayi, 26, kwa lengo la kumpatia mkataba wa kudmu. (Footmercato - in French)', 'Villa pia wanamtaka mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 33. (Sun)', 'Mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, ameelezea kujitolea kwake kwa Arsenal na kutuliza tetesi za kuondoka kwake mwezi Januari. (Evening Standard)', "Arsenal imeingia katika kinyang'anyiro cha kumsaka beki wa Bournemouth na Uholanzi Nathan Ake, 24. (Telegraph)", 'Inter Milan ni moja ya klabu zilizowasiliana na wawakilishi wa kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen. Kandarasi ya kiungo huyo wa miaka 27 inakamilika msimu huu wa joto. (Sky Sports)', 'Manchester City inatarajiwa kurefusha kwa mwaka mmoja mkataba wa kiungo wa kati wa Brazil Fernandinho, 34. (Sun)', 'Dau la Chelsea la yuro milioni 40 la kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Moussa Dembele ,23, limekataliwa na Lyon. (Footmercato - Kwa Kifaransa)', 'Aston Villa inatafakari uwezekano wa kuweka dau la kumnunua kipa wa Stoke City Muingereza, Jack Butland, 26. (Mail)', 'Ajax imesitisha mpango wa kumnunua beki ya Tottenham na Ubelgiji Jan Vertonghen kwa sababu bei ya mchezaji huyo wa miaka 32 ni ghali sana . (De Telegraaf - Ujerumani)', 'Southampton wanataka kumsaini beki wa Valladolid raia wa Ghana Mohammed Salisu, 20. (Sky Sports)', "Leicester imeipiku Arsenal katika kinyang'anyiro cha usajili wa beki wa Juventus na Italia, Daniele Rugani, 25. (Express)", 'Arsenal imemuulizia winga wa Atletico Madrid na Ufaransa Thomas Lemar, 24. (Marca - ya Uhispania)', 'Real Madrid imewasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mane, 27. (Le10Sport)', 'Manchester United na Tottenham wanatarajiwa kukabiliwa kwa ushindani mkali wa kumnunua kiungo wa kati wa Lille Mfaransa Boubakary Soumare,20, huku ofa sita za kumnunua zikiripotiwa kupokelewa na klabu yake. (Mail)']
michezo
2
Wachezaji wa Simba na viongozi wao wamewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) muda mfupi uliopita wakiwa njiani kwenda Arusha kupambana na African Lyon keshokutwa.'Wekundu wa Msimbazi' wamekwenda huko wakiwa na furaha ya kuwanyuka watani wao Yanga 1-0 jana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Meddie Kagere alikuwa shujaa wa Simba akiifungia bao katika ushindi huo mechi ya Ligi Kuu Bara.Kagere alifunga bao hilo kwa kichwa katika dakika ya 71 akiunganisha pasi safi ya nahodha John Bocco na kupeleka kilio mitaa ya Jangwani.Pamoja na kwamba mechi ya watani lolote hutokea, lakini Simba ilikuwa ikipewa nafasi kubwa kutokana na ubora wa kikosi chao na hasa baada ya kufanya vizuri katika mechi yake ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Ahly huku wachezaji wake wakionesha kiwango bora.Kutokana na mwenendo wa ligi ulivyo, Simba ilihitaji ushindi zaidi ili kujiweka vizuri kwenye mbio za kutetea taji lake la ubingwa kwa vile Yanga iko kileleni ikiwa na pointi 58 katika mechi 24 ilizocheza.Ushindi wa jana umeifanya Simba kufikisha pointi 39 na kurejea nafasi ya tatu huku ikicheza mechi pungufu 16, kutokana na kuwa kwenye michuano ya kimataifa.Katika mechi ya jana, Simba ilitawala sehemu kubwa ya mchezo huku washambuliaji wake wakifika langoni mwa wapinzani wao mara kwa mara na kama si uhodari wa safu ya ulinzi ya Yanga, hadithi ingekuwa nyingine. Mpira ulianza kwa kasi Simba ikimiliki na kushambulia zaidi kwa dakika 25 za mwanzo lakini haikufunga.Katika dakika hizo 25 za mwanzo Simba ilikosa mabao kadhaa takriban matatu ikiwemo lile la dakika ya 16 ambapo Paschal Wawa akiwa kwenye nafasi nzuri alishindwa kufunga.Baada ya dakika hizo, Yanga ilianza kucheza kwa kuzuia na kufanya mashambulizi ya kushtukiza na Paul Godfrey nusura apate bao lakini shuti lake lilipaa juu. Dakika hizo pia Herieter Makambo alikosa bao akiwa kwenye nafasi nzuri baada ya shuti lake kupaa juu.Simba ilikianza kipindi cha pili kwa shambulizi la Mohammed Husein ‘Zimbwe Jnr’ lakini shuti lake lilipaa lango. Dakika tano baada ya kuanza kipindi cha pili, nusura Feisal Salum ‘Fei Toto’ aifungie Yanga bao lakini shuti lake la nje ya 18 lilipaa juu.Simba:Aishi Manula, Zana Coulibaly, Mohamed Hussein, Juuko Murshid, Paschal Wawa, James Kotei, Clatous Chama/ Hassan Dilunga, Jonas Mkude, John Bocco, Meddie Kagere/ Haruna Niyonzima na Emmanuel Okwi/ Mzamiru Yassin.Yanga: Ramadhan Kabwili, Paulo Godfrey, Gadiel Michael/ Mateo Antony, Andrew Vicent, Kelvin Yondani, Abdallah Shaibu, Feisal Salum, Papy Tshishimbi, Heritier Makambo, Amiss Tambwe/ Mrisho Ngassa na Ibrahim Ajibu/ Mohamed Issa ‘Banka’.
michezo
2
KOCHA Mkuu wa timu ya Mbao FC ya mkoani Mwanza, Amri Saidi amesema timu yake iko tayari kwaajili ya mchezo wao wa kesho dhidi ya Stand United utakaochezwa katika Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Shinyanga. Amri alisema timu yake imeendelea na mazoezi tangu Alhamisi na wachezaji wake wote wapo katika hali nzuri kwakuwa hakuna majeruhi.Alisema anawapongeza wadau na mashabiki wa klabu yao kwa sapoti yao na amewaomba wajitokeze kwa wingi mkoani Shinyanga kushuhudia mchezo dhidi ya Stand united. Kocha huyo wa zamani wa timu ya Lipuli FC alisema atatumia mbinu ya kushambulia na kulinda zaidi katika mchezo wake dhidi ya Stand United. Mbao FC inayodhaminiwa na Kampuni ya Gf Truck & Equipment ipo katika nafasi ya tano ikiwa na alama tatu baada ya mchezo mmoja iliyocheza. Kwa upande wake, kiungo wa timu hiyo Ibrahim Njohole ‘ Dunyu’ alisema wamejipanga vyema kuhakikisha wanaifunga Stand United.
michezo
2
Kwa Mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez, nyongeza ya fedha hizo inatoa fursa kwa wateja wa Tigo Bima kumudu gharama za huduma za afya zinazopanda kila kukicha.“Tunafahamu mzigo wanaobeba wananchi katika kulipia huduma za afya ni mkubwa. Hivyo malipo katika huduma ya Pona na Tigo Bima yatasaidia kupunguza gharama hizo. Maamuzi ya kuongeza mara mbili fedha tunayowalipa kwa ajili ya matibabu mahospitalini ni udhihirisho wa jitihada zetu katika kuhakikisha wateja wetu wanapata thamani stahiki ya huduma za afya,” alisema Gutierrez.
Biashara
1
MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dk. Amos Nungu amesema hivi sasa wamejipanga kutoa elimu vyuoni ya kuwajengea uwezo wanafunzi kwa kuanzisha kumbi za ubunifu ili waelewe ni bunifu gani zinaweza kuleta majibu chanya kwa watanzania.Dk. Nungu alisema hayo leo ikiwa ni siku ya mwisho ya kufungwa kwa maonyesho ya 14 ya Elimu ya Juu ambayo yamefanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Alisema lengo la kuwajengea uwezo ni kuwawezesha wabunifu mbalimbali kubuni vitu ambavyo vinatokana na changamoto mbalimbali katika jamii na vinavyoweza kupatiwa majibu chanya yatakayosaidia.“Kazi kubwa tunajenga uwezo kwa kumbi za ubunifu. Kuna bunifu ambazo mbunifu kaangalia changamoto na kutengeneza majibu yake. Tuna jukumu kubwa la kuchambua bunifu zinazouzika,” alisema.Alisema katika suala la ubunifu Costech ipo tayari kufanya kazi na kila mtu ili kuhakikisha wabunifu wanasaidika.Alisema katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda, Costech inataka kuwafikia wabunifu huko waliko kwa kutoa elimu.
Kitaifa
0
Agizo hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, wakati alipokuwa Arusha kwenye soko la vinyago lililoungua mwishoni mwa mwaka jana na kuteketeza maduka 223 ya wajasiriamali wa bidhaa za vinyago vya watalii.Nyalandu alisema tozo zilizojitokeza kwenye viwanja vya ndege, zisimame mara moja kwa sababu zinaua soko la vinyago na kukosesha mapato wajasiriamali.“Hizi tozo zipo kinyemela, zimeanzishwa kinyemela na wanatoza mara tatu ya bei ya kinyago kilichonunuliwa, jambo linalowakera watalii kununua vinyago hivyo,” alisema.Aidha, aliwapa mchango wajasiriamali hao mchango wa Sh milioni 100 ili kuharakisha kukamilika kwa soko hilo, ambalo lipo eneo la CCM.“Mchango huu nataka uje mara moja na naagiza Shirika la Hifadhi za Taifa - TANAPA waandae mara moja ili pesa hii ije hapa iwasaidie hawa wajasiriamali,” alisema.Nyalandu pia aliwataka wajasiriamali hao, wawe mabalozi wa kuitangaza TANAPA na utalii Tanzania na mabalozi wa ukarimu wa watanzania. Mwenyekiti wa soko hilo, Mgaya Ally Kondo alishukuru kwa zawadi hiyo kwa niaba ya wenzake.Alisema wafadhili mbalimbali wamejitolea, lakini kufika hatua iliyopo sasa wanahitaji Sh milioni 130 ili kukamilisha kila kitu na wajasiriamali waanze kazi. “Lakini kwa msaada huu, tunamshukuru sana Mungu na tunaamini sasa kilio chetu kimefika mwisho.Soko hili lina wafanyakazi zaidi ya 500, sababu kila duka kati ya 223 limeajiri wasaidizi watatu au wawili, hivyo waathirika na moto huo ni wengi,” alisema
Biashara
1
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amesema haijakatazwa mtu kumiliki zaidi ya kadi moja za simu ilimradi ziwe za mitandao tofauti.“Tunatamani kila Mtanzania awe na ‘line’ moja ya simu kwa mtandao mmoja, akitaka nyingine atoe taarifa,” amesema.Nditiye ameyasema hayo bungeni wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu kwenye kikao cha Bunge la 11 kinaoendelea jijini Dodoma.Ameongeza kuwa lengo kuu ni kupunguza wingi wa kadi hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zinachangia vitendo vya uhalifu wa simu ikiwa ni pamoja na wizi akitolea mfano mbinu ya “ile pesa nitumie kwa namba hii.”
Kitaifa
0
KAMPUNI inayotoa huduma za usafi ri kwa njia ya mtandaoni nchini (Bolt), imezindua kitufe cha dharura (SOS) kwa lengo la kuimarisha usalama wa madereva kipindi wanapokutana na hatari yoyote.Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Meneja wa Bolt Tanzania, Remmy Eseka alisema madereva wanaotumia programu hiyo ya Bolt sasa wanaweza kutumia huduma hiyo mpya ya usalama muda wowote watakapohisi kuwa wapo hatarini au eneo ambalo si salama.Alisema matumizi hayo ya kitufe cha dharura (SOS) yamekuwa kama mwendelezo wa Bolt kutumia teknolojia kuimarisha usalama wa madereva wanapokuwa barabarani. “Usalama wa dereva na abiria ni suala la muhimu kwetu. Tunaongeza safu ya usalama wa dereva zaidi ya ule uliopo tayari wa kufuatilia mubashara safari kwa kutumia GPS na mfumo wa thathmini.“Kitufe cha dharura (SOS) kilichopo kwenye programu ya Bolt ya dereva, huwezesha taarifa kuwafikia kampuni ya ulinzi ya SGA Tanzania Limited, kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma hizi Afrika Mashariki,” alisema meneja kampuni hiyo ambayo zamani ilifahamika kwa jina la Taxify.Meneja wa Mauzo na Masoko wa SGA, Faustina Shoo akisema kitufe cha dharura (SOS) kilichowekwa kwenye programu ya madereva kinapotumika, simu hupelekwa kituo cha dharura cha SGA, ambao baada ya kuhakiki uhalali wa dereva, wanapeleka gari la wagonjwa au timu ya askari kuelekea alipo dereva. “Bolt italipia gharama hizi na zitakazopitishwa kwa kila tukio.Tunaendeleza nia yetu ya kujibu mahitaji ya wateja/wabia kwa kutoa huduma ya uokoaji wa dharura kwa madereva wa Bolt kutokana na ubia huu. “Madereva wa Bolt wanahakikishiwa kupata huduma ya masaa 24 kupitia kitengo chetu cha dharura iwapo watapata tatizo wakiwa safarini,” alisema.
Kitaifa
0
Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa kumi wa wanahisa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Donald Kamori alisema ongezeko hilo linatokana na usimamizi mzuri wa Bodi ya Wakurugenzi wa TCCIA Investment Company Limited.“Miaka kumi iliyopita mtaji wetu ulikuwa ni kiasi cha Sh bilioni 2 lakini kwa sasa tunaongelea Sh bilioni 33 kuishia Desemba mwaka 2014,” alisema Kamori.“Sisi ni wadogo, lakini tunakwenda vizuri, hii inatokana na usimamizi mzuri wa watu wetu wa hesabu kwa kushirikiana na Bodi,” aliongeza.Alisema mwaka 2014 kampuni ilipata faida ya jumla ya Sh milioni 784 kabla ya kulipa kodi ambayo aliielezea kuwa ongezeko kubwa kulinganisha na mwaka 2013 ambapo faida ilikuwa ni Sh milioni 588. Kutokana na kupata faida kubwa, kampuni imeridhia kutoa gawio kwa wanahisa wake ambapo itatumika jumla ya Sh milioni 274.“Kutokana na hilo, Bodi imeridhia kulipa gawio la Sh 48 na senti 26 kwa kila hisa moja kwa hesabu zilizokaguliwa za mwaka 2014 kulinganisha na gawio la Sh 36 na senti 96 kwa mwaka 2013 kwa hisa moja,” aliongeza.Akizungumzia mwenendo wa kampuni na ukuaji wake, Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Aloyce Mwamanga, alisema kwa sasa kampuni ipo katika mchakato wa kubadilisha jina kutoka TCCIA Investment Company Limited na kuwa TCCIA Investment Public Limited Company.
Biashara
1
Kiongozi wa upinzani, Felix Tshisekedi, ameshinda uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Tume ya Uchaguzi (CENI) yatangaza kuamkia leo. Matokeo yaliyochapishwa na BBC yanaonesha kuwa, kati ya wapigakura asilimia 48 waliojitokeza, Tshisekedi amepata jumla ya kura 7,000,000, akifuatiwa na Martin Fayulu aliyepata kura 6,400,000 huku Emmanuel Shadary akiambulia kura 4,400,000.Endapo akithibitishwa, Tshisekedi anakuwa kiongozi wa kwanza kutoka upinzani kushinda urais wa DRC, tangu taifa hilo lipate uhuru mwaka 1960.Rais Joseph Kabila anaachia madaraka baada ya kudumu kwa miaka 18, akipokea kiti hicho kutoka kwa baba yake, Laurent Kabila aliyeuawa kwa risasi.
Kimataifa
3
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema kama Watanzania wanataka kufanya vizuri katika michezo, wanatakiwa kutojivuta katika ushiriki wao kwenye mashindano.Akizungumza katika michuano ya Michezo ya Shule za Msingi na Sekondari ya Afrika Mashariki (Feasssa) yaliyomalizika jijini Arusha, Mwakyembe alisema ni aibu kwani Tanzania haijafanya vizuri katika mashindano hayo.Alisema kuna mambo ambayo yanatakiwa kupatiwa ufumbuzi, ikiwemo suala la Watanzania kujivuta kushiriki katika michuano mikubwa kama hiyo na kusema ni aibu kwa Tanzania kama wenyeji kuleta wanafunzi 650 wakati wageni Kenya 750, Uganga 950.Alisema nah ii sio mara ya kwanza kutokea tatizo kama hilo, ambalo linatokana na kujivuta kwa kutokuwa na mawasiliano mazuri.Alisema tukitaka kushindana tushindane kweli na tukiendelea kufanya mambo nusu nusu tunaiaibisha nchi, ambayo jina lake ni kubwa na kusisitiza kuwa mwaka ujao watahakikisha Tanzania itarudi na medali za kutosha.“Tanzania imepata medali chache na hii inaonesha itilafu kubwa sana katika timu za Tanzania, wageni wamekuja na shule za kimataifa sisi kitu gani kimetuzuia kuja na shule za kimataifa hii inaonesha hatuna mawasiliano ya pamoja kila mmoja anakuwa na lake na kutokana na hilo, Wizara tutakaa pamoja kulishughulikia na kuhakikisha hatuzitengi baadhi ya shule,”amesema Mwakyembe.Hawa ni wanafunzi na sio klabu za soka lazima wasome na wacheze kuna muda wa kufanya mazoezi na muda wa kusoma.Akizungumzia kuhusu maandalizi alisema maandalizi yaliyofanyika ni yale yale ambayo hata nchi zingine zinayafanya na kusema kusiwe na visingizio, kwani hao walioshiriki ni wanafunzi na sio klabu au taaisi za soka watenge muda wa kufanya mazoezi na muda wa kusoma.Alieleza kuwa kutofanya vyema ni kutokana na kutojipanga katika kuhakikisha kila kijana ambaye ana uwezo anashiriki katika michuano hiyo ya Feasssa.“Timu iliyoibuka bora katika michuano ya Umiseta kwa soka mwaka huu ilikuwa Ruvuna na kwa shule za msingi ilitoka Geita, hatujafanya vibaya sana lakini kwa nchi kubwa kama yetu tungehitahi kuwa na medali nyingi ili kila mtu anayekuja ajue anakwenda katika nchi yenye uwezo kimichezo, “alisema.Michuano ya Feasssa imemalizika jijini hapa ambapo nchi ya Uganda ilifanikiwa kuibuka mabigwa wa jumla kwa kuondoka na jumla ya medali 27, ambazo ni dhahabu, fedha na shaba.
michezo
2
MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kama Sugu, amemwambia Rais John Magufuli kuwa anaunga mkono jitihada zake za kuwaletea maendeleo Watanzania.Sugu alizungumza hayo mjini Mbeya jana katika mkutano wa Rais Magufuli na wananchi. Alisema kuwa pamoja na kwamba yuko chama kingine, lakini anatambua na kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli.“Tunaambiwa tunapinga kila kitu, No, kuna vitu vingi sana tunakuunga mkono, lakini vile tunavyokuunga mkono hawakwambii kwamba tunakuunga mkono, lakini hii haiondoi uhalali wetu wa kutoa maoni yetu... mimi naunga mkono bila kuhama chama changu” alisema Mbilinyi, ambaye ni mbunge wa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).Alisema mwaka jana kipindi kama hicho, alikuwa gerezani na alisikia yuko Iringa, akajua angekwenda Mbeya ambako asingeweza kuonana naye, lakini aliondoka. Hivyo, alisema anashukuru jana wameonana. Akizungumzia changamoto za mkoa huo, Sugu alisema tatizo la kwanza ni maji. Alisema wakazi wa Halmashauri ya Jiji Mbeya wanaopata maji ni asilimia 60.Alisema halmashauri hiyo walifanya upembuzi, wakasema zinahitajika Sh bilioni 70 kuyatoa maji mto Kiwira ili kumaliza tatizo hilo. Hivyo, alimuomba Rais kufanikisha suala hilo na kwamba suala hilo likifanikiwa, ataacha sifa kubwa kwani maji hayo ni mengi, yataweza kufika hata mkoa jirani wa Songwe Alitaja changamoto nyingine ni wafanyabiashara ndogo (machinga), ambapo aliitaka uwekwe utaratibu mzuri kwa machinga.Badala ya kuwatafutia sehemu moja ya kuwaweka kufanyia biashara zao, waachwe wawe huru wawekewe utaratibu wao wa kufanya biashara. Pia, Sugu (pichani) alizungumzia tozo na kodi nyingine kwa wafanyabiashara. Kwa upande wake, Rais Magufuli alisema anapenda wafanyabiashara hao, kufanya shughuli zao kwa uhuru, ambapo alifanya uamuzi hapo wa kuwapatia Uwanja wa Ndege wa Mbeya kufanyia biashara zao.Uwanja huo, ambao ni wa zamani, hautumiki kwa hivi sasa. Aidha, Rais alisema serikali imetoa vitambulisho maalumu ili kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa uhuru. Lakini, alisisitiza wasitumiwe na wafanyabiashara wakubwa.“Wamachinga ndio mlionifanya niwe kiongozi wenu, mnataka mahali pa kufanyia kazi ambapo ni mjini, Uwanja wa Ndege wa Mbeya eneo hilo tunabadilisha matumizi hapa, eneo hilo viongozi wa mkoa wa Mbeya mliandae vizuri, ndilo litakuwa la wamachinga wa Mbeya, lakini pia lazima kiwekwe kituo cha magari,” alisema Rais.Aliwakumbusha wafanyabiashara wote nchini kwamba anapowatetea, haimaanishi wanaruhusiwa kufanyia biashara popote, bali mikoa itengeneze mazingira wafanye biashara zao mjini. Hata hivyo, alisema eneo la wafanyabiashara hao kuungua moto mara kadhaa, inawezekana kuwa linachomwa moto kwa makusudi. Rais Magufuli alisema baada ya kuchaguliwa, alikuwa na kazi moja tu ya kufanya kazi kuwaletea maendeleo Watanzania.“Ndio maana nimefika hapa Mbeya kuwashukuru kwa imani mliyonipa, imani hii ilioneshwa na watanzania wote na ninaamini maendeleo hayana chama, hivyo tuiendeleze taifa letu, lakini nafahamu ninayofanya hata yako kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi,” Mfuko Bima Afya Rais Magufuli aliupongeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kazi kubwa inayofanya.Alisema hayo kwenye mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Ruanda Nzove wakati akizungumza na wananchi, baada ya kuzindua jengo la NHIF Tower Mbeya. Jengo hilo litatumika kuhudumia wanachama pamoja na kitega uchumi. “Leo nimepata heshima ya kufungua jengo zuri sana la NHIF na nimpongeze sana Mwenyekiti wa Bodi, Mama Makinda ambaye aliona umuhimu wa kujenga jengo hili huku ambalo ni zuri sana.Hakika alitambua umuhimu wa Mbeya na kilichonifurahisha zaidi ni kusikia jengo lina wapangaji zaidi ya asilimia 91,” alisema Rais. Rais alipongeza watendaji wa mfuko huo kwa kazi kubwa wanayofanya. Aliutaka uongozi kujielekeza katika uwekezaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba ili kuboresha zaidi huduma za matibabu. “Majengo ni mazuri lakini tusiendeleze sana kujenga, jielekezeni kujenga viwanda vya madawa na vifaa hospitalini.Kwa hili nakupongeza sana na sijilaumu kukuteua, naomba unipelekee pongezi hizi kwa watendaji wa NHIF,” alisema Rais. Aliwaomba watanzania kujiunga na NHIF ili kupata huduma kupitia mfumo wa Bima ya Afya. Ahadi Alisema alipokuja kwenye kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015, aliahidi mambo kadhaa na ahadi kubwa ilikuwa kudumisha amani na kuimarisha muungano. Alisema serikali imedumisha amani Tanzania na ni nchi yenye amani.Alipongeza viongozi mbalimbali, ikiwemo viongozi wa dini kwa kudumisha amani Pia, alisema serikali imedumisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya, rushwa, nidhamu kwa utumishi wa uma, ulinzi katika rasilimali, kuongeza ukusanyaji mapato kutoka Sh bilioni 50 hadi Sh trilioni 1.3, kupambana na wizi, ubadhilifu na safari za nje kwa viongozi.Aidha, alisema serikali imetekeleza miradi mingi ya maendeleo, ambapo kwenye miundombinu kwa Mbeya, serikali imekamilisha ujenzi wa barabara ya Mbeya-Chunya. Kwamba ataweka mawe ya msingi ujenzi wa barabara nyingine katika mkoa huo. “Imechosha kuona magari yanaangukia mengine na watu wanapoteza maisha, hiki kitu kinanikosesha amani, hili suala sasa nalichukulia kwa umakini, ndio maana tumeanza na upembuzi yakinifu na tutamaliza na usanifu baadaye kutengeneza barabara,” alisema.Alisema serikali imeanza pia kufanya upanuzi wa bandari za Dar es Salam, Mtwara na Tanga na Kiwira inafanyiwa ukarabati. Pia , alieleza kuwa serikali inakarabati meli za maziwa makuu. Alisema serikali sasa inatekeleza sera ya kukuza utalii ikiwemo Mbeya, ambapo kuna vivutio vingi vya utalii, lakini havitangazwi. Rais Magufuli alisema watalii wanashindwa kwenda maeneo mengi yenye vivutio kwa sababu ya usafiri, kwani asilimia 70 wanatumia usafiri wa anga.Alisema ndio maana serikali inafanya upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Songwe. Pia serikali imejitahidi watanzania kupata elimu bure, imeboresho sekta ya afya, kufuta tozo 80 za kilimo, saba za ufugaji na tano za uvuvi na kuondoa tozo ya ushuru chini ya tani moja.“Iwe ni marufuku kuwatoza watu hizo ni miongoni kwa tozo tulizofuta, ukiwa na mahindi yasiyovuka tani moja wewe safirisha, ukiwa na viazi, miwa ilimradi isizidi tani moja, na ukitaka kuwakomoa wanaokaa barabarani kutoza wewe asubuhi saa mbili safirisha tani moja, saa nne tani moja, saa sita tani moja kufika jioni umesafirisha tani 100, hakuna wa kukutoza na wakuu wa mikoa na wakurugenzi simamieni hili,” alisema.Alisema kero nyingine katika mkoa huo ni kiwanda cha nyama, ambapo aliutaka uongozi wa mkoa huo kuhakikisha kiwanda hicho kilichojengwa enzi za Mwalimu Julius Nyerere kinafufuliwa, hata kama ni kumtafuta mwekezaji mwingine. Azungumzia uongozi Mbeya Alisema hakufanya makosa kumteua mkuu wa mkoa huo aliyopo sasa, na kwamba kabla hajaja makusanyo yalikuwa Sh bilioni 2.5 lakini sasa ni Sh bilioni 5.“Ndio maana hata Mkurugenzi wa Jiji hili nikaleta polisi, nilifanya kwa makusudi, sikuja kujaribu, kwamba akusanye mapato hata kama ni polisi mwenye cheo kikubwa,” alisema Rais Magufuli. Alisema kila mkoa una watu wa aina yake. Alisema kwamba anapenda mkoa huo na ndio maana amewapelekea viongozi hao. Rais Magufuli alishukuru watu wa Mbeya kwa mapokezi makubwa waliyompa, kwani alipokelewa kwa kishindo katika maeneo mbalimbali, alikopita na kuhutubia.Kuhusu Muungano Alisema Tanzania ina kila sababu ya kufurahia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwani kuna nchi ambazo zilijaribu kuungana na kushindwa “Muungano wetu leo unatimiza miaka 55, ni suala la kushukuru sana. Nawapongeza waasisi wa Muungano huu kwa uamuzi wa busara, napongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kulinda Muungano huu na pia kwa watanzania kwa kuendelea kuenzi na kuutunza,” alisema Rais na kusisitiza kuwa Muungano utaendelea kulindwa.
Kitaifa
0
IDADI ya Watanzania wanaofanya shughuli za ulinzi wa amani katika nchi mbalimbali imefikia 100,000 huku 3800 wakiwa wamepoteza maisha tangu kuanzishwa kwa utaratibu wa kutoa walinzi mwaka 1948.Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi jijini Dare s Salaam katika siku ya kuwakumbuka na kuwapongeza walinzi wa amani katika nchi mbalimbali.“Idadi walinda amani karibu 100,000 sasa hivi wako katika nchi mbalimbali za Afrika, hivyo tunawapongeza kwa kazi nzito waliyonayo lakini pia kuwakumbuka walinzi 3,800 waliopoteza maisha kuanzia mwaka 1948 tangu ilipoanza kazi ya ulinzi wa amani,” alisema Dk Mwinyi.Dk Mwinyi alisema Tanzania ina jukumu la kulinda amani, ndio maana inawajibika kuwapeleka walinzi katika nchi mbalimbali ili kuwalinda raia wasiokuwa na hatia wanaotaabika na kukosa amani katika nchi zao.Alizitaja baadhi ya nchi ambazo kwa sasa Tanzania imepeleka walinzi wa amani kuwa ni pamoja na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Afrika ya Kati, Lebanon na Sudan na kwamba bado Tanzania inaendelea kuwapeleka kila itakavyokuwa ikihitajika naUmoja wa Mataifa au Umoja wa Afrika.Alisema Tanzania imekuwa mstari wa mbele kuioyesha dunia kama nchi iko tayari kutoa msaada hasa itakapohitajika lengo likiwa ni kuifanya dunia maeneo salama kwa ajili ya watu kuishi.Kwa upande wake Mratibu Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Umoja wa Mataifa (UN), Alvaro Rodriguez alisema operesheni ya UN ya ulinzi wa amani ni uwekezaji wa amani na ulinzi kidunia.Alisema ulinzi wa amani umekuwa msaada mkubwa kila siku kwa mamilioni ya wahitaji na kuipongeza Tanzania kwa mchango wake wa kutoa walinzi wa amani ili kuhakikisha amani inarejea kwa nchi hizo.
Kitaifa
0
Maombi hayo yamekuja kutokana na suala la mafuta na gesi kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano katika mchakato uliomalizika hivi karibuni wa Katiba Inayopendekezwa na Bunge Maalumu la Katiba.Hayo yalisemwa na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi wakati alipozungumza na wananchi wa jimbo la Kitope huko Kichungwani mkoa wa Kaskazini Unguja, baada ya kushiriki kazi za usambazaji majisafi na salama.Balozi Iddi ambaye ni mbunge wa jimbo hilo alisema miongoni mwa mambo ambayo yalikuwa yakipigiwa kelele na wananchi wengi wa Zanzibar kuondolewa katika orodha ya Muungano ni suala la mafuta na gesi.“Wananchi mambo ambayo tumeyapigania kwa nguvu zote kuhakikisha kwamba yanaondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano ni suala la mafuta na gesi,” alisema.Alisema hatua hiyo imeanza kuleta manufaa makubwa kutokana na baadhi ya wawekezaji, taasisi na mashirika ya kimataifa yanayojishughulisha na kazi za utafutaji wa nishati hiyo kuwasilisha maombi yao.Aidha, balozi aliwataka wananchi kutokubali kuyumbishwa na kudanganywa na wanasiasa ambao hivi sasa wamekuwa wakifanya kazi kubwa kuwababaisha wananchi na kupita kila sehemu wakidai kwamba katiba inayopendekezwa haina maslahi kwa wananchi wa Zanzibar.
Biashara
1
MUSWADA wa Baraza la Vijana la Afrika Mashariki wa mwaka 2017 na Ripoti za Kamati za Utalii, Kilimo na Maliasili ni baadhi ya ajenda zinazotarajiwa kujadiliwa katika Mkutano wa 5 na Kikao cha Pili cha Bunge la Afrika Mashariki (EALA) lililoanza jana jijini Arusha.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya Bunge la EALA kwa vyombo vya habari jijini Arusha, bunge hilo lilianza jana na litaendelea kwa wiki tatu hadi Mei 18, 2019 litapomalizika. Mambo mengine yanayotarajiwa kuwasilishwa na kujadiliwa wakati wa vikao vya bunge hilo ni Ripoti za Kamati za Bunge kwa ajili ya Mwaka wa Fedha unaoishia Juni 30, 2017.Taarifa hiyo ilieleza kuwa lengo la muswada huo wa vijana wa mwaka 2017 ni kutoa mwongozo wa kisheria ili kuweka sawa sheria na sera, zinazowahusu vijana katika jamii ya nchi husika.Muswada huu wa sheria upo katika kipengele cha 120 katika Sheria za Mkataba wa Uundwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambao una dhima ya kusimamia utekelezwaji wa Sera ya Vijana wa Afrika Mashariki, 2014. Mwezi uliopita Bunge la Afrika Mashariki, liliendesha majadiliano ya umma katika nchi wanachama ili kupata mawazo ya vijana kama wadau mojawapo katika muswada huo.Pia kutakuwa na vikao vya Kamati zote za Bunge, ambapo katika wiki ya kwanza kutakuwa na majadiliano ya mambo mbalimbali katika vikao vya kamati. Bunge la Afrika Mashariki lina Kamati sita za Bunge, ambazo ni Kamati ya Hesabu, Kamati ya Kilimo, Utalii na Maliasili, Kamati ya Mambo ya Jumla, Kamati ya Mambo ya Kikanda, Kamati ya Mawasiliano, Biashara na Uwekezaji, Kamati ya Mambo ya Kisheria na Kamati ya Usuluhishi wa Migogoro.Bunge hilo pia linatarajiwa kukutana na baadhi ya wadau wa Mpango wa Usafiri na Usafirishaji (TTTFP), ambao unatarajiwa kuimarisha sekta ya miundombinu hasa barabara kwa ajili ya usafiri na usafirishaji.Mpango huo unaunganisha Jumuiya za Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo ya kusini mwa Afrika (SADC) na Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA).
Kitaifa
0
ZINEDINE Zidane na Real Madrid bado wanawania saini ya nyota wa Manchester United, Paul Pogba.Uongozi wa Madrid unaangalia namna ya kuboresha nafasi ya kiungo msimu ujao na Pogba amekuwa kwenye mipango yao kwa muda mrefu.Vyanzo vya habari vililiambia shirika la habari la ESPN kwamba Zidane anataka kumsajili Pogba lakini United inatarajia kuweka ada ya pauni milioni 120 na Rais wa Madrid Perez anadai ni fedha nyingi.Real Madrid bado inataka kuboresha safu yake ya kiungo licha ya kufanya vizuri kwa Fede Valverde msimu huu.Mchezaji huyo wa Uruguay mwenye umri wa miaka 21 ameonekana kufanya vizuri Bernabeu. Wakati kukiwa bado na sintofahamu juu ya Pogba, mipango mingine ni kumsajili kiungo wa Napoli na Hispania Fabian Ruiz.Fabian, 23, ni mdogo kwa miaka mitatu dhidi ya Pogba, hivyo itakuwa rahisi kumnasa ambapo gharama yake inadaiwa ni kati ya pauni milioni 80 mpaka 100.Kiungo mwingine anayewaniwa na klabu hiyo ni wa Tottenham, Christian Eriksen na Donny van de Beek wa Ajax.Mchezaji huyo wa Spurs mkataba wake unatarajiwa kumalizika Juni mwakani, jambo linalofanya iwe rahisi kumpata.Vyanzo vinasema Zidane anashawishika kumsajili ama Eriksen au Van de Beek, lakini pia anapambana kumnasa Pogba ama Fabian.
michezo
2
Hayo yalisemwa mjini hapa jana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano la uwekezaji la Ukanda wa Ziwa Tanganyika, litakalofanyika mjini Sumbawanga kuanzia Oktoba 26 hadi Novemba Mosi mwaka huu.Alisema baada ya makongamano ya uwekezaji kwenye Ukanda wa Ziwa Tanganyika yaliyofanyika miaka iliyopita wawekezaji kadhaa wameonesha nia ya kuwekeza katika ukanda huo wa mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma.Alisema baadhi yao wametembelea mkoa na halmashauri kwa lengo la kupata taarifa zaidi na kuona maeneo husika.Alisema orodha ya wawekezaji waliopo Mkoa wa Rukwa pekee na kila halmashauri zake ni 56 na kati ya hao walioanza kuwekeza ni 39 na wapatao 17 wanaendelea na taratibu za uwekezaji katika hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na hatua za umilikaji wa ardhi.Alisema kutokana na mazingira ya Ukanda wa Ziwa Tanganyika kuna fursa kubwa za kufanya biashara za kimataifa kati ya Tanzania na nchi za Kongo, Burundi na Zambia.Alisema mikoa ya Ukanda wa Ziwa Tanganyika ina fursa nyingi za uwekezaji ambazo bado hazijawekezwa ipasavyo ikiwemo sekta za viwanda, madini, kilimo, mifugo, uvuvi, maliasili, afya, elimu, utamaduni, michezo, usafiri na usafirishaji kwa njia ya barabara, anga na majini, katika Ziwa Tanganyika.Pia vivutio vya kihistoria vinavyohitajika kuhifadhiwa na kuendelezwa, vivutio vya kitaliii ikiwemo Maporomoko ya Kalambo, samaki wa mapambo, mbuga za Lwafi, Katavi, Gombe na Mahale pamoja na mabwawa ya asili ya Kwela, Sundu na Chimchemi ya Majimoto.
Biashara
1
MAMLAKA ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imebuni kifaa chenye umbo la ndege aina ya tai aliyetengenezwa kufukuza ndege waharibifu wa mazao shambani na anatoa milio kufukuza ndege hao akitumia umeme wa jua.Kutokana na ubunifu huo, Veta imepewa Sh milioni 30 na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kuendeleza tai na hivi karibuni wanatarajia kutengeneza ndege hao wanne watakaofanyiwa majaribio katika mashamba ya mpunga Turiani, Morogoro kwa mwaka mmoja.Ndege huyo mwenye macho yanayowaka na mwanga unaotoka kutisha ndege waharibifu shambani akiwashwa anatoa milio na ndege waharibifu hukimbia anapokuwa shambani.Akizungumza katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Mwalimu wa Veta Chang’ombe , Emmanuel Bukuku alisema ndege huyo ni mwendelezo wa mradi wa awali wa ubunifu.Alisema baada ya kutengeneza awamu ya kwanza, Tai walitakiwa kuwa wengi katika shamba moja hivyo wakamboresha ambapo tai mmoja anaweza kulinda shamba kubwa.Alisema wanaweka nguzo ambazo ndege huyo aina ya tai mmoja anaweza kulinda eneo kubwa kutoka upande mmoja wa shamba kwenda upande mwingine katika shamba la ekari 20.Amesema tai ana uwezo wa kulinda hata ekari 20 kwa sauti kutokana na anavyokuwa katika waya na nguzo huku akitembea kama tai wa ukweli kwa kupeperusha mabawa kama tai wa kawaida.Amesema ili kupata fedha ya ruzuku, walipeleka pendekezo la ndege huyo kwa ajili ya ulinzi wa mashamba na waombaji ruzuku walikuwa 600 na kupatikana 47 nchi nzima na kupewa fedha kupeleka vifaa kwa majaribio na baadaye kutengeneza vifaa vingi ili vitumiwe mashambani.Amesema baada ya kupata Sh milioni 30 wataunda ndege tai wanne na kutengeneza miundombinu yake kisha kufanya majaribio katika mashamba ya mpunga huko Turiani mkoani Morogoro kwa mwaka mmoja.Aliwaeleza wakulima wa mpunga, ngano na uwele na mashamba ya mazao ya asili ya mbegu ambao wamekuwa wakivamiwa na ndege waharibifu wamepata mkombozi mkubwa wa teknolojia
Kitaifa
0
['Uganda inashuka dimbani saa mbili usiku wa leo dhidi ya Zimbabwe katika mchezo wa pili wa Kundi A. ', 'Endapo Uganda itashinda mchezo huo, itaandika historia ya pili katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Africa (Afcon). ', 'Siku ya Jumamosi Uganda iliandika historia kwa kushinda mchezo wake wa kwanza wa Afcon, ikiwaadhibu jirani zao DR Congo goli 2-0.', 'Mwaka 2017 Uganda ilishiriki Afcon lakini ilishindwa kuandika ushindi walau kwenye mchezo mmoja. ', 'Leo hii wanavaana na Zimbabwe, Uganda wanahitaji ushindi kwa hali na mali ili wafuzu moja kwa moja hatua ya mtoano. ', 'Katika mechi ya kwanza dhidi ya DRC Uganda hawakupigiwa sana upatu kuondoka na ushindi. ', 'DRC kwa takwimu za ubora wa viwango ipo juu ya Uganda, ina wachezaji wenye uzoefu zaidi na ni mabingwa mara mbili wa kombe hilo. ', 'Lakini magoli ya Patrick Kaddu katika dakika ya 14 na Emmanuel Okwi katika dakika ya 48 yalitosha kuzamisha jahazi la DRC.', 'Wenyeji Misri pia wapo kwenye Kundi A, na mchezo wa kwanza walipata ushindi mwembamba wa goli moja dhidi ya Zimbabwe. ', 'Japo Zimbabwe wanaonekana ni vibonde katika kundi hilo, kufungwa goli moja na wenyeji Misri inaonesha kuwa si timu ya kubeza. ', 'Tayari kocha wa Uganda, Sebastien Desabre amekanusha kuidharau Zimbabwe na kusema anatarajia mchezo mgunu hii leo.', 'Kwa Uganda, wakishindwa kupata ushindi, walau sare itawafaa katika kujiimarisha na hesabu za kufuzu kwa hatua ya mtoano. ', 'Katika mpambano mwengine hii leo, wenyeji Misri watacheza na DRC. ', 'Mchezo huo utapigwa kuanzia saa tano usiku. ', 'Misri, itataka kuonesha kiwango bora zaidi kulinganisha na mechi dhidi ya Zimbabwe, na kupata ushindi utakaowavusha mpaka hatua ya mtoano.', 'DRC wao wanataka kuonesha kuwa bado ni timu nzuri ambayo kwa kiwango chao hawawezi kufungwa mechi mbili mfululizo. ']
michezo
2
MAKAMISHNA na Warajisi Wasaidizi wa Mikoa wameshauriwa kuhamasisha Vyama vya Akiba na Mikopo (Saccos) na Ushirika vianze kuwekeza katika miradi mikubwa itakayovipa maendeleo zaidi na wanachama kwa ujumla.Saccos na Vyama vya Ushirika vinaweza kujenga majumba ya kupangisha, kujenga vitega uchumi vikubwa, kujenga njia za usafiri na kuwekeza katika miradi mingine mingi. Akizungumza katika Kikao Kazi cha Makamishna na Warajisi Wasaidizi wa Mikoa jijini hapa, Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Nchini, Dk Titus Kamani alivitaka vyama hivyo kufanya uwekezaji katika miradi.Alisema vyama vya ushirika na Saccos nchini, zinatakiwa kuwekeza kwenye miradi mikubwa kama zinataka kushiriki katika mkakati wa serikali ya awamu ya tano ya kuingia katika uchumi wa kati na maendeleo ya viwanda.Pia aliwataka wale wote wanaodaiwa madeni au waliojimilikisha mali za vyama vya ushirika ngazi za juu hadi chini kuzirudisha mali hizo. Alisema warajisi ndio wasimamizi wa rasilimali za ushirika za maeneo yao, hivyo wawaagize waliopora mali hizo kuzirejesha kwa ngazi zote.Alisema wadaiwa waliokopa au kujimilikisha maghala, majengo, miundombinu mbalimbali, mashamba na raslimali nyingine za ushirika na Saccos wote wanatakiwa kurudisha mali hizo.Aliagiza wakopaji hao wasipoteze fedha zao kwenda mahakamani kwani wanapoteza bure fedha zao, hakuna njia nyingine zaidi ya kulipa. Alisema vyama vya ushirika na Saccos zinatakiwa kuunganisha nguvu kukuza mitaji na kujiingiza katika uwekezaji badala ya kufanya shughuli ndogo zinazoleta maendeleo kidogo.Alisema warajisi wa mikoa na maafisa ushirika wa wilaya na ngazi za chini, wanatakiwa kufanya kazi wakishirikiana na wakuu wa mikoa, wilaya na maofisa tawala, wakurugenzi na walezi wa vyama hivyo katika ngazi zote.Alitaka wahakikishe wakulima, wafugaji na wavuvi na taasisi wanaanzisha shughuli zao kwa ushirika, kwani una nguvu na sauti kubwa zaidi kama walivyofanya wakulima wa korosho.Alisema watu wanatakiwa kuuamini ushirika na Saccos kwani ni benki za nyumbani, kutokana na urahisi wake wa kutoa mikopo yenye riba ndogo, hivyo wananchi wajiunge na ushirika na waumini ni mkombozi wa wananchi wengi. Katibu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini, Tito Haule aliwataka Warajisi Wasaidizi kufanya kazi hiyo kwa weredi na kuhakikisha ushirika katika maeneo yao unakuwa imara.Aliwataka viongozi hao kujipima uongozi wao kwa kufanya mambo ya maendeleo ikiwemo la kukusanya fedha za Mfuko wa Usimamizi wa Mrajisi ambao ni muhimu kwa maendeleo yake. Haule alisema katika kujipima wanatakiwa kuunda bodi na taasisi nyingine kwa umakini na siyo kisiasa ili kupata uongozi bora zaidi. Aliwataka warajisi hao kukusanya mapato kutokana vyama vya ushirika kwani baadhi ya mikoa haijafanya vizuri katika makusanyo.
Kitaifa
0
SERIKALI imesisitiza kuwa haitatoa leseni kwa wachimbaji wa madini wanaofahamika kuwa si waaminifu na wamekuwa wakitumia sababu mbalimbali za kujitungia kukwepa kulipa kodi.Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila alisema hayo kijijini Itumbi kata ya Matundasi wilayani Chunya alipokuwa akijibu hoja za wachimbaji wadogo juu ya kuchelewa kwa leseni kwa watu walioomba.Alikuwa akifungua mafunzo ya siku mbili yaliyolenga kutoa matokeo ya utafiti wa kina wa kijiosayansi wa dhahabu.Msanjila alisema pamoja na kuwa serikali ilisitisha kwa muda utoaji leseni, kwa sasa baadhi ya wachimbaji walioomba wameshaanza kupewa.Hata hivyo aliwataka kutambua kuwa kwa wale wanaofahamika kuwa si waaminifu wasitarajie kupata leseni mpya.Katibu mkuu huyo pia alionesha kusikitishwa na hatua ya idadi ya maduhuli ya kodi yanaokusanywa kutoka kwa wachimbaji wadogo kuwa ndogo kuliko ya wachimbaji wakubwa, licha ya kuwa takwimu zinaonesha kada hiyo ndiyo iliyo na leseni nyingi zaidi.Aliwataka wachimbaji kutanguliza uzalendo wa kulipa kodi wakitambua kuwa serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili ya mikakati mbalimbali ya kukuza sekta ya wachimbaji wadogo, ikiwamo kuendesha tafiti kubwa kama hiyo ya kijiosayansi iliyogharimu Sh bilioni saba."Wizara ya madini tutaendelea kushirikiana nanyi kwa kufuatilia matokeo ya tafiti hizi, namna zinavyotumika na pia itaendeleza nyingine. Lengo hapa ni kuongeza uzalishaji kwenu ili siku moja muwe wachimbaji wakubwa,"alisema.Alisema serikali inafanya jitihada kubwa na sasa kuna vituo saba vya mafunzo vinavyojengwa. Kati ya hivyo kimoja kiko wilayani Chunya.“Pia kipo kituo cha mfano cha uchenjuaji dhahabu kinajengwa hapa hapa Itumbi,” alisema na kuhimiza ulipaji kodi.Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Madini (Stamico), Sylvester Ghuliku alisema utafiti huo uliofanywa na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti madini (GST) na Stamico uliofanyika kati ya Septemba 2016 na Machi mwaka huu, utawezesha wachimbaji wadogo kutoka walipokuwa wachimbaji wa kati hadi wakubwa.Mjiolojia kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti madini Tanzania, Joseph Matalu alisema matokeo ya uchunguzi uliofanyika yaliwezesha ukadiriaji wa mashapo.Wakizungumzia mafunzo na matokeo ya utafiti huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wadogo mkoani Mbeya (Mbelema), Leonard Manyesha alisema yamekuja kwa muda muafaka kwa kuwa yatawaondolea adha ya kuchimba kwa mazoea pasipokujua ulalo wa mwamba wenye madini chini ya ardhi.
Biashara
1
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wananchi kwenye Kata ya Mnacho wilayani Ruangwa washirikiane kujenga mabweni katika Shule ya Sekondari Mnacho ili kuwaondolea wanafunzi adha ya kutembea umbali mrefu kwenda shuleni hapo.Aliyasema hayo wakati alipotembelea shule hiyo kwa ajili ya kukagua mradi wa ujenzi wa bweni, ambalo ujenzi wake unagharimu Sh milioni 92.4 ikiwa ni mchango uliotolewa na wadau wa elimu.“Bweni hili likikamilika litawapunguzia wanafunzi kutembea umbali mrefu kuja shuleni hususani wanaoishi vijiji vya mbali kwa sababu wataishi hapa, jambo ambalo litachangia kuongeza ufaulu wa watoto wetu.”Kadhalika, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi waishio katika kata hiyo na za jirani washirikiane na kuanzisha mradi wa ujenzi wa mabweni mengine kwa kuwa hilo moja lililojengwa na wadau halitoshi kulingana na idadi ya wanafunzi.Alisema yeye yuko tayari kuendelea kuwaunga mkono wananchi hao kwenye mipango yao yote ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kata yao, lengo likiwa ni kuhakikisha mikakati ya serikali ya kuboresha huduma za jamii inatimia.Hata hivyo, Waziri Mkuu aliwataka wananchi hao washirikiane na walimu kufuatilia maendeleo ya taaluma kwa watoto wao shuleni na kujiridhisha kama wanafanya vizuri darasani na iwapo watabaini changamoto waweze kuzitatua kwa pamoja.Akisoma taarifa ya ujenzi wa bweni hilo, Mkuu wa Shule ya Sekondari Mnacho, Mwalimu David Mwakalobo alisema ujenzi wa bweni hilo lenye uwezo kulaza wanafunzi 80 ulianza Septemba 19, mwaka huu na unatarajiwa kukamilika Januari, 2019.
Kitaifa
0
RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Makampuni ya Bakhresa, Said Salim Bakhressa kutokana na vifo vya wafanyakazi watano wa Azam Media Limited kutokana na ajali ya barabarani.Ajali hiyo Jumatatu katika eneo la katikati ya Igunga (Tabora) na Shelui (Singida) ambapo wafanyakazi hao pamoja na madereva wawili waliofariki dunia baada ya basi aina ya Coaster waliokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na gari la mizigo wakati wakielekea wilayani Chato kwa ajili ya uzinduzi wa hifadhi hiyo ya Taifa ya Chato-Burigi.Katika salamu hizo za rambirambi Rais Shein alieleza kuwa amepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa ya ajali hio na kwamba yeye binafsi pamoja na wananchi wote wa Zanzibar na Tanzania nzima kwa jumla wamejawa na simanzi nzito kutokana na vifo vya wafanyakazi hao.“Kutokana na msiba huu, natoa salamu za rambirambi kwako Said Salim Bakhressa, ndugu, wanafamilia wa marehemu, marafiki, wafanyakazi wote wa Makampuni ya S.S. Bakhressa pamoja na watazamaji, wasikilizaji na wafuatiliaji wa vipindi na habari mbali mbali zinazotolewa na Azam Media Limited, ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”, ilieleza sehemu ya salamu za rambirambi alizozituma Dk Shein.Hata hivyo, Jeshi la Polisi mkoani Singida limesema kuwa uchunguzi wa ajali hiyo bado unaendelea. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike, alisema bado wanaendelea kumshikilia dereva wa lori lenye namba za usajili T287 DFR lililogongana uso kwa uso na gari aina ya Coaster lenye namba za usajili T 319 DMQ. Alisema taarifa kamili za chanzo cha ajali hiyo iliyotokea Jumatatu asubuhi wiki hii atazitoa wakati wowote uchunguzi utakapokamilika.Waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo ni pamoja na Salim Mhando ambaye alizaliwa mwaka 1985 ambaye alikuwa mtaalamu wa kuchanganya picha, Florence Ndibalema (1989) mtaalam wa sauti, Said Haji (1989) mpiga picha, Silvanus Kassongo (1989) Injinia na Charles Wandwi (1980) mpigapicha. Wengine waliokufa kwenye ajali hiyo ni Juma Hatibu Juma (dereva wa Coaster) na Hussein Habibu.Majeruhi katika ajali hiyo ni Mohamed Mwinshehe, Mohamed Mahige na Datus Masawe. Wafanyakazi hao wa Azam Media Limited walipoteza maisha waliagwa juzi Dar es Salaam kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Kampuni hiyo. Marehemu Salim Mhando alizikwa juzi kwenye makaburi ya Manzese- Sweetcorner jijini Dar es Salaam, Charles Wandwi alizikwa jana kwenye makaburi ya Sinza, Said Haji alizikwa juzi Hale-Tanga, Kassongo alizikwa jana mkoani Iringa na Florence Ndibalema anatarajiwa kuzikwa leo Bukoba. Watu mbalimbali akiwemo Rais Magufuli walitoa salamu za rambi rambi kufuatia msiba huo ulioikumba Azam Media Limited.
Kitaifa
0
TIMU ya taifa ya Soka ya Wanawake ya Tanzania Bara, ‘Kilimanjaro Queens’ jana ilimaliza kwa kishindo hatua ya makundi ya Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) baada ya kuifunga Zanzibar mabao 7-0.Mchezo huo wa kukamilisha ratiba baada ya Zanzibar kuwa tayari ilishatolewa kutokana na kufungwa mabao yote, Kilimanjaro Queens walitawala muda wote na kulishambulia lango la wapinzani kama nyuki.Mchezaji Deonisia Minja aliifungia Kilimanjaro Queens mabao mawili, katika dakika ya 26 na 55, huku Diana Msewe aklifunga bao katika dakika ya 30 huku Philomena Kizima alifunga katika dakika ya 69 kwa shuti kali.Mabao mengine ya Kili Queens yalifungwa na Asha Rashid katika dakika ya 83 na 85, huku Anastazia Katunzi akifunga la saba katika dakika ya 87 na kuwafanya wenyeji kuondoka na ushindi mnono wa mabao 7-0.Stars imefunga magoli 20 katika michezo yake mitatu huku golikipa, Zubeda Mugunda pamoja na safu yake ya ulinzi wakiwa hawajaruhusu goli hata moja huku Zanzibar ikibeba kapu la magoli 17 bila kufunga goli hata moja katika michezo yake yote mitatu.Katika mchezo wa awali jana, Burundi waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Sudan Kusini na kuifanya Burundi kutinga hatua ya nusu fainali na kuzifuata Kilimanjaro Queens, Kenya na Uganda.Kundi B mechi zake wanamaliza kesho kwa Kenya kucheza dhidi ya Uganda na hapo ndipo atajulikana mpinzani wa Kilimanjaro Queens kwani timu hizo kila moja ina pointi 14 na imefungwa bao moja tu. Mshindi wa pili wa Kundi B ndiye atakayecheza dhidi ya Kilimanjaro Queen wakati mshindi wa kwanza atacheza na Burundi, ambaye ndiye mshindi wa pili wa Kundi A.
michezo
2
Vikundi hivyo 10 vinatarajia kushiriki maonesho hayo yatakayoshirikisha vikundi vingine vya Kanda ya Ziwa.Maonesho hayo yatashirikisha mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Kagera, Mara, Geita pamoja na wenyeji Mwanza hivyo kutoa fursa nzuri kwa vikundi na watu binafsi vinavyojishughulisha na uzalishaji mali kuonesha bidhaa zao.Ofisa Ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Masatu Magafu amesema vikundi vitatu na watu binafsi saba wamepatikana baada ya kuzingatia vigezo vinne kwa kufanyika mchujo kuanzia ngazi ya kata na tarafa.Vigezo hivyo ni pamoja na kuzingatia ubora wa bidhaa, mazao na mifugo ,uwezo wa kujieleza , uhusiano wa bidhaa na maonesho hayo pamoja na ubunifu na teknolojia iliyotumika.
Biashara
1
VIJIJI 48 kati ya 57 Wilayani Mpwapwa katika mkoa wa Dodoma, tayari vina huduma ya umeme huku vikisalia vinane pekee ambavyo navyo vinatarajiwa kuwekewa wakati wowote.Mara utaratibu wa kupeleka umeme katika vijiji kukamilika, watahamia katika ngazi ya vitongoji katika uwekaji umeme. Akizungumza wakati wa ziara wilayani humo katika kijiji cha Igoji One na Chipogolo, Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani alimtaka Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wilayani Mpwapwa kuhakikisha anakamilisha kuwawekea umeme wanakijiji wa eneo hilo.Alisema lengo la serikali ni kuhakikisha kwamba wanawafungia umeme wananchi ili hadi kufikia Desemba mwaka huu, wote wawe wamepata huduma ya umeme. Hata hivyo katika kijiji hicho, Waziri Kalemani aliwasha umeme katika zahanati ya Igoji One ambapo wameanza kutumia umeme baada ya kuunganishiwa. Alisema meneja anapaswa kuendelea kuwawekea umeme wananchi wake huku akikisisitiza vijengwe vituo vidogo vya umeme katika vijiji ili kuwapunguzia mwendo wa kutembea kwenda kupata huduma za Tanesco.Pia aligawa Umeme Tayari (UMETA) 280 kwa wanakijiji hicho bure kwa ajili ya kuunganishiwa umeme. Alisema UMETA hizo zinatakiwa kugawiwa bure kwa wananchi ili wote waweze kuwa na umeme kwa sababu umeme ni biashara.Alisema UMETA hizo pia alizigawa katika kijiji cha Ipogolo ili wananchi waweze kuwashiwa umeme. Pia alimuagiza mkandarasi Ikandam kuwaajiri vijana wa kijijini hapo ili kusaidia kazi za kuunganisha umeme kijijini hapo na akamtaka kuwalipa posho na sio kuwadhulumu kama alivyopata malalamiko kutoka kwa vijana hao. Alisema hakuna kuajiri watu wengine na badala yake awaajiri vijana wa kijiji hicho.Naye, Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene alimshukuru Waziri Kalemani kwa kuwasaidia kuleta umeme kijijini hapo. Alisema wamekuwa wakilalamika kukosa umeme lakini sasa wanashukuru wameunganishiwa baadhi ya vijiji na wana imani vingine vitafikiwa na huduma ya umeme.Aliwataka wananchi wake kuwa na subira umeme utawafikia muda sio mrefu katika vijiji ambavyo bado. Kalemani aliagiza mkandarasi wa kampuni ya OK kukamatwa kutokana na kutokamilisha kuwasha umeme katika kijiji cha Chibwegere. Alisema ufungaji umeme katika kijiji hicho ilibidi ukamilike tangu mwaka jana, lakini hadi sasa hakuna alichofanya na haonekani katika kutekeleza kazi hiyo.
Kitaifa
0